October 8, 2016

UWT MUFINDI WALAANI TUKIO LA MWANAFUNZI MBEYA DAY KUSHAMBULIWA KWA KIPIGO ........

UMOJA  wa  wanawake Tanzania  (UWT) wilaya  ya  Mufindi  mkoani Iringa  umelaani  vikali adhabu iliyotolewa kwa mwanafunzi wa  shule ya  sekondari  ya  Mbeya Day kwa  kumshambulia mwanafunzi  kikatili  na  kuomba    walimu  wilayani  humo na Tanzania   kujiepusha na utoaji wa adhabu  hatari  kwa  wanafunzi .

Mwenyekiti  wa UWT  wilaya ya  Mufindi na mjumbe wa NEC  Taifa  Marcelina  Mkini  aliwaeleza  waandishi wa habari jana  kuwa  pamoja na kazi kubwa  na  nzuri  inayofanywa na walimu  nchini  kwa  kufundisha  na  kulea  watoto  ila  bado baadhi yao  wameingia katika fani   hiyo  kimakosa  kutokana na unyama  wanaoufanywa kwa  wanafunzi  pindi  wanapokosa .

Mkini  alisema  kuwa  ni  vema  walimu  kutoa adhabu   stahiki kwa  wanafunzi badala ya  kutoa adhabu  kipigo  kikali kama  ilivyofanywa na  wanafunzi  wanne  wa   mazoezi   waliokuwepo katika  shule  hiyo ya  Mbeya  kwa  mwanafunzi Sebastian Chinguku (17)  kuwa  kipigo  kile  hakukulenga  kumwonya  mwanafunzi  bali  kilikuwa ni  kipigo chenye hatari  ya  kumsababishia ulemavu ama  kupoteza maisha ya  mwanafunzi huyo .

" Tukio  la  walimu  hao  wanafunzi  lililofanywa shule ya  Mbeya  Day  si la  kufumbiwa macho  na  tukio  hili  liwaongoze  walimu  kote nchini  kujitathimini aina ya adhabu  wanazozitoa kwa wanafunzi "

Alisema   UWT ni  jumuiya ndani ya  CCM inayounganisha  wanawake na kwa kuwa mama  ndio mwenye  uchungu  zaidi  wa  mwana   kutokana na  tukio   hilo la Mbeya   wameona  si  vema  kubaki  kimya  pasipo  kuwaonya  walimu wenye  tabia  kama  hizo  za  kutesa  wanafunzi  kuziacha mara  moja .

Hivyo  alisema hategemei katika wilaya  yake ya  Mufindi  kuona ama  kusikia mwalimu akifanya  vitendo vya kinyama kama  hivyo  dhidi ya  watoto na kuwa  kwa  walimu  wanaofanya   hivyo kuacha mara moja  na  kutaka  wazazi  kuwa karibu na  watoto  wao na iwapo itabainika kuna  mwalimu ama  shule  inayotesa  wanafunzi kama Mbeya  Day  basi  wazazi  wasiache  kupeleka malalamiko yao kwa mkuu wa  wilaya  ili  kuchukua hatua.

Hata   hivyo alipongeza hatua za haraka  zilizochukuliwa na waziri wa mambo ya  ndani  dhidi ya  walimu hao ,waziri wa TAMISEMI na  waziri wa elimu na  kuwa iwapo  kuna shule  nyingine yenye mateso kama  shule  hiyo ya  Mbeya  Day  ni  vema jamii  kuiweka   wazi ili  kukomesha vitendo vya  ukatili mashuleni .

Kuhusu  wanafunzi aliwataka  wanafunzi kujenga nidhamu ya  kuheshimu  walimu pamoja na kufuata taratibu za shule kwa  kuzingatia masomo na kuepuka vitendo  vyote  vyenye chembe ya  utovu wa  nidhamu  ili  kuwawezesha walimu  kuwafundisha  pasipo  makwazo.


Akizungumza na vyombo vya habarijuu ya  tukio hilo wa Elimu, Prof Joyce Ndalichako alimesema kuwa kitendo hicho ni cha kikatili, jinai na walimu hao wanafunzi hawafai kuendelea na taaluma hiyo ya ualimu na kuwa hatua zaidi za kisheria zinaendelea kuchukuliwa.

Waziri Ndalichako alisema kwa mujibu wa taratibu za vyuo vikuu kitendo kilichofanyika ni kosa la jinai na kuwa hakiwezi kufumbiwa macho.
Waziri pia ametoa onyo kali kwa wanafunzi wanaokwenda kwenye mazoezi kwa vitendo na kuwa kwenda kinyume na taaluma mwanafunzi wa vitendo anakuwa amepoteza sifa, hivyo amewataka kuzingatia maadili ya fani na taaluma wanazozisomea.

Katika hatua nyingine, Waziri wa TAMISEMI George Simbachawene alitangaza kumvua madaraka Mkuu wa Sekondari ya Mbeya Kutwa kwa kufumbia macho ukatili dhidi ya mwanafunzi.

Simbachawene amesema kuwa tukio hilo lilitokea tarehe 28.09.2016 ambapo walimu wa mazoezi kutoka chuo kikuu cha elimu Dar es salaam DUCE na walimu wenzao wa mazoezi kutoka chuo kikuu cha kumbukumbu cha Mwalimu Nyerere walishirikiana kumwadhibu mwanafunzi wa kidato cha tatu Sebastian Chingulu kwa maelezo kwambza aligoma kufanya adhabu alizopewa na mwalimu Frank Msigwa .

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Simachawene amewataja walimu hao kuwa ni pamoja na
(i) Frank Msigwa - Ndiye aliyesababisha tukio hilo pia ndiye aliyempiga zaidi, huyu anatoka DUCE
(ii) John Deo – Anatoka DUCE
(iii) Sante Gwamoka – Anatoka DUCE
(iv) Evans Sanga – Anatoka Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere
Amesema kuwa baada ya kuona tukio hilo kwenye mitandao ya kijamii, ofisi yake ilifuatilia na kuamua kuchukua hatua kadhaa ikiwemo kuagiza mamlaka husika kumvua madaraka mkuu huyo wa shule Magreth Haule .
Sehemu ya taarifa ya Waziri inasema kama ifuatavyo:-
"Nilimuagiza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kwenda na Vyombo vyake vya ulinzi na Usalama kwenda na kwamba mahojiano kati ya walimu na polisi yanaendelea

Kwa kuwa waliotenda tukio hilo wametoweka tangu tar 29 Sept 2016 na hawajulikanai walipo, nimesikitishwa na kiteno cha mwalimu mkuu wa shule hiyo kutochukua hatua yoyote ikiwa ni pamoja na kutotoa taarifa hadi leo tulipoona kwenye mitandao ya kijamii, hii ni dalili ya kuwepo kwa dalili ya kulitaka kulificha

MWISHO


0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE