October 19, 2016

UCHAGUZI MKUU MAREKANI , NDUGU WA OMBAMA MGENI RASMI MDAHALO WA TRUMP

Malik Obama alikuwa awali amesema angependa sana kukutana na Bw Trump 
 
Maafisa wa kampeni wa mgombea urais wa chama cha Republican Donald Trump wamepanga kumwalika kaka wa kambo wa Rais Barack Obama kuhudhuria mdahalo wa mwisho wa urais nchini Marekani.

Maafisa hao wamesema Malik Obama, ambaye alizaliwa Kenya, atakuwa miongozi mwa hadhira itakayofuatilia mdahalo huo wa runinga, Bw Trump alikabiliana na mpinzani wake wa chama cha Democratic Hillary Clinton.

Malik, aliambia gazeti la New York Post kwamba ana furaha isiyo na kifani kwamba atahudhuria mdahalo huo.

"Trump anaweza kuirejeshea Marekani fahari yake tena," amesema, kwa mujibu wa shirika la habari la AP.
Wagombea wamekuwa wakitumia wageni kwenye midahalo kama njia ya kuwakabili wapinzani wao.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE