October 21, 2016

POLISI IRINGA WAKAMATA WATUHUMIWA WATATU WALIOTEKA MALORI YA MNADANI NA KUUA MFANYABIASHARA MMOJA WA MNADANI

Kamanda  wa  polisi mkoa wa Iringa ACP Julius Mjengi   akionyesha simu zilizokutwa kwa  watuhumiwa wa ujambazi wa kutumia silaha  walioteka malori matatu na kuua mfanyabiashara  mmoja  hivi  karibuni pili  kulia ni Joseph  George  wamahe (25) mkazi wa Mbagala jijini  Dar es salaam , James  Flavianus Itembe  (35) mkazi wa Ukonga Mombasa  jijini  Dar es Salaam  na Machage Magwe  Mwita (38) mkazi wa Buguruni jini  Dar es Salaam
Kamanda  wa  polisi  mkoa wa Iringa ACP Julius Mjengi   akitoa  taarifa kwa wanahabari  ofisini kwake  kuhusiana   na  kukamatwa  kwa  watuhumiwa  watatu wanaodaiwa  kuteka  magari matatu ya mnadani  katika  kata  ya  Ruaha Mbuyuni wilaya ya  Kilolo na  kuua mmoja  ambao  walikamatwa  jijini Dar es salaam  kulia  ni  watuhumiwa hao   wakiwa chini ni ulinzi wa  polisi   wa  pili  kulia ni Joseph  George  wamahe (25) mkazi wa Mbagala jijini  Dar es salaam , James  Flavianus Itembe  (35) mkazi wa Ukonga Mombasa  jijini  Dar es Salaam  na Machage Magwe  Mwita (38) mkazi wa Buguruni jini  Dar es Salaam
Askari  wakiwa wameweka  ulinzi mkali wakati  kamanda wa  polisi mkoa  wa Iringa  akitoa taarifa ya watuhumiwa wa mauwaji kwa  waandishi wa habari
Watuhumiwa  wa ujambazi  wanaodaiwa  kuteka  wafanyabiashara wa mnadani wilaya ya  Kilolo  wakiwa  chini ya ulinzi
 
Na MatukiodaimaBlog 
JESHI  la  polisi  mkoani  Iringa  limewakamata  watuhumiwa  watatu  kati ya nane  wanaodaiwa  kuhusika kuteka  wafanyabiashara   waliokuwa   wakitoka mnadani  na  kuua mmoja   huku  wengine  zaidi ya 10  wakijeruhiwa  vibaya  katika  tukio  hilo la  unyang'anyi wa  kutumia  silaha  lililotokea  katika  kitongoji cha  Kichangani kijiji  cha Mtandika  kata ya  Ruaha Mbuyuni  wilaya ya  Kilolo mkoani hapa  hivi  karibuni .

Watuhumiwa hao  pia  wamekiri kuhusika na matukio mbali mbali ya unyang'anyi wa  kutumia  sialaha  katika  mikoa ya  Tanga , Morogoro  na maeneo mbali mbali ya  nchi  wamekamatwa  jijini  Dar es Salaam  na makachero  wa  polisi  kutoka mkoa  wa Iringa ambao  walikuwa wakiendesha msako kufuatia  tukio  hilo  la unyang'anyi  wa  kutumia  silaha  lililotokea   Septemba 25 mwaka huu wilayani  Kilolo.

Kamanda  wa  polisi wa mkoa wa  Iringa ACP  Julius Mjengi  aliwaambia  waandishi wa habari leo   ofisini  kwake  kuwa   septemba  25  mwaka  huu majira ya  3  usiku  katika  kitongoji  cha Kichangani kata ya Ruaha  Mbuyuni  wilaya ya  Kilolo  majambazi waliteka  malori  matatu ya  wafanyabiashara   waliokuwa wakitoka mnada wa Nyazwa  malori  hayo ni T 517 AWG aina ya Mitsubishi Fuso , T 922 AMJ aina ya  Toyota Dyna na T  496 ADE aina  ya Tata 

Alisema  kuwa  katika   tukio hilo watu hao  wanaosadikiwa ni  majambazi  waliwajeruhi  wafanyabiashara  kadhaa na  kuwapora  fedha  na  simu aina  mbali mbali  na mmoja kati ya majeruhi  aliyefahamika kwa  jina la Felemoni  Edward Mboya  alifariki dunia   wakati akipatiwa matibabu  katika  Hospitali ya Mikumi  mkoa  wa Morogoro .

 Kamanda  Mjengi  alisema kufuatia  tukio  hilo jeshi  la  polisi  mkoani hapa lilianza msako mkali wa  kuwatafuta  waliohusika na tukio hilo na  kufanikiwa  kuwakamata  watuhumiwa  watatu  wa  tukio hilo  ambao ni Joseph  George  wamahe (25) mkazi wa Mbagala jijini  Dar es salaam , James  Flavianus Itembe  (35) mkazi wa Ukonga Mombasa  jijini  Dar es Salaam  na Machage Magwe  Mwita (38) mkazi wa Buguruni jini  Dar es Salaam .

 Kuwa  watuhumiwa hao  walikiri   kushiriki katika  tukio hilo la  ujambazi na  walipopekuliwa  mtuhumiwa Joseph Wamahe  alikutwa na simu mbili aina ya Itel 5320 ambazo  ziliporwa  katika  tukio hilo kutoka kwa  wafanyabiashara  hao wa mnadani na mtuhumiwa James Itembe alikutwa na simu  moja aina ya Tecno ambazo  pia  ni moja  kati ya  simu zilizoporwa katika  tukio hilo .

Kamanda  Mjengi  alisema  watuhumiwa  hao  wote  watatu  upelelezi wao  umekamilika  na watafikishwa  mahakamani kwa kosa la mauwaji na msako bado unaendelea   kuwatafuta   washiriki  wengine  waliobaki ambao  walihusika na tukio  hilo la mauwaji .

 Hata   hivyo  alisema  watuhumiwa hao  wamekiri  pia   kuhusika na mtandao wa ujambazi  wa kutumia  silaha katika mikoa mbali mbali hapa nchini ukiwemo mkoa wa Tanga , Morogoro  ,Dar es Salaam na maeneo mengine  pamoja na Iringa .

Hivyo  kamanda  huyo  alitaka  wakazi wa mkoa wa Iringa  kuendelea kutoa  ushirikiano kwa  jeshi la polisi na kuwafichua  wale  wote wanaojihusisha na matukio ya uharifu ama  kuhifadhi  wahalifu .

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE