October 24, 2016

NYUMBA YAUNGUA MOTO KIMAUZA UZA IRINGA


Baadhi ya  vitu  vilivyoungua na moto  huo

                                  Kamanda  wa  kikosi  cha  Zimamoto  Iringa 


                            Na Dajari Mgidange MatukiodaimaBlog


Nyumba moja imeungua moto na kuteketeza baadhi ya vitu vilivyomo ndani  maeneo ya Mlandege Mjini Iringa bila kufahamu wenyeji wa nyumba hiyo chanzo chake. 

Akizungumza na MATUKIO DAIMA mama ambaye anakaa kwenye nyumba hiyo ambayo imeungua  Joyce Moses amesema kua, wakati moto unatokea nyumbani hapo yeye alikua ameenda msibani na alipigiwa simu na majirani zake kua nyumba inaungua lakini yeye alijua ni utani kutokana na majirani hao kua na mazoea ya kutaniana.

Mmoja wa shuhuda wa tukio hilo Zuwena amesema kua wakati anakunywa chai aliona moshi mkubwa ukitoka nyumbani hapo na akajua kua ni maharage yanaungua ndio alipoinuka kwenda kuangalia alikuta moshi mkubwa ndani alishindwa kuingia ndani hapo kutokana na moshi mkubwa ndipo alipopiga kelele kuomba msaada kwa majirani wenzake.

Bwana Cathbeth ni mmoja wa shuhuda ambaye aliweza kupiga simu kituo cha kuzima moto FIRE na yeye akafika eneo hilo la tukio na kuweza kutoa msaada kwa kuchukua kifaa cha kuzimia moto yaani Fire Extinguisher na kuuzima moto huo wakati gari la zima moto likiwasili hapo halikupata shida kwani majirani waliweza kuudhibiti moto kwa kiasi na wakashirikiana na majirani kuzima moto huo na kuokoa baadhi ya vitu vilivyomo ndani ya nyumba hiyo.

Akithibitisha kutokea kwa Tukio hilo Kamanda wa Jeshi la Zima Moto Mkoani Iringa Bwana Kennedy Komba amesema kua chanzo cha moto ni kigai ambacho ni kilikua na moto na kutokana na hali ya hewa moto uliruka na kushika mito ya makochi na kuanza kuwaka.

Aidha Komba amewataka wananchi kuchukua taahadhari ya majanga ya moto kwa kuweza kua na vitu ambavyo vinaweza kuzima moto ikiwemo fire extinguisher pamoja na madebe ya mchanga majumbani mwao .

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE