October 10, 2016

MKURUGENZI MKUU WA PPF, WILLIAM ERIO ATEMBELEA ENEO LITAKALOTUMIKA KUJENGA KIWANDA KIPYA CHA KUCHAKATA NGOZI NA KUTENGENEZA VIATU, GEREZA LA KARANGA MJINI MOSHI

 Mkuu wa gereza la Karanga, mjini Moshi, mkoa wa Kilimanjaro, ambako ndiko kilipo kiwanda cha kutengeneza viatu, Kamishna Msaidizi wa Magereza, (ACP), Hassan Bakari Mkwiche, (kushoto), akionyesha kitu, wakati Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, (wakwanza kulia), alipotembelea kiwanda hicho ili kuona eneo lililotengwa kwa ujenzi wa kiwanda kipya cha kisasa cha viatu, Oktoba 9, 2016. Wengine pichani ni Mkurugenzi wa Uwekezaji wa PPF, Steven Alfred, (wapili kushoto), Mkuu wa magereza mkoani Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi wa Polisi, (ACP), Anderson Kamtera.
 Bw. Erio, na maafisa wake, wakipatiwa maelezo na maafisa wa Jeshi la Magereza alipokagua moja ya maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda hicho


Naibu Kamishna wa Magereza, (DCP), Editha Malya, aliyemuwakilisha Mkuu wa Jeshi la Magereza Nchini, (CGP), akizungumza wakati wa kikao cha kupeana taarifa na ujumbe wa PPF ulioongozwa na Mkurugenzi Mkuu Erio Oktoba 9, 2016
 Bw. Erio, akizungumza wakati wa mkutano huo mfupi kabla ya kukagua maeneo hayo ya ujenzi
 Mkurugenzi wa Uwekezaji wa PPF, Steven Alfred, (katikati), akizungumza jambo wakati wa mkutano huo. Kulia ni Meneja Uhusiano wa Mfuko huo, Bi. Lulu Mengele, na kushoto ni Naibu Kamishna wa Magereza, Editha Malya
 Afisa magereza ambaye ni fundi viatu wa kiwanda cha viatu cha gereza la Karanga, akishona viatu
 Bw. Erio, akiongozwa na DCP Malya, na maafisa wengine akitembelea kiwanda
 Kaimu Mkuu wa Kiwanda cha kutengeneza viatu cha Karanga, Mrakibu Msaidizi wa Magereza, (ASP), Michael Minja, akitoa taarifa ya utendaji wa kiwanda
 Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bw. Erio, na Mkurugenzi wa Uwekezaji Bw. Alfred, wakiangalia viatu vilivyotengenezwa kiwandani hapo
 Bw. Erio(kushoto), akiangalia moja ya viatu vilivyotengenezwa kiwandani hapo
 Mkurugenzi wa Uwekezaji wa PPF, Bw. Steven Alfred, akionyeshwa namna kiatu kinavyotengenezwa, (katikati) ni mwakilishi mkuu wa ofisi ya PPF mkoani Kilimanjaro, Bw. Jacob Cornel Sulle
 Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bw. Erio, na Mkurugenzi wa Uwekezaji Bw. Alfred, wakiangalia viatu vilivyotengenezwa kiwandani hapo. Kushoto ni Mkuu wa Gereza la Karanga, Kamishna Msaidizi wa Magereza, (ACP), Hassan Bakari Mkwiche
 Mkuu wa kitengo cha umeme wa Kiwanda cha viatu Karanga, Staff Surgent, Aulelia Mushi, akziungumzia mahitaji ya umeme kiwandani hapo
 Maafisa wa wa Jeshi la Magereza, wakisikiliza mazungumzo hayo
 Picha ya Pamoja baada ya kutembelea kiwanda
 Ukaguzi wa moja ya maeneo ya ujenzi wa kiwanda
 Jiwe la msingi aliloweka Mwalimu Nyerere wakati wa ufunguzi wa kiwanda Juni 3, 1977
 Meneja Uhusiano wa PPF, Bi. Lulu Mengele, (watatu kushoto), akiangalia moja ya viatu vinavyotengenezwa kiwandani hapo, Kushoto ni Naibu Kamishna wa Magereza, Editha Malya, Mwakilishi Mkuu wa PPF, Mkoani Kilimanjaro, Jacob Cornel Sulle, Mkuu wa Magereza mkoani Kilimanjaro, (RPO), Kamishna Msaidizi wa Magereza, Anderson Kamtera, na maafisa wengine
Bw. Erio akisalimiana na Kamishna wa Magereza, DCP Editha Malya


NA K-VIS MEDIA, MOSHI
MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw.William Erio, ametembelea kiwanda cha kutengeneza viatu cha Karanga mjini Moshi mkoani Kilimanjaro Oktoba 9, 2016, ili kuona eneo ambalo kitajengwa kiwanda kipya na cha kisasa.

Bw. Erio ambaye alifuatana na Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Mfuko huo, Bw. Steven Alfred, na Meneja Uhusiano, Bi.Lulu Mengele, pia alipata fursa ya kupokea taarifa ya uendeshaji wa kiwanda cha sasa na gharama za awali za uboreshaji wa kiwanda hicho.
Bw. Erio alisema, ziara yake inalenga kujua mambo mawili ambayo ni namna bora na ya haraka ya kuboresha kiwanda cha sasa ili kuongeza uzalishaji wa kiwandacha sasa wakati kiwanda kipya  hicho.
 Pia ziara hiyo ililenga kuangalia eneo la ujenzi wa kiwanda kipya ambacho kitakuwa cha kisasa cha kuchakata ngozi na kutengeneza bidhaa zitokanazo na ngozi.
“Kama mtakumbuka, wiki iliyopita PPF na Jeshi la Magereza tulisaini mkataba wa makubaliano ya  kuboresha kiwanda cha sasa na kujenga kiwanda kipya cha kisasa cha kuchakata ngozi na kutengeneza bidhaa zitokanazo na ngozi.” Alianza kwa kusema.

Alisema, nia ya Mfuko ni kuona kazi ya ujenzi wa kiwanda kipya inakamilika na kuanza uzalishaji kabla ya mwisho wa mwaka 2018 ili kutekeleza azma ya serikali ya awamu ya tano ya kujenga uchumi wa viwanda.
Aliagiza wataalamu wa PPF kwa kushirikiana na wenzao wa Magereza (kiwanda cha Karanga), wakutane haraka ili kuainisha gharama zinazohitajika kuboresha kiwanda cha sasa ili kuongeza uzalishaji,  Alifafanua Mkurugenzi Mkuu Bw. Erio.
Awali Kaimu Mkuu wa kiwanda cha viatu Karanga, Naibu Mrakibu wa Magereza,( ASP), Michael Minja, alisema kiwanda cha sasa kinakabiliwa na changamoto mbalimbali, ikiwa ni pamoja na uchakavu wa mitambo, ambapo alisema baadhi ya mashine zimepitwa na wakati na zingine zimeharibika na hivyo zinahitaji kufanyiwa ukarabati.
“Mambo yanayotakiwa kufanyiwa kazi ili kuwezesha uendeshaji bora wa kiwanda, ni pamoja na kununua vipuri kwa ajili ya ukarabati wa baadhi ya mashine, lakini pia kuna upungufu wa baadhi ya mashine hivyo tunahitaji kuongeza idadi yake.” Alisema ASP Minja.
Akizungumza kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Magereza, Naibu Kamishna wa Magereza, (DCP), Editha Malya, alisema, Jeshi la Magereza limefurahishwa na hatua iliyochukuliwa na PPF katika kushirikiana katika uendeshaji wa kiwanda cha viatu Karanga ikiwa ni pamoja na ujenzi wa kiwanda kipya na cha kisasa.
“Tutashirikiana kwa karibu ili kuhakikisha azma yetu inatimia kwa haraka,” alisema DCP Malya.
Kiwanda cha viatu Karanga, kilichoko kwenye eneo la Gereza la Karanga mjini Moshi, kilizinduliwa na Rais wa awamu ya kwanza, Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, Juni 3,  1977 na wateja wakubwa wa bidhaa za kiwanda hicho ni taasisi za kijeshi, ikiwa ni pamoja na JWTZ, JKT, Magereza na Jeshi la Polisi.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE