October 12, 2016

WANAKIJIJI KIMALA KILOLO WALIA NA AHADI YA SERIKALI KUCHELEWA KUJENGA MNALA WA KUMBUKUMBU YA WANAFUNZI 9 WALIOKUFA KWA KIFUSI ....

Mbunge  wa  jimbo  la  Kilolo Venance  Mwamoto  akishuka  katika  ngazi  wakati  akikagua ujenzi  wa vyumba  viwili  vya madarasa  vinavyojengwa  kwa  ufadhili  wa kampuni ya  New Forest katika  shule ya  msingi  Kimala
Mbunge  wa  jimbo la  Kilolo Venance  Mwamoto akizungumza na wananchi  wa  Kimala  wakati wa  ziara  yake  ya  kuhamasisha shughuli  za  kimaendeleo jana

Mbunge  Mwamoto  katikati  akikabidhi  vifaa vya  michezo  kwa ajili ya  vijana wa Kimala
Mwamoto  akizungumza na wananchi wa  Kimala  kuwataka  kuendelea  na  ujenzi  wa shule  ya  sekondari  iliyosimama kwa  zaidi ya miaka  miwili   sasa
Mwamoto akimtambulisha  kijana Zakayo ambaye ni mtoto   wa aliyekuwa mbunge  wa kwanza wa  Kilolo Askofu Mwamasika
Kushoto  ni  mmoja kati ya  wagombea  udiwani kata ya Kimala  kupitia Chadema  akiungan na Mwamoto  katika  ziara yake  hiyo
Mbunge  Mwamoto  akionyesha choo  cha  kisasa alichowajengea  wanafunzi shule ya  msingi  Kimala
Mwamoto  akikagua  vyoo vya shule ya Msingi  Kimala

Mwamoto  akitoka  kukagua  jengo  la vyumba  viwili  vya madarasa  linalojengwa  na kampuni ya  New Forest shule ya  msingi  Kimala

Mbunge  Mwamoto  wa pili  kulia  akiongozwa na viongozi  wa kata ya  Kimala  kukagua  jengo la sekondari  ya  Kimala ambalo  limeanza kubomoka  kutokana na ujenzi  wake  kusimama kwa  miaka  zaidi ya  miwili  sasa

Wanafunzi  wa  shule ya Msingi  Kimala  wakimsikiliza  mbunge  wao  Venance  Mwamoto

Mbunge wa Jimbo La Kilolo Venance Mwamoto amejitolea kushughulikia kilio cha wananchi wa Kimala kuweka kumbukumbu eneo la makaburi la wanafunzi 9 wa shule ya msingi Kimala waliopoteza maisha mwaka 2002  kwa kufukiwa na kifusi.

Kwani  walisema  wakati  huo aliyekuwa  waziri  wa  elimu Joseph  Mungai ambaye  alifika  kwa niaba ya  serikali aliahidi kuweka  eneo ambalo  wanafunzi hao  walifukiwa na  kifusi  la  lile  la makaburi  yao mnala  wa  kumbukumbu pamoja na makaburi hayo  kuzungushiwa  uzio ila hadi  sasa ni  zaidi ya miaka  zaidi ya 13  imepita bila hata  utekelezaji .

 Hivyo  kumwomba  mbunge  wao  huyo  kuikumbusha  serikali  juu ya  utekelezaji  wa ahadi hiyo  kutokana na mazingira ya makaburi  hayo  kuanza kupoteza kumbukumbu hiyo wakisubiri  serikali  kutekeleza ahadi yake.

Kwa  upande  wake Mbunge Mwamoto  akifafanua  kilio  hicho cha  wananchi hao jana katika mkutano wake alisema alisema  atafikisha serikalini  japo  kwa upande wake ataanza kutekeleza sehemu ili  serikali  itakapofika  kumalizia kabisa

Alisema wakati tukio hilo lilitokea hakuwa mbunge ila alifika hivyo kabla ya kulifikisha serikalini bungeni suala hilo kwa upande wake atachagia mifuko 15 inayohitajika kwa ujenzi wa makaburi hayo ama kuweka uzio.

Katika hatua nyingine mbunge huyo alisema kuwa kuanzia wiki hii maeneo korofi ya barabara ya kimala pamoja na barabara hiyo itaanza kujengwa ili kuwezesha usafiri wa basi katika eneo hilo.

Huku akiwataka wananchi hao kuendelea kushiriki shughuli za kimaendeleo zikiwemo za ujenzi wa shule ya kata na kuwa ndani ya miaka yake mitano kata hiyo katika vijiji vyake vyote itakuwa na umeme

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE