October 17, 2016

MBUNGE MWAMOTO ATAKA WANANCHI KILOLO KUKATAA MIRADI ILIYOJENGWA CHINI YA KIWANGO.....

Mbunge  wa  jimbo la  Kilolo  Venance Mwamoto  akiingia kukagua  ujenzi wa  vyumba  viwili  vya madarasa  vinavyojengwa  shule ya msingi Kimala kwa  ufadhili wa  wadau  wa maendeleo kampuni ya  New Forest
Mbunge  wa  Kilolo Veanance  Mwamoto wa pili  kulia  akikagua  ujenzi  wa  vyumba  viwili  vya madarasa  vinavyojengwa  shule ya msingi Kimala kwa  ufadhili wa  wadau  wa maendeleo kampuni ya  New Forest 
Na MatukiodaimaBlog 
 
MBUNGE wa   jimbo la  Kilolo mkoani  Iringa Venance Mwamoto  amewataka   viongozi  wa kata ya  Kimala  kuwakataa madandarasi  wanaojenga  miradi  ya mbali mbali  ikiwemo ya  barabara  chini ya  kiwango .

Akizungumza na  wananchi hao  wakati wa mkutano wake wa  kukagua  miradi ya maendeleo  juzi  Mwamoto  aisema  kuwa  chanzo  cha miradi  mingi  kujengwa  chini ya  kiwango ni  kutokana na  wananchi  wanaozunguka  miradi hiyo  kuwafumbia macho  wajenzi wa miradi hiyo ambao  wanapewa kazi katika maeneo yao.

Hivyo  alisema ni  vizuri kabla ya  mradi  wowote  unaotumia   fedha za  serikali kuanza  ikiwemo ile ya ujenzi wa barabara  lazima  kwanza ajira  itolewe  kwa wananchi  wenye sifa  waliopo maeneo  husika pia kabla ya  mradi kuanza mkandarasi anapaswa  kutambulishwa kwa  wananchi  kupitia mkutano wa  hadhara  na pale atakapojenga  mradi  chini ya  kiwango mradi huo  usipokelewe .


" Hii  barabara  ya  Kimara  inaanza  kujengwa  hivyo kabla ya mkandarasi  kuanza  kazi lazima mhandisi  wa ujenzi  wa wilaya ya  Kilolo kufika katika makao makuu ya kata na mkandarasi   ili kumtambulisha kwa  wananchi kwanza na wananchi  washirikiane  pia kuonyesha maeneo korofi ili  kujengwa  vizuri "

Mbunge    huyo  aliwataka   wananchi hao wa  kimala  kuteua  wenzao watakaoongozana na mkandarasi  kumuonyesha maeneo korofi   ili  pindi kazi inapoanza  basi yafanyiwe  kazi vizuri .


Kuhusu  kusimama  kwa  ujenzi wa  shule ya  sekondari ya kata ya  Kimala ,Mwamoto  alisema  kuwa   wananchi wanapaswa    kuendelea  na  ujenzi  wa  shule  ya kata  hiyo  ujenzi ambao  ulisimama kwa zaidi ya mwaka mmoja  sasa  ili  kuwezesha  watoto kuwa na  shule ya  sekondari jirani  tofauti na  ilivyosasa  kwa  kata   hiyo  kutokuwa na shule   yake  na  kuwa wananchi  hawana sababu  ya  kususa  kuendelea na ujenzi  wa  shule   hiyo  kutokana na baadhi ya viongozi  kutafuna  fedha  za  michango yao na  kuagiza  afisa mtendaji  mpya wa  kata   hiyo  kuchukua  hatua kali kwa  waliohusika na utafunaji wa  fedha  za michango ya  wananchi.

Alisema   kwa  upande  wake  atakuwa tayari  kuwaunga mkono  wananchi hao  kwa  kuchangia bati ama saruji  pindi  watakapoanza ujenzi  huo japo kwa  sasa pamoja na  kuwataka  kujenga shule   hiyo bado anawataka  kuendelea na  ujenzi  wa  nyumba  bora  za kuishi kwa ramani elekezi zitakazotolewa bure  na atakayeanza  kujenga atamchangia bati 10.

Pia aliahidi kujitolea  ukarabati  wa ofisi ya  walimu  wa  shule ya Msingi Kimala ambayo sakafu  zake  zimechakaa kwa  kurudishia  sakafu   hiyo na  kuwaeleza  wananchi hao  kuwa suala la umeme jimbo lake maeneo mbali mbali yatapatiwa  umeme  vijijini vikiwemo  vijiji  vya kata   hiyo ya  Kimala


Wakati  huo  huo wananchi  wa  kijiji  cha Kimala kata ya  Kimala wilaya ya  Kilolo mkoani Iringa wamemtaka mbunge Mwamoto kuwasaidia kuikumbusha serikali juu ya utekelezaji  wa ahadi yake  ujenzi wa mnala  wa  kumbukumbu eneo la makaburi ya wanafunzi 9 wa shule ya msingi Kimala waliopoteza maisha mwaka 2002  kwa kufukiwa na kifusi.

Kwani  walisema  wakati  huo aliyekuwa  waziri  wa  elimu Joseph  Mungai ambaye  alifika  kwa niaba ya  serikali aliahidi kuweka  eneo ambalo  wanafunzi hao  walifukiwa na  kifusi  la  lile  la makaburi  yao mnala  wa  kumbukumbu pamoja na makaburi hayo  kuzungushiwa  uzio ila hadi  sasa ni  zaidi ya miaka  zaidi ya 13  imepita bila hata  utekelezaji .

 Hivyo  kumwomba  mbunge  wao  huyo  kuikumbusha  serikali  juu ya  utekelezaji  wa ahadi hiyo  kutokana na mazingira ya makaburi  hayo  kuanza kupoteza kumbukumbu hiyo wakisubiri  serikali  kutekeleza ahadi yake.

Kwa  upande  wake Mbunge Mwamoto  akifafanua  kilio  hicho cha  wananchi hao jana katika mkutano wake alisema alisema  atafikisha serikalini  japo  kwa upande wake ataanza kutekeleza sehemu ili  serikali  itakapofika  kumalizia kabisa

Alisema wakati tukio hilo lilitokea hakuwa mbunge ila alifika hivyo kabla ya kulifikisha serikalini bungeni suala hilo kwa upande wake atachagia mifuko 15 inayohitajika kwa ujenzi wa makaburi hayo ama kuweka uzio.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE