October 28, 2016

DC KILOLO AWAONYA VIJANA WANAOJIFUNZA MAFUNZO YA MGAMBO KUWA WAADILIFU ......

Vijana  wa Kilolo  wakiwa katika mafunzo ya Mgambo  kwenye kijiji  cha Isuka
Mkuu wa  wilaya ya  Kilolo Asia Abdalah kushoto  akizungumza na  vijana  wanaofundishwa mafunzo ya  Mgambo 
MKUU  wa  wilaya ya  Kilolo  mkoani Iringa Asia abdalah  amewataka  vijana  wanaojifunza mafunzo ya  mgambo katika  wilaya ya  Kilolo  kuyatumia mafunzo hayo  kwa  ajili ya kujiongezea  kipato halali  badala ya  kujiingiza katika vitendo vya uharifu.

Akizungumza jana  wakati  akitoa msaada wa sare kwa  vijana  na  vijana   zaidi ya  50  waliopo katika mafunzo ya mgambo kijiji  cha Isuka   ,mkuu   huyo wa  wilaya  alisema mafunzo hayo  yanafaida kubwa kwa   vijana hao  iwapo  watayatumia vizuri  kwa  kufanya kazi halali .

Kwani  alisema  kwa  upande wake pindi  wanapohitimu mafunzo hayo anawaunganisha   vijana  hao na makampuni ya  ulinzi  ili  kupata ajira kwenye makampuni  mbali mbali  yaliyopo wilayani Kilolo na ndani ya  mkoa  wa Iringa ila  watakaopata  nafasi hiyo  ni  wale  waadilifu .

"Ni  matumaini  yangu pindi  mtakapohitimu mafunzo haya mtakuwa vijana  waadilifu ambao  mtafanya kazi za ulinzi na usalama katika maeneo  yenu  kama  njia ya  kuimarisha  ulinzi na  kuzisaidia  jamii mnazozizunguka .....sitegemei  kuona kati  yenu hapa  mnajiingiza katika matukio ya uharifu "alisema  mkuu  huyo wa  wilaya 

Kuwa  amefurahishwa na  witikio mkubwa ambao  unaonyeshwa na  vijana  wa  wilaya  ya  Kilolo  kujiunga na mafunzo  hayo ya  mgambo  na  kuwa  iwapo  vijana  hao  watafanya kazi kwa uaminifu  na umakini mkubwa  upo uwezekano wa  vijana hao  kupata  ajira katika maeneo  mbali mbali.


Katika  hatua  nyingine  mkuu  huyo wa  wilaya amekabidhi  vyeti  maalum kwa  wanafunzi  zaidi ya 10  na wananchi  wanaozunguka  shule ya  sekondari  lutangiri ambao  walishiriki  kutafuta  mwili wa Mwanafunzi Frank  Kastiko aliyekuwa akisoma  kidato  cha  pili  aliyekufa maji  wakati  akioga mtoni.


Akikabidhi  vyeti  hivyo  alisema  kuwa   uzalendo  ulioonyeshwa na wananchi hao  pamoja na wanafunzi katika  kutafuta  mwili wa  mwanafunzi  huyo ni uzalendo  wa  kipekee ambao  unapaswa  kuendelezwa na  wananchi wote wa  wilaya ya  Kilolo.

Mkuu   huyo  alisema kazi  kubwa  iliyofanywa na  wadau hao katika  kujitolea kutafuta  mwili wa mwanafunzi  huyo inapaswa  kupongezwa na kwa  upande wake amelazimika  kuwatunuku vyeti maalum wanafunzi hao  na wote  walioshiriki  kama heshima na  kumbukumbu kwao .

Hata  hivyo  alisema  mbali ya  ofisi yake  kuwatambua  wazalendo hao kw  mchango wao pia ofisi ya  mkuu wa  mkoa wa Iringa imeungana kupongeza kazi hiyo  kubwa na  kuwataka  wananchi  kuendelea  kujitolea  kwa ajili ya maendeleo ya  Kilolo.

MWISHO

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE