October 15, 2016

CHANJO YA MINYOO NA KICHOCHO YAZINDULIWA MKOANI IRINGAMkuu  wa  wilaya ya  Iringa  Richard  Kasesela  akizungumza na  watoto  waliokuwa katika  chanjo (

 
Na Dajari Mgidange MatukiodaimaBlog


Minyoo na Kichocho ni magonjwa yanayowaandama  watoto wadogo kipindi cha wakati mvua zikiendelea kunyesha. Miezi ya karibuni msimu wa mvua unakaribia kuanza na manispaa ya Iringa imejipanga kuhakikisha wanagawa chanjo hiyo ili kuweka ulinzi kwa watoto kwani ndio waathirika wakubwa wa magonjwa haya.

Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela alifika shule ya UMMUSSALAMA kutekeleza na kuhakikisha azma hiyo ya utoaji chanjo kwa watoto unafanyika kama ulivyopangwa. Zoezi hili litadumu kwa muda wa wiki 2 kwa kuhakikisha watoto wote waliopo mashuleni anapewa chanjo hiyo.

“Zoezi zima limekwenda vizuri mimi ni mwenyekiti wa zoezi hili la Afya Wilaya, nimefurahishwa sana na shule hii ya ummusalama kwa kuweza kuandaa chakula kizuri kwa hawa watoto kwani hawatakiwi kumeza dawa hizo bila ya kula”, Alisema Kasesela. Pia alisema kua manispaa wamegawana uongozi kwa maana ya kwenda kufanya uzinduzi kwenye maeneo baadhi ya manispaa ya Iringa mheshimiwa Mayor amekwenda Igumbilo na Msigwa mbunge wa jimbo la Iringa amekwenda Njia Panda ya Tosa.

Kasesela amewaomba wazazi wasiwazuie watoto wao kupewa chanjo kwani ni muhimu sana kwa watoto hao kupata chanjo hiyo ya Minyoo na Kichocho. Wakati akizindua Chanjo eneo hilo la shule kuna baadhi ya wanafunzi walisema kua wamezuiliwa na wazazi wao kupokea chanjo hiyo lakini Mkuu akaweza kuongea na Wazazi hao waliofika eneo hilo kutilia shaka Chanjo hiyo kuwatoa hofu wananchi hao na kuwaahidi kama watapata madhara yoyote wawasiliane na mkuu huyo na atabeba dhamana hiyo.

Mwalimu AMOS ni Mkuu wa shule hiyo ya UMMUSSALAMA  amesema kua amelipokea vizuri sana kwa upande wake na alilifikisha swala hilo kwa wazazi wa wanafunzi hao lakini akasema shida iliyopo ni kwamba wazazi walikua na pingamizi kuhusiana na chanjo hiyo na amemshukuru mkuu wa Wilaya Richard Kasesela kufika eneo hilo na kuweza kuwaelimisha baadhi ya wazazi waliofika katika shule hiyo kushuhudia nini ambacho kilikua kinaendeleaa.

Deodata Lukupwa ni mratibu wa magonjwa yasiyokua yanapewa kipaumbele mojawapo ikiwa ni hilo la kichocho na amesema wamekua wakiendesha zoezi hilo salama kwa kua wamekua wakihakikisha kua watoto wote wamaekula na ndipo wanapatiwa chanjo hiyo.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE