Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

October 30, 2016

RC -PAUL MAKONDA AONGOZA MAHAFALI YA KIDATO CHA NNE SHULE YA SEKONDARY JITEGEMEE JKT MGULANI JIJINI DAR ES SALAAM

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (katikati), akizungumza na wanafunzi wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari ya Jitegemee JKT Mgulani katika mahafali ya 32 yaliyofanyika jana. Makonda alikuwa mgeni rasmi. Kulia ni Mkuu wa Shule hiyo, Luteni Kanali Robert Kessy na kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi wa Shule hiyo, Brigedia Generali Laurance Magere.
RC Makonda akimkabidhi cheti Mwalimu Bora wa Shule hiyo, Grace Eliyatosha Moshi.
RC Makonda akimkabidhi zawadi Mwanafunzi Bora,  Samuel Ndebeto.
RC Makonda akipeana mkono na mhitimu wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari ya Jitegemee JKT, Samina Rajab baada ya kumkabidhi cheti  katika mahafali ya 32 kwa ushiriki wake wa masuala ya Skauti shuleni hapo. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi wa Shule hiyo, Brigedia Generali Laurance Magere.
Huyu ndiye ni Mwanafunzi Bora wa Shule hiyo,  Samuel Ndebeto.
Mkuu wa Mkoa Paul Makonda (katikati), akiwa meza kuu na viongozi mbalimbali. Kutoka kulia ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Kigamboni, Luteni Kanali, Laurent Mgongolwa, Mkurugenzi wa Mipango ya Huduma Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Luteni Kanali Festus Mang'wela, Mkuu wa Shule ya Sekondari Jitegemee, Luteni Kanali, Robert Kessy, Mwenyekiti wa Bodi wa shule hiyo, Brigedia Generali mstaafu, Laurence Magere, Mwakilishi wa Katibu Tawala wa Wilaya ya Temeke, Hashim Komba na Mjumbe wa Bodi wa Shule hiyo, Sebastian Enosh.
Mgeni rasm Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na walimu na wafanyakazi wa shule hiyo.
Wahitimu wakiwa kwenye mahafali hayo.
Mhitimu wa kidato cha nne akisakata rhumba kwenye mahafali hayo.
Walimu na wanafunzi wakicheza kwaito.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Jitegemee JKT wakitoa burudani kwenye mahafali hayo.
Wahitimu ndani ya ukumbi.
Mgeni rasmi Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali waliokuwa jukwaa kuu.
RC Makonda akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu hao.
RC Makonda akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu hao.
Vijana wa Skauti wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi.
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na Kwaya ya shule hiyo.

Na Dotto Mwaibale

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewataka wazazi na walezi kuwaacha huru watoto wao kuendelea na masomo wayapendayo badala ya kuwachagulia.

Mwito huo ameutoa katika mahafali ya 32 ya kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Jitegemee JKT Mgulani Dar es Salaam jana ambapo alikuwa mgeni rasmi.

"Watoto wapewe uhuru wa kile wanachopenda kukisomea badala ya kuwachagulia kwa kufanya hivyo itawasaidia kupenda kazi watakayoifanya kutokana na masomo waliyosoma" alisema Makonda.

Alisema hivi sasa kuna changamoto kubwa kwa watumishi kujiingiza katika vitendo vya ubadhirifu kutokana na kutokuwa wazalendo kutokana na kufanya kazi ambayo imetokana na masomo ambayo hawakuyapenda.

Alisema kama mtoto anapenda kuwa mtaalamu wa kompyuta muache aendelee na masomo ya kompyuta badala ya kumlazimisha kuwa na taaluma nyingine.

Mkuu wa Shule hiyo, Luteni Kanali Robert Kessy alisema wahitimu hao wameandaliwa vizuri kwa ajili ya kufanya mtihani wao watakao uanza Jumanne wiki ijayo na kuwa wanategemea wote watafanya vizuri.

Kessy alisema kuhitimu kidato cha nne ni hatua nyingine ya kuendelea na elimu ya juu hivyo aliwataka wahitimu hao kuondoa wasiwasi katika kipindi hiki cha kuelekea kufanya mtihani wa mwisho.

Wakisoma risala yao kwa mgeni rasmi Paul Makonda wanafunzi hao walisema changaoto kubwa waliyonayo na uchakavu wa miundombinu shuleni hapo kama mapaa ya vyumba vya madarasa kuezekwa kwa mabati aina ya Asbestors ambayo si mazuri kiafya pamoja na uchakavu wa sakafu ambapo Makonda aliahidi kutoa mabati 2,000 kwa ajili ya kuezekea vyumba 25.

Katika hatua nyingine Makonda amezitaka shule za sekondari za jeshi katika mkoa wa Dar es Salaam kuhakikisha zinaunda kamati kwa ajili ya kurudisha heshima ya michezo mashuleni kama ilivyokuwa awali.


EDMARK INTERNATIONAL WAPO MKOANI IRINGA WANATIBU KWA MIMEA LISHE .....

Huna   sababu ya  kusumbuliwa na magonjwa  sasa fika  Edemark Intar ational  upate  matibabu  kwa kutumia dawa  lishe zinazotengenezwa kwa  mimea na matunda  tupo  jirani na  wihanzi  Guest Makorongoni mjini Iringa au  piga  simu  0755 920 740 /0656749512

October 29, 2016

UBALOZI WA MAREKANI NCHINI KENYA WAFUNGWA

Mwanamume huyo aliuawa kwa kupigwa risasi kichwaniMwanamume huyo aliuawa kwa kupigwa risasi kichwani 
 
Ubalozi wa Marekani nchini Kenya umefungwa kwa muda leo Ijumaa kufuatia kisa ambapo mwanamume aliyekuwa na kisu alijaribu kumshambulia afisa wa usalama karibu na ubalozi huo Alhamisi.
Mwanamume huyo aliuawa kwa kupigwa risasi.

Hakuna afisa yeyote wa ubalozi huo aliyeathiriwa na kisa hicho.

"Ubalozi utafungwa Oktoba 28. Huduma zote za kibalozi zimesitishwa, lakini huduma za kibalozi za dharura kwa raia wa Marekani zitaendelea kutolewa," taarifa kwenye tovuti ya ubalozi huo imesema.

Maafisa wa ubalozi huo wametoa wito kwa raia na wafanyakazi wake kuwa makini kuhusu usalama wao.
Polisi nchini Kenya wanachunguza kubaini iwapo mwanamume huyo aliyepigwa risasi alikuwa na washirika, afisa mmoja mkuu wa polisi Vitalis Otieno aliambia shirika la habari la AFP.

Bw Otieno alisema mwanamume huyo alimdunga kisu afisa mmoja wa polisi lakini akapigwa risasi na kichwani na kuuawa na afisa aliyekuwa karibu.

Maafisa watano wa idara ya uchunguzi wa jinai ya Marekani (FBI) walifika eneo la tukio muda mfupi baadaye pamoja na polisi wa Kenya kufanya uchunguzi.

Msemaji wa polisi Kenya George Kinoti alisema mwanamume huyo wa miaka 24 alikuwa "mhalifu wa kuendesha shughuli zake kivyake", kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters.
Hata hivyo, alisema uchunguzi unaendelea.

KIKWETE , NAOMBA NIACHWE NIPUMZIKE

Rais Mstaafu Jakaya KikweteRais mstaafu wa Tanzania Jakaya Kikwete amelalamika kutokana na kile alichosema ni kutumiwa vibaya kwa picha zake mtandaoni na 'kulishwa maneno'.

Takriban mwaka mmoja tangu astaafu, Bw Kikwete, rais wa awamu ya nne, amesema anafaa kuruhusiwa apumzike.

Aidha, amesema anamuunga mkono Rais wa sasa Dkt John Pombe Magufuli, pamoja na serikali yake.
"Nimestaafu naomba niachwe nipumzike. Nisingependwa kuhusishwa na siasa za mtandaoni dhidi ya Serikali. Namuunga mkono Rais na Serikali yake," ameandika kwenye Twitter.

"Nasikitishwa sana na matumizi mabaya ya picha zangu mtandaoni hususan watu kunilisha maneno kwa kutaka kutimiza malengo yao ya kisiasa."
Bw Kikwete aliondoka madarakani mwishoni mwa mwaka jana baada ya kuongoza taifa hilo kwa miaka kumi.

Tangu aondoke madarakani, ameonekana kujiepusha na masuala ya kisiasa.
Ni nadra sana kwa rais mstaafu Jakaya Kikwete kujibu shutuma ambazo zinahusanishwa naye.

Hivi karibuni watu wamekuwa wakitumia sehemu ya hotuba anazozitoa kumhusisha na ukosoaji wa serikali utendaji kazi wa serikali ya Rais Magufuli.
Bw Kikwete na mrithi wake Dkt MagufuliBw Kikwete na mrithi wake Dkt Magufuli
Siku chache zilizopita Kikwete alikuwa anahutubia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na katika hotuba yake alitamka haya: "Unapokuwa mpya watu wanataka mambo mapya pia, lakini yawe mapya ya maendeleo na siyo (mapya) ya kuharibu kule tulikotoka." Sasa watumiaji wa mitandao ya kijamii wamekuwa wakiitumia nukuu hii kuashiria Bw Kikwete alikuwa akiukosoa utawala wa Rais Magufuli

KILELE CHA IKUNGI HALF MARATHON 2016 CHARINDIMA WILAYANI IKUNGI MKOANI SINGIDA


Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe akishiriki kutazama washiriki wa Ikungi Half Marathon 2016 walivyoanza mbio hizo katika Kijiji Cha Kimbwi Kuelekea Uwanja wa Shule Ya Sekondari Ikungi pembeni yake ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu na Hassan Tati Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ikungi
Wananchi wakifatilia kwa makini Ikungi Half Marathon katika maeneo yao vijiji vyao


Washiriki wa Ikungi Half Marathon wakianza kukimbia Riadha katika Kijiji cha KimbwiMkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe, Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu na viongozi wa ngazi ya Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Ikungi wakitazama namna wakimbiaji wanavyowasili katika uwanja wa shule Ya Sekondari Ikungi