Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

September 29, 2016

Askari ajiua Iringa

Askari polisi mjini Mafinga wilaya ya Mufindi ajiua kwa kujipiga risasi

Tukio limetokea jana chanzo bado hakijafahamika habari kamili itakujia pynde

September 28, 2016

MISA TANZANIA YAADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA HAKI YA KUPATA TAARIFA MWAKA 2016 KWA KUZINDUA CHAPISHO NA KUTOA

Afisa Habari na Utafiti wa MISA-Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa akizungumzia vigezo vilivyotumika kuchagua taasisi zilizofanyiwa utafiti mwaka huu, Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA-TAN) katika katika Siku ya Kimataifa ya Haki ya Kupata Taarifa ambayo huadhimishwa kila mwaka Septemba 28.

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wameibuka washindi wa TUZO ya UFUNGUO WA DHAHABU kwa kuwa taasisi inayofunguka zaidi kwa wananchi hapa Tanzania kwa mwaka 2016. Hafla ya utoaji tuzo hizo imefanyika katika hoteli yaa Sea Shells hapa Dar es Salaam.
Katika tuzo hizo Wizara ya Sheria na Katiba imeambulia Kufuli la Dhahabu kwa kuwa taasisi ngumu kwa upatikanaji wa taarifa kwa Umma.
MISA Tanzania pia walizindua Ripoti ya kila mwaka ya Upatikanaji Taarifa katika Taasisi za Umma kwa mwaka 2016.
Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania,Bw. Roeland Van De Geer akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa (hawapo pichani) kwenye siku ya Kimataifa ya Haki ya Kupata Taarifa zinazoadhmishwa Septemba 28 kwa kila mwaka. Hapa ni ukumbi wa Hoteli ya Sea Shells iliyopo jijini Dar es Salaam

Afisa Habari kutoka UNESCO, Christopher Regay akichangia mada

September 27, 2016

WAFANYAKAZI WA AIRTEL WASHEREHEKEA SIKU YA WANAFAMILIA WET N WILD KUNDUCHI.

 Mmoja wa watoto wa  wafanyakazi wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel, Beatrice Moses akifurahia mchezo wa kuraka ndani ya bwawa la kuogelea katika bonanza la siku ya wanafamilia wa Airtel jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. 
Afisa Rasilimali wa watu, Mubaraka Kibarabara wa Kampuni ya Simu za Mkononi YA Airtel (kulia), akimpa zawadi Beatrice Nalingigwa baada ya kuibukas kidedea katika shidano la kuogelea katika  shamrashamra za siku ya wanafamilia wa Airtel jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Baadhi ya watoto wa wafanyakazi wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel,Warren Kanga (kushoto) na Umilkheri Matata wakichuana wakifanya vitu vyao katika shindano la kucheza muziki ikiwa ni sehemu ya burudani kusherehekea siku ya wanafamilia wa Airtel jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Watoto wa wafanyakazi wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel, wakifurahia ndani ya bwawa la kuogelea katika  shamrashamra za siku ya wanafamilia wa Airtel jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
  Baadhi ya wafanyakazi na familia zao wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel wakichukua chakula kwa pamoja kuonyesha upendo na mshikamano wao ambao ni sehemu ya mafanikio ya kampuni hiyo wakati wa hafla ya Siku ya Wanafamilia wa kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana.
 Mwanafamilia wa Airtel akiwapa chakula watoto ikiwa ni ishara ya upendo ulio ndani ya wafanyakazi wa kampuni hiyo wakati wa hafla ya Siku ya Wanafamilia wa kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana.

Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel Tanzania yasherehekea siku ya wanafamilia mwishoni mwa wiki hii Kunduchi Wet n Wild .

Ni muda muafaka kwa familia mbali mbali kuwezakujuana na  kujumuika kwa pamoja na kuweza kubadilishana mawazo na hata kufurahia mafanikia ya matunda waliyoyapata kwa mwa huu.

 Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Airtel Tanzania, Patrick Foya alisema ni desturi yao kuwa na siku maalumu kila mwaka ya kuwakutanisha wafanyakazi wao na familia zao ili pamoja na kushiriki michezo na mambo mengine ya kuburudisha nyoyo zao zao lakini pia huitumia siku hiyo kuzidi kuimarisha mshikamano miongoni mwao. "Umoja na mshikamano ni nyenzo muhimu mahali pa kazi, lakini pia ukiwa na mfanyakazi anayetoka katika familia iliyokosa utulivu, lakini pia mfanyakazi legelege hawezi kufanya kazi zake kwa ufanisi," akaongeza Bwana Foya.

Zaidi ya wafanyakazi na wanafamilia  600 walishiriki katika bonanza hilo na kushiriki michezo mbalimbali kama vile kucheza muziki, kuvutaka kamba, soka la baharini, wavu na kuogelea.  Baadhi ya watoto wa wafanyakazi wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania wakishindana.

Rais magufuli kuzindua ndege mbili za ATC kesho

 
Na Lilian Lundo-MAELEZO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli anatarajiwa kuzindua ndege mbili za Shirika la Ndege la Tanzania (ATC) zilizonunuliwa kwa kutumia kodi za wananchi.

Uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika kesho Septemba, 28 mwaka huu katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Terminal 1).

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu (Uchukuzi), Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. Leonard Chamuriho leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa ndege hizo.

Dkt. Chamuriho alisema kuwa ndege ya kwanza iliwasili nchini tarehe 20/09/2016 na ndege ya pili inatarajiwa kuwasili nchini leo tarehe 27/09/2016 kuanzia saa 6:00 mchana.

Vile vile Katibu Mkuu huyo alisema kuwa ndege hizo zimenunuliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuhudumia wananchi wa ndani ya nchiya Tanzania na nchi jirani.

“Ndege hizo aina ya Dash 8 Q400 zimetengenezwa na kiwanda cha Bombadier nchini Canada ambapo kila moja ina uwezo wa kubeba abiria 76 na zitatumika katika kuhudumia soko la ndaniya Tanzania na nchi jirani,” alifafanua Dkt. Chamuriho.

Aidha, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inawakaribisha wananchi wote kushuhudia uzinduzi wa ndege hizo unaotarajiwa kuanza saa mbili kamili (2:00) asubuhi.

UWT watoa saruji mifuko 200 kwa wahanga wa tetemeko Kagera


Mkuuwa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu akipokea moja ya mfuko wa saruji kutoka kwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania UWT-CCM) Sophia Simba ukiwa ni miongoni mwa mifuko 200 sa saruji iliyotolewa na UWT kusaidia maafa Kagera.
Baadhi ya wanawake wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT-CCM) wakipakia mifuko ya saruji kwenye gari tayari kwa kupelekwa kwenye ghala la kukusanyia misaada inayyotolewa ili kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi.

………………………………………………………………..

Na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Bukoba.

Mkoa wa Kagera bado unaendelea kupokea misaada kutoka taasisi, mashirika ya dini, mashirika binafsi, vyama vya siasa pamoja na nchi mbalimbali ili kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi lililoathiri maeneo mbalimbali ya mkoa.

Katika kuhakikisha wakazi wa mkoa huo walioathiriwa na tetemeko la ardhi, wadau nchini wanendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma za kijamii ikiwemo vifaa vya ujenzi, vyakula pamoja na vifaa tiba.

Akikabidhi msaada wa mifuko 200 ya saruji iliyotolewa na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT-CCM) Katibu wa umoja huo Amina Makiragi amesema kuwa mchango ni chachu inayolenga kupaza sauti ili kuhamasisha wananchi na wadau wengine kuendelea kutoa misaada yenye lengo la kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.

Katibu huyo wa UWT-CCM ameipongeza Serikali kwa hatua walizochukua katika kutatua la tetemeko la ardhi kwa umahiri mkubwa na kuanza kuchukua hatua za kurejesha miundombinu mbalimbali ya kutolea huduma za kijamii ikiwemo shule, vituo vya afya na barabara.

Aidha, Mwenyekiti wa taifa wa chama hicho Sophia Simba amesisitiza kuwa katika maafa yeyote, wanawake na watoto mara kwa mara ndio wamekuwa waathirika wakubwa wa majanga yanayoikumba jamii.

Ili kuhakikisha misaada inayotolewa na wadau mbalimbali nchini, Mwenyekiti Sophia ametoa wito kwa Kamati ya maafa kusimamia misaada hiyo ipasavyo na kuigawa kwa wakati kwa walengwa hasa wahitaji ambao wameathiriwa na tetemeko hilo na kuongeza kuwa ni fahari kuona ghala lipo wazi baada ya misaada iliyokusanywa kupelekwa kwa wahusika.

Akipokea msaada huo Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu ametoa shukrani kwa UWT kwa moyo wa kuwajali waathirika wa maafa yaliyotokana na tetemeko la ardhi mkoani humo. Aidha, Mkuu huyo wa mkoa amewaasa wadau wengine kuendelea kutoa misaada na michango yao na kuwahakikishia kuwa misaada hiyo itatumika kulingana na malengo yaliyokusudiwa

Burundi yawafuta machozi Wanakagera kwa tani 183 za vyakula.


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba (kushoto) akikabidhiwa msaada na Waziri wa Afrika Mashariki Bi. Leontine kutoka Serikali ya Jamhuri ya Burundi kwa lengo la kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba (kushoto) akiongea na wajumbe kutoka Burundi na Tanzania wakati wa kukabidhi msaada kutoka nchini Burundi kwa lengo la kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Ujumbe wa Burundi uliongozwa na Waziri wa Afrika Mashariki Bi. Leontine Nzeyimana (kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu kushoto (kushoto).
Waziri wa Afrika Mashariki kutoka Serikali ya Jamhuri ya Burundi Bi. Leontine Nzeyimana akiongea na wajumbe kutoka Tanzania na Burundi wakati wa kukabidhi msaada kwa lengo la kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Kushoto ni Waziri wa Afrika Mashariki Bi. Leontine Nzeyimana na wa kwanza kulia Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu kushoto.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu akiwakaribisha wajumbe kutoka Burundi na Tanzania wakati wa mkutano kabla ya kukabidhi msaada kwa lengo la kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Wa kwanza kulia ni Waziri wa Afrika Mashariki kutoka Serikali ya Jamhuri ya Burundi Bi. Leontine Nzeyimana na katikati ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba.
Waziri wa Afrika Mashariki kutoka Serikali ya Jamhuri ya Burundi Bi. Leontine Nzeyimana (katikati) akifafanua jambo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba (kushoto) mara baada ya kukabidhi ya kukabidhi msaada kutoka nchini Burundi kwa lengo la kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Kulia ni Mkurugenzi Idara ya Kuratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brigedia Jenerali Mbazi Msuya.
Waziri wa Afrika Mashariki kutoka Serikali ya Jamhuri ya Burundi Bi. Leontine Nzeyimana (kushoto) akifafanua jambo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba (kulia) mara baada ya kukabidhi ya kukabidhi msaada kutoka nchini Burundi kwa lengo la kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu kushoto (kushoto) akitoa maelezo kwa Waziri wa Afrika Mashariki kutoka Serikali ya Jamhuri ya Burundi Bi. Leontine Nzeyimana (wa kwanza kulia) Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania Dkt. Suzan Kolimba (wa pili kulia)
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania Dkt. Suzan Kolimba akimaribisha Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchi hiyo Bw. Pascal Barandagiye mara baada ya kuwasili mpakani mwa Tanzania na Burundi katika eneo la Kabanga wilayani Ngara.
Viongozi kutoka Serikali za Tanzania na Burundi wakiwa katika picha ya pamoja na madereva wa malori yatakayosafirisha shehena ya vyakula vya msaada vilivyotolewa na serikali ya Burundi ili kusaidia waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Wa nne kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania Dkt. Suzan Kolimba na Waziri wa Afrika Mashariki kutoka Serikali ya Jamhuri ya Burundi Bi. Leontine Nzeyimana (wa tano kutoka kushoto).
Viongozi kutoka Serikali za Tanzania na Burundi wakielekea kwenye eneo yaliposimama malori yaliyobeba shehena ya vyakula vya msaada vilvyotolewa na serikali ya Burundi ili kusaidia waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.

(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO, Ngara, Kagera)

…………………………………………………………

Na Eleuteri Mangi-MAELEZO, Ngara, Kagera.

Serikali ya Tanzania imepokea msaada wa tani 183 za vyakula mbalimbali kutoka Serikali ya Burundi kwa ajili ya kuwafuta machozi waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea mkoni Kagera mapema mwezi huu na kuathiri maisha ya wakazi wa mkoa huo.

Makabidhiano ya msaada wa vyakula hivyo kutoka nchini Burundi yamefanyika mpakani mwa Tanzania na Burundi katika eneo la Kituo cha Ushuru cha Pamoja (OSBP) cha Kabanga wilayani Ngara ambapo Serikali ya Tanzania iliwakilishwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu wakati Burundi iliwakilishwa na Waziri wa Afrika Mashariki Bi. Leontine Nzeyimana na Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchi hiyo Bw. Pascal Barandagiye.

Akikabidhi vyakula hivyo, Waziri Bi. Leontine amesema kuwa Serikali ya Burundi na Warundi wote walipatwa na mshtuko mkubwa na majonzi baada kusikia taarifa ya maafa yaliyowatokea ndugu zao wa mkoani Kagera.

“Kwa Kirundi tunasema, “Umubanyi niwe muryango” ikimaanisha jirani yako ni ndugu yako, kwa maana hiyo imekuwa ni wajibu kwa Serikali ya Burundi kuagiza wawakilishi wake ili waweze kufika hapa nchini Tanzania mkoani Kagera kuwaona ndugu zetu Watanzania na kuwapa pole”.

Waziri Bi. Leontine aliendelea kusema “Ndio maana tumekuja na kifurushi kidogo tu ili tuweze kuwaliwaza ndugu zetu waliofikwa na matatizo hayo” alisema Waziri Bi. Leontine

Waziri Bi. Leontine alivitaja vyakula hivyo kuwa ni pamoja na mchele tani 100, mahindi tani 50, sukari tani 30 na majani ya chai tani 03.

Akizungumzia suala la mahusiano ya Tanzania na Burundi, Waziri Bi. Leontine amesema kuwa udugu uliojengeka baina ya nchi hizo mbili na wananchi wake ni wa kihistoria, si wa leo au wa jana na kusema Serikali yake inadhamira ya kuendeleza udugu huo vizazi na vizazi huku akiamini Tanzania nayo ina dhamira hiyo hiyo.

Akitoa shukrani baada ya kupokea msaada huo, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba ameishukuru Serikali ya Burundi kwa msaada waliotoa kwa Tanzania na kuongeza kuwa msaada waliotoa ni kielelezo cha mahusiano ya karibu na ya kidugu baina ya nchi hizo mbili na watu wake.

Pia Naibu Waziri Dkt. Suzan amewataka viongozi wa Serikali ya Burundi wafikishe salamu na shukrani za dhati za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa Rais wa Jamhuri ya Burundi Pierre Nkurunzinza na kuwathibitishia kuwa Tanzania itaendeleza uhusiano mzuri uliopo baina ya nchi hizo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kagera ambao ndio umeathirika na tetemeko hilo Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu ambaye pia ni Mkuu wa Ulinzi na Usalama wa mkoa huo ameihakikishia Serikali ya Burundi kuwa msaada walioutoa utawafikia walengwa kama ilivyokusudiwa.

Msaada huo uliotolewa na Burundi umekuwa ni mwendelezo wa misaada inayotolewa na nchi za Afrika Mashariki kwa Tanzania kufuatia tetemeko la ardhi lililotokea Septemba 10 mwaka huu na kuathiri mikoa ya kanda ya ziwa.

Burundi imeungana na nchi za Uganda na Kenya kwa kutoa misaada kwa waathirika wa tetemeko hilo ambapo September 17 mwaka huu Rais Dkt. John Pombe Magufuli alipokea mchango wa fedha taslimu kiasi cha Dola za Kimarekani laki 2 ambazo ni sawa na takribani Shilingi za Kitanzania milioni 437 kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Kaguta Museveni na mchango wa mabati, blanketi na magodoro vyenye thamani ya Shilingi za Kitanzania milioni 115 kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Kenya Uhuru Kenyatta kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi Mkoani Kagera.