Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

August 31, 2016

MATUKIO YA KUPATWA KWA JUA.

Kupatwa kwa jua kunatokea kama dunia, mwezi na jua zinakaa kwenye mstari mmoja mnyoofu yaani wakati mwezi unapita kati ya dunia na jua. Katika hali hiyo kuna kivuli cha mwezi kwenye uso wa dunia. Kivuli hiki hakifuniki dunia yote. Kwa hiyo kupatwa kwa jua kunaonekana kwa watu wengi kama kupungua kwa mwanga wa jua.
Kuna aina mbalimbali za kupatwa kwa jua.
  • kupatwa kabisa: jua lapotea kabisa kwa dakika chache. Hali hii yaonekana kwenye kanda nyembamba duniani kinapopita kitovu cha kivuli.
  •  
  • kupatwa kipete: mwezi huonekana mdogo kuloko jua. Kwa hiyo duara ya kung'aa ya jua ni kubwa kuliko duara ya mwezi na mwanga wa jua waonekana kama pete.
  •  
  • kupatwa kwa jua kisehemu: Katika eneo kubwa la kivuli cha kando watu hona upungufu wa mwanga; kiasi chake hutegemea umbali na kitovu cha kivuli. Wakitazama jua kwa filta kwa mfano kioo kilichopakwa dohani katika moshi ya mshumaa huwa wanaona sehemu ya duara ya jua imefunikwa.
Kesho  nchini Tanzania jua litapatwa  na  kwa  nchi  nzima eneo  ambalo wananchi watashuhudia  kupatwa kwa  jua ni eneo la Rujewa wilayani Mbarali mkoani Mbeya na eneo la Wanging'ombe  katika mkoa wa Njombe na macho  ya  watanzania wengi yameelekezwa  huko na mtandao huu wa matukiodaima.co.tz tutakuletea matukio hayo Live 

MNEC MUFINDI AWATAKA WANANCHI KUJIANDAA NA MILIONI 50 ZA RAIS DR MAGUFULI .......

                                                    Na MatukiodaimaBlog
WANANCHI  wilayani  Mufindi  mkoani  Iringa  wametakiwa  kuanza  maandalizi ya  kunufaika na milioni 50  kwa  kila  kijiji zilizopangwa  kutolewa na Rais Dr  John Magufuli kwa kuanza kujiunga  vikundi  vya  ujasiriamali na  kuvisajili  .

Wito   huo  umetolewa na  mjumbe  wa Halmashauri  kuu ya  Chama  cha mapinduzi (CCM)  Taifa kutoka wilaya ya  Mufindi ,Marcelina Mkini  wakati  akizungumza na  wanahabari  kuhusu utaratibu   huo mzuri  ulioahidiwa na Rais Dr  Magufuli  wakati wa kampeni .

Alisema  kuwa   ili  wananchi  kuweza  kunufaika na utaratibu   huo ni lazima   kujiunga katika  vikundi vya  watu  wenye  malengo  yanayofanana  na  kuvisajili  ili  pindi  pesa  hizo  zitakapotolewa  kuweza  kuzipata .

Mkini  alisema  kwa utaratibu wa  fedha  hizo  hazitatolewa  kwa  mtu  mmoja mmoja hivyo  kwa wale  ambao  wanazitamani  fedha  hizo  ni lazima  kuanza  kujiunga  katika  vikundi ambavyo vimesajiliwa .

" Lengo la  Rais   wetu  ni  kuona    wananchi   wananufaika na matunda  ya  nchi   hii ndio  sababu ya  kuahidi  kusaidia  vijiji fedha   hizo  shilingi  milioni 50 kwa  kila kijiji fedha  ambazo ni  nyingi  sana na  zitasaidia  wananchi  kujikwamua  katika  dimbwi la umasikini ........lazima  tumpongeze  sana kwa mtazamo  huu ambao  haujapata  kutokea "

Hivyo alitaka   vijana  ,wanawake na  wazee  kujiunga makundi  yenye malengo yanayofafa  yakiwemo ya  ufugaji kwa  wazee ama  kilimo na makundi  mengine  ambayo yatapelekea  vijiji   kuwa na vyama  vya  kuweka na  kukopa (SACCOS)  zao .

Mkini  ambae pia  ni  mwenyekiti  wa   umoja  wa  wanawake  Tanzania (CWT)  wilaya  hiyo ya  Mufindi  aliwataka  viongozi  wote  wa UWT   ngazi  zote  kusaidia  kuhamasisha  wanawake   kuonyesha mfano katika kuanzisha  vikundi  vya   uzalishaji mali .

Huku  akiwataka  kwa  kipindi   hiki  cha  kuelekea  kupata fedha   hizo  kuwa makini na matapeli  ambao  baadhi ya mikoa  wameanza   kujipitisha  kudanganya  wananchi  kuwa   fedha  hizo  zitapitia katika NGOs zao .

CHADEMA WAAHIRISHA MAANDAMANO YA UKUTA KESHOMuungano wa vyama vya upinzani nchini Tanzania umeahirisha maandamano ya kitaifa ambayo yalikuwa yamepangiwa kufanyika kesho.

WAPENZI WA MPIRA WAPEWA SOMO

Na Jacquiline  Mrisho - MAELEZO

Wapenzi wa mpira wa miguu wamejipanga kurasimisha jukwaa la kandanda kuwa jukwaa rasmi litakalozungumzia changamoto zinazohusu mpira wa miguu na jinsi ya kuzitatua ili kuongeza kasi ya maendeleo ya mpira nchini.

Mipango hiyo imejitokeza baada ya wapenzi wa mpira huo kuona kuwa kuna haja ya kuandaa kongamano litakalowaunganisha ili kuzungumzia masuala hayo kuliko kuendelea kuongelea suala hilo katika grupu waliloliunda katika mtandao wa kijamii wa ‘WhatsApp’.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti  wa Kamati ya Maandalizi ya Kongamano hilo, Henry Tandau alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu lengo la Kongamano hilo litakalofanyika  kwa siku mbili kuanzia Septemba 3 mwaka huu katika uwanja wa Taifa.

“Sisi wapenzi wa mpira wa miguu tumeamua kuandaa kongamano la kubadilishana mawazo na kutoa maoni kuhusu mpira huu ambapo lengo kubwa ni kupanga namna ya kurasimisha jukwaa hili kuwa chombo rasmi kitakachozungumzia masuala ya maendeleo ya mpira huu”, alisema Tandau.

Tandau ameongeza kuwa malengo mengine ya kongamano hilo ni kuongelea changamoto zinazokabili uendeshaji wa mpira wa miguu nchini, kuangalia jinsi ya kuubadilisha mpira wa miguu wa Tanzania kuwa wa kitaalam zaidi pamoja na kuchangia mawazo juu ya matatizo yanayozikwamisha klabu za Tanzania kushindwa kukidhii vigezo vya kushiriki mipira ya nje ya nchi.

Ametaja baadhi ya washiriki watakaoshiriki katika kongamano hilo kuwa ni wanachama wa jukwaa hilo, wawakilishi kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),  Bodi ya Ligi, Viongozi wa Klabu mbalimbali za mpira wa miguu, Baraza la Michezo Tanzania (BMT) pamoja na  Waandishi wa habari.

Mwenyekiti huyo amesema kuwa anategemea Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye kuwa mgeni rasmi atakayelifungua kongamano hilo kwa kuwa ndiye waziri mwenye dhamana katika masuala ya michezo pia ni mmoja wa wadau wakubwa wa Jukwaa hilo.

August 30, 2016

MAANDAMANO YA UKUTA LABDA YAFANYIKE NDANI KUZUNGUKA KITANDA NJE TUTAPAMBANA VIKALI - DC KASESELA

                                                Na MatukiodaimaBlog 

MKUU wa wilaya ya  Iringa  Richard  Kasesela (pichani) amesema amekwisha  zungumza na makundi  mbali mbali ya  vijana katika wilaya ya  Iringa na  kukubaliana kutoshirikia maandamano ya umoja  wa kupinga  udikteta  Tanzania (UKUTA)  japo anayehitaji   kuandamana  ruksa  ila aandamane ndani ya  nyumba yake  kuzunguka  kitanda na  sio kutoka mitaani.

Akizungumza na vijana  katika  ukumbi wa Highlands mjini hapa wakati wa uzinduzi wa Filam ya  Figisu  ya  Ndoa ,mkuu  huyo  alisema  kuwa  vijana  wanapaswa   kufanya kazi  za  kuwapatia  kipato  na  sio  kutumikishwa  kufanya  maandamano hayo ambayo  kwao hayana faida  yeyote .

"Tumejipanga   kuwashughulikia   wote  watakakaidi agizo  la  serikali kuhusu maandamano ya  UKUTA ......kama  mtu yeyote ana hamu  ya  kufanya maandamano afanye  ndani ya  nyumba  yake   kuzunguka  kitanda  chake na sio  nje mara  baada ya  kumaliza kufanya maandamano ndani kwake anapotoka  nje ni kwa ajili ya  kwenda  kufanya kazi  itakayomuigizia  kipato na sio kwenda  vijiweni ama kwenye  maandamano ya  UKUTA ole  wake mtu  akutwe akiandamana  ama  kupanga kuandamana "alisisitiza Kasesela 

Kuwa  serikali iliyopo madarakani  ni  serikali yenye uchungu na maisha  ya  watanzania na  kuwa  moja katika  ya  mikakati  yake ni kuona kila mtanzania anakuwa na maisha  bora  na  hakuna   njia ya  mkato ya  kuyafikia maisha  bora zaidi ya  kufanya kazi na sio  kutumika  kufanya maandamano ya  kuvutana na  serikali .

Mkuu  huyo  wa  wilaya  alisema amekwisha pata  taarifa  za  mmoja kati ya viongozi wa Chadema ambaye  ameendelea  kuhamasisha vijana  kufanya maandamano kwenye maeneo  mbali mbali ya  wilaya  hiyo  na  kuwa mipango yote tayari ameipata  hatua  mbali mbali kuchukua hatua  dhidi ya kiongozi  huyo  zinafanyika japo alisema mpango  wao  huo katika wilaya  ya  Iringa hautafanikiwa .

" Wakati  serikali  imezuia  mtu ama   chama  chochote  cha  siasa  kufanya mikusanyiko siku ya Septemba mosi  mwaka  huu  yupo mmoja kati ya  viongozi wa  Chadema ambaye anaendelea  kusambaza ujumbe  kwa  ajili ya kuandaa maandamano  ya  UKUTA .....nasema hakuna  aliyejuu ya  sheria  tutashughulika na uvunjaji  huu wa sheria unaofanywa na kiongozi  huyo"

Aidha  aliwataka  vijana kutokubali  kuingizwa katika matatizo  na kiongozi  mmoja mwenye lengo  baya  dhidi  yao na  badala  yake  kupuuza wito  wake  na  kuendelea na shughuli  zao za  kila  siku .

Kasesela  alisema amepata   kufanya  vikao na makundi  mbali mbali kwa  kuwashirikisha baadhi ya madiwani wa kata  mbali mbali  wakiwemo  wa Chadema na wameapa  kutoshiriki maandamano  hayo .


MWISHO

DC KILOLO APIGA MARUFUKU MAANDAMANO YA UKUTA


MKUU wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah amewataka vijana wanaojishughulisha na kazi ya kusafirisha abiria kwa kutumia pikipiki maarufu kama boda boda katika wilaya hiyo kuyaepuka maandamano ya umoja wa kupinga udikteta Tanzania (UKUTA) yanayopangwa na chama cha demokrasia na maendeleo (chadema) kuwa maandamano hayo yamepigwa marufuku .
Akizungumza kwa nyakati tofauti jana katika vikao vyake na boda boda wa Ilula na mjini Kilolo mkuu huyo alisema kuwa imekuwa ni kawaida ya vijana wa boda boda kutumiwa kufanya maandamano mbali mbali jambo ambalo hapendi lifanyike katika wilaya hiyo na kuwa kikundi chochote kitakachokutwa kikifanya maandamano ya aina yoyote siku ya septemba mosi hatua kali zitachukuliwa .
Kwani alisema ndani ya wilaya ya Kilolo anatamani kuona siku hiyo ya maandamano ya UKATA boda boda na wananchi wote wa wilaya ya Kilolo kila mmoja akiwa katika eneo lake la kazi akiendelea na shughuli yake ya kujitafutia kipato na sio kushiriki maandamano yasiyo na msingi kwa maisha yao .
"Sitakuwa tayari kuaona mkazi wa Kilolo anaacha kufanya kazi yake ainaingia barabara kufanya maandamano ambayo serikali imekwisha yapiga marufuku ......serikali ya wilaya ya kilolo na vyombo vyake vya ulinzi na usalama imejipanga kuona hakuna mtu anayefanya maandamano katika wilaya hiyo ....nawaombeni vijana wa boda boda acheni kutumika siku hiyo ikifika tulieni katika vijiwe vyenu fanyeni kazi "
Pia mkuu huyo wa wilaya aliwataka vijana wa boda boda kuangalia namna ya kuepusha ajali za mara kwa mara kwa kuzingatia sheria za usalama barabarani na kuwa iwapo hawata kuwa makini vifo na ulemavu vitazidi kuongezeka zaidi kuwa toka amefika wilaya ya Kilolo kwa miezi miwili pekee amepata kushuhudia ajali za boda boda tatu na baadhi yao kupoteza maisha .
Asia alisema kuwa hakuna faida ya vijana kuendelea kuifanya kazi hiyo ya boda boda kama wataendelea kupoteza maisha ama kupata ulemavu kutokana na ajali za mara kwa mara .
Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Kilolo Venance Mwamoto aliwataka vijana katika wilaya hiyo ya Kilolo kujiunga katika vikundi vya kiuchumi vya watu kati ya 30 na kuendelea ili pindi fedha za Rais Dr John Magufuli kiasi cha Tsh milioni 50 kwa kila kijiji zitakavyoanza kutoka basi waweze kunufaika na mpango huo ,Kuwa fedha hizo zitatolewa kwa vikundi na sio kwa mtu mmoja mmoja na ili kuweza kunufaika na fedha hizo ni lazima kujiunga vikundi vilivyosajiliwa
Pia alisema mbali ya fedha hizo kuna fedha asilimia 10 ya mapato ya ndani ya halmashauri ambazo zinaelekezwa kwa vijana hivyo kazi kubwa ya vijana ni kusajili vikundi vyao vya kiuchumi kwa kujiunga vijana kati ya 30 wenye malengo yanayofanana.
Mbunge Mwamoto alisema uchaguzi mkuu umekwisha na tayari yeye ni mbunge wa Kilolo na madiwani wapo ambao baadhi yao wawili ni wa Chadema japo alisema kwa sasa si wakati wa kuvutana kivyama bali ni wakati wa kuchapa kazi bila kutazama itikadi za vyama na kuwa ni kosa kwa Chadema kuanza kuwadanganya vijana na maandamano hayo ya UKUTA badala ya kuwawezesha kiuchumi .
Mwenyekiti cha chama cha boda boda Ilula Ndoro Mtenga pamoja na kumpongeza mkuu wa wilaya kwa kikao hicho kwao bado alisema kuwa wao kama boda boda hawaungi mkono maandamano ya UKAWA na kuwa wamepanga siku ya maandamano hayo boda boda wote kukaa katika vijiwe vyao kuendelea na kazi kama kawaida na hawatakuwa tayari kubeba abiria ambao wataonekana kwenda kuhamasisha maandamano .

August 29, 2016

CCM YAOMBOLEZA VIFO VYA POLISI WALIOUAWA NA MAJAMBAZI, SENDEKA AIVAA CHADEMA, AMJIBU TUNDULISU

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

 Ndugu wanahabari,
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimepokea kwa majonzi na masikitiko makubwa sana taarifa ya kushambuliwa na kuuawa kwa askari wa jeshi la Polisi wakiwa katika kutekeleza majukumu yao ya ulinzi eneo la Mbande, Temeke jijini Dar Es Salaam.

CCM tayari imemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Ernest Mangu pamoja na familia za marehemu waliofikwa na umauti katika tukio hilo baya katika historia ya nchi yetu.

Tunalaani tukio hilo na kutoa wito kwa wananchi kuvipa ushirikiano wa kutosha vyombo vya dola ili kufanikisha wahusika wa tukio hilo kusakwa popote pale na kupatikana ili wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria haraka.

Serikali ya Chama Cha Mapinduzi itaendelea  kuhakikisha amani ya Taifa letu inalindwa dhidi ya wachache wanaofurahia madhila kwa wananchi wetu. Wananchi wetu wanapenda, wamezoea na wanastahili amani. Ndio maana Tanzania imekuwa nchi ya kupigiwa mfano, ikionesha uongozi katika maeneo mengi. Tuendelee kuilinda taswira hii.

MAFANIKIO YA AWAMU YA TANO

Ndugu wanahabari,
CCM inachukua nafasi hii kumpongeza Rais Mhe Dkt John Pombe Magufuli na Serikali yake kwa mafanikio makubwa yaliyopatikana katika muda mfupi wa uongozi wake.

Rais Magufuli aliahidi mabadiliko. Tunampongeza kwa kusimamia vema utekelezaji wa ilani ya CCM. Katika muda mfupi wa miezi tisa tu, Rais Dk Magufuli amefanya mambo makubwa.

Sote tunafahamu kuwa Shirika letu la Ndege, ATCL, limekuwa linafanya kazi na ndege moja. Serikali ya Dk Magufuli imekwisha lipia ndege tatu za abiria toka Canada, ndege mbili zitaingiza nchini mwezi ujao.

Reli ya kati inajengwa kwa kiwango cha Standard Gauge. Meli katika ziwa viktoria inanunuliwa ktk bajeti ya mwaka huu. Elimu ya msingi na sekondari inatolewa bure. Wanafunzi wetu sasa wanakalia madawati na kujifunza vizuri zaidi. 
Barabara zimeendelea kujengwa. Makusanyo ya kodi yameongezeka. Huduma za jamii zinaendelea kuimarika. Lakini pia, nidhamu katika utumishi wa umma sasa imeimarika. Wananchi wanastahili huduma nzuri na kuthaminiwa na wafanyakazi wa Umma.

Mataifa mengi ya Afrika na nje ya Afrika yanaiga mbinu za Rais wetu katika kuleta mabadiliko nchini mwao. Hapa Kenya tu, Waziri mmoja wa Elimu anayesifika kwa utendaji kazi mzuri, anajiita “MAGUFULI.” Hata Australia, baadhi ya wananchi waliwahi kumtaka Waziri Mkuu wao afanye kazi kama Dk Magufuli.

Dk. Magufuli ameazimia kujenga uchumi wa viwanda. Ifikapo mwaka 2025, Tanzania itakuwa nchi yenye uchumi wa kati. Maisha ya wananchi wetu yataboreka. 
Vijana wetu wapate ajira katika viwanda, watauza malighali na mahitaji mbalimbali ya viwanda. Wakulima watapata masoko ya bidhaa zao katika viwanda hivyo. Kilimo kitaongezeka thamani kutokana na mahitaji mbalimbali ya viwanda vyetu.  Hatua za kuelekea huko tayari zimechukuliwa.

Wapo wachache wanaelekea kutafuta mbinu chafu za kuhujumu mafanikio haya, lakini hawatafanikiwa. Watanzania wamemchagua Dk Magufuli ili awaletee maendeleo.  

Serikali ya CCM, itawasaidia vijana wa Tanzania kuendesha uongozi wa Taifa lao. Kamwe tusikubali ndoto ya kuongoza mapinduzi haya makubwa kwa ajili ya Taifa na Bara letu ikapokonywa na watu wachache wasiokuwa na dira ya kuliletea maendeleo Taifa letu. Tuwapuuze.

UPINZANI KUSUSIA VIKAO VYA BUNGE

Ndugu Wanahabari,
Bunge kama ilivyo kwa mhimili mingine linaongozwa kwa katiba, sheria na kanuni katika mijadala na maamuzi yake. Kama Mbunge hajaridhika na maamuzi ya Spika, Naibu Spika au Mwenyeki wa kikao, kuna taratibu za kufuata. Utaratibu wa kikanuni ni kuulalamikia uamuzi huo kwa Katibu wa Bunge. 
Wakiwa wanafahamu taratibu za kikanuni, kama kawaida yao, WAPINZANI, waliamua kuzisigina na badala yake wakataka Naibu Spika aondolewe.

Hivyo wakaratibu kupigwa kura ya kutokuwa na imani na Naibu Spika. Ambapo suala hilo lilipelekwa kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge. 
Kutokana na kutokuwepo kwa Spika nchini, hoja hiyo haikufikia ukomo. Tunamshukuru Mungu afya ya Spika imeimarika. Sasa hoja hiyo huenda itafikishwa katika mkutano wa Bunge litakalokaa mwezi ujao.

Kana kwamba hiyo haitoshi, kama kawaida yao, hawakuwa na subira ya kufuata taratibu. Wakaamua kufanya kihoja. Wakaamua kutohudhuria vikao vyote vya Bunge vilivyokuwa vikiongozwa na Naibu Spika.

Na hata walipoingia Bungeni waliziba midomo yao na kuamua kutowasalimia wabunge wenzao wa CCM, kutopeana mikono na hata kutohudhuria misiba na sherehe zao. 
Vitendo vyao hivi ndivyo vimeasisi chuki ndani ya jamii yetu iliyozoea UPENDO, UDUGU, UMOJA NA MSHIKAMANO. Watanzania tunafahamika na tunaona fahari kuishi kama ndugu.

Baada ya kitendo hicho cha kuwasaliti wapigakura wao kulaaniwa kila kona ya nchi, sasa wamekubali kutumiwa kama vibaraka kuichafua taswira ya nchi yetu, nao kwa hila iliyo wazi, wamekubali kuwafitinisha watanzania kwa kuandaa maandamano ya nchi nzima, yasiyo na ukomo. Hatua hii ni uvunjaji wa katiba ya nchi, Sheria na inalenga kuvunja amani, utulivu na mshikamano wa watu wetu.

Ileleweke kwamba, wanachokifanya hawa CHADEMA ni kuchochea wananchi kwa makusudi kutotii maagizo halali ya vyombo vya dola na Serikali kwa visingizio mufilisi kuwa katika Katiba imewapa uhuru huo. Katika haitoi haki na uhuru usio na ukomo. Ibara ya 29 (5) inasema;

 “Ila watu wote waweze kufaidi haki na uhuru vinavyotajwa na katiba hii kila mtu ana wajibu wa kutenda na kuendesha shughuli zake kwa namna ambayo haitaingilia haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma”

Baada ya kusema hayo, ninaomba CHADEMA wakumbuke na kutilia maanani kuwa kila haki ina wajibu na hakuna haki au uhuru usiokuwa na ukomo hususani pale inaposababisha kuingiliwa ama kukatizwa kwa haki na uhuru wa watu wengine. Rejea ibara ya 30 (1) na (2) ya Katiba.

Ndugu wahabahari,
Mwisho tunatoa pole kwa wenzetu wa CUF kutokana na mapambano huko kwao. Tumestushwa sana na yanayoendelea huko. CCM inawapa pole na tunawatakia maelewano ili waje tusaidiane kuwaletea watanzania maendeleo.


MSEKWA:WATANZANIA WAACHE KUFUATA MKUMBOSpika wa zamani wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Pius Msekwa


Na Fatma Salum na Sheila Simba, MAELEZO  
Spika wa zamani wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Pius Msekwa amewaasa watanzania kuacha kufuata mkumbo wa kisiasa badala yake watii mamlaka ili kuepuka kuvunja sheria na kuleta madhara kwao binafsi na taifa kwa ujumla.
Msekwa aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akizungumzia masuala mbalimbali kuhusu mwenendo wa siasa za hapa nchini na utendaji kazi wa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. Alieleza kuwa watu wengi wana hulka ya kufuata mkumbo kwenye mambo fulani bila ya kuchunguza na kufahamu ukweli wake kabla ya kushabikia.
“Ni hulka ya watanzania kushabikia mambo wasiyoyafahamu ilimradi tu yanawafurahisha masikioni   au machoni mwao kwani hata huko mitaani wanakimbilia ngoma bila ya kujua inatokea wapi au inaelekea wapi, hivyo nawasihi wajaribu kuwa makini na mbinu za siasa zinazotumiwa na baadhi ya vyama kwa kuwa nyingine zina madhara ndani yake.” Alisema Msekwa.
Akifafanua mwenendo wa siasa za hapa nchini, Mzee Msekwa alisema kuwa bado wanasiasa wengi hawafuati kanuni za ushindani wa kisiasa katika kutafuta madaraka badala yake wanatumia mbinu ambazo zinavunja sheria za nchi na hatimaye wanapambana na mamlaka.
“Ushindani wa kisiasa ni jambo la kawaida na linalokubalika ingawa ushindani huo ni lazima ufuate sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa ili kufikia lengo, hivyo kubuni vitu ambavyo vinachochea utovu wa nidhamu na uvunjifu wa amani sio jambo zuri, ' alisisitiza.
Aidha, Msekwa alieleza kuwa utendaji wa Mhe. John Magufuli ni wa kuridhisha na wa aina yake kwa kuwa amekusudia kuleta mabadiliko chanya kwa watanzania na kuondoa mfumo wa utendaji kazi kwa mazoea jambo ambalo limesaidia kurudisha nidhamu kwa watumishi wa Serikali.
Akizungumzia uzoefu wake katika masuala ya kuongoza Bunge, alieleza kuwa tofauti ya Bunge la zamani ni kwamba lilikuwa na nidhamu kubwa na linaheshimika lakini Bunge la sasa halina utii na hicho ndio chanzo cha malumbano yanayojitokeza mara kwa mara katika vikao vya Bunge.
Aliongeza kuwa tangu awali wapinzani kazi yao ni kuipinga Serikali iliyo madarakani lakini kwenye Bunge la uongozi wake walikuwa wakipinga kwa kutumia hoja na kufuata kanuni bila ya kudharau mamlaka ya Spika wala Serikali iliyoko madarakani.
“Kanuni zinatoa nafasi kwa mbunge asiyeridhika na maamuzi ya Spika kushitaki kwenye Kamati ya Kanuni za Bunge, na kamati hiyo itasikiliza na kutoa uamuzi kama mahakama inavyosikiliza lakini wabunge wa sasa hawataki kutumia utaratibu bali hutumia mbinu za tofauti ili waweze kupata sifa ambazo hazina tija kwa wananchi waliowachagua,” alisema.
Msekwa pia amewaasa vyama vya upinzani kutumia mbinu nzuri katika kutafuta madaraka bila ya kuvunja sheria au kuhatarisha amani ya nchi kwani waliowachagua wanategemea zaidi matokeo ya kazi waliyoahidi kuwatumikia kuliko malumbano yasiyo na tija kwa ustawi wao na taifa.
mwisho

August 28, 2016

MAGAZETINI LEO,Aug 28


August 26, 2016

SERIKALI YA MKOA WA IRINGA YAPONGEZA TUZO YA UBORA WA MAZIWA AFRIKA ILIYOPATA KAMPUNI YA ASAS DAIRIES LTD

Kaimu  mkuu wa mkoa wa Iringa Richard  Kasesela (wa tatu kushoto )ambae ni mkuu wa wilaya ya  Iringa akiongoza  washiriki wa warsha  ya  wiki moja ya kilimo  biashara  yaliyoandaliwa na  Shirika la umoja wa mataifa linalojishughulisha na kilimo (UNCTAD)  kwa ufadhili  wakampuni  ya Asas Dairies Ltd na  SAGCOT kupongeza ubora  wa maziwa ya kampuni ya  Asas Dairies Ltd  baada ya kushinda  tuzo ya ubora wa bidhaa  za maziwa Afrika  tuzo ya ARSO leo wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo ,wengine  pichani  kutoka kushoto  wa  kwanza ni  Meneja maendeleo na biashara  Roy Omulo ,mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Asas Dairies Ltd Ahmed Abri  na mwakilishi wa  katibu mtendaji wa SAGCOT CTF Mbosela John Mosela kulia
Kaimu  mkuu wa mkoa wa Iringa Richard  Kasesela ( mwenye suti katikati) akiwasili  eneo la  warsha  kwa ajili ya ufungaji  kushoto  kwake ni mkurugenzi wa Asas Dairies Ltd Ahmed Abri na  washiriki  wengine
Kasesela kulia  akiongoza wana  warsha  kupiga makofi
Kaimu  mkuu wa mkoa wa Iringa Richard  Kasesela (wa tatu kushoto )ambae ni mkuu wa wilaya ya  Iringa akiongoza  washiriki wa warsha  ya  wiki moja ya kilimo  biashara  yaliyoandaliwa na  Shirika la umoja wa mataifa linalojishughulisha na kilimo (UNCTAD)  kwa ufadhili  wakampuni  ya Asas Dairies Ltd na  SAGCOT kufungua maziwa kabla ya kupongeza ubora  wa maziwa ya kampuni ya  Asas Dairies Ltd  baada ya kushinda  tuzo ya ubora wa bidhaa  za maziwa Afrika  tuzo ya ARSO wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo ,wengine  pichani  kutoka kushoto  wa  kwanza ni  Meneja maendeleo na biashara  Roy Omulo ,mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Asas Dairies Ltd Ahmed Abri  na mwakilishi wa  katibu mtendaji wa SAGCOT CTF Mbosela John Mosela kulia
Kaimu  mkuu wa mkoa wa Iringa Richard  Kasesela (katikati)ambae ni mkuu wa wilaya ya  Iringa akifunga warsha ya  wiki moja ya kilimo  biashara  yaliyoandaliwa na  Shirika la umoja wa mataifa linalojishughulisha na kilimo (UNCTAD)  kwa ufadhili  wakampuni  ya Asas Dairies Ltd na  SAGCOT kwa  wafugaji 35 kutoka mkoa wa Iringa , Mbeya na Njombe leo ,kushoto wa kwanza ni meneja biashara na maendeleo  wa kampuni ya maziwa  ya Asas akifuatiwa na mkurugenzi wa kampuni ya Asas Dairies Ltd Ahmed Abri na kulia  ni mwakilishi wa  katibu mtendaji wa SAGCOT CTF Mbosela John Mosela
Kasesela  akimnyoshea  kidole mkurugenzi wa Asas Dairies Ltd  Ahmed  Abri  wakati akipongeza jitihada  zao
Mkurugenzi wa Asas Dairies Ltd  Ahmed Abri  akifurahia hotuba ya Kasesela
Washiriki wa warsha hiyo wakifuatilia  hotuba ya Kasesela
Kasesela  akiwa katika  picha ya pamoja na mkurugezi wa Asas Dairies Ltd Ahmed Abri (katikati) na Ahmed Bin Is Haq
wawakilishi wa taasisi  za kifedha Iringa  wakiwa katika  warsha  hiyo
Mwakilishi  wa Finca  akieleza aina  ya mikopo  iliyopo
washiriki wa warsha  hiyo
Kaimu  Rc Iringa Richard  Kasesela  akigwa  vyeti kwa washiriki wa warsha  hiyo
Mshiriki Asha Lukasa kutoka  kikundi cha Syukula Kisegese Tukuyu  akipozi na kaimu RC Iringa Richard Kasesela baada ya  ukupewa  cheti  chake  cha ushiriki
Na MatukiodaimaBlog
SERIKALI  ya  mkoa  wa  Iringa  imeipongeza kampuni ya  maziwa ya Asas Dairies Ltd ya  mkoani Iringa  kwa kushinda tuzo  ya (ARSO) kwenye  mashindano ya  kimaifa ya nchi  za Africa ya  ubora  wa bidhaa za maziwa   kuwa ni tuzo yenye heshima kubwa kwa mkoa huo na Tanzania kwa ujumla .

Pamoja na pongezi hizo  pia imepongeza  jitihada  zinazofanywa na kampuni ya  Asas Dairies  Ltd  kwa  kuwawezesha mafunzo  mbali mbali wafugaji  wa mikoa ya Mbeya , Njombe na  Iringa  kubadili  ufugaji wa  kienyeji na  kufuga  kibiashara  zaidi  .

Huku  ikiwataka wenye  viwanda  vya  usindikaji  maziwa kujenga utamaduni  wa  kuwafikia  wafugaji na  kuwapa   elimu  ili  kuwezesha  bidhaa zao  za maziwa  kuendelea   kuwa  zenye  ubora  zaidi  na  ikiwezekana  kuwawezesha  kupata vifaa vya  kisasa  vya  kukamulia maziwa.

Kaimu  mkuu  wa  mkoa wa Iringa Richard Kasesela  aliyasema hayo leo  kwenye ukumbi wa Asas mjini hapa  wakati wa  ufungaji wa mafunzo ya wiki moja kwa wafugaji 35  kutoka Iringa , Mbeya  na Njombe  mafunzo yaliyoandaliwa kilimo  biashara  yaliyoandaliwa na  Shirika la umoja wa mataifa linalojishughulisha na kilimo (UNCTAD)  kwa ufadhili  wakampuni  ya Asas Dairies Ltd na  SAGCOT  CTF


Alisema kuwa kampuni  hiyo  imeupa mkoa wa Iringa  heshima  kubwa na kuwa ukiacha mashindano mbali mbali ya maziwa kwa viwanda  vya ndani ya  Tanzania kampuni  hiyo imekwisha  shinda mara nne  sasa jambo ambalo ni la kujipongeza na kujivunia kuwa bidhaa  zinazozalishwa ni bora na hivyo si wakati wa watanzania  kukimbilia bidhaa za nje na kuacha zinazozalishwa ndani ya nchi .

Kasesela ambae  pia ni mkuu wa wilaya  ya Iringa  alisema kuwa mbali ya  wadau na wawekezaji  waliopo katika wilaya  yake na mkoa wa Iringa  wamekuwa msaada katika maendeleo  ila bado kampuni  hiyo ya  Asas Dairies Ltd  imekuwa ni msaada  zaidi si tu kwa mambo ya  serikali bali hata katika kuwawezesha   wakulima na  wafugaji   kupatiwa elimu .

Alisema  ni  vema  wamiliki  wa  viwanda   kuwa na mbinu ya  kuwafikia  wafugaji na  kuwapa  elimu na  mbinu ya  kuongeza kasi  ya uzalishaji wa maziwa  bora   ili  kuviwezesha   viwanda  vyao  kuwa na maziwa  mengi  zaidi na  bora  na  sio  bora  maziwa .

Kuwa  serikali  ya mkoa wa Iringa  inatambua  faida ya mafunzo hayo kwa  wafugaji na pia  jitihada za wahisani  mbali mbali  wakiwemo SAGCOT ,Asas Dairies Ltd   na wengine  na kuwa  jitihada  hizo  zinafanywa na SAGCOT kwa makubaliano ambayo yamefikiwa kati yao na  serikali ya awamu ya tano kwa  lengo la kuwakomboa  wakulima wadogo na wafugaji .
Hivyo  aliwataka  wafugaji hao ambao  wamepewa  elimu   hiyo  kwenda kuitumia   vizuri  ili  kufanikisha azma ya  serikali ya awamu ya tano kwa  kuona  kilimo  na ufugaji  inakuwa ni  fursa nzuri ya  kumkomboa  mwananchi .

Kasesela  alisema kuwa kwa  mujibu wa tafiti  inaonyesha  kasi ya  watanzania  kunywa maziwa  bado  ni ndogo  sana  kuliko  unywaji wa pombe jambo   hali  ambayo ni hatari  kwa afya   na hivyo ni vema  kuendelea  kuhamasisha  wananchi  kunywa maziwa  zaidi  kwa afya  zao  kuliko pombe ambazo  kimsingi  kiafya hazina  faida  yeyote  mwilini .

Mkurugenzi  wa kampuni ya  Asas Dairies  Ltd   Ahmed Abri  kampuni   yake  ilianza  mwaka 2000 kwa  kuanza  kusindika  maziwa  kati ya  lita 1000 – 1500 kwa  kutengeneza maziwa mgando  na maziwa halisi baada  kuoa  bidhaa hiyo  inahitajika  zaidi mjini Iringa  walazizimika  kuanza  kukusanya maziwa kutoka maeneo mbali mbali ukiacha yale  ambayo  yalikuwa  yakitoka  shambani kwao .

“ Tuliamua  kuanza  kuwatembelea  wafugaji maeneo mbali  mbali  na  mwaka 2005 -2006  idadi ya  wafugaji  iliongezeka  zaidi  kufikia  wafugaji  43 hivyo  kuanza  kutengeneza  bidhaa mpya ya  Yoghurt ila bado chagamoto  ilikuwa ni maziwa hivyo  kulazimika kwenda  nje  ya mkoa wa Iringa kama Njombe na Mbeya wilaya ya Rungwe  na  kuwa kiwanda  chetu  kilikuwa na uwezo wa kuzalisha maziwa lita 50,000 kwa siku   kutoka  lita 12,000 “

Abri  alisema kwa  sasa baada ya  kutoa  elimu mbali mbali kwa mikoa ya Iringa ,Njombe na Mbeya  hivi sasa  kiwanda  hicho  kinawafugaji  1800 ambao wanapeleka maziwa hapo .
Aidha  alisema  wakati shirika la afya Duniani linasisitiza kila binadamu  kunywa maziwa lita 200 kwa mwaka  ila kwa  watanzania  hata  lita  mbili kwa mwaka mtu  hanywi maziwa na kama atakunywa kwa  wingi  basi ni baada ya  kuandikiwa na daktari .

“ Sisi  kama kama kampuni  tumekuwa tukihamasisha  unywaji wa maziwa na  kila mwaka  tumekuwa  tukihamasisha mashuleni  na lengo kuona  watanzania  wanajenga utamaduni wa kupenda  kunywa maziwa zaidi kwani Tanzania kwa siku  inazalisha maziwa  lita  300,000 pekee ambazo haziishi sokoni kutokana na watu  kutopenda  kunywa maziwa  huku Kenya  inazalisha maziwa lita milioni moja  kwa  siku na bado  wanalalamika  haziwatoshi .

Kuwa maziwa yanayozalishwa nchini ni lita kama 100,000 pekee  ndizo  zinapelekwa kiwandani na maziwa yanayobaki  yanauzwa  mitaani ambayo hayana  ubora hivyo rai  yao kwa watanzania ni  kupenda  kunywa maziwa yaliyosindikwa kutoka  viwandani  kuliko  kunywa maziwa yasiyo na ubora  yanayozungushwa mitaani .

Abri  alisema kutokana na kuzingatia ubora  wa maziwa na  wafugaji  kuzalisha maziwa  bora  kampuni  ya  Asas Dairies Ltd imeendelea   kuongoza nchini   kwa  kushinda  tuzo  za  ubora  wa bidhaa zake kwa miaka minne mfululizo na mwaka  huu imeshinda tuzo nyingine ya mashindano ya  kimaifa ya nchi  za Africa  tuzo ya ARSO  yaliyofanyika Julay  mwaka  huu mjini  Arusha  yaliyoshinisha makampuni zaidi  ya 60 toka ndani na nje .