Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

June 30, 2016

SERENGETI BOYS YAPAA, MCHAWI MWEUSI ATAMBA

 
Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ imeondoka saa 9.45 alfajiri ya leo Juni 30, 2016 kwa ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia kwenda Visiwa va Hame-Shelisheli kwa ajili ya kuwavaa wenyeji katika mchezo wa marudiano kuwania nafasi ya kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana.

Serengeti Boys inaondoka na matumaini makubwa ya kuiondoa Shelisheli katika mbio hizo baada ya kuvuna ushindi mnono wa mabao 3-0 katika mchezo wa kwanza uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Jumapili ya Juni 26, 2016. Ili ifuzu, Serengeti Boys inahitaji kusimama imara katika matokeo hayo ama kwa kupata sare ya aina yoyote, kushinda au ikitokea kupoteza, basi isifungwe zaidi ya mabao 2-0.

Lakini Kocha Mkuu wa vijana hao, Bakari Shime maarufu kama Mchawi Mweusi kutoka Tanga, amesema, “Nawaheshimu Shelisheli, lakini vijana wangu hawawezi kuwapa nafasi hata kidogo wapinzani wetu. Hapa tulishinda, na kwako tunakokwenda tunakwenda kushinda. Vijana wangu wa Serengeti Boys wako vizuri. Nawapenda na wao wanatupenda makocha wao na viongozi wote wa TFF.”

Katika mchezo wa Dar es Salaam waliozifumania nyavu walikuwa Nickson Kibabage, Ibrahim Abdallah na Ally Hussein ambaye alifunga ambao kila mmoja amepania kufunga kama kocha akiwapa nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza kwa sababu Mchawi Mweusi amefunga safari hiyo akiwa na kikosi cha nyota 20 wa timu hiyo inayolelewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) chini ya Rais Jamal Malinzi.

Nyota waliosafiri ni pamoja na makipa, Ramadhani Awm Kabwili na Samwel Edward Brazio wakati mabeki wako Kibwana Ally Shomari, Nickson Clement Kibabage, Israel Patrick Mwenda, Dickson Nickson Job, Ally Hussein Msengi, Issa Abdi Makamba.

Viungo ni Kelvin Nashon Naftal, Ally Hamisi Ng’anzi, Asadi Ali Juma Ali, Syprian Benedictor Mtesigwa, Ibrahim Abdallah Ali, Yassin Muhidini Mohamed, Shaban Zuberi Ada huku washambuliaji wakiwa ni Rashid Mohammed Chambo, Mohammed Abdallah Rashid, Yohana Oscar Mkomola, Muhsin Malima Makame na Enrick Vitalis Nkosi.

Serengeti Boys ambayo haina mdhamini badala yake ikihudumiwa na TFF yenyewe ilikuwa kambini tangu Juni 14, 2016 kujiandaa na mechi hizo za kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya Shelisheli na Afrika Kusini ambayo itapambana nayo baadaye mwezi ujao.

Katika kuajindaa na mchezo huo, Serengeti Boys ilifanya ziara India ambako walishiriki mashindano ya vijana ya Kimataifa yanayotambuliwa na FIFA (AIFF International Youth Tournament 2016) kabla ya kurudi na rekodi ya kupigiwa mfano si tu katika Tanzania na kwa nchi za Afrika Mashariki. Ilishika nafasi ya tutu nyuma ya Korea Kusini na Marekani.

…………………………………………………………………….
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA SOKA TANZANIA

TAARIFA KAMILI YA AJALI ILIYOTOKEA MJINI IRINGA LEO HII HAPA

Eneo la  ajali  kona ya  kisima  cha  bibi
Damu  zikiwa zimetapakaa eneo la  tukio  baada ya  kumtoa majeruhi  aliyekuwa hoi kwa kubanwa na gari

Wananchi  wakitazama ajali  hiyo
Baadhi ya majeruhi wa ajali   hiyo  wakiwa wanasubiri msaada
Eneo  ambalo  ajali imetokea  ni  hapa  katika  foleni  gari  namba tatu  toka  kushoto ni la mwenyekiti wa kamati ya  usalama barabarani  mkoa wa Iringa  Salim Asas   likiwa eneo la  tukio baada ya ajali  kutokea

 Baadhi  ya  majeruhi wa ajali  hiyo  wakiingia katika gari la  polisi kwa  ajili ya  kukimbizwa  Hospitali  ya  rufaa ya  mkoa wa Iringa 

..................................................................................

 

Na  MatukiodaimaBlog

WATU  zaidi ya 10 wamejeruhiwa   huku  wengine   wakinusurika baada ya   Coster ya  abiria  inayofanya safari zake kati ya Iringa mjini ,Ifunda na Igomtwa kupinduka  eneo la  Kisima cha  Bibi Ipogolo mjini Iringa eneo  ambalo  mwezi  Mei 28  basi la Abiria la Lupondije lilipinduka  na  kuua watu 6 na kujeruhi zaidi ya 35 .

Majeruhi  wa ajali   hiyo  Iddy Kambaya na  Selfu Nyanginywa  wameueleza mtandao huu wa matukiodaimaBlog  kuwa chanzo cha ajali ni breki kufeli  na  kupelekea  basi  hilo kukosa  mwelekeo  kabla  ya  kupinduka .


Majeruhi  hao  walisema  kuwa  ajali  hiyo imetokea  majira ya saa 8;45 mchana   wakati   gari hilo likitoka  mjini  kuelekea  Igomtwa na   kuwa  toka  wametoka   stendi  hakukuwa na tatizo  lolote  ila  baada ya  kufika   eneo la  Samora   wakianza  kushusha  mteremko  huo mkali wa Ipogolo walifanikiwa  kupita  tuta  la kwanza la  kupunguza  mwendo  lililopo  barabarani  bila  tatizo  ila  baada ya  kuingia  tuta  la  pili  gari  lilifeli  breki na   hivyo  kuanza  kuporomoka   kwa  mwendo mkali  zaidi .


Alisema Bw  Kambaya  kuwa  kutokana na  hali  hiyo  dereva wa  gari hilo aliweza  kujiongeza zaidi kwa  kujaribu  kunusuru  gari hilo  kutumbukia  katika korongo la mto Ruaha   .


“ Dereva  mbali ya  kupata  ajali  ila  amejitahidi  sana   kuokoa maisha  yetu  maama  kama  si jitihada  binafasi  gari  lilikuwa  linatumbukia  korongoni na  huenda maafa  yangekuwa  makubwa  zaidi  ila mimi  ni majeruhi  ila  nampongeza  dereva ameokoa maisha  yetu ……..gari  baada ya  breki  kugoma   watu  wote  walianza kupiga kelele  huku  wengine wakisali “


 Miongoni mwa majeruhi  ambao   walikutwa katika  Hospitali ya  Rufaa ya  mkoa wa Iringa  wakisubiri  kupatiwa matibabu ni pamoja na  Rahma  Malekela  (22) mkazi wa Kibwabwa  Iringa , Andrew ambae ni mtoto wa miaka  mitatu ,  Mathew Lungo(4) , Selfu Nyanginywa (31) na Iddy Kambaya  huku  wengine  walikuwa katika  chumba  cha daktari na  baadhi yao wakiwa  njiani  kufikishwa  Hospitalini  hapo .


 Jitihada  mbali mbali za  jeshi la  polisi  kikosi  cha  usalama  barabarani na  askari wengine  ambao walikuwepo  eneo la tukio kuweka  ulinzi  wakiongozwa na mkuu wa usalama  barabara mkoa  wa Iringa Bw Leopold Fungu wamepongezwa  kwa  kuweka  ulinzi  eneo  hilo ambalo kimsingi vibaka   huwa ni  wengi katika  maeneo  ya  ajali kama  hayo .

Taarifa  ambayo  imethibitishwa na mkuu wa  usalama  barabara  mkoa wa Iringa (RTO) Fungu zinadai kuwa  ni abiria  mmoja  pekee ambae ni mwanamke  ndie  hali yake ni mbaya  zaidi ukilinganisha na  majeruhi   wengine na kuongeza  kuwa katika  ajali  hiyo  hakuna  aliyepoteza maisha .

MWISHO 

TAARIFA  HII KWA  UDHAMINI WA  KITUO  CHA MAFUTA  CHA  PUMA MJINI IRINGA JAZA  MAFUTA  HALISI NA  BORA KITUO  CHA  PUMA TUPO IPOGOLO LANGO KUU LA KUINGIA MJINI IRINGA 

 

RAIS DR MAGUFULI AMTUMBUA MFANYABIASHARA


RAIS Dk. John Magufuli amemtumbua mfanyabiashara mmoja maarufu Dar es Salaam, aliyebainika kufanya miamala ya fedha ya Sh milioni saba hadi nane kwa kila baada ya dakika moja.

Kutokana na hesabu ya Sh milioni saba anayoingiza kwa dakika moja, mfanyabiashara huyo hutengeneza Sh milioni 420 kwa kila saa moja, sawa na Sh bilioni 5.2 kwa saa 12 na Sh trilioni 16 kwa mwezi ambazo halipi Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT).

Rais Magufuli amesema mfanyabiashara huyo aliyebainika kuwa na makampuni mengi, alikuwa akishirikiana na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni nchini (BRELA) pamoja na Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA).
Mkuu huyo wa nchi alitoa kauli hiyo Ikulu, Dar es Salaam jana, baada ya kuwaapisha wakuu wapya wa mikoa watatu katika hafla iliyohudhuriwa pia na wakuu wa wilaya wateule.

Alisema waligundua jipu hilo baada ya kufuatilia kwenye mapato.
“Tulikuwa tunafuatilia kwenye ‘revenue’ (mapato), kwenye zile VAT ambazo zinatumika ‘ku-collect revenue’ (kukusanya mapato), yupo mtu mmoja ambaye alikuwa ametengeneza kampuni zake nyingi, alikuwa anafanya ‘transaction’ (miamala) ya fedha kila dakika moja kati ya Sh milioni saba na nane.

“Na hizo risiti alikuwa anaziuza kwa wafanyabiashara wengine, kwenye VAT anatakiwa kulipia kwa asilimia 18. Wafanyabiashara wengine hao walikuwa wanauziwa kwa asilimia tano na wakishauza bidhaa wanakwenda kuomba TRA iwarudishie hiyo asilimia 18, kwa hiyo Serikali imekuwa ikipoteza asilimia 18.5, ni matrilioni na matrilioni ‘of money’ (ya fedha).

“Bahati nzuri huyo mtu yuko kwenye mikono salama, tunafuatilia namna tutakavyorudisha hizo fedha, na huyo mtu alikuwa ana-connection kati ya watu wa BRELA na TRA… hiyo ndiyo Tanzania.

“Najaribu tu kutoa mfano ili katika maeneo yenu mkasimamie mapato ya Serikali, kwa sababu tumepoteza mapato mengi kuliko tunavyofikiria, huku Watanzania wakiteseka sana, na mambo yanayofanyika ni ya ajabu,” alisema Rais Magufuli akiwaambia wakuu hao wa mikoa na wilaya.

Pamoja na mambo mengine, Rais Magufuli alisema mchakato wa kupata wakuu wapya wa wilaya ulikuwa mgumu, na kwamba amewaacha wengi wa zamani kwa kuwa hawakutimiza vigezo alivyovitaka.

“Mchakato wa kupata ma-DC ulikuwa mgumu kwa sababu ilibidi tuangalie historia ya kila mmoja.

Tuliangalia mambo mengi sana, lakini pia tuliangalia kwa ku-preview atatimiza haya tunayotaka kuyafanya kwa miaka mitano?

“Na ndiyo maana mnavyoona ma-DC wa zamani waliorudi ni 39, kwa hiyo wale 101 wote hawakurudi… niseme tu ukweli kwamba hawakufikia vigezo tulivyokuwa tunavitaka,” alisema Rais Magufuli.

Alisema katika uteuzi huo, alichukua wakurugenzi kwa kuwa walifanya vizuri katika maeneo yao waliyokuwa wakiyaongoza.

“Tulichukua wakurugenzi walio-perform vizuri katika maeneo yao. Wapya wako takribani 100 na waliobaki ni hao kati ya 38 na 39. Ni matumaini yangu kwamba mtakwenda kufanya kazi na kutimiza wajibu wenu.

“DC ni nafasi kubwa ya uongozi katika Serikali na ndiyo maana mfano mkubwa wa DC mstaafu ni Waziri Mkuu (Kassim Majaliwa), ni kwa sababu alitimiza wajibu wake na leo yuko hapa,” alisema.

Mkuu huyo wa nchi aliwapa mikakati ya kufanya kazi wakuu hao wa wilaya kwa kutimiza dhana ya kuchapa kazi kwa niaba ya Serikali.
“Nina matumaini makubwa mtakwenda kutimiza dhana ya kuchapa kazi kwa niaba ya Serikali, ninyi ndio wawakilishi wetu na ndio mnawakilisha wananchi wa maisha yote.

“Watanzania wana matatizo na changamoto kubwa. Ni matumaini yangu kwamba hamtaniangusha na hamtaiangusha Serikali. Nina imani mtakwenda kutatua matatizo ya wananchi, hasa walio masikini, sitegemei wala sifikirii kwamba mkawe chanzo cha kutengeneza matatizo,” alisema Rais Magufuli.

Kutokana na hali hiyo, aliwataka wasimamie haki, huku wakimtanguliza Mungu katika kufanya kazi, kusimamia maadili, kutenda haki, kutojihusisha na rushwa, kuwatumikia Watanzania bila kubagua dini, kabila wala vyama vyao.

“Kikubwa mkasimamie yale tuliyoyaahidi sisi wanaCCM, kwa sababu wakati tunazunguka tukiomba kura, yapo tuliyoyaahidi, hayo mkayatekeleze kwa nguvu zote.

“Na wala asitokee mtu yeyote wa kuwakwamisha kutekeleza hayo, ninyi ndio wakuu wa wilaya na ninyi watatu ndio wakuu wa mikoa. Mna mamlaka makubwa ya kuweka mahabusu mtu masaa 48 halafu kesho yake ukamwachia. Ila msiende kuonea watu, mkachape kazi.

“Imani tuliyoionyesha kwenu sisi viongozi wenu mkaionyeshe kwa Watanzania mnaowaongoza, mkashirikiane na viongozi mtakaowaongoza, wanasema umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu.

“Nina uhakika mkisimama vizuri kwa kuzingatia maadili mliyonayo, na bahati nzuri wengi mna uzoefu katika maeneo yenu. Mkawahamasishe Watanzania katika wilaya na mikoa yenu kufanya kazi. Watanzania wengi tumezoea kulalamika, tunataka tupewe, lakini hatufanyi kazi. Tukawasimamie kuchapa kazi,” alisema.

Aliwataka wakuu hao wa wilaya ambao pia ni wenyeviti wa kamati ya ulinzi na usalama, kukemea rushwa katika maeneo yao na kusimamia mapato ya Serikali.
“Huwa inatokea saa nyingine wakurugenzi kwa sababu kuna fedha nyingi tunapelekaga kule, wanadhani ni zao wakati ni za Serikali, mkawasimamie bila woga.

“Kupitia halmashauri zenu, mkahakikishe fedha hizo zinatumika kulingana na matakwa ya kanuni na sheria za nchi,” alisema Rais Magufuli.

RC MASENZA AKWEPA ADHABU YA RAIS DR MAGUFULI ,ATEKELEZA AGIZO LA MADAWATI

Mkuu  wa  mkoa  wa Iringa  Amina Masenza  akitazama  madawati  yaliyokamilika kulia ni  afisa  habari wa Manispaa ya  Iringa  Sima Bingileki

Mkuu  wa  mkoa  wa  Iringa  Amina Masenza  kulia  akimkabidhi  madawati 100  mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa Bw. Ahmed  Sawa   leo baada ya  mkoa kukamilisha utekelezaji wa agizo la Rais kuhusu madawati 
Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya  wilaya ya  Kilolo kulia  akipokea madawati  kutoka kwa  mkuu wa mkoa wa Iringa
Mwakilishi  wa mkurugenzi wa Halmashauri ya  Wilaya ya  Iringa Bi  Hawa akiwa na mkuu wa mkoa wa Iringa Bi Masenza mara  baada ya  kukabidhiwa madawati


Na MatukiodaimaBlog

SERIKALI    ya    mkoa wa  Iringa  imetekeleza  agizo la  Rais  Dr  John Magufuli  kwa kukabidhi  jumla ya madawati 21,304 kwa   shule  za  msingi  na   sekondari katika Halmashauri  zote  tano  za  mkoa   huo .

Mkuu  wa  mkoa  wa  Iringa Bi  Amina  Masenza  akikabidhi  mgao wa  madawati hayo kwa  wakurugenzi wa Halmashauri   hizo leo  zoezi  lililofanyika kwenye  karakana na  chuo  cha  ufundi  stadi  VETA , alisema  kuwa  utekelezaji  wa  agizo  hilo  umefanikiwa  kutokana na  mwitikio mzuri  wa  wananchi  wa  mkoa  huo  na  wadau mbali  mbali wa  maendeleo  ambao  kwa  umoja  wao wamesaidia zoezi hilo  kukamilika .


Alisema  kuwa Rais Dr  Magufuli  alitoa  agizo kwa  wakuu  wote wa  mikoa  nchini kuhakikisha  wanafunzi wote wanakaa katika madawati  ifikapo leo  Juni 30  mwaka  huu na  kuwa  kutokana na agizo hilo alilazimika  kuwashirikisha   wakuu  wake  wa  wilaya  na  wadau mbali  mbali  wakiwemo  wananchi  mmoja  mmoja na  kila  mmoja kwa  uwezo  wake  aliweza  kuchangia madawati hadi  kufanikisha  zoezi hilo.


Mkuu  huyo  alisema kwa Halmashauri za  mkoa wa  Iringa zimetengeneza madawati  kupitia  bajeti  zake  na  wadau  waliopo kwenye  Halmashauri   husika  na  kuwa  hadi sasa  mkoa   umetekeleza  kutengeneza madawati hayo 21,304 wakati  madawati 3665  huku   madawati  8,163 kwa  ajili ya  shule za msingi  wakati  madawati  1,264  ya  shule za  sekondari  yanaendelea  kutengenezwa  katika karakana  mbali mbali   na  fedha  kwa  ajili ya matengenezo hayo  tayari  zimelipwa .

Hivyo  alisema  madawati  yanayoendelea kutengenezwa  yanatarajiwa   kukamilika July 15 mwaka  huu kwani  yamechelewa  kukamilika  kutokana  na  wakandarasi wanaotumika  kutengeneza  madawati  hayo  kuwa na kazi  nyingi .Bi Masenza  alisema  kuwa  ofisi  yake  kwa  kushirikiana na  wadau  mbali mbali imeweza kutengeneza  madawati 700 kwa  lengo la  kuunga mkono  jitihada za  Halmashauri za kumaliza tatizo  la  madawati mapema ,ambayo yamegawiwa  katika Halmashauri tano za  mkoa wa  Iringa ambazo ni Iringa Manispaa madawati 200, Mji Mafinga  madawati 100 ,Halmashauri ya Iringa madawati 100 ,halmashaur i ya  Mufindi madawati 100 na  Kilolo madawati 100

Wakati  madawati  308 yanaendelea   kutengenezwa  katika karakana ya  VETA  pindi yatakapokamilika  yatafikisha idadi ya madawati 1,008  jumla ya  fedha  ambazo zimetumika  kutengeneza  madawati  hayo 1,008 ni milioni 50,400,000 na  baada ya madawati  yote  kukamilika   kutengenezwa mkoa  wa Iringa hautakuwa na  upungufu wa madawati  kwa  wanafunzi  zaidi ya  kuwa na ziada ya madawati .


Mkoa  wa  Iringa  una jumla ya   shule  za msingi 478 na  shule za  sekondari 107zinazomilikiwa na  serikali  na  mkoa  huo  ulikuwa na  upungufu wa madawati 29,347  ikiwa ni madawati 26,046 ya  shule  za Msingi na madawati  3301 kwa  shule za  sekondari.

Magazeti ya Leo Alhamisi

PUMA SASA TUMEINGIA MJINI IRINGA KWA UBORA HALISI WA MAFUTA

Tunapatikana  Ipogolo  barabara  kuu  ya Dar , Mbeya  lango la  kuingia mjini Iringa  tupo  masaa 24  kwa  huduma  bora  ya  mafuta  tembelea  leo