Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

May 31, 2016

MKOA WA SINGIDA KUUNGANISHWA NA CHINA

 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida Bi Martha Mlata  akimpongeza mwakilishi wa  balozi wa China Nchini baada  ya kutoa msaada wa madawati wilaya ya Iramba
..................................................................................................
 
CHAMA   cha mapinduzi (CCM) mkoa  wa Singida  kimempongeza Balozi  wa China nchini Tanzani Dr Lu Yong,ng kwa kuahidi kujenga mahusiano ya  kimaendeleo kati ya mkoa wa Singida na mkoa moja wapo  wa China .

Mwenyekiti  wa CCM mkoa  wa Singida Bi Martha Mlata alitoa pongezi   hizo kwa  balozi wa China juzi  mara baada ya balozi   huyo  kutembelea ofisi  ya CCM mkoa kabla ya  kuelekea wilayani Iramba kutoa msaada wa madawati na kutembelea maeneo yanayolima zao la Alizeti

Bi Mlata  ambae  pia  ni mbunge wa  viti maalum mkoa  wa Singida alisema  kuwa ziara ya balozi  huyo wa China katika wilaya ya Iramba imekuwa na mafanikio makubwa ya  kihistoria kwa mkoa mzima  wa Singida kutokanana balozi  kukubali kujenga mahusiano ya  kiuchumi kati ya China na mkoa  wa Singida.

Akizungumza na  wananchi  wa  kijiji  cha Ndago kwenye Hafla ya  kukabidhi  mgao wa   madawati 400 yaliyotolewa na ubalozi wa China na wadau  wake , Bi Mlata  alisema  kuwa kuanzishwa kwa  ushirikiano  huo  kutafungua milango ya kielimu ,uchumi na maendeleo  mengine kwa mkoa  wa Singida .

"Kwa  kuwa  balozi ameahidi  kutafuta  mkoa moja   wapo  wa nchi ya China ambao tutakuwa na urafiki nao kwa  maana  ya  kutembeleana ......huu ni mwanzo  mzuri  wa  watoto wetu kutoka  Singida kwenda China  kusoma na watoto wa China  kuja  Singida kusoma ila ni fursa kwa wachina  kuja  kuwekeza hapa kwetu na sisi kwenda  kuwekeza kwao"

Hata   hivyo  alisema pamoja na ahadi hiyo yua balozi wa  china kwa  mkoa wa Singida  kutafutiwa mkoa rafiki nchini China bado  balozi   huyo ameahidi  kusaidia kuanzisha Nasari za miche  ya  miti kwa ajili ya kugawa kwa  wananchi bure ili  kupanda  katika  maeneo  yao.

Kwa upande  wake  waziri  wa Kilimo ,Mifugo na uvuvi Bw Mwigulu  Nchemba ambae ni mbunge wa jimbo la Iramba pamoja na kushukuru jitihada  mbali mbali za nchi  ya  China kwa wilaya  ya Iramba na Taifa bado aliwataka  wananchi wa Iramba  kujikita katika  kilimo  cha Miti kama zao  jingine la biashara .

Kwani  alisema amepata  kuzunguka maeneo mbali mbali ya nchi  hii ukiwemo  mkoa  wa Njombe na Mkoa wa Iringa sehemu  kubwa ya wananchi  waliofanikiwa kiuchumi ni wakulima wa miti .

Hivyo  alishauri  wananchi wa wilaya ya Iramba na mkoa wa Singida  pamoja na kuendelea  kulima mazao waliyoyazoea ya chakula pia  wajikite katika kilimo cha miti ambayo baada ya miaka 10 utajiri wake ni mkubwa  zaidi.

MWISHO

RAIS WA WACHIMBA MADINI AJITOSA RASMI KUMSAIDIA RAIS DR MAGUFULI ........ Rais  wa  shirikisho la  wachimbaji madini Tanzania (FEMATA ) Bw  John Bina  akitambulishwa  mbele ya  balozi wa China nchini (hayupo pichani) kulia ni waziri wa Kilimo ,Mifugo na uvuvi Bw Mwigulu Nchemba
 Bw  John Bina  akihamasisha uchangiaji wa madawati  mashuleni


  balozi  wa Chini Nchini Tanzania Dr Lu  Yonq.ng  katikati  akiwa na viongozi wa mkoa wa Shingida  kutoka  kulia mkuu wa  mkoa wa Singida Bw Methew Mtigumwe,waziri wa  kilimo ,Mifugo na Uvuvi Bw Mwigulu Nchemba ,mbunge wa  viti maalum mkoa wa Singida Bi Martha Mlata  na Rais wa FEMATA Bw John Bina

Na MatukiodaimaBlog ,

RAIS wa shirikisho la vyama vya   wachimbaji    madini Tanzania (FEMATA) ametoa wito kwa wachimbaji wote  yakiwemo makampuni makubwa ya uchimbaji   wa madini  kujitokeza kumuunga mkono  Rais Dr John Magufuli   katika harambee ya kuchangia madawati kwa shule mbali mbali hapa nchini.

Huku akisifu  mwitikio mzuri  wa kampuni ya Sunshine Minning  kwa  kuunga kuitikia wito  huo kwa  kuchangia madawati 100 yenye thamani ya Tsh milioni 85,000 kwa Halmashauri ya wilaya ya Iramba mkoani Singida  .

Akizungumza na  waandishi wa  habari jana ,Rais  wa FEMATA  John Bina alisema  kuwa Shirikisho  lake  limelazimika  kumsaidia Rais Dr Magufuli kuhamasisha uchangiaji wa madawati  kwa  wanachama  wake ili kumaliza kabisa tatizo  hilo la uhaba  wa madawati  na  kuona   sekta ya  elimu nchini  inaboresheka  zaidi  kwa   kuhakikisha  wanafunzi  hawakai chini.

Bw Bina  alisema  kuwa katika   kuunga mkono  jitihada za  serikali wao kama sehemu ya  wadau wa maendeleo katika Taifa hawakupenda  kuwa  nyuma kujitokeza  kuchangia madawati hasa  ukizingatia  kuwa elimu  bora  ni mwanzo wa  kuwa na taifa  bora .

"Suala   hili la elimu si la  serikali pekee kila mmoja kwa nafasi yake ana umuhimu katika  kuboresha  elimu  nchini  na si  vema  kwa  kila  jambo  kuitazama  serikali ......serikali  ina  nafasi yake  ila  na sisi  wadau  tuna nafasi  yetu katika  kuiunga mkono serikali pia  wanafunzi  wananafasi yao .... walimu na  wazazi  pia " alisema rais Bina

Hata   hivyo  aliwataka   wadau  wengine  na  wananchi  mmoja  mmoja kwa nafasi yake  kujitokeza kuunga mkono uchangiaji wa madawati  ili  kumaliza kabisa kero  hiyo ya  uhaba wa madawati  mashuleni.

Alisema  wao kama wadau  wa maendeleo  kupitia FEMATA wataendelea  kuunga mkono  jitihada  mbali mbali  zinazoendelea  kufanywa na serikali ya Rais Dr Magufuli  jitihada  zenye  lengo la  kulifanya Taifa   kuzidi  kuwa mbele  kimaendeleo.

Pia  alisema  kwa wadau  wa  sekta   hiyo ya madini  pekee  kama  kila mmoja atajitolea  kuchangia madawati  upo  uwezekano mkubwa wa  zoezi   hilo kukamilika mapema   zaidi na kuwataka  wadau  wengine   mbali ya wale wa madini  nao kwa nafasi  zao  kujitolea madawati  badala ya  kuiachia  serikali pekee.

“ Ninakusudia  kama  Rais  wa FEMATA  kuwakutanisha  wachimbaji  wote mbali na mambo mengine  tutaangalia  ushiriki  wetu katika masuala  ya kijamii yakiwemo ya uchangiaji wa madawati”

Hata   hivyo mkuu  wa  mkoa  wa  Singida Bw Methew Mtigumwe mbali ya  kupongeza harakati  za Rais  huyo wa FEMATA  kwa  kuunga mkono agizo la rais kwa  kujitolea  kuhamasisha uchangiaji wa madawati  bado  alisema  kuwa jambo  hilo ni  jema na linapaswa  kupongezwa zaidi.

Alisema katika mkoa  wa Singida  kila mkuu wa  wilaya ameagizwa  kusimamia utekelezaji wa agizo la Rais la upungufu wa madawati katika eneo lake na  kuwa mkoa umejipanga  kumaliza kabisa  kero  hiyo ya uhaba wa madawati .
MWISHO

KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA LEO


 Baadhi ya mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao nchini Tanzania wakielekea ndani ya Ukumbi wa Bunge leo kusikiliza Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.


Waziri wa Elimu, Sayansi na Mafunzo ya Ufundi Prof. Joyce Ndalichako akisalimiana na Mbunge wa Afrika Mashariki Mhe. Shy-Rose Bhanji nje ya Ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma.


Mbunge wa Mafinga Mjini Mhe. Cosato Chumi akichangia kuhusu Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki iliyowasilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Augustine Mahiga leo mjini Dodoma.


Baadhi ya Mawaziri wakifuatilia michango mbalimbali ya wabunge wakati wa mjadala wa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki iliyowasilishwa leo mjini Dodoma.


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akizungumza jambo na Mbunge wa Iringa Mjini Mhe. Peter Msigwa nje ya Ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma.Wengine ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Augustine Mahiga(kushoto) na Madiwani wa jimbo la Iringa Mjini waliolitembelea Bunge.


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimweleza jambo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano Mhe. Januari Makamba nje ya Ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma.


Wabunge kutoka mkoa wa Iringa Mhe. Augustine Mahiga, Mhe. William Lukuvi na Mhe. Peter Msigwa wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya madiwani wa Iringa mjini waliolitembelea Bunge leo mjini Dodoma.


Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson akiwasikiliza waangalizi wa Uchaguzi Mkuu kutoka Umoja wa Nchi za Ulaya (EU) waliofika Ofisini kwake kuwasilisha Taarifa ya Umoja huo kuhusu Uchaguzi Mkuu uliofanyika nchini Oktoba 25, 2015.

Waangalizi wa Uchaguzi Mkuu kutoka Umoja wa Nchi za Ulaya (EU) wakizungumza na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson (hayupo pichani) ofisini kwake Dodoma.
 Balozi wa Umoja wa Ulaya Mhe. Roeland Van De Geer (kulia) akimkabidhi Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson Taarifa  ya Miradi inayotekelezwa na Umoja wa Ulaya nchini Tanzania.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson (kulia) akizungumza jambo na Waangalizi wa Uchaguzi kutoka Umoja wa Ulaya Mhe. Judith Sargentini (kushoto) na Balozi wa Umoja huo  Mhe. Roeland Van De Geer (katikati) waliofika Ofisini kwake Dodoma leo.
 Mwangalizi Mkuu wa Uchaguzi kutoka Umoja wa Ulaya Mhe. Judith Sargentini akimkabidhi Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson Taarifa ya Uchaguzi ya Waangalizi wa Umoja wa Ulaya (EU) kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Tanzania uliofanyika Oktoba 25, 2015. Hafla hiyo imefanyika leo mjini Dodoma.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Waangalizi wa Uchaguzi  kutoka Umoja wa Nchi za Ulaya (EU) waliomtembelea Ofisini kwake leo mjini Dodoma.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Augustine Mahiga akisalimiana na Mabalozi wa nchi mbalimbali nje ya Ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Augustine Mahiga akiwa katika picha ya pamoja na Waziri Kivuli wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mabalozi wa nchi mbalimbali nje ya Ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma.

PICHA/Aron Msigwa na Fatma Salum.