April 30, 2016

BREAKING NEWS WATUHUMIWA WAWILI WA UJAMBAZI WALIOUA NJOMBE WAUWAWA IRINGA MUDA HUU

WATU wawili wanaosadikika kuwa ni majambazi ambao wametokea Njombe wameuwawa katika majibizano ya risasi na polisi baada ya kuvamia Pub ya Mama Siyovelwa iliyopo eneo la mtaa wa Ikulu mjini Iringa
Tukio hilo limetokea majira ya saa 10:45 jioni ya leo baada ya watu hao kuvamia Pub hiyo kwa lengo la kupora kabla ya raia wema kutoa taarifa polisi
Baadhi ya mashuhuda waliokuwepo eneo hilo waliueleza mtandao huu wa matukiodaimaBlog kuwa watu hao walihofiwa mapema wakati wa kuingia eneo hilo ambapo inadaiwa walikuwa watatu na mmoja alijichanganya na Raia na kujificha.
Kazi kubwa iliyofanywa na polisi imefanikisha watu hao wawili waliokuwa na silaha kuuwawa bila raia wengine kujeruhiwa 
Miili miwili ya watu hao wanaosadikika ni majambazi ambao baada ya kupekuliwa wamekutwa na tiketi za basi la Hapy National kutoka Njombe imepelekwa hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa
Taarifa zaidi utazidi kuzipata japo Njombe kuna mauwaji ya kutumia silaha ambayo yalitokea jana

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE