Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

March 30, 2016

March 28, 2016

IDADI YA VIFO AJALI YA BASI IRINGA YAFIKIA 6 MAJERUHI 36,ASAS ATOA MSAADA WA DAWA KWA MAJERUHI WOTE

Majeruhi  wa ajali   Bi Janeth Raia  wa Rwanda  akiwa na mtoto  Ishine Jasmin ambae  pia  Raia wa Rwanda aliyepoteza mamake  mzazi katika ajali  hiyo
Mkuu  wa  wilaya ya  Iringa Bw  Richard  Kasesela  akiwa amejitwisha   kichwani  dawa  zilizonunuliwa na mwenyekiti  wa kamati ya usalama barabarani mkoa  wa Iringa Bw  Salim Asas  dawa  zenye thamani ya zaidi ya Tsh milioni 3  kwa ajili ya majeruhi wa ajali ya basi  la lenye  namba  za  usajili    T 798 AKV mali ya Lupondije Express ambalo  lilipata ajali mjini  Iringa usiku wa jana na kuua  watu 6 na kujeruhi  zaidi ya 36(picha na matukiodaimaBlog )

Mkuu  wa  wilaya ya  Iringa Bw  Richard  Kasesela  (kulia )  akiwa  na mkuu  wa mkoa  wa Iringa Bi Amina Masenza  wa  kwanza  kushoto na mwenyekiti  wa kamati ya  usalama  barabarani Bw  Salim Asas wakimsaidia mmoja kati  ya majeruhi  wa ajali hiyo Bi Sarafina Mkagasana  Rai wa  Rwanda ambae  alikuwa  mmoja kati ya majeruhi wa ajali  hiyo Bi Sarafia amempoteza  ndugu  yake Janeth Mkashena  katika ajali  hiyo (picha na MatukiodaimaBlog)

 Mwenyekiti wa kamati ya  usalama barabarani mkoa  wa Iringa  Bw  Salim Asas  akimjulia hali majeruhi  Sarafina  Mkagasana Raia wa aliyelazwa katika  Hospitali ya Rufaa ya  mkoa  wa Iringa baada  ya kupata ajali ya basi lenye  namba  za  usajili    T 798 AKV mali ya Lupondije Express aliyekuwa amelazwa Hospitalini hapo (picha na matukiodaimaBlog)
Mwenyekiti wa kamati ya   usalama barabarani mkoa  wa Iringa  Bw  Salim Asas kulia akiwa na mkuu  wa wilaya ya  Iringa Bw Richard Kasesela  kushoto  wakisaidia  kupakia  dawa zilizonunuliwa na kamati ya  usalama barabarani kwa ajili ya majeruhi wa ajali  ya basi
 lenye  namba  za  usajili    T 798 AKV mali ya Lupondije Express (picha na MatukiodaimaBlog)
 
WANANCHI  wa Manispaa ya  Iringa mkoa  wa Iringa washerekea Pasaka kwa kwa majonzi kufuatia vifo  vya watu  sita   waliokufa   papo  hapo akiwemo aliyekuwa mgombea uenyekiti  wa UVCCM mkoa  wa Iringa Makka Msigwa na  wengine  zaidi ya 20 kujeruhiwa  vibaya  baada  ya  basi lenye  namba  za  usajili    T 798 AKV mali ya Lupondije Express Kutoka  Mwanza kuja  Iringa  kupinduka  eneo la  Mteremko  wa Ipogolo  mjini  Iringa  wakati basi hilo   likielekea  kufaulisha  abiria  wa  Mbeya.Imeelezwa   kuwa baadhi ya  abiria    waliokufa  katika  ajali   hiyo na  majeruhi   ni  wale ambao   walitakiwa   kushuka stendi kuu ya mabasi  ya mabasi  yaendaye  mikoani mjini Iringa ila dereva  wa basi aligoma   kuwashusha  stendi na  kupitiliza nao  kwenda Ipogolo    kufaulisha abiria  wa Mbeya  kwanza  ndipo arudi   kuwashusha  stendi.Ajali   hiyo  imetokea  majira ya  saa 3 usiku wa Pasaka  baada ya  basi  hilo  kufeli  breki katika  mteremko  huo huo mkali kabla ya  kupinduka .Wema  Zuberi  ni  mmoja kati ya majeruhi  wa ajali  hiyo aliyekuwa ametoka mkoani  Dodoma  kuelekea  Mbeya  alimweleza  mwandishi  wa habari hizi    kuwa  mwendo  wa  basi hilo  toka  amepanda  Dodoma  kuja  Iringa  haukuwa  mkali  sana   ulikuwa ni  mwendo wa kawaida .Japo  alisema  kuwa   baada ya  kuingia  mjini  Iringa katikati ya  mji  ndipo dereva  wa basi   hilo alionyesha  kuendesha basi   hilo kwa mwendo mkali  zaidi  kiasi  cha  baadhi ya  abiria  kulalamika mwendo huo na  kutaka   kushushwa ila dereva  hakuweza  kusikia zaidi ya  kuwapuuza  abiria  hao.“Abiria  wengi   walionyesha   kumlalamikia   dereva   huyo kwanza  kutokana na  kuwapitiliza  stendi pasipo  kuwashusha na pili mwendo  kasi ambao  alikuwa  akienda nao   ili  kufanikisha  kutufaulisha abiria  tuliokuwa   tukielekea  Mbeya “Alisema kabla ya  kufika  eneo  hilo ambalo  basi  lilipinduka kuna kona kali na mteremko  mkali  na kilichoonekana haraka  haraka ni  dereva   kushindwa kukata  kona   hiyo baada ya Breki  kufeli   na   hivyo  kulazimika  kuhama  njia  na  kugonga kingo za  barabara  hiyo na  kupinduka .

Mkuu  wa  wilaya ya  Iringa  Bw  Richard Kasesela akizungumza na  mwandishi  wa  habari  hizi eneo la   tukio alisema  kuwa zoezi la  kuendelea  kutafuta  miili  iliyobanwa na basi  hilo imekuwa  ngumu  kutokana na kukosekana  kwa gari la kuinua  basi hilo na  tayari  amemwagiza  meneja  wa Tanesco kuleta  gari  hilo na  iwapo  dereva   hayupo  basi kuamka  na  kuendesha  mwenyewe .Hata   hivyo  alisema  kuwa kuanzia   sasa  dawa  ya  madereva  hao  ni  kuwashughulikia kwani kama Rai imekwisha   tolewa  mara  nyingi na  bado  ajali  zinaendelea   kutokea.

Kamanda   wa  polisi  wa mkoa  wa Iringa  Bw  Peter Kakamba  ambae  pia  alikuwepo  eneo la  tukio kusaidia  kuokoa majeruhi na kutoa maiti katika basi hilo  pamoja na mkuu  huyo  wa  wilaya wananchi  mbali mbali walioongozwa na askari  polisi ,alisema  kuwa  watu  watano  watu 6  wamepoteza maisha katika ajali  hiyo  huku  majeruhi ni 38 kati yao 11  wameruhusiwa Hospitali

Alisema   kuwa  jeshi la  polisi  linamshikilia  dereva wa basi hilo Kastory Mwalusako (35) mkazi  wa Mbeya ambae baada ya ajali  alijisalimisha  polisi na kuwa atafikishwa mahakamani  wakati  wowote kuanzia  sasa .

Wakati 

Wakati  huo  huo serikali ya  mkoa  wa Iringa  imeipongeza kamati ya  usalama  barabarani mkoa  wa Iringa  chini ya mwenyekiti  wake  Salim Asas kwa  kujitolea msaada wa dawa  za  kuwatibu  majeruhi  wote wa ajali ya basi   hilo.


Mkuu  wa mkoa  wa Iringa  Bi Amina Masenza  alitoa pongezi hizo jana baada ya  kupokea msaada wa dawa  hizo  kutoka kwa  mwenyekiti Bw  Asas kuwa  kamati hiyo  imeonyesha   upendo  mkubwa kwa  majeruhi hao  huku akitaka dawa  hizo kutumika vizuri na  kuhakikisha  zinawanufaisha  majeruhi hao.

Huku kwa upande wake  mwenyekiti wa kamati   hiyo ya usalama barabarani Bw  Asas  mbali ya  kuwapa pole  majeruhi  hao bado  aliwataka  abiria  kutoa ushirikiano kwa  jeshi la  polisi kwa  kutoa taarifa  haraka  pindi  dereva anapo  kuwa anaendesha gari  bila  kuzingatia  sheria  za usalama barabarani na  kuwa iwapo basi hilo  lingeshusha abiria  stendi yawezekana kusingetokea  madhara makubwa  hivyo kwani basi hili lilikuwa  limefika salama Iringa mjini ila dereva  aliendeleza safari ambayo kimsingi haikuwepo .


AJALI YA BASI LA LUPONDIJE EXPRESS KUTOKA MWANZA - IRINGA YAUA USIKU HUU IRINGA , DEREVA ALIKUWA AKIENDA KUFAULISHA ABIRIA WA MBEYA ...................

 Askari   polisi na  wasamaria  wema  wakisaidia  kutoa maiti  kutoka katika  basi la Lupondije Express namba T 798 AKV kutoka Mwanza - Iringa baada ya  kupinduka  eneo la Mteremko wa Ipogolo mjini Iringa usiku  wa  leo
 Gari la kikosi  cha  Zimamoto na uokoaji  likiwa  eneo la  tukio  kusaidia  kuokoa maisha ya majeruhi Mkuu  wa  wilaya ya  Iringa Bw  Richard  Kasesela   kushoto  akiwa na kamanda wa  polisi mkoa  wa Iringa Bw Peter Kakamba  wakisaidia  kuokoa  majeruhi na kutoa maiti


WATU  zaidi ya   wane  wakufa  papo  hapo na  wengine  zaidi ya 20 kujeruhiwa  vibaya  baada  ya  basi lenye  namba  za  usajili    T 798 AKV mali ya Lupondije Express Kutoka  Mwanza kuja  Iringa  kupinduka  eneo la  Mteremko  wa Ipogolo  mjini  Iringa  wakati basi hilo   likielekea  kufaulisha  abiria  wa  Mbeya.


Imeelezwa   kuwa baadhi ya  abiria    waliokufa  katika  ajali   hiyo na  majeruhi   ni  wale ambao   walitakiwa   kushuka stendi kuu ya mabasi  ya mabasi  yaendaye  mikoani mjini Iringa ila dereva  wa basi aligoma   kuwashusha  stendi na  kupitiliza nao  kwenda Ipogolo    kufaulisha abiria  wa Mbeya  kwanza  ndipo arudi   kuwashusha  stendi.


Ajali   hiyo  imetokea  majira ya  saa 2 usiku baada ya  basi  hilo  kufeli  breki katika  mteremko  huo huo mkali kabla ya  kupinduka .


Wema  Zuberi  ni  mmoja kati ya majeruhi  wa ajali  hiyo aliyekuwa ametoka mkoani  Dodoma  kuelekea  Mbeya  aliueleza mtandao  huu  wa matukiodaima Blog   kuwa  mwendo  wa  basi hilo  toka  amepanda  Dodoma  kuja  Iringa  haukuwa  mkali  sana   ulikuwa ni  mwendo wa kawaida .


Japo  alisema  kuwa   baada ya  kuingia  mjini  Iringa katikati ya  mji  ndipo dereva  wa basi   hilo alionyesha  kuendesha basi   hilo kwa mwendo mkali  zaidi  kiasi  cha  baadhi ya  abiria  kulalamika mwendo huo na  kutaka   kushushwa ila dereva  hakuweza  kusikia zaidi ya  kuwapuuza  abiria  hao.


“Abiria  wengi   walionyesha   kumlalamikia   dereva   huyo kwanza  kutokana na  kuwapitiliza  stendi pasipo  kuwashusha na pili mwendo  kasi ambao  alikuwa  akienda nao   ili  kufanikisha  kutufaulisha abiria  tuliokuwa   tukielekea  Mbeya “


Alisema kabla ya  kufika  eneo  hilo ambalo  basi  lilipinduka kuna kona kali na mteremko  mkali  na kilichoonekana haraka  haraka ni  dereva   kushindwa kukata  kona   hiyo baada ya Breki  kufeli   na   hivyo  kulazimika  kuhama  njia  na  kugonga kingo za  barabara  hiyo na  kupinduka .


Mkuu  wa  wilaya ya  Iringa  Bw  Richard Kasesela akizungumza na  mwandishi  wa  habari  hizi eneo la   tukio alisema  kuwa zoezi la  kuendelea  kutafuta  miili  iliyobanwa na basi  hilo imekuwa  ngumu  kutokana na kukosekana  kwa gari la kuinua  basi hilo na  tayari  amemwagiza  meneja  wa Tanesco kuleta  gari  hilo na  iwapo  dereva   hayupo  basi kuamka  na  kuendesha  mwenyewe .


Hata   hivyo  alisema  kuwa kuanzia   sasa  dawa  ya  madereva  hao  ni  kuwashughulikia kwani kama Rai imekwisha   tolewa  mara  nyingi na  bado  ajali  zinaendelea   kutokea.


Kamanda   wa  polisi  wa mkoa  wa Iringa  Bw  Peter Kakamba  ambae  pia  alikuwepo  eneo la  tukio kusaidia  kuokoa majeruhi na kutoa maiti katika basi hilo  pamoja na mkuu  huyo  wa  wilaya wananchi  mbali mbali walioongozwa na askari  polisi ,alisema  kuwa hadi majira  ya saa 5 usiku wakati tunakwenda mitamboni bado ilikuwa ni  mapema  kuweza kujua  ni  watu  wangapi    wamepoteza maisha  kwani  zoezi  lilikuwa  bado  linaendelea.Kamanda huyo aliahidi  kutoa  taarifa mara  tu zoezi hilo  litakapokamilika kwa kuinua  basi hilo na kutazama kwa  kina kama kuna  miili ambayo  imefunikwa   chini ama lah.


Mwandishi  wa habari  hizi  alishuhudia  miili  minne ikiwa tayari  imetolewa katika basi hilo huku majeruhi   wengi  wakiwa   wamepata majeraha  makubwa  mikononi ,miguuni na kichwani,Majeruhi  wa ajali   hiyo wamelazwa Hospitali ya  Rufaa ya  mkoa  wa Iringa 


Habari  zaidi  tutaendelea  kukujuza endelea   kutembelea www.matukiodaima.co.tz

March 27, 2016

ASKOFU DR MDEGELA ATAKA WATANZANIA KUENDELEA KUMWOMBEA RAIS DR MAGUFULI NA RAIS AJAYE .....................


 Askofu  Dr Mdegela  
 ..........................................................................................................................................................
Na MatukiodaimaBlog

ASKOFU   wa Kanisa la Kilutheri (KKT) dayosisi ya Iringa Dkt. Owdenburg Mdegela amewataka   watanzania  kuendelea  kumwombea  Rais Dr John Magufuli kuendelea  kuwatumikia  watanzania kwa kasi yenye mafanikio yenye maslahi  kwa  watanzania   wote pia kumwombea Rais ajaye mwaka 2020 ili  aongoze nchi kama  Rais Dr Magufuli .

Askofu Dr Mdegela aliyasema  hayo   wakati  akitoa    salam  za Pasaka   katika  usharika  wa Iringa  mjini leo  ,kuwa pamoja na  kuwa  wakati wa Taifa  likiwa katika  mchakato  wa  kumtafuta Rais wa awamu ya tano  baada ya  Rais Jakaya  Kikwete  kumaliza muda  wake mara  zote  alikuwa akitaka  watanzania kufanya mabadiliko na kuwa mabadiliko ambayo alikuwa akiyaomba   sio  ya  kuiondoa  CCM madarakani   wala  ya UKAWA ila  alikuwa akiomba nchi  kupata  kiongozi mwenye kuleta maendeleo kama  anavyofanya  Rais Dr Magufuli .

" Mara   zote  lilikuwa  nikiomba mabadiliko  ila  baadhi  ya  watu   walianza  kuninyoshea kidole   kuwa labda  mimi ni  UKAWA ila  ukweli sikuwa UKAWA wala chama  chochote  cha  siasa  ....haya  anayofanya  leo Rais Dr Magufuli  ndio mabadiliko ambayo  mimi  nilikuwa nikitamani  kuona Tanzania tunampata  kiongozi kama  yeye" alisema  Askofu  Dr  Mdegela


 Alisema  kuwa suala  la  mabadiliko ambayo  alikuwa  akitamani  kuona  halina   uhusiano  wowote na  UKAWA  ila mabadiliko aliyokuwa  akiomba  ni kuona raslimari za Taifa  zinawanufaisha    watanzania   wote na  Rais anakuwa  mbele  kupigania hayo na  si  vinginevyo

Hivyo  alitaka   wqatanzania   wote  kuendelea  kumwombea  Rais Dr Magufuli  na  viongozi  wengine  ili  kulitumikia Taifa  kwa  faida ya  watanzania   wote kama  anavyofanya Rais  Dr Magufuli ambaye  kwa  sasa  kila mtanzania  mpenda maendeleo anaona na  kupongeza utendaji kazi  wake.


"  Ninasema kwa  moyo  wa  dhati kabisa   naombeni  wote   tumuombee  sana  Rais Dr  John Magufuli ili  aweze  kuliongoza  Taifa  kwa  kasi hii  hata  kama  miaka  10  mbele aweze kuongoza Taifa  kwa kasi hii ....pia tumwombee  hata Rais ajaye baada ya  miaka 10  mbele ili aendeleze mazuri  hayo ya Rais Dr Magufuli "

 Hata    hivyo alisema  kuwa  Tanzania inafanikiwa   kuwa na amani  hii  kutokana na maombi ya  Watanzania  na  wasio  watanzania   na kuwa hakuna hata  chama  kimoja  cha  siasa ambacho  kinaweza kujisifu kuwa ndicho  kimefanikisha amani  hii   hivyo  alitaka  watanzania  kuendelea  kuomba kwa nguvu  zote  kwa  kila mmoja kwa  dini  yake  ili amani   izidi  kudumu .

MWISHO

March 26, 2016

Mgombea uwakilishi Marekani William Jawando ahojiwa Kilimanjaro Studio, azungumza na Diaspora

Mgombea uwakilishi katika Bunge la Marekani William Jawando, leo alihojiwa katika studio za Kilimanjaro zilizopo Beltsville, Maryland nchini Marekani ambapo alizungumzia kuhusu mikakati yake katika kuisaidia diaspora ya Afrika katika eneo lake na Marekani kwa ujumla.
Will, ambaye akishinda atakuwa ni mtu wa pili aliyezaliwa na Baba aliyetoka Afrika kuingia bungeni humo (baada ya Rais Obama) ameeleza mambo mengi ikiwa ni pamoja na namna ambavyo uchaguzi mkuu wa mwaka huu ni muhimu Zaidi nchini Marekani, na hasa kwa wakazi wenye asili ya Afrika waishio vitongoji vya Washington DC.
Ikumbukwe kwamba, inakadiriwa kuwa mmoja kati ya wazaliwa kumi wa Afrika walipo nchini Marekani, anaishi eneo hili, na nusu yao, wameingia nchini baada ya mwaka 2000. Hivyo amefafanua namna ambavyo kuwa na mtu mwenye kuelewa na kuwakilisha vema jamii hiyo, ni muhimu kwa jamii hiyo.
Aligusia pia namna ambavyo asili yake na makuzi yake yamechangia yeye kuingia katika kazi za kuihudumia jamii, akaeleza vipaumbele vyake kwenye uongozi wake ujao na pia wito alionao kwa jamii ya waAfrika walioko Marekani.
Uchaguzi wa kuteuliwa kugombea kupitia chama cha Democrat utafanyika Aprili 26, lakini kura za mapema zitapigwa kati ya Aprili 14 na 21.
Kujua mengi kuhusu Will Jawando, maisha yake, kampeni na mipango yake, tembelea willjawando.com
Anagombea kiti kilichoachwa wazi na mwakilishi Chris Van Hollen ambaye ameamua kugombea kiti cha Seneti kinachoachwa wazi na Seneta Barbara Mikulski anayestaafu
Mahojiano kamili na Will Jawando yatakujia hivi karibuni
Baada ya mahojiano, Will alipata nafasi ya kuzungumza na baadhi ya wanaDiaspora wa Afrika waliokuwa ndani ya jengo ilipo studio.
Mgombea uwakilishi kutoka jimbo la Maryland, Will Jawando akipata picha na Mubelwa Bandio baada ya mahojiano
Mgombea uwakilishi kutoka jimbo la Maryland, Will Jawando akizungumza na baadhi ya waAfrika waliohudhuria "Meet & Greet"

SPIKA WA BUNGE AKUTANA NA MKURUGENZI MKUU WA BUNGE LA ISRAEL

16
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na  Mkurugenzi Mkuu wa Bunge la Israel, Ronen Plot (wa kwanza kulia) aliyemtembelea Ofisini kwake leo tarehe 26 Machi, 2016,Jijini Dar es Salaam.
17Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Bunge la Israel, Ronen Plot  aliyemtembelea Ofisini.
18  Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akimkabidhi zawadi Mkurugenzi Mkuu wa Bunge la Israel, Ronen Plot  aliyemtembelea Ofisini.20Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na Mzee Ibarahim Kaduma ambaye ni Mweyekiti wa Kingdom Leadership Network Tanzania (KLNT). Mzee Kaduma aliambatana na Ujumbe wa Israel uliomtembelea Spika ambao ndio wafadhili wa KLNT.
19Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Bunge la Israel, Ronen Plot  na viongozi wengine waliombatana na ujumbe huo.
(Picha na Ofisi ya Bunge)

Walioteuliwa Kupata Uteuzi wa Wajumbe Wanawake Katika Baraza la Wawakilishi

index
 1. Ndugu Salama Aboud Talib
 1. Ndugu Shadya Mohamed Suleiman
 1. Ndugu Bihindi Hamad Khamis
 1. Ndugu Salma Mussa Bilali
 1. Ndugu Mwanaidi Kassim Mussa
 1. Ndugu Panya Ali Abdalla
 1. Ndugu Mgeni Hassan Juma
 1. Ndugu Zaina Abdalla Salum
 1. Ndugu Salha Mohammed Mwinyijuma
 1. Ndugu Zulfa Mmaka Omar
 1. Ndugu Lulu Msham Abdalla
 1. Ndugu Wanu Hafidh Ameir
 1. Ndugu Saada Ramadhani Mwenda
 1. Ndugu Tatu Mohamed Ussi
 1. Ndugu Amina Idd Mabrouk
 1. Ndugu Choum Kombo Khamis
 1. Ndugu Mtumwa Suleiman Makame
 1. Ndugu Mwantatu Mbaraka Khamis
 1. Ndugu Riziki Pembe Juma
 1. Ndugu Viwe Khamis Abdalla
 1. Ndugu Hamida Abdalla Issa
 1. Ndugu Hidaya Ali Makame

NAIBU WAZIRI LUHAGA MPINA – ASHIRIKI USAFI KATIKA MTAA WA TPDC MIKOCHENI DAR ES SALAAM

21Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina Kulia Akifyeka, katika Mtaa wa TPDC Mikocheni Jijini Dar es Salam leo kutekeleza agizo la Mh. Raisi la kufanya usafi, ambapo serikali imetenga kila Jumamosi ya mwisho wa Mwezi kuwa siku maalum ya usafi.
22Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina, akifanya usafi katika mtaro wa maji machafu katika mtaa wa TPDC, maeneo ya Mikocheni jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa siku ya usafi jumamosi ya mwisho wa mwezi.
23Kulia Bi Blandika Cheche Afisa Mazingira mkuu, na katikati Mkururugenzi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na usimamizi wa mazingira NEMC Bw. Boniventure Baya wakifanya usafi kwa pamoja katika mtaa wa TPDC, Mikocheni Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la serikali, la kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi la kufanya usafi wa mazingira.
25Aliyevaa shati ya blue Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira mh Luhaga Mpina akiweka taka katika gari la kuzolea taka katika mtaa wa TPDC Mikocheni JIjini Dar es salaam leo, Jumamosi ya mwisho wa Mwezi ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Serikali la usafi wa Mazingira .
(Picha zote na Evelyn Mkokoi wa Makamu wa Rais)