Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

February 29, 2016

MBUNGE KILOLO AWASAIDIA WANANCHI WASIOJIWEZA KIJIJI CHA IKOKOTO KUWALIPIA CHF

Mbunge wa  jimbo la Kilolo Bw Venance Mwamoto akiwahutubia  wananchi wa kijiji cha Ikokoto kata ya Ilula wakati wa mkutano wake wa kweanza wa kuanza kuwashukuru wapiga kura kwa kumchagua na kutekeleza ahadi zake alizoahidi wakati wa kampeni
Mbunge wa Kilolo Bw Venance Mwamoto  kulia  akiz\ungumza na  wazee wa kijiji cha Ikokoto ambao  walijitokeza mbele ya mkutano wake  kuomba  kusaidiwa  kulipiwa  fedha  kiasi cha Tsh 10000 ili kuingia katika mfuko wa afya ya jamii (CHF) kwa ajili ya  kutibiwa bure mwaka mzima
Mbunge wa Kilolo mkoani Iringa Bw Venance Mwamoto kulia akiwalipia fedha wazee wasiojiweza wa kijiji cha Ikokoto kwa ajili ya mfuko wea afya ya jamii (CHF) wakati wa mkutano wake kijijini hapo jana
Mwamoto akipongezwa na wazee wa kijiji  cha Ikokoto  baada ya  kusaidiwa kulipiwa CHF


Na MatukiodaimaBlog
WANANCHI  wasio na uwezo wa kifedha  katika  kijiji  cha Ikokoto kata ya Ilula wilaya ya  Kilolo mkoani Iringa wamelipiwa fedha  na mbunge wa  jimbo la Kilolo Venance Mwamoto kwa ajili ya  kuingizwa kwenye mfuko wa afya  ya jamii (CHF).

Hatua   hiyo  ya  wazee  hao  kuingizwa katika mfuko   huo  ilikuja baada ya wazee hao kumwomba mbunge  wao wakati wa mkutano wa hadhara  wa mbunge kwa ajili ya kuwashukuru kwa kumchangua na kuanza kutimiza ahadi zake za ujenzi wa vyumba vya madarasa na  vyoo ambazo alitoa wakati wa kampeni .

Akizungumza baada ya  kuwalipia fedha  kwa  ajili ya  kujiunga na CHF ,mbunge Mwamoto alitaka  wananchi  wote  kujiunga na mfuko   huo na  kuwa suala la kujiunga liwe ni la lazima kwa  wananchi wote  ili kuepuka usumbufu  pindi wanapougua.

Mbunge  huyo alitaka  viongozi wa vijiji na vitongoji  kujiunga na mfuko wa afya ya jamii (CHF) kama njia  mojawapo ya kuwavutia wananchi kujiunga na mfuko huo.Amedai kwamba ni muhimu kwa viongozi kujiunga na mifuko ya afya  ukiwemo  CHF, kwani  watakuwa wanatekeleza sera ya taifa na ilani ya uchaguzi wa CCM.
Alisema  kujiunga na CHF ni kujihakikishia matibabu stahiki kipindi chote hata kile ambacho watakuwa hawana fedha za kulipia matibabu .

Alisema kaya aslimia  chache  sana ambazo wananchi  wake wamejiunga na CHF na baadhi ya  wanasiasa wa upinzani  wamekuwa kikwazo kikubwa kwa  wananchi katika kufanikisha wananchi  kujiunga na CHF 

 “Uelimishaji unahitajika kuanzia ngazi ya vitongoji, vijiji, Kata na Tarafa kwa kufanya mikutano ya kuhamasisha na uelimishaji.....wenyeviti wa vitongoji, watendaji ... ambao bado hawajajiunga na mfuko huu, muoneshe mfano kwa kujiunga”,alisisitiza kwenye hotuba yake iliyosomwa na katibu tawala wa wilaya hiyo " 

Mwamoto  alisema   katika  suala  hilo ni vema wana siasa  kuachana na siasa na kampeni na badala  yake kuelimisha  wananchi faida ya kujiunga na mfuko   huo kwa gharama ya Tsh 10,000 pekee ila matibabu ni mwaka mzima.

February 28, 2016

MWAMOTO APOKELEWA KWA SHANGWE IKOKOTO KATA YA CHADEMA

Mbunge  wa  kilolo Bw Venance Mwamoto akipokelewa kwashangwe na wanafunzi wa shule ya Msingi mjimemwa kijiji cha Ikokoto kata  inayoongozwa na diwani wa Chadema ambae hakushiriki baada ya kufika kusaidia ujezi wa vyoo shuleni hapo