Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

January 31, 2016

AJALI NYINGINE YAUA NI ENEO LA SHIMO LA AJALI YA MAJINJA CHANGARAWE MUFINDI , MABASI YAKWAMA LIKIWEMO LA WACHEZAJI YANGA ....


WACHEZAJI Yanga wakiwa wamekwama Eneo la changarawe Mufindi baada ya lori kugongana na Gari Ndogo na kuziba barabara ya Iringa - Mbeya leo watu watatu wanasadikika kupoteza Maisha ( Picha na matukiodaimablog)
Shuhuda Matukiodaimablog  Bw Jackson akiwa katika Picha ya pamoja na   kocha wa Yanga Hans De Pluijm
 wachezaji wa Yanga wakiongozwa na Simon Msuva (mwenye nywele za kiduku cha kusuka) na Mnyarwanda Haruna Niyonzima(mwenye kapelo iliyogeuka)

Eneo ajali magari yakiwa yamekwama 


Na Matukiodaimablog 

SHIMO lililosababisha ajali ya Basi la Majinga lililoua watu zaidi 50 mwaka jana katika barabara ya Iringa - Mbeya limesababisha ajali nyingine tena kwa watu watatu kusadikika kufariki dunia baada ya lori na gari dogo kugongana

Ajali hiyo iliyotokea leo Majira ya  10 Jioni ilikwamisha pia wasafiri wa mikoa ya nyanda za juu kusini na wale wanaoelekea Dar es Salaa pamoja na basi la Wachezaji wa timu ya Yanga kukwama eneo hilo baada ya magari hayo yaliyopata ajali kuziba njia.

Mmoja kati ya mashuhuda wa ajali hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Jackison Daison aliueleza mtandao huu wa matukiodaima kwa njia ya siku kuwa ajali hiyo imesababishwa na shimo hilo ambalo mwaka jana lilisababisha ajali ya Basi Majinja na Lori

Kwani alisema inaonyesha Lori na gori Ndogo wote walikuwa wakikwepa shimo hilo .

"Lori lilikuwa likiyokea  Mafinga lilikwepa lile shimo likaacha njia yake na kuhamia upande wa pili Gari Dogo aina ya  Hilux lilikuwa likitokea  Mbeya ikahama kumpisha mwenyewe Lori ikahamia upande usio wake na kupaki pembeni..,...kumbe Lori likakata bearing na tela likayumba na kumfuata yule mwenye Hilux Kule upande wa pili alikotulia na kumgonga mbele"alisema Daison 

Kuwa Watu watatu wa kwenye gari ndogo walipoteza maisha  akiwepo dereva japo Mtoto   mtoto mdogo amejeruhiwa 

" Lori  Baada ya kugonga Gari ndogo pia liligonga lori jingine lililokuwa nyuma ya Hilux Halafu likaachana na tela kutumbukia korongoni na  tela kuziba barabara   "

Hata hivyo alisema mbali ya Eneo hilo kuwa ni mteremko Mkali ila bado ubovu wa barabara na uzembe wa madereva ni chanzo cha ajali hiyo.

Hivyo alishauri wakara wa barabara Mkoa wa Iringa kuangalia uwezekano wa kuziba mashimo katika barabara hiyo hasa Eneo la Changarawe hadi Nyololo badala ya kuendelea kuweka mabango ya kuwataka madereva kupunguza mwendo 

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa Peter Kakamba amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuwa tayari amemwagiza RTO kufika Eneo la tukio kwa msaada zaidi japo alisema taarifa za awali alizopokea zilidai kuwa ni mtu mmoja amepoteza Maisha na kuwa anafuatilia zaidi ili kujua idadi ya waliopoteza maisha 

mwisho 


Ban Ki-moon ataka askari watumwe Burundi


Image copyrightAFP
Image captionBan Ki Moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amewaambia viongozi wa Afrika kwamba anaunga mkono pendekezo lao la kutuma askari 5,000 wa kuweka amani huko Burundi.

Alisema hayo katika mkutano wa viongozi wa nchi za AU nchini Ethiopia, ambako viongozi hao watapiga kura kuunga mkono au kukataa pendekezo hilo.

Rais wa Burundi , Pierre Nkurunziza, amelipinga pendekezo hilo - Burundi inasema kutuma wanajeshi huko itaonekana kama uvamizi.

Uamuzi wa rais huyo kugombea muhula wa tatu wa uongozi ndiyo uliozusha ghasia za miezi kadha.

Kiongozi wa Gambia, Yahya Jammeh, ambaye alinyakua madaraka kwa kupindua serikali, alisema hatounga mkono pendekezo hilo iwapo Burundi haitoridhia.

Na rais wa Chad, Idris Deby, amepokea nafasi ya uenyekiti wa AU kutoka kwa kiongozi wa Zimbabwe, Robert Mugabe.

MAGAZETINI LEO JUMAPILI JAN 31

Ndugu Mdau tunapokea matangazo mbali mbali kwa gharama nafuu zaidi hivyo ukiwa na tangazo ambalo ungependa kuongeza idadi ya wateja zaidi usisite kuwasiliana nasi kwa namba 0622750199/0754026299 
Barua pepe : fgodwin94@gmail.com/francisgodwin2004@yahoo.com
Mtandao wetu wa matukiodaima unawafikia watu zaidi ya milioni 10 ulimwenguni kote
Tumia nafasi hii kuongeza idadi ya wateja Ktk Huduma yako , kumbuka taarifa za misiba ni bure


Tuma Maoni


January 30, 2016

SAMATTA APONGEZWA NA TFF

Mbwana SamattRais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Jamal Malinzi amempongeza mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” Mbwana Samatta kwa kufanikiwa kujiunga na klabu ya Racing Genk inayoshiriki Ligi Kuu ya nchini Ubeligiji.

Malinzi amempongeza Samatta kwa kupata nafasi ya kucheza ligi kuu ya Ubeligiji baada ya kusaini mkataba wa miaka mitatu na nusu kuichezea RC Genk inayoshika nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu nchini humo.

Kufuatia kupata nafasi hiyo, Malinzi amemtaka Samatta kujituma kwa nguvu zake zote na uwezo wake wote ili kuendelea kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania katika nyanja za kimataifa na kwa sasa barani Ulaya.

Aidha Malinzi amewataka wachezaji wengine kujituma na kutumia nafasi wanazozipata katika vilabu vyao kwa kufanya vizuri na kupata nafasi ya kuvuka kwenda kucheza soka la kimataifa nchi za nje.

MAMA YASSODA AFUNGA KOZI YA MAKOCHA WANAWAKE

Juliana Yassoda akiongea na washirki

Mkurugenzi Msaidizi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mama Juliana Yassoda leo amefunga kozi ya ukocha wa wanawake ngazi ya juu (High Level Course) iliyoandaliwa na TFF kwa kushirikiana na FIFA.

Akiongea wakati wa kufunga kozi hiyo, Mama Yassoda amesema anaishukuru TFF/FIFA kwa kuona wanawake wanapata nafasi ya kushiriki kozi mbalimbali, ikiwemo kozi hiyo ya ukocha kwa ngazi ya juu kwa wanawake.

Mama Yassoda amewataka washiriki wa kozi hiyo kuyafanyia kazi mafunzo waliyopatiwa katika kuhamasisha wanawake wengi kuupenda mpira wa miguu na kuzalisha vipaji vya wachezaji wengi wa kike kuanzia ngazi za chini, na sio kuhitimu na kuweka vyeti ndani tu.

Naye Mariam Mchaina akiongea kwa niaba ya washiriki wenzake, ameishukuru TFF kwa kuwakumbuka wanawake na kuwapatia kozi hiyo ya ukocha, na kuahidi watakaporudi sehemu wanazoishi watatumia ujuzi walioupata kufundisha wanawake mpira miguu kwa ngazi zote.

Kozi hiyo ya ukocha kwa wanawake, ilianza Jumatatu na kumalizika leo ambapo jumla ya washiriki 25 wameshiriki kozi hiyo ya awali kutoka katika mikoa ya Dar es salaam, Iringa, Ruvuma, Pwani na Tanga na kupewa vyeti ya ushiriki na mpira kama kifaa cha kuanzia kazi ya ukocha.

SERIKALI YAHIMIZA MATUMIZI YA TAKWIMU RASMI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt.
Servacius Likwelile akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Chama cha Watakwimu
Tanzania (TASTA) uliofanyika jana jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa
Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC). Mkutano huo ulihudhuriwa na
watakwimu zaidi ya mia tatu kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara.
MkurugenziMkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa
akizungumza katika MkutanoMkuu wa Chama cha Watakwimu Tanzania (TASTA)
uliofanyika jana jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Chuo cha Takwimu
Mashariki mwa Afrika (EASTC). Mkutano huo ulihudhuriwa na watakwimu zaidi
ya mia tatu kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara.
Baadhi ya watakwimu
ambao ni wanachama wa Chama cha Takwimu Tanzania (TASTA) wakifuatiliakwa
umakini hotuba ya mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango
Dkt.Servacius Likwelile katika Mkutano Mkuu wa Chama cha Watakwimu
Tanzania Bara(TASTA) uliofanyika jana jijini Dar es Salaam katika ukumbi
wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC). Mkutano huo ulihudhuriwa
na watakwimu zaidi yamia tatu kutoka mikoa yote ya Tanzania
Bara. 
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL GHULA-NBS)


.................................
NA EMMANUEL Ghula - NBS
SERIKALI imehimiza wadau wa Maendeleo, Taasisi na Mashirika mbalimbali kutumia takwimu rasmi katika kupanga, kutekeleza na kutathimni programu za maendeleo.
Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Chama cha Watakwimu Tanzania (TASTA), uliofanyika jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile amesema ni vyema wadau wa maendelo, taasisi na mashirika kutumia Takwimu rasmi ili kupata matokeo bora katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
“Leo mmejumuika hapa pamoja watakwimu kutoka sehemu mbalimbali za nchi yetu kwa lengo la kujadili na kupanga mipango mbalimbali ya chama chenu pamoja na mustakabali wa tasnia ya Takwimu kwa ujumla.
Takwimu rasmi ni macho katika kupanga, kutekeleza na kutathmini miradi ya kimaendeleo. Natoa wito kwa wadau, taasisi na mashirika mbalimbali kutumia Takwimu rasmi zinazotolewa na watakwimu ili kupata matokeo yaliyo bora katika utekelezaji wa miradi ya kimaendeleo,” alisema Dkt. Likwelile.
Dkt. Likwelile alisema ikiwa upangaji wa mipango ya maendeleo kwa wananchi hautazingatia matumizi ya Takwimu rasmi, kuna athari kubwa katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika nchi yeyote ile duniani hususani katika kipindi hiki cha utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo Endelevu (SDGs).
Aidha, alisema kuwa ni vyema wananchi na wadau wengine kufuata Sheria ya takwimu Na. 9 ya mwaka 2015 inayoipa mamlaka Ofisi ya Taifa ya Takwimu kuanzisha Mfumo wa Takwimu nchini pamoja na kuratibu na kusimamia shughuli zote za ukusanyaji wa takwimu rasmi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa alisema wamekutana kwa lengo la kuboresha na kuimarisha tasnia ya Takwimu na maslahi ya watakwimu.
“Mkutano huu ni wa watakwimu kutoka Tanzania Bara ambapo tupo hapa kwa lengo la kujadiliana ni jinsi gani tunaweza kuwa na umoja madhubuti na wenye nguvu pamoja na kuimarisha tasnia hii ya Takwimu ukizingatia Takwimu ndio msingi wa maendeleo,” alisema Dkt. Chuwa.
Alisema kupitia chama cha watakwimu Tanzania wataweza kuifanya tasnia hii kuwa na nguvu pamoja na kuboresha utendaji kazi wa watakwimu katika maeneo yao mbalimbali walipo ikiwemo katika Halmashauri, Wilaya na Mikoa.
Mkutano Mkuu wa watakwimu Tanzania Bara ulifanyika jana katika ukumbi wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) na kuhudhuriwa na watakwimu zaidi ya mia tatu kutoka mikoa yote ya Tanzania bara.
Mkutano huo umefanyika kwa siku mbili kuanzia Januari 28 hadi 29, 2016.

Mugabe alionya baraza la usalama la UN

Image copyrightAFP
Image captionMugabe

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amelitaka baraza la usalama la umoja wa Mataifa kufanyiwa marekebisho.

Akizungumza katika mkutano wa Umoja wa Afrika unaondelea mjini Addis Ababa Ethiopia,Mugabe amesema kuwa viongozi wa Afrika wana haki ya kupewa mamlaka zaidi katika maamuzi yanayofanywa katika baraza hilo.

Huku akishangiliwa na viongozi wenzake wa Afrika,rais huyo mwenye umri wa miaka 91, ametaka bara la Afrika kupewa viti viwili vya kudumu katika baraza hilo la usalama.

Mugabe amesema kuwa ombi hilo sio kubwa sana kutoka kwa bara ambalo lina zaidi ya wanachama 50 katika baraza hilo.

Amesema kuwa Bara la Afrika haliwezi kuwa na uanachama wa mda katika baraza hilo,huku akionya kujitoa kwa bara hili iwapo mahitaji yao hayatasikizwa.

Image copyrightun.org
Image captionBaraza la usalama la UN

Amelilaumu baraza la umoja wa kimataifa kwa kuendeshwa kiukubwa.MUgabe ameonya kwamba Baraza hilo la umoja wa Kimataifa litaendelea kudumu kupitia kufanya usawa miongoni mwa wanachama wake.

Hatahivyo aliunga mkono juhudi za katibu mkuu wa umoja wa kimataifa Ban Ki Moon kwa kuangazia maswala ya bara hili.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AONGOZA MBIO ZA HAPA KAZI TU DODOMA HALF MARATHON


4

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongoza mbio za  Wabunge  Hapa Kazi Tu Dodoma Half Marathon zilizoanzia Bungeni hadi uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Januari  30, 2016. Kushoyo kwake ni Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na  Michezo, Nape Nnauye na kushoto ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt Tulia  Ackson. Mwansasu.

2

 Mmoja wa wapigapicha walioshiriki mbio za Hapa Kazi Tu  Dodoma Half Marathon alilazimika kuomba msaada kwa askari wa usalama barabarani  Mjini Dodoma Januari 30, 2016..

5

Baadhi ya Washiriki wa mbio za Hapa Kazi Tu Dodoma Half Marathon wakishiriki mmbio hizo mjini Dodoma Januari 30, 2016.(P.T)

6

Mbunge wa Mbulu  Vijijini,Fratei Massay akifanya mazoezi kabla ya kuanza mbio za Hapa Kazi Tu Dodoma Half Marathon kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Januari  30, 2016.

7

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi zawadi ya Pikipiki mshindi wa kwanza upande wa wanawake wa Mbio za Hapa Kazi Tu  Dodoma Half Marathon, Angela Davile (kulia) kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Januari 30, 2016.

8

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi ufunguo wa pikipiki mshindi wa kwanza wa mbio za Hapa Kazi Tu Dodoma Half Marathon  upande wa wanaume, Emmanuel Giriki kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Januari 30, 2016.

9Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Dodoma ambao wamedhamini  pambano la mpira wa miguu kati ya wabunge na benki hiyo kwenye uwanja wa Jamhuri Januari 30,2016. Benki hiyo  pia ilitoa vifaa vya michezo kwa timu ya Bunge.

(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Na Raymond Mushumbusi MAELEZO.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa,Majaliwa ameyataka mashirikisho ya michezo mbalimbali kumpa mpango kazi wa muda mrefu na mfupi ili kuiwezesha Serikali kushirikiana nao kuleta maendeleo ya michezo nchini.

Mhe.Kassim Majaliwa,Majaliwa ameyasema hayo leo Mijini Dodoma wakati akifunga mashindano ya Hapa Kazi Tu Half Marathon yaliyoanzia katika Chuo cha Biashara (CBE) tawi la Dodoma na kumalizikia katika uwanja wa Jamhuri yenye lengo la kuadhimisha kilele cha  Siku 100 za uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt John Pombe Joseph Magufuli tangu aingie madarakani.

“ Serikali ya Awamu ya Tano tumejipanga kuendeleza michezo nchini kwani michezo ni moja kati ya sekta muhimu kwa maendeleo ya wanamichezo na nchi kwaujumla na pia ni moja ya kujitangaza kimataifa kupitia michezo mbalimbali”Alisema Mhe Majaliwa.

Aidha Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye amesema kupitia wizara yake atajitaidi kuimarisha michezo hasa ukuzingatioa Serikali imeweka mkazo katika michezo hivyo yeye kama waziri mwemye dhamana hiyo atalisimamia kwa karibu suala la maendeleo ya michezo yote .

“Naahidi kushirikiana na vyama vya michezo ili kuimarisha sekta ya michezo kwa kuweka mipango thabiti ya kusimamia na kuiendeleza michezo ili iweze kuleta tjia katika jamii ya watanzania”Alisema Mhe. Nnauye.

Mbio hizi za Hapa Kazi Tu Half Marathon zilmeshirikisha Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Tulia Ackson,baadhi ya mawaziri, wabunge na watu wa rika zote kwa kukimbia umbali wa kilometa 2, kilometa5 na kilometa21 na washindi kupewa zawadi za pikipiki, mabati na fedha taslimu.

Mashindano haya ya hapa kazi Half Marathon yaliyoandaliwa na Chama cha Riadha Tanzania na kudhaminiwa na kampuni ya GSM, TANAPA, Kilimanjaro International Airport,East Teanders, CRDB Bank na DSTV yameandaliwa kwa nia ya kuandaa timu ya Riadha ya Tanzania kujiandaa na mashindano ya Olompiki yatakayofanyika Rio de Janeiro nchini Brazil.

MWISHO