Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

November 30, 2015

MAAMUZI YA MATUMIZI YA FEDHA ZILIZOKUWA ZITUMIKE KWENYE SHEREHE ZA UHURU

Mwenge-Morocco (2)Barabara ya Mwenge hadi Morocco jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli, leo ameamuru fedha kiasi cha shilingi bilioni 4 zilizokuwa zimetengwa kama bajeti ya sherehe za siku ya Uhuru ambazo zingefanyika Desemba 9, 2015, zitumike kufanya upanuzi wa barabara ya Mwenge hadi Morocco jijini Dar es Salaam yenye urefu wa kilometa 4.3 kwa kuongeza njia mbili za barabara za lami.

UN WAKISHIRIKIANA NA UBALOZI WA PALESTINA WAADHIMISHA SIKU YA MSHIKAMANO KW AWATU WA PALESTINA

Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Abdallah Kilima (katikati), Kaimu Balozi wa Palestine Derar Ghannam (kulia) pamoja na Balozi wa Sudan nchini Tanzania, Dkt. Yassir Mohammed Ali wakikata utepe kwa ajili ya maonesho ya picha za matukio mbalimbali yanayoendelea nchini Palestina hiyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mshikamano na watu wa Palestina yaliyofanyika katika Chuo cha Diplomasia, Kurasini jijini Dar.
Kaimu Balozi wa Palestina Derar Ghannam (wa kwanza kulia) akimuonyesha picha Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Abdallah Kilima (katikati) za matukio ya mauaji ya watu nchini Palestina yanayofanywa na Waisraeli ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mshikamano na watu wa Palestina yaliyofanyika katika Chuo cha Diplomasia, Kurasini jijini Dar.
Baadhi ya picha zinazoonesha matukio ya mauaji pamoja na majeruhi yanayoendelea kutokea nchini Palestina kutokana na vita inayoendelea nchini mashariki ya Kati kati ya Palestina na Israeli.
Afisa habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi Stella Vuzo (kulia) akitazama picha za wananchi wa Palestina waliouliwa na kutokana na mapigano ya Palestina na Israel yanayosababisha vifo vya watu wengi wasiokuwa na hatia.
Baadhi ya wageni waalikwa wakiendelea kusikiliza kwa makini wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mshikamano na watu wa Palestina. Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Abdallah Kilima akisoma hotuba yake mbele ya Mabalozi, wanafunzi wa chuo cha Diplomasia pamoja na wageni waalikwa waliofika kwenye maadhimisho ya ya siku ya kimataifa ya mshikamano na watu wa Palestina yaliyofanyika katika Chuo cha Diplomasia, Kurasini jijini Dar.
Naibu Mkurugenzi wa Mipango Utawala na Fedha wa Chuo cha Diplomasia, Dk.Bernard Achiula akizungumza jambo wakati wa maadhimisho hayo yaliyofanyika chuoni hapo.
Prof Josephat Kanywanyi ,Chairperson Tanzania- Palestine Solidarity committee akitolea ufafanuzi kuhusu mahusiano ya Tanzania na Palestina wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mshikamano na watu wa Palestina.
Balozi wa Sudan nchini Tanzania, Dkt. Yassir Mohammed Ali akisoma hotuba yake wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mshikamano na watu wa Palestina.
Wanafunzi wa Chuo cha Diplomasia wakiendelea kusikiliza kwa makini kinachozungumzwa kutoka meza kuu.
Mshauri Mwandamizi wa Utawala kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa mataifa (UNDP), Steve Lee aliyemwakilisha Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza uhusiano wa Palestina na Umoja wa Mataifa katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mshikamano na watu wa Palestina yaliyofanyika katika Chuo cha Diplomasia, Kurasini jijini Dar.
Baadhi ya Mabalozi waliofika kwenye maadhimisho hayo wakiendelea kufuatilia yanayojiri.
Mgeni rasmi akiwa kwenye picha ya Pamoja na Viongozi mbalimbali pamoja mabalozi.
Viongozi wakiwa kwenye picha na wanafunzi wa Chuo cha Diplomasia. 

Na Mwandishi wetu
  UN Tanzania ikishirikiana na Ubalozi wa Palestina nchini waadhimisha Siku ya Kimataifa na Mshikamano na watu wa Palestina na Tanzania katika Chuo cha Diplomasia Kurasini jijini Dar es salaam mwishoni mwa juma na kukutana na mabalozi wa wa nchi mbalimbali akiwepo Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Abdallah Kilima, Kaimu Balozi wa Palestina Derar Ghannam na Balozi wa Sudan nchini Tanzania, Dkt. Yassir Mohammed Ali ambapo ikiwa kuendeleza ushirikiano pamoja na mfululizo wa maonesho ya picha mbalimbali za matukio yanayoendelea huko nchini Palestina. 
  Mabalozi hao ambao walikutana katika jijini Dar es salaam kwaajili ya kuadhimisha siku hiyo ya kumbukumbu za picha za mapigano ya Palestina kwa ajiri ya kudumisha upendo na mshikamano pia mabalozi hao wameuomba umoja wa mataifa kuweza kuchukua hatua za ziada zitakazo pelekea nchi hiyo kuwa huru na kuweza kuendelea kufanya shughuli mbalimbali za kimaendeleo. 
  Mshauri Mwandamizi wa Utawala kutoka UNDP, Steve Lee akizungumza kwa niaba ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez alisema kuwa uhusiano wa Palestina na Umoja wa Mataifa katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mshikamano na watu wa Palestina alisisitiza kuwa na na umoja baina ya nchi zote mbili hususani Palestina kuweza kupata uhuru na kutambulika kuwa ni nchi nyenye mipaka yake binafsi ili kuepusha mapigano hayo yasiweze kutokea na kila mtu aweze kuishi na amani akiwa ndani ya nchi yake na kuweza kufanya maendeleo ya nchi. Na aliweza kuziomba nchi mbalimbali kulitambua taifa la Palestina kama nchi kamili tofauti na inavyotambulika kwa sasa. 
  Akizungumza wakati wa hafla hiyo ya ufunguzi wa siku ya maonesho ya picha Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Abdallah Kilima amesema wamefanya hivyo kwani ni hari ya kuwatakia heri Wapalestine wote kwani watu wote waparestine walipoteza uhuru na kwa sasa wanautafuta uhuru kwani nchi wanayo lakin hawako huru kwahiyo ni lazima tuwaunge mkono kwa kuweza kuadhimisha siku hii sehemu mbalimbali tunayoishi. 
  Kwa upande wa Afisa habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa(UNIC), Bi Stella Vuzo amesema wameamua kuwa na maadhimisho kwani ndani ya miaka 50 Palestina wamekuwa hawajatambulika kama taifa lenye mipaka yake ambapo kumekuwa na migogoro ya mda mrefu ambao unawahusu wa Palestine na wayahudi ambao upo tangu mwaka 1947,wakati katika maadhimio walio fikiana ni kuwa na mataifa mawili ndani ya eneo moja ambap mpaka sasa Israel pekee ndo iliyo pata kuwa hali ya taifa lenye mipaka yake wakati . Kila siku Israel huwa wanaleta vita ndani ya Palestine, sasa maadhimisho haya ni kwa ajili ya kuwaunga mkono kwa vitendo vinavyo endelea huko si vizuri. Pia aliwaomba viongozi wa pande zote mbili kuweza kuketi na kuweza kuweka maadhimio mapya kwaajili ya kuepusha mapigano yanayokuwa yakitokea kila siku baina ya nchi hizo mbili. Pia katika siku hiyo waliweza kuzindua picha za matukio ya vifo pamoja na watu walioumia kutokana na vita Palestina na Israel zilizo kuwa zimeandaliwa kwa Tanzania kwa ajili ya kuonyesha dunia matukio yanayoendelea katika nchi za Mashariki ya mbali hii yote ni kwa kuwa Palestina ina ushirikiano na Tanzania na kuwaombea katika kuelekea hali ya utulivu.

PSPF WAANZISHA KAMPENI MPYA YA MTAA KWA MTAA


Balozi wa mfuko wa pensheni wa PSPF Mrisho Mpoto Maalufu kama (Mjomba)  akizungumzana vyombo vya habari kuhusu kampeni ya mtaa kwa mtaa iliyofanyika jijini Dar kushoto ni Afisa wa mfuko wa pensheni wa PSPF Hadji Hamis Jamadary.

Na Mwandishi Wetu
Mfuko wa hifadhi za jamii wa pensheni (PSPF) kwa kuwajali watanzania waanzisha kampeni ya mtaa kwa mtaa ili kuweza kuungana na wananchi wa maeneo mbalimbali kwa kuwapa elimu  inayohusu mfuko huo wa pesheni kampeni hizo zimeanzia jijini Dar es salaam kwa kutembelea wilaya zote tatu huku wakipita mitaa mbalimbali ya wilaya hizo.

Kampeni hiyo imeanza muda mfupi tu mara baada ya mfuko wa pensheni wa PSPF kuungana kwa kutoa huduma na Mfuko wa afya wa NHIF ambapo wanachama wote walio jiunga na kusajiliwa na mfuko wa PSPF watapata manufaa ya kutibiwa kupitia mfuko huo wa afya  wa NHIF kutokana na kuwa wanachama hai.

Balozi wa mfuko wa pensheni wa PSPF Mrisho Mpoto Maalufu kama (Mjomba) pia naye aliweza kuungana na maafisa wa PSPF kwa kwenda kutoa elimu juu ya uchangiaji wa hiari ambao unamuhusu kila mmoja katika jamii zetu Mpoto amesema kuwa kwa kuonesha mfuko wa PSPF hauko mbali na wala haujawatenga wananchi uliamua kuaznisha uchangiaji wa hiari ili kuwapa fursa watanzania na kunufaika na mifuko ya jamii hususani PSPF ambao wanamjali na kuthamini kila mtanzania

Naye kiongozi wa msafara katika kampeni ya mtaa kwa mtaa iliyoanza jijini Dar es salaam Afisa wa mfuko wa pensheni wa PSPF Hadji Hamis Jamadary amesema "Tumeweza kuzunguka katika maeneo mbalimbali ya jiji ndani ya wilaya zote tatu ambazo ni ILALA,KINONDONI na TEMEKE kwa kuwapa elimu wananchi ya namna watakavyo weza kunufaika na mfuko huu wa jamii" ambapo alisema wananchi wamekuwa na mwitikio mkubwa sana hasa kwakuona mfuko wa pensheni wa PSPF umeamua kuwafuata katika maeneo yao na kuwapa elimu hiyo ya uchangiaji wa hiari.

Pia Afisa matekelezo wa mfuko wa pensheni wa PSPF Albert Feruzi amesema katika kuendeleza kutekeleza majukumu waliyo pewa ni pamoja na kuwajuza wananchi kitugani kinacho toka katika mfuko wa PSPF ambapo alisema kwa kila mwananchi atakaye jiunga na kusajiliwa na mfuko ataweza kunufaika na huduma mbalimbali zinazopatikana PSPF pekee na wala sio kwingine alizitaja baaadhi ya huduma ikiwa ni pamoja na kupata mikopo mbalimbali kwa wajasiliamali,mkopo wa nyumba zilizopo katika mikoa mbalimbali ya Tanzania  cha muhimu ni kujiunga na kuwa mwanacha uliye hai ambaye kila wakati unakuwa na uwezo wa kuchangia kila mwezi

Aidha naye afisa uendeshaji wa mfuko wa pensheni wa PSPF Dolphin Richard aliweza kupata fursa ya kuongea na wananchi katika maeneo mbalimbali huku akisisitiza suala la kuwa  ni mmoja wa wanafamilia wa PSPF kutakupa faida nyingi ikiwa ni pamoja na kupata matibabu kwa bima kwakuwa wameweza kuungana na NHIF ilikuleta maendeleo katika taifa la Tanzania
 Pia kunukuu kauli mbiu ya Rais wa Jamuhuri Ya Muungano ya Tanzania Mh.John Pombe Magufuli  akisema (PSPF HAPA KAZI TU) amabapo watahakikisha wanakuwa bega kwa bega na wananchi ili kila mmoja awe na usawa wa maisha naye alitaja baadhi ya mafao wanayo yatoa  ambapo ni fao la kustaafu kazi,fao la elimu,fao la uzazi.
Balozi wa mfuko wa pensheni wa PSPF Mrisho Mpoto Maalufu kama (Mjomba) akitoa burudani pamoja na kutoa elimu kwa wananchi waliofika kupata elimu juu ya Mfuko wa Pensheni wa PSPF hasa katika uchangiaji wa Hiari kupitia kampeni ya mtaa kwa mtaa iliyofanyika jijini Dar
Afisa wa mfuko wa pensheni wa PSPF Hadji Hamis Jamadary akitolea ufafanuzi kuhusu umuhimu wa kujiunga na mfuko wa PSPF hasa katika uchangiaji wa Hiari ambapo aliwasisitiza wananchi kuwa kila mwananchi anaweza kujiunga na mfuko huo na kusisitiza hakuna makato yoyote anayokatwa mteja anapojiunga na mfuko huo.
Wananchi wakendelea kufuatilia kwa makini elimu iliyokuwa ikitolewa na maafisa wa PSPF kupitia kampeini yao ya Mtaa kwa Mtaa.
Afisa wa mfuko wa pensheni wa PSPF Hadji Hamis Jamadary akiwagawia wananchi fomu za kujiunga na uananchama wa mfuko wa PSPF 
 Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Delphin Richard akizungumza na wananchi hawapo pichani wakati wa zoezi ka kuwasajili wananchi kupitia kampeni ya Mtaa kwa Mtaa kuhusu huduma zitolewazo na Mfuko wa Pensheni wa PSPF hasa katika uchangiaji wa hiari ambapo mtu yeyote anaweza kujiunga
Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Delphin Richard akimpiga picha kwa ajili ya kutengenezewa kitambulisho mmoja wa wanachama waliojiunga na mfuko wa PSPF kupitia kampeni ya Mtaa kwa Mtaa iliyofanyika jijini Dar
Baadhi ya waananchi wakijaza fomu za kujiunga na mfuko wa PSPF  hasa katika uchangiaji wa hiari ambapo mtu yeyote anaweza kujiunga ambapo kila mwananchi anaweza kujiunga.

AIRTEL FURSA YAWA MKOMBOZI KWA VIJANA WA IRINGA ......


1 (3)Mshiriki wa mafunzo ya Airtel Fursa mkoani Iringa Bi Fatuma Mkini (kushoto ) akipokea cheti cha ushiriki wa mafonzo hayo kutoka kwa afisa mahusiano na matukio wa Airtel Bi Dangio Kaniki mara baada ya mafunzo ya Airtel Fursa kumalizika mkoani Iringa kwa vijana zaidi ya 200 kushiriki.
5 (1)Vijana washiriki wa mafunzo ya siku moja ya Airtel Fursa mkoani Iringa wakimsikiliza afisa mahusiano na matukio wa Airtel Bi Dangio Kaniki (kulia) wakati wa ufungizi wa mafunzo hayo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Highland mjini Iringa jana.
6 (1)wawakilishi wa vijana zaidi ya 200 mkoani Iringa walioshiriki kupata mafunzo ya ujasiriamali kupitia mradi wa Airtel fursa wakiwa katika picha ya pamoja na afisa mahusiano na matukio wa Airtel Bi Dangio Kaniki na wafanyakazi wengine wa Airtel mkoa wa Iringa mara baada ya kukabidhiwa vyeti kwa niaba ya wenzao.
Baada ya kukata tamaa ya maisha kwa muda mrefu baadhi ya vijana mkoani Iringa wameeleza kufurahishwa na kampuni ya simu ya Airtel Tanzania kwa kuwapatia mafunzo ya jinsi ya kuanzisha na kuendesha biashara zao kwa faida kupitia mpango wa Airtel FURSA
Wakizungumza na mara baada ya mafunzo ya siku moja ya Airtel FURSA yaliyofanyika katika ukumbi wa Highlands mjini Iringa kwa kuwashirikisha vijana zaidi ya 200,washiriki hao walisema kuwa mafunzo hayo ni ukomb0zi mkubwa kwao kwani baadhi yao walikuwa wakilazimika kushinda vijiweni kutokana na kukosa fursa ya mafunzo kama hayo .
Washiriki wa mafunzo hayo Bi Husna Sanga na Bw Okelo Kasim wakizungumza kwa niaba ya wenzao walisema kuwa mbali ya kuwa wa hatua ya kampuni hiyo ya simu ya Airtel kutoa mafunzo hayo si tu kunawasaidia kupata elimu kuendesha biashara na miradi mingine ya kiuchumi bali ni sehemu ya ukombozi kwao na familia zinazowazunguka .
Alisema Bi Sanga kuwa sehemu kubwa ya vijana hasa mabinti walikuwa wakirubunika na kujiingiza katika biashara zisizofaa kama za uuzaji wa miili yao kutokana na kutokuwa na elimu ya uanzishaji wa biashara ndogo ndogo ambao zingewakomboa kiuchumi hivyo kupitia mpango huo wa Airtel FURSA ni wazi kilio chao kimepata majibu.
“Wapo baadhi ya mabinti wenzetu ambao wanalazimika kufanya biashara ya kuuza miili yao ili kupata kipato na mwisho wa siku wanapoteza maisha kwa ugonjwa wa UKIMWI , ila kwa sisi ambao tumepata elimu hii kupitia Airtel FURSA tunaweza kuwa mfano kwa wengine ambao wanafikiri kazi ni kuuza miili yao pekee”
Huku Bw Kasim mbali ya kupongeza kampuni ya simu ya Airtel Tanzani kwa kuwakumbuka vijana bado alisema kuwa kama njia ya wao kupongeza kampuni hiyo ya simu kwa vijana wote waliopata mafunzo hayo kwenda kuonyesha mfano kwa wenzao kwa kufanya kazi ya kubuni miradi na kuendesha shughuli zao kifanisi zaidi.
Kwa upande wake afisa mahusiano na matukio wa Airtel Bi Dangio Kaniki kuwa Kutokana na mradi huo wa Airtel FURSA vijana wengi watanufaika zaidi na wanafaidika na mradi huo ni wale wenye miaka kati ya 18-24
Alisema kuwa mradi huo umelenga kuwafikia vijana kote nchini na hadi sasa zaidi ya mikoa tisa wamefikiwa na mradi huo wa Airtel FURSA .
Bi Kaniki alitaja mikoa ambayo tayari imefikiwa na mradi huo Mbeya, Arusha, Dodoma, Mtwara, Mwanza, Mtwara, Dar es Salaam , morogoro, Tanga, Tabora na Iringa kuwa hadi sasa zaidi ya vijana 1700 wamefikiwa.
Alisema kuna njia mbili za kuwawezesha vijana njia ya kwanza kupatiwa Mafunzo ya ujasiriamali na njia ya pili kupatiwa vitendea Kazi .
Hivyo aliwataka vijana wote nchini ambao watasikia taarifa ya kuwepo kwa Airtel Fursa katika Mkoa wao basi kuweza kuchangamkia Fursa hiyo ambao hutolewa bure.
Alisema ili kijana aweze kufaidika au kushiriki kwenye Airtel FURSA atatakiwa kutuma ujumbe mfupi kwenda kwa namba 15626 na kuweka maelezo yafuatayo:- Jina, Umri, aina ya biashara na eneo. Pia wanaweza kutuma maombi yao kwa kupitia barua pepe airtelfursa@tz.airtel.com ambapo watatakiwa kutuma jina kamili, umri, na aina ya biashara.
Maelezo kuhusu program ya Airtel FURSA pia yanapatikana kwenye tovuti ya Airtel www.airteltanzania.com
Alisema kuwa Airtel Fursa inawalenga vijana ambao wapo katika biashara na wale ambao hawana shughuli na wanataka kuanzisha shughuli pia kwao ni fursa kwao .
Aidha alisema kuwa tayari baadhi ya vijana wamepata kunufaika na mradi huo ambao umelenga kuwainua vijana na kuongeza kuwa mradi huo ulioanza mwaka huu utakuwa ni mradi endelevu.

AZMA YA KUWA NA KIZAZI KISICHO NA UKIMWI ,MUDA WA VITENDO NI SASA

Na Mark B. Childress, Balozi wa Marekani katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mwaka mmoja uliopita wakati wa maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani, niliandika makala kuhusu jitihada za kuwa na kizazi kisicho na UKIMWI nchini Tanzania.  Toka wakati huo, kwa pamoja tumepiga hatua muhimu kuelekea katika kufikia azma hiyo, tukielekeza rasilimali na shughuli zetu kwenye maeneo yenye mahitaji zaidi nchini kote. Hata hivyo, bado tunahitajika kuongeza nguvu na kufanya zaidi. Bila ya kuongeza kasi yetu katika mwelekeo huu, maambukizi mapya yataongezeka, jambo litakaloongeza idadi ya Watanzania watakaokuwa wakiishi na VVU hivyo kuathiri maendeleo na ukuaji wa uchumi wa Tanzania.

Kipindi cha miaka mitano ijayo ni kipindi muhimu sana katika kufikia lengo la kutokomeza kabisa UKIMWI duniani ifikapo mwaka 2030. Rais Obama ameweka malengo makubwa kwa Mpango wa Rais wa Marekani wa Kudhibiti UKIMWI (PEPFAR), akitangaza kuwa hadi ifikapo mwishoni mwa mwaka 2017, PEPFAR itakuwa inawasaidia watu milioni 12.9 kupata matibabu yanayookoa maisha ya  kufubaza VVU na kuwawezesha wanaume milioni 13 duniani kote kupata tohara.  Aidha, kwa kushirikiana na wadau wa kiserikali, asasi za kiraia na sekta binafsi, PEPFAR itajielekeza katika kupunguza maambukizi ya VVU kwa asilimia 40 miongoni mwa wanawake vijana na wasichana katika nchi zilizoathiriwa zaidi  zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara.

MKUU WA MKOA WA TANGA ATEMBELEA MIRADI YA MAJI KATIKA JIMBO LA MLALO


 Mbunge wa jimbo la Mlalo, Rashid Shangazi akizungumza na wananchi wa jimbo la mlalo wakati wa sherehe ya kumpongeza, katika hafla fupi ilifanyika maeneo ya Mlalo Mkongoloni mwishoni mwa wiki.
 Mkuu wa mkoa wa Tanga Mwantumu Mahiza atembelea wilaya ya Lushoto na kuangalia miradi ya maendeleo ya Serikali ikiwepo maabara na mradi wa maji wilayani Lushoto Mkoani Tanga  baada ya kabla ya hafla fupi ya Mbunge wa jimbo la Mlalo iliyofanyika maeneo ya Mlalo mwishoni mwa wiki.
 Mkuu wa mkoa wa Tanga Mwantumu Mahiza akisalimiana na wananchi wa jimbo laMlalo.
Mkuu wa mkoa wa Tanga Mwantumu Mahiza akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika jombo la Mlalo kushoto ni mkuu wa Wilaya ya Lushoto Mariam Juma, Mbunge wa jimbo la Mlalo ndugu Rashid Shangazi na diwani wa jimbo la Kwemshasha Anuari Kiwe.
Baadhi ya wananchi na madiwani wa jimbo la Mlalo waliokusanyika kwaajili ya kukubali wito wa Mbunge wa Mlalo,Rashid Shangazi mara baada ya Mkuu wa mkoa wa Tanga kukagua mradi wa maji katika jimbo la Mlalo, na Mbunge wa jimbo hilo kufanyiwa sherehe ya kumpongeza hafla hiyo iliyofanyika katika jimbo hilo wilayani Lushoto Mkoani Tanga.

RC KILIMANJARO AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA

Na Mwandishi Wetu, Moshi
MKUU wa Mkoa Kilimanjaro, Amos Makalla, amefanya ziara ya kushtukiza katika masoko manne ya Manispaa ya Moshi pamoja na dampo za kukusanyia uchafu, ili kujionea hali ya usafi na utendaji kazi katika mkoa huo. Katika ziara hiyo, RC Makalla alitumia muda huo kuwaagiza watendaji wake, hususan katika mchakato mzima wa kuifanya Moshi iwe kwenye usafi.
Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, RC Amos Makalla mwenye miwani, akikagua soko lililopo kwenye Manispaa ya Moshi, mkoani humo, baada ya kufanya ziara ya kushtukiza kujionea hali ya usafi katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.

Akizungumzia ziara yake hiyo, Makalla alitoa siku tatu kwa watendaji wa Manispaa ya Moshi kuhakikisha kwamba lundo la takataka katika soko la Kwasadala linaondoshwa haraka iwezekanavyo. Alisema hawezi kukubali kuona Manispaa hiyo inashuka kiwango chake cha kuifanya Moshi inaendelea kuheshimika katika suala zima la usafi.
Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, RC Amos Makalla aliyesimama mlangoni, akiendelea na ziara yake ya kushtukiza kwenye Manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro kujionea hali ya usafi katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.

“Pamoja na kuagiza kuondoshwa kwa uchafu huo, pia nataka kuona Mkoa wetu wote unakuwa kwenye hali ya usafi, magari ya usafi yazoe taka kwa wakati, uongozi wa masoko uthamini usafi bila kusahau uongozi wa Hospitali ya Hai unakamilisha haraka ukarabati wa vyoo,” alisema Makalla. Kwa mujibu wa RC Makalla, kitendo cha kuiweka Moshi katika mazingira ya uchafu si tu inaondosha kwa kasi ile heshima yake, bali pia itazalisha ugonjwa wa mripuko, ukiwamo ule wa Kipindupindu unaosikika kuweka katika kambi katika baadhi ya wilaya nchini Tanzania. 

Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, RC Amos Makalla akipata maelekezo kutoka kwa watendaji na watumishi katika Manispaa ya Moshi, mkoani humo, baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika sehemu mbalimbali kwenye manispaa hiyo. Bashir Nkoromo 15:27 (40 minutes ago) to Kambi, Josephat, pamojapure, othmanmichuzi, me, muhidinuk, josephat.lukaza, cathbert39, zainul.mzige21, fadhiliathuman., amichuzi, assengaoscar, dande15us Mbwana, kwa nini kwenye captions unaandika "Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, RC Amos Makalla"? RC si ndiyo mkuu wa mkoa kwa Kiingereza? Kumradhi, imebidi nikuambie kwa sababu umeirudia sana. Zaidi ya hapo nakutakia kazi.

TASWIRA MBALIMBALI JIJINI DAR LEO


 Kamera ya Mtaa kwa Mtaa yanasa muendesha Bajaji akivunja sheria kwa kupita pasipo ruhusiwa kupita, hii ni pamoja na kuharibu miondo mbinu ya Barabara ya  mabasi yaendayo haraka ya Morogoro jijini Dar es Salaam.
Madereva wa magari haya mambayo yameshindwa kupishana kwa usahihi  wakielewana mara baada ya kugongana leo katika Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam, kama walivyonaswa na kamera ya Mtaa kwa Mtaa.
 Kamera ya Mtaa kwa Mtaa yanasa madereva wasiopenda kuvaa kofia ngumu(Herement) pamoja na Serikari Jeshi la Polisi kutoa agizo la kuvaa kofia hizo lakini wamekuwa wakiakipuuza sheria hiyo. wakingoja ningejua ninge.......
Mchana huo marekebisho ya hali ya tumbo yakiendelea katika sehemu ya chakula kama ilivyonaswa na kamera ya Mtaa kwa Mtaa.

MAGUFULI AKUTANA NA MABALOZI


 Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa China hapa nchini Dkt. Lu Youqing Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 30, 2015
 Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Korea ya Kusini  hapa nchini Mhe. Chung IL Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 30, 2015. Balozi huyo pia alitumia nafasi hiyo kumuaga Rais kwa kuwa muda wake wa kufanya kazi nchini umemalizika.
 Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akutana na kufanya mazungumzo na aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba  Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba. Profesa Lipumba amempondeza Rais kwa kuchaguliwa kwake kwa kishindo na pia ameipongeza hotuba ya Rais Magufuli aliyoitoa wakati wa kufungua Bunge la 11 mjini Dodoma 30, 2015
PICHA NA IKULU