Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

September 30, 2015

MTENGA AMPA ONYO MCHUNGAJI MSIGWA ......


Bw . Hassan Mtenga Katibu wa Ccm Mkoa wa Iringa
.............,....................................,,

CHAMA cha mapinduzi ( CCM) Mkoa wa Iringa kimelaani  shambulio lililofanywa na wafuasi wa chama cha Demokrasia na maendeleo ( CHADEMA) kwa wananchi waliokuwa wakitoka katika mkutano wa kampeni za mgombea Urais wa CCM Dr John Magufuli juzi.

Katibu wa CCM mkoa wa Iringa Bw.Hassan Mtenga aliwaeleza waandishi wa habari jana kuwa chama chake kinawapa pole wananchi waliopigwa na wafuasi hao wa Chadema waliotumwa na Mgombea Ubunge wa Chadema jimbo la Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa.

Mtenga alisema kuwa idadi kubwa ya waliopigwa fimbo ni wanawake kuwa tukio hilo haliungwi mkono na udhalilishaji mkubwa kwa wanawake hao 

Hata hivyo alisema kuwa vitendo hivyo vya Mchungaji Msigwa kutumia vijana kupiga wananchi na wanachama wa CCM havivumiliki na kuwa iwapo Mchungaji huyo akiendelea na vitendo hivyo na kukimbia Kama ilivyokawaida yake sasa atambue wazi kuwa watamkamata na kumkapeleka polisi.

" Upole Wetu CCM ndio ambao umemfanya Mchungaji msigwa kuendelea kuwafanyia vurugu wanachama wetu ila kwa sasa tutajitolea kumkamata anaewatuma vijana hao kupiga wananchi"

Alisema hadi sasa zaidi ya wana CCM 7 katika jimbo la Iringa Mjini wamevamiwa na kupigwa na wafuasi hao wa Chadema ambao wahifadhiwa katika Gesti ya Sambala na nyingine hapa Mjini .

Akielezea kuhusu lugha za matusi anazozitoa Mchungaji Msigwa kwa Mgombea Ubunge wa CCM jimbo la Iringa Mjini Bw Frederick Mwakalebela alisema ni dalili za kuanguka kwa mchungaji Msigwa katika uchaguzi mkuu 

Kwani alisema Kama angekuwa ni mbunge aliyewatumikia vema wananchi kwa kutimiza ahadi zake asingekuwa anatumia muda mwingi kutukana badala ya kueleza wananchi nini amefanya kwa miaka mitano .

Hivyo alisema kuwa iwapo Mchungaji Msigwa angekuwa na uwezo basi angesimama jukwaani kujibu zilipo Pesa za mfuko wa jimbo na kiasi cha tsh milioni 340 alizopewa na Mgombea Urais wa Chadema Edward Lowasa .

Mtenga alisema ushindi wa Mwakalebela jimbo la Iringa Mjini upo wazi kabisa na kuwa katika Mkoa wa Iringa kwa uchaguzi huu hakuna jimbo litakalokwenda upinzani.
DR MAGUFULI AMPONGEZA ASAS AAHIDI KUMSAIDIAMGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk John Magufuli ameahidi kumpa msaada mkubwa Mkurugenzi Mtendaji wa makampuni ya Asas (Asas Group of Companies) wa mjini Iringa, Salim Asas; utakaomuwezesha kuwekeza kwenye viwanda ili atengeneze ajira mpya kwa vijana.

Mbali na kampuni yao kuendesha kiwanda cha kusindika maziwa cha Asas Dairies Ltd, kampuni hiyo ina shamba kubwa la ng’ombe na inafanya biashara ya usafirishaji, vituo vya kuuza mauta na inajenga nyumba za kupangisha.

“Lete viwanda vingi nakuhakikishia kukupa ‘support’ kwa asilimia 100. Serikali ya magufuli inataka wawekezaji kama wewe, wanaofanya mambo yanayoinua uchum wa Taifa na kutoa ajira kwa vijana wetu wanaomaliza vyuo vikuu,” alisema.

Kauli hiyo ya Dk Magufuli imepeleka simanzi kwa mpinzani mkubwa wa CCM mjini Iringa, Mchungaji Peter Msigwa ambaye hivikaribuni alinukuliwa akiwahimiza wafuasi wachama hicho na wapiga kura wa mjini Iringa kususia biashara zinazofanywa na kampuni hiyo kwa madai kwamba faida anayotengeneza katika biashara hizo anaitumia kukandamiza ukuaji wa demokrasia.

“Hata ukitaka kutengeneza kiwanda cha Ulanzi, wewe tengeneza tu kwani serikali yangu itakupa msaada unaouhitaji,”  Dk Mafuli alisema kwa msisitizo.

Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alimponda Mchungaji Msigwa anayegombea kwa mara nyingine tena ubunge wa jimbo la Iringa Mjini kupitia chama chake, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) akisema anataka ubunge kwa maslai yake binafsi.

Mchungaji Msigwa anayeelekea kupata ushindani mkubwa kutoka kwa mgombea wa CCM, Frederick Mwakalebela alikuwa mbunge wa jimbo la Iringa Mjini kati ya mwaka 2010 na 2015 ambazo Dk Magufuli alisema nyingi kati yake zilikuwa za wana CCM waliokasirika baada ya kusikia jina la Mwakalebela pamoja na kwamba alishinda kura za maoni mwaka 2010,kukatwa.

OBAMA ASEMA NI LAZIMA RAISN ASSAD AACHIE MADARAKA

Rais wa Marekani Barack Obama amesema kiongozi wa Syria Bashar Al Assad hana budi kuondoka madarakani ili vita dhidi ya wanamgambo wenye itikadi kali wa kundi la dola la kiislamu IS viweze kufanikiwa.
Maafisa wa Ufaransa kwa upande wao wameanzisha uchunguzi dhidi ya utawala wa kiongozi huyo wa Syria kwa madai ya kuhusika katika uhalifu wa kivita kati ya mwaka 2011 na 2013.
Siku moja baada ya kutofautiana na Rais wa Urusi Vladimir Putin kuhusu hatma ya Assad, Obama aliongoza mkutano hapo jana pembezoni mwa mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa kujadili namna ya kukabiliana na ugaidi, mwaka mmoja tangu kuanzisha kampeini ya mashambulizi ya kijeshi ya angani nchini Syria na Iraq kupambana na IS.
Obama asema kiongozi mpya anahitajika Syria
Obama amesema kuwashinda wanamgambo hao wa IS kunahitaji kuwepo kiongozi mpya Syria na kuwahimiza viongozi wengine wa dunia kumuunga mkono kukabiliana na wanamgambo hao wa IS.
Rais wa Marekani Barack Obama na wa Urusi Vladimir Putin wana msimamo tofauti kumhusu Assad Rais wa Marekani Barack Obama na wa Urusi Vladimir Putin wana msimamo tofauti kumhusu Assad
Urusi ambayo ni mshirika mkubwa wa Rais Assad na ambayo imeahidi kumsaidia kijeshi kupambana dhidi ya wanamgambo wa IS, iliususia mkutano huo uliohudhuriwa na takriban viongozi 100 na badala yake inatarajiwa kuendesha mkutano maalum hii leo wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kujadili kitisho cha ugaidi na jinsi ya kukabiliana nao.
Hatma ya Assad katika mustakabali wa siku za usoni wa Syria ndiyo chanzo cha mvutano kati ya Marekani na washirika wa Syria Urusi na Iran huku kukiwa na juhudi kabambe za kidiplomasia kujaribu kuvitatua vita vya Syria ambavyo vimedumu kwa miaka minne na kusababisha vifo vya zaidi ya watu laki mbili na elfu arobaini.
Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Laurent Fabius amesema wameanzisha uchunguzi kutokana na ushahidi uliotolewa na mpiga picha wa zamani wa jeshi la Syria aliyepewa jina Ceaser ambaye aliasi jeshi na kutoroka mwaka 2013 akiwa na zaidi ya picha 55,000 zinazoonyesha vitendo vya kikatili na kinyama vya vita hivyo vya Syria vinavyodaiwa kufanywa na utawala wa Assad.
Naye waziri wa mambo ya nje wa Saudi Arabia Adel al Jubeir amesema Assad sharti aondoke madarakani la sivyo ataondolewa kwa nguvu za kijeshi. al Jubeir ameonya kuwa nchi nyingine zitaimarisha misaada kwa waasi wa Syria wenye misimamo ya wastani na hivyo kumlazimu Assad kukosa namna nyingine bali kuachia ngazi.
Huku hayo yakijiri, nchi saba zenye nguvu zaidi za kiuchumi duniani G7 zikiongozwa na Ujerumani pamoja na nchi za Ghuba, zimeahidi kutoa misaada ya kifedha ya kima cha dola bilioni 1.8 kwa mashirika ya kutoa misaada na kushughulikia wakimbizi ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya wakimbizi.
Japan haiko tayari kuwapokea wakimbizi
Wakati huo huo, Japan pia imetangaza msaada wa dola bilioni 1.5 kuwasidia wakimbizi wa kutoka mashariki ya kati lakini waziri mkuu wake Shinzo Abe amesema nchi yake haiko tayari kuwapokea wakimbizi hivi sasa.
Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe
Zaidi wa wasyria milioni nne wametorokea nchi jirani na maelfu ya wengine wameingia barani Ulaya kutafuta maisha mapya. Kamishna mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu wakimbizi Antonio Guterres ameishukuru Ujerumani na nchi nyingine wafadhili kwa kuongeza misaada yao ya kifedha kuwasaidia wakimbizi.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon atafanya mkutano hii leo kuhusu wakimbizi na wahamiaji pembezoni mwa mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Waziri mkuu wa Uturuki Ahmet Davutoglu ambaye nchi yake inawahifadhi wakimbizi milioni mbili kutoka Syria anatarajiwa kuhutubia katika mkutano huo utakaohudhuriwa na viongozi kutoka takriban nchi sabini.

MTOTO WA PAUL WALKER KUISHITAKI KAMPUN YA PORSCHE KWA KUMUUA BABAAKE
Mwanawe marehemu msanii nguli wa 'Fast and Furious'' Paul Walker ameishtaki kampuni ya kutengeneza magari ya Porsche kufuatia ajali iliyokatiza maisha ya babake.
Meadow Walker,mwenye umri wa miaka 16 anailaumu Porsche kwa kifo cha babake ambaye aliteketea hadi kufa baada ya gari alimokuwa akisafiria kugonga taa ya barabarani na kuwaka moto Novemba mwaka 2013.
Idara ya mahakama ya Marekani imethibitisha kuwa kesi hiyo imesajiliwa.


 


Meadow anasema kuwa Porsche haikuzingatia usalama wa madereva na abiria ilipokuwa ikiunda mfumo wa usalama wa magari yake dhidi ya ajali.
Kampuni hiyo ya Porsche haijajibu mashtaka hayo yanayoikabili.
Uchunguzi wa Polisi uliotolewa baada ya miezi minne ulibaini kuwa gari hilo aina ya Porsche Carrera GT, lililokuwa likiendeshwa na na rafiki wa karibu wa marehemu Roger Rodas, lilikuwa likiendeshwa kwa kasi mno kilomita 151 kwa saa.
 
Eneo ilikotokea ajali hiyo haipaswi kuzidi kasi ya kilomita 72 kwa saa.
Msingi wa kesi hiyo unatokana na ushahidi kuwa gari hilo lilikuwa likienda kwa kasi ya chini ilipopoteza mwelekeo na kugonga taa kwa mujibu wa jarida la TMZ.
Jarida hilo linasema kuwa ukanda wa abiria ulimkata utumbo nyota huyo mbali na kuvunjavunja mbavu zake na kwa hivyo hangeweza kujinasua gari lilipowaka moto.
Mkewe dereva wa gari hilo Rodas aliwasilisha kesi kama hiyo mahakamani mwaka uliopita ila Porshe ikadai kuwa mumewe ndiye aliyekuwa wa kulaumiwa kwa ajali hiyo wala sio upungufu wa gari lao.
MADAKTARI SASA KUPANDIKIZA TUMBO LA UZAZI KWA WANAWAKE

 
Madaktari nchini Uingereza wamepata idhini ya kupandikiza tumbo la uzazi la wanawake kwa mara ya kwanza.
Madaktari nchini Uingereza wamepata idhini ya kupandikiza tumbo la uzazi la wanawake kwa mara ya kwanza.
Katika majaribio hayo ya kimatibabu, madaktari hao watapandikiza nyumba ya mtoto kwa wanawake kumi katika hatua ya kwanza.
Mtoto wa kwanza kuzaliwa baada ya mamake kupandikizwa tumbo la uzazi
Mwaka jana mtoto mmoja nchini Sweden, alikuwa mtu wa kwanza duniani kuzaliwa kupitia uhamisho wa kizazi kwa mamake.
Kinyume na wenzao wa Sweden, kikosi hicho cha madaktari kutoka Uingereza, kitatatumia viungo kutoka kwa wafadhili wa jamaa ya waliofariki.
Madaktari kutoka Uingereza, watatatumia viungo kutoka kwa wafadhili wa jamaa ya waliofariki
Madaktari hao wamefanya kazi hiyo kwa zaidi ya miaka 20 ili kupata idhini ya majiribio hayo.
Ziadi ya wanawake mia moja tayari wametambuliwa kwa nia ya kufanyiwa majaribio hayo.

POLISI WAWAFURUKUTA WANAOFANYA TAFITI ZA WAGOMBEA MTAANI


 Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas.

Wakati tafiti za kienyeji zenye lengo la kupima kukubalika kwa wagombea urais, hasa Dk John Magufuli na Edward Lowassa zikizidi kuongezeka, polisi jijini hapa mwishoni mwa wiki walitumia nguvu kutawanya vijana waliokuwa wakiendesha kura za maoni kwenye stendi ndogo ya mabasi na soko kuu.
Tangu kutangazwa kwa matokeo ya utafiti uliofanywa na taasisi za Twaweza na Ipsos, vijana kwenye maeneo mbalimbali yenye mikusanyiko, hasa sokoni na kwenye baa wamekuwa wakiendesha tafiti zao za kienyeji wakiwa na lengo la kuonyesha hali halisi ilivyo mitaani tofauti na matokeo ya tafiti hizo mbili.
Katika tafiti hizo za Ipsos na Twaweza, Dk Magufuli, ambaye anagombea urais kwa tiketi ya CCM, alikuwa mbele ya Lowassa anayegombea kwa tiketi ya Chadema na vyama vinavyounga mkono Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), lakini matokeo hayo yamepingwa vikali na wadau mbalimbali, huku yakiamsha tafiti za kienyeji mitaani.
Katika tukio lililotokea mjini Arusha, vijana walikuwa wakiendesha utafiti wao kwenye soko kuu la Arusha na eneo la kituo kidogo cha mabasi, lakini polisi walifika na kuwatimua wakidai wanavunja sheria. Wafanyabiashara hao wa soko hilo na stendi ndogo, waliandaa maboksi mawili ya kura, moja likiwa limeandikwa “Magufuli” na jingine “Lowassa”.
Baadaye walialika watu kwenda kupiga kura.
Kila aliyepita katika eneo hilo alielezwa utaratibu wa kupiga kura na alitumbukiza karatasi yake katika boksi lililoandikwa jina la mgombea anayeona anafaa kuwa rais.
Utafiti wa stendi ndogo ulikamilika baada ya muda na ulionyesha matokeo ya wagombea hao (tunayo).
Wakati watu waliokuwa stendi ndogo wakiendelea kushangilia matokeo hayo, wafanyabiashara wenzao wa soko kuu walikuwa wakiendelea kupiga kura na ghafla polisi walipofika maeneo hayo na kuwatimua vijana waliokuwa wakikusanya kura.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema waliokuwa wanafanya utafiti huo walikiuka sheria na kwamba kitendo chao kingeweza kusababisha uvunjifu wa amani kwa kuwa kulikuwa na watu wasioafikiana.
Aliwataka wakazi wa Arusha kuacha kufanya mambo ambayo hayana manufaa, badala yake wasubiri siku ya kupiga kura.
“Huo ni utafiti wa aina gani wa maboksi?” alihoji alipoulizwa kuhusu tukio hilo.
“Hizi ni vurugu za mitaani. Tunawaomba wananchi watulie, wasubiri siku ya uchaguzi wapige kura kwa amani.”
Hili ni tukio la pili la utafiti unaofanywa kienyeji mitaani baada ya wafanyabiashara wa Kariakoo, Dar es Salaam kuendesha utafiti wao kwa kuruhusu watu kumpigia kura mgombea wanayempenda kati ya Magufuli na Lowassa.
Mbali na utafiti huo wa wakazi wa Dar es Salaam, kwenye maeneo mengine nchini kumekuwapo na watu wanaoendesha tafiti kama hizo zenye lengo la kujua ni mgombea gani wa urais anakubalika zaidi.
Wakati vijana hao wakifanya tafiti za kienyeji mitaani, wadau mbalimbali wamekuwa na maoni tofauti kuhusu kushamiri kwa vitendo hivyo.
Baadhi ya wananchi waliohojiwa na gazeti hili wamesema kuanzishwa kwa tafiti hizo kunasadia kupata matokeo halisi ya joto la uchaguzi katika maeneo husika, huku wataalamu wa tasnia hiyo wakieleza kuwa ni matokeo ya kufeli kwa mfumo rasmi wa ufanyaji tafiti za kisayansi kutokana na misukumo ya kisiasa.
Mkazi wa Tabata, Isaiah Salmon alisema kutokana na taasisi zilizoaminiwa na wananchi kutofanya kinachotakiwa, yupo tayari kujitokeza kushiriki tafiti za mitaani hata kama Serikali inazikataza.
Alisema inasikitisha kuona mashirika makubwa kama Twaweza yanatoa matokeo ambayo hayaendani na hali halisi katika mwenendo wa siasa nchini.
Salmon alisema anaona Dk Magufuli na Lowassa wanachuana katika kampeni zinavyoendelea, lakini matokeo ya utafiti wa taasisi hizo ni tofauti.
“Unakumbuka wakati wa uchaguzi kule Kenya tulikuwa tukipata matokeo ya tafiti zilizokuwa zikibainisha Uhuru Kenyatta na Raila Odinga wanaachana kwa kiasi kidogo na ndivyo ilivyokuwa mitaani. Hata matokeo ya uchaguzi yalivyotoka yalionyesha kama tafiti zilivyosema,” alisema.
Pamoja na kuanza kushamiri kwa tafiti hizo, baadhi ya wananchi wanatatizika na masuala ya kisheria na kanuni za uchaguzi na pia kukosa imani na watu wanaoendesha tafiti hizo ambazo mara nyingi ni vijana wa maeneo yenye watu wengi kama sokoni au stendi.
Mjasiriamali, Telesphory Ndomba alisema yupo tayari kushiriki katika tafiti hizo, lakini hana uhakika na uhalali wa matokeo yanayotolewa na watu wanaoweka maboksi hayo kama ni kweli ya au yemetiwa chumvi.
“Tuna uhakika gani wale wanaochukua hayo maoni watawasilisha inavyotakiwa? Mimi sijajua iwapo taratibu na kanuni za uchaguzi zinaruhusu kufanya tafiti hizo za wananchi, lakini hata nikiziona na nikashiriki bado siwezi kujua kama taratibu hizo zimefuatwa na aliyetangazwa, kashinda kweli au la,” alisema.
Alisema pamoja na taasisi za kitafiti kuonekana zina upungufu katika kazi zao, bado wana uhalali wao na kwamba tafiti za mitaani zinafanyika kwa sababu wananchi wengi, akiwamo yeye, “wamechoshwa na ahadi hewa zisizotekelezeka hivyo wana hamu ya kufanya mabadiliko”.
Hata wakati baadhi wanaona kushiriki utafiti huo unaozidi kushamiri mtaani kama haki ya msingi, Emilia Masaka (29), alisema haoni kama kuna umuhimu wa kushiriki tafiti hizo.
“Binafsi utaratibu huo mimi sina kwa sababu nina kazi zangu nyingi za kufanya kwa sasa. Sina nafasi kabisa kushiriki hizo tafiti zao. Ila kama ningekuwa na nafasi ningekwenda tu kuwaangalia ila siyo kushiriki,” alisema Masaka anayefanya kazi katikati ya jiji.
Mtafiti kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Patience Mlowe alisema hatua ya wananchi kuanzisha kura zao maoni juu ya chama au mgombea atakayeshinda urais, ni ishara tosha kuwa hawana imani na tafiti zinazotolewa na mashirika mbalimbali wakati huu wa Uchaguzi Mkuu.
Mlowe alieleza kuwa tafiti nyingi zilizofanywa hivi karibuni zinaonekana kuwa na msukumo wa kisiasa kwa kuwa watafiti walitumia muda mwingi kuzielezea wakati kitaalamu inabidi mwananchi wa kawaida azielewe bila kufafanuliwa au kuachwa na maswali lukuki yasiyo na majibu.
“Hayo ni matokeo ya kuwa na tafiti zisizotoa hali halisi inayoendelea katika mchakato wa uchaguzi na wananchi hawakupata matokeo halisi, ndiyo maana wameanzisha tafiti zao.
“Tafiti za aina hii tuzitegemee tu katika maeneo mbalimbali nchini kwa kuwa wananchi hawana imani na tafiti zinazotolewa,” alisema Mlowe.
Alisema iwapo watu wanaoshirikishwa katika tafiti hizo za wananchi ni wakazi wa maeneo husika na wana sifa za kupiga kura, hapana shaka kuwa matokeo yanayopatikana yatasadifu hali halisi siku ya kupiga kura ambayo ni Oktoba 25.
Pamoja na tafiti zinazofanywa na wananchi kutoonekana ni za kitaalamu bado huenda zikaendelea kufanywa zaidi nchini kwa kuwa zinasadifu hamu ya kupiga kura iliyopo miongoni mwa wananchi kama alivyoeleza, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Damian Shumbusho.
“Huu utaratibu wa wananchi kufanya tafiti zao kwa kupiga kura sokoni na vijiweni unaonyesha bayana wananchi wamepata mwamko wa kushiriki uchaguzi. Wanaona siku ya uchaguzi inacheleweshwa hivyo wanatafuta matokeo ya haraka haraka,” alisema Shumbusho kutoka Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala.
Alisema tafiti za kupima kukubalika kwa vyama na wagombea zinaweza kuwakatisha tamaa au kuwaongezea mori wapiga kura wakati huu wa uchaguzi na hazitakiwi kutegemewa sana kwa kuwa muda zinaofanywa siyo sahihi na siasa zinabadilika mara kwa mara.
“Kitendo cha wananchi kusema hizo tafiti tupa kule ni sahihi kwa sababu zimechokoza wananchi walipopanga kupiga kura baada ya kusikia sera za wagombea,” alisema.
Ofisa habari wa Twaweza, Risha Chande alisema kitendo cha wananchi kufanya tafiti zao mitaani ni jambo jema kwa kuwa kinaonyesha wana hamu ya kushiriki katika tafiti mbalimbali za kitakwimu jambo ambalo halikuwapo hapo awali.
Chande alisema pamoja na wananchi hao kuonyesha hamasa ya maswala ya kitakwimu bado, methodolojia wanazotumia haziwezi kutoa matokeo halisi ukilinganisha na tafiti za kisayansi zinazohusisha uchaguzi makini wa sampuli za kutafiti.
“Lazima tufuate utamaduni wa kuangalia au kujihakikishia mambo hasa maswala ya kitakwimu na hilo ni jambo letu kama taasisi.
“Sasa kama ukiwa na ugomvi na kitu lazima utachukua hatua kama waliyofanya wananchi hao ila tutambue kuwa kuna tofauti nyingi baina ya utafiti wao na ule wa kwetu,” alisema.
Maoni ya wadau na Nuzulack Dausen

SAFARI NDEFU ZAIDI ZA NDEGE DUNIANI KWASASA

Unaweza ukaona safari ya kutoka Mwanza mpaka Dar es Salaam ni ndefu kwa sababu unatumia kati ya saa 12 mpaka 16 ndani ya basi, lakini kwa Usafiri wa Ndege ni kama saa moja tu hivi unakuwa umemaliza safari !!
Sasa hizo saa za kukaa kwenye basi safari ya Mwanza-Dar kuna watu wanazitumia wakiwa angani kwenye Ndege… Nimezipata Rekodi Mitandaoni, zinaonesha safari kumi za Ndege ambazo wasafiri wanatumia muda mwingi zaidi hewani kwenye safari moja.
1.Dubai Mpaka Panama– Hii ni Safari ambayo inachukua saa 17 na dakika 35 angani… yani Ndege ikiruka Dubai hakuna sehemu inatua mpaka ifike Panama. Hii ndio safari ndefu zaidi kwa sasa ambayo inafanywa na Ndege za Emirates… umbali toka Dubai mpaka Panama ni Kilometa 13, 820.
emirates (1) 
2. Dallas mpaka Sydney- Unaambiwa umbali toka Dallas Marekani mpaka Sydney Australia ni Kilometa 13,804. Hiyo ni safari ambayo inachukua saa 17 kwa Ndege za Qantas.
3. Atlanta mpaka Johannesburg– Hapo kuna umbali wa Kilometa 13,580.. safari hii inakamilika kwa Ndege za Shirika la Delta kukaa angani kwa saa 16 na Dakika 55 ambazo ni kama saa 17 hivi mwanzo mpaka mwisho wa safari.
60966325
4. Los Angeles mpaka Dubai– Kama kuna wakati unawaza kufanya safari kati ya hayo Majiji mawili, basi utambue kabisa kwamba umbali wake ni Kilometa 13,420.. na Ndege inatumia saa 16 na Dakika 30. Hii sio safari fupi hata kidogo mtu wangu !!
5. Los Angeles mpaka Jeddah– Shirika la Ndege la Saudi Arabia ndio ambao wamekamata hii njia, unaambiwa umbali toka Los Angeles Marekani mpaka Jeddah Saudi Arabia inakuchukua saa 17 pia kuimaliza hiyo safari yenye umbali wa Kilometa 13,409.
Picha ya muonekano wa juu wa Jeddah Airport mpya, Saudi Arabia.
Picha ya muonekano wa juu wa Jeddah Airport mpya, Saudi Arabia.
6. Los Angeles mpaka Abu Dhabi– Umbali kati ya hiyo Miji miwili ni Kilometa 13,500.. sio safari ndogo aisee, Ndege za Etihad zinakamilisha hiyo safari kwa saa 16 na Dakika 50 mwanzo mwisho.
7. Houston mpaka Dubai– Kilometa 13,145 zimetajwa kwamba ndio umbali kati ya Miji hiyo miwili, safari yake mwanzo mpaka mwisho kwa Ndege inachukua muda wa saa 16 na Dakika 10… Ndege za Emirates zinahusika pia kusafirisha watu kati ya Miji hii miwili.
8. San Francisco mpaka Abu Dhabi– Umbali kati ya hiyo Miji ni Kilometa 13,130.. na safari yake inachukua saa 16 kukamilika.
9. Dallas mpaka Hong Kong– Hapo unazungumzia Marekani na China, umbali wake ni Kilometa 13,700 na umbali huo kwa safari ya Ndege inachukua saa 16 na Dakika 15… Ndege za American Airlines zimeunganisha hii Miji miwili kwa Ndege za moja kwa moja.
American_Airlines_Boeing_777-200ER_N775AN_PVG_2013-5-21
10. San Francisco mpaka Dubai– Hii nayo imo kwenye list ya safari ndefu za Ndege, umbali wake ni Kilometa 13,040… Ndege za Emirates zimeunganisha hii Miji pia kwa safari ya Ndege ya moja kwa moja. Safari yote inakamilika ndani ya saa 16 na Dakika 40.

NEC : HAKUNA WIZI NA UDANGANYIFU WA KURA UCHAGUZI MKUU WA OKTOBA 25


1.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi  (NEC), JajiDamian Lubuva akisalimiana na Mwakilishi wa Chama chaKitaifa cha Watu Wasioona Zanzibar (ZANAB), AdiliMohamed wakati wa mkutano baina ya taasisi za watuwenye ulemavu nchini na NEC iliyofanyika leo JumanneSeptemba 29, 2015 Jijini Dar es Salaam.

2.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi  (NEC), JajiDamian Lubuva akisalimiana na Mwakilishi wa Shirikishola Watu Wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA), Mkoawa Dar es Salamm Mohamed Chazi  wakati wa mkutanobaina ya taasisi za watu wenye ulemavu nchini na NECiliyofanyika leo Jumanne Septemba 29, 2015 Jijini Dar esSalaam.

Mwenyekiti wa Shirikisho la Watu wenye UlemavuTanzania (SHIVYAWATA) Mkoa wa Mwanza, AlfredKapole akichangia mada wakati wa mkutano mkutanobaina ya taasisi za watu wenye ulemavu nchini na Tume yaTaifa ya Uchaguzi (NEC) uliofanyika leo JumanneSeptemba 29, 2015 Jijini Dar es Salaam.
...,,,,......................................,...........
Na Jovina Bujulu

MAELEZO

 

KATIBU MKUU wa Wizara ya Fedha na Uchumi,Servacius Likwalile anarajia kuwa mgeni rasmi katikauzinduzi wa Chama cha Wanawake WanataalumaWahasibu Nchini (TAWCA) utakaofanyika tarehe 6 Oktobamwaka huu.


Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyotolewa leoJumanne (Septemba 29, 2015) Jijini Dar es Salaam,Mratibu wa TAWCA Rose Majuva alisema uzinduziunatarajia kufanyika katika hotel ya Hyatt Regency Kilimanjaro Jijini Dar es Salaam.


Majuva alisema chama hicho chenye jumla yawanachama 500 kinajumuisha wanawake wahasibuwenye shahada ya juu ya uhasibu walioandikishwa naBodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA).


Alisema Lengo la taasisi yao ni kuwahamasishawanawake wote wenye taalamu ya uhasibu ambaohawajasajiliwa katika  Bodi hiyo kujiunga na Bodi hiyopamoja na kuwahimisha wasichana waliopo katika taasisimbalimbali za elimu ya juu kutoogopa somo la hisabati,ambalo ndio kiungo muhimu katika taalauma ya uhasibu.


Aidha Majuva alisema Chama hicho kipo kisheria nakinaongozwa na katiba ambapo malengo ya taasisi hiyo nikujenga mtandaokupanua wigo wa elimu ya uhasibu,uongozi na shughuli mbalimbali za kiuchumi nchini.

MWISHO

 

 

Maji na ya Mahujaji 18 YAPATIKANA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA

Barua pepe: nje@nje.go.tz
Barua pepe: gcu@nje.go.tz
Tovuti : www.foreign.go.tz
               
                20 KIVUKONI FRONT,
                           P.O. BOX 9000,
                  11466 DAR ES SALAAM,  
                                    Tanzania.


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Taarifa za kupatikana kwa majina 18 ya Mahujaji kutoka Tanzania waliopotea huko Saudi Arabia

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa imepokea majina 18 ya Mahujaji kutoka Tanzania ambao hadi sasa hawaonekani kufuatia tukio la mkanyagano wa Mahujaji lililotokea eneo la Mina, Makkah tarehe 24 Septemba, 2015 na kusababisha vifo vya watu 769 na wengine 934 kujeruhiwa.

Itakumbukwa kuwa tarehe 28 Septemba, 2015 Wizara ilitoa taarifa kuwa Mahujaji wa Tanzania wapatao 50 bado hawajaonekana huku wengine watano wakiwa wamefariki dunia.

Majina ya baadhi ya Mahujaji wa Tanzania ambao mpaka sasa bado hawajaonekana ni kama ifuatavyo:- 

1. Abdul Iddi Hussein 
2. Awadh Saleh Magram 
3. Burhani Nzori Matata 
4. Yussuf Ismail Yusuf 
5. Saleh Mussa Said 
6. Adam Abdul Adam 
7. Archelaus Antory Rutayulungwa 
8. Farida Khatun Abdulghani 
9. Rashida Adam Abdul 
10. Hamida Ilyas Ibrahim 
11. Rehema Ausi Rubaga 
12. Faiza Ahmed Omar 
13. Khadija Abdulkhalik Said
14. Shabinabanu Ismail Dinmohamed 
15. Salama Rajabu Mwamba 
16. Johari Mkesafiri Mwijage 
17. Alwiya Sharrif Salehe Abdallah 
18. Hafsa Sharrif Saleh Abdallah

Mbali na taarifa za kupatikana kwa majina hayo, Wizara imepokea taarifa ya kutambuliwa kwa mwili wa hujaji mmoja wa Tanzania anayeitwa Hadija Shekali Mohammed wa kikundi cha Ahlu Daawa. 

Aidha, Serikali ya Saudi Arabia imetoa picha za maiti za Mahujaji waliokufa Makkah ambao wamehifadhiwa katika vyumba vya kuhifadhia maiti kwa ajili ya utambuzi. Hivyo, Ubalozi wa Tanzania nchini humo kwa kushirikiana na Tanzania Hajj Mission pamoja na vikundi vya Mahujaji unaendelea na zoezi la kuzihakiki picha hizo ili kubaini kama zinalingana na sura za Mahujaji wetu waliopotea.

Vilevile, Mamlaka ya Serikali ya Saudi Arabia imesema kuwa imechukua alama za vidole za Mahujaji waliokufa ili wazilinganishe na zile walizozichukua Uwanja wa Ndege wakati Mahujaji hao wakiingia nchini humo. Wizara inaamini kuwa taarifa za alama za vidole zitakapotolewa zitasaidia sana kuwatambua Mahujaji wetu.

Pamoja na jitihada zote hizo, Ubalozi pia unaendelea na juhudi za kuwatambua Mahujaji wengine wa Tanzania ambao hawajaonekana kwa kutembelea katika hospitali zilizohifadhi maiti na kulaza majeruhi wa ajali hiyo.


Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, 
Dar es Salaam
29 Septemba, 2015
Kutoka group jingine

September 29, 2015

WAFUASI 60 WA CHADEMA AKIWEMO MGOMBEA UBUNGE MCHUNGAJI MSIGWA MATATANI KWA TUHUMA ZA KUMPIGA MAWE MKUU WA FFU NA WANANCHI WALIOKUWA WAKITOKA KUMSIKILIZA DR MAGUFULI .....................

 
 
 Aliyekuwa  mbunge wa  jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa akishuka katika gari la  polisi  baada ya  kufikishwa mahakamani  wakati wa vurugu za machingaji  eneo la mashine tatu  mjini Iringa mwaka  jana(picha na maktaba ya matukiodaima)
............................................................................................................................................................
Na MatukiodaimaBlog
JESHI  la polisi kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) mkoani  Iringa watumia mabomu ya machozi kuwakamata wafuasi  zaidi ya 60  wa  chama  cha  Demokrasia  na maendeleo (chadema ) akiwemo mgombea  ubunge wao  jimbo la  Iringa mjini  mchungaji Peter Msigwa matatani  kwa kumpiga mawe mkuu wa kikosi cha  kutuliza ghasia (FFU) Iringa na   wananchi  waliokuwa  wakitoka katika mkutano  wa mgombea  Urais wa chama cha mapinduzi (CCM) Dr John Magufuli.

Baada ya  polisi kufatua mabamo mawili ya machozi kwa ajili ya  kusambaratisha  wafuasi hao baadhi yao  walikimbia huku  mgombea  ubunge  huyo Mchungaji Msigwa akienda kujisalimisha mwenyewe  polisi baada ya  kutakiwa  kufanya   hivyo kabla ya  kukamatwa na  polisi.

Imeelezwa  kuwa   wafuasi hao ambao  wengi  wao ni vijana walikuwa  wamekutana katika  eneo la kambi ya  kampeni ya Chadema  iliyopo  eneo la Hoteli  ya  Sambala jirani na kambi ya kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) kwa  ajili ya kikao cha ndani toka  majira ya mchana na jioni  ndipo  walipofanya  vurugu   hizo  wakati wananchi  wakitoka katika  mkutano wa kampeni za mgombea  huyo wa Urais wa CCM.
 
Kamanda  wa  polisi  wa  mkoa  wa Iringa Rmadhan Mungi aliwaeleza  jana  waandishi  wa habari  kuwa tukio  hilo  lilitokea   jana  majira ya saa 12;30   jioni baada  ya  wafuasi hao  kufunga barabara  kuu ya  Iringa –Dodoma  na  kufanya  vurugu  hizo kwa  kuwarushia mawe  wananchi  waliokuwa  wakitoka katika  mkutano wa kampeni za Dr Magufuli uwanja  wa  Samora.
 
Alisema  kuwa  wakati  jeshi la polisi  likiwa katika mkutano wa mgombea  huyo wa Urais wa CCM walipokea taarifa kuwa  kuna  vijana wa  boda  boda  zaidi ya 150 walikuwa  wakijikusanya  kuelekea  katika eneo hilo la Sambala Lodge  na baada ya  kufuatilia ndipo  walibaini  kuwa  wanakwenda katika  kikao chao cha  ndani  na kwa  kawaida  jeshi la  polisi halikatazi  watu  kufanya  vikao  vyao vya  ndani .

“Jeshi  la  polisi  halizuii  wanachama wa  chama  chochote cha siasa  kufanya vikao  vya ndani kwani  ni haki yao ya  kisheria na kikatiba …..lakini  baada ya  kikao chao  kumalizika  vijana hao  walitoka  nje ya ukumbi  huo uliopo kando kando ya  barabara na  kuanza  kufunga  barabara  na kucheza muziki katikakati ya barabara na kuzuia watumiaji wengine wa barabara  kushindwa  kupita  ……baada ya   vurugu hizo nilimuagiza mkuu wa FFU  kwenda  kuwatoa watu  hao  barabara ila  walipuuza na  kuishia kumpiga mawe  na  baadae  kukimbilia kujifungia katika Lodge hiyo ya  Sambala  eneo  ambalo  wamefanya kama makao makuu ya Kampeni za Chadema  “ alisema kamanda Mungi
Alisema  wakati wa vurugu  hizo baadhi ya  vijana  waliumia kwa  kuruka ukuta  na  wengine kwa  kuanguka wakati wa  kujaribu  kukwepa  kukamatwa na  kuwa wale  wote  waliokamatwa  watafikishwa mahakamani wakati  wowote  kuanzia  sasa na  kuwa miongoni mwao  yumo mgombea  ubunge  jimbo  hilo Mchungaji Msigwa .

Mbali ya  mchangaji  Msigwa   wengine  waliokamatwa kwa tuhuma  za  vurugu  hizo  ni pamoja na mgombea  udiwani  kata ya  Gangilonga  ambae  pia ni mkuu wa kambi hiyo Dady Igogo
 
Kamanda  Mungi  alisema  watuhumiwa  wote  watafikishwa mahakamani  wakati  wowote  kuanzia sasa mara baada ya upelelezi  kumamilika  alisema  kuwa mchungaji Msigwa hakuwepo katika  eneo la  tukio wakati  vurugu hizo  zikitokea  ila ameingizwa katika  orodha  ya  watuhumiwa kwa  wakosaji wakuu  wapo  makundi manne likiwemo moja la  yule  anaendenda kosa kwa  mikono  yake ,kundi  la  pili  muwezeshaji au  mshauri  na  kundi la nne kutoa hamasa kwa  wakosaji hivyo  alisema mgombea  huyo anashikiliwa kwa kutuma za  kutoa hamasa kwa watuhumiwa hao  kufanya  vurugu.
 
Wakati  huo  huo jeshi  hilo la  polisi  limepiga marufuku  vyama  vyote  vya  siasa kuwahamasisha wafuasi ama  wanachama  wake  kufanya  vurugu  za wakati  huu  wa kampeni na  kuwa kamwe jeshi  hilo halitamvumilia kiongozi ama mtu  yeyote atakayejihusisha na uvunjifu wa amani.

“Amani ni  kitu cha kwanza na yeyote anayetishia  kuvuruga amani ya Iringa anatishia kazi  za  polisi Iringa kamwe  hatavumiliwa  zaidi ya  kuchukuliwa hatua kali na  kuwataka  vijana  kuepuka  kutumiwa na wanasiasa  kufanya vurugu 

Kuhusu  mwenendo  wa  kampeni toka  zianze alisema  kuwa  hadi  sasa  tupo  nusu ya kampeni  hizo  toka  zianze na  kuwa  toka  tarehe 22 hadi 30  mwezi wa nane  hakukuwa na  kosa  lolote   lililoripotiwa kutokea  kuhusiana na kampeni  ila  tarehe 1 hadi 5 mwezi wa tisa  kulikuwa na makosa 9  yaliyoripotiwa kituoni na  tarehe 5- 19 kulikuwa na makosa 17 yaliyoripotiwa na makosa 15  yalitokea  jimbo la Iringa mjini na  makosa mawili  wilaya ya  Mufindi huku katika wilaya ya Kilolo hakuna  kosa hata  moja
Hivyo amewataka  wagombea na  wafuasi wao  kufuata maelekezo  yaliyomo katika kitabu  cha maadili ya uchaguzi kilichotolewa na tume ya Taifa ya  uchaguzi .
 
Kwa  upande  wake  mgombea  ubunge  wa  jimbo la Iringa mjini mchungaji Msigwa katika ukurasa  wake wa fecaboook alithibitisha kukukamatwa kwa  vijana  hao na kiongozi wa kambi  hiyo Bw Igogo wakiwa katika ngome    hiyo ya kampeni.
MWISHO