Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

August 31, 2015

LOWASA AKWAMA KUFANYA MKUTANO LUDEWA


BAADA ya Mgombea urais wa CCM Dr John Magufuli kufanya mkutano mkubwa mjini Ludewa jana leo Mgombea urais wa Ukawa Edward Lowasa leo amekwama kufanya mkutano Ludewa.

Pamoja na Ukawa kufanya maandalizi makubwa ya mkutano huo ikiwa ni pamoja na kusafirisha wapambe wake kutoka Maeneo mbali mbali ya Ludewa na nje ya Ludewa hali imekuwa tofauti 

Kutokana na kukosekana kwa mkutano huo baadhi ya wapambe waliosafiri jana kwa malori kuja Ludewa walilazimika kuanza safari ya kurudi kwa miguu kwenda Njombe na vijijini.

Wakizungumza kwa jazba wafuasi hao John Haule kutoka Njombe na Kefa Mbilinyi walisema kuwa waliahidiwa kupewa pesa kwa Kazi ya kuweka ulinzi kwenye mkutano huo ila kwa kukosa kufika kwa Lowasa na kushindikana kwa mkutano huo wamelazimika kutembea kwa miguu kutoka Ludewa kwenda Njombe .

Hata hivyo walisema baada ya kufika Ludewa hali ya upepo kwa UKAWA waliona imebadilika zaidi na kuwa hata Mgombea huyu angefika bado asingemzidi Mgombea wa CCM

Taarifa zilizopatikana zinadai kuwa kutofika Ludewa kwa Mgombea huyo ni kutokana na kushindwa kusafiri kwa gari toka Njombe hadi Ludewa zaidi ya km 70 katika barabara ya vumbi 

Katibu wa Chadema Wilaya ya Ludewa hakuweza kupatikana ili kuelezea sababu ya Mgombea wao urais kutofika Ludewa mbali ya mkutano huo katika ratiba kuonyesha ungefanyika Kati ya saa 5 asubuhi hadi saa 6:30 Mchana .

Akiwa katika ziara ya kampeni ya Mgombea Urais wa CCM Wilaya Ludewa Waziri wa Ardhi Wiliam Lukuvi aliwataka wana Ludewa kujenga Imani na CCM chini ya Dr Magufuli kwani ni mtu wa Kazi zaidi.

Lukuvi alisema wapo wagombea wengi zaidi ila Mgombea bora na anaefaa kuwa Rais wa awamu ya tano baada ya Dr Jakaya Kikwete ni Dr Magufuli ambae uchapakazi wake umeonekana.

Huku mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe akiwaomba wana Ludewa kutoa kura zote kwa Dr Msgufuli na Lowasa kumpa sifuri.

Hali ya kipindupindu Morogoro bado tete idadi ya wagonjwa yaongezeka.


Hali ya ugonjwa wa kipindupindu mkoani Morogoro imeendelea kuwa tete baada ya idadi ya wagonjwa wa kipindupindu kungezeka hadi  kufikia wagonjwa 45 ambao wanaendelea na matibabu katika kambi maalum katika hospitali ya sabasaba mjini Morogoro.
 
Akizungumza na mtandao huu afisa afya mkoa wa Morogoro Carlesilas Lyimo amesema kutokana na kasi ya ongezeko la kipindupindu maafisa afya wamefanya operesheni katika maeneo mbalimbali yanayotoa huduma za chakula na vinywaji na kufanikiwa kukamata na kumwaga pombe za kienyeji zaidi ya lita 770, kuwachukulia hatua wafanyabiashara wa chakula wanauza vyakula bila utaratibu pamoja na kutoa dawa za kuwakinga na kipindupindu majumbani kwa watu 410 wengi wao wakitokea kata ya kilakala.
 
Nao wananchi wa mji wa Morogoro wameeleza wasiwasi wao juu ya kuongezeka idadi ya wagonjwa wa kipindupindu ambapo wametupia mamlaka ya maji safi na maji taka Moruwasa kushindwa kutoa huduma ya maji kwa wananchi katika baadhi ya maeneo hali inayosababisha wananchi kulazimika kutumia maji ya mito ambayo si salama.

Watanzania watakiwa kutafakari kauli ya mgombea wa UKAWA kuachia watuhumiwa.


Watanzania wametakiwa kutafakari kwa kina kauli iliyotolewa na mgombea wa kiti cha urais kupitia UKAWA Mh Edward Lowassa ya kuwaachia huru baadhi ya watuhumiwa wa makosa ya kigaidi yaliyosababisha vifo na ulemavu wa kudumu kwa baadhi ya viongozi wa dini wa kiislamu na kikristo pamoja na wageni kutoka nje ya nchi sambamba na watuhumiwa wengine wa makosa ya kijinai bila kujali athari zinazosababishwa na matukio ya kigaidi ulimwenguni.
Tahadhari hiyo imetolewa mjini Ludewa mkoani Njombe Bwana Amoni Mpanju wakati akizungumza na mamia ya wananchi waliojitokeza kusikiliza sera za Dr Magufuli na kuongeza kuwa wakati dunia ikihaha kupambana na janga la matukio ya kigaidi yanayosababisha vifo na ulemavu wa kudumu kwa binadamu bila ya kujali imani zao za kidini na mataifa yao baadhi ya viongozi wanaowania kuliongoza taifa la Tanzania wanatangaza hadharani kuwaachia huru watuhumiwa wa ugaidi waliosababisha vifo na majeruhi kwa viongozi wa dini za kikristo na kiislamu na wageni wa mataifa mengine na kuwataka watanzania kutafakari kauli hiyo ya Mh Lowassa.
 
Dr John Pombe Magufuli akiwa katika ubora wake amefanya mikutano zaidi ya mitano akiwa njiani kutoka mkoano Njombe kuelekea Ludewa Songea kwa njia ya barabara ambapo amekuwa pia akisikiliza kero za walemavu alioonana nao na kuongeza kuwa uongozi ni msalaba na si kila mtu anaweza kuwatumikia kwa dhati wananchi na kwamba kiongozi anapaswa kuzifahamu kero za wananchi na kuziishi na kwamba ili Tanzania iwe na amani ni lazima majeshi yetu yaendeshwe kisayansi na kuahidi kuayaboresha.
 
Aidha Dr Magufuli ambaye amekuwa akishangiliwa na umati mkubwa wa wananchi waliokuwa wanaziba barabara kwa lengo la kutaka kumsikia amewataka wananchi kumchagua yeye kupitia CCM kwa kuwa ndio chama chenye ilani bora na ahadi za ukweli huku akiwazodoa UKAWA kwa kutokuwa na ilani ambayo ni mkataba kati ya watawala na watawaliwa.
 
Dr Magufuli anatarajiwa kuendelea na ziara yake ya kusaka ridhaa ya watanzania kuliongoza taifa la Tanzania ambapo jumatatu ya Septemba mosi anatarajiwa kuendelea na kampeni zake mkoani Ruvuma

August 30, 2015

MAGARI YANAYOPAA,ANGALIA UFANYAJI KAZI WAKE HAPA NA BEI YAKE

Fikiria magari kama haya iwapo yatakuja nchini Tanzania ni kwa jinsi gani yanaweza kusaidia kero ya foleni zisizokuwa na kikomo katika Jiji la Dar es Salaam?
 
Fikiria magari kama haya iwapo yatakuja nchini Tanzania ni kwa jinsi gani yanaweza kusaidia kero ya foleni zisizokuwa na kikomo katika Jiji la Dar es Salaam?
Haya siyo mengine ni magari ya kupaa ambayo yametengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu yanayoyawezesha kupaa inapostahili pia hutembea ardhini.
Kuna magari mengi yanayopaa lakini iliyozinduliwa hivi karibuni na kampuni ya Uingereza iitwayo Terrafugia ni aina nyingine ya gari inayopaa.
Gari hilo lenye uwezo wa kupaa kwa saa 20 angani, linaweza kuwa ndege binafsi yenye viti viwili matairi manne na mabawa yanayofunga na kufungua ili kuweza kuendeshwa kama gari la kawaida barabarani.
Aina hii ya gari ina uwezo wa kusafiri kilometa 180 kwa saa, huhitaji eneo kubwa kama la kutua na kupaa ndege ili liweze kupaa na kushuka iwapo dereva atahitaji.
Teknolojia hii sasa imekukua pia kampuni nyingine kutoka nchini Slovakia iitwayo AeroMobil inatarajia kuingiza sokoni magari yanayopaa itakapofika mwaka 2017 na kutumika kama magari mengine ya kawaida, huku yakihitaji nafasi ndogo kupaa na kutua tofauti na yale ya Terrafugia ambayo yanahitaji nafasi kubwa.
Kwa mujibu wa tovuti ya kampuni hiyo, mpaka sasa wameweza kuunda gari kwa kutumia teknolojia mpya ambalo hubadilika na kuwa ndege iwapo mtuamiaji atahitaji kupaa.
“Hapo awali tulikuwa tukitumia teknolojia ya zamani kuunda magari ijulikanayo kama Aeromobil 1.0 na Aeromobil 2.5 lakini sasa gari hili litakuwa likitumia gesi na litakuwa na mabawa yanayoweza kufunguka na kulisaidia kupaa,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.
Gari hilo halitahitaji kukimbia kwa umbali mrefu kwenye lami ili kupaa, badala yake litanyanyuka moja kwa moja kutoka mahali liliposimama.
Hata hivyo, gari hilo litabeba abiria wawili ambao ni rubani na abiria wake lakini pia litakuwa na uwezo wa kuruka umbali wa kilometa tatu pekee kutoka ardhini na kabla ya kujazwa mafuta litasafiri kilometa 700.
Kabla ya gari hizo, gari nyingine zilizokuwa zikipaa zilikuwa zikijulikana kama “SKYWORTHY na zikiwa zinatembea kawaida na huwezi kuona mbawa zake wala kudhani kuwa zinaweza kupaa jambo ambalo lilifanya ziivutie zaidi.
Gharama ya gari hizo ni Dola za Marekani 300,000.

YALIYOJIRI KWENYE KAMOENI ZA CHADEMA IRINGA HII LEO!!
 "Umati huu unajitokeza katika mikutano ya UKAWA  Mhe. Edward Lowassa akiwa Iringa katika viwanja vya Gagilonga leo Jumapili 30/08/2015

 

UMOJA WA ULAYA NA MKUTANO MAALUM KUHUSU WAHAMIAJI

Mawaziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani,Ufaransa na Uingereza Jumapili (30.08.2015)wataka kuitishwa mkutano maalum wa mawaziri wote 28 wa nchi za Umoja wa Ulaya kujadili mzozo wa sasa wa wahamiaji wanaoingia Ulaya.
Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani Thomas de Maiziere. Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani Thomas de Maiziere.
Mawaziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani,Ufaransa na Uingereza Jumapili (30.08.2015)wametowa wito wa kuitishwa mkutano maalum wa mawaziri wote 28 wa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya kujadili mzozo wa sasa wa wahamiaji wanaoingia Ulaya.
Umoja wa Ulaya unakabiliana na wimbi la wakimbizi wanaoingia Ulaya ambao haikuwahi kushuhudiwa tokea Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.Wengi wao wanazikimbia nchi zilizokumbwa na vita kama vile Syria na Afghanistan na kuhatarisha maisha yao katika safari ngumu za kuwafikisha Ulaya magharibi.
Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani Thomas de Maiziere amekaririwa akisema " Sote tumekubaliana kwamba hatuwezi kupoteza muda zaidi. Hali iliopo hivi sasa inahitaji hatua ya haraka na mshikamano ndani ya Umoja wa Ulaya."
Katika taarifa ya pamoja na mwaziri wenzake wa mambo ya ndani wa Ufaransa Bernard Cazeneeuve na Theresa May wa Uingereza kufuatia mazungumzo yao ya Jumamosi wametowa wito kwa Luxembourg ambayo inashikilia urais wa kupokezana wa Umoja wa Ulaya kuitisha mkutano katika kipindi kisichozidi wiki mbili.
Mkutano ujao wa kawaida wa mawaziri wa mambo ya ndani wa nchi za Umoja wa Ulaya umepangwa kufanyika tarehe nane Oktoba.
Kuanzishwa maeneo ya hatari
Waziri wa Mambo ya ndani wa Ufaransa Bernard Cazeneuve na mwenzake wa Uingereza Theresa May. Waziri wa Mambo ya ndani wa Ufaransa Bernard Cazeneuve na mwenzake wa Uingereza Theresa May.
Mawaziri hao watatu pia wametowa wito wa kuanzishwa kwa haraka maeneo ya hatari kusajili na kuchukuwa alama za vidole na kuwajuwa wakimbizi wa kweli hali kadhalika kufikia makubaliano ya haraka ya orodha pana ya Umoja wa Ulaya juu ya nchi zinazotambulika kama salama ambapo kwayo wahamiaji wanaweza kurudishwa.
Ugiriki hususan iko katika shinikizo kutokana na matatizo ya kiuchumi na imekuja kuwa kituo kinachopendwa kutumiwa na watu wanaojaribu kuingia Ulaya ya magharibi.
Repoti kutoka Ugiriki hapo Jumapili zimesema mhamiaji mwenye umri wa miaka 17 ameuwawa baada ya kunasa katika mashambuliano ya risasi kati ya polisi doria wa mipaka wa Umoja wa Ulaya na kundi la watu wanaosafirisha wahamiaji kwa magendo.
Tukio hilo limetokea karibu na kisiwa cha Ugiriki cha Symi wakati maafisa wa shirika la udhibiti wa mipaka ya Ulaya Frontex walipopambana na kujaribu kuwazuwiya watu wenye silaha waliokuwa wakiwasafarisha wahamiaji 60 kwa kutumia boti ya mwendo wa kasi.
Kuuwawa mhamiaji
Wahamiaji wa Syria baada ya kuvuka kuingia Hungary kutoka mpaka wa Serbiá. Wahamiaji wa Syria baada ya kuvuka kuingia Hungary kutoka mpaka wa Serbiá.

Kwa mujibu wa repoti ambazo sio rasmi kutoka duru za walinzi wa mwambao kundi hilo lenye kusafirisha watu kwa magendo lilifyetulia risasi boti hiyo ya doria jambo lililopelekea majibizano ya risasi na kuzuiliwa kwa boti hiyo yenye wahamiaji ambapo watu watatu walikamatwa.
Kijana aliyewawa alipatikana akiwa sehemu ya chini ya boti akiwa na jeraha la risasi.Kila siku feri za Ugiriki zinawaingiza nchini humo maelfu ya wahamiaji wengi wao wakiwa wanataka kuelekea magharibi mwa Ulaya kwa kutumia njia ya Balkan kupitia Macedonia na Serbia ilii kuingia upya Umoja wa Ulaya kwa kutokea Hungary.
Vyombo vya habari vya ndani ya nchi vimeripoti kwamba wahamiaji 4,000 wametolewa kwenye boti 100 nje ya kisiwa cha Ugiriki cha Lesbos Jumamosi pekee.
Hungary ambayo imekamilisha kujenga uzio wake uliokosudia kuwazuwiya wahamiaji kuingia nchini humo kutoka Serbia hapo Jmamosi imeshutumiwa na waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Laurent Fabius ambaye amesema hatua hiyo haiendani na maadili ya Ulaya.
Mwandishi : Mohamed Dahman/dpa

KENYA NDIYO MABINGWA WA IAAF


 

Kenya kwa mara ya kwanza kabisa imeibuka mshindi wa mashindano ya riadha ambayo yamekamilika mjini Beijing nchini China.
Kenya ilimaliza kileleni kwa Jumla ya medali kumi na sita, saba za dhahabu , sita za fedha na tatu za shaba. Nafasi ya pili ilichukuliwa na Jamaica huku nayo Marekani ikishika nasafi ya tatu.


 Katika siku ya mwisho ya mashindano hayo waamerika walishinda dhahabu katika mbio za mita 400 kupokezana vijiti ambapo Trinidad na Tobago walishinda fedha huku nao Uingezea wakishinda shaba. Jamaica nayo ilishinda mbio hizo upande wa akina dada.

SHEREHE ZA MABINTI KUCHEZA NUSU UTUPU MBELE YA MFALME MSWATI KUFUTILIWA MBALI

             

Utawala wa kifalme nchini Swaziland unaongozwa na mfalme Mswati umetakiwa kufutilia mbali sherehe maarufu za kitamaduni baada ya wasichana kadha waliokuwa wakisafiri kwenda kwa sherehe hizo kufa kwenye ajali ya barabarani.
Kundi linalounga mkono demokrasia nchini humo la (the Swaziland Solidarity Network) limetoa wito kwa mfalme Mswati kufutilia mbali sherehe hizo ambazo wasicha walio nusu uchi hucheza mbele ya mfalme.

 

Kundi hilo linasema kuwa zaidi ya wasichana 60 waliangamia wakati lori walilokuwa wakisafiria lilihusika kwenye ajali ya barabarani.
Utawala nchini Swaziland unasema kuwa idadi ya wasichana waliokufa ni 13.

UZINDUZI WA KAMPENI KWA ACT WAZALENDO PALE MBAGALA ZAKHEEM LEO


Mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Anna Mghwira (kushoto), akihutubia katika uzinduzi wa kampeni ya chama hizo uliofanyika viwanja vya Zakhem Mbagala jijini Dar es Salaam leo.

Kiongozi Mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo, Kabwe Zitto akihutubia katika uzinduzi huo.


Mshauri wa chama cha ACT-Wazalendo, Prof. Kitila Mkumbo akihutubia kwenye uzinduzi huo.

Kiongozi Mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo, Kabwe Zitto (kushoto), akiteta jambo na Mgombea urais wa Tanzania kupitia chama cha ACT-Wazalendo, Anna Mghwira.

Viongozi mbalimbali wa chama hicho wakiimba wimbo wa taifa.

Kiongozi Mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo, Kabwe Zitto, akiwatambulisha wagombea ubunge wa majimbo yote ya Dar es Salaam.

Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Kabwe Zitto, akigawa ilani ya chama hicho kwa mgombea urais na mwenza wake.

Mgombea Mwenza, Hamad Mussa Yusuph akihutubia kwenye uzinduzi huo.

Mwana muziki Bwana misosi, akitoa burudani katika uzinduzi wa kampeni wa Chama cha ACT-Wazalendo uliofanyika viwanja vya Zakhem Mbagala Dar es Salaam leo.

Umati wa Wananchi ukiwa katika uzinduzi wa kampeni wa chama cha ACT-Wazalendo uliofanyika viwanja vya Zakhem Magala Dar es Salaam leo.

MCHUNGAJI MSIGWA APOTOKA AZUIA WAPIGA KURA WAKE KUNYWA MAZIWA ...........PAMOJA na  kuwa aliyekuwa mbunge wa jimbo la Iringa mjini ni mchungaji leo ameingia katika sura mpya  baada ya kuwazuia  wapiga kura  wake kunywa maziwa ama kujaza mafuta katika magari yao .

Mchungaji Msigwa ambae alionyesha  kuwa na umaarufuzaidi kwa uchangia  wake  leo katika mkutano wa UKAWA uliofanyika  Iringa mjini kawakwaza wengi baada ya kuonyesha chuki binafsi na kutafuta  kura za huruma kwa  kuhamasisha wananchi wa jimbo la Iringa mjini kutojaza mafuta katika magari yao ama kunywa maziwa  jambo ambalo limechukulia  kwa sura tofauti na mbunge huyo ambae pia ni mwanasiasa .

Mbali ya  viongozi wa dini kumshangaa na siasa na maji taka za mbunge huyo kwa kuwataka  watu wasinywe maziwa bado wamesikitishwa na uelewa wake finyu kati ya siasa na uhai  wa watu .

Mchunagi Dan Sanga  amesema mbali ya kumpenda mgombea Urais wa Chadema Edward Lowasa ila mchungaji Msigwa kamfanya asimpende tena mgombea huyo wa Urais kupitia Chadema na mchungajiMsigwa kama mgombea ubunge wa chadema Iringa mjini kutokana na chuki na visa binafsi kwa wana Iringa.

Kwani alisema hakutegemea kwa mchungaji huyo kushindwa kueleza sera  zake na  badala ya kufanya kazi kuchafua biashara za watu jambo ambalo wao kama watumishi wa Mungu wenzake wamemuona kama  si chochote katika huduma ya kiroho .

Huku wananchi wa jimbo la Iringa mjini wakimtaka Mchungaji Msingwa  kabla ya kufanya kazi ya kuvuruga uchumi wa jimbo la Iringa aeleze kafanya nini toka alipochaguliwa mwaka 2010 zaidi ya  maandamano na kuvuruga uchumi wa jimbo la Iringa .TAARIFA YA UMOJA WA VIJANA WA CCM ( UVCCM) MAKAO MAKUU DAR ES SAALAM KWA VYOMBO VYA HABARI JUMAPILI 30 AUGUST 2015. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Agosti 29 kimezindua kampeni zake katika viwanja vya Jangwani Jijini Dar es Salaam. 

Katika uzinduzi huo viongozi kadhaa wa Chama  hicho wakiwemo na waliokuwa Mawaziri waandamizi katika Setikali ya CCM, Waziri Mkuu mstaafu Fredrick Sumaye, Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya Ufisadi, Edward Lowassa pamoja na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Lawrance Masha wakihutubia mkutano huo.

Ni jambo la kushangaza kumsikia mgombea wa nafasi ya  Urais kupitia CHADEMA, Edward Lowassa akihemewa na Kujikuta  akishindwa kuikabili hadhira ya Watanzania wanaofikia milioni 45  kuwaelezea ana malengo gani ya urais, Chama chake kina dira na sera zipi za msingi, pia akizungumza bila kuonyesha mtiririko  wa sera kusudiwa  kama muongozo wa uendeshaji Serikali ukikosa kuainishwa kwenye kitabu cha Ilani ya Uchaguzi ya chama hicho.

Kwa msingi huo, CHADEMA/UKAWA wameonesha jinsi gani wasivyo na maandalizi ya mkakati wa kitaalam na mipango endelevu kwa maendeleo ya kisekta katika dhamira ya kujenga uchumi imara utakaoimarisha huduma za jamii, kuheshimu misingi ya utawala bora wa sheria huku akionesha kukosa dira makini ikiwemo  mipango ya muda mfupi na muda mrefu ya Serikali yao ikiwa itatokea muujizq wa wa kushinda na kujikuta  wakitaja  changamoto zinazozikabili nchi nyingi zinazoendelea.

Mgombea wa CHADEMA Lowassa ni dhahiri ameshindwa uchaguzi mkuu mapema, amebakia akilalama, kupiga soga na kujenga matumaini hewa kwa Watanzania huku akishindwa kujua ni changamoto zipi za msingi zinazowakabili wananchi katika maisha ya kila siku na hatimaye atoe majawabu mbadala ya utatuzi wa msingi unaoweza kuaminiwa na wananchi wanaoishi aidha mijini au  vijijini.

Lowassa ameshindwa kabisa kukonga nyoyo na kugusa hisia za Watanzania katika mambo ya msingi kwa sababu ya kuandamwa kwake na pupa, kiherehere na kukurupuka toka Chama kimoja hadi kingine huku akiwa hana maandalizi yanayoweza kutoa majibu halisi yanayowakabili wafanyakazi, wakulima, wavuvi, wafugaji, walimu, madaktari, wauguzi pia wasanii na wanamichezo.

Lowassa na CHADEMA, wameshindwa kubainisha dhamira na maandalizi ya kuleta chachu ya maendeleo mbadala kwa sababu sehemu kubwa ya changamoto zilizokuwepo zimetatuliwa hatua kwa hatua kwa kipindi cha miaka kumi iliopita chini  uongozi wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete ambapo sasa mashirika ya Kimataifa ya kusimamia uchumi na fedha ikiitaja Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo uchumi wake unakua kwa kasi kuelekea uchumi wa kati.

Sisi UVCCM, tulitegemea sana kuona labda  ile shauku , mikiki , hamu na kiu alionayo Lowassa ya kutamani Urais kwa gharama yoyote huenda angekuwaa na mikakati. , sera au mipango mipya ya kushughulikia matatizo yaliyobaki ambayo aidha yamekawia kiutekekezaji kwa ukosefu wa fedha  au utatuzi wa matatizo hayo miradi husika imeanzishwa na kutofikiwa suluhisho kwa wakati au baadhi ya viongozi waliopewa dhamana hizo kushindwa kutekeleza kwa muda na wakati muafaka.

Hotuba ya Lowassa kuhusu azma na dhamira yake katika kukuza uchumi, UVCCM tunaifananisha na orodha ya manunuzi (shop list) maana haioneshi viashiria , njia au vyanzo vya mapato ya kukuza uchumi kwa mwendo haraka wa kisera na kujikuta akipiga porojo akifanana na kasuku aliyekariri maneno aliyofundishwa  akiyatumia bila kujuwa tija , faida, hasara na maana ya jambo analolikusudia.

Tumeshangaa kumuona akishindwa kuzungumzia masuala ya ufisadi na kutowataja wezi waliopora rasilimali za umma na maliasili za nchi, waliofuja uchumi, wala rushwa watu waliokosa kuwajibika  na kutochukuliwa  hatua za kisheria kwa masuala mazima ya kukiuka maadili ya uongozi ikiwemo sakata zito za mradi wa kufua umeme wa dharura kupitia kampuni hewa ya RICHMOND ambayo ilimsababishia Lowassa kulazimishwa na Bunge ajiuzulu Uwaziri Mkuu akiwa ni Waziri Mkuu aliyekaa muda mfupi zaidi kuliko yeyote katika historia ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

UVCCM tunachukua nafasi hii kuwaasa na kuwaomba sana Watanzania wenzetu kwamba mabadiliko au mageuzi ya kiuchumi na kisiasa hayahitaji pupa na papara kama iliyotokea kwa  wananchi wa Taifa la Libya ambao sasa wako katika dimbwi la majuto.

Viongozi wa Upinzani akiwemo Lowassa na kundi la UKAWA hawana dhamira njema kwa nchi yetu na UVCCM  tunawafanisha sawa na manahodha ambao muda mfupi ujao toka sasa watagombea sukani wakiwa katika kina kirefu cha bahari jambo ambalo ni hatarishi kwa maisha na mustakabali wa wasafri waliomo kwenye chombo chenye amani, utulivu, umoja, upendo na mshikamano wa kitaifa kinachoitwa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Lowassa ameonyesha dalili za kuwa kiongozi dikteta asiyeheshimu hata misingi ya utawala bora hasa pale aliporejea kwa mara ya pili akisisitiza msimamo wake wa kuwaachia huru Masheikh wanaokabiliwa na tuhuma za makosa ya ugaidi ambapo suala hilo sasa lipo mbele ya mahakama na hatutakiwi kuingilia mwenendo wa kesi kulingana na matakwa ya mgawanyo wa madaraka kati ya mihimili ya dola.

Mbali na suala hilo, pia ameonekana  kulizungumzia suala ambalo tayari mahakama ya juu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limekwisha litolea hukumu kesi ya Mwanamuziki Nguza Viking na mwanawe Papii Kocha waliohukumiwa kifungo cha maisha jela kwa makosa ya ubakaji kana kwamba Lowassa anaona vyombo vya sheria vimewaonea na kuwakandamiza.

Ifahamike kati ya makosa ambayo yameainishwa katika sheria za Tanzania, kosa la ubakaji halina msamaha.

Aidha, Lowassa na UKAWA wameonekana kuzungumzia sana dhana ya uzalendo wakati mfumo utokanao na itikadi ya Chama chao imejiegemea katika uliberali usiojali wala  uzalendo zaidi ya kuthamini utajiri binafsi, kujilimbikizia mali zisizo na vyanzo na uvukaji wa mipaka isiyozingatia mila, desturi na utamaduni.

UVCCM tumeshangazwa sana na ujasiri uchwara ulionyeshwa na Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye anapothubutu kuzungumzia ufisadi wakati yeye mwenyewe ni miongoni mwa viongozi wanaotuhumiwa kwa kashfa ya uanzishaji wa Televesheni ya Taifa {TVT} na ufufuaji wa fedha za umma , soko la Kibaigwa, tuhuma ya uporaji  ardhi huko Tondoloni akitumia madaraka yake vibaya pia chini ya  usimamizi wake akiwa mtendaji mkuu wa Serikali, halmamshauri nyingi za wilaya nchini ziliongoza kupata hati chafu kutokana na  matumizi holela ya ruzuku toka serikali kuu kama ilivyofichuliwa  na ofisi ya CAG kufuatia upotevu wa fedha za miradi ya maendeleo ya jamii.

Sumaye kinywa chake wakati mmoja kikitoa moto na baridi ndiye aliyekitaka Chama cha Mapinduzi kutompitisha Lowassa kuwa mgombea  urais kwa madai ya kuhusika kwake na tuhuma za ufisadi huku akitishia kuhama CCM. Matamshi ya Sumaye yameushangaza ulimwengu na sasa anapopania kumsafisha Lowasa kwa kutumia maji taka akifikiri atasafika  ili aaminiwe na watanzania  werevu na wazalendo ajijue fika anatwanga maji kwenye kinu. 
 
SHAKA HAMDU SHAKA (MNEC)
KAIMU KATIBU MKUU UVCCM TANZANIA

DR MAGUFULI AMPONGEZA FILIKUNJOMBEA AWAKUNA MLANGALI

Wananchi  wa Mlangali  Ludewa wakimsikiliza mgombea urais wa CCM Dr John Magufuli  leo

 Dr Magufuli kulia  akizungumza na wanachi wa  Mavanga  baada  ya wananchi hao  kuzuia njia  ili kusalimiana nae  kulia ni Deo Filikunjombe

 Dr Magufuli kushoto  akimupongeza  Filikunjombe
 Filikunjombe  kulia  akiwapungia mkono  wananchi wa Mavanga  kushoto ni Dr Magufuli
 Wananchi wa kijiji cha Mlangali

 Deo Filikunjombe akimuombea kura mgombea Urais wa CCM Dr Magufuli leo


Mgombea udiwani kata ya Mlangali Bw Khamis Kayombo kulia na mbunge aliyepita bila kupingwa wa Ludewa Deo Filikunjombe kushoto wakiwa na mgombea Urais Dr Magufuli  wakishangilia ushindi 

......................................................................................................................................................

MGOMBEA urais wa CCM Dr John Magufuli amempongeza mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe kwa kupita bila kupingwa huku akiahidi Neema kwa wakazi wa Mlangali kuwa ahadi Yake ya kwanza ni barabara ya lami na maji.

Mgombea huyo wa Urais alitoa kauli hiyo leo kwa nyakati tofauti wakati akizungumza na wananchi wa Mavanga na kata ya Mlangali wakati wa kampeni zake za kutafuta ushindi wa CCM

Alisema kuwa shida za watanzania si vyama Bali kutatuliwa matatizo Yao na kuwa yeye atakuwa Rais wa vyama vyote bila kujali itikadi zao

Hivyo alisema iwapo ataingia ikulu kwanza kwa wakazi wa Ludewa ataanza na barabara ya Lami pia umeme wa uhakika na Huduma ya maji ikiwa ni pamoja na elimu bure kutoka shule ya msingi hadi sekondari kidato cha nne .

Alisema kuwa kikubwa anachojivunia kwa mbunge  wa Ludewa Bw Filikunjombe ni uchapakazi wake hivyo kwa pamoja wananchi wakichagua CCM kwa ngazi zote tatu ni uhakika maendeleo yatasonga mbele .

Dr Magufuli alisema kuwa akiwa Ikulu atahakikisha serikali yake inakuwa na mawaziri watendaji wachapakazi na si vinginevyo 

Hata  hivyo  alisema kuwa mawaziri atakao wateua  katika serikaliyake  watakuwa ni maziwari wa kazi na kamwe hatapenda kuona  waziri  akishindwa kuwajibika katika nafasi yake.

"Nimekuwa waziri wa kuteuliwa nikitumwa kazi ila mkinichagua nitakuwa juu ya mawaziri hivyo kama mimi nilivyofanya kazi ya kuwatumikia nataka kila waziri wangu afanye kazi ya kuwatumikia wananchi si vinginevyo"

Huku Filikunjombe akipongeza utendaji wa Dr Magufuli akiwa waziri wa ujenzi kwa  kufanikisha Ludewa kuwa na maendeleo  zaidi kwa uboreshaji wa barabara na kuwa vyama vya upinzani hazina uwezo wa  kuleta maendeleo zaidi ya vurugu 

DR MAGUFULI AFUNIKA NJOMBE,ATAKA WANANCHI KUPUUZA UKAWA


 Mgombea wa Urais kwa kupitia Chama Cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa kijiji cha Kikondo kata ya Ilungu Mbeya vijijini akiwa njiani kuelekea mkoa wa Njombe .
 Mgombea wa Urais kwa kupitia Chama Cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa kijiji cha Ujuni Makete mkoani Njombe .
 Mwenyekiti wa Shirikisho la vyama vya Watu wenye ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) Amon Anastaz Mpanju akisalimia wakazi wa Iwawa kwenye mkutano wa Kampeni za CCM uliofanyika stendi ya Mabehewani Makete.
 Mgombea wa Urais kwa kupitia Chama Cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Ikonda  kata ya Tandala ambapo aliahidi kumaliza matatizo ya msingi ya wananchi hao ikiwa kujengwa kwa barabara ya lami, kujenga visima vya maji, elimu bure mpaka kidato cha nne.
 Mgombea wa Urais kwa kupitia Chama Cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Wanging'ombe mkoani Njombe kwenye mkutano wa Kampeni za CCM ambapo leo ameingia mkoa wa tatu.
 Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula (kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe Ndugu Deo Sanga na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Mhe. Wiliam Lukuvi  wakimsikiliza Mgombea wa Urais kwa kupitia Chama Cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli kwenye mkutano wake katika wilaya ya Wanging'ombe.
 Mgombea wa Urais kwa kupitia Chama Cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akimkabidhi mgombea Ubunge wa Jimbo la Wanging'ombe  Eng.Gerson Lwenge ilani ya uchaguzi ya CCM

 Mhe. Pindi Chana akiwasalimu wakazi wa Wanging'ombe
 Mgombea wa Urais kwa kupitia Chama Cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akiagana na wagombea wa nafasi ya udiwani wa jimbo la Wanging'ombe mkoani Njombe.
 Mgombea wa Urais kwa kupitia Chama Cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akiwaaga wananchi wa wanging'ombe.
 Mgombea wa Urais kwa kupitia Chama Cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli (kulia) akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Mhe.Philip Mangula

 .Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Mhe. Wiliam Lukuvi akihutubia wakazi wa njombe mjini kwenye uwanaja wa Saba Saba.
 Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mhe. Philip Mangula akihutubia wakazi wa Njombe mjini kwenye mkutano wa kumnadi mgombea urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa mji wa Njombe kwenye uwanja wa sabasaba ambapo aliwahakikishia serikali yake itakuwa ya wachapa kazina kuelta maendeleo kwa wananchi.
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa mji wa Njombe kwenye uwanja wa sabasaba ambapo aliwahakikishia serikali yake itakuwa ya wachapa kazina kuelta maendeleo kwa wananchi.
Waziri wa Afrika Mashariki Dk. Harrison Mwakyembe akihutubia wakazi wa Njombe kwenye uwanja wa saba saba na kuwataka kuwa makini na viongozi wa kisiasa wanao walaghai wananchi.

BOFA HAPA KWA PICHA ZAIDI