Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

July 31, 2015

MCHAKATO WA KURA ZA MAONI NDANI YA CCM IRINGA KUMPATA MGOMBEA MMOJA KATI YA 13 WAKAMILIKA KWA AMANI,WATIA NIA WAPONGEZWA


Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Manispaa ya Iringa(kushoto) akiwa na Katibu wa Chama Hicho Elisha Mwampashi wakitoa taarifa ya mchakato wa kuwanadi watiania Iringa.
.................................................................................
Mchakato wa kujinadi kwa watia nia wanaowania kuteuliwa kupeperusha bendera ya chama cha mapinduzi(CCM) kwenye nafasi ya Ubunge katika jimbo la Iringa Mjini hapo kesho umekamilika bila kujitokeza mgogoro wowote.

      Akizungumza na wanahabari katibu wa chama hicho manispaa ya Iringa Bw Elisha Mwampashi alisema mchakato huo umekamilika kwa wagombea wote kujinadi kwa wapigakura katika kata zote za manispaa ya Iringa.
      Mwampashi alisema zaidi ya 18, 000 wa Chama cha Mapinduzi (CCM) jimbo la Iringa Mjini kesho wanatarajiwa kujitokeza kwa wingi wao kuwapigia kura waombaji 13 waliojitokeza kutafuta ridhaa ya chama hicho ili wapeperushe bendera ya ubunge katika Jimbo la Iringa Mjini.
      Kura hizo za maoni zinafanyika baada ya wagombea hao kutumia siku 12 kuzunguka katika matawi 81 ya chama hicho kunadi sera zao ikiwa ni azma ya kila mgombea kutafuta kuungwa mkono ili achaguliwe kuwania ubunge katika jimbo hilo.
       Minyukano ya kura hizo inatarajiwa kujitokeza kwa wagombea hao ambao ni pamoja na Dk Augustino Maiga, Frederick Mwakalebela, Jesca Msambatavangu, Mahamudu Madenge, Nuru Hepautwa, Dk Yahaya Msigwa, Michael Mlowe, Addo Mwasongwe, Aidan Kiponda, Fales Kibasa, Frank Kibiki na Peter Mwanilwa.
      Aidha Mwampashi alisema vituo 88 vitatumika kupigia kura hizo za maoni na matokeo ya kila kituo yatatangazwa vituoni ili kuepuka hofu ya kuwepo kwa mizengwe.
     “Kila mgombea ameteua wakala wake ambao pamoja na wasimamizi wa kila kituo  leo tumewapa mafunzo elekezi ya namna ya kuendesha kura hizo za maoni,” alisema.
      Alisema vifaa kwa ajili ya kura hizo za maoni vimekamilika na kwamba vituo vyote vitafunguliwa kuanzia saa 2.00 asubuhi hadi saa 10 jioni,” alisema.
      Alisema wanachama watakaoruhusiwa kupiga kura ni wale watakaokwenda katika vituo hivyo wakiwa na kadi zao za uanachama na kitambulisho cha mpiga kura.
      “Tunahitaji pia kitambulisho cha mpiga sio kwa maana ya kukichukua, ni kwa maana ya kujiridhisha kwamba mwanachama anayeshiriki kuchagua mgombea ubunge atapiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25,” alisema.
      Alisema matokeo ya jumla ya kura hizo za maoni yatatangazwa rasmi Jumapili asubuhi katika zoezi litakaloshirikisha waalikwa mbalimbali wakiwemo wazee wastaafu wa chama hicho, makada mashuhuri, viongozi wa taasisi  mbalimbali za chama na waalikwa wengine.
       Alisema kuibuka mshindi katika kura hizo hakumuhalalishii mgombea kwamba ameteuliwa na CCM kupeperusha bendera ya chama hicho mpaka pale vikao halali vya uteuzi vitakapothibitisha kwamba ushindi wake haukuwa na hila yoyote.
      Kwa miaka mitano iliyopita Jimbo la Iringa Mjini limekuwa likiongozwa na Mchungaji Peter Msigwa aliyechaguliwa katika uchaguzi mkuu wa 2010 kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

BALOZI DR MAHIGA DAWA SI KUHAMA CCM ASEMA YEYE NI MKOMBOZI WA CCM IRINGA MJINI, MWAMOTO KILOLO NIPENI MIMI, MGIMWA NIMEFANYA MENGI KALENGA ,WAZIRI LUKUVI NEEMA KUBWA ISIMANI INAONEKANA .......................

Balozi Dr Mahiga -Iringa mjini
>...........................................................................................................................
Na matukiodaimaBlog

ALIYEKUWA balozi wa kudumu  wa umoja  wa mataifa (UN) na mgombea urais katika mchakato  wa ndani ya chama cha mapinduzi (CCM) balozi Dr Augustono Mahiga anayeomba kuteuliwa kuwa mgombea ubunge jimbo la Iringa mjini kupitia CCM amewashangaa makada  maarufu wa chama  hicho  walioshindwa katika mchakato wa ndani ya chama kwa nafasi ya urais kuhama chama hicho kuwa hao hawakuwa na mapenzi ya kuwatumikia  watanzania na kuwa watazunguka kote ila chama makini ni CCM pekee na kuwataka wana CCM jimbo la Iringa mjini kumpa nafasi yeye ili kuondoa masalia ya Chadema .

Balozi Dr Mahiga  alisema kuwa wana CCM hao  walioanza kuhama chama  kwa kukosa nafasi ya urais hawakuwa na mapenzi mema na CCM bali  walikuwa wawametanguliza  maslahi yao mbele na  kuacha kuangalia maslahi ya Taifa na chama hivyo ni vema watanzania  kuwatazama kwa jicho la tatu na ikiwezekana kuwachunguza japo kwa miaka 5 bila kuwachagua kuwa  viongozi  wao.

Alisema kuwa kama  suala ni uongozi kwa ajili ya  kuwatumikia  wananchi na chama kulikuwa hakuna  sababu ya kuhama chama ama kuanza kutukana chama kwa sasa ila wangeweza  kushuka chini na  kugombea nafasi za chini ukiwemo udiwani ama ubunge kama ambavyo  yeye alivyoshuka na kugombea ubunge ili kuwatumikia watanzania kwa ngazi ya ubunge.

"Kila nafasi ndani ya chama ina maana  kubwa katika kutumikia  watu hivyo kuhama chama si jambo jema na upande wa vyama lazima kuwa makini na wanachama wanaohama vyama kwa sasa ili  kupata nafasi za uongozi iwapo  watakosa nafasi hizo  bila shaka  watachukua hatua ya  kuvuruga nguvu ya vyama  hivyo ama kuhama vyama "

Balozi Dr Mahiga amesema kuwa chakato mzima wa kumpata mgombea Urais wa CCM Dr  John Magufuli na mchakato wa kura  za maoni  katika ngazi ya udiwani na ubunge katika  jimbo la Iringa mjini ambako  ni mmoja kati ya  wana CCM 14  wanaoomba kuteuliwa kuwa wagombea wa ubunge .


Alisema akiwa kati ya  wana CCM 41 waliojitokeza  kuchukua fomu ya Urais hana kinyongo na uteuzi wa mgombea  Urais wa CCM Dr Magufuli kwani ni mtu  makini na safi ambae  viatu  vya Rais wa awamu ya nne Dr Jakaya Kikwete ataweza  kuvimudu  vema kutokana na kutokuwa  mtu wa kulipisha  kisasi na hana  makuu na mtu  zaidi ya  kulitumikia Taifa  .

Hivyo alisema iwapo wana CCM  jimbo la Iringa mji watamchagua yeye  kuwa mgombea ubunge  jimbo  hilo wawe imani  ya  kulikomboa jimbo hilo asubuhi  saa 12 kutoka kwa  Chadema  chini ya aliyekuwa mbunge  wa jimbo hilo mchungaji Peter Msigwa kwani alisema  si kweli kama Chadema Iringa mjini wananguvu kubwa kuliko  ya CCM na ukitazama idadi ya wenyeviti wa mitaa ambao CCM inao wenyeviti  104  huwezi linganisha na  wale 64 wa  Chadema kabla ya wenyeviti wake 13 kuvuliwa nafasi zao  na mahakama.

Alisema dawa ya ushindi  wa kishindo kwa CCM Iringa mjini ni moja pekee  kuvunja makundi na kuwa kundi moja la ushindi baada ya zoezi la kura za maoni kumalizika .


Dc Mwamoto  kulia akiwa na mbunge wa Kalenga Godfrey Mgimwa ,mwamoto ni mgombea ubunge Kililo
...........................................................................


Mkuu wa wilaya  ya Kaliuwa mkoani Tabora Bw  Venance Mwamoto ambae anawania kuteuliwa kuwa mgombea ubunge  jimbo la Kilolo mkoani Iringa amesema kuwa tishio la  kutaka kuuwawa kwake  majuzi baada ya  kufyatuliwa risasi katika gari lake  wakati akitoka katika kampeni  kata ya  Ilula bado haimtishi  katika safari yake ya  kuwatumikia  wananchi  wa jimbo la Kilolo linaloongozwa na Prof. Peter Msolla .

Kwani alisema moja kati ya ahadi yake  kubwa kwa wananchi wa Kilolo ni  kuona amawatumikia kwa kasi zaidi na kumaliza kero ya maji katika mji  wa Ilula na changamoto nyingine ambazo hazijapatiwa ufumbuzi kwa kipindi kilichopita na mbunge  aliyekuwepo .

Mwamoto  alisema kuwa kazi nzuri  aliyoifanya kwa nafasi ya  ukuu  wa wilaya  kwa kipindi  kifupi ambacho  Rais Dr Jakaya kikwete alipomteua kwa  kuwa mkuu  wa wilaya ya  Kibonde na Kaliuwa ni wazi ni  kipimo tosha na heshima kubwa ya wananchi  wa Kilolo kujivunia na  wategemee makubwa zaidi  iwapo  watamchagua kuwa mbunge  wao kwa  sasa .
                                             waziri Lukuvi - Isimani
................................................................................................
Mbunge  wa  jimbo la Isimani Bw  Wiliam Lukuvi amewaomba wananchi  wa jimbo  hilo hasa  wanachama wa CCM kuendelea  kujenga imani kwake na kuwa ndani ya CCM kuna Demokrasi  na kila mwanachama ana sifa ya  kugombea nafasi  yoyote ndani ya  chama japo  kipimo  cha kuchaguliwa bado kipo  kwa wananchi  wenyewe ambao  wanaweza kumpima kwa kazi alizofanya badala ya kushawishiwa kwa manenio bila vitendo.

Lukuvi ambae ni waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi amesema kama  si wana Isimani kuonyesha ushirikiano  wao kwake na hata  kumchagua katika nafasi hiyo ya  ubunge basi heshima ambayo  ambayo  wana Iringa wameipata  kupitia  wizara yake leo  isingekuwepo .

Alisema suala la migogoro  ya ardhi  amepata  kulishughulikia kwa umaniki mkubwa na kuwa sulaa  hilo pia  lilikuwa ni kero kubwa hata kwa wananchi wake wa jimbo la Isimani ila kwa sasa kwa kiasi  limeanza kupungua na kuwa iwapo wataonyesha imani yao tena  wategemee kuona maendeleo makubwa zaidi katika jimbo hilo na kutaka baadhi ya kazi kubwa ambazo zimefanyika kuwa ni pamoja na barabara ya lami ya Iringa- Dodoma, umeme  vijini , ujenzi wa shule pamoja na ujenzi wa nyumba bora  kwa kupata bati za ruzuku .

"Tumekuwa pamoja  muda  wote katika maendeleo  na matatizo  hivyo lazima  kila  safari ina  wasindikizaji  wake na siku  zote penye maendeleo ndipo panapopendwa na wengi  ila bado kwa tathimini yetu Ismani ya  leo  sio ya jana . nimekomesha ulanguzi wa mazao kama mpunga ,alizeti  kwa kufunga mashine"

                   Godfrey Mgimwa -Kalenga

Mbunge wa jimbo la Kalenga  Godfrey Mgimwa anayeomba kuteuliwa tena kuwa mgombea wa CCM nafasi ya ubunge  amewashukuru wananchi  wa kalenga kwa kuonyesha ushirikiano kwake na kuwa hadi  sasa amepata  kutekeleza ahadi zake kwa wananchi kwa asilimia 99 na kuwa zipo changamoto mbali mbali ambazo  watampa tena nafasi ya ubunge atakwenda  kuzifanyia kazi .

Mgimwa ambae  amepata  kuongoza jimbo hilo kwa mwaka mmoja pekee akichukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Dr Wiliam Mgimwa aliyefariki duni mwaka jana mwanzioni ,alisema zilikuwepo ahadi mbali mbali ambazo ziliachwa na mbunge aliyepita na tayari zote amezikamilisha kwa kipindi cha mwaka mmoja na kubwa anajivunia kuanzisha vikundi vya Vicoba  zaidi ya 60 ,ujenzi wa barabara , maji  vijiji ,umeme na uchangiaji wa ujenzi wa zahanati ,shule  na maabara na kuwa zaidi ya Tsh milioni 100 amepata  kutumia kwa kuchangia miradi ya maendeleo jimboni.

(imetayarishwa  na kikosi kazi cha matukiodaimaBlog)

FILIKUNJOMBE; MAFISADI WAMETUMA WATU WANING'OE UBUNGE NAOMBA WANANCHI WANYIMENI KURA

mbunge  wa Ludewa  Deo Filikunjombe kulia akiwa na mlemavu wa ngozi (ALBINO) mara  baada ya kumaliza mkutano wake wa kampeni za ubunge 
.....................................................................................................................................
Na Matukiodaima Blog Ludewa

WAKATI wanachama wa chama cha mapinduzi (CCM)  kesho   wanashiriki  zoezi la kupiga kura  za maoni kuwapata  madiwani na  wagombea  watakao gombea kwa CCM ,mbunge  wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe amewashukuru wanachama wa CCM  katika jimbo hilo kwa kuonyeha  imani kubwa kwake  ukilinganisha na wagombea  wenzake  wawili na kuwa hadi  sasa anauhakika mkubwa wa kushinda tena ila ushindi utakaompa heshima ni ule wa kupata kura zote na wenzake kuambulia patupu

Filikunjombe  aliyasema hayo   wakati wa mkutano  wa kujinadi kwa  wagombea wa nafasi ya  ubunge katioka kata ya Ludewa mjini ,kuwa hadi  sasa kutokana na mapokeo  ya wananchi na  wana CCM kote walikopata kupita kwenye kata 26 za  jimbo hilo la Ludewa wamekuwa wakitamka  bayana kuwa kura  zote kwake  hivyo  kuwaomba wana CCM kwa umoja  wao kumpa moyo zaidi wa kuwatumikia tena kwa kuhakikisha  wanampatia kura  zote za ndio.

Alisema kwa kauli zao wagombea wenzake wawili  waliojitokeza wanaeleza bila kuficha kuwa wametumwa na watu  ambao  aliwaondoa bungeni kutokana na vitendo vyao vya ufisadi  ili  waje Ludewa  kugombea ubunge kwa ajili ya kulipa kisasi kwa kumtoa jambo ambalo hadi sasa  limegonga mwamba kutokana na wananchi na wana CCM Ludewa kuliona hilo.

"Niliifanya kazi  ile ya  kupambana na mafisadi bungeni kwa faida ya  wananchi wa Ludewa na watanzania kwa ujumla ila nashangazwa  kuona  leo wana Ludewa wachache wanakubali  kutumika na mafisadi hao kutumwa kuja kunitoa ubunge kweli ni aibu  kubwa kwa kazi kubwa ambayo mimi nimeifanya katika  jimbo la Ludewa  sikutegemea kupata mpinzani tena ndani ya chama changu.....ila naomba sana  wana Ludewa  tuungane katika vita  hii ya maendeleo na kupinga ufisadi kwa kuwanyima kura hawa "

Alisema kuwa wilaya ya  Luudewa itajengwa na wana Ludewa kwa kushirikiana na yeye kama mbunge wao na sio wale wanaotumika  kuwadanganya wananchi wa Ludewa hata kupinga kazi kubwa iliyofanyika kwa kipindi kifupi cha miaka mitano .

Filikunjombe  alisema kuwa hawezi kusema kuwa amemaliza changamoto  zote za wilaya hiyo ya Ludewa kwani kama atasema hivyo atakuwa anawadanganya  wananchi wake na kuwa pamoja na kuwa amefanya mengi ila hajamaliza changamoto  zote za jimbo la Ludewa hivyo iwapo  watampa tena nafasi hiyo ua ubunge atahakikisha anaendelea kupunguza changamoto zilizobaki.

" nimefanya kazi kubwa ya kuleta maendeleo jimbo la Ludewa ila nitakuwa nadanganya kama nitasema nimemaliza changamoto  zote pia hata wabunge  wenzangu walifanya kulingana na wakati  ule  na kila mmoja a namchango  wake katika  maendeleo ya Ludewa .....ninachowaomba wananchi mtupime  wagombea kwa kazi  tulizofanya msitupime kwa maneneo kwangu mimi ni kazi zaidi maneno kidogo"

Hata  hivyo alisema iwapo wananchi  wa kata ya  Ludewa watamchagua kuwa mbunge kwa kura za kishindo atahakikisha kero ya maji anaanza kuitatua kabla ya  serikali kuanza kufanya hivyo kwani kati ya changamoto kubwa kwa mji wa Ludewa ni pamoja na maji .

Pia  aliwataka  wananchi kupuuza  uongo unaosambazwa na wagombea hao kuwa  vikao vya juu vya chama vimepanga  kukata  jina lake  baada ya  kushindwa na kudai kuwa huo ni upotoshaji na kuwa CCm ni chama makini na hakuna mtu wa kukatwa iwapo ametekeleza sera  vema za chama.

Huku mgombea injinia Zephania Chaula akiwaomba  wananchi hao kumchagua kuwa mbunge kwani tayari ameahidiwa na  na mwenyekiti wa DP mchungaji Christopher Mtikila na aliyekuwa mbunge wa  jimbo hilo kabla ya  kuangushwa na mbunge filikunjombe mwaka 2005 Prof Raphael Mwalyosi kuwa watamsaidia  kufanya kazi pamoja .

Chaula ambae  alipingwa vikali katika mkutano huo kiasi cha kuzomewa baada ya kudai moja kati ya kazi aliyoifanya ni kuanzisha  mfereji wa umwagiliaji kata ya  Ruhuhu baada ya mkazi wa kata  hiyo aliyekuwepo mkutanoni hapo kunyosha mkono na kumpinga kuwa hakuna mradi huo ni uongo na kuwa wao  wanamtegemea mbunge wao Filikunjombe ambae amefanya mengi kwenye kata  hiyo.

Wakagti Injinia Chaula ambae  siku za hivi karibuni aliambulia kura  11 katika nafasi ya ujumbe wa NEC akipingwa  vikali mkutanoni hapo mgombea Kepten (mstaafu) Jacob Mpangala akijikuta katika wakati mgumu kufuatia mbunge Filikunjombe kuwasilisha vielelezo sahihi mbele ya viongozi wa chama na kugawa kwa wananchi hao viinavyoonyesha mgombea  huyo anavyodanganya  wananchi  kuwa alistaafu kazi wakati kuna barua ya  kufukuzwa kwake kazi kutoka TAMISEMI.

Filikunjombe alifikia hatua  hiyo ya  kukabidhi  ushahidi huo kwa chama baada ya kauli ya  vitisho ya mgombea  huyo Mpangala kumtaka aonyeshe hadharani ushahidi unaoonyesha kufukuzwa kakwe kazi kabla ya kuchukua hatua .

FILIKUNJOMBE AWATAKA WANA CCM KUWANYIMA KURA WAGOMBEA WENZAKE ,PIA AMJIA JUU DIWANI WA CCM KUWA AKIHAMA CHAMA BAADA YA KUSHINDWA ATAMFUATA


Mbunge wa  jimbo la  Ludewa akisalimia na  wananchi wa Manda  ambako ni ngome ya mtiania Mpangala
Mbunge  wa Ludewa Bw Filikunjombe akiwa na kada wa CCM
Na MatukiodaimaBlog

  MBUNGE wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe amtolea uvivu Mgombea udiwani wa kata ya Luana anaegombea tena udiwani kata hiyo kuwa ni diwani mzigo mwenye Kadi mbili ya CCM na chadema anaesubiri kuhamia upinzani.

 Filikunjombea alitoa kauli hiyo jana wakati akijibu swali la wananchi ambao walitaka kujua ushirikiano wake na diwani huyo katika kuwaletea maendeleo wananchi wa kata ya Luana baada ya kila wakati kushuhudia mbunge akifanya Kazi mbali mbali za maendeleo na wananchi bila ushiriki wa diwani wao huyo Thomas Haule. Hivyo kumtaka mbunge huyo kueleza kwanini diwani wao amekuwa mpinzani wa mbunge wa Ccm wakati nae ni diwani wa CCM.

 Akijibu swali hilo mbali ya kuwapongeza wananchi hao kwa kumshukuru kwa maendeleo aliyoyafanya jimboni hadi kumpigia magoti ,Filikunjombe alisema ni kweli hatataka kuficha uovu kwani yeye ni msema kweli na uongo ama uoga kwake ni mwiko. 

Huku akishangiliwa na wananchi hao mbele ya diwani Thomas aliyekuwa ameketi meza kuu ,alisema lazima wananchi hao wakae ni diwani wao kama kweli wanampenda kwani ni diwani mzigo 

 "Wote mashihidi nimekuja kushirikiana nanyi kuleta umeme ,barabara na miradi mingine bila diwani wenu kuwepo sasa naweka wazi kuwa kama kweli mnampenda diwani wenu kaeni chini mmwambie kuwa ajirekebishe vinginevyo hatufai Mimi nakwenda mbio yeye anatembea" 

 Alisema kuwa amesikia kuwa diwani huyo ana Kadi mbili ya CCM na Chadema anasubiri ashindwe udiwani CCM ili ahamie chadema jambo ambalo hatakubali atamfuata huko huko kuona kuwa hapati tena udiwani.
 Huku wananchi hao wakishindwa kujizuia kumbeba juju mbunge huyu huku wenzake wakionyesha kukwazika kwa kukosa mtu wa kuwashangilia 

Wakati huo huo wanachama wa chama cha mapinduzi ( CCM) kata ya Mawengi ambayo ni kata aliyozawali Mgombea ubunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe wasukuma gari lililombeba Filikunjombe kwa zaidi ya kilometa 3. 

Tukio hilo lilitokea Majira ya saa 6 mchana baada ya kumalizika kwa mkutano wa wagombea ubunge hao watatu wa jimbo la Ludewa kumaliza mkutano huo wa kujinadi na kuomba kura zao.

 Mbali ya wagombea wenzake wawili Injinia Zaphania Chaula na kepteni (mstaafu )Jacob Mpangala kubanwa kwa maswali mbali mbali ya nini wamefanya katika Wilaya hiyo ya Ludewa ,hali ilikuwa tofauti kwa Filikunjombe baada ya wananchi kukataa kumuuliza swali kwa kile walichodai kuwa Kazi zake za kimaendeleo zinawakosesha maswali zaidi ya kumpongeza.

Filikunombe ambae ndie alikuwa wa kwanza kuanza kuomba kura kwa wananchi hao alijikuta alitumiwa muda wa ziada kuwatuliza wananchi hao kutotawanyika baada ya kumaliza kuomba kura na kuwataka wawasikilize wagombea wenzake pia badala ya kuwazomea na kususa kuwasikiliza.

 " Ndugu zangu wananchi nawashukuru sana kwa kuonyesha imani na kutambua wazi Kazi nilizofanya hadi kutaka kunipongeza katika mkutano huu wa kuomba kura na kutaka kunipongeza .... Kweli mmenitia moyo sana kwa hawa wenzangu wanaulizwa maswali magumu hadi katika vijiji wakivyozaliwa na hata kuzomewa... Ila naomba hapa msiwazomee wasikilizeni na kura zenu zote kwangu" 
 Filikunjombe alisema Kazi alizofanya Ludewa ni nyingi na kila Mwananchi wa Wilaya hiyo ni shahidi na kuwa hakufanya kosa kuwatumikia bungeni na nje ya bunge hivyo bado ubunge unautamani kamwe hatapenda kumwachia mtu mwingine jimbo hili kwa sasa kabla ya kuwafikisha wananchi wake kwenye maendeleo makubwa zaidi ya hayo yaliyopo.

 Alisema katika ubunge wake wa kipindi kimoja yapo mambo mazuri mengi ambayo ameyafanya katika miundo mbinu kwa maana ya barabara,miradi ya makaa ya mawe na Liganga na miradi mingine mingi. 

" Nawaombeni sana siku ya kupiga kura ikifika kila mmoja amkumbushe mwenzake kwenda kunichagua Deo Filikunjombe kuendelea kuwatumikia tena hawa wenzangu wametumwa kuja kunitoa ubunge naomba msidanganyike"

 Pazia la kampeni kwa watiania hao wa CCM kuomba kuteuliwa kuwa wagombea wa nafasi ya ubunge kwa jimbo la Ludewa zimemalizika jana kwa kata zote 26 na kesho wana Ccm watapiga kura kumchagua mgombea ubunge atakayepeperusha bendera ya CCM. Mwisho

Uganda:Mbabazi kuwania urais nje ya NRM

Waziri mkuu wa zamani wa Uganda John Patrick Amama Mbabazi ametangaza kuwa hatawania urais kwa chama tawala NRM katika uchaguzi mkuu mwakani.
Mbabazi ametangaza hilo muda mchache uliopita akiwa nyumbani kwake Kololo katika siku ya mwisho ya kurejesha fomu za uwaniaji wadhfa katika chama hicho tawala.
''kamwe sitatoka NRM''.
''Lakini sitaweza kugombea urais katika tikiti ya chama hicho cha NRM ilihali vipengee vingi tu vya vya chama vinakiuka katiba ya nchi''.
'' sitawania urais kwa tikiti ya NRM lakini wakati wa uchaguzi nitawania urais'
''kama mwanzilishi wa chama ,wakili na mwananchi Mzalendo,sitajiingiza katika maswala yanayokiuka sheria''
NRM sharti ijipige msasa''
Tangazo hilo la Mbabazi limetokea baada ya rais Yoweri Museveni kutangaza kuwa atarejesha fomu zake za kuwania uwenyekiti wa chama tawala NRM leo.
Mwenyekiti wa jopo la kuchagua viongozi wa chama hicho bwana Tanga Odoi alikuwa ametanga ijumaa tarehe 31 (leo) kuwa siku ya mwisho ye kurejesha fomu za uwaniaji nyadhfa za chama hicho.
Mbabazi anasemekana kuwa alitembelea makao makuu ya chama tarehe 16 akikusudia kuwasilisha ombi lake lakini akakurupuka akidai kuwa gharama ya juu iliyowekwa kwa wagombea itawanyima maskini uwezo wa kuwania nyadhfa katika chama hicho.
Mbabazi alikuwa ameahidi kumpinga rais Museveni kama mwenyekiti wa chama na hivyo mgombea wa urais katika uchaguzi mkuu ujao mwakani.
Mpinzani wake rais Museveni anatarajiwa kurejesha fomu zake mwendo wa saa sita adhuhuri.
katika makao makuu ya chama, wafuasi wake wamemiminika wakiwa wamevalia rangi za chama wakiimba nyimbo za kumsifu.

Viongozi wa bara la Afrika wametakiwa kutoweka mbele masilahi yao.

 
Viongozi wa bara la Afrika wametakiwa kutoweka mbele masilahi yao  binafsi na uchu wa madaraka na badala yake  wakubali kupoteza hadhi na vyeo vyao ili kuhakisha kuwa bara la Afrika linakuwa nchi moja.
Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na wakuu wa nchi saba za Afrika ambao ni wastaafu waliopo hapa nchini kwa ajili ya kushiriki katika  mkutano wenye lengo la kujua ni nini kifanyike ili kuweza kutatua changamoto zinazosabisha malengo ya nchi za Afrika kushindwa kufikiwa.
 
Mh  Jerry Rawlings ni rais mstafau wa Ghana ambaye anasema  ushirikino baina ya nchi moja na nyingine katika nchi za Afrika kutasaidia kuomngeza tija na uhuru wa maingiliano baina ya nchi moja na nyingine kuliko kukimbilia kuwa na mahusiano ya mbali.
 
Namibia iliwakilishwa na Mh Hifikikepunye Pohamba ambaye alisema viongozi waliotangulia baada ya uhuru wamesaidia sana kuliinua bara la Afrika kwa kuwapatia elimu vijana wengi ambao hivi sasa ni nguzo muhimu katika bara la Afrika na hivyo watu wanapaswa kujipongeza  japo bado ipo kazi kubwa mbele.
Mh Festus Mogae anachukua miki na kusema kuwa viongozi wa Afrika wanapaswa kuangalia mambo kwa kina kabla ya kuamua kufanya maamuzi huku akitolea mfano hali ya machafuko iliyotokea huko Afrika Kusini na kuwa yaweza pia ikawa funzo bora kwa vingozi wengine wa Afrika.
 
Aidha kiongozi mkongwe katika viongozi wa Afrika Mh Yoweri Museveni ambaye kwa miaka mingi amekuwa madaraki tangu enzi za rais wa kwanza wa Tanzania hayati Mwalimu Julias Nyerere amesema umoja wa bara la Afrika ungeweza kufanikiwa mapema sana ila tatizo kubwa ni kwa sababu baadhi ya viongozi wanaonekana kutoweka mbele jambo hilo.
 
Mh Bakili Muluzi ambaye ni rais mstaafu nchini Malawi akizungumza katika mkutano huo amesema moja jambo muhimu na zuri ambalo viongozi wa Afrika walipaswa kulifanyia kazi haraka ni kuondoa hati ya kusafiria katika nchi zao ili kuongeza uhuru wa watu kufanya biashara  kwani vibali hivyo vimekuwa havina tija.
 
Rais wa awamu ya tatu wa Tanzania Mh Benjamni Mkapa na ambaye ni kiongozi wa taasisi ya uongozi waliondaa mkutano huo amesema ni zaidi ya miaka hamsini tangu harakati za kutaka bara la Afrika kuwa  nchi moja lakini utekelezaji wake umekuwa wa kusua sua kutokana na kila mtu kudhani kuwa wakiunganna uhuru na nanafsi yake itakuwa imepotea na hivyo ni lazima wabadilike.
 

HILI NDILO GARI LA KISASA LA KUBEBA MAJENEZA NCHINI TANZANIA

IMG_0469
Pichani juu na chini ni muonekano wa Gari maalum la kukodisha kwa ajili ya shughuli za kubebea majeneza katika misiba limeingia nchini.
Kwa wanaohitaji kukodi kwa shughuli za misiba wanaweza kuwasiliana kupitia barua pepe kiwiaadavidson@hotmail.com au simu namba +255 715 213213, +255 713 616606 na +255 784616606
IMG_0459 IMG_0481
Muonekano wa ndani sehemu maalum linapowekwa jeneza.
IMG_0477

July 30, 2015

MKUTANO WA KUJADILI CHANGAMOTO ZA WALEMAVU WA CHAMA CHA WATAALAM WA USTAWI WA JAMII NCHINI(TANZANIA ASSOCIATION OF SOCIAL WORKERS) WAFANYIKA KWA SIKU MBILI IRINGAViongozi wa Chama cha wataalamu wa Ustawi wa Jamii katikati ni Mgeni rasmi Katibu tawala Mkoa wa Iringa(kushoto)ni Dr Labikila Mushi Kaimu Kamishina wa Ustawi wa Jamii na (kulia ni Mwenyekiti wa chama hicho akizungumza na washiriki wa Mkutano huo.

Bw.Hussen Kashindye Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi ofisi ya DCI akizungumza na wandishi wa habari.
Mwanaharakati wa masuala ya walemavu nchini Bw Fredrick Msigala akizungumza na wanahabari Iringa
Mwenyekiti wa Chama Cha Walemavu mkoani Iringa Helen Machibya akizungumza na wanahabari.
Maofisa ustawi wa Jamii Manispaa ya Iringa katika mkutano.
Wataalamu na washiriki wa Mkutano wa (TASWO) wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi.
Wadau mbalimbali wa masula ya ustawi wa Jamii wamekutana mkoani Iringa kwa mkutano wa mwaka wa Chama cha  wanataluma ya Ustawi wa jamii kwaajili ya kujadili na kutafuta mbinu mbalimbali za kutatua changamoto zinazo  wakabili watu wenye ulemavu.
       Akizungumzia mkutano huo Kaimu Kamishina wa Ustawi wa Jamii Dr Labikila Mushi alisema mkutano huo umelenga kujadili changamoto pamoja na kutafuta njia za kuzitatua changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu nchini hususani watu wenye ulemavu  pia kujadili tatizo la mauaji ya watu wenye ulemavu wa Ngozi yaani Albino.
       Alisema wataalamu hao wamekutana ili kuweza kutafuta njia sahihi ya kulisaidia Taifa kuondokana na Aibu ya mauaji ya Albino ambapo Katika mkutano huo umewahusisha Maofisa ustawi wa Jamii,Jeshi la Polisi kitengo cha Upelelezi,maofisa wa Tuma ya haki za binadamu,Ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali,ambao kwa pamoja watajadili kwa kina namna ya kuliondoa taifa kwenye aibu hiyo ya mauaji ya Albino.
     “hapa wapo wataalamu mbalimbali kutoka maeneo na ofisi mbalimbali ambao watatoka na jibu moja za namna ya kuzitatua changamoto hizo ninaamini tutapokea michango mingi ya mawazo ya jinsi ya kukabiliana na kuziondoa imani potofu walizonazo miongoni mwa wanjamii kuwa kiungo cha albino kinaweza kumletea utajiri na kuendelea kuwamaliza watu wasio na hatia” alisema Mushi
       Akielezea takwimu ya matukio yanayowahusisha Albino kuanzia Mwaka 2006 hadi Much 2015 kamishina msaidizi wa Polisi kutoka ofisi ya mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya Jinai Bw Hussen Kashindye alisema Katika kipindi cha miaka kumi yapo matukio 56 yanayo wahusisha walemavu wa ngozi ambapo matukio 43 yalihusu kuuawa wa walemavu na matukio 13 ni Kujeruhiwa ambapo alisema Katika matukio hayo yote watuhumiwa 12 walihukumiwa adhabu ya kifo na mengine 10 yapo Katika hatua ya upelelezi.
     Alisema moja kati ya mambo yanayokwamisha kukamilika kwa upelelezi ni kushindwa kupata ushirikiano kutoka kwa wananchi jambo ambalo amesema linakwamisha jitihada za kuwapata wahalifu hivyo alisema ikiwa wananchi watashiri kikamilifu kutoa taarifa kwa sahihi za waharifu zitasaidia kumaliza tatizo.             “tumejitahidi sana kutoa elimu kwa jamii kupitia kitengo cha polisi jamii ambapo tumepeleka mpaka Katika kata ili kufanya kazi kwa ukaribu zaidi bila shaka endapo tutawatumia wale askari kata na wakaguzi wa Tarafa tutakomesha matukio yote ya kiharifu” alisema kashindye
       Wakizungumza Katika mkutano huo  Bw Fredrick Msigala mwanaharakati wa watu wenye ulemavu pamoja naye Helen Machibya ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha watu wenye ulemavu wa ngozi Mkoa wa Iringa  wamesema kuwa kumekuwa na changamoto nyingi  Katika sekta ya afya ambazo zimekuwa zikikwamisha jitihada za watu wenye ulemavu kupata huduma hizo.
       Walisema kuwa Katika maeneo mengi ambayo huduma za afya zinatolewa miundombinu siyo rafiki hususani uwepo wa majengo marefu ambayo hayana njia maalum kwa ajili ya kuwawesha watu wenye ulemavu kupanda na kuonana na wataalamu,pia walisema kumekuwa na wahudumu wasio na uelewa wa namna ya kumhudumia mtu mwenye ulema hususani wa ngozi jambo linalowefanya kupoteza maisha pamoja na uwepo wa vitendo vya unyanyapaa kwa walemavu vitendo ambavyo mara nyingi vinawafanya kukosa haki zao za msingi.

Cameron atakiwa asiwadhalilishe wahamiaji

 
Waziri mkuu wa Uingereza ameibua utata, kwa kuwafananisha wahamiaji haramu wanaojaribu kuvuka mpaka na kuingia Uingereza kama ''bumba la nyuki''.
        Baraza linalowashughulikia wakimbizi Nchini Uingereza, limesema kuwa hiyo ni "Lugha ya kuwadunisha watu'' hususan maneno hayo yakitoka kinywani mwa kiongozi kama mwenye hadhi kubwa ''duniani". ''Ni lugha ya kutamausha''.
       Waziri huyo mkuu ambaye yuko ziarani Vietnam alikuwa akitoa maoni kuhusiana na purukushani katika mji wa Calais, nchini Ufaransa, ambapo mamia ya wahamiaji,
wanajaribu kwa usiku wa tatu kuvuka mpaka na kuingia Uingereza wakitumia kivukio cha chini kwa chini.
        Bwana Cameron amesema kuwa Uingereza haitakuwa ''mahala salama'' kwa wahamiaji wanaotokea mji huo wa Calais.
Aidha bwana Cameron ameonya kuwa serikali yake itafanya kila iwezalo kulinda mipaka ya Uingereza.
      Afisa wa Umoja wa mataifa, Peter Sutherland, anawashutumu wanasiasa wa Uingereza kwa kushughulikia jambo hilo kwa matamshi ya ''chuki dhidi ya wageni'' na matumizi ya lugha ya kuwadhalalisha.

SHULE YA MSINGI YAFUNGWA MIEZI MIWILI KWA KUKOSA CHOO CHA WANAFUNZI MOROGORO


Katika hali isio ya kawaida shule ya msingi juhudi wilaya Morogoro imefungwa kwa  zaidi ya miezi miwili kutokana na kukosa choo ambapo  wazazi wamelazimika kuchangishana na kujenga matundu ya vyoo lakini hadi sasa serikali haijafungua shule hiyo huku wanafunzi wakizagaa mitaani kwa zaidi ya miezi miwili bila kusoma.
Wakizungumza kwa jaziba wazazi  wananchi  wa kijiji cha Mtego wa Simba ilipo shule hiyo  wamemlalamikia kuwa baada ya shule kufungwa wamelazimika kuchangishana fedha na kutengeneza matundu ya vyoo 13 lakini hadi sasa shule haijafunguliwa huku walimu wanaonekana wakizagaa mitaani na wakiendelea kupokea mishahara bila kufanya kazi ambapo wazazi hao wametishia kuhamisha watoto wao endapo serikali haitafungua shule hiyo.
 
Naye afisa elimu wa wilaya ya Morogoro Bw.Donald Pambe akijibu tuhuma za malalamiko ya wazazi amesema ni kwelishule zilifungwa kwa utaratibu kutokana  na kukosa matundu ya choo lakini ameahidi kutuma timu yake kufanya ufuatiliaji

July 29, 2015

KONGAMANO LA WADAU WA SEKTA YA AFYA TANZANIA ASSOCIATION OF SOCIAL WORKERS(TASWO) KUFANYIKA KWA SIKU MBILI IRINGA.

Viongozi wa Mradi wa Uimarishaji wa mifumo ya afya na ustawi wa jamii wakizungumza na wandishi wa habari juu ya kongamano hilo.
Wandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali Iringa
Wadau wa sekta ya afya nchini wanatarajia kukutana mkoani Iringa kwa siku mbili kuanzia Tarehe 30-31,july 2015katika kongamano maalum linalolenga kujadili changamoto mbalimbali zinazoyakabili makundi mbalimbali ya jamii.
      Akizungumzia adhima ya kongamano hilo Katika kikao na wandishi wa habari Katika ukumbi wa mganga mkuu wa Hospitali ya Rufaa Iringa Katibu Mkuu wa Chama Cha Wataalamu wa ustawi wa jamii Tanzania “TANZANIA ASSOCIATION OF SOCIAL WORKERS”(TASWO)Bw Nicolaus Mshana alisema wadau hao watakutana mkoani humo kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya kiafya pamoja na Changamoto mbalimbali zinazo ikabili jamii na kupata nafasi ya kujadili njia za kuzitatua.
       Alisema kongamano hilo lililoandaliwa na mradi wa Uimarishaji wa mifumo ya afya na ustawi wa jamii unaolenga kuunganisha nguvu ya pamoja Katika kupambana na vitendo vya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi yaani Albino pamoja na kupiga vita maambukizi mapya ya virus vya Ukimwi kwa watu wenye changamoto.

      Bw Mshana alisema Katika kongamano hilo wadau hao watajadili changamoto hiyo inayoendelea kulitia doa Taifa na kuona namna wadau hao wanavyoshiriki Katika kupiga vita vitendo hivyo na kujadili mbinu za kulitatua. “tunatambua tuna changamoto nyingi lakini kuna hili suala la mauaji ya Albino ni suala ambalo limeikera jamii,limeiabisha serikali yetu,hivyo sisi kama wanataaluma tunahusika Katika hili ndo maana tukaona tujikusanye na wataalam wengine tukae wote kwa pamoja tuone nini tunaweza kufanya kwa pamoja ili tujikwamue” alisema Mshana
         Aidha Katika kongamano hilo alisema watajadili masuala ya Maambukizo ya Virusi Vya Ukimwi ambalo alisema kuwa kwa upande wa watu wenye ulemavu linaonekana kuwa kwao ni tatizo lenye uzito zaidi kutokana na imani mbaya iliyojengeka miongo mwa walemavu hususani wa Ngozi.

        “tukiunganisha nguvu lazima tutashinda vita hivi dhidi ya madhira  wanayotapata watu wenye ulemavu ikiwemo kutengwa na jamii” alisema

         Kwa upande wake mshauri wa jamii Katika mradi huo Bw Joseph Kayinga alisema kwa kiasi kikubwa jamii ya watu wenye ulemavu ina kabiliwa na changamoto ya kutopata huduma bora zinahusiana za maambukizi ya virusi vya ukimwi pengine kutokana na woga.

         “sasa Katika kumuangalia huyu ambaye changamoto hizi zina muhusu yeye kongamano hilo litajibu yale yote ambayo kundi la walemavu linahatarishiwa zaidi” alisema kayinga

          Naye Afisa Ustawi wa jamii mkoani Iringa Bw Samwel Nyagawa akitolea maelezo ya namna mradi huo utakavyofanya kazi Katika mkoa wa Iringa alisema wamejikita zaidi Katika wilaya mbili ambazo ni Wilaya ya Mufindi na Manispaa ya Iringa ambapo Katika wasitani wa maambukizi ya virusi vya UKIMWI wilaya hizo ndizo zinazoongoza kwa mujibu wa takwimu.