Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

June 30, 2015

MAJAJI WA BONGO STAR SEARCH WAJUMUIKA NA WATOTO YATIMA KULA IFTAAR YA PAMOJA

Majaji wa Bongo Star Search kuelekea msimu wa nane wa BSS2015 wamejumuika na watoto Yatima wa kituo cha Chakuwama kilichopo mwenge, Dar Es Salaam na kula Iftaar kipindi hiki cha mfungo wa Ramadn na kutoa misaada mbali mbali.

Kituo hicho ambacho kina jumla ya watoto yatima 100 kuanzia wachanga mpaka miaka 16 na wahudumu 10.

Madam Rita na Master Jay Kwenye Iftaar kituo cha watoto Yatima Chakuwama

Madam Rita na Bi Hadija Mlezi wa kituo cha Chakuwama

Mmoja wa watoto wanaolelewa kwenye kituo cha Chakuwama

Mtoto akipiga picha

Baadhi ya watoto wakisubiri Iftaar

Watoto wakichukua Iftaar tayari kwa kufuturuMaster Jay na Madam Rita wakifuturu

Madam Rita akichukua Iftaar

Master Jay Akichukua Iftaar

Baadhi ya Watoto wakipita kuchukua Iftaar

Mmoja wa watoto akionesha kipaji cha kucheza

Mmoja wa watoto akionesha kipaji cha Kuimba

Majaji wa BSS wakipiga picha ya pamoja na watoto
Madam Rita na Master Jay wakitoa Misaada kwa katibu wa kituo

Bi Hadija ambaye ni Mlezi wa Watoto kwenye kituo cha Chakuwama


Kiongozi wa mbio za mwenge Kitaifa ampongeza Filikunjombe

Kiongozi wa Mbio za mwenge Kitaifa Bw Juma Chum akimpongeza mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe kwa jitihada zake za kimaendeleo 
Mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe akizungumza na wananchi 

MWILI WA MKE WA MWANAHABARI THOBIAS MWANAKATWE WA KAMPUNI YA THE GUARDIAN ALIYEFARIKI KWA KUGONGWA NA GARI NJE YA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE WAAGWA JIJINI DAR ES SALAAM KUZIKWA KARATU MKOANI ARUSHA

 Mhariri wa Gazeti la Nipashe, Jesse Kwayu (kushoto), na waombolezaji wengine wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa mke wa mwanahabari wa Kampuni ya The Guardian, Thobias Mwanakatwe, Levina Genda wakati wakilipekeka kwenye gari tayari kwa safari ya kwenda Karatu mkoani Arusha kwa mazishi yatakayofanyika kesho.
 Mwanahabari wa Kampuni ya The Guardin Ltd, Thobias Mwanakatwe akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa mke wake, Levina Genda wakati wa ibada ya kumuaga iliyofanyika Hospatali ya Amana Dar es Salaam leo a. Mke wa Mwanakatwe alifariki kwa kugongwa na gari maeneo ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere mwishoni mwa wiki.
 Waombolezaji wakiwa kwenye ibada ya kumuaga Levina Genda, iliyofanyika Hospitali ya Amana Ilala Dar es Salaam leo asubuhi.
 Hapa ni huzuni umetawala.
 Wafanyakazi wenzake na Thobias Mwanakatwe wa Kampuni ya The Guardian wakiwa wamejiinamia kwa huzuni.
 Thobias Mwanakatwe (katikati), akiwa na wafanyakazi wenzake waliofika kumfariji.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Levina na waombolezaji wengine wakiwa kwenye ibada ya kumuaga mpendwa wao.
 Kiongozi wa dini kutoka kanisa la Katoliki akiongoza ibada ya kumuombea marehemu.
 Ibada ikiendelea.
 Mwakilishi wa wanahabari kutoka mkoani Mbeya ambako Mwanakatwe alikuwa akifanyakazi kabla ya kuhamia Dar es Salaam, Patrick Kosima akitoa akizungumza katika ibada hiyo kabla ya kutoa rambirambi ya sh.220,000.
 Mhariri wa Gazeti la Nipashe, Jesse Kwayu (katikati), akizungumza katika ibada hiyo wakati akiwasilisha salamu za rambirambi za Kampuni ya The Guardian.
 Mdau Fabiola Bula wa Karatu, akitoa heshima za mwisho kwa marehemu. 
 Heshima za mwisho kwa marehemu zikiendelea.
 Wafanyakazi wa Kampuni ya The Guardian wakitoa heshima za mwisho kwa wifi yao, Levina Genda. 'Hakika ni huzuni tupu'
Jeneza likiingizwa kwenye gari tayari kwa safari ya kwenda Karatu kwa mazishi.
(Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com

MWENYEKITI WA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA IRINGA AWA MMOJA KATI YA WASHINDI WA TUZO ZA TANAPA

Meneja Mawasiliano wa Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) ,Pascal Shelutete akitoa neno la ukaribisho katika hafla ya utoaji tuzo kwa wanahabari waliofanya vizuri katika uandishi wa masuala ya Uhifadhi.Hafla iliyofanyika katika Hotel ya Gorden Crest jijini Mwanza.  
Baadhi ya wageni waalikwa katia hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Hifadhi za Taifa ,Tanzania (TANAPA) Allan Kijazi akizungumza katika hafla hiyo juu ya lengo la kuanzishwa kwa tuzo hizo kwa wanahabari nchini.
Mkuwa wa Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza,Baraka Konisaga akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Mwanza wakati wa hafla ya utoaji tuzo kwa Wanahabari waliofanya vizuri katika uandishi wa masuala ya Uhifadhi.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo,Waziri wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu akizungumza wakai wa hafla ya kukabidhi tuzo kwa washindi wa Tuzo zitolewazo na TANAPA kwa wanahabari.
Mkuu wa Majaji walioshiriki kupatikana kwa washindi wa tuzo zitolewazo na TANAPA kwa wanahabari,Dkt Ayoub Ryoba akizungumza katika hafla hiyo.
Dkt Ryoba akitambulisha majaji wenzake walioshiriki katika kupata washindi.
Mgeni Rasmi katika hafla hiyo,Waziri wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu akimkabidhi Frank Leonard mwenyekiti  wa chama  cha  waandishi  wa habari  mkoa wa Iringa (IPC)akitoa ,Ngao,Vyeti pamoja na mfano wa Hundi kwa washindi wa tuzo za TANAPA 2014 zitolewazo kwa wanahabari .
Mkuu wa Majeshi Mstaafu,Meja Jenerali ,Mirisho Sarakikya akizungumza katika hafla hiyo zaii akizungumzia historia ya namna alivyoshiriki zoezi la kupanda Mlima Kilimanjaro zaidi ya mara 38.
Mgeni Rasmi katika Hafla hiyo,Lazaro Nyalandu ,akitunuku tuzo kwa Meja Jenerali,Mirisho Sarakikya pamoja na kitambulisho maalumu ambacho kitamuwezesha kuingia bila malipo katika hifadhi 16 za Taifa.
Meja Jenerali ,Sarakikya akifurahia zawadi hiyo iliyotolewa na TANAPA.
Mwandishi wa Habari wa Channel ten Cassius Mdami akizungumza kwa niaba ya washindi wa tuzo hizo.
Mgeni rasmi ,Lazaro Nyalandu akiwa katika picha ya pamoja na washindi.
Mgeni rasmi ,Lazaro Nyalandu akiwa katika picha ya pamoja na wahariri katika vyombo mbalimbali vya habari.
Mgeni rasmi ,Lazaro Nyalandu akiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari walioshiriki katika hafla hiyo.
 

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini aliyeko jijini Mwanza.