Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

April 30, 2015

TFF YAIKABA KOO SIMBA YAITAKA IMLIPE CHANONGO MIL 11


Klabu ya Simba SC inatakiwa kumlipa mchezaji Haruni Chanongo sh. 11,400,000, kufikia Aprili 30, 2015 vinginevyo Sekretarieti ya TFF itaanza kukata mapato ya Simba ili kumlipa mchezaji huyo. Iwapo Simba itakuwa na vielelezo vingine katika kikao kinachofuata cha Kamati kitakachofanyika Mei 3, 2015 itafanywa hesabu na Simba kurejeshewa fedha itakayokuwa imezidi. 

 Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF imeagiza kwa klabu ya Simba na klabu nyingine zote kuwa kwa wachezaji wa mkopo, maslahi yao (mishahara na posho) yote yailipwe na klabu husika kwa klabu ambayo mchezaji anakwenda kwa mkopo ili malipo yake yawe yanafanyika kutoka kwenye klabu moja badala ya kufuatilia malipo yake katika klabu mbili tofauti, hali hii inaweza msabababishia usumbufu mchezaji aliye kwenye mkopo. 

 Amissi Tambwe vs Simba Sports Club Mchezaji Amissi Tambwe aliwasilisha malalamiko dhidi ya Simba ya kutolipwa dola 7,000 za Marekani zilizotokana na klabu hiyo kuvunja mkataba wake Desemba 15, 2014. 

Uamuzi wa kuvunja mkataba ulikuwa ni wa makubaliano ya pande zote ambapo Simba ilitakiwa iwe imemlipa fedha hizo mlalamikaji kufikia Desemba 17, 2014. Katibu Mkuu wa Simba SC , Steven Ally alikiri klabu yake kudaiwa na mchezaji huyo na kuwa wameshafanya mawasiliano na wakili wake aliyepo Ureno, Felix Majani na kupanga utaratibu wa kulipa isipokuwa kinachosubiriwa ni kusaini hati ya makubaliano ya malipo (Deed of Settlement).
 
 Kamati imesikitishwa na klabu ya Simba kushindwa kumlipa mchezaji huyo kama ilivyokuwa katika makubaliano ya kuvunja mkataba yaliyofikiwa na pande zote mbili Desemba 15, 2014. Klabu ya Simba inatakiwa kumlipa Amissi Tambwe fedha hizo kwa awamu mbili. 

Awamu ya kwanza ya dola 5,000 malipo yawe yamefanyika kufikia Aprili 30, 2015. Salio la dola 2,000 ili kukamilisha jumla ya dola 7,000 liwe limelipwa kufikia Mei 10, 2015, uamuzi ambao upande wa Simba ulikubaliana nao.

 Amiri S. Msumi vs Ndanda SC Klabu ya Ndanda SC imeamuriwa kumlipa mchezaji Amiri S. Msumi kiasi cha fedha sh. 2,600,000. Pia Kamati ilihoji mkataba kutokuwa na kipengele cha mshahara, na kusema ni lazima mkataba uonyeshe Kaiser ambacho mwajiriwa analipwa. 

 Pia Kamati imeagiza kuwa vilabu vifahamishwe kuwa fedha ya kusaini mkataba (sign on fee) hazitakiwi kulipwa kwa mafungu. 

Tafsiri ya fedha ya kusaini, ni mchezaji kulipwa fedha yote baada ya kusaini, na si kwa mafungu. 

Pamoja na uamuzi huo, Katibu Mkuu wa Ndanda SC ametakiwa kuwepo kwenye kikao cha Mei 3, 2015. 

Malalamiko mengine yataendelea kusikilizwa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji Mei 3, mwaka huu. 

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

NMB YAKABIDHI HUNDI YA SH. BILIONI 1.5 KUCHANGIA MADAWATI WAZIRI MKUU

 
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipokea kutoka kwa Kaimu Mtendaji  Mkuu wa Benki ya NMB, Bw. Tom Borghols  mfano wa hundi ya shilingi Bilioni 1.5 ukiwa ni mchango wa Benki ya NMB kwa  Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ili zisaidie kutatua tatizo la madawati kwa shle za msingi nchini. Kiasi hicho cha fedha kitatolewa kwa miaka mitano. Makabidhiano hayo yalifanyika ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Aprili 29, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 .........................................................................................................................................................
Mizengo Pinda amepokea hundi ya mfano (dummy cheque) yenye thamani ya sh. bilioni 1.5 kutoka benki ya NMB zikiwa ni mchango wa taasisi hiyo kwenye kampeni ya uchangiaji madawati kitaifa.

 Akizungumza na Waziri Mkuu ofisini kwake Magogoni jijini Dar es Salaam jana jioni (Jumatano, Aprili 29, 2015), kabla ya kukabidhi hundi hiyo, Kaimu Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Bw. Tom Borghols alisema wameamua kutoa mchango ili kusaidia kupunguza tatizo la uhaba wa madawati linalozikabili shule za msingi na za sekondari hapa nchini. 

 “Tunaelewa kwamba shule nyingi hapa nchini zinakabiliwa na uhaba wa madawati … tunaamini kuwa elimu bora inachangiwa pia na mazingira mazuri ya kusomea ikiwa ni pamoja na kukaa kwenye madawati wanapoandika.

 Kama sehemu ya mchango wetu kwa jamii (CSR), tumeamua kutenga sh. bilioni 1.5 ili zisaidie kupungua tatizo hilo,” alisema. 

Akipokea mchango huo, Waziri Mkuu aliushukuru uongozi wa benki hiyo ulioambatana na Bw. Borghols kwa kuamua kusaidia juhudi za Serikali kutatua tatizo hilo. Alisema mchango huo ni mkubwa na anaamini kwamba utawachochea wadau wengine kuchangia juhudi za Serikali kutatua tatizo la madawati nchini. 

 “Nimecheki na watu wangu kwa kweli mahitaji ni makubwa lakini naamini mchango wenu utasaidia kupunguza tatizo la madawati kwa kiasi fulani. Tunawashukuru kwa uamuzi wenu wa kuchangia suala hili la kitaifa,” alisema. 

 Hadi sasa Serikali inahitaji kununua madawati 1,016,476 kwa ajili ya shule za msingi na za sekondari. 

Kati ya hayo, madawati 892,772 yanahitajika kwa ajili ya shule za msingi na madawati 123,704 yanahitajika kwa ajili ya shule za sekondari. Madawati hayo yote yataigharimu Serikali kiasi cha sh. bilioni 91.4/- kwa gharama ya sh. 90,000/- kwa kila dawati.

 Hata hivyo, Serikali iliamua kutenga fedha za chenji ya RADA ili zitumike kununua madawati na vitabu. Fedha hizo, zilisaidia kununua madawati 168,163 kwa bei ya sh. 90,000/- kwa dawati moja. 

 (mwisho)

AJALI MBILI LEO IRINGA ZAUA MMOJA ,18 ABIRIA WA BASI LA EMBAKASY WANUSURIKA KIFO

Baadhi ya  wananchi  wa  mjini Iringa na abiria  wa basi la Embakasy  wakitazama basi hilo  lililopinduka leo eneo la Ipogolo mjini Iringa .

AJALI yanua mmoja  Iringa huku abiria  18  wakinusurika   kifo baada ya  basi  la kampuni ya  Embakasy  lenye namba  za  usajili  T 997 AKJ kuacha  njia ya  kupinduka  eneo la Ipogolo  mjini Iringa.

Wakizungumza na mtandao huu  wa martukiodaima    eneo la  ajali  baadhi ya abiria  wa  basi hilo  walidai  kuwa basi  hilo  lilikuwa  likitaka kuingia katika  kituo  kimoja  wapo  cha  mafuta eneo hilo  na  wakati  likitoka  ndipo  liliponusurika  kugongana na lori  lililokuwa barabara  kuu ya Iringa - Mbeya   .

Hivyo  kutokana na kunusuri kugongana ndipo  dereva wa  basi hilo alipoamua  kulikwepa lori  hilo kwa  kukata  kuna kubwa  zaidi  iliyopelekea  basi hilo  kuacha  njia na  kupinduka kando ya  barabara  hiyo .

Walisema  kuwa  basi  hilo  limekuwa  likifanya  safari  zake kati ya Ilandutwa wilaya ya  Iringa vijijini na Iringa mjini na  kuwa pona  yao katika ajali  hiyo ni  kutokana na kuwa katika  mwendo  wa kawaida  zaidi .

konda  wa  basi hilo  Bw  Esack  Mtandi  alielezea  tukio  hilo  alisema  kuwa  basi   hilo  lilikuwa  likitaka  kuingia kujaza mafuta  katika  kituo  kimoja wapo cha  mafuta kilichopo  eneo  hilo na  mbele  kulikuwa na  lori  na  wakati   dereva  akijiandaa  kuingia  kituoni  hapo  ghafla usukani  uligoma na  hivyo  kumtoa  dereva  nje ya barabara kabla ya  kupinduka .

Alisema  katika basi  hilo kati ya abiria  18  waliokuwepo  abiria  6  ndio  waliojeruhiwa akiwemo  dereva na  hakuna  aliyepoteza masisha .

Kwa  upande  wake  jeshi la  polisi  mkoani Iringa  limethibitisha  kutokea kwa ajali hiyo na  kuwa  ajali   hiyo  ilitokea majira  ya saa 3  kasoro asubuhi ya  leo   na  kumtaja  dereva  wa  basi hilo  kuwa ni Abdalah Nyalusi 

Alisema  kamanda  wa  polisi  mkoa  wa  Iringa Ramadhan  Mungi na  kuwa katika  ajali  hiyo  hakuna abiria  aliyepoteza maisha .
 
Wakati  huo  huo mmoja kati ya  wafanyabiashara  maarufu mji  wa Ilula   wilayani  Kilolo  mkoani hapa  aliyefahakika  kwa jina  moja la kasim aliyekuwa  akiendesha gari  lenye namba za  usajili T 111 GRE RAV4 amekufa  papo  hapo baada  ya kugongana  uso  kwa  uso la lori .

Kamanda  Mungi  alisema  kuwa mfanyabiashara   huyo  alikuwa  akitokea  Ilula  kuja  Iringa  mjini na baada ta  kufika  eneo la kona  ya Igumbilo  barabara  kuu ya  Iringa - Dar es salaam  wakati  akijaribu kulipita daladala  lililokuwa mbele yake  katika  kona    hiyo ghafla  alikutana na lori  hilo na kugongana  nalo .

Hata  hivyo  alisema  jina kamili  la mtu  huyo bado  kufahamika na  kuwa  wanasubiri  ndugu zake  ili  kujakutambua mwili  huo na  kutoa  jina kamili.


Watuhumiwa watatu wa ujambazi kidondo wauwawa wakutwa na silaha nzito na mabomu


Jeshi la polisi Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma  usiku wa kuamkia leo limefanikiwa kuwaua watuhumiwa watatu wa ujambazi  ambao walikuwa   na SMG moja mabomu matatu pamoja na risasi ishirini na mbili 

April 29, 2015

RAIS KIKWETE AZINDUA MELI MBILI ZA KIVITA


Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua mara baada ya kuzindua rasmi meli vita mbili za doria bahari kuu TNS Msoga na TNS Mwitongo kwenye sherehe zilizofanyika Kamandi ya Jeshi la Maji Kigamboni jijini Dar es salaam leo April 28, 2015

 Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata picha ya kumbukumbu na makamanda wa meli vita mbili za doria bahari kuu TNS Msoga na TNS Mwitongo kwenye sherehe zilizofanyika Kamandi ya Jeshi la Maji Kigamboni jijini Dar es salaam leo April 28, 2015( picha na Ikulu)

April 27, 2015

SERIKALI KUIIMARISHA OFISI YA TAKWIMU – WAZIRI MKUU


WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema Serikali imedhamiria kuiimarisha Ofisi ya Takwimu ya Taifa ili iweze kutoa huduma bora siyo tu kwa Serikali bali hata kwa wananchi kwa sababu wana haki ya kupatiwa takwimu sahihi.

Ametoa kauli hiyo leo asubuhi (Jumatatu, Aprili 27, 2015) wakati akifungua kongamano la siku tatu kuhusu Uongozi na Usimamizi wa Mifumo ya Takwimu liliondaliwa na Taasisi ya Kimataifa ya Takwimu (International Statistical Institute – ISI) kwenye hoteli ya Giraffe jijini Dar es Salaam.

 

Akizungumza na wakuu wa taasisi za takwimu barani Afrika wanaoshiriki mkutano huo, Waziri Mkuu alisema Kongamano hilo limekusanya washiriki zaidi ya 50 kutoka nchi 31 za Afrika zinazozungumza Kiingereza kwa nia moja ya kuweka msukumo kwenye umuhimu wa matumizi ya takwimu katika kuleta maendeleo ya nchi husika.

 

“Kama nchi, Tanzania tunakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa takwimu lakini tumeanza kulitazama jambo hili na ndiyo maana nimesema Serikali imedhamiria kuiwezesha taasisi hii ya takwimu ili itoe takwimu sahihi kwa Serikali kwa upande mmoja na kwa wananchi kwa upande mwingine…wao ni wadau wakuu wa takwimu hizi,” alisema Waziri Mkuu.

 

“Tuna lengo la kuifanya taasisi hii iwe na hadhi ya kimataifa katika kutoa takwimu zake. Sote tunatambua kwamba ulimwengu wa sasa ni wa kidigitali, na bila kuwekeza kwenye hilo hatuwezi kufika mbali,” alisema.

 

Aliwataka wakuu wa taasisi za takwimu barani Afrika waangalie uwezekano wa kufanya kazi kwa karibu pamoja Halmashauri za miji na wilaya kwani huko ndiko kwenye rasilmali kubwa ya takwimu na ndiko maendeleo ya wananchi yaliko.

 

“Ukichukua mfano wa Tanzania, tuna Halmashauri za Wilaya na Miji zaidi ya 160. Mkiamua kufanya kazi kwa karibu na Serikali za Mitaa mtapata takwimu za ajabu kwani huko ndiko kwenye miradi yote ya maendeleo. Tukumbuke kuwa asilimia 75 hadi 80 ya Watanzania wote wanaishi vijijini,” alisema.

 

Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kufungua kongamano hilo, Waziri wa Nchi (OWM-TAMISEMI), Bibi Hawa Ghasia alisema takwimu ni mali ya umma na hazipaswi kutolewa kwa upendeleo.

Waziri Ghasia ambaye alizungumza kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Bibi Saada Mkuya, alisema takwimu zenye ubora na ubunifu ni muhimu sana kwa ajili ya kupanga kazi za maendeleo ya Taifa.

 

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Takwimu ya Taifa, Dk. Albina Chuwa alisema kuna haja ya Serikali za nchi za Afrika kuweka kipaumbele kwenye suala la upatikanaji wa takwimu na lisiwe suala la kuchukuliwa kijuujuu tu, bali lichukuliwe kama sekta kamili ya kipaumbele.

 

“Naziomba nchi za Afrika zianze kuchukulia takwimu kama sekta ya kipaumbele kwenye mipango yao ya maendeleo ya Taifa… tunapokaribia kuhitimisha muda wa kutekeleza malengo ya milenia (MDGs), tunapaswa kujielekeza kwenye viashiria vipya zaidi ya 300 ambavyo vimeainishwa, hivi viko kwenye ngazi ya kitaifa, kikanda na kimataifa”.

 

“Katika bara la Afrika, kama hatutaamua kuainisha viashiria vyetu wenyewe kuanzia ngazi ya Kitaifa, wataibuka watu na kututengenezea viashiria ambavyo havina uhalisia kwa sababu hawajui matatizo ambayo bara la Afrika linakumbana nayo,” alisema Dk. Chuwa.

MALINZI AFUNGUA KOZI YA WAKUFUNZI

Rais wa TFF Malinzi

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF, Jamal Malinzi leo amefungua kozi ya walimu wakufunzi wa mpira wa miguu chini inayofanyika katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam.

 

Malinzi amesema kozi hiyo ni muhimu kwa mustakabali wa soka la Tanzania, walimu wakufunzi watasaidia kuwafundisha walimu wengine wa mpira, ili kuweza kufundisha mpira kwa watoto wadogo ambao ndio hazina ya baadae.

 

Malengo ya TFF ni kuhakikisha timu ya vijana ya U17 inafuzu kwa fainali za Mataifa Afrika 2017 nchini Madagscar, na baadae kuwa na kikosi bora wakati tunapotarajia kuwa wenyeji wa fainali za U17 Afrika mwaka 2019 "alisema Malinzi".

 

TFF ina program mbili za kuwaandaa vijana wenye umri chini ya miaka 13, 15 kwa kuwaweka kambini na kucheza michezo ya kirafiki mikoani na kufanya ziara katika nchi za Malawi, Zambia, Zimbabwe, Bostwana na Afrika Kusini.

 

Aidha Malinzi amewaomba walimu wakufunzi kuwa karibu na makocha wa timu za Taifa, na kuwapa ushauri makocha hao ili kuweza kuwasaidia katika kuboresha vikosi vyao na maendeleo ya soka la Tanzania kwa ujumla.

 

Naye Rais wa CECAFA na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya CAF, Leodgar Tenga alimshukuru Malinzi kwa kuweza kufungua kozi hiyo ambayo inawakutansisha walimu wakufunzi wa mpira miguu kutoka sehemu mbalimbali nchini.

 

 Akiongea kwa niaba wa walimu wakufunzi, Dr. Mshindo Msolla alisema wanaishukuru TFF kwa kuandaa kozi na kuomba kuendelea kushirikishwa katika mipango mbalimbali ya soka nchini ikiwa ni pamoja na kutambulika kuanzia katika ngazi za juu mpaka katika maeneo waliyopo.

 

Kozi hiyoiliyoanza leo jumatatu itamalizika Mei 2 mwaka huu, inawajumuisha walimu 18, wenye leseni A, B na C za CAF kutoka mikoa mbalimbali Tanzania bara na Zanzibar.

 

 

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)


-- 
Best Regards,
 
Baraka Kizuguto
MEDIA & COMMUNICATION OFFICER
A:I P.O.BOX 1574 Karume Memorial Stadium /Shaurimoyo/Uhuru Street I Dar es salaam ITanzania  
 

 
 

TFF KUKUTANA NA WANAHABARI APRIL 27Kesho jumatatu Aprili 27, 2015 kutakua na Mkutano na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa TFF uliopo Karume.

Waandishi wa habari mnaombwa kuhudhuria bila kukosa.

April 25, 2015

LUDEWA HATUHITAJI MGOMBEA UBUNGE MWINGINE ZAIDI YA FILIKUNJOMBE -WANANCHI

Mbunge  wa Ludewa Deo Filikunjombe akishirikiana,viongozi wa CCM , wananchi na mafundi  wa mradi wa umeme kubeba nguzo za  umeme katika  kitongoji cha Ngalawale Ludewa kijijini kama  sehemu ya kuhamasisha wananchi kushiriki maendeleo

Mbunge Filikunjombe wa kwanza  kulia na katibu mwenezi wa CCM mkoa wa Njombe Honoratus Mgaya wa  kwanza  kulia wakishirikiana na mafundi wa maradi wa  umeme vijiji kuvuta kama kwa ajili ya kusimamisha nguzo ya  umeme

 mbunge Filikunjombe kulia  na diwani wa kata ya Ludewa Monica Mchilo wakifukia  nguzo ya  umeme
 wananchi na  mbunge  wakisaidiana kufukia nguzo ya  umeme

wananchi na mafundi wa  umeme  wakijiandaa kubeba  nguzo


mbunge Filikunjombe  akishiriki  kubeba  nguzo ya  umeme

wananchi na  mbunge Filikunjombe wakiwa  wamebeba nguzo ya  umeme
katibu  mwenezi wa CCM mkoa wa NJOMBE Honoratus Mgaya akichimba shimo la nguzo ya umeme

mbunge Filikunjombe akiwa  chini ya shimo akishiriki  kuchimba shimo la nguzo ya  umeme  kitongoji cha ngalawale  kijiji  cha ludewa wengine ni diwani wa kata ya  Ludewa MONICA MCHILO ,katibu mwenezi wa ccm mkoa wa Njombe Honoratus Mgaya na katibu mwenezi  wa CCM ludewa FELIX Haule  wakishirikiana na mbunge  wao

 mbunge Filikunjombe akitoka  katika  shimo baada ya  kumaliza  kuchimba  shimo  moja la mfano kama kuhamasisha wananchi kushiriki katika maendeleo 
........................................................................................................................................

Na MatukioDaima BLOG Ludewa
WANANCHI wa  Ngalawale kata ya Ludewa  wilaya  ya Ludewa  mkoani Njombe  wameelezwa kufurahishwa na jitihada  za  kimaendeleo  zinazofanywa na mbunge  wao Deo Filikunjombe na kukionya chama   cha  mapinduzi (CCM) katika wilaya   hiyo kutowaletea mgombea mwingine  wa ubunge  zaidi ya Filikunjombe.

Akizungumza kwa  niaba ya  wananchi wa  kata  hiyo ya Ludewa  diwani wa kata  hiyo Monica  Mchilo alisema   kuwa toka  jimbo  hilo la Ludewa kuanza kuwa na wabunge pamoja na  kuwa  kila mmoja ana jambo la  kukumbukwa ambalo amepata  kulifanya katika   jimbo hilo ila hakuna hata  mbunge  mmoja kati ya wabunge  zaidi ya  watano waliopata  kuongoza  Ludewa  ambae amepata kutekeleza ahadi zake hata robo ya ahadi  alizopata   kutoa.

Diwani Mchilo alitoa kauli   hiyo leo  wakati wa mkutano wa hadhara  wa mbunge Filikunjombe  kuwapongeza  wananchi  hao kwa kukamilisha uchimbaji  wa mashimo ya nguzo  za  umeme katika  kijiji  chao .

Alisema   kuwa wakati mbunge huyo  akiingia madarakani  mwaka 2010 moja kati ya ahadi yake ni kuhakikisha wananchi  wa  vijijini ambao  wapo pembezoni na mji  wa Ludewa  wanapatiwa  umeme na  kuwa kabla ya kumaliza  muda  wake wa ubunge tayari ahadi  hiyo  imetekelezeka na ahadi nyingine  nyingi alizopata  kuzitoa  kwa  wananchi  wa  jimbo   hilo.

Hivyo  alisema kuwa inapendeza  kuwa wana Ludewa  kuendelea kumpa muda zaidi mbunge  Filikunjombe  ili azidi  kuleta maendeleo zaidi katika  jimbo hilo badala ya kuendelea  kubadili   wabunge kila   wakati jambo  linalokwamisha maendeleo ya jimbo hilo na kuishia kuwapata   wabunge wasio na mapenzi mema na maendeleo ya wananchi.

'Ludewa  kwa  miaka  mingi   tumeteseka  kwa  kumkosa  mbunge  mwenye  uchungu  wa  maendeleo ya  wananchi  wa jimbo hilo ila  kwa mara  ya kwanza Mungu  ametupatia mbunge mwenye uchungu  wa kweli na maendeleo  yetu  hivyo lazima tumkumbatie azidi  kutawala daima'


Akielezea   kuhusu  miradi mbali mbali iliyofanyika katika  kata  yake alisema  kuwa awali umeme ulikuwepo mjini Ludewa  pekee  kwa  kipindi chote  toka  nchi ipate  uhuru  wake mwaka 1961 na  kuwa umeme  huo  aliuleta aliyekuwa  mbunge  wao stanley kolimba ambae  kwa  sasa ni mwenyekiti  wa CCM wilaya ila  kwa  kipindi cha Filikunjombe  vijiji  zaidi  vimeendelea  kupatiwa umeme na maendeleo mengine  mengi  ikiwemo  barabara ya lami Ludewa mjini.

Diwani  huyo aliwataka  wananchi  wa Ludewa kutoyumbishwa na wale wote wenye uchu wa madaraka ambao wapo kwa  maslahi yao  na badala yake  kubaki njia kuu kwa  kuendelea kuwa na mbunge  Filikunjombe kwa  kipindi kingine  zaidi.

'kwa  kuwa utaratibu wa  chama ni kutangaza uchaguzi wa  kura za maoni ila kama ingeruhusiwa tungezuia chama kutoa fomu kwa wagombea wengine wa ubunge ....lakini tunakuhakikishia wewe endelea kufanya maendeleo bila hofu kwani ni mbunge wetu wa 2015-2020 na zaidi hadi mwenyewe utakaposema basi sisi tupo na wewe'

Katibu  mwenezi  wa CCM mkoa  wa Njombe Honoratus Mgaya  alisema mbali ya kubahatika   kuwa katibu mwenezi  wa mkoa  wa Iringa uliokuwa na wilaya zaidi ya 6 na majimbo zaidi ya 10 hakupata  kuona  mbunge anayejituma  kama Filikunjombe na  kuwa mbali ya  ubunge  wake  kuwanufaisha wananchi  wa Ludewa ila bado amefanikiwa  kuutangaza  mkoa  wa Njombe na kuwa moja kati ya  wabunge wa mfano katika bunge.

Mgaya alisema  kama wabunge wote wa CCM wangeifanya kazi  ya  kuwatumikia  wananchi kama anavyofanya mbunge  huyo  wa Ludewa uwezekano wa  wapinzani kwenda bungeni ungekuwa mdogo  zaidi  na kuwa chuki ya wananchi dhidi ya CCM  ni  kutokana na baadhi ya wabunge ,madiwani na viongozi wengine wa umma kushindwa kuwajibika katika kuwatumikia wananchi .

Nae mbunge Filikunjombe akiwashukuru wananchi hao  alisema  kuwa moja kati ya ndoto  yake ni kuona wananchi  wa Ludewa wanaungana na watanzania wengine  katika kunufaika na uhuru wao kwa  kupatiwa umeme na huduma  nyingine za kijamii.

Kwani  alisema amepata  kupigania  kuona wananchi  wa vijiji 14 vya jimbo la Ludewa ambao walikuwa  gizani kwa muda  wote wa nchi ilipopata uhuru wanapatiwa umeme kabla ya kumaliza kipindi chake  cha kwanza na ubunge na kuwa kamwe hatakubali  kuona mtu yeyote anashiriki kukwamisha ndoto yake  hiyo ya  kuwaletea maendeleo wananchi .

UZINDUZI WA CHANJO MKOA WA IRINGA-MUFINGA

Mkuu wa Wilayaya Mufindi Bi MBONI MHITA amewatakawazazinawaleziMkoaniIringakutosikilizamanenoyauzushikuwachanjozinazotolewakwaWatotonchinihuwazinamadhara, badalayakewajitokezekwawingikwenyevituovyakutoleachanjoilikuwakingawatotonauwezekanowakushambuliwanamaradhimbalimbali.TaarifayaofisiyahabarinamawasilianoyahalmashauriyaWilayayaMufindi, imeelezakuwa  ,Mkuuwawilayaaliyasemahayokatikakijiji cha SawalaWilayaniMufindiMkoaniiringawakatiakimwakilishaMkuuwaMkoawaIringakwenyeuzinduziwa wiki yachanjokwawatotowenyeumriwachiniyamiaka 5
Mhita

Alisema  ndapowazazinawaleziwatasikilizamanenoyasiyonaukweliwowote, watakuwawanahatarishaafyazawatotowaokwanikuzikosachanjohizomuhimukwaustawiwaMtotokutasababishawashambuliwenamaradhi, kituambachokinahatarishauhaiwaMtoto.

AmesemachanjonimkakatimuhimunamuafakakatikakutokomezamaradhinakupunguzavifovyawatotolakinipiakupunguzagharamakubwaambazoFamilianataifakwaujumlalingetumiakatikakutibumaradhiyatokanayonamagonjwayanayozuilikakwachanjo.
Wataalamyaafyawamethibitishakuwa, chanjohuzuiatakribanivifomilionimbilihaditatukilamwakakutokananamaradhiyanayokigwakwachanjoikiwanipamaojanaNdui, Polio, KifaduronaPepopunda,ujumbewachanjomwakahuuunasemaJamiiiliyochanjwanijamiiyenyeafyahukukaulimbiuikisemaChanjonizawadiyaMaisha.

KAMANDA WA MAFUNZO WA CHADEMA AKAMATWA NA VIFAA VYA KIJESHI TUNDUMA MBEYA


SIKU chache baada ya Jeshi la polisi kupitia IGP Ernest Mangu kupiga marufuku vikundi vya ulinzi vilivyoanzishwa na vyama vya siasa hapa nchini, Kiongozi wa mafunzo wa kikundi cha Red Briged (CHADEMA) wilaya ya Momba (TUNDUMA), mkoani Mbeya, Methius Mwafongo, @ RASTA, amekamatwa akiwa na vifaa vya Jeshi la ulinzi wa Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Taarifa zilisema kuwa, kiongozi huyo wa Red briged, alikamatwa na vyombo vya dola baada ya kuwepo taarifa za kwenda kutoa mafunzo kwa wafuasi wa chama hicho cha siasa.
Mbali na vifaa vya kijeshi ambavyo alikamatwa navyo zikiwemo sare za Jeshi hilo, pia alikutwa na mapanga, Manati na mawe yake.
Wakati tunaenda mitamboni, kuna taarifa kuwa, Katibu wa Itikadi na uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Mbeya, Bashiru Madodi, amekutana na waandishi wa habari mchana wa leo na kuzungumzia tukio hilo na kuitaka serikali kufanya uchunguzi wa kina zaidi.

Katibu wa Siasa na uenezi wa CCM Mkoa wa Mbeya, Bashiru Madodi akisoma Tamko hilo.


Alipotafutwa kwa njia ya simu, Madodi amekiri kukutana na waandishi wa habari na kwamba amethibitisha taarifa za kuwepo kwa tukio hilo ambalo linahusisha mafunzo ya vijana 600 kila wilaya ya mkoa wa Mbeya kwa nia ovu.
“Chadema mara kadhaa wamenukuliwa kuwa nchi hii haitakalika, haya bila shaka ndiyo mafunzo wanayoyaandaa hivyo naitaka serikali kupitia vyom,bo vyake vya ulinzi na usalama vifanye uchunguzi wa kina kila mkoa na kuwachukulia hatua stahiki za kisheria kwa yeyote anayetaka kuharibu nchi” alisema Madodi.
Aidha alieleza kuwa kuna taarifa chama chake kimezipata pia kuwa, mafunzo hayo ya vijana wa Chadema, yanalenga kuwatisha wapiga kura kila Jimbo ili wasiweze kujitokeza kujiandikisha na kupigia kura kura ya maoni katiba inayopendekezwa vinavyotarajiwa kufanyika hivi karibuni.
Baadhi ya viongozi wa Chadema ambao hawakutaka majina yao kuandikwa, wamekiri kuwepo kwa mafunzo mbalimbali na kukamatwa kiongozi huyo na kwamba viongozi wa ngazi za juu wanafanya mpango wa kuwasiliana na vyombo vya dola ili kufahamu tatizo kubwa la Mwafongo.
Mpaka sasa, kiongozi huyo wa mafunzo wa Chadema (RASTA), anahojiwa na vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Mbeya.
Mtandao huu unaendelea kufauatilia na kesho utazungumza na ofisi ya kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya kwa ajili ya kufahamu taratibu za kumfikisha mahakamani ama ataachiwa mikononi mwa Polisi. (na kalulunga blog)

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI WATANZANIA WALIOKUWA AFRIKA KUSINI WAMEREJEA NYUMBANI

 


Kundi la Watanzania 26 limerejea nyumbani kutokaAfrika Kusini  leo tarehe 26 Aprili, 2015 kufuatiamashambulizi ya wazawa dhidi ya wageni.  Kundi hilola kwanza kurejea nyumbani liliwasili katika Uwanjawa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyereresaa 11 alfajiri na Ndege ya Fast Jet.  

 

Watanzania hao walikuwa wanaishi katika kambi zadharura za Isipingo na Phoenix zilizopo jijini Durban.Walisindikizwa kurudi nyumbani na  Afisa wa Ubaloziwa Tanzania nchini Afrika KusiniBwElibahatiLowassaZoezi la kuwarejesha wananchi haolilisimamiwa na kuratibiwa na Ubalozi wa Tanzanianchini Afrika Kusini.  

 

Wakati huo huoUbalozi wa Tanzania nchini AfrikaKusini umepata taarifa kuwa kuna Watanzania wenginewapatao 20 wanaishi kwenye Kambi ya Hillbroughjijini Johannesburg. Ubalozi umetuma Afisa kwendakatika kambi hiyo ili kufanya uhakiki wa taarifa hizokwa madhumuni ya kuwarejesha nyumbani Tanzaniaharaka iwezekanavyo.

MWISHO.

 

Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma,

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano waKimataifa,

25 Aprili 2015

 

April 24, 2015

WANANCHI LUILO WAMCHOKA DIWANI WAO MPINGA MAENDELEO ,WAMWOMBA MBUNGE AMCHARAZE BAKORA


mbunge  wa Ludewa Deo Filikunjombe akipongezwa na masisita  wa parokia ya Luilo kwa kuwapigania  kupata  umemembunge Filikunjombe kushoto na diwani  wa  Ludewa  mjini Monica Mchilo wakishirikiaana kushusha saruji mifuko 50 na bati 50 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa shule ya songambele
mbunge Filikunjombe kushoto na diwani  wa  Ludewa  mjini Monica Mchilo wakishirikiaana kushusha saruji mifuko 50 na bati 50 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa shule ya songambele
mbunge Filikunjombe  akizungumza na wananchi wa kitongoji cha Ngalawale


mbunge Filikunjombe akishuka katika trekita baada ya kusaidia kushusha saruji na bati
mwenyekiti  wa kijiji  cha kipangala akimchongea diwani  huyo kwa  mbunge  juu ya kuzuia kushiriki mqaendeleo
wananchi Luilo wakimpinga  diwani  wao mbele ya  mbunge

mbnge Filikunjombe akiwahutubia wananchi wa Luilo

mkazi  wa Ngalewale
mmoja  kati ya  wazee  wa  mtaa  wa Ngalewala   kushoto akimpongeza  mbunge Filikunjombe kulia huku  akimtaka achukue fomu wao wanampenda aendelee  kuwa mbunge wao
Diwani  Matei Kongo

    Na matukiodaimablog

WANANCHI wa  kijiji  cha Luilo kata ya Luilo  wilaya ya  Ludewa  mkoani  Njombe  wamemkataa mbele  ya  mbunge  Deo  Filikunjobe ,diwani  wao  wa kata ya  Luilo  Matei kongo (CCM) ambae ni mwenyekiti  wa Halmashauri ya  Ludewa  na kutaka acharazwa  bakora hadharani kutokana na kuwa  mpinzani  wa maendeleo katika kata ya Luilo.

Wananchi hao  walimlalamikia  diwani   huyo  katika  mikutano  ya hadhara wa mbunge Filikunjombe  aliyoifanya  kwenye  vijiji vya Lifua na Luilo kwa  lengo la   kuhamasisha wananchi kushirikiana na  mkandarasi  wa mradi  wa umeme  kati
ka  shughuli za  kuchimba mashimo .
 

Wakizungumza katika  mkutano  huo wananchi hao walisema  kuwa  wanashangazwa na  hartua ya   diwani  wao mbali ya  kuwa ni diwani  wa CCM  ila  ameendelea  kuwa mpinzani  mkubwa wa maendeleo  katika  kata  yake  kwa   kupinga kila shughuli ya maendeleo inayofanywa mbunge  katika kata  yake.


mkazi  wa kijiji  cha  Luilo  Osward  Haule alisema  wakati  serikali ya  CCM ikihimiza wananchi kushiriki  katika  shughuli za kmaendeleo kwa  kujitolea  nguvu  zao  diwani   huyo amekuwa akienda  kinyume  kwa  kuzuia  wananchi kushiriki katika shughuli za  kimaendeleo na  kuwa katika kata   hiyo kuna ujenzi  wa  zahanati unaoendelea kwa  zaidi ya  miaka minne sasa  bila  kukamilika kutokana na ubinafsi  wa  diwani  huyo.

' mbunge wetu umekuwa  ukifanya kazi kubwa  sana  ya  kutuletea maendeleo katika jimbo la Ludewa na  hatujapata    kuwa na mbunge anayejituma  kuleta  maendeleo kama  wewe  toka  nchi  hii  ipate  uhuru  ila kikwazo kikubwa kipo hapa  mbele kwenu  viongozi  kwani diwan wetu kweli  tunashindwa  kumuelewa na mpinzani ama  ni diwani  wa ccm kila jema   linalofanywa na  mbunge yeye kazi  yake ni  kupinga ......sasa inapendezwa  sana wapinga maendeleo wakati  mwingine kuonywa kwa viboko'

Alisema   kuwa sababu  kubwa ya kata   hiyo kukwama  baadhi ya miradi  ya  kimaendeleo ni  kutokana na  diwani wao kuwa kibinafsi  zaidi na  kuonyesha   wazi  wazi upinzani wa kazi zinazofanmywa na mbunge  hivyo kwa  upande  wao wanamtaka diwani   huyo  kukaa pembeni  ili  wao wateue diwani  wao  wa  muda atakayeshirikiana na  mbunge kuwaletea maendeleo kwa  muda  uliobaki na baada ya hapo  muda  wa  uchaguzi ukifika  wamchague diwani  wa  wananchi nje ya diwani  huyo.

kwani  alisema  wao  kama  wananchi  wapo tayari  kwenda  kushiriki  maendeleo  ila  shida  ipo  kwa  diwani ambae  amekuwa  akiwazuia kushiriki shughuli za kimaendeleo hasa  katika  miradi  inayoanzishwa na  mbunge .

Hata  hivyo  alisema kwenye  kijiji   hicho  kuna mradi wa  ujenzi  wa  zahanati  ambao umeendelea kukwama kwa zaidi ya  miaka  minne  sasa  huku kazi kubwa ya diwani  wao ni kujitolea gari la kusafirisha maiti kutoka Halmashauri  pindi  wananchi  wa kata hiyo  wanapopatwa na msiba  badla ya kusimamia ujenzi  wzahanati hiyo ili  kupunguza vifo.

mwenyekiti  wa kijiji  cha kipangala Jeremia kayombo alimweleza  mbunge  huyo  katika mkutano  kuwa  diwani  huyo  alimpigia  simu siku moja  baada ya mbunge kupita  kuhamasisha  wananchi kushiriki shughuli za uchimbaji mashimo ya  nguzo za  umeme akimtaka  azuie wananchi wasishiriki maendeleo japo viongozi na wananchi  walimpuuza.

'mimi kama  mwenyekiti  wa kipangala ninae  tokana na ccm sipotayari  kusema uongo hapa  nitasema kweli tupu kama chama  chetu  ccm kinavyotaka huyo  diwani ni mpinzani mkubwa wa maendeleo alinipigia simu kutaka nizuie  wananchi kushiriki katika maendeleo'

Alisema  hata  sababu ya  kutoshiriki  katika  mikutano  hiyo ya  mbunge kwa  diwani  huyo ni  kutokana na kukwepa hasira  za  wananchi dhidi  yake  japo mara kwa mara mbunge anapofanya ziara katika kata yake  huwa anatoa sababu mbali mbali za  kutoshiriki .

Akiwahutubia  wananchi hao mbunge  Filikunjombe mbali ya  kuwapongeza  kwa  hatua  waliyoichukua ya kumpuuza diwani  huyo bado  alisema kwa  upande  wake kama mbunge hatapenda kuona  wananchi wakikosa maendeleo kutokana na vikwazo  vya  kiongozi mmoja na  kuwa kwa nguvu  zake na ushirikiano  wa wananchi wa kata   hiyo lazima umeme  ufike.

Filikunjombe  alisema yupo tayari kugombana na  mtu  mmoja anayekwamisha  maendeleo  na mara baada ya umeme  kuwaka  atapatana  ila  si vinginevyo  kwani  wanaopata  shida ni wananchi na sio viongozi .
Alisema  kuwa ni  kweli serikali  imetoa pesa  kwa mkandarasi  kwa  ajili ya  umeme ila kwa kasi ya mkandarasi  uwezekano  wa  umeme   huo  kukamilika mwaka   huu ni  ndoto kutokana na kasi  ndogo na mkandarasi  aliyepewa kazi hiyo ni  mmoja kwa  mkoa mzima  wa Njombe hivyo kwa  upande wake kwa  kutumia mbinu  zake amefanikiwa  kupata nguvu na  kutaka umeme   huo kuwaka baada ya  miezi miwili kwa vijiji vyote  zaidi ya 12 vya jimbo la Ludewa .

Mbunge  huyo  alisema  kuwa baadhi ya maeneo umeme  umekuwa  ukichelewa  kufika kutokana na wananchi kuleta  vikwazo vya  kudai fidia ya miti na mazao  ila kwa  wilaya ya  Ludewa amefanikiwa  kuwaomba  wananchi  wasidai fidia ya miti na  wao  wenyewe  kushiriki kuchimba mashimo na  wamekubali  katika kata zote na madiwani  wanashiriki vizuri katika maendeleo  ila shida ni kwa diwani  huyo wa Luilo .

kuwa gharama  ya  uchimbaji shimo moja ni Tsh 5000 na  kuwa jumla  ya mashimo kama 15   hivyo ni kiasi  cha sh 75,000 ambazo kama  kulipwa  wananchi hao  wangelipwa na ukigawa kwa  kila mwananchi  ni kama sh 150 na kama kazi   hiyo ya uchimbaji ingefanywa na mkandarasi kwa mafundi wake ingechukua muda  mrefu zaidi hivyo ndio  sababu ya kuwaomba wananchi kujitolea  nguvu zao.

Pia  alisema kwa  upande wake kwa ajili ya kuwaunga  mkono atawasaidia kukamilisha zahanati  hiyo ili  kuepukana na shida  ya zahanati

 Akizungumza kwa  njia ya simu  kuhusiana na malalamiko ya wananchi  wake diwani Kongo alikiri kuwazuia  wananchi  kushiriki katika maendeleo ya mradi  huo  wa umeme huku akidai kuwa  yeye ni mwenyekiti wa halmashauri ya  Ludewa .

Kongo  alisema  kwa  kuwa mkandarasi kapatikana hata kama wananchi  watapata  umeme kwa kuchelewa  ni sawa tu .

mkandarasi  wa  mradi  huo wa  umeme Bw Aron  Makulu alisema alisema  kuwa kampuni  yake uwezo haina  uwezo  wa  kuwalipa wananchi pesa ila fedha  zilizopo za  kulipa wafanyakazi pekee.


katibu mwenezi  wa ccm mkoa  wa Njombe Honoratus Mgaya  alisema  kuwa chama  cha mapinduzi ni chama  kizuri  sana  kinachowajali  wananchi wake  ila shida ni baadhi ya viongozi ndio  wanaokichafua chama na kuwafanya  wananchi  wakione  chama kibaya na  kuwa kama chama hakitakubali kuchukiwa na  wananchi kwa ajili ya mtu  mmoja na  kuwataka  wananchi  hao kuwapuuza viongozi wasiopenda maendeleo.