Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

February 28, 2015

Breaking news mbunge Kepten John Komba afariki Ghafla


Mbunge wa jimbo la Nyasa  mkoani Ruvuma Kepten John Damian Komba amefariki dunia katika hospitali ya TMJ jijini Dar es salaam leo .

Komba pia alikuwa ni mjumbe wa halmashauri kuu ya Ccm Taifa .

Komba inadaiwa amefariki Baada ya kupandwa na sukari Baada ya Kifo cha Rodha George .
Huu ni msiba wa pili mkubwa kwa wilaya ya Nyasa Mkoa wa Ruvuma Baada ya Jana aliyekuwa katibu wa wilaya ya Nyasa ambae inadaiwa alikuwa shabiki na msaada mkubwa kwa mbunge Kombea Rhoda George kufariki dunia katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa 

Taarifa zaidi zitaendelea kujia hapa 

Magazeti leo jumamosi
February 27, 2015

SERIKALI KUFUFUA BANDARI 14 ZA ZIWA NYASA – WAZIRI MKUU

WAZIRI MKUU Mizengo amesema Serikali imeamua kufufua bandari ndogo 14
kwenye mikoa mitatu inayozunguka Ziwa Nyasa ili kuimarisha usafiri wa
majini kwa wakazi wa Ruvuma, Njombe na Mbeya.

“Tangu mwaka 2006 bandari za kwenye mikoa ya Ruvuma, Njombe na Mbeya
zilikufa na hivyo kuleta shida ya usafiri kwa wakazi wa maeneo hayo
lakini Serikali imeamua kuzifufua bandari hizo na Itungi itakuwa ndiyo
kituo kikuu cha bandari zote katika Ziwa Nyasa,” alisema Waziri Mkuu.

Alikuwa akizungumza na wakazi wa Wilaya ya Kyela kwenye mkutano wa
hadhara uliofanyika jana jioni (Jumatano, Februari 26, 2015) kwenye
uwanja wa michezo wa Mwakangale na kuhudhuriwa na maelfu ya wakazi wa
wilaya hiyo.

Alizitaja bandari hizo kuwa ni Ndumbi, Lundu, Njambe, Mkili, Liuli, na
Mbamba bay ambazo ziko mkoani Ruvuma. Nyingine ni Lumbila, Ifungu,
Nsisi, Lupingu na Manda ambazo ziko Njombe wakati bandari za Mbeya ni
Itungi, Kiwira na Matema.

Alisema ili kufanikisha hilo, Serikali imehamisha chelezo (Dry Dock)
kutoka bandari ya Mwanza na kwamba mkandarasi kutoka Kampuni ya
Songoro Marines, ameshaanza  ujenzi wa chelezo hiyo.

“Baada ya kukamilika, Chelezo hiyo, itatumika kutengenezea meli mpya
yenye uwezo wa kubeba abiria 200 na tani 200 za mizigo na kufanya
ukarabati wa meli pindi zinapohitaji matengenezo. Nimeambiwa na
mkandarasi kutaka watamaliza hii kazi ifikapo Juni, mwaka huu,”
alisema huku akishangiliwa na umati huo.

Waziri Mkuu alisema, mbali ya hilo, chelezo hiyo pia itatumika
kutengeneza matishari mawili ya kubebea mizigo ambayo yatakuwa na
uwezo wa kubeba mizigo tani 1,000  kila moja.

“Yatatumika kusafirisha mizigo hiyo hususan mazao ya wakulima kupitia
bandari ndogo zilizopo lakini pia yatasafirisha tani 60,000 za makaa
ya mawe, tani 72,000 za saruji kutoka Mbeya kwenda Malawi na mikoa
jirani; tani 10,000 za mbolea kutoka Dar es Salaam pamoja na chuma
kutoka Liganga na Mchuchuma,” alisema.

“Chelezo hiki kitakapokamilika kitakuwa kikubwa na cha aina yake…
hakuna kingine cha kulinganishwa nacho katika nchi jirani za Malawi,
Zambia na Msumbiji. Itumieni fursa hii kwa kutunza ule mto kwenye
mdomo wa kuingilia bandari ya Itungi, msilime kwenye kingo za mto,”
aliongeza.

Mapema, akizungumza na wakazi wa kata ya Lusungo mara baada ya kuweka
jiwe la msingi la ujenzi wa daraja la Lusungo, Waziri Mkuu Pinda
alisema daraja hilo ni kiungo muhimu kwenye barabara hiyo iendayo
kwenye bandari ya Matema.

Aliwataka wakazi wa kata hiyo walitunze daraja hilo ili liweze
kuwasaidia kusafirisha bidhaa na mazao wanayolima. Ujenzi wa daraja
hilo, ambalo limejengwa kupitia mfuko wa barabara, lina urefu wa mita
50 na upana wa mita 7.3 pamoja barabara yenye urefu wa mita 600 kutoka
kwenye maingilio ya daraja hilo, limegharimu kiasi cha sh. bilioni 3.7
huku ujenzi wake ukiwa umekamilika kwa asilimia 99.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu Pinda alipewa jina la MWAKABULUFU
na Chifu Ernest Mwailemale wakati akisimikwa kuwa kiongozi wa eneo
hilo la Lusungo. Waziri Mkuu alivishwa mgolole na kupewa mkuki ili
autumie kuilinda nchi dhidi ya maadui kutoka pande zote.

Akizungumza mara baada ya kumsimika Waziri Mkuu, Chifu Mwailemale
mwenye umri wa miaka 91, alisema jina hilo ni la babu yake mzaa baba
ambaye aliwahi kutawala eneo hilo. Hata hivyo, hakutaja ni mwaka gani.

Alipoulizwa maana ya jina hilo, Chifu Mwailemale ambaye wakati wote
alikuwa akizungumza Kiswahili kwa ufasaha alisema: “Jina hili halina
maana maalum bali na heshima kwa sababu lilikuwa la Chifu aliyetawala
eneo hili,” alisema na kufafanua kuhusu umri wake: “Nina miaka 91 kwa
maana nilizaliwa tarehe 25 Septemba mwaka 1924,” alisema Chifu huyo
ambaye anaelezwa kupigana Vita Kuu ya Pili ya Dunia.

February 26, 2015

AJITOLEA KUUZA BIKIRA YAKE MACHI 8


Mwanamume mmoja amejitolea kutoa ubikira wake wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya wanawake.


Sorin Gorgian Salinievcici mwenye umri wa miaka 24 amejitolea kuuza ubikira wake kwa pauni 1,476 baada ya kusoma kuhusu wanawake wanaofanya hivyo.
Alielezea kuwa :''mimi husoma kuhusu wasichana wanaofanya hivyo na nikafikiri kwamba iwapo wanafanya hivyo hata mimi naweza kufanya''.


Amesema kuwa mwanamke yeyote atakayenunua ubikira wake ni sharti awe mwenye heshima.
''Sisemi kuwa ni lazima awe mrembo lakini awe mwanamke wa kawaida, mzuri na mwaminifu''.alisema.
Katika bango aliloandika nyumbani kwake huko Romania,alisema kuwa inaweza kuwa zawadi nzuri katika maadhimisho ya siku hiyo ya wanawake mnamo mwezi machi tarehe 8.
Je,unadhani kitendo hiki kinakubalika?

Washindi wa Promesheni ya Airtel yatosha Zaidi wakabithiwa magari

Afisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde (katikati), akifafanua jambo kwa mmoja wa washindi wa droo ya tatu ya promosheni ya ‘Airtel Yatosha Zaidi’, Jastini William Dodoo (kulia), baada ya kumkabidhi gari lake jipya aina ya Toyota IST lililosajiliwa kwa namba T 465 DDD, katika hafla iliyofanyika katika Makao Makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam jana.

Meneja Biashara wa Airtel Kanda ya Dar es Salaam, Fredrick Mwakitwange (kulia), akikabidhi funguo za gari jipya aina ya Toyota IST lililosajiliwa kwa namba T 782 DCZ, kwa mmoja wa washindi wa droo ya tatu ya promosheni ya ‘Airtel Yatosha Zaidi’, Donald Fred Baruti katika hafla iliyofanyika nyumbani kwa mshindi huyo, Mtaa wa Ngala, eneo la Magomeni Mwembechai jijini Dar es Salaam jana. Anayeshuhudia (katikati) ni Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando.
Mmoja wa washindi wa droo ya tatu ya promosheni ya ‘Airtel Yatosha Zaidi’, Donald Fred Baruti akilijaribu gari lake jipya aina ya Toyota IST lililosajiliwa kwa namba T 782 DCZ, baada ya kukabidhiwa na Airtel, katika hafla iliyofanyika nyumbani kwake, Mtaa wa Ngala, eneo la Magomeni Mwembechai jijini Dar es Salaam jana.
Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando (kushoto), akikabidhi kadi ya umiliki wa gari jipya aina ya Toyota IST lililosajiliwa kwa namba T 782 DCZ, kwa mmoja wa washindi wa droo ya tatu ya promosheni ya ‘Airtel Yatosha Zaidi’, Donald Fred Baruti katika hafla iliyofanyika, Mtaa wa Ngala, eneo la Magomeni Mwembechai jijini Dar es Salaam jana. Anayeshuhudia (wa pili kushoto) ni Meneja Biashara wa Airtel Kanda ya Dar es Salaam, Fredrick Mwakitwange.
Mmoja wa washindi wa droo ya tatu ya promosheni ya ‘Airtel Yatosha Zaidi’, Donald Fred Baruti akiteremka kutoka kwenye gari lake jipya aina ya Toyota IST lililosajiliwa kwa namba T 782 DCZ, baada ya kukabidhiwa na Airtel, katika hafla iliyofanyika nyumbani kwake, Mtaa wa Ngala, eneo la Magomeni Mwembechai jijini Dar es Salaam
Meneja Masoko wa Airtel, Upendo Nkini (katikati) akikabidhi funguo za gari jipya aina ya Toyota IST lililosajiliwa kwa namba T 465 DDD, kwa mmoja wa washindi wa droo ya tatu ya promosheni ya ‘Airtel Yatosha Zaidi’, ambaye ni Kondakta wa Malori, Jastini William Dodoo katika hafla iliyofanyika katika Makao Makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Afisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde.
Meneja Biashara wa Airtel Kanda ya Dar es Salaam, Fredrick Mwakitwange (kushoto), akikabidhi funguo za gari jipya aina ya Toyota IST lililosajiliwa kwa namba T 464 DDD, kwa mmoja wa washindi wa droo ya tatu ya promosheni ya ‘Airtel Yatosha Zaidi’, ambaye ni Wakala wa Mtandao huo, John Fred Kiwale katika hafla iliyofanyika, Mtaa wa Togo, eneo la Kinondoni jijini Dar es Salaam jana. Wa (pili kushoto) ni Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando na (kulia) ni Mke wa mshindi huyo, Anna Kiwale na motto wake, Sylvia John.