Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

January 31, 2015

BREAKING NEWSSss AJALI YAUA WATATU IRINGA USIKU HUU NI BAADA YA KUGONGANA NA LORI NA BODA BODA

Lori  aina  ya  fuso  likiwa  limeharibika  kupita  kiasi baada ya  kugongana na boda  boda  eneo la  Kihesa  Kilolo mjini Iringa usiku  huu na kusababisha   vifo vya  watu  watatu  waliokuwa  wamepakizana katika  boda  boda  hiyo
Hizi ndivyo  lori  hilo  lilivyoharibika
Wananchi  wakishuhudia  ajali  hiyo  ya  Lori na boda  boda  leo usiku
Hii  ndio  pikipiki  iliyoteketea  kwa moto baada ya ajali
Hili  ndilo  eneo ambalo miili ya  vijana  hao  watatu  iliteketea kwa moto baada ya ajali
WATU   watatu   waliokuwa  wamepakizana mishikaki  wamekufa  kwa  kuteketea kwa moto  mjini  Iringa  usiku  huu  baada ya  usafiri aina ya  pikipiki (Boda  boda)waliyokuwa  wakisafiri  kutoka mjini Iringa  kuelekea Nduli nje  kidogo na  mji  wa Iringa  kugongana na lori aina ya  fusu  na  kupelekea  pikipiki  hiyo  kuwaka  moto.

Ajali   hiyo  imetokea  majira ya saa  2 usiku  huu  wakati boda  boda hiyo  ikiwa katika mwendo mkali  kugongana na lori  hilo ambalo  pia  lilikuwa katika mwendo na  kusababisha   vifo  hivyo .

Mashuhuda  wa  tukio  hilo  waliozungumza na  mtandao  huu  wa  www.matukiodaima.co.tz  wamesema  kuwa  kijana  mmoja  ambae  inasadikika  ndie  dereva  wa boda  boda  hiyo ametambuliwa kwa jina moja la  Julius huku  wengine  wawili  bado  kutambuliwa .

Kutokana na  ajali  hiyo mbali lori  hilo upande wa mbele  ngao yake  ilipinda   huku  eneo  hilo la mbele  likiharibika   vibaya  mfano wa  kugongana  gari kwa gari na  baada ya  hapo  pikipiki  hiyo  ilishika  moto  na kuteketea   yote  pamoja na watu hao  ambao  miili yao  ilizimwa kwa  mchanga  na  wasamaria wema.
Miili  ya  marehemu hayo  imehifadhiwa katika  chumba  cha maiti  cha  Hospitali  ya  Rufaa ya  mkoa  wa Iringa  kwa  utambuzi  zaidi

January 29, 2015

Sakata la anayedaiwa kuteswa Afrika ya kusini na wauza unga

HABARI ZA UHAKIKA JUU YA SAKATA LA JUMAANNE TEVEZ. Nikweli kwamba huyu bwana yuko South Africa Pretoria. Bwana Tevez alodhaminiwa mzigo na vijana wenzake huko Bondeni kwamba akauze kisha alete Mpunga.

Mdhamini alikuwa ni Kijana wa Kibongo anayeonekana pichani anayeitwa Jeff Katili mtoto wa Ilala ambaye maskani yake ni South.  TEVEZ baada ya kuchukua mzigo uliokuwa na thamani ya takriban milioni mia moja na hamsini (150,000,000/=) aliingia mitini hakurudi tena. Kilichotokea Jeff baada ya kubanwa na wana akawaambia kuwa tulieni nitamleta tu. Basi Jeff akamrubuni Tevez kuwa njoo Kuna kazi..

Tevez akaingia mzima mzima akaenda hadi Pretoria wiki iliyopita na kufikia kwa Jeff Katili na kupata mapokezi mazuri kama kawaida. Baada ya kufika walitoka kwenda matembezi KWAZULU NATAL... wakiwa huko walifikia kwa washkaji zao wa kibongo lakini kwenye nyumba ambayo ilikuwa kama holi haina chochote ndani. Chini lilitandikwa karatasi la nailoni ili kuepusha damu isitapakae.


Alibaini juu ya mzigo na mtesaji mkubwa alikuwa Jeff Katili mwenyewe ambaye ni mdhamini. Tevez hajang'olewa jicho bali alipigwa Ngumi hadi jicho likaenda ndani... NGUMI YA MTOTO WA KIUME.


Ameteswa sana na amekatwakatwa na viwembe mwili mzima. Zakari yake haijakatwa kama picha zilivyoonyesha bali imekatwa na viwembe. Taarifa zilitumwa kwa kaka yake na akina Jeff na kuwataka watume pesa la sivyo wanamuua.


 familia kupitia kaka yake imeshatuma pesa nusu na sas anatibiwa hukohuko South na atarejea punde. Uzushi kuwa amekufa hauna ukweli na hizi ni habari kamili kutoka kwa watu wa karibu na familia hiyo.