Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

December 31, 2015

MKUU WA MKOA WA IRINGA AWAONGOZA WANANCHI IRINGA KATIKA IBADA YA MAKANISA YA KUAGA MWAKA 2015 KUKARIBISHA MWAKA 2016

Msaidizi wa Askofu wa KKKT Dayosisi ya Iringa Blaston Gavile akitoa salama za mwaka Mpya kanisani 
Waumini wa kanisa la Kilutheri Usharika wa Iringa Mjini wakiwa katika mkesha 
Viongozi wa Dini ya kikristo na serikali wakiwa ukumbi wa Highlands kuaga mwaka 
Askofu Dr Mdegela akiwa na mkuu wa mkoa wa Iringa 
HOTUBA YA MKUU WA MKOA WA IRINGA MHE. AMINA JUMA MASENZAKWENYE MKESHA MKUBWA KITAIFA – (DUA MAALUMU KWA TAIFA,IRINGA TAREHE 31/12/2015)

Mhe. Mkuu wa Wilaya,

Katibu Tawala wa (M),

Mstahiki Meya wa Manispaa yaIringa,

Wahe. Wabunge,

Kamati ya Ulinzi na Usalama (M),

Viongozi WA CCM, viongozi WAvyama vya siasa,

NduguMkurugenzi wa Manispaa,

NduguViongozi wa Dini na Siasa,

NduguWaandishi wa Habari,

Waandaaji,

NduguWaumini,

Asalamu Alkumu,

Bwana Yesu asifiwe,

 

 

Awali ya yote napenda kumshurukuMungu aliyetuwezesha afya njema nahatimae leo hiitumekutana hapa kwenyeMkesha huu mkubwa Kitaifa wa Dua –Maalum kuliombea Taifa letu.

 

Aidhanapenda kumshukuru Mungu kwakuwapa nguvu  na uwezo mkubwawaandaaji wa siku hii ya leo ambayokwetu sisi waumini wa madhehebumbalimbali na wananchi kwa ujumla inafaida kubwa sana kwetu na kwa Taifaletu.

Pia nawashukuru wote kwa ujumla wenukwa kuja kushiriki kwenye Mkesha huu,sote pamoja tunaliombea Taifa letu,tunamshukuru Mungu kwa kutuwezeshakuona Mwaka Mpya 2016tunamtukuzana kumuomba Mungu alizidishie kheri naBaraka Taifa letuAidha, atuzidishieupendo sisi Watanzania, ili amani ya kweliipate kutawala kuanzia ngazi ya familiazetu hadi Taifa.

 

Nawashukuru waumini na na wakazi wotewa Mkoa wa Iringa, IdaraTaasisi namashirika mbalimbali kwa kufanikishajambo hili.

 

Ndugu waumini,

Itakumbukwa kwamba Mwezi Oktoba2015 nchi yetu ilifanya Uchaguzi Mkuuambapo Mwenyezi Mungu alitujaliatukamchagua Rais wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli pamoja naWabunge na madiwaniTunamshukurusana Mwenyezi Mungu kwa kutupakiongozi shupavumzalendona mwenyemapenzi ya  dhati kwa nchi yetu.  Sote nimashahidi kwani katika kipindi kifupiMheshimiwa Rais amefanya kazi kubwasanaSote tumwombee kwa MwenyeziMungu azidi kumtia nguvu katikamajukumu yake ya kila siku ili nchi yetuipate maendeleoNinaamini MwenyeziMungu atamlinda na kuzidi kumuimarishakama maandiko yanavyo sema:-

ISAYA 41:10 USIOGOPE KWA MAANA MIMI NI PAMOJA NAWE, USIFADHAIKE KWA MAANA MIMI NI MUNGU WAKO, NITAKUTIA NGUVU NAAM, NITAKUSAIDIA NAAM, NITAKUSHIKA KWA MKONO WA KUUME WA HAKI YANGU.

ISAYA 41:13-15 KWA MAANA MIMI BWANA MUNGU WAKO, NITAKUSHIKA MKONO WAKO WA KUUME NIKIKUAMBIA USIOGOPE, MIMI NITAKUSAIDIA, NITAKUFANYA KUWA CHOMBO KIKALI KIPYA CHENYE MENO.

ZABURI 9:4-6 KWA MAANA UMENIFANYIA HUKUMU NA HAKI, UMEKETI KITINI PA ENZI UKIHUKUMU KWA HAKI, UMEWAKEMEA MATAIFA NA KUMWANGAMIZA MDHALIMU.

Wananchi wote tumuunge mkono Raiswetu katika jitihada anazozifanya.

 

Ndugu waumini, mabibi na mabwana;

Mkoa wetu na Nchi yetu kwa ujumlaumekuwa na upendoamani, utulivu namshikamano wa kitaifa kwa sababu yawatu wa Mungu ambao mmekuwamkiomba na ndiyo maana tumekusanyikaleo ili kushukuru na kuliombea Taifa letu.Maombi ni msingi mkubwa kwa Taifa letuna ni ukweli kuwa Mungu atatupa upendowa kweliamani, utulivu na mshikamano,mambo ambayo ndiyo msingi mkubwa wamaendeleo ya nchi yetu.

Ili tuweze kuwa na amani ya kweli,yatupasa kutii na kufuata amri za Mungu,maadili na mafundisho mbalimbali yamaandiko matakatifu na sheria za nchi ilikudumisha upendo katika nchi yetu nahatimaye kudumisha amani.

 

 

 

 

Ndugu wauminimabibi na mabwana;

Katika Jamii yetu, tumeshuhudiammonyoko wa maadilitumeona ugomvi,ulevindoa kuvunjika kukosa hekima,dharaukuto lea watoto – hili ni tatizo. Ilitufanikiwe lazima tujenge Jamiiinayofuata mafundisho ya munguKwakufuata mafundisho ya Munguwazazi nawatoto wao wataheshimianamaadilimema kuanzia ngazi ya familia hadi taifayatatawala na kuimarika kwa amani naupendo miongoni mwetu bila kujali Dini,Itikadi, Kabila, Jinsiana uwezo wakifedha.

 

Ndugu wauminimabibi na mabwana;

Nitumie fursa hii kutoa wito kwa wauminina wananchi wote kwambatunapokaribisha mwaka mpya 2016kilammoja wetu atafakari ni mambo gani auchangamoto zipi zilizojitokeza katika jamiina kusababisha uvunjifu wa amani,vurugu na kutoelewana.

Kutokana na matendo hayo kila mmojawetu awe mwalimu na taa inayomulika nakuongoza, katika kutenda mema ilikumpendeza Mungu.

Waheshimiwa viongozi wa dini zote nimuhimu sana tuhimize waumini wetukutii sheria za nchi na kufuata taratibu nakanuni za nchiUvunjifu mwingi waamani hutokea pale watu wanapoachakuzingatia sheria za nchiUtii wa sheria nikinga ya amani yetuAidhanawaombaviongozi wa Dini nikiwaita mniitike  kwavile  nia yangu ni kuwa na uongozi wapamoja na kupashana habari,kubadilishana mawazo na kuona vipi nivipaumbele ili tuvisimamie kwa pamoja.  Kama kuna kikwazo chochote karibuniOfisini ili munifahamishe.

 

Ndugu wauminimabibi na mabwana;

Kabla ya kumaliza hotuba yangu natoawito kwa waumini wote kuwaombeaviongozi wote ili wawe na hekima, busarana ujasiri wa kuwatumikia Watanzaniakwa moyo, upendo na uadilifu mkubwa.Lengo liwe kutenda haki kudumishauzalendo na uwajibikaji kwa faida ya Taifaletu.

Aidhakila mmoja wetu kwa nafasi yakekatika jamii awajibike kuleta maendeleoyake binafsi kwa kufanya kazi kwa bidii.

 

Naomba yafuatayo yazingatiwe:-

1.
Watoto wote waliofaulu darasa lasaba wapelekwe kuanza kidato cha kwanza na hapatakuwa na ada namichango.
2.
Watoto waliofikisha umri wa kuaanzadarasa la kwanza wakaandikishwe nahakuna michango.
3.
Kwa wananchi wanaoishi katikamaeneo yanayopata mvua kidogo nilazima wapande mazao ambayoyanahimili ukame hususani zao lamtama.
4.
Muhimu kuchukua tahadhari kwawote wanaolima mabondenikuwa natahadhari ya wingi wa mvuainayotabiriwa isije ikasomba mazaoyenu mtakayopanda. Mamlaka ya haliya hewa imetahadharisha kwambamwaka huu kutakuwa na mvua nyingihivyo tuchukue tahadhari mapemahasa wanaoishi mabondeni.
5.
Swala la UKIMWI, madawa ya kulevyani tatizo ndani ya jamiini vematuliwekee mkakati wa kulidhibiti.Shida hii ni ya familia ya wana Iringanaomba tusaidiane.
6.
Nyamba zilizo maeneo hatarishi nazilizojengwa kwenye maeneo ya wazina maeneo ya michezo zibomolewe ilikuepusha mivutano na srikaliAidha,tusaidiane kutoa elimu kwa wauminiwetu umuhimu wa maeneo waziyaliyotengwa na Manispaa.
7.
Hali ya magonjwa ya kuhara nakipindupindu ni tishiohivyo lazimatujenge vyoo ili kuepukana na kulauchafu ambao hutupelekea kuumwana kufa.
8.
Kuhusu miundombinuNaombatutunze miundombinu yote Mkoni iliidumu.  Serikali inaweka taa mtaa waGangilonga ili mji wetu uendeleekupendeza na waumini mkipitaasubuhi kwenda kusali pawe namwanga kwa ajili ya ulinzi na walewanaochelewa kurudi nyumbaniwabaki salama.
9.
Katika Mkoa wetu wa Iringatunachangamoto ya lishenawaombawote kwa pamoja kupitia maafisalishe tutafakari swala la lishe ambalohuathiri maendeleo ya jamii katikaMkoa wa Iringa. Ni muhimu tuzingatielishe boraAidhautamaduni wetu wakukoboa na kuosha mahindi tuachena tutayarishe kwa kuzingatiamahitaji halisi na mchanganyikomzuri wa lishe (wangaprotini,mboga za majanina matunda).

 

10.
UKIMWI

Hali ya maambukizi ni kubwa katikaMkoa wetu (9.1). Juhudi za pamojazinahitajika ili kupunguza maambukizimapyaHii ni vita isiyohitaji silaha ilikila mmoja aamue ndani ya nafsiyake na achukue hatua.

Baada ya kusema hayonapendakushukuru tena kwa kunialika nijenishirikiane nanyi kwenye mkesha huumkubwa wa kuliombea taifa letu. Serikaliinaahidi kuendelea kutoa ushirikianowowote utakaohitajika kwa madhehebuyote ya dini ili kufanikisha utekelezaji wakuwaletea wananchi maendeleo.

Mwishonawatakia kila la kheri nahongera kwa kumaliza Mwaka 2015 nakuingia mwaka mpya 2016.

Amina, MWENYEZI MUNGU AWABARIKI.SERIKALI WILAYA YA IRINGA YAONYA WALIMU KUHUSU MICHANGO NA ADA ILIYOFUTWA


Na Matukiodaimablog,Iringa

MKUU  wa  wilaya ya  Iringa  Bw  Richard  Kasesela  (pichani)ameagiza wazazi  wa  wanafunzi  wote ambao walichaguliwa    kujiunga na  elimu ya  sekondari  kati  ya mwaka juzi na mwaka jana na kushindwa kujiunga na sekondari  kutokana na kukosa uwezo  wa kulipa ada na michango  kurudi shuleni   kunufaika na  agizo la Rais Dr  John Magufuli la kutaka elimu ya Msingi na  sekondari kutolewa bila malipo yoyote .

Huku akiwataka wale  wote  waliojenga maeneo yasiyo ruhusiwa wakiwemo  waliojenga mabondeni na  milimani kuanza  kutafuta maeneo ya kujenga yanayoruhusiwa kisheria kabla ya kuanza  kwa  zoezi la kuvunja nyumba   hizo baada ya  kuukaribisha  mwaka mpya  wa 2016.

Mkuu huyo  wa  wilaya  alitoa agizo  hilo leo ofisini  kwake  wakati akitoa  salamu za serikali ya wilaya ya  Iringa kwa  wananchi  wa  wilaya  hiyo  mbele ya  waandishi  wa habari ofisini  kwake ,kuwa serikali  ya Rais Dr Magufuli ni  serikali  inayofanya mambo  yake kwa  kufuata sheria za nchi  hivyo baada ya agizo la Rais la  kufuta  michango yote na ada kwa  shule  za msingi na  sekondari  jukumu lake kama  mkuu wa  wilaya  kuona agizo  hilo  linatekelezwa .

Alisema hatakubali  kuona mwalimu mkuu  wa  shule  ya msingi ama  sekondari  akishindwa  kumpokea mwanafunzi kwa kukosa ada wala  michango kwani suala la michango ya aina  yeyote ile kwa mzazi ama  mwanafunzi imefutwa hivyo ni  uvunjifu  wa serikali iwapo mwanafunzi atakosa  elimu kwa kudaiwa  michango ama ada ambayo  imefutwa .

"Sitakubali  kuona watoto  wanakosa  elimu eti  kwa  walimu  kuwadai michango nitachukua hatua kali kwa  mwalimu yeyote atakayefukuza  ama  kushindwa  kupokea  mwanafunzi kwa madai ya  kukosa mchango ama ada .......pia  naagiza  wanafunzi  waliochaguliwa  kujiunga na kidato  cha kwanza mwaka 2014/2015 ambao  walishindwa kujiunga kutokana na kukosa michango ama ada kama inawezekana  kuangaliwa  uwezekano  wa  kurudishwa  shule  ili  kunufaika na neema hiyo ya  serikali ya  Rais Dr John Pombe Magufuli ya elimu  bure"

Hata  hivyo  hivyo  alisema kuwa  serikali imefuta michango  na ada  kwa  shule  za msingi pamoja na sekondari na  sio  imefuta michango ya  wananchi  kushiriki kujenga vyumba vya madarasa ama nyumba  za  walimu  hivyo  alisema ni jukumu la  kila mwananchi  kushiriki katika  shughuli  za  kimaendeleo pale  zinapojitokeza katika eneo lake.

Kuhusu wananchi  waliojenga katika maeneo yasiyo  ruhusiwa  wakiwemo  waliojenga  milimani na mabondeni  pamoja na  wale  waliojenga katika maeneo ya  wazi mkuu  huyo  wa  wilaya  aliwataka  kuanza  kutafuta maeneo yanayoruhusiwa  kisheria na  kuwa serikali ya wilaya  hiyo ipo katika utekelezaji wa agizo la  serikali  lililotolewa na waziri wa Ardhi ,nyumba na maendeleo ya makazi Bw Wiliam Lukuvi la  kutaka watu hao  kuanza  kuondoka wenyewe kabla ya  kuvunjiwa  nyumba  zao .

Kuwa  kwa  wilaya ya Iringa zoezi  hilo  linataraji  kuanza  wakati  wowote  kuanzia mwezi Januari 2016 na  kuwa hawatakuwa na huruma katika  utekelezaji  wa agizo hilo la  serikali na  kuwataka pia  wananchi  ambao  nyumba  zao zimechakaa zipo hatarini kubomoka basi  kuzifanyia kuzivunja na kujenga  upya ama  kuweza  kutafuta  wabia ili  kunusuru uhai  wao.

Bw Kasesela  aliwataka  wananchi  wanaoegesha magari katika maeneo yasiyoruhusiwa mjini Iringa wakiwemo  wale  waliogeuza gereji eneo la barabara mbili kuondoka mara  moja kwani suala  hilo halikubaliki na hatua kali  zitachukuliwa kwa  wote  wanaoendesha  shughuli zao kinyume na taratibu wakiwemo  wanaouza vyakula  na matunda katika mazingira hatarishi.

Pia  alisema serikali ya  wilaya ipo katika mchakato  wa kuwachukulia hatua kali watumishi  wa huduma za afya ambao  wanauza dawa katika maduka  yao na  kuwafanya  wananchi  kukosa dawa  pindi  wanapofika  kupatiwa matibabu katika vituo  vya afya ,zahanati na Hospitali za  serikali na  kuwa watumishi hao dawa yao imekwisha chemka bado kunyweshwa .

Wakati  huo  huo  mkuu  huyo wa wilaya amepongeza jitihada za  vyombo vya habari mkoani Iringa katika kuhamasisha  jamii kushiriki zoezi la usafi na kipekee  kupongeza  kituo  cha Radio Nuru Fm ya mkoani Iringa kwa kuhamasisha  zoezi hilo kwa vitendo  baada ya wafanyakazi  wake wote kushiriki  kufanya usafi katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa siku ya Desemba 9 mwaka jana.