Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

November 30, 2014

RC IRINGA AMTUPA MAHABUSU DIWANI WA CCM,KISA KURUHUSU MAFUNDI KWENDA KANISANI KUSALI

UTEKELEZAJI        wa  agizo la Rais Jakaya  Kikwete juu ya  ujenzi  wa maabara katika  shule za  sekondari  nchini  umeendelea   kuwa mwiba mkali baada ya  mkuu  wa  mkoa  wa Iringa Amina Masenza  kumpeleka  polisi diwani  wa kata ya Ulanda tarafa ya Kalenga  Philimon Temaigwe (CCM) kufuatia  mkuu  huyo wa mkoa  kufika kukagua ujenzi wa maabara  shule ya sekondari Kalenga na kutowakuta mafundi na diwani huyo alipoulizwa alimjibu  kuwa  leo ni  jumapili watu wanaimani  zao  wapo kanisani .

Wakizungumza na mtandao huu wa matukiodaima  baadhi ya  wananchi na  viongozi  wa kijiji  cha Kalenga   waliofika mjini Iringa  kulalamikia uamuzi wa mkuu  huyo wa mkoa  kumkamata  diwani  wao ,walisema  kuwa  mkuu  huyo  wa mkoa na msafara  wake wa kamati ya  ulinzi na usalama mkoa na  wilaya   walifika eneo hilo mida ya saa 5 asubuhi  ikiwa ni mwendelezo wa  ziara  yake ya  kukagua maendeleo ya ujenzi wa maabara  hizo .

 Alisema  mmoja kati ya  viongozi wa  serikali katika kata  hiyo ambae  aliomba  jina  lake  lisitajwe hapa kwa  kuhofia usalama  wake  kuwa  mbali ya  kuwa jana  ilikuwa ni  siku ya ibada  wananchi   waliweza  kujitokeza kwa  wingi  kumpokea mkuu  huyo wa mkoa ila baada ya  kufika  eneo  la ujenzi na  kuona  hakuna mafundi  ndipo alipoanza kuuliza  juu ya sababu ya mafundi kutokuwepo eneo la ujenzi.

" Mkuu  huyo wa mkoa  aliuliza swali  kuwa mafundi   wapo  wapo mbona  sioni kazi ikiendelea  hapa  ndipo  diwani  alipojibu kuwa  mheshimiwa mkuu wa mkoa  leo ni jumapili  watu wanaimani  zao   wapo kanisani .......ndipo alipouliza  tena  umesema mafundi  wapo wapi ....kanisani  hujui  kuwa huu  ujenzi  wa maabara ni kama  vita  iwapo vita ingetokea   wangekuwa kanisani " alihoji mkuu  huyo wa mkoa.

Hata   hivyo  diwani   huyo aliendelea  kumjibu  kuwa  kuwa shida ya mafundi  kutofika katika kazi ni kwa ajili ya  jumapili  hivyo  wapo ibadani  alijibu  diwani huyo kwa  kujiamini zaidi.

Kutokana na majibu  hayo  ndipo mkuu  huyo wa mkoa  alipouliza  viongozi    aliokuwa nao katika  ziara   hiyo  kuwa  huyo anayemjibu hivyo ni nani  swali ambalo  kaimu mkurugenzi  wa Halmashauri ya Iringa  vijijini Gowike  alimjibu mkuu  wa mkoa  kuwa  huyo ni mheshimiwa   diwani

"  Huwezi  kunijibu hivyo  mimi   wewe  RPC (kamanda wa polisi) kamata  huyo nilitee ofisini  jumatatu  saa 6 mchana " alisikika  akitoa maagizo  hayo  mkuu  huyo wa mkoa  huku  akiingia katika  gari lake na  kuondoka na msafara  wake na wakati huo  diwani akiwa chini ya ulinzi kwa kuingizwa katika gari la polisi alisema  kiongozi huyo  wa  serikali .

Pia  alisema  wamesikitishwa  sana  kuona  diwani  wao akidhalilishwa  mbele ya  wapiga  kura  wake   huku mkuu  huyo wa mkoa  akitambua  wazi kuwa hata  wananchi waliofika walikusanyika  hapo kwa jitihada za  diwani na ushirikiano mzuri alionao na wananchi wake.


Akizungumzia  suala  la kukamatwa kwa  diwani  huyo mwenyekiti wa  Halmashauri ya  Iringa Stivin Mhapa  alisema  kuwa amejulishwa  juu ya kukamatwa kwa  diwani huyo  japo kwa  upande wake  hakuwepo katika msafara  huo ila diwani alimpigia  simu na kumweleza .

Bw Mhapa  alisema  kuwa pamoja na kuwa ni mapema   kutoka majibu kwa  sasa  juu ya baraza lake la madiwani  juu ya hatua   iliyochukuliwa na mkuu  huyo wa mkoa lakini bado anatambua  kuwa  ujenzi wa maabara  hiyo umefikia hatua nzuri  kutokana na jitihada za  diwani huyo ambae amejitolea  zaidi  kuchangia ujenzi huo na siku  zote amekuwa akishinda  eneo la ujenzi  kushirikiana na wananchi wake  katika  shughuli za maendeleo ya ujenzi huo.

" Leo  ni  jumapili kweli  sasa  hata kama tunataka  ujenzi ukamilike  bado  hatuwezi  kuwazuia  wananchi  kwenda  kuabudu  eti  kwa  kuwa ni ujenzi wa maabara  ila labda  kama  kuna  sababu nyingine ila  kweli kitendo cha kumkamata diwani kwa kumjibu  swali  aliloulizwa  ......hapana  nakuja  mjini kuja  kufuatilia kwa karibu  suala   hili"

Mtandao huu wa matukiodaima  ulimtafuta kwa njia ya simu   kamanda wa  polisi mkoa wa Iringa  Ramadhan Mungi  ili  kuthibitisha  taarifa  hizo alisema  kuwa kwa upande  wake hakuwepo katika msafara   huo kwani  yupo nyumbani anasumbuliwa na homa hivyo  alitaka atafutwe  mkuu  wa mkoa mwenyewe ili  kujibia  hilo.

Huku mkuu  wa mkoa huyo Amina Masenza  alipopigiwa  simu na mwandishi wa habari hizi ili kutolea ufafanuzi zaidi hakuwa tayari kulizungumzia mbali ya kupokea simu na baada ya Mwandishi wetu kujitambulisha na kumhoji sababu ya kumkamata diwani huyo aliishia kuguna na kusema nakuomba ofisini kisha kukata simu

" Ndio naomba uje ofisini napokea simu nyingine" alisema mkuu huyo wa mkoa na kukata simu 

Diamond hashikiki azoa tuzo za Channel O Music Video Awards 2014 .


Macho ya Watanzania wengi kwa siku ya Jumamosi Nov  29 yalielekezwa kwenye ukumbi wa Nasrec Expo Centre Afrika Kusini sehemu ambako zilikua zikitolewa tuzo za wateule wa Channel O Music Video Awards ‘CHOMVA’
Furaha tuliyokuwa nayo Watanzania ilikua kubwa baada ya kuona kijana kutoka nyumbani Tanzania kuwa ni miongoni mwa vijana walioshinda tuzo hizo katika vipengele (3) ambavyo ni Most Gifted East,Most Gifted Afro Pop na Most Gifted Newcomer.
Hii ndio orodha kamili ya washindi
Most Gifted R&B video
Crazy but Amazing-Donald
Most Gifted West Video
‘Turn Up-Olamide
Most Gifted Ragga/Dancehall
Buffalo Soulja
The Most Gifted Kwaito
Uhuru ft Oskido & Professor Kalawa -tjukutja
Most Gifted East Video 
Diamond Platnumz
Most Gifted Dance Video 
Busiswa-Ngoku
Most Gifted Hip Hop Video 
AKA- Congratulate
Most Gifted Newcomer
Diamond Platnumz
Most Gifted Male Video 
Casper Nyovest-Doc Shebeleza
Most Gifted Female Video
Tiwa Savage-Eminado
Most Gifted Afro Pop Video
Diamond Platnumz
Most Gifted duo/group/featurning
KCEE ft Wizkid-Pull Over
Most Gifted Video of the Year
Carsper  Nyovest- Dos Shebeleza

Taarifa ya bank ya Mkombozi juu ya sakata la Escrow

TAARIFA YA BENKI YA MKOMBOZI KWA UMMA

Utangulizi

Taarifa hii inatolewa kwa umma kutokana na ripoti mbalimbali zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari mitandao ya kijamii na taarifa iliyotolewa kwenye mjadala katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

1. Ufunguzi wa akaunti ya VIP engineering and Marketing (VIP)

Kampuni ya VIP engineering and Marketing ni kampuni ambayo imesajiliwa kwa mujibu wa sheria za Tanzania. Kampuni hii ilifungua akaunti katika benki ya biashara ya Mkombozi na hivyo kuwa moja kati ya wateja wa benki. Benki ilijiridhisha na ilizingatia taratibu zote za ufunguzi wa akaunti husika kwa kuzingatia sheria za nchi na kanuni zinazozitaka benki kupata nyaraka muhimu kutoka kwa mteja wakati wa ufunguzi wa akaunti hiyo.

Nyaraka hizo ni pamoja na kuwepo kwa cheti cha usajili wa kampuni, kanuni za kampuni, idhinisho la kampuni kumruhusu moja kati ya wanahisa wake kuendesha akaunti pamoja na picha na hati ya kusafiria ya mhusika wa kuendesha akaunti hiyo.

2.0 Mauzo ya hisa za VIP

Kampuni ya VIP ilileta mkataba kwenye benki ya Mkombozi wa mauziano ya hisa za asilimia 30 baina ya VIP na kampuni ya Pan Africa Power Solutions (PAP) ambazo inamiliki katika kampuni ya IPTL. Mkataba huo ulisainiwa tarehe 19 Ogasti, 2013. Bei ya asilimia 30 ya hisa hizo ilikuwa ni dola za Marekani milioni 75. Katika kifungu namba 2.4 cha mkataba wao kinaelekeza fedha za mauzo ya hisa zilipwe kwenye akaunti ya VIP iliyopo benki ya Mkombozi. Mkataba huo wa mauziano ya hisa baina ya kampuni hizi mbili ulitambuliwa na hukumu ya Mahakama Kuu ya Tanzania iliyotolewa na Jaji J.H.K Utamwa tarehe 5 Septemba, 2013.

3. Mchakato wa kulipa kodi ya serikali

Benki ilitambua kwamba katika mauziano hayo ya hisa ni lazima kodi ya Serikali ilipwe na hivyo iliizishauri pande zote mbili kupeleka mkataba husika katika ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili kufanyiwa makadirio ya kodi husika. Tarehe 20 Januari, 2014 TRA iliiandikia barua kampuni ya VIP na nakala ya barua hiyo kuletwa kwenye benki ya Mkombozi. Katika barua hiyo TRA iliitaarifu kampuni ya VIP kuwa makadirio ya kodi yatokanayo na mauzo ya hisa ni shilingi 38,186,584,322.00 ikiwa ni kodi ya mauzo ya hisa ya asilimia 30 za mauzo ya hisa kutoka VIP kwenda kwa PAP.(Capital gains and stamp duty).

TRA pia iliiagiza benki ya Mkombozi kuhakikisha kuwa inalipa kodi hiyo kwa niaba ya VIP mara tu fedha zitakapoingia kwenye akaunti yake.

Malipo ya kodi ya shilingi 38,186,584,322.00 yalilipwa TRA kwenye akaunti 11120100 iliyopo katika Benki Kuu ya Tanzania na TRA ilikiri kupokea kodi hiyo kwa barua yake yenye kumbukumbu namba 3-4/100/100/223/4 ya tarehe 24 Januari, 2014.

4. Ufafanuzi wa mambo mbalimbali

4.1 Benki ya mkombozi kuhusika katika kusafisha fedha chafu

Fedha zote zilizoingizwa kwenye akaunti ya VIP iliyopo kwenye benki ya Mkombozi zilitokana na mauziano ya hisa kati ya VIP na PAP kwa mkataba uliotambuliwa na Mahakama Kuu ya Tanzania. Chanzo cha malipo hayo ni kuhamisha fedha kutoka kwenye akaunti ya PAP iliyopo katika benki ya Stanbic na kuingizwa kwenye akaunti ya VIP iliyopo katika benki ya Mkombozi.

Fedha hizo zilihamishwa katika mafungu mawili. Fungu la kwanza ilikuwa ni shilingi 73,573,500,000.00 zilihamishwa kwa njia ya TISS kwa kumbukumbu namba 000000050720 ya tarehe 23 Januari, 2014 na fungu la pili ni dola za Kimarekani 22,000,000.00 zilihamishwa kwa TISS kwa kumbukumbu namba000000050812 ya tarehe 23 Januari, 2014. Malipo mengine ya asilimia kumi ya mauzo ya hisa yalilipwa kwenye akaunti ya Mkombozi iliyopo Benki Kuu ya Tanzania. Kutokana na mchakato huo benki ya Mkombozi ilijiridhisha kuwa fedha hizo ni malipo halali na siyo fedha chafu.

Benki ya Mkombozi haijihusishi na utakasishaji wa fedha chafu na haramu katika uchumi wa Tanzania.

4.2 Malipo yatokanayo na akaunti ya VIP

Malipo toka kwenye akaunti ya mteja hufanywa kutokana na maelekezo ya mteja. Benki ikishajiridhisha kuwa fedha ya mteja ni halali na ipo kwa mujibu wa sheria na hamna zuio lolote toka katika mahakama hapa nchini hutekeleza malipo kwenye akaunti ya mteja kutokana na maelekezo yake.

Benki ilijiridhisha kuwa malipo yote yaliyofanywa kutoka kwenye akaunti ya VIP ni halali kwa kuwa chanzo cha pesa hizo ilikuwa ni halali kutokana na mauzo ya hisa na ulipwaji wa kodi ya Serikali kama ilinyoelezwa hapo juu. Kutokana na sababu hiyo benki haikuwa na shaka juu ya malipo hayo.

4.3 Malipo taslimu kwa wateja na kubeba fedha kwenye viroba, mifuko ya rambo na magunia

Benki inatoa tamko kuwa malipo yote yaliyofanywa katika akaunti ya VIP yalilipwa kupitia akaunti za walipwaji. Hakuna fedha zilizolipwa taslimu kwa wateja na kubebwa kwenye viroba au magunia kama ilivyoripotiwa Bungeni. Pesa iliyotoka kwenye akaunti ya VIP tarehe 6 Februari, 2014 kiasi cha shilingi 3,314,850,000.00 ililipwa kwenye akaunti nane za wateja tofauti na siyo kubebwa kwenye viroba au magunia.

Na zile zilizotoka toka benki ya Stanbic zilizotajwa hapo juu zilitumwa kwa njia ya TISS na siyo kubeba kwenye magunia au viroba.

4.4 Malipo kwa mfanyakazi wa benki ya Mkombozi

Gazeti la Mawio la tarehe 20-26, Novemba, 2014 tolea namba 0122 liliandika kuwa mwanasheria wa benki ya Mkombozi ajulikanaye kwa jina la Rweyengeza Alfred alipokea malipo toka akaunti ya VIP ya shilingi milioni 40.2.

Benki inatoa tamko kuwa haina mfanyakazi anayetambuliwa kwa jina hilo na wala hakuna mfanyakazi yeyote wa benki aliyelipwa fedha toka kwenye akaunti ya VIP.

Wito kwa umma

Benki ya Mkombozi inachukua fursa hii kuwatarifu wateja wake na umma kutopotoshwa na taarifa au tuhumma zilizofafanuliwa hapo juu na kuwataka wateja wake wote kutokuwa na hofu yeyote kwani benki ipo imara na inafanya kazi kwa kufuata misingi ya sheria, taratibu na kanuni zilizowekwa na Benki Kuu ya Tanzania. Benki inawataarifu wateja wake na Watanzania kwa ujumla kutoyumbishwa na tuhumma hizo ambazo hazina ukweli ndani yake na badala yake waitumie benki yao kwa shughuli za maendeleo ya nchi yetu.

Pamoja tunajenga nchi na uchumi wa nchi yetu.

Hitimisho

Benki ya biashara ya Mkombozi haijihusishi na haitajihusisha na utakasishaji wa fedha chafu.

Imetolewa na:

MKURUGENZI MTENDAJI BENKI

Soma mapendekezo ya PAC juu ya wezi wa Escrow

MAAZIMIO YA BUNGE KUHUSU HOJA YA TAARIFA MAALUM YA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA HESABU ZA SERIKALI KUHUSU TAARIFA YA UKAGUZI

MAALUM KUHUSIANA NA MIAMALA ILIYOFANYIKA KATIKA AKAUNTI YA ‘ESCROW’ YA TEGETA

PAMOJA NA UMILIKI WA KAMPUNI YA IPTL

_____________________________________1.    KWA KUWA, Taarifa Maalum ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali Kuhusu Ukaguzi Maalum wa Malipo yaliyofanyika katika Akaunti ya Escrow ya Tegeta uliofanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (‘CAG’) pamoja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (‘TAKUKURU’) imeonesha kwamba kwamba Harbinder Singh Sethi, James Rugemalira (VIP), Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Waziri wa Nishati na Madini, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (‘TANESCO’) walihusika kwa namna moja au nyingine katika kufanikisha kufanyika miamala haramu ya fedha za Akaunti ya Escrow ya Tegeta kwenda kwa makampuni ya Pan African Power Solutions Ltd. (‘PAP’), na VIP Engineering & Marketing (‘VIP’);


KWA KUWA, kwa sababu ya kuhusika kwa watu hao na miamala iliyofanyika kwenye Akaunti ya Escrow imeliingizia Taifa hasara ya mabilioni ya fedha za umma zinazotokana na kutokulipwa kwa kodi mbali mbali za Serikali na kushindwa kwa TANESCO kukokotoa upya kiwango cha malipo ya gharama za uwekezaji (‘capacity charges’) wa IPTL;


KWA KUWA, mabilioni ya fedha yaliyotolewa kwenye Akaunti ya Escrow yametumika kuwapa kile kinachoonekana kuwa ni rushwa baadhi ya viongozi na maafisa wa serikali kama vile Mawaziri, Majaji, Wabunge, Wenyeviti wa Kamati za Bunge, wakuu wa taasisi za umma, viongozi wa dini, mawakili wa kujitegemea na watu binafsi.


NA KWA KUWA, vitendo vilivyofanywa na watu hawa vinaashiria makosa mbali mbali ya jinai kama vile uzembe, wizi, ubadhirifu, kutakatisha fedha haramu, matumizi mabaya ya madaraka, rushwa na kupokea mali ya wizi;


HIVYO BASI, BUNGE LINAAZIMIA KWAMBA, TAKUKURU, Jeshi la Polisi na vyombo vingine husika vya ulinzi na usalama viwachukulie hatua stahiki za kisheria, kwa mujibu wa sheria za nchi yetu, watu wote waliotajwa na Taarifa Maalum ya Kamati kuhusika na vitendo vyote vya kijinai kuhusiana na miamala ya Akaunti ya Escrow, na watu wengine watakaogundulika kuhusika katika vitendo hivyo vya jinai kufuatia uchunguzi mbali mbali unaoendelea;


2.    KWA KUWA, vitendo vya kijinai wanavyhohusishwa navyo viongozi wa umma na maafisa wa ngazi za juu serikalini vinakiuka pia maadili ya viongozi wa umma na kuwanyima viongozi na maafisa hao uhalali wa kuendelea kushikilia nafasi za mamlaka katika uongozi wa umma;


HIVYO BASI, BUNGE LINAAZIMIA KWAMBA, Waziri wa Nishati na Madini, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa TANESCO wawajibishwe, kwa kuishauri mamlaka yao ya uteuzi kutengua uteuzi wao;


3.    KWA KUWA, katika watu walioshiriki kwa namna moja au nyingine katika kashfa ya miamala ya Akaunti ya Escrow wapo pia viongozi wa Kamati za Kudumu za Bunge kama vile Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TANESCO;


NA KWA KUWA, Bunge na/au Kamati zake za Kudumu zina uwezo na mamlaka, kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge, ya kuwawajibisha viongozi hawa wa Kamati kwa kuwavua nyadhifa zao;


HIVYO BASI, BUNGE LINAAZIMIA KWAMBA, Kamati husika za Kudumu za Bunge zichukue hatua za haraka, na kwa vyovyote vile kabla ya Mkutano wa Kumi na Nane wa Bunge, kuwavua nyadhifa zao Wenyeviti tajwa wa Kamati husika za Kudumu za Bunge;


4.    KWA KUWA, Taarifa Maalum ya Kamati imeonesha kwamba katika watu waliotajwa kuhusika kwa namna moja au nyingine katika kashfa ya miamala ya Akaunti ya Escrow wapo pia Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania;


KWA KUWA, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 (‘Katiba’) imeweka utaratibu mahsusi wa kushughulikia nidhamu ya Majaji;


KWA KUWA, utaratibu wa kushughulikia nidhamu ya Majaji kwa mujibu wa Katiba unamtaka Rais kuunda Tume ya Uchunguzi ya Kijaji kuchunguza tuhuma za utovu wa maadili dhidi ya Majaji;


NA KWA KUWA, utaratibu wa kushughulikia nidhamu ya Majaji kwa mujibu wa Katiba unamruhusu Rais kumsimamisha kazi Jaji au Majaji husika wakati uchunguzi wa tuhuma dhidi yake unaendelea;


HIVYO BASI, BUNGE LINAAZIMIA KWAMBA, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aunde Tume ya Kijaji ya Uchunguzi kuchunguza tuhuma za utovu wa maadili dhidi ya Jaji Aloysius Mujulizi na Jaji Profesa Eudes Ruhangisa wa Mahakama Kuu ya Tanzania;


5.    KWA KUWA, Taarifa Maalum ya Kamati imeonesha kwamba Stanbic Bank (Tanzania) Ltd. ilishiriki kupokea na kutakatisha fedha zilizotolewa kwa njia haramu kutoka katika Akaunti ya Escrow na kupelekwa katika akaunti zilizofunguliwa na PAP katika benki hiyo;


KWA KUWA, Taarifa Maalum ya Kamati imeonesha kwamba akaunti za PAP  katika Stanbic Bank Tanzania Ltd. zimekwishafungwa baada ya fedha zote zilizotolewa katika Akaunti ya Escrow kumalizika na Akaunti ya ya VIP katika Mkombozi Commercial Bank imebakiza kiasi fulani cha fedha;


NA KWA KUWA, Taarifa Maalum ya Kamati inaonesha kwamba kuna uwezekano fedha zilizotolewa kutoka kwenye akaunti za PAP na VIP zilipelekwa katika benki nyingine;


NA KWA KUWA, vitendo vya Stanbic Bank (Tanzania) Ltd., na benki nyingine kupokea na kutakatisha fedha zilizotolewa kwenye Akaunti ya Escrow ni vitendo vya jinai kwa mujibu wa Sheria ya Udhibiti wa Fedha Haramu;


HIVYO BASI, BUNGE LINAAZIMIA KWAMBA, mamlaka husika za kifedha na za kiuchunguzi ziitaje Stanbic Bank (Tanzania) Ltd. na benki nyingine yoyote itakayogundulika, kufuatia uchunguzi wa mamlaka za kiuchunguzi, kujihusisha na utakatishaji wa fedha zilizotolewa katika Akaunti ya Escrow, kuwa ni taasisi zenye shaka ya utakatishaji wa fedha haramu (institutions of money laundering concern);


6.    KWA KUWA, vitendo vya wizi, ubadhirifu wa mali ya umma, hujuma ya uchumi na ufisadi vimeongezeka, kushamiri na kushirikisha viongozi wa kisiasa na maafisa wa serikali pamoja na wafanya biashara wakubwa;


KWA KUWA, kwa mujibu wa sheria iliyoiunda, TAKUKURU inashughulikia vitendo vya aina zote za rushwa zikiwemo rushwa ndogo ndogo (petty corruption) na rushwa kubwa na ufisadi (grand corruption) na matumizi mabaya ya madaraka;


NA KWA KUWA, kwa sababu ya majukumu yake mapana kisheria, TAKUKURU inaelekea kuelemewa katika vita ya kupambana na kudhibiti vitendo vya rushwa kubwa, ufisadi na hujuma za uchumi zinazotishia uhai wa taifa letu kiuchumi, kijamii na kisiasa;


HIVYO BASI, BUNGE LINAAZIMIA KWAMBA, Serikali iandae na kuwasilisha Muswada wa marekebisho ya Sheria iliyoiunda TAKUKURU kwa lengo la kuanzisha taasisi mahsusi itakayoshughulikia, kupambana na kudhibiti vitendo vya rushwa kubwa, ufisadi na hujuma za uchumi zinazotishia uhai wa taifa kiuchumi, kijamii na kisiasa;


7.    KWA KUWA, Taarifa Maalum ya Kamati imeonesha jinsi ambavyo TANESCO imekuwa ikitumia mabilioni ya fedha kulipa gharama za umeme unaozalishwa na IPTL na hivyo kuathiri hali ya kifedha ya Shirika hilo;


KWA KUWA, Taarifa Maalum ya Kamati inaonesha kwamba TANESCO itaendelea kulipa fedha nyingi kwa ajili ya gharama za umeme huo wa IPTL;


HIVYO BASI, Bunge linaazimia kwamba Serikali iangalie uwezekano wa kununua mitambo ya kufua umeme ya IPTL na kuimilikisha kwa TANESCO kwa lengo la kuokoa fedha za Shirika hilo.


8.    KWA KUWA, kwa miaka mingi mikataba mibovu ya kuzalisha umeme kati ya TANESCO na makampuni binafsi ya kufua umeme imeisababishia TANESCO hasara ya mabilioni ya fedha na hivyo kutishia uhai wake wa kifedha;


KWA KUWA, Bunge lilikwishaazimia kwamba serikali iwasilishe mikataba husika Bungeni au kwenye Kamati zake kwa lengo la kuliwezesha Bunge kutekeleza vyema wajibu wake wa kuisimamia na kuishauri serikali;


NA KWA KUWA, Serikali haijatekeleza Azimio hilo la Bunge hadi sasa;


HIVYO BASI, Bunge linaazimia kwamba Serikali itekeleze Azimio husika la Bunge mapema iwezekanavyo na kwa vyovyote vile kabla ya kumalizika kwa Mkutano wa Bu

RAIS Kikwete awasili nchini

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mmoja wa abiria wakati ndege aliyopanda ilipotua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Katibu wa Rais Bw. Morris Mbena baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea

Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam baada ya kuwasili akitokea Marekani kwenye matibabu leo

Novemba 29, 2014
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia mkono wafanyakazi  katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam baada ya kuwasili akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba

29, 2014
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkuu wa Majeshi Jenerali davis Mwamunyange baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP  Ernest Mangu baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja  baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama Bw. Rashid Othman baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mama Maria Nyerere baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikumbatiana kwa furaha  na Mama Maria Nyerere baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimshukuru  Mama Maria Nyerere baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na viongozi mbalimbali baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na viongozi mbalimbali baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014
 Mama Maria Nyerere akiongea na Mama Salma Kikwete katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam baada ya Rais Kikwete kuwasili akitokea Marekani kwenye matibabu leo

Novemba 29, 2014
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiongea na Mama Maria Nyerere aliyefika kuwapokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na waandishi wa habari na viongozi mbalimbali waliokuja kumlaki baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na waandishi wa habari na viongozi mbalimbali waliokuja kumlaki baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014
Dua ilisomwa na viongozi mbalimbali wa dini  baada ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete kumaliza kuongea na wanahabari mara tu alipowasili  katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia wafanyakazi wa ikulu waliojitokeza kumpokea mara baada ya kuwasili ikulu akitokea nchini Marekani kwenye matibabu
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia kwa furaha wafanyakazi wa ikulu waliojitokeza kumpokea mara baada ya kuwasili ikulu akitokea nchini Marekani kwenye matibabu
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea mashada ya maua kutoka kwa wafanyakazi wa Ikulu waliojitokeza kumpokea mara baada ya kuwasili Ikulu akitokea nchini Marekani kwenye matibabu. Kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue aliyeongoza mapokezi hayo ya Ikulu 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea kadi ya pole toka kwa mjukuu wake Aziza Ridhiwani Kikwete mara baada ya kuwasili Ikulu 

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa kwa furaha na mwanaye Khalfani baada ya kuwasili nyumbani salama

November 29, 2014

Serikali kuunda timu ya kuchunguza wizi wa pesa za escrow

SERIKALI imeunda timu ya wataalam kwa ajili ya kupitia mapendekezo ya taarifa ya CAG kubusiana na wizi wa fedha uliofanyika katika kaunti ya Tegeta Escrow .

Mwandishi wetu wa MATUKIO daima  Joyce Kasiki anaripoti kutoka Dodoma kuwa ,Waziri Mkuu Mizengo Mizengo alitoa kauli hiyo wakati akihitisha mkutano wa 16 na 17 wa Bunge la 10 ambapo alisema mapendekezo hayo ni lazima yatekelezwe na Serikali.

Alisema timu hiyo imeundwa ili kupitia mapendekezo hayo kila eneo ili kuandaa majibu ambayo  baadhi yake , yanahusisha kwa karibu  na maazimio ambayo nayo yatatengenezewa utaratibu wake  .

Alisema Serikali itahakikisha   maazimio yote yanafanyiwa  kazi kikamilifu.

"Mimi ni mmoja Kati ya watu tunaoamini katika kauli inayosema yaliyopita si ndwele tugange yajayo,nataka niungane na wenzangu waliosema katika kujadili suala hili kulikuwepo na mambo mengi,kutiliana mashaka katika maeneo mbalimbali,lugha kali,lakini yote ilikuwa ni katika kuhitimisha jambo hili kwa maslahi ya Nchi yetu,

" Nataka niwaahidi  wabunge na watanzania wote,Serikali itaendelea kusimamia kwa  nguvu zake  zote kuhakikisha mali  na rasilimali za Taifa hili  zinalindwa na kusimamiwa kikamilifu ." alisema Pinda

Aidha alisema kuwa kama ilivyopendekezwa,Seriali itachukua hatua kwa wale wote  watakaopatikana na ushahidi wa kutosha kuhusu  mambo yoyote ambayo yatakuwa yamefunja  Sheria za Nchi na watashughulikiwa kwa mujibu wa Sheria na watafikishwa kwenye vyombo vya Sheria ili iweze kuchukua mkondo wake.

Vile vile alisema kwa wale   ambao watalazimika kutumia taratibu za kiutawala ,hatua stahiki zitachukuliwa kwa mujibu wa Sheria,kanuni na taratibu za nchi  hii .

Hata hivyo Pinda alisema Katima taarifa ya CAG imeacha giza swali ambalo bado Serikali haijaelewa kama fedha zilizoibwa katika akaunti ya Tegeta Escrow ni za IPTL au ni fedha za Umaa kwa kauli aliyoitoa ya 'inawezekana' katika taarifa yake.

Kutokana na utata huo,Pinda alisema,Serikali itafuatilia kwa kina na kutoa majibu ili kuondoa giza  hilo.

Bunge limeahirishwa hadi Januari 27 ,2015 litakapokutana tena.

MATUKIO KATIKA PICHA MAHAFALI YA CHEKECHEA 2014 SHULE YA SOUTHERN HIGHLANDS MAFINGA NA SIKU YA WAZAZI

Mkurugenzi mtendaji  wa  Shule za  Southern Highlands Mafinga  Mary  Mungai akishirikiana na mgeni rasmi  kuwalisha  keki wanafunzi wa  shule  hiyo  leo wakati wa mahafali ya  chekechea na siku ya  wazazi
Wanafunzi  wakionyesha  michezo mbali mbali 
Baadhi ya  wanafunzi wa shule  hiyo  wakifuatilia  michezo mbali mbali
Mgeni rasmi  akitoa  vyeti kwa  wahitimu wa  Chekechea  shuleni hapo
Mkuu  wa shule   hiyo  na  watumishi  wengine  wakijitambulisha na  kupewa   zawadi na mkurugenzi  wao
Mkurugenzi mtendaji  wa  Southern Highlands Mafinga Bi  Mary  Mungai  akitoa historia  ya  shule  hiyo
Tunatangaza nafasi za masomo kuanzia darasa la kwanza hadi la tatu wanaotokea kiswahili medium schools na la tano pia wakati ,Darasa la 4 na 6 wanaotoka English medium. 
Kwa la nne na sita wale wanaotoka English medium schools. 
 Fomu za kujiunga zinapatikana shuleni na kutakuwa na interviews tarehe 13 / 12/2014 maeneo uafuatayo. Shuleni Southern Highlands   Mafinga, Oyster Bay Primary school, Dar es salaam, chuo cha Nursing Ilembula na Misufini primary school, Songea ama  kuwasiliana na  uongozi  wa  shule kwa simu  hii 0756749151 au 0754651966 Pia  alisema  sekondari form one wanazo  nafasi na  jina la sekondari; Mufindi Highlands School