Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

August 31, 2014

ROSE JOHN MAYEMBA NI MPIGANAJI MWENYE NDOTO KUPELEKA NGUVU ZAKE BAVICHA TAIFA

 Rose John Mayemba
..........................................
 JINA la Rose John Mayemba  ( 25) si  jina  geni katika harakati  za  chama  cha  Demokrasia  (CHADEMA)  mkoa  wa  Iringa na mikoa ya  nyanda za  juu  kusini 

TWPG WATAKA KATIBA MPYA ITAMBUE MASUALA YA JINSIA

Na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma.
UMOJA wa Wabunge Wanawake Tanzania (TWPG) kwa kushirikiana na Mtandao wa Wanawake na Katiba wamezungumzia juu ya umuhimu wa uwepo wa masuala ya jinsia katika Katiba Mpya na masuala muhimu ya jinsia ya kuzingatiwa katika katiba.
 

August 30, 2014

CRISTIANO AMTAABIRIA MAFANIKIO DI MARIA UNITED
MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo, amemtabiria mafanikio mchezaji mwenzake wa zamani Angel Di Maria katika klabu yake mpya ya Manchester United.

ASKARI WA UMOJA WA MATAIFA WASHAMBULIWA


Serikali ya Philippines inasema kuwa askari wake kama 70 katika kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini Syria, wameshambuliwa na wapiganaji.

SEND OFF YA MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI IRINGA NA MWALIMU WA CHUO KIKUU CHA IRINGA TULLA TWEVE -LIVE

Bibi  Harusi  mtarajiwa  Tulla  Tweve  akipunga  mkono  kusalimia waalikwa  katika   Send Off  hiyo

NI WAKATI WA JAPAN KUHAMIA AFRIKA – WAZIRI MKUUWAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema umefika wakati wa Japan kuhamia barani Afrika na na kuwekeza kwa nguvu hasa kwenye ukanda wa Afrika Mashariki.

WATAKIWA KUZAA WATOTO KWA MPANGO NA SIYO BAHATI.


Watanzania wametakiwa kuzaa watoto kwa kwa kupanga na siyo kwa bahati mbaya kama wenge wao wanavyosema  ikiwa ni pamoja na kuondokana na dhana kwamba kila mtoto anazaliwa na Bahati yake.

Bodi ya ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) yatembelea Eneo la Mradi wa Ujenzi wa Bwawa la Maji Kidunda

Meneja Usimamizi, Uendeshaji na Mazingira toka Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) Bi.Modesta Mushi akiwaonesha wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) ramani ya maeneo yatakayoguswa na Ujenzi wa Mradi wa Bwawa la Kidunda lenye ujazo wa Mita milioni 190, wakati wa Ziara ya Bodi hiyo katika eneo la Mradi Mkoani Morogoro.

RAIS KIKWETE AHITIMISHA ZIARA YA MKOA WA MOROGORO, AFANYA MAJUMUISHO NA WATENDAJI

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Mbunge wa Morogoro kusini ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa huo Mh Innocent Kalogeris  alipowasili katika ukumbi wa shule ya msingi Gairo ya kwenye kikao cha majumuisho na watendaji wa mkoa huo baada ya kuhitimisha ziara yake ya mkoa wa Morogoro

BOKO HARAM WATEKA KANISA
Kundi la kigaidi la Boko Haram nchini Nigeria  limeshambulia na kuteka  kanisa la katoliki nchini humo. 

Kwa mujibu wa vyombo vya habari  tukio hilo limetokea katika mji wa Madagali, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo ambapo inaelezwa kuwa, wanachama wa Boko Haram, baada ya kuvamia kanisa hilo wanaendelea kulidhibiti hadi sasa.

 Jason Obasuyi, mmoja wa makasisi wa mji huo amenukuliwa akisema kuwa, hali ya Wakristo wa mji wa Madagali ni mbaya sana. Aidha ameitaka serikali ya Abuja kuchukua hatua za haraka kurejesha usalama katika mji huo. 

Katika siku za hivi karibuni, wanachama wa kundi hilo la kigaidii lenye uelewa potofu wa mafundisho ya dini Tukufu ya Kiislamu, wameelekeza mashambulizi yao katika maeneo ya kaskazini mashariki mwa Nigeria, sambamba na kuidhibiti miji mingi ya maeneo hayo na kutangaza utawala wao. 

Hivi karibuni wanamgambo wa kundi hilo walitangaza kuanzisha kile walichokitaja kuwa eti ni utawala wa Khilafa huko kaskazini mashariki mwa mji wa Gwoza. 

Abubakar Shekau kiongozi wa kundi la Boko Haram alisema katika mkanda wa video kwamba, ameanzishai utawala wa khilafa katika mji wa Gwoza baada ya kuuteka mji huo mapema mwezi huu.

RAIS KIKWETE ATEMBELEA SOKO LA NAFAKA LA KIMATAIFA LA KIBAIGWA, DODOMA


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitembelea soko la nafaka la kimataifa la Kibaigwa mkoani Dodoma katika siku ya kwanza ya ziara yake mkoani humo Agosti 28, 2014 , 
 
ambapo alijionea shehena kubwa sana ya mahindi iliyoletwa kutoka mashambani na kusafirishwa kila pembe ya nchi. Mwaka huu, kama ilivyokuwa mwaka jana,
 

UINGEREZA YANYEMELEWA NA UGAIDI

Serikali ya Uingereza inasema kuwa matukio yanayoendelea  nchini Iraq na Syria yameongeza tishio la kufanyika kwa mashambulizi ya kigaidi nchini Uingereza.

AFRIKA INACHANGIA ASILIMIA 3 TU YA HEWA CHAFU DUNIANI - WAZIRI MKUU


WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema tatizo la mabadilko ya tabianchi ni kubwa sana na kama hazitachukuliwa hatua stahiki Dunia itaisha.

August 29, 2014

WATU KUMI WAMEFARIKI DUNIA NA MAJERUHI SABA KATIKA AJALI MBAYA

Hivi ndivyo ambavyo Daladala hiyo ilivyojibamiza muda mchache uliopita 

MASHINDANO YA POOL MKOA YA YAZINDULIWAMganga Mfawidhi wa hosptali ya wilaya ya Iringa Dk. Mbaraka Mgangachuma akipanda mti uliotolewa na chama cha pool mkoa wa Iringa walipokwenda kutoa msaada wa kiti cha kubebea wagonjwa na kupanda miti katika hospitali hiyo.

PINDA AFUNGUA MKUTANO WA MAWAZIRI WA MAZINGIRA
Waziri  Mkuu, Mizengo Pinda akitia saini kitabu cha maombolezo ya kifocha Waziri Mkuu wa zamani wa Ireland, Albert Reynolds kwenye ubalozi wa Ireland jijini Dar es salaam August 28, 2014. kulia ni Balozi wa nchi hiyo nchini, Fionnuala Gilsenan. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Matukio katika picha Bunge Maalum la Katiba leo 29 Agosti, 2014Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samia Suluhu Hassan (aliyebeba mkoba) akiwasili Bungeni kuendelea na majukumu ya Bunge Maalum la Katiba. Aliyemtangulia mbele ni Mkuu wa Idara wa shughuli za Bunge John Joel.

ZITTO KABWE AOMBWA KUWA MGENI RASMI KATIKA JUBILEI YA MIAKA 25 YA POMERINI SEKONDARI


Mkuu  wa  shule ya  Sekondari Pomerin Bw  Shadrack Nyaulingo

WAZIRI MKUU ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI IRELAND                                                    
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

 WAZIRI MKUU ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI IRELAND
* Asaini kitabu cha maombolezo ya Waziri Mkuu wa zamani

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ametumua salamu za rambirambi kwa Serikali ya Ireland kufuatia kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani wa nchi hiyo, Bw. Albert Reynolds.

August 28, 2014

BIOLANDS YAKABIDHI MSAADA WA AMBULANCE NISSAN PATROL KWA HALMASHAURI YA WILAYA YA KYELA.


Jukwaa ambapo sherehe ya Makabidhiano ilifanyika

Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta avitaka Vyombo vya Habari kuandika habari bila kupotosha Umma.


Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta akiongea na waandishi wa Habari huku akiwaasa kuacha chuki katika masuala yanayohusu mchakato wa Katiba.

Vijana wapewa changamoto ya kutumia uzazi wa mpango


Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Sabasaba Bw.Ibrahim Mwita akizungumza na Vijana wa kikundi cha Bank Club wakati wakati wa Jamvi la Vijana ni program ambayo inaendeshwa na UMATI kupitia Kituo cha Vijana YAM kutoka Manispaa ya Temeke, Jamvi hilo la vijana limebeba kauli mbiu ya “Kijana ana haki ya juu ya uzazi wa mpango?”Kulia ni Afisa Vijana wa UMATI Bibi. Upendo Daud.

Baadhi ya shule: Walimu, Wanafunzi na mazingira yao ya kufunza na kujifunza

Hali halisi. Pichani Darasa la awali katika shule ya msingi Sima B katika halmashauri ya mji wa Bariadi mkoa wa Simiyu likiendelea.

RAIS KIKWETE KATIKA SHEREHE ZA UZINDUZI WA PROGRAMU YA UIMARISHAJI WA MIPAKA YA KIMATAIFA MKOANI KAGERA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi alipowasili
eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare  kwa upande wa Burundi wakati wa sherehe za  uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014.

August 27, 2014

Viongozi na Wasanii wa Vyama vya Mashirikisho ya Sanaa wasisitiza kuhusu ujio wa Ujumbe wao Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma.


Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanamuziki Tanzania (TAMUNET) Bw. John Kitime (kushoto) akiwahutubia waandishi wa Habari pamoja na Wasanii waliohudhuria mkutano uliofanyika mjini Dodoma 27 Agosti, 2014. Kulia ni Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania Bw. Simon Mwakifwamba.

Serikali yasisitiza matumizi ya ya vyeti halisi wakati wa uombaji wa kazi Secretariati ya Ajira. Naibu Katibu Kitengo cha Udhibiti na Ubora toka Ofisi ya Rais, Sekretariat ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw.Humphrey Mniachi akiongea na waandishi wa Habari (Hawapo Pichani)Jinsi wanavyoshirikiana na Vyombo vingine serikalini katika Mchakato wa Ajira,wakati wa Mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Ofisi Hiyo Bi. Riziki Abraham. Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano toka Ofisi ya Rais, Sekretariat ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bi. Riziki Abraham akieleza kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mambo ya kuzingatia kabla ya kuomba kazi nchini kwa waombaji waliopotelea na vyeti, kuibiwa vyeti au kubadilisha majina,wakati wa Mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.Kulia ni Naibu Katibu Kitengo cha Udhibiti na Ubora toka Ofisi hiyo Bw.Humphrey Mniachi. Baadhi ya waandishi wa habari wakiwasikiliza wawasilishaji toka Ofisi ya Rais, Sekretariat ya Ajira katika Utumishi wa Umma leo Jijini Dar es Salaam. (Picha na Hassan Silayo) Na Georgina Misama Serikali imewataka waombaji kazi waliobadilisha majina, waliosoma nje ya Nchi, kupoteza, kuibiwa, kuharibikiwa au kuunguliwa na vyeti kufuata taratibu pindi wanapoomba kazi secretariati ya ajira. Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Ofisi ya Rais, Sekretariat ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bi. Riziki Abraham wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam. Riziki alisema kuwa kumekuwa na baadhi ya malalamiko toka kwa waombaji wa kazi kuwa secretariati ya Ajira imekuwa na upedeleo kwa kutowaita au kuwazuia kufanya usaili waombaji wasiokuwa na nyaraka halisi. Riziki alifafanua kuwa pindi waombaji wanapokabiliwa na hali hiyo hawana budi kutoa tarifaa katika mamlaka husika ili taratibu za kupata vyeti vingine zifanyike na taarifa zao kutumwa Secretariati ya Ajira kwa wakati. Akizitaja Mamlaka hizo Riziki alisema ni Polisi, Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), Elimu ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Tume ya Vikuu (TCU), na Baraza la Usimamizi wa Elimu ya Vyuo vya Ufundi (NACTE). Aidha, Riziki aliongeza kuwa kwa waombaji wenye majina tofauti kwenye vyeti wanapaswa kwenda mahakamani na kula kiapo kwa kamishna wa viapo au kwa wakili ili waweze kupata (Deedpal) au (Affidavity) kwa mujibu wa sheria na kwakufanya hivyo itasaidia kuthibitisha uhalali wa tofauti ya majina na kutambulika kisheria. Sekretarieti ya Ajira inapenda kuwafahamisha wadau wake, hususani waombaji kazi Serikalini kwamba haipokei barua ya utambulisho kutoka polisi inayohusu kupoteza, kuungua, kuibiwa, utofauti wa majina kati ya cheti kimoja na kingine kutokana na baadhi yao kuzitumia vibaya.

 
Naibu Katibu Kitengo cha Udhibiti na Ubora toka Ofisi ya Rais, Sekretariat ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw.Humphrey Mniachi akiongea na waandishi wa Habari (Hawapo Pichani)Jinsi wanavyoshirikiana na Vyombo vingine serikalini katika Mchakato wa Ajira,wakati wa Mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Ofisi Hiyo Bi. Riziki Abraham. 

Mtanzania DABO ametajwa kuwania tuzo za reggae za kimataifa na muziki wa dunia 2014 (IRAWMA)

10349153_841207622565532_7288991937464718532_n
Unaweza kuwa humfahamu kwa vile hana kelele nyingi....TUONYESHE UZALENDO KWA KUMPIGIA KURA SASA

MAELFU YA WANANCHI WAMLAKI RAIS KIKWETE GAIRO, KATIKA ZIARA YAKE YA MKOA WA MOROGORO

Rais Jakaya Kikwete akilakiwa na maelfu ya wananchi alipowasili kwenye uwanja wa mkutano wa mji wa Gairo mkoani Morogoro  kuhutubia mkutano wa hadhara Agosti 26, 2014

Umoja wa Machifu Tanzania (UMT) wawasilisha mapendekezo yao kuhusiana na Rasimu ya Katiba Mpya.Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samia Suluhu akiwaeleza jambo Wawakilishi wa Umoja wa Machifu Tanzania (UMT) kuhusu mapendekezo yao waliyoyawasilisha kwake kwaajili ya Katiba Mpya jana 26 Agosti, 2014.

August 26, 2014

MBUNGE KABATI ASEMA KATIBA MPYA IVIONDOE VITI MAALUMU VYA UBUNGE


Ritta Kabati alipokuwa kitoa mtazamo wake kuhusu viti maalumu vya ubunge
MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa, Ritta Kabati (CCM) amesema moja ya mambo anayounga mkono katika mchakato wa Katiba Mpya ni kufutwa kwa viti maalumu vya ubunge.

Akizungumza hivikaribuni nje ya jengo la CCM Mkoa wa Iringa, Kabati alisema Viti Maalumu vinafaida zake katika mchakato wa maendeleo lakini vinawadhalilisha sana wanawake.

“Siku hizi wabunge wanawake wa viti maalumu tunaitwa wabunge wa vitanda maalumu, huu ni udhalilishaji kwasababu wengi wanahisi upatikanaje wake una mahusiano yasiofaa,” alisema.

Alisema utaratibu unaotumiwa na nchi kama Uganda na Rwanda kupata wawakilishi wanawake katika mabunge yao ndio unaopaswa kutumiwa na Tanzania na kama ikishindikana basi wanawake nao wapewe nafasi sawa na wanaume ya kugombea moja kwa moja kwenye majimbo ya Uchaguzi.

“Tumetembelea Uganda na Rwanda, kule hawaiti viti maalumu vya wanawake, wanaita viti vya wilaya vinavyoshindanisha wanawake wa vyama mbalimbali katika wilaya hizo,” alisema.

Katika kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwakani, Kabati alisema endapo viti maalumu vitafutwa ataamua wapi atupe karata yake kati ya jimbo la Iringa Mjini au Kilolo.

“Kilolo ni kwetu na Iringa Mjini ni kwetu, kwahiyo kama Katiba Mpya itaondoa viti maalumu basi nitaamua wapi niende kati ya majimbo hayo,” alisema.

Mifuko ya Pensheni yawapiga msasa watumishi wapya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo

Muwasilishaji Toka Mfuko wa Pensheni wa NSSF Bw. Feruzi Mtika akiongea na waajiriwa wapya wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kuhusu aina ya Mafao wanayotoa iwapo watajiunga na Mfuko huo, wakati wa Semina iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

Ofisi ya Bunge yatoa ufafanuzi kuhusu malipo ya posho za Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba.

Mkurugenzi wa Habari na Itifaki, Bw. Jossey Mwakasyuka (kushoto) akitoa ufafanuzi mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na malipo ya posho za Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba leo katika ukumbi wa mikutano ofisi ya Bunge mjini Dodoma.

WAZAZI WAASWA KUWASOMESHA WATOTO WA KIKE

Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Iringa(ccm)Lita Kabati akizungumza na wanawake viongozi wa chama hicho hawapo pichani.


 baadhi ya wanawake walihudhuria mafunzo ya kuwajengea uwezo yaliyofanyika katika ukumbi mdogo wa ccm mkoani Iringa. (Picha na Denis Mlowe)

MAMEYA NA WAKURUGENZI WA TANZANIA WATEMBELEA NYUMBA ZILIZOJENGWA KWA MBAO FINLAND

Badhi ya nyumba za ghorofa zilizojengwa kutumia mbao katika jiji la LAHTI nchini Finland ambazo zilitembelewa na madiwani wa majiji sita ya Tanzania waliokuwa katika ziara ya mafunzo nchini humo iliyoratibiwa na taasisi ya Uongozi ya Tanzania.
Finland ni miongoni mwa nchi zenye maeneo makubwa ya misitu ya kupandwa dunaini, zaidi ya asilimia 80 ya eneo la nchi hiyo ni misitu na wenyewe wanasema nyumba zinazojengwa kwa kutumia mbao zina gharama nafuu kuliko kujenga kwa matofali au mawe.
Mkurugenzi wa jiji la LAHTI, Kari Porra akitoa maelezo kuhusu ujenzi wa nyumba hizo za mbao kwa mratibu wa ziara hiyo Godfrey Nyamrunda kutoka taasisi ya Uongozi ya Tanzania, nyuma yao ni Meya wa jiji la Dar Esa Salaam Dk Didas Masaburi

 
 
  Viongozi kutoka majiji sita ya Tanzania wakiwa kando kando ya ziwa Maji ambako mkondo wa maji machafu kutoka majumbani huingia ziwani baada ya kuchujwa, viongozi hawa kutoka kushoto ni Stanslaus Mabula ambaye ni Meya wa jiji la Mwanza, Athanas Kapunga ambae ni meya wa jiji la Mbeya, Mussa Zungiza,mkurugenzi mtendaji wa jiji la Mbeya na Philoteus Mbogoro ambae ni mratibu wa mtandao wa majiji Tanzania TACIN

na fredy mgunda

MO AZINDUA JARIDA LA IRIS EXECUTIVE NA KUSEMA UTAJIRI HAUJI "KIRAHISI RAHISI"

DSC_0281
Mgeni rasmi Ofisa Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP Mh. Mohammed Dewji (Mb) ambao ndio wadhamini wakuu wa sherehe za uzinduzi wa jarida la IRIS Executive (katikati), Ofisa Mtendaji Mkuu wa IRIS Executive Development Centre, Phylisiah Mcheni (kulia) na Makamu wa Rais wa MeTL GROUP, Bw. Vipul Kakad wakiwa meza kuu kwenye hafla fupi ya uzinduzi rasmi wa jarida IRS Executive ambalo tolea la jipya ukurasa wa mbele limepambwa na picha ya Mh. Mohammed Dewji "MO". (Picha na Zainul Mzige wa MOblog)

WANAHABARI MKOANI MBEYA WATAKIWA KUVITANGAZA VIVUTIO VYA MKOANI HAPO

Safari hiyo ambayo moja kwa moja ilianzia Mkoa wa Mbeya Wilaya ya Rungwe-Tukuyu kwenda kujionea vivutio hivyo mbalimbali kikiwepo cha kwanza kabisa ambacho ni Kijungu eneo ambalo ni la kipekee na lenye historia ya aina yake.

Hivi ndivyo safari ilivyokuwa Fuatilia hapa kwa makini.

WAKONGWE WA REAL MADRID WAKWEA MLIMA KILIMANJARO

  1. Wakongwe wa Klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania wakipiga picha za kikundi cha ngoma kilichokuwa kikiwatumbuiza mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro kabla ya kuelekea Mlima Kilimanjaro

BODABODA IRINGA WAMEGUKA, MCHUNGAJI MSIGWA KUCHANGIA CHAMA KIPYA SH MILIONI 3 NA BODABODA 10

Mchungaji Msigwa akisisitiza jambo alipokuwa akizungumza na madereva wa bodaboda wanaotaka kuanzisha chama kipya

August 25, 2014

BODABODA IRINGA WAWALIZA CHADEMA WAZIDI KUDHIHIRISHA KWAMBA WAO NI CCM DAMU


madereva bodaboda wa mjini Iringa wakiingia uwanjani

WAZEE WA KIMILA WA WILAYA YA IRINGA WAMSAFISHIA MWIGULU NCHEMBA NJIA YA KUELEKEA IKULU

Mwigulu Nchemba akipokea silaha ya mapambano kutoka kwa wazee wa Kimila wa wilaya ya Iringa

NCHEMBA AMUAPISHA SALIM ASAS KUWA KAMANDA WA UVCCM MKOA WA IRINGA, SHEREHE ZAPAMBWA NA WASANII LUKUKI


Naibu Katibu Mkuu CCM Tanzania Bara, Mwigulu Nchemba akimuapisha Salim Asas kuwa Kamanda wa UVCCM Mkoa wa Iringa, Salim Asas jana
Alipokuwa akimvalisha gwanda la ukamanda

Shule zaidi ya 30 zilizochaguliwa ni kutokana na mahitaji makubwa waliyonayo tukisaidiana na Wizara ya Elimu Tanzania. Na huu si mwisho wa zoezi hili, bali mwendelezo wa huduma za kijamii ambazo Airtel inaendelea kuzitoa ikitambua changamoto mbali mbali zinazoikabili sekta ya elimu Tanzania


Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa mradi wa “Airtel Shule Yetu” kwa mwaka 2014/15, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Mradi huu wa vitabu umeweza kufikia shule zaidi ya 1,000 toka ulipoanza miaka kumi iliyopita. Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (katikati), na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya.

PMO PHOTOS- PINDA AONGOZA HARAMBEE YA MKAPA FELLOWS


MAKANISA SINGIDA YAONYA MATUSI NA UBAGUZI BUNGENI

DSC00479
Askofu wa kanisa la Evanglist Assembels of God Tanzania (E.A.G.T) Singida mjini, John Mafwimbo akizungumza kwenye mkutano wa Injili uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Ukombozi mjini Singida.Pamoja na mambo mengi, askofu Mafwimbo amewasihi wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, kufanya mambo waliyotumwa na Watanzania.