Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

June 30, 2014


SITA WAJITOKEZA KUWANIA NAFASI ILIYOACHWA WAZI NA MAHANJI YA KATIBU WA CHAMA CHA MPIRA WA MIGUU MKOA WA IRINGA

Dk Ngala
Elliud Mvella
WATU sita wamejitokeza kujaza nafasi wazi ya Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Iringa (IRFA) iliyoachwa na Elliud Mvella ambaye hivi karibuni aliajiriwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kushughulikia masuala yanayohusu wanachama wa shirikisho hilo.

Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Septemba 8, mwaka huu kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kamati ya uchaguzi huo.

Walioonesha nia mpaka hii leo ni pamoja na mwanamichezo kijana Omary Majaliwa ambaye ni kiongozi wa klabu ya African Wanderers ya mjini Iringa na Abou Siria ambaye ni mdau maarufu wa mchezo huo mkoani hapa. Katika Uchaguzi uliopita Siria alitupa karata yake akitaka achaguliwe kushika nafasi hiyo lakini aliangushwa na katibu aliyeondoka madarakani.

Mwingine ni Dk Alli Ngala wa hospitali ya mkoa wa Iringa ambaye kwa muda mrefu amekuwa kiongozi wa mpira akiratibu shughuli mbalimbali za klabu ya Lipuli inayoshiriki ligi daraja la kwanza.

Yumo pia Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Manispaa ya Iringa, Ramadhani Mahano; mbali na nafasi hiyo Mahano pia ni mjumbe wa mkutano mkuu wa TFF na Mwenyekiti wa Chama cha Waamuzi Mkoa wa Iringa.

Mwingine ni Pascal Bella ambaye mbali na kazi yake ya ualimu wa mchezo huo amewahi kuwa kiongozi wa mpira wa klabu ya Lipuli ya mjini Iringa.

Katika kinyang’anyiro hicho yupo pia mwamuzi wa soka David Lugenge huku wadau wengine wakimtaja Stanford Mwakasala kwamba anaweza kuwa kiongozi mzuri kama atawania nafasi hiyo.Kwasasa Mwakasala ni Makamu Mwenyekiti wa IRFA.

Kamati ya uchaguzi ilitarajia kutangaza tarehe ya kuchukua fomu na kuanza kwa kampeni za uchaguzi huo hii leo.

No comments:

Post a Comment


Breaking newss mwanafunzi wa Ruco aliyechomwa moto afariki dunia

Mwanafunzi (LEMA) aliyejeruhiwa kwa moto
Mwanafunzi ambaye amefahamika kwa Daniel LEMA Alikua akisoma mwaka wa 4 kozi ya sheria katika chuo kikuu kishiriki cha Mt.Augustino Tawi la Iringa (Ruaha University College-RUCO) ambae alichomwa moto wiki iliyopita kwa kuhisiwa mwizi amefariki leo saa 8 mchana

Mwanachuo huyo alilazwa ktk hospitali ya Rufaa ya MKOA wa Iringa kwa matibabu zaidi na mwili wake kuagwa kesho kuanzia majira ya saa moja asubuhi kabla ya kuanza safari kwenda mkoani kilimanjaro kwa mazishi yatakayofanyika siku ya jumatano wiki hii. Hapa chini ni habari iliyoripotiwa awali na mtandao huu

MBUNGE MGIMWA AWAHAKIKISHIA UMEME MGAMA

Mbunge wa  jimbo la Kalenga  Godfrey Mgimwa wa nne  kulia akikagua nguzo za umeme ambazo zimeanza kushushwa kwa ajili ya mradi wa umeme vijijini kama alivyoahidi  wakati wa kampeni  zake ni takribani miezi miwili  sasa utekelezaji umeanza 
Hizi ni nguzo za umeme ambazo zimeshushwa kijiji cha Mgama kwa ajili ya mradi wa umeme 
Mbunge  wa jimbo la kalenga akizungumza na wananchi wa Mgama baada ya kutembelea kijiji hicho na kujionea utekelezaji wa ilani ya CCM na ahadi yake ya kuwaahidi umeme wa uhakika  wananchi hao 

BREAKING NEWssss CHADEMA KATAVI YASAMBARATIKA YOTE UONGOZI WAKE WOTE WAHAMIA ACT

Displaying IMG_20140630_133252.jpg
HII  NI  OFISI  YA  CHAMA  CHA  CHADEMA MKOA  WA  MPANDA IKIWA  WAZI  UKU  WANACHAMA  WAKE  NA  VIONGOZI  WA  MKOA  WAKIKIHAMA  CHAMA  HICHO NA PEMBENI  NI  OFISI  MPAYA  YA  CHAMA  KIPYA  CHA ACT MKOA  WA KATAVI
Displaying IMG_20140630_125556.jpg
Displaying IMG_20140630_134001.jpgAliyekuwa   katibu wa jimbo la mpanda  mjini kupitia  chama  cha  chadema  akitoa  tamko wakiwa  na  wajumbe wenzake wamekihama  Chadema na kujiunga na chama kipya ya ACT leo habari kamili inakujia pia  wamo viongozi wa mkoa  huo wa katavi Displaying IMG_20140630_130333.jpg
ALIOKUWA  VIONGOZI  WA  MKOA  NA WILAYA  WA  CHAMA  CHA  CHADEMA WAKIWA  PICHA  YA  PAMOJA  MARA  BAADA  KUTANGAZA  RASMI  KUONDOKA  KATIKA  CHAMA  HICHO(picha na A. Mbata)
Displaying IMG_20140630_132847.jpg
katibu  wa  sasa  aliebaki  madarakanai  chama  cha chadema  bwana  Mangweshi akifafanua  jambo  juu  ya  kuondoka  kwa  viongozi  hao  ambao  anadai  ni  wasaliti  wanaotumiwa  na  chama  cha  mapinduzi kwa  kuanzisha  chama kipya cha ACT chini katibu wa mbunge Kativa Displaying IMG_20140630_125547.jpg
viongozi  wa  chama  cha  demokrasia  na  maendeleo  chadema  mkoa wa  katavi  hatimae  wamejiondoa  rasmi  katika  chama  hicho  na  kwenda  chama  cha  ACT  Allince for  change  and  Transparency  ambacho  kinakuja  kwa  kasi  kubwa  hasa  mikoa  ya  ukanda  wa  ziwa  Tanganyika.

Akizungumza  na  waandishi  wa  habari wa  mtandao  huu  Joseph  Mona  ambae alikuwa  katibu  wa  chama  hicho  mpanda mjini alisema  kuwa  kumekuwa  na sintofahamu  ya  muda  mrefu  ndani  ya  chama  hicho  hatua mbayo  imewafanya  wao  kujiengua  richa  ya  baadhi  ya  viongozi  wao  kusimamishwa  uongozi  akiwa aliekuwa  mwenyekiti  wa  chama mkoa  Mzee  John  Malaki 

Ata hivyo Mona    amesema chanzo  cha  malumbano  ndani  ya  chama  hicho  kimetokana  na  baadhi  ya  viongozi  wa  kitaifa kutowajali  wanachama  na  uongozi uliokuwa  madarakani  uku  wakiwatuhumu baadhi  ya  viongozi na  mbunge  wa  chama  hicho  jimbo  la  mpanda  Said Amour Arfi kuwa  walitumiwa na ccm  kuacha  nafasi  wazi  ya  jimbo  la mlele na  kumuachia  kupita  bila  kupingwa mh waziri  mkuu  mizengo  Pinda  maarufu  kama mtoto  wa mkulima uku wakidai  mbunge  wa  chama  hicho  hausiki  kwa  namna  yoyote juu  ya suala hilo.

viongozi  hao  waliotoka madarakani wamekituhumu  chama  hicho  kutotoa  fedha za  ruzuku  kwa  wakati  ama  kutotoa  kabisa  na  kukifanya  chama  hicho  kutojiendesha chenyewe 

Alisema  pia  kumekuwa  na  matumizi  mabaya ya  fedha  ndani  ya  chama  hicho  uku  kikao  cha  mawasiliano  ndani  ya  mkoa  kikifumbia  macho  hali  hiyo

Mona  amewataja  wanachama  waliofukuzwa  hapo  na  chama  hicho  ambao  sasa  wamejiengua  kabisa  kuwa  ni  pamoja  na  Cnraradi Sinkala(mwenyekiti  kata  ya  makanyagio) IDEPHONCE  KITUNDU (mwenyekiti  kata ya ilembo)YASINI LUDANGA (MWENYEKITI  KATA  YA nsemlwa, medadi  khalfan  katibu  kata  nsemlwa,Mohamed kazyoba mjumbe  kamati  tendaji jimbo,SEFU  JUMA mwenyekiti  wa  BAVICHA jimbo la  mpanda  mjini,Clispin Salya mjumbe  kamati  tendaji  jimbo,Ana Paulo mwenyekiti  wa  BAWACHA mkoa,Rukia Juma Mhasibu wilaya mpanda,

wengine  ni  Charles  mwenyekiti  kata  ya  Misungumilo,Beatrice  Baraga mwenyekiti  BAWACHA jimbo,GODI  KAPUFI mwenezi  jimbo mjini mpanda,joseph  mona  katibu  jimbo  mjini,Sefu Said Spia mwenyekiti  jimbo  la  mpanda  na  aliekiuwa  mwenyekiti  wa  mkoa  Jonh  Malaki ambao  wote hawa  walifukuzwa ndani  ya  chama  kwasababu  ya  kuhoji  na  kufatilia  matumizi  ya  pesa  za uendeshaji  wa  chama  hicho

ata  hivyo  wanadai  walifukuzwa  kupitia kikao cha Mashauriano  ya mkoa na  kusema  hakikuwa  kikao  halali  chenye  mamlaka  ya kufukuza  na  kusema  kikao  chenye  mamlaka  ya  kufukuza  kinidhamu ni  kikao  cha  baraza  la uongozi  mkoa 

akijibu  hoja  hizo  kaimu  mwenyekiti wa  mkoa  ambae  pia  ni  mwenyekiti  wa  baraza  la  vijana  sasa  Mangweshi  anadai  viongozi  hao  walifukuzwa  kwa  sababu  ya  kuwa  mamalukli  wa  chama  cha  mapinduzi na  kusema  chadema itaendelea  na  kwamba  imeanza  na  mungu,ipo  na  mungu  na  itamaliza  na  Mungu  uku  akishangazwa  kuanzishwa  kwa  chama  hicho  kwa  kuwa  watu  wanataka  maendeleo  na  sio n vyama.

MANISPAA YA IRINGA ILIYOONGOZA KWA USAFI KITAIFA ,SASA YAJISAHAU KINYESI CHATAPAKAA MITAANI

Mbali ya  Manispaa ya  Iringa  kuongoza  kitaifa kwa usafi mwaka  2014  ila imeonyesha kujisahau  baada uchafu huu wa kinyesi  kutapakaa eneo la Miyombini kando ya barabara  kuu ya Iringa- Dodoma karibu na msikiti wa ijumaa

RAIS MSTAAFU BENJAMINI MKAPA KUTUA IRINGA LEO KWA AJILI YA KUSHEREKEA MIAKA 25 YA UASKOFU NA MIAKA 40 YA UPADRE YA ASKOFU TARCISIUS NGALELALEKUMTWA

RAIS MSTAAFU  BENJAMINI MKAPA  KUTUA IRINGA LEO KWA  AJILI YA KUSHEREKEA  MIAKA 25 YA UASKOFU NA MIAKA 40  YA UPADRE YA ASKOFU TARCISIUS NGALELALEKUMTWA SHEREHE ITAKAYOFANYIKA KESHO MAKAO MAKUU YA ASKOFU KIHESA 

June 29, 2014

PICHA ZA WIKI ,MBUNGE GODFREY MGIMWA ALIVYOTUMIA USAFIRI WA BAISKELI KUTEMBELEA WAPIGA KURA WAKE KALENGA

Mbunge  wa  jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa akiwa katika usafiri wa Baiskeli akienda kutembelea wapiga kura wake kata ya Ifunda eneo la Kivalali wiki iliyopita ,kandop ni wananchi  na viongozi wa kata hiyo
Wananchi wa Kivalali kata ya Ifunda  wakijiandaa kupeana mikono na mbunge Mgimwa mwemnye baiskeli
Mbunge Mgimwa akisalimiana na wanakikundi cha burudani Kivalali kata ya Ifunda

WANACHUO WA SUA NA UTALII WA NDANI..


 kaimu  mkurugenzi  wa TANPA Dr Ecekiel Dembe wa pili  kulia akiwa na viongozi mbali mbali wa  serikali na TANAPA  ,pamoja na wakufunzi wa mafunzi ya waongoza  watalii katika hifadhi za Taifa

Mkuu wa UNDP duniani akitembelea askari wa Ruaha
Na Msafiri Mgumba wa matukiodaima.co.tz

UTALII ni kitendo cha mtu au kundi la watu kusafiri kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine yenye kivutio/vivutio kwa lengo la kujifunza, kutembea na kujionea hali halisi ya mahali hapo kwa muda fulani. Vivitio hivyo vinaweza kuwa; sehemu za kihistoria, fukwe, hifadhi za wanyama pori n.k

Kuna aina takribani mbili kuu za utalii, utalii wa ndani na utalii wa nje. Utalii wa ndani ni ule ambao mtu au watu kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine yenye kivutio ndani ya nchi husika kwa kipindi fulani, inawezekana ikawa ni kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine au wilaya moja kwenda nyingine.

Mfano, wanachuo toka Chuo Kikuu cha kilimo cha Sokoine  (SUA) kwenda Hifadhi ya Taifa ya wanyama pori Udzungwa, Kilombero. Na utalii wa nje, ni ule unaohusisha mtu/watu kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine yenye vivutio vya kitalii, Kama wazungu kutoka Amerika na Ulaya wanapokuja Tanzania kuona vivutio tulivyonavyo.


Utalii wa ndani ndio unaopewa kipau mbele katika kuuendeleza, kutunza na kunufaika zaidi na vivutio vyetu. Jamii ya kitanzania ime kuwa na dhana kuwa utalii na vivutio vilivyopo nchini ni kwa ajili ya wageni wanaotoka nje ya nchi pekee.

HOTUBA YA MHESHIMIWA MIZENGO P. PINDA (MB), WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

 PG4A9702 HOTUBA YA MHESHIMIWA MIZENGO P. PINDA (MB), WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WAKATI WA KUHITIMISHA MKUTANO WA KUMI NA TANO WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA TAREHE 28 JUNI, 2014
UTANGULIZI
a)    Masuala ya Jumla
Mheshimiwa Spika,
1.    Naomba nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu mwenye wingi wa Rehema kwa kutupatia uzima na afya hadi kufikia siku ya leo. Tumekuwepo hapa kwa takriban miezi miwili ambapo tumeweza kupokea na kujadili Taarifa za Mapitio ya Utekelezaji wa Kazi za Serikali kwa mwaka 2013/2014 na Mwelekeo kwa mwaka 2014/2015 kwa Wizara mbalimbali na hatimaye kupitisha Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2014/2015.

AIRTEL YAZINDUA SIMU MPYA AINA YA IPHONE 5S


Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Bi. Beatrice Singano Mallya (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati Kampuni ya Airtel kwa kushirikiana na Apple ilipofanya uzinduzi wa simu mpya ya iPhone 5s pamoja na ofa kabambe kwa wateja wa Airtel, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.
 
 Ofa hiyo itawawezesha wateja wa Airtel kupata sms 5000, muda wa maongezi dakika 1500 pamoja na kifurushi cha internet cha 3GB. Wanaoshuhudia ni Meneja Masoko wa Airtel, Prisca Tembo (kulia) na wafanyakazi wa kitengo cha huduma kwa wateja wa kampuni ya Apple.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Bi. Beatrice Singano Mallya (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati Kampuni ya Airtel kwa kushirikiana na Apple ilipofanya uzinduzi wa simu mpya ya iPhone 5s pamoja na ofa kabambe kwa wateja wa Airtel, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.

BRAZIL YATINGA ROBO FAINALI YAIGAGADUA CHILE

Wild emotion: Brazil's players celebrate their dramatic 3-2 penalty shootout against Chile in the last 16
 Furaha bab kubwa!: Wachezaji wa Brazil wakishangilia ushindi wao wa penati 3-2 dhidi ya Chile na kufanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali.

TAMWA kutoa elimu kupambana na ulevi kupindukia

Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Valerie Msoka akisisitiza jambo katika mkutano na wahariri wa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam leo. Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Valerie Msoka akisisitiza jambo katika mkutano na wahariri wa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam leoMkutano wa wahariri wa vyombo vya habari na TAMWA ukiendelea. Mkutano wa wahariri wa vyombo vya habari na TAMWA ukiendelea

KANISA LA YESU KRISTO LA WATAKATIFU WA SIKU YA MWISHO WAKARIBISHA WATU MBALIMBALI KATIKA KANISA

Kiongozi wa shule ya jumapili wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa siku za mwisho,Dr, Emanuel Kandusi akiwapatia maelezo mbalimbali kwa watu waliotembelea kanisa hilo wakati wa siku ya wazi kwa ajili ya watu mbalimbali kuangalia shughuli zinazofanywa na kanisa hilo

June 28, 2014

MAUREEN GODFREY KUTOKA NJOMBE AWA REDDS MISS KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI 2014 , IRINGA ,NJOMBE NA RUVUMA KWENDA TAIFA

 Mrembo  Maureen Godfrey katikati akiwa na washindi  wa nafasi ya  pili Martha John na mshindi wa tatu Naba Magambo katika  picha ya pamoja

Risala ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akitoa salamu za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa   Wananchi  wa Zanzibar na Tanzania kwa Ujumla,pia aliwatakia mfungo mwema  wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa kufanya ibada mbali mbali.[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.].

RAIS KIKWETE AKUTANA NA RAIS MPYA WA MISRI MHE ABDEL FATTAH Al-SISI

a3 a4Rais Jakaya Mrisho Kikwete akutana na kufanya mazungumzo na Rais mpya wa Misri Mhe Abdel Fattah Al-Sisi mjini Malabo, Equatorial Guinea, pembeni ya Mkutano wa kawaida wa Umoja wa Afrika Juni 26, 2014 
PICHA NA IKULU

MTEMVU: WAPINZANI HATA WAKIUNGANA VIPI CCM ITAWABWAGA, ASHANGAA KUAMBIWA ANA MASLAHI BINAFSI KUWATETEA MAMALISHE

Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu akifungua Kikao cha Baraza Kuu la Jumuia ya Wazazi ya CCM, wilaya ya Temeke, leo katika ukumbi wa Manispaa ya wilaya hiyo jijini Dar es Salaam.

SIO MUDA MUAFA WA KUMUITA COUTINHO `MUUZA MADAFU` BRAZIL

Afisa habari wa Yanga sc, Baraka Kizuguto (kushoto) akiwa na Coutinho (kulia) baada ya kuwasili  nchini  jana akitokea kwao nchini Brazil.