Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

May 31, 2014

SERIKALI YATOA ZAIDI YA SHILINGI 6.7 BILIONI KUJENGA HOSPITALI YA RUFAA SINGIDA

DSC_0473
Katibu Mkuu wa CCM Taifa Abdulrahamani Kinana akiongozwa na Mkuu wa Moa wa Singida Dk, Parseko Kone, Katibu Tawala Lianna Hassan na viongozi wengine wa Mkoa wa Singida kukagua hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida, wakati Kinana alipokuwa Mkoani Singida kwa ziara ya kikazi ya siku saba.(Picha na Zainul Mzige wa modewjiblog).
Na Nathaniel Limu, Singida
MKUU wa Mkoa wa Singida,Dk.Parseko Vicent Kone amesema serikali imetoa zaidi ya shilingi 6.7 bilioni kwa ajili ya kugharamia ujenzi wa hospitali ya rufaa ya mkoani hapa iliyoko kijiji cha Madewa nje kidogo ya Singida mjini.
Dk.Kone amesema hospitali hiyo itakapokamilika,itahudumia wagonjwa kutoka mikoa yote ya kanda ya kati.
Mkuu huyo alitoa rai hiyo wakati akitoa akitoa taarifa yake kwa katibu mkuu CCM taifa,Abrahamani Kinana aliyetembelea hospitali hiyo hivi karibuni.
Amesema mkoa umetegewa eneo la ekari 283 kwa ajili ya uendelezaji wa mradi wa hospitali hiyo, ambayo itakuwa ya mfano hapa nchini.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk Dorothy Gwajima amesema lengo la mradi huo ni kuimarisha huduma za afya mkoani pamoja na mikoa jirani.
DSC_0429
Katibu Mkuu wa CCM akiweka saini kwenye kitabu cha hospitali ya Rufaa huku Naibu Katibu Mkuu wake Mwigulu Nchemba na mkuu wa Mkoa wa Singida Kone wakishuhudia.
Dk.Gwajima amesema mradi huo utakapomalizika,utakuwa na majengo 29 yatakayotumika kutoa huduma mbali mbali.
Mganga huyo mkuu,amesema changamoto inayowakabili ni pamoja na uhaba wa watumishi,nyumba za kuishi watumishi na ufinyu mdogo wa bajeti ya dawa kutoka bohari kuu ya madawa (MSD).
Kwa upande wake Kinana,alitumia fursa hiyo kumpongeza Dk.Kone kwa utendaji kazi wake ambao umesaidia kujengwa kwa hospitali hiyo.
DSC_0446
Mganga mkuu wa hospitali ya Mkoa wa Singida (RMO) Bi. Doroth Bwajima akisoma taarifa ya ujenzi wa hospitali hiyo.
Amesema baada ya mradi huo kukamilika mkoa wa Singida utaondokana na matatizo ya huduma za afya.
"Ili kumuunga mkono Dk.Kone kwa hili jambo nzuri la ujenzi wa hospitali ya rufaa ambayo itasaidia Watanzania wengi kupata huduma ya afya kwa kiwango kizuri,nitahakikisha nina muunganisha na baadhi ya marafiki zangu wa ndani na nje ya nchi ili waweze kusaidia kumalizika kwa ujenzi wa hospaitali hii inayovutia",amesema Kinana.
DSC_0453
Mganga mfwawidhi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida, Dkt Joseph Malunda, akiwaonesha michoro ya hospitali hiyo viongozi walioambatana na Kinana.
DSC_0463
Viongozi mbalimbali wa mkoa huo wakimsikiliza Dkt Malunda.
DSC_0481
Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida Pendael Maasai akisisitiza jambo kwa Kinana.
DSC_0499
Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida Pendael Maasai akimwonyesha Katibu Mkuu kinana vifaa mbalimbali vilivyopo kwenye hospitali hiyo ya rufaa.
DSC_0506
Mbunge MO akiangalia mojawapo ya vifaa vya hospitali ya rufaa ya singida.
DSC_0496
Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mohammed Dewji akisalimiana na Daktari bingwa wa magonjwa ya kina mama wa mkoa wa Singida Dkt, Seleman Mutani wakati wa ukaguzi wa hospitali hiyo.
DSC_0522
Katibu Mkuu wa CCM Taifa akiongozana na mkuu wa Mkoa Kone, Mbunge wa jimbo la Singida Mjini Mh. Mohammed Dewji, wasaidizi wa Mbunge Duda Mugheny na David Mkufya wakimwongoza Kinana kutoka nje mara baada ya kukagua hospitali ya Rufaa ya Mkoa huo.(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog).

FAMILIA YA JAMES MWAISUMBE IRINGA NA MBEYA ,INAMKUMBUKA MAMA YAO MPENDWA GRINA JAMES MWAISUMBE NI MWAKA MMOJA SASA

Familia ya James Mwaisumbe ya Iringa na Mbeya inapenda  kuwashukuru  wote  walioshiriki mazishi ya mama yao mpendwa na pia  wale  wote  wanaoendelea  kuelekeza maombi yao kwa famili  hii.

Ikumbukwe ni Tarehe 1/6/2013 ndipo mpendwa  wetu Grina James Mwaisumbe alipotutoka hapa duniani na  sasa  kesho  jumapili anafunga mwaka mmoja toka alipotutoka ,hivyo familia inaendelea kumwombea na kumkumbuka  kutokana  na ucheshi wake na ukarim na upendo mkubwa alioonyesha enzi  za uwepo  wake hapa duniani.

Grina anaendelea  kukumbukwa na mume  wake mpendwa mchungaji James Mwaisumbe ,watoto Frank ,Mpeli ,Tukuswiga,Neema, Anna na  wajukuu zako wote pamoja na ukoo wote wa akina Mwaisumbe na Msika popote  walipo.

Tunaendelea  kuamini  kuwa tulikupenda  sana na ulitupenda  zaidi ila Mungu muweza wa  yote amekupenda  zaidi yetu  hivyo hatuna budi kuendelea kukuombea kwa Mungu .

Zaidi tutaendelea kuenzi yale  yote  uliyoonyesha  enzi za uhai  wake  ikiwa ni pamoja na kuishi vema na  watu .

Bwana alitoa na Bwana ametwaha  jina lake na lihimidiwe  milele  Yote
Amina

PIGO TENA BONGO MUVI: GEORGE TYSON AFARIKI DUNIAGeorge Tyson enzi za uhai wake.
George Tyson akimlisha keki Yvonney Chery ‘Monalisa’ wakati mtoto wao Sonia alipopata kipaimara.
NI pigo tena kwa tasnia ya Bongo Muvi, mwongozi filamu Bongo na aliyekuwa mume wa staa wa filamu za Kibongo, Yvonny Cherry 'Monalisa', George Tyson amefariki dunia baada ya kupata ajali mbaya ya gari maeneo ya Gairo, Morogoro akitokea mkoani Dodoma. Tyson alikuwa ameambatana na watu kadhaa katika safari hiyo ambao wanadaiwa kuumia vibaya. Mwili wa marehemu Tyson pamoja na majeruhi wa ajali hiyo wamepelekwa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro. Tyson enzi za penzi lake na Monalisa walifanikiwa kupata mtoto aitwaye Sonia.
Marehemu Tyson akiwa na Monalisa (kushoto), kulia ni Tyson na mwanae Sonia.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Monalisa amemlilia Tyson kwa kuweka picha hiyo juu na kuandika maneno yafuatayo:

Monalisa akimnywesha kinywaji Tyson wakati wa kipaimara cha Sonia.
MUNGU AIPUMZISHE ROHO YA MPENDWA WETU MAHALI PEMA PEPONI. AMEN!

Mwanamitindo Rodney afariki dunia, kuzikwa Jumamosi Mei 31

rodney 2
Na Andrew Chale
MBUNIFU na mwanamitindo (model) Rodrick Charles maarufu kwa jina la ‘Rodney de lativo’ amefariki dunia jana (Mei 30) baada ya kuugua kwa muda alipokuwa amelazwa Hospitali ya Jeshi, Lugalo.
Akizungumza na  Mtandao huu mapema leo kwa njia ya simu,  Rafiki wa karibu wa familia ya marehemu, David Msangi  alisema marehemu alipatwa na umauti alipokuwa akiendelea na matibabu katika Hospitali ya Lugalo, alipokuwa amelazwa na msiba huo upo nyumbani kwa marehemu Tabata Bonyokwa.
“Tumempoteza mtu muhimu sana ambaye alikuwa na mawazo mengi ya kufikia mafanikio yake. Tutaendelea kumkumbuka.”  Alisema Msangi ambaye pia alikuwa mshahuri wa karibu wa marehemu.
Msangi alisema kwa mujibu wa familia ya marehemu, anatarajiwa kuzikwa  Jumamosi Mei 31 huko huko kwenye makaburi ya Tabata Segerea.
Wakati wa uhai wake, marehemu alifanya kazi kwenye majukwaa mbalimbali na wabunifu na wanamitindo wakubwa wakiwemo wabunifu Ally Remtullah, Mustapha Hassanali, Asia Idarous. Wanamitindo Rio Poul, Martin Kadinda, Justine, Faustine Simon na wengine wengi.
Rodney mpaka anakutwa na umauti, alikuwa mshauri na model  wa kampuni ya  Crisswelly African Fashion.
Marehemu alizaliwa Mei 26, 1994.  Elimu yake alisomea Magoze Sekondari  na kuhitimu 2011 na kuingia moja kwa moja kwenye  fani ya uwanamitindo na kuendelea hadi alipokutwa na umauti.
Aidha, kwa jamaa wa karibu na wabunifu na wanamitindo  watakaotaka maelezo ya kufika kwa marehemu wanaweza kuwasiliana na David Msangi kwa namba hii 0652901684
..Rest In Peace Rodney. I remember you forever.
……………………………………………………………………………….
TAARIFA ZA FAMILIA NI KWAMBA MSIBA UPO BONYOKWA PANDA GARI YA TABATA SEGEREA SHUKA MWISHO WA GARI KISHA PANDA GARI ZA BONYOKWA SHUKA MWISHO NDIPO MSIBA ULIPO WA NDUGU YETU MPENDWA RODNEY TUTA MUHIFADHI KESHO SIKU YA JUMAMOSI SAA 9 ALASIRI UKIWA NI MMOJA WAPO WA MDAU WA TANZANIA FASHION NA Crisswelly African International Fashion, MODEL AU DESIGNER NIVEMA KUJITOKEZA NA KUSHIRIKI KUMSINDIKIZA SAFARI YA MWISHO YA MPENDWA WETU #RODNEY PIA WAWEZA KUTUMA MCHANGO WAKO KWA MAMA Asia Khamsin KWA TIGOPESA NO 0713263363 MUNGU AKUBARIKI TAFADHALI SHARE UJUMBE HUU KWA MARAFIKI ZAKO UTABARIKIWA AMEN!!!!!!!!!!!!!!
KWA MAELEZO WASILIANA NA #CRISSWELLY NO 0714802527

Matokeo ya uchaguzi wa Rais Malawi ni Prof Peter Mutharika Rais mteule Malawi


Peter Muthirika anayeongoza chama cha DPP ndiye rais mteule nchini Malawi
.............................................................................
Hatimaye Malawi imepata Rais mpya baada ya mivutano ya kisheria kwa wiki nzima. 

Mwandishi wa BBC Baruan Muhuza amesema kutoka mjini Blantyre kuwa Profesa Peter Mutharika ameshinda uchaguzi huo kwa kupata asilimia 36.4 ya kura zote akifuatiwa na Dr Lazarus Chakwera mwenye asilimia 27.8 huku Rais anayemaliza muda wake Dr Joyce Banda akishika nafasi ya tatu kwa asilimia 20.2 na Atupele Muluzi amekuwa wa nne na asilimia 13.7
Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Jaji Mackson Mbendera amesema uchaguzi huo ulikumbwa na changamoto nyingi lakini mwishowe nchi ni lazima ipate kiongozi wake na kuwaomba wananchi kuwa na utulivu .

Kesi Mahakamani
Awali Jaji Kenyata Nyirenda wa mahakama kuu mjini humo jana usiku alitoa uamuzi kuwa hawezi kuvunja sheria kwa kuruhusu tume iongeze muda wa kuhesabu upya kura kwenye maeneo yenye utata.

Na kwamba sheria inaitaka tume kutangaza matokeo ndani ya siku nane na si vinginevyo.

Uchaguzi wa Malawi ulifanyika Mei 20 nchini kote lakini siku moja tu baada ya kupiga kura, malalamiko yakiambatana na mapingamizi ya kisheria yakatawala kwenye mahakama kuu za Lilongwe na Blantyre.

May 30, 2014

MATOKEO YA UCHAGUZI MALAWI KUTANGAZWA HIVI PUNDE ,POLISI WATUMIA MABOMU KUTULIVU VURUGU MMOJA AFA

Wakati  tume ya uchanguzi nchini Malawi inataraji kutangaza matokeo ya uchaguzi mkuu wa Rais nchini humo hivi punde ,zimezuka vurugu kubwa kati ya makundi yanayomuunga mkono Rais Joyce Banda na wapinzani wake.

Imeelezwa  kuwa katika  vurugu  hizo zilizozuka mchana wa leo polisi  wamelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya  wananchi hao na kumna taarifa  ya mtu mmoja  kupoteza maisha kutokana na vurugu  hizo.

Duru  za kisiasa  kutoka nchini Malawi zinadai kuwa  hali ya amani kwa  sasa nchini  humu si swari kutokana na vurugu  hizo ambapo watu kadhaa wanaripotiwa  kujeruhiwa  vibaya na kukimbizwa Hospital kwa matibabu  zaidi

MWONEKANO WA KISASA WA CLUB V.I.P ITAKAYOFUNGULIWA LEO MJINI IRINGA

Hii ni kaunta ya  kisasa zaidi ya zote mjini Iringa
Sakafu  ya Club V.I.P Iringa
Vyoo vya kisasa ndani ya Club V.I.P Iringa
Sehemu ya kucheza muziki ni sehemu ambayo imeweka vioo na taa zinazowaka ardhini
Msosi upo wa ukweli
Chumba maalum kwa  wavutaji wa sigari hiki hapa,Karibuni leo Club V.I.P mshuhudie starehe ya ukweli sehemu nzuri na tulivu ,Club V.I.P inapatikana  barabara ya kuelekea Ikulu ipo jirani na lango la chuo  cha RUCO

Mchawi mtanzania jela miaka 3 Kenya


Vifaa walivyopatikana navyo washukiwa walipokamatwa na polisi
Mchawi kutoka Tanzania amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu nchini Kenya kwa kumlaghai mwanamke mfanyabiashara mkenya na kumuibia shilingi milioni tisa.

Mchawi huyo alimhadaa mama huyo kuwa kwa kupitia njia za kichawi angeweza kuzifanya pesa hizo kuwa maradufu yaani milioni 18.
Bwana Amos Chipeta pia ataongezwa kifungo cha miezi tatu kwa kupatikana na vifaa vinavyoumiwa kufanya uchawi kama vile chupa, visu na ngozi ya Paka. 

Kwa mujibu wa mtandao wa Daily Nation, Chipeta alihukumiwa pamoja na mwenzake bwana Peter Christopher aliyepatikana na hirizi zinazotumika kufanyia uchawi.

Bwana Chipeta alimlaghai Bi Catherine Njeri hela zake tarehe tofauti tofauti kati ya mwezi wa Agosti na Decemba 2012 baada ya mwanamke huyo kuwaendea na kumwomba wazifanye pesa hizo ziwe maradufu
Walijitetea kwa kusema kuwa mwanamke huyo aliwaendea ili wampe nguvu za kichawi aweze kuwashinda wapinzani wake wa kisiasa

Maafisa wa polisi walipata hirizi hizo na vifaa walivyotumia kwa uchawi mwezi Februari 1, 2014 katika nyumba ya kukodisha iliyo kando ya barabara ya Juja viungani mwa mji mkuu Nairobi.

Hakimu aliyesikiliza kesi hiyo alisema kuwa wanaume hao waliona mwanamke huyo kuwa mjinga na basi kumnafiki kwa urahisi na kuwa hawana majuto au toba.

India:Ghadhabu kwa ubakaji wa wasichana


Eneo ambako miili ya wasichana waliobakwa ilipatikana ikining'inia kwenye mti
Watu nchini India wameghadhabishwa na uzembe wa polisi katika jimbo la Uttar Pradesh kufuatia tukio la wasichana wawili kubakwa na kuuawa na mili yao kuwekwa juu ya mti.

Babake mmoja wa wasichana hao amesema kuwa polisi walimkejeli alipokwenda kwao kutaka usaidizi wa kumtafuta msichana wake aliyetoweka kabla ya kupatikana akining'inia kwenye mti na mwenzake.
Alisema kuwa wakati polisi walipogundua kuwa anatoka katika tabaka linalotazamiwa kuwa la hadhi ya chini, walikataa kumsaidia kutafuta msichana wake.

Watu watatu akiwemo polisi mmoja wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo.
Familia za waathiriwa zimelalamika kwamba polisi walikataa kuwasaidia kutafuta wasichana hao waliokuwa na umri wa miaka 14 na 16 mtawalia na ambao pia wanatoka familia moja.

"nilipokwenda kwa polisi, kitu cha kwanza nilipoulizwa ni tabaka langu , nilipowaambia wakaanza kunitukana, '' alisema baba huyo wa mmoja wa wasichana hao waliobakwa kisha kuuawa.

Polisi walisema kuwa wanaume hao walikamatwa kwa kuwabaka kisha kuwaua wasichana hao.
Polisi mmoja pia alizuiliwa kwa kushirikiana na washukiwa na pia kwa kukosa kuchukua hatua. Bado mshukiwa mmoja anasakwa na polisi.

KIWANJA KINAUZWA ENEO LA MIYOMBONI

Kiwanja  hiki  kipo jirani na Hospital ya Aga khan mjini Iringa eneo la jirani na Uhindini katikati ya mji  wa Iringa skinauzwa Tsh milioni 75 maelewano  yapo 
wasiliana nasi  kwa simu 0754 026 299

JUKWAA LA KATIBA LAZUNGUMZIA UCHAGUZI WA MALAWI KUWA NI FUNZO LA KIDEMOKRASIA

Mwenyekiti wa jukwaa la katiba Deus Kibamba akizungumza na  wanahabari  leo juu ya uchaguzi wa Malawi

KATIBU MKUU KIONGOZI AKUTANA NA NCHI WASHIRIKA WA MAENDELEO JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akibadilishana mawazo na mabalozi na wawakilishi wa nchi washirika wa maendeleo kabla ya  mkutano aliowaandalia leo Mei 30, 2014 katika hoteli ya Hyatt Kilimanjaro hotel jijini Dar es salaam kuzungumzia  michango katika Kapu la Afya (Health Basket Fund) pamoja na mpango wa serikali wa kuiingiza sekta ya afya katika  kutekeleza Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN)
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (wa saba kutoka kushoto) akiwa katika mazungumzo  na mabalozi na wawakilishi wan chi washirika wa maendeleo katika mkutano aliowaandalia leo Mei 30, 2014 katika hoteli ya Hyatt Kilimanjaro hotel jijini Dar es salaam kuzungumzia  michango katika Kapu la Afya (Health Basket Fund) pamoja na mpango wa serikali wa kuiingiza sekta ya afya katika  kutekeleza  Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN)

PICHA NA IKULU

SERIKALI YA KIJIJI CHA MTANDIKA KILOLO YAWAPIGA MARUFUKU WANANCHI KUINGIA MSITU WA HIFADHI KUCHUMA UYOGA,YAPONGEZA MMANDEA

Mwananchi akiwa ameshika Uyoga ambao ameupata porini
Wananchi wa Mtandika Kilolo  wakiwa katika mdahalo wa MMADEA

Meneja mradi wa hifadhi misitu kwa maendeleo kutoka shirika la MMADEA Felista Kasuga akitoa elimu ya uhifadhi kwa wananchi wa kijiji cha Mtandika
 Wananchi wa Mtandika  wakiwa katika mdahalo huo 
.................................................................................
UONGOZI  wa  serikali ya  kijiji  cha Mtandika wilaya ya Kilolo mkoani Iringa  umepiga marufuku wananchi  kuingia  katika misitu ya  hifadhi kutafuta uyoga ama kuni bila ya  kuwa na kibali kutoka ofisi ya  kijiji

Mbali ya kupiga marufuku hiyo pia umepongeza jitihada zinazofanywa na  shirika lisilo la  kiserikali la The Mazombe Mahenge Development Association (MMADEA)  katika utoaji wa elimu ya uhifadhi wa mazingira  kwa wananchi.

Mwenyekiti wa serikali  ya kijiji  hicho cha Mtandika Bw Mrisho Ngecha aliyasema hayo leo wakati   wa mdahalo  wa pamoja kati ya MMADEA na wananchi  wa  kijiji  hicho .

Alisema  kuwa mbali ya  kuwa  wilaya  ya Kilolo inaongoza  kwa  kuhifadhi mazingira ila bado baadhi ya maeneo kumekuwepo na uharibifu mkubwa wa mazingira  kutokana na  wananchi  wake  kutokuwa na elimu ya kutosha juu ya uhifadhi wa mazingira .

Hivyo  kutokana na elimu  hiyo inayotolewa na  shirika   hilo kuna uwezekano mkubwa wa maeneo mbayo  wananchi  walikuwa  wakiharibu mazingira  kujenga utamaduni wa  kuhifadhi zaidi kutokana na elimu  hiyo.

Mwenyekiti huyo alisema  kuwa katika  kijiji  hicho  ipo misitu mitatu ambao imehifadhiwa kama misitu ya  kijiji na mwananchi anayehitaji  kuingia kwa shughuli yeyote ndani ya maeneo hayo yaliyohifadhiwa ni lazima afike  ofisi ya  kijiji kwa ajili ya kupewa kibali na bila  kufanya  hivyo sheria kali  huchukuliwa kwa mhusika pindi anapokamatwa .

" Utaratibu  wa  kijiji  katika kuhifadhi misitu na mazingira ni pamoja na kuweka  adhabu kali kwa  wananchi  wanaoharibu  mazingira na kuingia katika misitu iliyohifadhiwa  bila ya  kibali na tayari baadhi ya  watu  wameadhibiwa kwa  kuingia katika misitu ya  hifadhi  bila kibali cha serikali"

Wakati  wananchi  wa  kijiji  hicho  wakiitaka serikali ya kijiji kuweka matangazo yanayoelieweka katika maeneo hayo ya  hifadhi  za  misitu  ili kuepusha wananchi kupewa adhabu ya  kuingia maeneo hayo ambayo si  wananchi wote  wanayatambua kama ni maeneo ya  hifadhi alisema Rashid Ally.

Kuwa serikali ya  kijiji hicho  imekuwa  ikitangaza maeneo ya  hifadhi wakati maeneo hayo yanamilikiwa na  watu  hali ambayo mbele inaweza  kuleta migogoro mikubwa.

Akizungumza na wananachi hao meneja wa mradi  wa hifadhi misitu kwa maendeleo Bi Felista Kasuga  alisema  kuwa lengo la mradi hiyo unaotekelezwa na MMADEA ni kuona misitu  ndani ya maeneo ya mradi inahifadhiwa  vema ili  kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Bi Kasuga  alisema kuwa matumizi  endelevu ya misitu na utumiaji wa maliasili zilizopo katika misitu ni jukumu la kila mwananchi  kuona kuwa misitu hiyo inatunzwa na hata pale penye uhitaji wa miti ama maliasili zilizopo mstuni  kuona taratibu  za kuzivuna zinafuatwa .

ZITTO KABWE AFUNGUKA ATOA UFAFANUZI MZURI KUHUSU TANAPA NA NSSF

Nasikitika kwamba katika hali niliyonayo ya kumwuguza mama yangu naingizwa kwenye siasa za majitaka.

Kampuni ya LekaDutigite inamilikiwa na wasanii. Gombe Advisors ni kampuni isiyofanya faida (Company limited by guarantee) na haina maslahi yeyote ya kibiashara.

Wasanii wa Kigoma wamefanya kazi na TANAPA na NSSF, kazi ambazo zinajulikana na zipo.

Leo mpigie simu mfanyakazi yeyote wa NSSF utasikia kazi ya wasanii hao. Kwa namna yeyote ile hii ni ishara ya kukosa ubinaadam maana waliyoyasema wanajua sina faida yeyote ya kifedha Leo wala kesho kwa LekaDutigite na Gombe Advisors.

Kipindi ambacho mama yangu yupo mahututi, tena mjumbe wa kamati kuu ya chama chao, pole ninayopewa ndio hiyo.

Hakuna namna ya kukosa ubinaadamu zaidi ya hivi.

Zitto Zuberi Kabwe: Hata hivyo, ni vema CAG afanye ukaguzi haraka sana na Mimi binafsi nitawajibika iwapo itaonekana kwa namna yeyote ile nina maslahi ya kifedha katika LekaDutigite na gombe advisors.

By Zitto Kabwe

---------------------------

Maelezo zaidi kutoka kwa Zitto Kabwe

AJALI IRINGA ENEO LA ZEBRA ASUBUHI HII MAGARI MANNE YAGONGANA

Daladala  inayodaiwa  kusababisha ajali  hiyo kwa kuligonga  gali  hili mbele ambalo pia liligonga jingine mbele  na kufanya jumla ya magari manne kugongana eneo hilo la Zebra japo hakuna madhara kwa binadamu
Hili gari aina ya Taxi iliyogongwa na gari lililogongwa na daladala nalo kuligonga gari hilo mbele mali ya serikali
Askari  wa usalama barabarani  wakikagua ajali  hiyo
Haya ni magari manne  yaliyogongana leo  mjini Iringa
Wananchi wakishuhudia ajali hiyo

NYUMBA INAUZWA ENEO LA KIHODOMBI IRINGA BEI TSH MILIONI 13.1


Nyumba  hii  iliyopo  eneo la Kihondombi katika Manispaa ya  Iringa  inauzwa  kiasi cha Tsh  milioni 13.1 maelewano  yapo nyumba ina umeme  ,maji  yapo  mlangoni  bado  kuingizwa  ukubwa wa  eneo ni urefu mita 14 na upanda  mita 14 KWA  MAWASILIANO TUPIGIE NAMBA     0754 026 299

LADY JAYDEE, JULIANA KANYOMOZI AND JAMILA MBUGUA NAMED ORIFLAME BEAUTY AMBASSADORS

KK,HJ,JM,JD standing  
From left: Henrik Johannesson( Vice President of Oriflame Africa), Lady Jaydee, Jamila Mbugua(Kenyan Musician), Klas Kronaas (Managing Director Oriflame East Africa) posing for a photo after announcing them to endorse Oriflame beauty and cosmetic line in East Africa.

Swedish beauty company, Oriflame Cosmetics, has announced the appointment of three renowned Eastafrican celebrities as brand ambassadors. The three Lady Jaydee, Juliana Kanyomozi and Jamila Mbugua, will represent the Oriflame brand in Uganda, Tanzania and Kenya respectively.

The partnership is in line with the company’s growth strategy underlined by growing its East Africa sales force and expansion to other African markets. The strategy is anchored on four main pillars including network marketing, world class service, brands & products and people and culture.

Oriflame East Africa Managing Director, Mr. Klas Kronaas, expressed delight that the East African operation had brought on board authentic brand evangelists who are as passionate about the brand as the company is to nature inspired beauty products.

“Lady Jaydee , Juliana and Jamila have been named because their style and approach to beauty is the ideal representation for the Oriflame brand. They are strong and talented women who many people across East Africa readily identify with,” said Kronaas.

Oriflame East Africa Head of Marketing and Sales Support, Mr. Harry Njagi said the three brand ambassadors will feature in Oriflame’s Catalogue, and will also be engaged in selected brand events to represent the Oriflame brand throughout the year. The partnership will also extend to joint CSR activities with the celebrities.

“Our products - inspired by nature are very popular with women of all ages across East Africa, especially owing to the fact that we have the widest range in personal care and the signing of these three passionate women is expected to deepen our market access and increase our brand visibility,” said Mr. Njagi.

Lady Jaydee is one of the best known female artistes in East Africa and was among the first to sing R & B in Swahili. She has won over 6 Best Female Awards at the prestigious Tanzania Music Awards and many other Awards in the region including collaboration of the year 2011 (Nitafanya) with Kidum and also 2008 (Anita) with Matonya.

She has also recorded with a number of artists including Samba Mapangala (Congo), Chameleone (Uganda), Mad Ice (Uganda / Tanzania), and Mina Nawe (South Africa) amongst others. She is married to Times FM presenter Gardner Habbash.

Uganda’s Juliana is a well known musician, actress and entertainer who has, since 2009, graced East African TV screens as one of the Judges of Tusker Project Fame. She collaborated with Bobi Wine on songs such as: "Taata Wa Baana Yaani?" (Who is the Father of her Kids?) and "Maama Mbiire". She also worked with Sweet Kid on the track "Sirinaayo Mulala" (I don't have anyone else) and with Klear Kut on the song "All I Wanna Know".

Kenya’s Jamila Mbugua is a TV personality, who has worked for various TV stations in Kenya for over 10 years and currently runs a popular show on K24.

Oriflame, which celebrated its 5th anniversary last December, has designated the next 3 years as a period of rapid growth as the company consolidates its East African operations and plans to expand to other African markets.

May 29, 2014

WATATU WAFARIKI DUNIA IRINGA KTK MATUKIO TOFAUTI LIKIWEMO LA AJALI

Watu watatu wafariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa katika matukio tofauti tofauti mkoani Iringa likiwemo la abiria mmoja wa IT aliyejulikana kwa jina la Sandes Kazeze (22) mkazi wa Malawi kufariki dunia baada ya gari alilokuwa amepanda kuligonga loli.
 
Akizungumza na mtandao huu wa www.matukiodaima.com ofisini kwake Kamanda wa polisi mkoani Iringa ACP Ramadhani Mungi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea mnamo tarehe 28 mei majira ya saa 12 za Alfajiri huko katika Kijiji cha Iramba barabara kuu ya Iringa – Mbeya wilaya ya Mufindi.
 
Kamanda Mungi alisema marehemu alikuwa amepanda gari aina ya Toyota Hiace yenye namba za usajili IT 0116 mali ya Davious Timeson wa Malawi lililokuwa likiendeshwa na Madilisto Tambala (34) aliigonga gari aina ya scania lenye namba za usajili T 181 ARC likiwa na Trella namba T 972 AGR mali ya Mikoani Traders iliyoko Dar Es Salaam iliyokuwa ikiendeshwa na Edwin Komba (29) mkazi wa Dar Es Salaam na kusababisha kifo cha abiria mmoja na wengine wawili kujeruhiwa.
Kamanda aliwataja majeruhi hao ni Madilisto Tambala pamoja na Peter Malunda wote ni wakazi wa Malawi ambao kwa sasa wanapatiwa matibabu katika hospitali ya Ilembula na kusema chanzo cha tukio hilo ni mwendo kasi wa dereva.
 
Wakati huohuo, huko katika maeneo ya Mlima Chanagarawe barabara kuu ya Iringa – Mbeya wilayani Mufindi gari aina ya Mitsubishi Fuso yenye namba za usajili T 167 AVE mali ya Safina wa Makambako iliyokuwa ikiendeshwa na Jailet Kimbe (25) akitokea Dar es Salaam kuelekea 
 
Makambako aligongana na gari aina ya Scania lenye namba za usajili T 849 CHP lenye trella namba T 984 CNE mali ya Super star wa Dar es Salaam lililokuwa likiendeshwa na Hamad Mkubwa (47) na pia kuligonga gari jingine aina ya Scania lenye namba za usajili T 612 ASF lenye trella namba T 120 AFT mali ya Eawadhi kisha kuacha njia na kupinduka na kusababisha kifo cha tingo wa Mitsubishi Fuso aliyetambulika kwa jina la Noel Nyika (22) mkazi wa makambako.
 
Na katika tukio lingine, mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Simon Mlomo (80) mahabusu na mkazi wa Nyololo mwenye CC namba 20/2013 aliyekuwa anakabiliwa na tuhuma za mauaji amefariki dunia wakati akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya Mufindi mkoani Iringa.
 
Mbali na matukio hayo ya vifo, Kamanda alisema watu wasiofahamika waliiba gari aina ya Toyota Carina yenye namba za usajili T 794 AYN lenye rangi nyeupe na thamani ya shilingi 6,000,000/= ambayo ni mali ya Edward Lucas (43) mkazi wa Kihesa.
 
Tukio hilo lilitokea mnamo tarehe 28 mei na kusema gari hilo lilikutwa maeneo ya Mshindo likiwa limetelekezwa.
NA DIANA BISANGAO WA MATUKIO DAIMA.COM, IRINGA
 
 

COASTAL U-20 KUCHEZA MECHI YA KIRAFIKI NA VIVA DYNAMO JUMAPILI WILAYANI MKINGA

MABINGWA wa Kombe la Uhai ambalo hushirikisha wachezaji wanaotumikia vikosi vya pili kwenye timu zinazoshiriki ligi kuu soka Tanzania bara,Coastal Union U-20 Jumapili wiki  hii wanatarajiwa kufanya ziara ya kimichezo Tarafa ya Maramba wilayani Mkinga .

Timu hiyo itacheza mchezo mmoja wa kirafiki na Viva Dynamo ya Maramba lengo likiwa kujenga undugu na kuwapa burudani wapenzi wa soka wilaya pamoja na kuwapa fursa kuiona timu hiyo ikicheza kwenye viwanja vyao vya nyumbani.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa kwenye uwanja wa soka JKT Maramba unaomilikiwa na Jeshi la Kujenga Taifa wilayani humo ambapo msafara huo utaongozwa na mwenyekiti wa Klabu ya Coastal Union,Hemed Aurora wakiwemo viongozi wengine.

Akizungumza na waandishi wa habari ,Ofisa Habari wa timu ya Coastal Union,Oscar Assenga alisema ziara hiyo ni miongoni mwa mikakati ya timu hiyo kuzunguka wilaya zote za mkoa wa Tanga kwa ajili ya maandalizi  ya msimu mpya wa Ligi kuu pamoja na mashindano ya Rolling Stone ambayo hufanyika kila mwaka.