Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

April 30, 2014

TANESCO WAAMUA KUCHUKUA UAMUZI WA KUFUNGA NYAYA JUU YA MTI BAADA YA NGUZO KUVUNJIKA

 Nguzo hii ina zaidi ya Mwezi mmoja ikiwa ndani ya nyumba ya mtu na hatari zaidi kwa sababu imelalia katika miti mibichi
 Hivi ndivyo nguzo hiyo inavyo onekana kwa Jirani ikiwa imelalia miti
Hizi  ni waya zilizopita chini kabisa katika Geti la mtu na ndani ya miti.

 Nguzo ya umeme ya TANESCO ikiwa imekatika katika eneo la Jirani na Daraja la Mlalakuwa ambapo ipo mpaka sasa ikiwa ni zaidi ya mwezi ipo eneo hilo.
 Hii ndio Njia Mbadala waliyo iona TANESCO kutumia kwa kufunga nyaya hizo juu ya Miti baada ya kubadirisha nguzo iliyo haribika
Hizi ni nyaya za umeme ambazo zimepita Chini ,pia ni hatari kwa watembea kwa miguu
*****

Kutokana na mvua zilizonyesha hivi karibuni   jijini Dar es salaam ambapo mvua hizo zimesababisha uharibifu mkubwa wa mali na  miundo mbinu mbalimbali .

Uharibifu mkubwa na wahatari  ni katika nguzo za umeme zilizo vunjika  na baadhi ya nyaya zinazo pitisha umeme kushuka chini ambazo ni hatari kwa wananchi.

Katika eneo la Mlalakuwa  mbele kidogo baada ya kulivuka daraja ukiwa unaelekea kawe  pana nguzo tatu ambapo nguzo moja imevunjika  kabisa na nyingine mbili zimelegea  katika nguzo iliyo vunjika ni mali ya Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) liliweza kufika katika eneo hilo wakachukua hatua ya kufungua nyaya za ile nguzo iliyo katika na kuzifunga juu ya mti ulio pandwa pembeni  mti huo si mkavu ni mbichi.

Je shirika la umeme la Tanzania madhara ya umeme wananchi watayafahamu vipi wakati ninyi wenyewe wataalamu wa kazi hiyo mnatupotosha, pili sehemu mulipo fungia na nyaya zilipo legea ni sehemu watu wanapo ishi ,hivi huku nikuwajali wateja wenu ?

Tunaomba  muchukue hatua harakaiwezekanavyo ili kuepusha madhara yanayo weza kujitokeza hapo baadae  kwani ni hatari sana

Wafanyakazi 'Katiba na Sheria' waaswa kuchapa kazi

 Baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya Katiba na Sheria katika mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam leo (Jumatano, Aprili 30, 2014).

 Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) Mkoa wa Dar-es-salaam Bw. Hassan Kaumo akiongea na wafanyakazi wa Wizara ya Katiba na Sheria katika mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara hiyo jijini Dar es Salaam leo (Jumatano, Aprili 30, 2014). Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Fanuel Mbonde. (Picha na Martha Komba - Wizara ya Katiba na Sheria).

Na Martha Komba, Dar es Salaam
Watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria wametakiwa kufanya kazi kwa bidii ili kuongeza ufanisi katika utendaji wao.
 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Fanuel Mbonde amesema hayo katika mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara hiyo uliofanyika leo (Alhamisi April 30, 2014) jijini Dar-es-salaam.
 
“Uwajibikaji ni suala muhimu sana katika utumishi wa umma,” alisema katika mkutano huo wa siku moja uliofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo jijini Dar-es-salaam.
 
Aidha, Katibu Mkuu huyo aliwasihi watumishi wote wa Wizara yake kuungana na wafanyakazi wote nchini na duniani kushiriki katika sherehe za Siku ya Wafanyakazi zinazofanyika kesho (Alhamisi, Mei 1, 2014).
 
Awali akiongea katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) Mkoa wa Dar-es-salaam Bw. Hassan Kaumo aliwataka watumishi wa Wizara hiyo kutimiza wajibu wao katika sehemu zao za kazi.
 
“Tunapodai maslahi ni lazima pia tusisitize kutimiza wajibu. Wafikishieni salamu hizi wafanyakazi wote, wachape kazi ili watupe viongozi nguvu ya kudai maslahi bora,” alisema Kaumo katika mkutano huo uliohudhuriwa na viongozi na wawakilishi wa wafanyakazi kutoka Idara na Vitengo vyote vya Wizara hiyo.
  
Mkutano huo, pamoja na mambo mengine, ulijadili maslahi ya watumishi na kupitia na kuridhia Taarifa ya Mpango wa Bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka ujao wa fedha 2014/2015.

BILA UWEKEZAJI TUNAJIDANGANYA - WAZIRI MKUU

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema bila uwekezaji nchi haiwezi kusonga mbele na akawataka watendaji serikalini kubadili mtazamo wao kuhusiana na suala zima la uwekezaji.
Ametoa kauli hiyo jana usiku (Jumanne, Aprili 29, 2014) wakati akizungumza na wafanyabiashara na wajasiriamali mbalimbali wa hapa nchini kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa Taasisi ya Mkoba Private Equity Fund inayojishughulisha na utoaji mitaji kwa wajasiriamali wadogo na wa kati.

"Bila uwekezaji tunajidanganya... ni ukweli usiopingika kwamba uwekezaji mkubwa unatoka kwenye sekta binafsi, kwa hiyo watendaji wetu serikalini wanapaswa kubadili mtazamo wanaposhughulikia masuala ya sekta binafsi," alisema.

Alisema watendaji serikalini wanapaswa kubadili mitazamo yao hasa wanapokuwa wanawasiliana na watu wa sekta binafsi kwa sababu kwa mfanyabiashara yeyote wakati ni mali.

"Tanzania imejipanga kuelekea kuwa Taifa lenye uchumi wa kati, kama kweli tunataka kufika huko mapema ni lazima tuwachukulie wadau wa sekta kwa mtazamo wa tofauti. Siyo anakuja kutaka taarifa unaanza kumzungusha bila sababu, anataka kusajili kampuni unamwambia unajua mafaili hayaonekani wakati hakuna cha mafaili wala nini bali unatafuta mwanya wa kudai chochote," alisema.

Akizungumzia kuhusu utoaji mikopo kwa ajili ya mitaji ya kibiashara, Waziri Mkuu aliitaka Taasisi ya Mkoba Equity Fund ihakikishe inajenga kwanza uwezo wa wahusika ili waweze kuzalisha mali kama ilivyokusudiwa.

Akitoa mfano wake binafsi, Waziri Mkuu alisema wakati anaanza biashara ya ufugaji nyuki miaka mitatu iliyopita, hakuwahi kuandaa mchanganuo wowote (write-up) wala hakuwahi kuandaa mpango wa biashara (business plan). Matokeo yake, alikuwa anatoa tu fedha mfukoni na kununua vifaa kadri mahitaji yalivyokuwa yakijitokeza, jambo ambalo alisema si sahihi.

"Ninawasihi sana viongozi wa Mkoba Equity Fund wasitoe mikopo kwa watu wanaotaka kufanya biashara kama nilivyoanza mimi. Wekezeni kwanza kwa kuwajengea uwezo wajasiriamali watakaoomba fedha za mitaji kutoka kwenye taasisi hii," alisisitiza.

Akitoa ushauri kwa wajasiriamali wadogo waliotoa shuhuda zao kuhusu changamoto walizokabiliana nazo wakati wakianzisha biashara zao, Waziri Mkuu aliwataka wasirudi nyuma wala wasikate tamaa. "Fursa ni nyingi sana na mnaweza kufanya mambo mengi. Kitu cha msingi ni kuwa na nia thabiti (determination).

Wajasiriamali walitoa shuhuda zao ni Mkurugenzi wa kampuni ya Montage, Bi. Teddy Mapunda; Mkurugenzi wa kampuni ya Go-Financing, Bw. Geoffrey Ndossi, Mkurugenzi wa kampuni ya SIGA Ltd, Bw. Marwa Busigara na Mkurugenzi wa kampuni ya WIA, Bw. Eric Mwenda.

HALMASHAURI KUU YA CCM LUDEWA YAMPONGEZA MBUNGE FILIKUNJOMBE

 Mwenyekiti  wa CCM wilaya ya Ludewa Stanley Kolimba akifungua kikao cha Halmashauri kuu ya CCM wilaya  leo kutoka kulia ni mbunge wa jimbo la Ludewa  Deo Filikunjombe na mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa (MNEC) kutoka Ludewa Elizabeth Haule 
........................................................................................................................................
CHAMA  cha mapinduzi (CCM) wilaya ya  Ludewa  mkoani Njombe  kimempongeza mbunge wa  jimbo  hilo Deo Filikunjombe kwa  jitihada zake  mbali mbali za utekelezaji  wa ilani ya CCM katika jimbo hilo.

Pongezi  hizo  zimetolewa na mwenyekiti  wa CCM wilaya  hiyo Stanley Kolimba  wakati  akifungua  kikao  cha Halmashauri  kuu ya CCM  wilaya mjini Ludewa leo

Kolimba  alisema  kuwa mbunge utendaji kazi  wa mbunge huyo umeendelea  kuwa chachu ya  kimaendeleo  katika jimbo  hilo na  kuwafanya wananchi kuendelea kuwa na imani kubwa na CCM.

Alisema mbunge huyo amekuwa mfano wa  kuigwa katika kufanikisha utekelezaji  wa ilani ya CCM na  kudai  kuwa jitiihada kubwa zinazofanywa na Filikunjombe zitasaidia  kuwafanya  wananchi  kuendelea  kuwa na mapenzi zaidi na CCM.

"Kweli  mbunge  wetu  amekuwa ni mfano wa  kweli katika kufanikisha maendeleo ya jimbo letu na wilaya  na hata majirani wamekuwa  wakipongeza utendaji kazi  wake "

Katika  hatua  nyingine CCM  wilaya  ya  Ludewa  kimewapa pore wananchi wa kata ya Rupingu ambao wamepatwa na majanga  ya mali zao mbali mbali yakiwemo mazao kuharibiwa na mvua kubwa  zinazoendelea kunyesha katika maeneo  mbali mbali  hapa nchini.

"Mbali ya  mvua  zinazoendelea  kunyesha kusaidia  kutupa neema  ya mazao  yetu  ila wenzetu  wa Rupingu  wamepatwa na majanga  makubwa  kutokana na mvua  hizo hivyo tunawapa pore kwa majanga  haya yaliyowakuta."

Hata  hivyo  baadhi ya wajumbe  wa Halmashauri kuu ya  CCM Ludewa  walipongeza  jitihada  za  serikali ya  awamu ya nne  na jitihada za mbunge  wao katika  suala  zima la uboreshaji wa miundo mbinu katika  wilaya  hiyo ya Ludewa kutokana na kuwa na miundo  mbinu rafiki isiyosumbua sana ukilinganisha na maeneo mengine.

Pia  waliiomba serikali kwa  mwaka huu  kuangalia  uwezekano wa  kutenga  bajeti  kubwa  zaidi ya fedha kwa ajili ya ununuzi wa mahindi ya  wananchi wote  kutokana na kuwepo kwa dalili nzuri  zaidi ya wakulima katika  wilaya  hiyo  kupata mazao zaidi  ukilinganisha  na miaka iliyopita.

Kwani  walisema kutokana na jinsi ambavyo  wakulima wengi  walivyopata mazao na kulima  zaidi  upo  uwezekano  wa  wakulima  kukosa  soko la mazao  yao yote ama  wenye  fedha  ndio  watakaonufaika  zaidi na soko  hilo.

Kwa  upande  wake  mbunge Filikunjombe  aliipongeza  serikali ya Rais Jakaya  Kikwete kwa  kuendelea  kuboresha maisha ya  wana Ludewa kwa  kufungua milango  mbali mbali ya kimaendeleo ikiwa ni pamoja na kuanza  uboreshaji wa miundo mbinu ya  wilaya  hiyo.

Kwani  alisema  mbali ya kuanza  uboreshaji wa miundo mbinu  hiyo tayari  wilaya ya  Ludewa  kwa mara  ya kwanza  toka nchi ipate  uhuru  wake  mwaka 1961  kwa  kipindi  hiki ambacho amekuwa mbunge wa  jimbo  hilo tayari  wananchi  wa Ludewa  wameanza  kuona ujenzi wa barabara ya lami ukianza pamoja na  wananchi wa pembezoni ambao hawajafanikiwa kuwa na umeme  hivi sasa zoezi la kuwafikishia  umeme  limeanza.

AJALI YAUA MMOJA YAJERUHI 40 WILAYANI SUMBAWANGA

Na Elizabeth Ntambala
Sumbawanga
MTU mmoja amefariki dunia na wengine 40 kujeruhiwa baada ya ajali ya gari lililokuwa likitokea  katika kijiji cha Mkima Wilayani Sumbawanga kuacha njia na kupinduka na kutumbukia mtaroni.

Gari hilo aina ya Fuso lililokuwa limebeba  wachezaji wa mpira ambao walikuwa wakielekea  kijiji cha Mkima wakitokea Ilembo kwa ajili ya mechi ya kirafiki na kusababisha ajali baada ya kutumbukia mtaloni.

Kamanda wa polisi Mkoani Rukwa Jacob  Mwaruanda alisema mara baada ya gari hilo kupinduka lilisababisha kifo cha mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Hassan Enani(18) aliyekuwa kapanda juu ya bomba na kusababisha kifo chake.

Kamanda Mwaruanda aliwataja baadhi ya majeruhi waliotibiwa na kuondoka kuwa ni Edmundy Nkalawa,Henrk Kaulule,Revokatus Malambika,Philibeth Zumba,Omary Jeusha,Joel Raphael na Lukas Kang’nga.

Wengine ni Daudi Sabino,Novakatus malambika,Seris Kisanzo,Aman Shaban,Crispin Nkalawa na Menady Msumbachika  ambao wote ni wakazi wa Lembo na  walitibiwa na kuondoka katika Hospital ya Mkoa.

Jeshi la polisi  lisema kuwa mara baada ya ajali hiyo kutokea dererva huyo alitoroka na upelelezi wa awali unafanyika na mara atakapo kamatwa atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma inayiomkabili.
MWISHO

HALMASHAURI NA WADAU WA JIJI LA MWANZA WAANZA MAANDALIZI YA SHEREHE ZA KUADHIMISHA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA JUNI 16.


Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi inayoundwa na wadau wa watoto jijini Mwanza Bw. Godfrey Salumu akifafanua utaratibu mzima wa utendaji kazi wa kamati ndogo ndogo zilizoundwa kwa wajumbe (hawapo pichani) ili kuweza kufanikisha maadhimisho hayo.

Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya jiji la Mwanza Bi Eluminata Mwita akisikiliza jambo kwa makini toka kwa wajumbe (hawapo pichani). 

Mkurugenzi wa Shirika la Kutetea Haki za Wanawake na Wasichana, KIVULINI Bw Ramadhani Masele (kushoto) ambae pia ni mjumbe wa kamati ya ndogo ya Uratibu, Mipango na Fedha akiteta jambo na mjumbe mwenzake wakati wa kikao hicho.


Wajumbe wa Kikao cha kwanza cha maandalizi ya Sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika itakayofanyika Juni 16 chini ya kauli mbiu ya “Kuondoa Mila Zenye Kuleta Madhara kwa Watoto ni Jukumu Letu Sote”. 


Uongozi wa kamati ya maandalizi ya sherehe ya siku ya Mtoto wa Afrika wilaya ya Nyamagana, Mwanza. Kulia ni Bw Godfrey Salumu ambae ni Mwenyekiti wa kamati, Bw. Devis Mrope (katikati) ambae na Katibu, kushoto ni Katibu Msaidizi Bi. Francisca Michael.

HABARI NA PICHA NA HASSAN MROPE WA MATUKIODAIMA.COM, MWANZA


Halmashauri pamoja na wadau toka mashirika na taasisi za kutetea na kulinda haki za watoto jijini Mwanza wameanza rasmi vikao vya maandalizi ya kuadhimisha sherehe za siku ya mtoto wa Afrika inayoadhimishwa kila Mwaka Juni 16.
Kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri wa Jiji la Mwanza chini ya Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri hiyo Bi. Eluminatha Mwita wajumbe walikubaliana kuadhimisha siku hiyo katika Kata ya Buhongwa, kwa Wilaya ya Nyamagana.
Siku ya mtoto wa Afrika huadhimishwa kimataifa kote duniani kwa lengo la kutambua thamani, utu, na umuhimu wa mtoto duniani. Maadhimisho haya hufanywa kila juni 16 tangu ilipotangazwa kuwa siku rasmi mwaka 1991 na jumuiya ya umoja wa Afrika.
Akizungumza wakati wa kufungua kikao hicho Afisa Maendeleo Jamii wa Jiji la Mwanza Bi. Eluminatha Mwita alisema kuwa kauli Mbiu ya mwaka huu ni “Kuondoa Mila Zenye Kuleta Madhara kwa Watoto ni Jukumu Letu Sote” na kufafanua kuwa kauli hiyo inalenga kuwasisitiza wazazi na walezi kuacha mila potofu zenye kuleta madhara kwa watoto.
Bi Eluminatha alisema kuwa “Kauli mbiu hiyo ina lenga kuangalia mila zote kandamizi na potofu zinazotokana na jamii husika katika malezi ya mtoto na kusababisha madhara mbalimbali ikiwemo kuongezeka kwa watoto wa mitaani, kubakwa kwa watoto, kukosa elimu, afya na malezi bora pamoja na vifo kwa watoto hawa”.
Kikao hicho cha kwanza kiliweza kuchagua viongozi wa kamati hiyo ya maandalizi, mwenyekiti aliyechaguliwa ni Godfrey Salum huku katibu ni Devis Mrope na katibu msaidizi akichaguliwa Francisca Michael, baada ya kupata viongozi kamati nne ziliundwa na wajumbe, Kamati ya Uratibu, Mipango na Fedha, Kamati ya Usafiri na Ulinzi, Kamati ya Mapambo na Burudani pamoja na kamati ya Hotuba na Habari.