Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

March 31, 2014

WAJAWAZITO SHINYANGA WAJIFUNGUA KWA MWANGA WA TOCHI YA SIMU NA CHEMLI..!

Na william Bundala
Matukio daima kanda ya ziwa

Kituo  cha afya cha Ikonongo kilichopo kata ya Salawe  wilayani Shinyanga  kinakabiliwa na changamoto mbalimbali  ikiwemo ukosefu  wa huduma ya maji na  nishati ya umeme hali ambayo inawalazimu  akina mama wajawazito kutumia tochi  ya simu au taa wakati wa kujifungua huku watoto wanaougua kuchanganywa na wakubwa.

Baadhi ya wananchi wa kata hiyo  walieleza kuwa   kumekuwepo na tatizo la kupata huduma iliyo bora kwani  vifaa vya kupimia maradhi yanayowasumbua hakuna, mama wajawazito kutumia  mwanga wa simu ya tochi wakati wa kujifungua , wamalizapo kujifungua nguo  zao hulazimika  kwenda kufulia  kwenye malambo  sehemu ambayo maji hutumiwa na watu wote. 
  
 
Walisema  wamekuwa wakipata  shida ya kupata huduma katika kituo hicho  kwani hakuna  maji  hivyo wanapokwenda kujifungua hulazimika kwenda na maji yao.
 

Mwenyekiti wa kijiji cha  Azimio  Twiga  Mashimba  alisema kuwa  kituo hicho kinahudumia  vijiji zaidi ya vitano  na kata nne  ambazo ni Mwakitolyo,Mwenge na Salawe  ambapo kijiji chake kina watu  zaidi ya 3000  na kwamba kituo kinakabiliwa na changamoto ya uhaba wa wodi  ya watoto  ambao hulazimika  kuchanganywa na wakubwa, kina mama hujifungua kwa kutumia mwanga wa simu ya tochi pia uhaba wa maji upo.
“ Kijiji hiki kinahudumia zaidi ya watu 21,000, awali kulikuwepo na sola ambayo ilikuwa ikisaidia  kurahisisha huduma mbalimbali kwa wagonjwa lakini ilikwisha ibiwa na sasa hakuna sola vifaa vya kupimia  maradhi mbalimbali ikiwemo malaria hakuna ,wodi ya kulaza watoto  hakuna inawalazimu kuwachanganya na wakubwa hata  wenye magonjwa ya kifua kikuu na kuhara”alisema .
Naye  mkuu wa kituo hicho Dkt  Saimon Wilson alisema   vifaa vya kupimia baadhi ya maradhi vipo   ila kuna wengine wagonjwa hulazimisha  kupata vipimo vyote vingine havipo ila kwa upande wa  kupima malaria kipimo kipo, suala la kujifungulia tochi  ya simu sio kweli bali wanatumia taa ikiwa sola iliyopo haina nguvu na huzimishwa ifikapo  saa tano usiku.
"Kituo hiki  kinakabiliwa na  changamto ya maji na nishati ya umeme,  suala la sola kuibiwa siwezi kulizungumzia   mimi nilikuta  sola iliyopo  na  inatumika  mpaka sasa ni hii nayo haina nguvu huwashwa  na kuzimishwa saa tano usiku ,tunatumia taa za kawaida,pia wagonjwa kwa siku ni zaidi ya 80",aliongeza.
Diwani wa kata hiyo   Joseph  Budonho  alisema kuwa  kweli  kituo hicho cha afya  kina changamoto ya ukosefu wa  nishati ya umeme na maji  ila tatizo hilo linashughulikiwa   ikiwa tayari nyaya za umeme zimekwisha wekwa   isitoshe kuondoa  tatizo la maji lililopo, kuhusu sola  ilikuwepo  zamani lakini iliibiwa na kesi bado ipo mahakamani.

ACHOMWA KISU HADI KUFA AKITUHUMIWA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA

Watu wawili wafariki dunia na wengine wawili kukamatwa mkoani Iringa katika matukio tofauti tofauti likiwemo la mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Magdarena Ng'akala (76) kufariki dunia wakati akiwa anaendelea na matibabu katika hospitali ya mkoa Iringa baada ya kuchomwa  kisu upande wa kulia wa ubavuni mwake.

Akizungumza na mtandao huu wa www.matukiodaima.com ofisini kwake Kaimu Kamanda wa polisi mkoani Iringa ACP Wankyo Nyigesa alithibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea mnamo tarehe 29 machi majira ya saa 5 kamili asubuhi maeneo ya Kijiji cha Image, tarafa ya Mazombe wilaya ya Kilolo.
Kamanda alisema marehemu alichomwa kisu na mtu aliyefahamika kwa jina la Gabriel Msave na kusema chanzo cha tukio hilo ni imani za kishirikina, mtuhumiwa anatafutwa.
 
Tukio lingine, Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Agrister Chaula (30) amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia kipande cha khanga.
Tukio hilo lililotokea mnamo tarehe 30 machi majira ya saa 2 kamili asubuhi huko pori la mninga tarafa ya Kasanga wilaya ya Mufindi na kusema marehemu alijiua baada ya kutoroka hospitali ya Lugoda na kuacha kitoto kichanga cha siku 5.
JESHI la polisi mkoani Iringa linawashikilia watu wawili kwa kosa la kukutwa na vipande 9 vya meno ya tembo vikiwa ndani ya gari aina ya Corolla lenye namba za usajili T. 306 AJW.
Kamanda aliwataja watuhumiwa hao ni Fatuma Athumani (50) mkazi wa Dar Es Salaam na Joel Antony (31) mkazi wa Bagamoyo na kusema watuhumiwa hao walikamatiwa maeneo ya Kinanyambo tarafa ya Ifwagi Zone 1 wilaya ya Mufindi.
Mbali na matukio hayo matatu, kamanda alisema watu wasiofahamika waliiba pikipiki aina ya Work Mashine yenye namba za usajili T. 403 BRZ yenye Thamani ya Shilingi 1,170,000/= ambayo ni mali ya Ruben Joseph (40) mkazi wa Igula wilaya ya Iringa Vijijini.
NA DIANA BISANGAO WA MATUKIO DAIMA.COM, IRINGA

KISWAGA AKIWEZESHA KIKUNDI CHA VIKOBA CHA TWIYENDAGE KALENGA

Wanachama  wa  kikundi  cha Vicoba cha Twiyendage  Kalenga  wakimpokea Jackson Kiswaga  leo
Mtendaji  wa kijiji cha Kalenga  akimkaribisha Kiswaga  kuzindua  kikundi hicho
Wanachama wa  Twiyendage Vicoba  wakisoma Risala yao kwa  Kiswaga
Kiswaga  akifuatilia risala kwa makini
wanachama  wa  Twiyendage Vicoba  wakifurahia hotuba ya Kiswaga
Kiswaga  akizindua kikundi  cha Vicoba  cha Twiyendage Kalenga
Kiswaga akiwa na  wanachama wa kikundi  cha Vicoba Twiyendage Kalenga mara  baada ya kuzindua  kikundi hicho
Aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa kikundi   cha Twiyendage   Vicoba Kalenga ,mkurugenzi  wa kampuni ya Tigo nyanda za  juu  kusini Bw Jackson Kiswaga  akimkabidhi mwenyekiti  wa kikundi hicho Bi Mwahija Witala msaada  wa fedha kiasi cha Tsh 500,000 kati ya shilingi 700,000 alizoahidi kwa kikundi hicho
MKURUGENZi  wa  kampuni ya  simu ya Tigo kanda  ya nyanda za  juu  kusini  Jackson  Kiswaga  amechangia  kiasi cha Tsh 700,000 kwa  ajili ya  kukiwezesha  kiuchumi kikundi cha Vicoba cha Twiyendage kata  ya Kalenga  wilaya ya Iringa .

Kiswaga  alikabidhi msaada  huo leo wakati wa   uzinduzi  wa kikundi  hicho  chenye  wanachama 30 kama  njia ya  kuunga  mkono  jitihada za  wanawake  hao katika  kujiletea maendeleo.

Akizungumza  wakati  wa   uzinduzi  wa  kikundi  hicho  Kiswaga  aliwataka  wanachama wa  kikundi hicho kuzidi  kuwahamasisha  wenzao  kujiunga na  vikundi  kama  hivyo kama  njia ya  kujikwamua  kiuchumia na  kuwataka  wanachama  kujenga utamaduni  wa  kurejesha  mikopo  pindi wanapokopeshana .

Kwani  alisema  iwapo  wanachama  wengi  zaidi  watahamasishwa  kujiunga na vikundi hivyo  vya  kiuchumia upo uwezekano mkubwa  wa  serikali na  taasisi  mbali mbali za kifedha kuunga mkono  jitihada za  vikundi  hivyo.

"Awali  ya  yote ninapenda  kuwashukuru wanachama kwa  kunialika  kuwa mgeni rasmi hapa  leo ila bado napenda  kuwatia nguvu kwa  kuwachangia  kiasi  cha Tsh 700,000 ili  kuongeza mtaji  wenu zaidi ... ili  kuweza kujikomboa  kimaisha  ni lazima  kuanzisha  vikundi kama  hivi vya kiuchumia"

Awali  mwenyekiti  wa  kikundi hicho Mwahija Witala alisema  kuwa  kikundi  hicho kina  wanachama  30  kutoka makundi  mbali mbali ya  kijamii  wakiwemo   walimu, wakulima wafanyabiashara  na wa wale  wasio  kuwa na ajira .

Witala  alisema  hadi  sasa  kikundi  hicho  kina mtaji wa Tsh milioni 3 na lengo ni  kuendelea  kusaidiana  zaidi ikiwa ni pamoja na  kusaidia makundi mbali mbali ya jamii yaayowanzunguka  wakiwemo  watoto  yatima.

MKURUGENZI WA TIGO NYANDA ZA JUU KUSINI ATEMBELEA OFISI YA TIGO IRINGA

Mkurugenzi  wa  Tigo  nyanda za  juu kusini Bw Jackson Kiswaga  akizungumza na  wafanyakazi wa TIGO Iringa  leo
watenda kazi  wa Tigo  wakiwa  nje ya makao makuu ya Tigo Iringa leo
Kiswaga  mwenye suti akipokea taarifa  ya utendaji kutoka kwa  viongozi wa Tigo  Iringa
Kiswaga  akitoa maelezo  jinsi ya  kuendelea  kuongeza  wateja mkoa wa Iringa ambapo hadi sasa Tigo imeendelea kuteka soko na kuwa  kimbilio la wengi
Kazi  inaendelea  vema
Kiswaga  akitazama simu za bei poa  ambazo zinauzwa na Tigo
Tupo  kikazi zaidi
Kiswaga akiwa na  wafanyakazi  wa Tigo  leo

ZIARA YA KINANA NKASI LEO, MAMIA WAHUDHURIA MKUTANO WAKE MJI MDOGO WA NAMANYERE Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimiana na kinamama wa hamasa, baada ya kuwasili kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika, Jumapili, Machi 30, 2014, katika mji mdogo wa Namanyere, wilayani Nkasi akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM na kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia za kizitatua, katika mkoa wa Rukwa.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia mamia ya wananchi katika mkutano huo uliofanyika katika mji mdogo wa Namanyere wilayani Nkasi mkoani Rukwa, Jumapili, Machi 30, 2014.
 Kijana Elias Yeremia akimuuliza swali Kinana jukwaani, katika mkutano huo wa Namanyere, Nkasi mkoani Rukwa
 Mjumbe wa NEC, Balozi Ali Karume akihutubia mkutano huo wa Namanyere
 Vijana wa Namanyere wakiwa wamepanda juu ya lori siyo kwa lengo la kusafiri bali kuhakikisha wanamuona Kinana kwenye mkutano huo wa Namanyere
Wazee wakimsikiliza kwa makini Kinana kwenye mkutano huo wa Namanyere 
 Mamia ya wananchi kwenye mkutano huo wa Kinana katika mji mdogo wa Namanyere
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Rukwa, Hypolitus Matete, akimshukuru Kinana kwa hotuba nzuri, mkuatno huo wa Namanyere 
 Kikundi cha matarumbeta kikitoa burudani kwenye mkutano huo wa Kinana katika mji mdogo wa Namanyere
 Mzee Rogas Nkana akimpatia ushahidi wa vielelezo na nyaraka mbalimbali kuhusu mirathi ya binti yake ambayo amefuatilia kwa muda mrefu hadi sasa bila mafanikio. Mzee Nkana alidai mbele ya Kinana kwamba madai hayo kwa ajili ya mirathi ya kifo cha binti yake ambaye alifariki dunia mwaka 2000 akiwa mtumishi wa Wirzara ya Mambo ya Ndani katika Jeshi la Uhamiaji yamekuwa kitendawili licha ya kufuatilia katika ofisi husika. Mzee Nkana alipata fursa hiyo wakati Kinana alipoamua kukutana na waasisi wa Chama na mabalozi kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali katika ukumbi wa Community Centre katika mji mdogo wa Namayere wilayani Nkasi. Picha zote na Bashir Nkoromo wa theNkoromo Blog

MGEJA AKABIDHI LUNINGA KWENYE KIJIWE CHA KAHAWA CHA BBC KATIKA

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja akikabdhi Luninga kwa Wajasiliamali wa BBC katika Mji mdogo wa Isaka wilayani Kahama
Wa pili kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa shinyanga Khamis Mgeja akikabidhi  fedha kwa ajili ya kebo ya TV muda mfupi baada ya kukabidhi Luninga kwa kijiwe cha Kahawa cha BBC katika Mji mdogo wa Isaka wilayani Kahama.

Na Wiliam Bundala wa  matukiodaima.com kanda ya Ziwa
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja jana amekabidhi msaada wa luninga yenye thamani ya shilingi 260,000/= kwenye kijiwe maarufu cha wajasiliamali cha  Kahawa maarufu kwa jina la BBC kilichopo katika mji mdogo wa Isaka Wilayani Kahama wakati akiwa katika ziara ya kikazi kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM.
 
Wajasiriamali hao walimwomba mwenyekiti huyo wa CCM msaada huo wa Luninga ili waweze kupata habari kupitia chombo hicho hasa nyakati za asubuhi na jioni kabla ya kazi na baada ya kazi ili kwenda sambamba na mambo yanatokea ndani na nje ya nchi.
 
Akizungumza na wajasiriamali hao baada ya kukabidhi luninga hiyo Mgeja aliwataka wazee na vijana kujenga utamaduni wa kuridhika na vipato vidogo wanavyovipata kulingana na hali waliyonayo badala ya kukimbilia vipato vya juu ambavyo vipo nje ya uwezo wao wa kimahitaji.
 
Kufuatia msaada huo mwenyekiti wa Wajasilimali hao wa BBC Ally Salumu Msangi alishukuru na kuongeza kuwa msaada huo umefika katika kipindi muafaka hasa wakati wa kipindi hiki cha bunge la katiba linaloendelea mjini Dodoma.

WANAHARAKATI WAMUUNGA MKONO RAIS KIKWETE KWA KUPAMBANA NA UJANGILI

DSC_0079
Mgeni rasmi Mwenyekiti wa Chama Cha Msalaba Mwekundi (Red Cross), Dr. George Nangale, akizindu rasmi kampeni ya ‘Save The Elephant’ (Okoa Tembo) kwa niaba ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete, kama jitihada za kumuunga mkono Rais Kikwete katika kupambana na ujangili wa wanyamapori nchini. Kushoto ni Mratibu wa Taasisi ya Tembo Marathon Tanzania, Bw. Robert Zangi, Wa pili kushoto ni Meneja Uhusiano wa Bodi ya Utalii (TTB), Geofrey Tengeneza, na Kulia ni Dr. Herry Muhando kutoka International Evangelist.(Picha na Zainul Mzige).
Na. Zainul Mzige.
Taasisi ya Tembo Marathon Tanzania imezindua kampeni ya ‘Save The Elephant’ (Okoa Tembo) kama jitihada za kumuunga mkono Rais Jakaya Kikwete katika kupambana na ujangili wa wanyamapori nchini.
Mratibu wa taasisi hiyo, Robert Zangi, amesema wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo kwamba wameamua kumuunga mkono Rais Kikwete kutokana na kukithiri kwa matukio ya ujangili wa wanyamapori miaka ya hivi karibuni.
Aliongeza kwamba kampeni hiyo itawalenga zaidi watu ambao wanaishi jirani na mbuga za wanyama.
“Watu wanaoishi jirani na mbuga za wanyama ni rahisi kufahamu nani ni jangili na nani ni raia mwema miongoni mwao,” alisema.
Aliongeza kusema kwamba kampeni hiyo itawafikia watu wanaoishi jirani na mbuga za wanyama kwa lengo la kuwaelimisha umuhimu wa kupambana na jangili dhidi ya wanyamapori.
DSC_0037
Mratibu wa Taasisi ya Tembo Marathon Tanzania, Bw. Robert Zangi, akizungumza na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ‘Save The Elephant’ (Okoa Tembo) kupitia Taasisi yake kama jitihada za kumuunga mkono Rais Jakaya Kikwete katika kupambana na ujangili wa wanyamapori nchini. Wa pili kushoto ni Meneja Uhusiano wa Bodi ya Utalii (TTB), Geofrey Tengeneza, Wa pili kulia ni Mgeni rasmi Mwenyekiti wa Chama Cha Msalaba Mwekundi (Red Cross), Dr. George Nangale (kwa niaba ya Rais Kikwete) na Kulia ni Dr. Herry Muhando kutoka International Evangelist.
Kampeni hiyo ina mpango wa miaka mitano ambao kwa kuanzia kutakuwa na matukio matatu makubwa mwaka huu kati ya sasa hivi na mwezi Mei.
Tukio la kwanza, alisema, ni la uzinduzi wa kampeni hiyo na la pili ni kuwasilisha ujumbe wa kampeni kwenye Umoja wa Mataifa nchini Marekani tarehe 9 mwezi Aprili na la tatu litakuwa ni semina juu ya kupambana na mauaji ya Tembo, Vifaru na wanyamapori wengine.
DSC_0030
Meneja Biashara wa Qatar Airways Tanzania, Bw. Basel Haydar (kushoto) pamoja na Meneja Mauzo wa Qatar Airways Tanzania, Bw. Emmanuel Okware.
DSC_0171
Meneja Uhusiano wa Bodi ya Utalii (TTB), Geofrey Tengeneza akisisitiza jambo ambapo ametoa rai kwa wadau mbalimbali pamoja na mataifa mengine kuunga mkono jitihadi hizi kuhakikisha ujangili unatokomezwa.
Nae Mwenyekiti wa Chama Cha Msalaba Mwekundi (Red Cross), Dr George Nangale, amesema kwamba wanaunga mkono kampeni hiyo kwani mauaji ya wanyamapori ni majanga na kwamba watu wanaoishi jirani ya mbuga za wanyama wanaweza kusaidia sana kwenye mapambano dhidi ya ujangili.
Nangale alikuwa anamwakilisha mgeni rasmi ambaye alikuwa awe Rais Kikwete.
Meneja Uhusiano wa Bodi ya Utalii (TTB), Geofrey Tengeneza, alisema ni vizuri kuendelea kuwalinda Tembo na wanyamapori wengine na kuongeza kwamba kampeni hii ni muhimu sana na akaomba jitihada hizi ziungwe mkono na nchi jirani pamoja na mataifa mengine.
DSC_0095
Meneja Biashara wa Qatar Airways Tanzania, Bw. Basel Haydar akizungumzia udhamini wao wa kuwapelekea Marekani wanaharakati wa Kampeni ya "Save The Elephant".
DSC_0106
Meneja Biashara wa Qatar Airways Tanzania, Bw. Basel Haydar (kushoto), akikabidhi mfano wa tiketi ya ndege kutoka shirika la ndege ya Qatar watakaosafirisha msafara wa kampeni ya"Save the Elephant" kuelekea nchini Marekani kwa Mratibu wa Taasisi ya Tembo Marathon Tanzania, Bw. Robert Zangi ( wa pili kushoto). Wanaoshuhudia tukio hilo ni Meneja Uhusiano wa Bodi ya Utalii (TTB), Geofrey Tengeneza (wa pili kulia) na Mwenyekiti wa Chama Cha Msalaba Mwekundi (Red Cross), Dr. George Nangale, (kulia).
DSC_0108
Meneja Biashara wa Qatar Airways Tanzania, Bw. Basel Haydar (kushoto) akipeana mkono na Mratibu wa Taasisi ya Tembo Marathon Tanzania, Bw. Robert Zangi.
DSC_0032
Meneja Mkuu wa Le Grande Casino, Bw. Costa Cambanis (kushoto) pamoja na timu yake kutoka Le Grande Casino Tanzania.
DSC_0111
Afisa Mtendaji Mkuu wa UBL Bank, Bw. Muhammad Tanveer, akizungumzia udhamini wao kwa wanaharakati wa kampeni ya "Save the Elephant" ambao ni kuwalipia ada za uwanja wa ndege kutoka Dar, Doha, Chicago na Denver Colorado.
DSC_0121
Afisa Mtendaji Mkuu wa UBL Bank, Bw. Muhammad Tanveer (wa pili kushoto) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Dola za Kimarekani 1000 kwa Mratibu wa Taasisi ya Tembo Marathon Tanzania, Bw. Robert Zangi (katikati). Wanaoshuhudia tukio hilo ni mgeni rasmi aliyemwakilisha Rais Kikwete, Mwenyekiti wa Chama Cha Msalaba Mwekundi (Red Cross), Dr George Nangale (kulia), Meneja Uhusiano wa Bodi ya Utalii (TTB), Geofrey Tengeneza (wa pili kulia) na kushoto ni Head of Risk wa UBL Bank, Farooq Hashim Randeri.
DSC_0124
Afisa Mtendaji Mkuu wa UBL Bank, Bw. Muhammad Tanveer ( wa pili kushoto) akipongezana na Mratibu wa Taasisi ya Tembo Marathon Tanzania, Bw. Robert Zangi (katikati) pamoja na Meneja Uhusiano wa Bodi ya Utalii (TTB), Geofrey Tengeneza (wa pili kulia).
DSC_0127
Meneja Mkuu wa Le Grande Casino, Bw. Costa Cambanis, akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni ya "Save the Elephant" inayoendeshwa na Taasisi ya Tembo Marathon Tanzania ambapo kwa kuunga mkono jitihada hizo za kupamba na ujangili wametoa udhamini wa Malazi kwa timu nzima itakayoenda nchini Marekani.
DSC_0134
Meneja Mkuu wa Le Grande Casino, Bw. Costa Cambanis (kushoto) akipeana mkono na Mratibu wa Taasisi ya Tembo Marathon Tanzania, Bw. Robert Zangi (wa pili kushoto) wakati wa hafla hiyo fupi ilyodhaminiwa na hoteli ya DoubleTree by Hilton ya jijini Dar es Salaam.
DSC_0086
Afisa Mtendaji Mkuu wa UBL Bank, Bw. Muhammad Tanveer (wa pili kushoto) akiwa pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo.
DSC_0067
Pichani juu na chini ni baadhi ya wadau kutoka mashirika ya kimataifa, taasisi za serikali, Frankfurt Zoology Society, WWF pamoja wawakilishi wa balozi mbalimbali nchini waliohudhuria uzinduzi huo.
DSC_0089
DSC_0059
DSC_0042
DSC_0176
Wadau wakisalimiana baada ya uzinduzi rasmi wa Kampeni ya "Save The Elephant".