Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

February 28, 2014

MWIGULU NCHEMBA AENDELEA KUTIKISA KALENGA,ASHIRIKI SHUGHULI ZA KIJAMII

Mwigulu anasema"Mchakamchaka Unaendelea Kalenga,Hii leo kazi imefanyika Kijiji Cha Kidamali.Tunafanya kazi ya Kuhakikisha Tar.16/03/2014 Ushindi wa Kishindo Unapatikana kwa Chama Cha Mapinduzi.
Asanteni Wanakalenga Kijiji Cha Kidamali,Kura Zote za NDIO Kwa Kijana Godfrey William Mgimwa.
UMOJA NI USHINDI"

Pichani ni Mh:Mwigulu Nchemba akimnadi Mgombea wa CCM Jimbo la Kalenga Mbele ya Maelfu ya Wananchi wa kata ya Nzi hii leo 28/02/2014.
 
Naibu Katibu Mkuu CCM Bara Mh:mwigulu Nchemba akifanya kampeni za Kijiwe kwa Kijiwe,Mtaa kwa Mtaa Kata ya NZI hii leo.Kwenye Picha akikutana na Vijana,Wazee na Watu Mbalimbali kuandi Sera za Chama cha Mapinduzi na kumnadi Mgombea.
Wakati Kampeni zikiendelea,Mh:mwigulu Nchemba aliamua Kusitisha Kampeni na Kuungana na Wananchi wa Nzi kushiriki kwenye Mazishi msiba uliopo Kijijini hapo.Pichani Mgombea Ubunge wa CCM William Mgimwa na Mh:Mwigulu Nchemba wakisaidia kufanya Mazishi.
Kwa kuwa Marehemu Mgimwa alikuwa anasomesha Watoto yatima ndani ya Jimbo lake,Hivyo Mh:Mwigulu Nchemba ameagiza kuwa Mbunge Mtarajiwa Godfrey Mgimwa atakapotangazwa kuwa ameshinda,Jukumu la kwanza ni kuhakikisha anabeba Mzigo wa Watoto walioachwa na Marehemu na kuanza kazi ya Kuwasomesha.
Kampeni hapa Kalenga Zimepamba Moto,CCM wanafanya kampeni za Jukwaani na Nyumba kwa Nyumba,Kijiwe kwa Kijiwe kuhakikisha Wanatetea Jimbo kwa Ushindi wa Kishindo Tar.16/03/2014. 

ALILAZIMIKA KUKEKETWA ILI ASOMESHWE

ESTER CHARLES (16) ambaye anasoma kidato cha tatu katika shule ya Sekondari Rebu iliyoko wilayani Tarime mkoani Mara, alishindwa kujizuia na kudondosha machozi katika ukumbi wa kantini ya jeshi la polisi wilayani Tarime baada ya kueleza masaibu aliyokumbana nayo kwa kufanyiwa ukeketaji na wazazi wake.

Anapofanyiwa ukeketaji huaminika kuwa mwanamke kamili aliyeondolewa mkosi na ambaye anastahili kuolewa. Wakati anafanyiwa ukatili huo, Esta alikuwa anasoma darasa la saba katika shule ya msingi Rebu, ambapo mara baada ya kukeketwa, anasema alipata maumivu makali ikiwa ni pamoja na kutokwa na damu nyingi.

Anasema alikubali kufanyiwa ukeketaji na wazazi wake baada ya kufaulu mtihani wa darasa la saba na alikuwa na hamu ya kuendelea na masomo, lakini akapewa masharti na wazazi wake kuwa ili aendelee na masomo lazima akeketwe.

“Sikuwa na jinsi, nilijua ningeenda kukumbana na maumivu makali na kwasababu nilikuwa napenda  shule ilinibidi kukeketwa” anaeleza.
Kutoka maktaba ni moja ya nyenzo za ukeketaji.
UKEKETAJI UNAFANYIKAJE?
Anasema aliamshwa saa 11:30 alfajiri akiongozana na mama yake na wanawake wengine watatu alikwenda kuungana na wasichana wenzake waliokuwa kwenye orodha ya kufanyiwa ukeketaji na kupelekwa mtoni kuogeshwa!

Tuliogeshwa na kupewa maneno ya ujasiri ili tusilie wakati wa kukeketwa “ anasema na kuongeza kuwa Ngariba alilipwa kiasi cha Sh. 10,000/= kwa kila msichana aliyekeketwa (kwa wakati huo). Esta anasema kuna eneo maalum lililotengwa kwaajili ya shughuli hiyo na msichana hushikwa mikono yake kwa nyuma na mama aliyekeketwa.

“Baada ya kufika eneo lile, tulitangaziwa na ngariba kuwa kila mmoja awe na wembe wake, ambao ndiyo alitumia kukeketa” anasema.

Anachokumbuka siku hiyo ni kujikuta tayari amekwisha keketwa huku akitokwa na damu nyingi na maumivu makali. Anasema baada ya kukeketwa, wasichana wote waliwekwa katika uangalizi wa akina mama wasaidizi wakiwemo baadhi ya ngariba, huku wakiwapatia dawa za kienyeji wale wanaovuja damu iliisiedelee kuvuja.

“Nilishindwa kula, nilikunywa uji tu, siku ya pili nilipata maumivu makali baada ya kuamshwa asubuhi kwenda kuogeshwa” anaeleza.
Wakisikiliza kwa makini ni washiriki wa Kongamano hilo lililokuwa mahususi kwa ajili ya kuibua changamoto zilizopo katika jamii kuhusu suala la ukeketaji
Anasema msichana anapotoka jandoni inambidi ashiriki tendo la ndoa na mwanaume ambaye amefanyiwa tohara kama ishara ya kukubali kuwa binti aliyekeketwa kuwa mwanamke kamili na anayestahili kuolewa. Msichana aliyekeketwa huitwa ‘Omonke’.

Anaiomba serikali, asasi za kiraia na waandishi wa habari kutoa elimu ya madhara ya ukeketaji kwa watoto wa kike, na kwa ngariba wapewe elimu ya kutosha dhidi ya madhara ya ukeketaji.

“Wengi huku Tarime wanafanya hivyo, wakijivunia kukeketwa kutekeleza mila lakini pia ngariba bado hawajapata elimu ya madhara ya ukeketaji, naiomba serikalia na wadau wengine watoe elimu zaidi juu ya madhara ya ukeketaji” anasema na kuongeza kuwa jamii yao huamini kuwa wakimkeketa motto wa kike huleta Baraka katika familia.
NI MADHARA GANI ALIYOKUMBANA NAYO?
Anasema baada ya kukeketwa aliumia sana na aliathirika kisaikolojia ikiwemo kuzomewa nna wasichana wa rika yake ambao hawakuwa tayari kukeketwa.

“Siku niliyokeketwa, nilipata shida sana, nilikuwa na hofu hata wenzangu walikuwa wakinicheka, hata nilipopona nilichukua muda kurudi shule, niliathirika sana” anasema madhara mengine aliyo yapata ni pamoja na kuchanika sehemu zake za siri, kutokana na kukeketwa akiwa na wasiwasi kama atajifungua salama siku za baadaye.

“Mimi nahisi hata wakati wa kujifungua, nitapata matatizo, naomba wazazi wetu wabadilike waanze kwenda na wakati na watambue kuwa wanapotufanyia ukeketaji wanatufanyia ukatili wa kijinsia na kilema cha maisha” anasema.

Anasema kuwa kuna uwezekano wa wasichana wanaokeketwa kupata virusi vya ukimwi kutokana na kukeketwa ba ngariba mmoja, ambaye hukeketa zaidi ya wasichana 50 kwa siku.

Ester anaahidi kuhakikisha wadogo zake Neema na Happy kuwa hawato keketwa kwani yeye kashakuwa mkubwa anayejitambua ana kujua kujieleza.

NDOTO ZA BAADAYE ZA ESTA.
“Nitasomea uandishi wa habari, nitafanya kazi kwa bidii na natamani niwe kama Waziri wa Maendeleo ya Wanawake, Jinsia na Watoto, Sophia Simba. Nampenda jinsi anavyo wahudumia wanawake” anasema.

Ameiomba serikali kupitia jeshi la polisi kuwakamata mangariba wote wanao husika kufanikisha ukeketaji na kuwafikisha mahakamani, ili sheria ichukuemkondo wake .

Anaitaka jamii ya Wakurya kuendeleza watoto wa kike kitaaluma zaidi badala ya kuwaoza wakiwa katika umri mdogo, na hivyo kushindwa kuhilili kutunza familia.
Kamanda Emmanuel Mkoma.
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Tarime – Rorya, Emmanuel Mkoma anasema kuwa jeshi la polisi kwa kushirikiana na wadau wengine wilayani Tarime, limeanza kutoa mafunzo ya tohara mbadala itakayo iwezesha jamii kutambua athari za ukeketaji kwa watoto wa kike.
Askari polisi, wanafunzi wa shule za sekondali na tiba ni sehemu ya kusanyiko la washiriki wa Kongamano lililokuwa mahususi kwa ajili ya kuibua changamoto zilizopo katika jamii kuhusu suala la ukeketaji.
Hisia za mmoja kati ya wanafunzi wa kiume na uelewa wa suala la ukatili wa kijinsia na ukeketaji wilayani Tarime mkoani Mara.
Wakisikiliza kwa makini ni wadau wa KIVULINI, Jeshi la Polisi na Wanahabari.
Lengo la mafunzo hayo ni kutoa elimu kwa jamii, ambapo watoto wa kike watapewa elimu ya malezi ya Afya zao itakayo wasaidia wasikeketwe, msisitizo wake ni kuelimisha jamii ione madhara ya ukeketaji na kadri siku zitakavyo kwenda jeshi la polisi linaimani kuwa jamii itaachana na ukeketaji.Imeandaliwa na  mwandishi  Wiliam Bundala  wa matukiodaima.com kanda ya ziwa 

VISIMA VYA TBL RUHUHU LUDEWA VIMEKUFA BILA KUTOA MAJI

Visima vilivyotolewa msaada  wa kampuni ya bia ya TBL kata ya  Ruhuhu Ludewa  choka  mbaya  baada  ya kukosa kutoa maji  toka  vilipochimbwa mwaka jana

KAYA ZAIDI YA 5000 ZA MANISPAA YA IRINGA KUFIKIWA NA MAJI SAFI NA SALAMA


????????
Mhandisi wa maji wa Manispaa ya Iringa, Taphali Ngwada (Kulia) akiwasilisha taarifa ya maendeleo ya mradi wa maji unaolenga kuzifikia zaidi ya kaya 5000 za manispaa hiyo wakati wa ukaguzi uliofanywa na wataalam kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Wataalam hao waliongozwa na Naibu Katibu Mtendaji (Huduma za Jamii na Masuala ya Idadi ya Watu), Bibi Florence Mwanri (Watatu Kulia mwenye koti jeusi) na Naibu Katibu Mtendaji (Uchumi Jumla, Prof. Longinus Rutasitara (Wapili Kulia).????????Viongozi wa msafara wa wataalam wa ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Naibu Katibu Mtendaji (Huduma za Jamii na Masuala ya Idadi ya Watu), Bibi Florence Mwanri (Kushoto) na Naibu Katibu Mtendaji (Uchumi Jumla, Prof. Longinus Rutasitara (Kulia) wakitaka ufafanuzi juu ya maendeleo ya mradi.????????Kaimu Mhandisi wa maji wa Mkoa wa Iringa, Mhandisi Kingazi William (Kulia) akitoa ufafanuzi kuhusu maendeleo ya mradi wa maji unaolenga kuzifikia zaidi ya kaya 5000 za manispaa hiyo wakati wa ukaguzi uliofanywa na wataalam kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.????????Kaimu Mhandisi wa maji wa Mkoa wa Iringa, Mhandisi Kingazi William (aliyenyanyua mkono) akitoa ufafanuzi kuhusu maendeleo ya tanki la kuhifadhia maji kwa ajili ya mradi wa maji unaolenga kuzifikia zaidi ya kaya 5000 za manispaa ya Iringa.????????Kamanda wa Kikosi cha Zimamoto wa Uwanja wa Ndege wa Iringa (Nduli) ambao ni wanufaika wamradi wa maji unaolenga kuzifikia zaidi ya kaya 5000 za manispaa ya Iringa , Bw. Ranier Nyimbo (Mwenye Fulana nyeusi) akitoa maelekezo wakati wa ukaguzi uliofanywa na wataalam kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango kwenye uwanja huo.????????Baadhi ya wanavijiji wa Nduli na Kigonzile kutoka manispaa ya Iringa wakichota maji katika bomba pekee linalopatikana katika mpaka wa vijiji hivyo. Adha hii itaisha mwezi Juni mwaka huu mara baada ya kukamilika  kwa mradi wa maji unaolenga kuzifikia zaidi ya kaya 5000 za manispaa ikiwemo wanavijiji hawa.????????Mhandisi wa maji wa Manispaa ya Iringa, Taphali Ngwada (Watatu Kulia) akiwaonesha wataalam kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango moja ya mabomba yatakayotumika kusambaza maji.
PICHA NA SAIDI A. MKABAKULI
………………………………………………………………………………………..
Katika kukamilisha ahadi na Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2011 – 2016), Serikali imejidhatiti kuwafikishia maji safi na salama wakazi wa zaidi ya kaya 5000 za Manispaa ya Iringa kufikia katikati ya mwaka huu wa fedha.
Hayo yalibainishwa na Naibu Katibu Mtendaji (Huduma za Jamii na Masuala ya Idadi ya Watu), Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri wakati wa ukaguzi wa miradi ya maendeleo inayodhaminiwa na serikali na wafadhili.
Bibi Mwanri alisema kuwa katika kutimiza Mpango wa huo wa Maendeleo Serikali inawekea mkazo katika Kuendeleza adhma yake ya utekelezaji wa miradi ya maji iliyoibuliwa katika Programu ya Matokeo Makubwa Sasa (BRN) hasa katika maeneo sugu yenye upungufu wa maji hasa maeneo ya vijijini ili kuweza kuwafikia wananchi wengi zaidi na kuuendelea kuimarisha usimamizi vyanzo vya maji.
Akizungumza wakati wa ukaguzi huo, Kaimu Mhandisi wa maji wa Mkoa wa Iringa, Mhandisi Kingazi William alisema kuwa kupitia Mpango huo wa Maendeleo wa Miaka Mitano zaidi ya vijiji 10 vya mkoa wa Iringa vitanufaika na miradi hiyo ya maji ambayo inagharimu zaidi ya milioni 600.
Maji ni eneo mojawapo la kipaumbele la kutekeleza Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano unaoratibiwa na kusimamiwa na Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Maeneo mengine
ya vipaumbele yaliyoainishwa katika mpango ni pamoja na: miundombinu ya usafiri, nishati; kilimo; viwanda; maendeleo ya rasilimali watu; na huduma za jamii.

GESI INASAIDIA KUBORESHA HUDUMA ZA JAMII KILWA .


 MKURUGENZI  MKUU  WA  TANESCO  INJINIA  FELSCHEMI  MRAMBA  AKISHUKA   KWENYE  MOJA  YA  GARI  BAADA  YA  KUJARIBU   JIJINI  DAR  ES  SALAAM,  NA  PICHA  YA  PILI  NI  MKURUGENZI  MKUU  WA  TANESCO   INJINIA  FELSCHEMI  MRAMBA  AKIFANYA  MAHOJIANO  NA  WAANDISHI  WAHABARI  BAADA  YA  KUPOKEA  MAGARI 14  ,PICHA  YA  TATU  NI  BAADHI  YA  MAGARI  YALIYOKABIDHIWA  KWA  SHIRIKA  LA  TANESCO    JIJINI  DAR  ES  SALAAM

Mwandishi  Kenneth John  wa matukiodaima.com Dar 

Imebainika  kuwa  fedha  zinazotokana  na  gesi  asilia,  katika  Halmashauri   ya  wilaya  Kilwa  Mkoani  Lindi  zimekuwa  zikitumika  katika  kuboresha  huduma  mbalimbali  za  kijamii  mkoani  humo , ikiwa  ni  pamoja  na  miradi  ya  maji, umeme, elimu, afya,pamoja  na  ulinzi  na  usalama.

Hayo  yamebainishwa  na  mkurugenzi  Mtendaji  wa  halmashauri  ya  wilaya  ya  kilwa   mkoa  wa  lindi  Bw; Mapunda  Adoh  Stephen  ambapo  amesema  kijiji  cha  Songosongo  kimeendelea  kupata  huduma   mbalimbali  za  kijamii  ambapo  wananchi  wa  kijiji  hicho  wanapata   huduma  ya  maji  safi  na  salama  kwa  wastani  wa  lita  elfu  30  kwa  siku  kutoka  kampuni  ya  PAN AFRICAN  ENERGY.

Na  kuhusu  umeme  Mapunda  amesema  kuwa   wananchi  wa  Songosongo  wanapata  umeme  bure  isipokuwa  muhitaji   anahitajika  kulipia   gharama  za  uingizaji   pekee.Halikadharika  kuhusu  elimu  Mapunda  amesema  kuwa  wamejenga  darasa  la  chekechea lakini  pia  wamekuwa  wakitoa  fursa  kwa  watoto  10  kusomeshwa  kila  mwaka  katika  shule  ya  Makongo  iliyopo  jijini  Dar es  salaam, Huku  wakijenga  bweni  la  kulala  watoto  wa kike  lenye   thamani  ya  shilingi  194,000,000.00/=

Aidha  Mapunda  amesema  kuwa kwa  sasa  serikali   inampango  wa  kujenga  kituo   cha  polisi  cha  kisasa  kitakacho  gharimu  shilingi   625,000,000.00/= ambapo  ameongeza  kuwa  michoro  ya  kituo  hicho  tayari  imekamilika.

Akifafanua  namna  Kilwa  ilivyokuwa  ikikosa  mapato  yatokanayo na  Gesi  asilia  hapo  awali,  Mapunda  amesema  kulikuwa  na  visingizio  mbalimbali  vilivyokuwa  vikitolewa  na  kusababisha  halmashauri  hiyo kukosa  mapato  tangu  mwaka  2005, lakini  jitihada  zilifanyika  za  kudai  haki  hiyo  ndipo  mwaka  2012  shirika  la  TPDC  lIlikubali  kuanza  kulipa  deni  lote  la  tangu  mwaka  2005,  ambapo  jumla  ya  shilingi  608,800,00  zilifanikiwa  kulipwa  na  baada  ya  hapo  kampuni  ya  PAN  AFRICAN  ENERGY inayochimba  Gesi  huko  Songosongo   wakaendelea  kulipa  ushuru wa  tozo  la  huduma   kwa  asilimia  0.3.

Pamoja  na  hayo  Mapunda  amesema   kuwa  tangu  septemba  2012  baada  ya  baraza  la  madiwani  kupendekeza  na  kuamua  ushuru  uanze  kuplekwa  kwa  asilimia  20   katika  kijiji  cha  Songosongo  wamekuwa  wakipokea  pesa  kutoka  kampuni  ya  PAN  AFRICAN  ENERGY   na  kuzipeleka  Songosongo  ikiwa  ni  kama mchango  wa  Halmashauri  ambapo  hadi  kufikia   Februari  18,mwaka  huu  zimeshapelekwa  jumla  ya shilingi  139,600,191/= na  kuongeza  kuwa  fedha  ambayo  inaandaliwa  kupelekwa  Songosongo   ni  shilingi  22,663,647.00/=

Sambamba  na  hayo  Bwa;  Mapunda  amesema  kuwa  kwa  sasa  wilaya  ya  Kilwa  kwa  kushirikiana  na  wadau  wa  Gesi  wanatarajia   kujenga  hospitali  ya  kisasa   itakayokuwa  na  hadhi  ya  kimataifa,  ambapo   hadi  sasa  eneo  la  ekari   30  limeshatengwa  na  michoro   yote   imekamilika  tayari.Lakini  pia  Bw;Mapunda  ameongeza  kuwa    halmashauri  inataraji  kujenga  ukumbi  wa mikutano  wa  kimataifa  utakaogharimu  shilingi  3.8  bilioni  na  kazi  hiyo  itafanyika  kwa  kushirikiana  na  UTT.


Halikadharika  Bw;Mapunda  amebainisha  kuwa  Kilwa  ni  wilaya  iliyotangazwa  na  UNESCO  kuwa  ni  sehemu  muhimu   yenye  urithi  wa  Dunia   kwa  kuwa  kuna  vivutio  vingi  vya  mambo  ya  kale  na  ni  eneo   la  utali, ustaarabu  pamoja  na  samaki  kwa  wingi  sana.

MTOTO WA KIKE ABURUZWA NA BABA YAKE MTAA MZIMA KWENYE PIKIPIKI KWA KUSHINDWA KWENDA SHULEMtoto Anastazia Jumanne akiwa amefungwa mikono yake kwenye pikipiki kwa mpira.
Na Valence Robert-Geita
Mtoto Anastazia Jumanne (12) ambaye ni mwanafunzi wa shule ya msingi katika wilaya na mkoa wa Geita amefanyiwa ukatili wa kutisha baada kufungwa mpira kwenye pikipiki na baba yake mzazi na kisha kuanza kumburuza mtaani.

Tukio hilo la kusikitisha limetokea jana majira ya sa tatu asubuhi katika moja ya mitaa ya mjini humo ambapo inadaiwa kuwa binti huyo anayesoma darasa la nne katika shule hiyo alikataa kwenda shule kitendo ambacho kilimkasirisha baba yake aitwaye Jumanne Nkoyogi ambaye pia ni mfanyabiashara wa samaki mjini Geita.

Mashuhuda wa tukio hilo baada ya kuona asubuhi hiyo mtoto huyo akiburuzwa huku amefungwa kwenye pikipiki walianza kupiga makelele na kukusanyana kwa lengo la kumkamata baba huyo aliyekuwa anafanya unyama huo.
 
 Baada ya kumkamata na kumtia kumtia mikononi mwao walimpeleka kwenye ofisi ya sungusungu iliyopo Ihayabuyaga kata ya Kalangalala na kufungiwa humo kwa usalama wake.


Akizungumzia tukio hilo katibu wa sungusungu kata ya Kalangalala aliyempokea mtuhumiwa huyo Abel Richard alisema tukio hilo liliwafanya wananchi kujaa jazba dhidi ya mzazi huyo na kutaka kumpiga.
 
Alisema mzazi huyo kwa sasa anashikiliwa na jeshi la polisi wilayani Geita baada ya katibu huyo kuwasiliana na uongozi wa jeshi hilo na kuwatuma askari kwake kumchukua haraka kwa usalama wake.

Afisa upelelezi wa mkoa wa Geita Simon Pasua amekiri kuwepo kwa tukio hilo na kusema kuwa mtuhumiwa anashikiliwa na jeshi la polisi hadi sasa kwa upelelezi zaidi.

MSAADA WAKO NI UHAI WA MTOTO HUYU

MTOTO Adolotea Njavike(1.4) ambae Kichwa na Kiwiliwili vimeungana baada ya kupata na ajali ya Moto akiwa na mama yake Mzazi.


Mama Mkubwa wa Mtoto huyo, Salome Kiegu(35) mkazi wa Mtaa wa Maendeleo Iyunga Jijini Mbeya anasema Mtoto huyo akiwa na mama yake walipata janga la moto katika mazingira ya kutatanisha waliangukia kwenye moto ambapo Mtoto huyo aliungua vibaya.


Joseph Mwaisango wa Mbeya yetu akiwa amempakata mtoto huyo

Baadhi ya waandishi wa habari wakiongea na mama mkubwa wa mtoto huyo


MTOTO Adolotea Njavike(1.4) anaomba msaada wa matibabu kutoka kwa wasamaria wema ili aweze kufanyiwa upasuaji kutokana na Kichwa na Kiwiliwili kuungana baada ya kupata na ajali ya Moto akiwa na mama yake Mzazi.

Akizungumza kwa masikitiko Mama Mkubwa wa Mtoto huyo, Salome Kiegu(35) mkazi wa Mtaa wa Maendeleo Iyunga Jijini Mbeya anasema Mtoto huyo akiwa na mama yake walipata janga la moto katika mazingira ya kutatanisha waliangukia kwenye moto ambapo Mtoto huyo aliungua vibaya.

Anasema tukio hilo lilitokea Mwaka jana Mwezi wa Nane lakini alipopatiwa matibabu katika kituo cha afya mtoto huyo aliungana ngozi ya kidevu na kifua hali inayomletea shida ya kula na kufurahi na wenzake.

Anasema tangu kipindi hicho alimchukua mtoto huyo kwa mama yake na kuanza kuomba msaada wa matibabu baada ya kumpeleka katika Hospitali ya Ikonda iliyoko Makete Mkoani Njombe ambapo Wataalamu walimwambia atafute Shilingi Milioni Moja ili mtoto wake aweze kutibiwa.

Ameongeza kuwa baada ya muda wataalamu hao walimwambia asubiri Wazungu kutoka Ulaya ambao wataweza kumtibia mwanaye ambapo baada ya kusubiri kwa muda kidogo Wazungu hao walifika na kumcheki Mwanaye kisha kumwambia wao hawana utaalamu isipokuwa aende CCBRT Dar Es Salaam ambako ataweza kutatuliwa tatizo lake.

Aidha kutokana na kuambiwa hivyo Mama huyo anaomba msaada kutoka kwa wasamaria wema ili aweze kumpeleka Mtoto wake kwa matibabu kutokana na kutokuwa na uwezo wa kuweza kusafiri hadi DSM pamoja na gharama za matibabu kuwa kubwa.

Amesema anahitaji zaidi ya shilingi Milioni 2 ili ziweze kumsaidia kusafiri kugharamia matibabu pamoja na huduma za Kawaida kipindi atakachokuwepo Jijini Dar Es Salaam wakati akisubiri matibabu ya Mwanaye.

Mtu yeyote mwenye kuguswa na tatizo hilo anaweza kuwasiliana moja kwa moja na Mama huyo kupitia simu yake ya Mkononi namba 0752 986879 au Nyumbani kwake Iyunga Mtaa wa Maendeleo Jijini Mbeya.

WACHIMBAJI WADOGO MKOANI SHINYANGA WALIA NA WATENDAJI MIZIGO WA WIZARA YA NISHATI NA MADINI WANAOKAA MAOFISINI NA BADALA YAKE KAZI ZAO KUFANYWA NA WAKUU WA WILAYA.

  
MWANDISHI WA BLOG YA MATUKIO DAIMA KANDA YA ZIWA WILLIAM BUNDALA ALIYEINAMA AKIPEWA MAELEKEZO NA WACHIMBAJI WADOGO JINSI YA KUKAMATA DHAHABU KWA KUTUMIA NJIA YA MAJI.

.............................................................................

WATENDAJI wa Wizara ya Nishati na Madini waliopewa Dhamana ya kusimamia sheria za Wachimbaji wadogo hapa Nchini wametakiwa kutoka maofisini badala yake wazunguke kwa wachimbaji wadogo  ili kutoa Elimu juu uchimbaji wa kufuata sheria.

Hayo yamesemwa na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji wadogo Mkoa wa Shinyanga(SHIREMA) Nicodemus Majambe wakati akiongea na MATUKIO DAIMA BLOG juu ya vikwazo wanavyovipata Wachimbaji wadogo hapa nchini katika kupata maeneo ya Uchimbaji.

Majabe alisema kuwa Wachimnbaji wadogo hawana Elimu juu ya kupata maeneo ya uchimbaji wa Madini na kuongeza kuwa kama maofisa wa Madini wasingekaaa maofisini basi kusingekuwa na migogoro yeyote juu ya kupata maeneo ya Uchimbaji.

Alisema kuwa katika meneo ya Uchimbaji wa Madini Wakuu wa Wilaya wamekuwa wakipata kazi ya kutoaa Elimu ya uchimbaji katika maeneo hayo kazi ambayo ilitakiwa kutolewa na maoafisa wa Madini wa Sehemu husika.

Makamu Mwenyekiti huyo alisema kuwa katika Mkutano waliokaa na Waziri wa Niashati na Madini Mjini Dodoma walikubali kuwa na ushirikiano mkubwa baina ya Viongozi wa Wachimbaji wadogo na Watendaji wa Wizara ya madini kwa ujumla.
MAKAMU MWENYEKITI WA CHAMA CHA WACHIMBAJI WADOGO MKOA WA SHINYANGA (SHIREMA) NICODEMUS MAJABHE MWENYE KOFIA AKIONGEA NA MWANDISHI WA MAUKIO DAIMA KANDA YA ZIWA KUHUSU MIGOGORO ILIYOPO KATIKA MACHIMBO MAOO NCHINI.

Pia alisema kuwa urasimu uliopo kati ya Watendaji wa Wizara ya Madini na Nishati Tanzania ndio unaosababisha kuwepo migogoro mingi baina ya Wachimbaji wadogo na Makampuni makubwa ya uchimbaji.

“Kuna kesi nyingi ambazo  zipo baina ya Wachimbaji wadogo na Makampuni makubwa ya uwekezaji  zinazosababishwa na watendaji wa Wizara hiyo katika sehemu mbalimbali hapa nchini Waziri Mwenye dhamana na kuwa hana taarifa juu  Migogoro hiyo ambayo  inaleta mvutano mkubwa baina yapande hizo mbili”, Alisema Nicodemus Majabe.

Aidha alisema kuwa baadhi ya migogoro hiyo ni pale wachimbaji wadogo wanapoomba leseni za maeneo ya kuchimba lakini  wamekuwa wakipewa maeneo tofauti na yale waliyoomba huku yale ya awali wakipewa wawekezaji wenye uwezo.

“Kuna maeneo kama yale ya Ny’angwale, Mwazimba, Kishapu na Mengine mengi katika Wilaya ya Kahama ambayo yaliombwa na Wachimbaji wadogo kwa ajili ya kufanya shughuli za uchimbaji lakini maeneo hayo walipewa wawekezaji wakubwa”, Alisisitiza Makamu Mwenyekiti huyo.

Makamu Mwenyekiti huyo amemuomba Naibu Waziri anayehusika na kitengo cha Madini Stephen Masele kujitahidi katika kuondoa migogoro hiyo ambayo kwa kiasi kikubwa imekuwa ni kero kwa Wachimbaji wadogo na Wawekezaji wa migodi na Serikali kwa ujumla.

WACHIMBAJI WADOGO KATIKA LASHI YA NYANGARATA WAKIWA KAZINI

MSHIKAKI KUELEKEA SHAMBA

Mwendesha  boda boda  mkazi wa Tagamenda  wilaya ya  Iringa vijijini  akiwa amebeba abiria  wake wawili katika usafiri huo  jambo  ambalo ni hatari  kwa  usalama  wao kama alivyokutwa  leo na mtandao wa matukiodaima.com

CHIFU WA WAHEHE AWAKANA CHADEMA, AWATAKA WANA KALENGA KUPUUZA WAMCHAGUE GODFREY MGIMWA WA CCM


Chifu wa Wahehe, Abdu Sapi Mkwawa akiwakana Chadema
Wananchi wakishangilia
 
Mwigulu Nchemba akimuonesha aliyetobolewa jicho
Akimuonesha aliyemwagiwa tindikali
Akimnadi Godfrey Mgimwa
 CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimefanya uzinduzi rasmi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Kalenga, huku Chifu wa Wahehe, Abdu Sapi Mkwawa akikisuta Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa kutoa taarifa za uongo kwamba anamuunga mkono mgombea wao, Grace Tendega.

Katika uchaguzi huo, CCM imemsimamisha Godfrey Mgimwa, mtoto wa marehemu Dk William Mgimwa baada ya kushinda kwa kishindo kura za maoni za chama hicho dhidi ya wagombea wengine nane.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba ndiye aliyezindua kampeni hizo zilizofanyika katika kata ya Ifunda jimboni humo juzi.

Akishangiliwa na mamia ya wafuasi na wanachama wa chama hicho, Mkwawa alisema “ukoo wetu una historia isiyopingika ndani ya CCM, mimi ni kada wa CCM ninayehenzi historia hiyo na hata siku moja siwezi kufanya vinavyotangazwa na Chadema kwenye mitandao na magazeti.”

Huku akichanganya Kiswahili na Kihehe ili aeleweke vyema na watu wa jimbo hilo, alisema kama Chifu hakuwa na hiyana pale mgombea wa Chadema na viongozi wa chama chake walipokwenda kumjulia hali na kumuomba awe pamoja nao katika uzinduzi wa kampeni zao.

“Ilikuwa Februari 22 siku ambayo chama hicho kilikuwa kinazindua kampeni zake za uchaguzi; kama ambavyo angefanya kiongozi yoyote anayeheshimu mila za kabila lake, nami sikuwa na sababu ya kuwakatalia, nilichofanya ni kudumisha mila kwa kuzingatia kwamba mgombea wao ni mhehe pia” alisema.

Alisema “nafahamu kwamba uchaguzi huu ni huru na wa kidemokrasia, nilipoombwa kupanda katika jukwaa lao sikuona tatizo pia na nilipopewa fursa ya kuwasalimia nilisisitiza vyama vilivyosimamisha wagombea Kalenga viendeshe kampeni zao kwa amani na utulivu na huo ndio ujumbe ulionisukuma kupanda katika jukwaa lao.”

Alisema baada ya wananchi waliohudhuria uzinduzi wa kampeni hizo kuitikia mwito wake huo aliondoka jukwaani kwa kumtaka mgombea wao huyo aendelee na kampeni kwa amani na utulivu.

“Sikutoa baraka za kumtakia ushindi mgombea wa Chadema kwasababu mimi ni CCM na wao wanajua hivyo, wanajua pia kwamba sina ugomvi na chama changu; nilichowaomba ni kufanya kampeni zao kwa amani kwasababu kama Chifu nataka kuona uchaguzi huu hauwi na machafuko,” alisema.

Akizindua kampeni hizo, Nchemba alisema CCM imetawala nchi hii kwa miaka 37 na hakuna mtu hata mmoja aliyeuawa katika mikutano yake kama inavyotokea kwa Chadema.

“Katika kipindi cha miaka mitatu, watu nane wamafariki kwenye mikutano tofauti tofauti ya chama hicho,” alisema.

Akidhihirisha kwa umma wa Kalenga vurugu zinazofanywa na chama hicho, Nchemba aliwapandisha jukwaani watu wawili, mmoja akiwa ni yule aliyemwagiwa tindikali katika uchaguzi mdogo wa Igunga na wa pili aliyetobolewa jicho katika uchaguzi mdogo wa udiwani Kahama.

Nchemba alipongeza hekima na busara alizonazo Rais Jakaya Kikwete akisema zinasaidia sana kuifanya nchi hii iendelee kuwa ya utulivu na amani vinginevyo uvumilivu wa chokochoko dhidi ya CCM usingevumilika.

Kwa masikitiko makubwa, Katibu wa CCM Wilaya ya Mufindi, Miraji Mtaturu alionesha vibao virefu vitatu vye misumari alivyodai vilivyowekwa na wafuasi wa Chadema katika moja ya barabara za jimbo hilo ili kutoboa tairi za magari ya kampeni ya CCM.

“Tunawajua kwa majina wahusika wa tukio hili la kidhalimu; na taarifa hii tumekwishawasilisha Polisi, wanaendelea kuifanyia kazi; hii ni hatari kuendelea kushabikia chama kinachoshindwa kuwaeleza wananchi kitawafanyia nini na badala yake kuhamsisha vurugu,” alisema.

Akiomba kura kwa wapiga kura wa jimbo hilo, Godfrey Mgimwa alisema “mimi sio mropokaji kama wenzetu wa Chadema, mimi ni mtendaji, nipeni kura zenu nikamalizie kazi iliyoanza kutekelezwa na marehemu baba yangu.”

Alisema alikuwa mshauri mkuu wa marehemu baba yake wakati wa uhai wake kwasababu ya uwezo wake mkubwa kitaaluma.

“Mimi ni mtaalamu wa biashara, masoko na fedha; na mpaka nakuja kugombea ubunge nilikuwa mwajiriwa wa benki, kwahiyo marehemu mzee alikuwa anaujua uwezo wangu kichwani na alikuwa akitaka ushauri wa mara kwa mara kutoka kwangu,” alisema.

Alisema analifahamu vyema jimbo lake la Kalenga na amafanya utafiti uliomuwezesha kuyajua vyema matatizo ya wana Kalenga.

“Nipeni kura zenu zote, nazifahamu changamoto katika sekta ya elimu, afya, maji, barabara, mawasiliano na kilimo; nitazifanyia katika kwa kushirikiana na nyinyi kuzitatua kwa kupitia Ilani yetu ya CCM,” alisema.

Wengine waliopata fursa ya kuhutubia mkutano huo ni pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu na wabunge mbalimbali wa chama hicho mkoani hapa.

Wabunge hao ni pamoja na Naibu Waziri wa Wanawake Jinsia na Watoto, Dk Pindi Chana, Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa, Leadiana Mng'ongo na Ritta Kabati na Mbunge wa Mufindi Kusini Medrad Kigola.