Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

December 31, 2014

Breaking news Tetemeko kubwa latokea Njombe usiku huu

Wakati wananchi wa Mkoa wa Njombe Na mikoa mbalimbali ya nyanda za juu kusini wakisubiri kuaga mwaka 2014 na kuukaribisha mwaka 2015 ,wananchi hao wamekumbwa na taharuki kufuatia tetemeko kubwa lililopita kwa muda wa dakika moja .

Tetemoko hilo limetokea usiku huu Majira ya saa 4:49 hivi wakati wananchi wa mji wa njombe wakiwa ktk hekaheka za kuaga mwaka japo maeneo mengine ambayo tetemeko hilo limepita ni pamoja na Mafinga wilaya ya Mufindi na Ludewa Mkoa wa Njombe hadi sasa bado haijafahamika kama kuna madhara kwa binadamu ama lah

HERI YA MWAKA MPYA 2015

Tunawatakia heri ya mwaka mpya 2015, Kila wakati tumia maziwa ya Asas. Miaka miwili sasa twaongoza nchini Tanzania kwa ubora


BUNDI LATUA CHADEMA IRINGA VIONGOZI WAPELEKANA POLISI


Bw  Frank Nyalusi
 Na Matukiodaimablog
HALI  ya  kisiasa  ndani ya  chama  cha Demokrasia na maendeleo (chadema)  mkoa wa Iringa si shwari  baada ya mwenyekiti wake mkoa  wa Iringa Mustapher Msowela  kumfikisha polisi  mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya Iringa mjini , Frank Nyalusi

Nyalusi  ambae  pia ni  diwani  wa kata ya Mvinjeni jimbo la Iringa mjini juzi alitiwa nguvuni na  jeshi la Polisi kabla ya kuachiwa kwa dhamana.
 
Nyalusi aliyeshitakiwa katika kituo cha Polisi cha kati cha mjini Iringa jana, anatuhumiwa kumtusi mwenyekiti wake huyo wa mkoa kupitia mitandao ya simu; matusi yanayoendelea kuchunguzwa na jeshi hilo.
Nyalusi amekamatwa kwa tuhuma hiyo ikiwa ni siku chache tu baada ya kudaiwa kutoa tuhuma za uongo kwa lengo la kujipatia umaarufu dhidi ya mfanyabiashara maarufu wa mjini Iringa, Salim Asas ambaye pia ni Kamanda wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Iringa.
 
Katika mkutano wa hadhara uliofanywa na Chadema Desemba 21 kwenye uwanja wa Mwembetogwa mjini Iringa, Nyalusi ambaye pia ni diwani wa kata ya Mivinjeni alitoa tuhuma zinazowahusisha vijana watatu ambao hata hivyo hakuwataja majina kwamba walitumwa na Asas kwenda kumuua.
 
Asas kwa kupitia kwa wakili wake, Alfred Kingwe amekanusha tuhuma hizo alizoziita ni za kipuuzi ambazo haziwezi kubebeka hata kwa mzani mdogo wa kupimia madini.
 
Ili kumsafisha mteja wake, Kingwe alisema ndani ya siku 14 toka akabidhiwe hati ya madai (Demand Note), Nyalusi anatakiwa kuitisha mkutano katika eneo lile lile alilotolea tuhuma hizo na kuzikanusha vinginevyo atafikishwa mahakamani.
 
Akizungumza na wanahabari jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi alisema;  “Kuhusu tukio la kumtukana mwenyekiti wake wa mkoa, Nyalusi alikamatwa jana mara baada ya Msowela kuwasilisha malalamiko yake polisi, akahojiwa na kuachiwa baada ya kukamilisha taratibu za dhamana.”
 
Alisema jeshi la Polisi linaendelea kuchunguza tukio hilo la kijinai na endapo litathibitika kuwa la kweli, Nyalusi ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mivinjeni mjini Iringa atafikishwa mahakamani.
 
Kuhusu tukio linalomuhusisha na Asas, Kamanda Mungi alisema jeshi la Polisi limefanya mahojiano ya awali na wahusika hao.
 
“Jambo hili lipo, tunachunguza; yapo maneno Nyalusi ameyatamka kwenye mkutano wao wa hadhara kwamba ametishiwa kuuawa, ametumiwa watu watatu kwenda kumuua wakiwa na visu. Kumtishia mtu ni kosa la jinai na kumtuma mtu kwenda kumdhuru mtu mwingine ni kosa la jinai, kwahiyo tunachunguza” alisema.
 
Alisema katika mazingira ya uwazi, Polisi inachunguza suala hilo ili kujua Nyalusi alitishiwa katika mazingira gani; alitishiwa na nani na kwanini hakwenda kutoa taarifa hiyo Polisi na kufungua kesi ili Polisi iwakamate wahusika na kulinda maisha yake.
 
“Lakini tunajaribu kuangalia kama hakutishiwa na ametamka vile katika mkutano wa hadhara, lengo lake lilikuwa ni nini na kama anajua madhara yake kwa jamii iliyosikia taarifa hiyo ni yepi,” alisema.
 
Alisema kama itabainika taarifa zilizotolewa na Nyalusi ni za uongo, sheria itachukua mkondo wake na kama itadhihiri ni za kweli sheria pia itachukua mkondo wake.
 
MWISHO.

BREAKING NEWS POLISI DAR WAUA KWA RISASI MTUHUMIWA

Mtuhumiwa  ambae  ameuwawa  na  polisi  jijini Dar esa Salaa asubuhi ya  leo  wakati akijaribu  kuwatoroka
Askari   wakisaidiana  kuutoa  mwili  wa mtuhumiwa aliyeuwawa  muda  mfupi  leo  wakati akijaribu  kuwatoroka  polisi katika mahakama  ya  Kisutu

December 30, 2014

HABARI KWA UFUPI, WATU 6 WAFA AJALINI MKOANI KILIMANJARO

Watu  6  wamefariki  dunia  na  wengine   zaidi ya 10  kujeruhiwa  vibaya  baada  ya magari  mawili  kugongana  eneo la  uchira  Moshi  mkoani  Kilinanjaro

UNYAMA MWANZA MTOTO ALBINO ATEKWA

Bw .Ernest Njama Kimaya (42) ni mwenyekiti wa chama cha albino Taifa
Nchini Tanzania katika Kijiji cha Ndami, tarafa ya Mwamashimba wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza watu wasiofahamika wamevunja nyumba na kumteka mtoto mwenye ulemavu wa ngozi maarufu kama albino na kutoweka naye.

Watu hao walivamia nyumba ya wazazi wa mtoto Pendo Emmanuel, mwenye ulemavu wa ngozi wakiwa na mapanga na kisha kutoweka naye gizani baada ya kuwazidi nguvu wazazi wake.

Emmanuel Shilinde mzazi wa mtoto huyo ameieleza polisi kuwa majira ya saa nne usiku watu wawili waliuvunja mlango wa nyumba yake kwa jiwe wakamchukua mtoto kwa nguvu kisha wakakimbilia gizani kwa pikipiki.

Kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi mkoani mwanza Valentino Mlowola , ameitaarifu BBC kuwa leo ni siku ya tatu na polisi bado ina matumaini ya kumpata akiwa hai motto huyo, kwa kuwa bado hawajaupata mwili wake akiwa amepoteza uhai.

 Msako unaendelea na tayari kuna watu watano wanazuiliwa na polisi ili kusaidia kufahamu mtoto huyo yuko wapi.

Takwimu za kuanzia mwaka 2006 zinaonyesha kuwa Albino 74 wameshauawa kikatili, huku 56 wakinusurika kifo, na kati yao 11 wamepata ulemavu mwingine wa kudumu.

BREAKING NEWS MIILI 40 YA ABIRIA WA NDEGE YA AIR ASIA YAPATIKANA BAHARINI LEOKufuatia kupotea kwa ndege ya shirika la ndege la Asia ndege namba QZ8501At ,miili arobaini imeopolewa kutoka baharini katika utafutaji wa mabaki ya ndege hiyo na utafutaji unaendelea.

Miili hiyo ilionekana ikielelea karibu na taka za bahari pwani ya Indonesia,eneo la Borneo moja ya eneo la utafutaji mabaki ya ndege hiyo.Na taarifa kutoka serikali ya Indonesia zimethibitisha kwamba miili hiyo inatoka katika ndege iliyopotea.

Ndege hiyo aina ya Airbus A320-200,ilikuwa imebeba abiria mia moja na sitini na wawili ikitokea Surabaya nchini Indonesia kuelekea Singapore,ilipotea siku ya Jumapili.
Utafutaji wa mabaki ya ndege hiyo umeingia katika siku ya tatu,na eneo la utafutaji limeongezwa na kufikia kanda kumi na tatu hii inashirikisha nchi kavu na baharini.

Wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliooneshwa wazi kwenye runinga ya taifa la Indonesia picha za taka bahari zilioneshwa zikiwa zimechanganyika na mabaki ya miili ya abiria ikielea majini.

Ndugu wa mabaki hayo walipoona picha hizo walipigwa na fadhaa kuu na walionekana kushtushwa na picha hizo.Baadaye askari wa majini nchini Indonesia wameeleza kuwa miili hiyo arobaini iliopolewa na meli ya kivita .
 Sala za kuwaombea waliokuwa wasafiri katika ndege hiyo zinaendelea 

Mkurugenzi mtendaji wa AirAsia Fernandes ali ingia katika mtandao wa twitter na kueleza huzuni yake kwa ndugu waliopoteza ndugu zao katika ndege QZ 8501. Na kwa niaba ya shirika la ndege la AirAsia ametuma salamu za rambi rambi .

Utafutaji miili na mabaki ya ndege hiyo unashirikisha meli thelathini,ndege kumi na tano na chopa saba.

WIZARA YA NISHATI NA MADINI YATOLEA UFAFANUZI UDALALI WA WAZIRI PROF MUHONGO

Waziri Prof Muhongo 

Katika gazeti la moja la  kila  siku  hapa nchini la Jumatatu tarehe 08 Desemba, 2014 ziliandikwa habari kuhusu Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo (Mb) chini ya kichwa cha habari “Wanaomtetea Muhongo Wajibu haya”. 

Hoja zilizotolewa katika gazeti hilo zililenga kupotosha ukweli. Wizara inapenda kutoa maelezo kuhusu hoja zilizotolewa kama ifuatavyo:

Utendaji wa Wizara chini ya Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo (Mb)

Taarifa za gazeti hilo zilieleza kuwa utendaji wa Wizara ya Nishati na Madini hasa katika uongozi wa Waziri Muhongo umekuwa ni wa kukatisha tamaa. Moja ya mifano iliyotolewa ni kuendelea kuwepo kwa wachimbaji madini wanaozidi kutorosha madini kwa nia ya kukwepa kodi. 

Hoja hii haina ukweli wowote kwani chini ya uongozi wa Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo (Mb) utendaji wa Wizara umeimarika kwa kiasi kikubwa. 

Chini ya Uongozi wake kumekuwepo na uwajibikaji mkubwa kwa watumishi wa wizara ili kuhakikisha kuwa wanawatumikia wananchi ipasavyo.

  Ni katika kipindi chake kumekuwepo na uanzishwaji wa madawati ya ukaguzi wa madini katika viwanja vikubwa vya ndege vya JNIA,

 KIA na Mwanza chini ya Wakala wa Ukaguzi wa madini (TMAA) ili kudhiditi wachimbaji madini na watu wengine wenye nia ya kutorosha madini nje ya nchi bila kuzingatia sheria. Kutokana na hatua hiyo madini mbalimbali yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 15 yameweza kukamatwa. 

Madini yaliyokatwa bila kuwa na vibali halali yametaifishwa na Serikali. Serikali ilianza kuuza baadhi ya madini yaliyokamatwa kwa njia ya mnada kwenye Maonyesho ya Vito yaliyofanyika Mjini Arusha kuanzia tarehe 18 - 20 Novemba, 2014. 

Katika mnada huo jumla ya zaidi ya shilingi milioni 70 zilipatikana na kuingia Serikalini. Serikali itaendelea kupiga mnada madini mengine yaliyokamatwa kwa manufaa ya taifa. 

 Wizara inaendelea kuimarisha udhibiti ili kuhakikisha kuwa mtu yeyote anayekusudia kutorosha madini anakamatwa na kuchukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na madini yake kutaifishwa na Serikali. Katika kusimamia sheria na taratibu, chini ya Uongozi wa Prof.Muhongo, 

  Wizara imedhibiti tabia ya kuchukua vitalu vya madini na kuhodhi ili wale tu wanaozingatia masharti ya leseni ndio waendelee kuvifanyia kazi vitalu. 

Hili limewaumiza waliokuwa na tabia hiyo ambao kimsingi walikuwa wanavunja sheria. 

 Baadhi ya vitalu vilivyopokonywa vimekuwa vikigawiwa kwa wachimbaji wadogo.Hivyo, si kweli kwamba utendaji wa Wizara ya Nishati na Madini chini ya Prof. Sospeter Muhongo (Mb) ni wa kukatisha tamaa katika kudhibiti utoroshaji wa madini nje ya nchi na katika ukiukwaji wa masharti ya leseni mbalimbali za madini kama ilivyodaiwa.

Upitiaji Mikataba ya Madini

 Taarifa za moja kati ya magazeti ya  kila  siku nchini  Tanzania ya  Jumatatu tarehe 08 Desemba, 2014 zilieleza kuwa chini ya Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo (Mb) Serikali imeshindwa kupitia mikataba ya madini ili taifa linufaike zaidi.

 Taarifa hizo si za kweli zinalenga kupotosha umma.

Ukweli ni kuwa chini ya Uongozi wa Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo (Mb), Wizara imepitia mikataba ya madini kwa kufanya majadiliano na Kampuni za uchimbaji madini zenye mikataba ili kurekebisha vipengele vya mikataba ambavyo vinalenga kuleta manufaa zaidi kwa Taifa. 

 Kazi hiyo imefanyika kwa Kampuni zote zenye mikataba na tarehe 9 Oktoba, 2014 Kampuni ya Geita Gold Mine (GGM) imetiliana saini mkataba wa kurekebisha vipengele katika mkataba uliosainiwa huko nyuma baada ya majadiliano kukamilika.

 Aidha, majadiliano na Kampuni ya ACACIA (zamani Kampuni ya African Barrick Gold –ABG) yamekamilika na kilichobaki ni pande mbili (Serikali na Kampuni) kusaini marekebisho yaliyofanyika kwa ajili ya mikataba ya migodi yake ya Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara.

  1. KUKATIKA KWA UMEME

Kukatika kwa umeme kunasababishwa na kuzeeka kwa miundombinu ya usafirishaji na usambazaji umeme. Ikumbukwe kuwa, kwa kipindi cha karibu miaka kumi TANESCO iliwekwa chini ya PSRC kwa nia ya kubinafsishwa mwaka 1997 – 2007.

 Katika kipindi hiki TANESCO haikuruhusiwa kuwekeza wala kufanya ukarabati wa miundombinu yake hivyo hali hiyo ilipelekea kuchakaa kwa miundombinu hiyo ikiwemo mfumo wa usafirishaji na usambazaji wa umeme.

 Hata hivyo baada ya Serikali kubadili mtazamo wake wa kulibinafsisha Shirika, TANESCO mipango kabambe ya kufanya ukarabati wa miundombinu hiyo na kujenga mipya ili kuwa na mfumo wa usafirishaji na usambazaji umeme ulio wa uhakika.

 Kazi hiyo inaendelea katika sehemu mbalimbali nchini ikiwemo jiji la Dar es Salaam ambako kazi ya kukarabati na kupanua miundombinu ya usambazaji umeme inaendelea. Aidha, TANESCO ilishaelekezwa kutoa taarifa kwa umma kuhusu katizo lolote la umeme lililopangwa kwa ajili ya matengenezo ya miundombinu ya umeme

. TANESCO imekuwa ikifanya hivyo kwa kutumia vyombo vya habari vikiwemo televisheni, radio na magazeti na pia kwa kutumia magari ya TANESCO kufikisha taarifa kwa maeneo yanayoathirika. Kwa upande wa katizo la umeme usiotarajiwa, TANESCO inacho kikosi cha dharura ambacho watumishi wake wanafanya kazi masaa ishirini na nne kwa zamu ili kuhakikisha kuwa hitilafu ndogondogo zinatatuliwa mara moja zinapojitokeza. Jamii ya Watanzania wanalishuhudia hilo.

  1. DENI LA TANESCO LAPAA.

Mpaka kufikia mwanzoni mwa mwaka 2014, deni la TANESCO lilikuwa limefikia takribani Shilingi bilioni 695.30. TANESCO kwa kutumia vyanzo vyake vya fedha kutokana na ukusunyaji wa maduhuli ndani ya kipindi cha miezi 11 imepunguza deni hilo mpaka kufika takribani Shilingi bilioni 355.11. Kukua kwa deni la TANESCO kulisababishwa na hali ya ukame uliolikumba taifa kuanzia miaka ya 2011 ambapo TANESCO ililazimika kununua umeme aghali kutoka kwa wazalishaji wa umeme binafsi ikiwemo mitambo ya kukodi ya dharura. Deni hilo lilikua kama ifuatavyo:

Mwaka Deni (Bilioni Sh.)

2011           538.47

2012            563.02

2013           695.30

2014 (9 Disemba) 355,11

TANESCO imeongeza ufanisi wake katika kukusanya maduhuri na kufikia kiwango cha asilimia 97 na fedha inayopatikana inatumika kupanua huduma ya umeme nchini, kuendesha Shirika na kulipa madeni inayodaiwa.

Ukweli ni kwamba deni la TANESCO limeshuka kwa kiasi kikubwa na kwa sasa TANESCO imeweka mkakati maalumu wa kuwalipa wadeni wake wakubwa kiasi cha Shilingi bilioni tatu kwa wiki kwa kila mdai, hivyo ni matarajio ya Shirika kumaliza deni hilo mwaka kesho (2015).

  1. NCHI ITASONGA MBELE

Wazo la kuanzishwa kwa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) lilibuniwa na watumishi na viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini mwaka 2005/6 chini ya uongozi wa Nazir Karamagi akiwa Waziri wa Nishati na Madini. Taratibu za kuanzishwa kwa REA zilikamilika mwaka 2007 ambapo REA ilianza kutekeleza majukumu yake.

Mheshimiwa Sospeter Muhongo baada ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Nishati na Madini ameisaidia REA kupata fedha kutoka kwa wadau mbalimbali wa maendeleo na hivyo amesaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza kwa kasi ya kupeleka huduma ya umeme vijijini.

Aidha, Ili kufikia lengo la kuwaunganishia umeme asilimia 30 ya watanzania ifikapo mwaka 2015, Chini ya uongozi wa Waziri Muhongo Serikali kupitia TANESCO, ilipunguza gharama za kuunganisha umeme wa njia moja (single phase) kwa wateja wadogo kwa wastani wa kati ya asilimia 30 na 77 kama ifuatavyo:

  1. Kwa wateja watakaojengewa njia moja (single phase) kwenye umbali usiozidi mita 30 bila kuhitaji nguzo, katika maeneo ya vijijini watalipa Shilingi 177,000 na wa mijini watalipa Shilingi 320,960 badala ya Shilingi 455,108 zinazolipwa na wateja hao kwa sasa.

  1. Kwa wateja watakaojengewa njia moja (single phase) na kuwekewa nguzo moja, katika maeneo ya vijijini ni Shilingi 337,740 na wa mijini ni Shilingi 515,618 badala ya Shilingi 1,351,884 zinazolipwa na wateja hao kwa sasa.

  1. Kwa wateja watakaojengewa njia moja na kuwekewa nguzo mbili katika maeneo ya vijijini ni Shilingi 454,654 na wa mijini ni Shilingi 696,670 badala ya Shilingi 2,001,422 zinazolipwa na wateja hao kwa sasa.

Kwa ujumla katika kipindi hiki huduma ya umeme nchini imepanuka na kuwa bora zaidi kuliko siku za nyuma. Ni matarajio ya Serikali kuwa huduma hii itazidi kuwa bora zaidi katika siku chache zijazo kutokana na juhudi kubwa zinazoendelea katika sekta ndogo ya umeme.

  1. DALALI WA FEDHA ZA ESCROW

Waziri wa Nishati na Madini ndiye msimamizi mkuu wa masuala yanayohusu sekta za Nishati na Madini nchini. Mtambo wa IPTL ulijengwa kwa ajili ya kufua umeme unaotumiwa na jamii ya watanzania.

  Kuwepo kwa mgogoro kungeweza kuondoa azma ya uwepo wa mtambo huo ya kufua umeme ili kuliepusha Taifa kuingia katika mgawo wa umeme kutokana na upungufu wa upatikanaji wa nishati hiyo, hivyo lilikuwa ni jukumu lake kuona kuwa mgogoro wa wawekezaji wa mitambo ya IPTL unakwisha ili mitambo iendelee kutoa huduma ya umeme kwa Taifa.

  Jukumu la Waziri ni kusimamia Sera, Sheria na taratibu katika sekta anazozisimamia. Katika kufanya hivyo, Waziri hukutana na wadau na kujadili masuala kwa uwazi bila kificho kwa nia ya kujenga nchi na kuhakikisha kuwa maslahi ya Taifa ndiyo kipaumbele.

 Kwa hiyo mikutano na Wadau ikiwa ni pamoja na wawekezaji hufanyika si kwa udalali. Suala la fedha za akaunti ya Escrow lilihusu uamuzi wa mahakama iliyojiridhisha kuwa mnunuzi wa hisa zote za VIP na MECHMAR ni halali na alitakiwa kukabidhiwa mali na madeni ya IPTL. Mali ni pamoja na kiasi cha fedha stahiki kwenye Akaunti ya Escrow ambazo hata hivyo ilidhihirika kuwa hazitoshi kukidhi deni halali.

Akaunti hiyo ilikuwa na Sh. 182 bilioni wakati malipo yaliyokubalika kwa pande zote (IPTL na TANESCO) kwa mujibu wa maamuzi ya ICSID I yalikuwa Sh. 306 bilioni. Kumwita Waziri wa

Nishati na Madini kuwa ni dalali ni kupotosha ukweli.

 
   

BUNDI ATUA YANGA ?

-Awafunga watumishi Yanga: Aagiza Polisi ‘Marafiki’ kuwakomesha
Baada ya kumtimua kocha Mkuu wa timu yake na baada ya kubwaga chini sekretariati ya klabu hiyo, Mwenyekiti wa Klabu ya Young Africans Sports Club (Yanga) Bw. Yusuf manji, ameamua kuwafanyizia baadhi ya waliokuwa watumishi wa Klabu hiyo akiwemo Beno Njovu, Katibu Mkuu aliyepita.
Wakandamize haswa

Kulingana na mawasiliano yaliyonaswa na makachero wetu kati ya Mwenyekiti huyo na viongozi wa juu wa Klabu hiyo, Manji amewapa maelekezo wanasheria wake na Sekretariati ya sasa kuwafungulia mashtaka Sekretariati iliyopita  kwa madai  ya  ufujaji pesa, huku akiwataka viongozi hao kutumia ‘marafiki’ zao waliooko katika jeshi la polisi ‘kuhakikisha wanashugulikiwa’

Katika mawasiliano hao kupitia email ya tarehe 22 Desemba , Manji pia anamwagiza mtu aliyetambulika kuwa mhasibu  anayaenda kwa jina la Amit kugaramia ‘maagizo hayo yote’, na kumpa taarifa kila siku.

Vyombo vya habari kutumika
Manji pia  ameagiza wafanyakazi hao wazamani ‘wachafuliwe’  kupitia kampeni kali magazetini, huku akielekeza ‘Press Release’ yenye saini yake itolewe ikionesha ‘masikitiko yake’.

Adhabu mbele, hukumu nyuma
Huku akitoa maagizo wafanyakazi hao washugulikiwe ipasavyo na polisi ‘marafiki’ zake, Bwana Manji ametupilia mbali haki za wafanyakazi hao kusikilizwa kukiwa hakuna uchunguzi wowote uliokwishafanyika kuhusu madai yake dhidi ya watumishi hao zaidi ya hisia zake mwenyewe na Sekretariati mpya inayotekeleza kila alitakalo bila kuhoji.

 Maagizo yazua mpasuko ndani ya kamati tendaji
Kufuatia maagizo ya Manji, mmoja wa watumishi wapya aliyetambulika kama Frank Chacha alitekeleza maamuzi hayo ambayo mwenyekiti huyo alikuwa amesema hayapingiki wala hayahojiki kwa email yake, huku wakifungua kesi katika kituo cha Polisi kati Dar es salaam na kufanikiwa kuweka wafanyakazi wawili ndani huku wakiendelea kumuwinda Beno Njovu
Lakini masaa machache baada ya hatua hizo, kuna dalili kuwa baadhi ya viongozi ndani ya klabu hiyo wanapinga vikali hatua hizo za Manji na wametishia ‘kuaachia’ ngazi.

Mpasuko huo ndani ya Yanga umedhihirishwa na email kutoka kwa Bwana Omar, Mkurugenzi mpya wa Fedha na Utawala akimjulisha Manji kuwa jana Jumanne, baada ya kutekeleza maagizo ya Mwenyekiti huyo alipokea simu kutoka kwa  Isaac Chanji, mjumbe wa Kamati Tendaji akitishia kuwa  hatua ambazo zilikuwa zimeshachukuliwa zilikuwa za hatari kwa Klabu hiyo na kuwa yeye Chanji na wajumbe wengine wengelazimika kuwaachia akina Omari na Chacha timu hiyo.

Maswali tata
Kufuatia hatua hii ya Manji mtu unaweza kujiuliza maswali kadhaa:
1.       Je kwa nini Yanga inakuwa na kesi kila wakati? Gharama za kesi hizi, ambazo nyingine siyo za lazima, si mzigo usiokuwa na faida kwa Yanga? Mara wachezaji, makocha, na Sekretariati za nyuma.

2.       Ni dhahiri kuwa hata kama kesi hii ya sasa ina msingi wowote, basi uchunguzi ungetangulia. Lakini, labda kwa jeuri ya hela, Manji ameshawahukumu watumishi wale na ni wazi kuwa yuko tayari hata kupindisha sheria ili afikie lengo lake.

3.       Lengo la Manji hasa ni nini? Anajaribu kuwaadhibisha hawa watumishi kweli au ni kujenga hoja za Mkutano Mkuu wa Klabu hiyo unaotegemewa kufanyika Januari 2015 kwa kujenga mazingira ya kuwasahaulisha wanachama wa Yanga baadhi ya  ahadi alizotoa na ambazo hadi sasa bado ni ahadi hewa  tu?

Mtandao  huu wa matukiodaima unaendelea  kufuatilia sakata   hili  ili  kupata  ukweli  wake na nini  hasa  chanzo 

THE MBONI SHOW YAANZA KUUNGURUMA JANUARY 2 NDANI YA TBC

Mkurugenzi wa Mboni Show, Mboni Masimba (wa pili ktoka kulia) akizungumza na waandishi wa habari jana katika  ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam wakati akitangaza kuanza kwa msimu wa tatu wa kipindi chake 'The Mboni Show' kinachotarajia kuanza Jan 2, 2015. Kushoto ni kiti Simpompa na kuanzia kulia ni Afisa Masoko wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (PSPF) Magira Werema na Kaimu Mkurugenzi wa Masoko TBC,Bw.Fadhili Chilumba.
Kutoka Kulia Afisa Masoko wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (PSPF) Magira Werema akizungumza wakati wa uzinduzi kipindi cha Mboni Show uliofanyika katika Ukumbi wa Idara Habari Maelezo jijini Dar es Salaam. Pembeni ni Kaimu Mkurugenzi wa Masoko TBC,Bw.Fadhili Chilumba pamoja na Mkurugenzi wa Mboni Show, Mboni Masimba.
Na Mwandishi Wetu.
Mkurugenzi wa Mboni Show, Mboni Masimba ameamua kuhamishia kipindi cha Mboni show katika kituo cha utangazaji cha Taifa (TBC) kutoka EATV ili kuvutia watazamaji wengi na wapya kwa wazee pamoja na vijana.
Kipindi cha Mboni Show kitaanza kurushwa TBC kuanzia January 2 mwaka 2015 siku ya
Ijumaa saa 3 Usiku-4 Usiku na marudio Jumanne saa 9:00 mchana-10:00mchana.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar ndani ya ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Mboni Masimba ametoa shukrani kwa EATV kwa ushirikiano wao kwa kipindi chote alichokuwa nao,na kusema kuwa amehamishia kipindi cha Mboni Show katika kituo cha TBC ili kuvutia watazamaji wengi hakuna atakaye tumia jina la Mboni Show na hakuna kitakachomkwamisha kwa vile ana hati miliki.
“Nimeamia TBC kwa kuwa nahitaji watazamaji wengi ,wote wazee na vijana na hakuna atakaye tumia jina langu la Mboni Show kwa kuwa nina hati miliki ya jina hili”alisema Mboni.
Kwa upande wake,Kaimu Mkurugenzi wa Masoko TBC, Bw.Fadhili Chilumba amesema wamefurahi kuwepo kwa Mboni Show katika kituo cha Taifa(TBC) na kutoa wito kwa mashabiki kuweza kuwadhamini watu kama wakina Mboni na wanamkaribisha sana.
Nao wadhamini wa Mboni Show,Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (PSPF) Magira Werema wamesema wanamwezesha Mboni kuwepo hewani ili kuhamasisha,kuelimisha pamoja na kuburudisha umma wa Watanzania(.na
Cathbert KajunaBlog)

RAIS KIKWETE AHANI MSIBA WA SHEIKH ALI MZEE KOMORIAN KARIAKOO, DAR ES SALAAM

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiifariji familia ya Marehemu Sheikh
Ali Mzee alipokwenda kuhani msiba huo jana Jumapili Desemba 29, 2014.Marehemu Sheikh Komorian
alifariki juzi Jumamosi Desemba 28, 2014 na kuzikwa jana Jumapili
Desemba 29, 2014
:Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishiriki katika dua na familia ya
Marehemu Sheikh Ali Mzee alipokwenda kuhani msiba huo jana Jumapili
Desemba 29, 2014. Marehemu Sheikh Komorian
alifariki juzi Jumamosi Desemba 28, 2014 na kuzikwa jana Jumapili
Desemba 29, 2014
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiifariji familia ya Marehemu Sheikh
Ali Mzee alipokwenda kuhani msiba huo jana Jumapili Desemba 29, 2014.
Marehemu Sheikh Komorian
alifariki juzi Jumamosi Desemba 28, 2014 na kuzikwa jana Jumapili
Desemba 29, 2014(picha na Ikulu)

HABARI KWA UFUPI LEO ,SACCOS YA SOKO KUU IRINGA YAFUNGWA KWA DENI LA TSH MILIONI 9

KAMPUNI ya  Udalali  ya Majembe  imeifungwa kwa  muda wa  zaidi ya miezi  mitatu  sasa  ofisi  ya  chama  cha  kuweka na  kukopa cha  Soko kuu Saccos  baada ya  kushindwa  kulipa deni la pango la nyumba  kiasi cha Tsh milioni 9

Mmoja kati ya  viongozi wa Saccos   hiyo  ameuthibitishia  mtandao huu wa matukiodaima  kuwa ni  kweli  wanadaiwa  deni   hilo na  wapo katika mchakato wa kulipa  deni  hilo  ili  kuweza  kufungua tena  ofisi  hizo  zilizopo  jengo la Highlands  barabara  ya Uhuru mjini Iringa

 

WADAU CHIPUKIZI WA MTANDAO HUU

wadau  chipukizi wa matukio  daima Ahmed Arif na mdogo  wake  wakikutakia  heri ya  Mwaka mpya  wa  2015 wewe  mdau  wa mtandao  huu wa  www.matukiodaima.co.tz

Mwaka unakatika....Tumesonga mbele ama nyuma???

 Amani, Heshima na Upendo kwa wana-blog wote.

Kwanza namshukuru MUNGU kwa baraka ya uhai ambayo mimi nawe tunayo mpaka sasa.
Pili nikupe pole kwa harakati za maisha ambazo sote twazipitia kufanikisha yale mema tupendayo.

 Ni harakati kubwa sana hasa katika kusonga na maisha yetu ya kila siku na pia kuendeleza gurudumu hili la blogs

Nimekuwa nikituma makala, vipindi na kazi zangu kwenu nanyi mmekuwa wakarimu sana kuzipokea. 

Ushirikiano ambao umenifanya nizidi kujivunia kuwa mmoja wa bloga
Lakini pia, najivunia sana kuwasiliana na kila mmoja wetu hivi sasa ili kuanzisha mjadala wa changamoto zilizo mbele yetu kama JAMII YA WANA-BLOG wenye lengo la kuigusa jamii.

Ningependa tuanze kwa kujiuliza, Je! Tunasonga mbele ama nyuma katika harakati zetu.

Nashukuru kwa blogs na tovuti mpya ambazo zinachipuka na kuendeleza nia njema ya kuigusa jamii. Kaka Luta Kamala aliwahi kuandika akijuliza KWANINI TUNA-BLOG? (Bofya hapa) na hata Kaka Chambi Chachage aliuliza kama uwepo wa blogu zetu unakuza ama kufifisha tasnia nzima ya uandishi (Ipitie hapa)

Jibu halisi tunalo mioyoni mwetu kulingana na dhamira tulizonazo.
Lakini kwa ujumla, haijalishi ni sababu gani ilikufanya u-blog, mwisho wa safari sote tunajikuta na zao moja ama "mlaji" mmoja ambaye ni JAMII.

Bloga awekaye picha anataka kuionesha jamii alichokiona.
Bloga ahabarishaye anataka kuihabarisha jamii. Yule aandikaye Utambuzi anataka jamii ijitambue. Anayeweka kumbukumbu ni sababu anataka jamii ije isome baadaye. Atangazaye biashara anataka jamii ijue palipo na huduma ama biashara husika. Afunzaye mapishi, mitandao, mavazi, mitindo nk, woote wanalenga katika kuielimisha jamii.

Kwa maana nyingine sote twaiandikia JAMII.
Na hili ni lengo jema.

Lakini swali linarejea kuwa......
Mwaka huu ambao unaomalizika wiki hii unaonekana kuwa hatua gani kwetu?
Logo hapo juu inaonyesha hatua iliyopihgwa katika siku za mwisho za mwaka. Kuanzishwa kwa mtandao wa bloga ambao (ukitumiwa vema) utakuwa chachu ya mabadiliko ya nchi hasa kwa mwaka huu wa uchaguzi.
Ninalowaza ni hili
.....
Vipi tunaweza kuweka nguvu na jitihada zetu pamoja kuweza kuitumikia vema na kwa ufasaha jamii yetu???

Mafanikio ya bloga mmoja mmoja yanaweza kudhihirisha kuwa TUNAWEZA, lakini tunalostahili kufanya sasa, ni kushirikiana na kuwa makini katika kila jema tutendalo.

Tunapoumaliza mwaka 2014, tuangalie nyuma na kujiuliza, mwaka unakatika....Tumesonga mbele ama nyuma??


Na jibu la swali hili, liwe CHANGAMOTO YETU sote

Baraka kwenu nyote

Heri ya Mwaka Mpya 2015

December 29, 2014

KAMANDA WA UVCCM IRINGA ,MWAKALEBELA AMWANGA VIFAA VYA MICHEZO IRINGA

Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Iringa (IRFA), Cyprian Kwihyava akikadhi vifaa vya michezo vilivyotolewa na Frederick Mwakalebela kwa timu zinazoshiriki ligi ya wilaya Iringa Mjini 
Gangilonga Fc ikipokea jezi vifaa vyake
Mkwawa FC ikipokea vifaa vyake
Ilala FC ikipokea vifaa vyake
Miyomboni FC ikipokea vifaa vyake
Baadhi ya mameneja wa timu ziatakazoshiriki ligi hiyo

KAMANDA wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Iringa Mjini, Frederick Mwakalebela ametoa tena zaidi ya Sh Milioni 14 kudhamini ligi ya soka ngazi ya wilaya, Iringa Mjini.
Hii ni mara ya pili kwa mdau huyo wa soka aliyewahi pia kuwa Katibu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuidhamini ligi hiyo ambayo kabla yake ilikuwa ikichezwa bila washindi kupata zawadi yoyote ile.
Katibu Msaidizi wa Chama cha Soka Iringa Mjini (IMFA), Rashid Shungu alisema katika hafla fupi ya uzinduzi wa ligi hiyo mjini hapa jana kwamba: “baada ya Mwakalebela kujitokeza kudhamini ligi hii, timu zote zinapata vifaa vya michezo, mshindi wa kwanza hadi wa tatu wanapata zawadi na waamuzi na viongozi wanaosimamia ligi hiyo wanapata posho.
Alisema kwa kupitia udhamini huo, mshindi wa kwanza anapata kikombe, Sh 500,000 na mipira mitano, mshindi wa pili anapata sh 300,000 na mipira mitatu na mshindi tatu anapata Sh 200,000 na mipira miwili.
Akikabidhi vifaa (jezi na mipira kwa timu hizo), Mwenyekiti wa Chama cha soka Mkoa wa Iringa (IRFA), Cyprian Kwihyava aliahidi kumuongezea mshindi wa kwanza wa ligi hiyo, Sh 500,000 na hivyo kufanya mshindi atakayepatikana mwaka huu kuondoka na jumla ya Sh Milioni moja.
Kwihyava alisema wananchi wa mkoa wa Iringa wana kiu kubwa ya kuona moja au zaidi ya timu zake zinapata mafanikio katika mchezo huo na kushiriki ligi kuu Tanzania bara.
Akitoa sababu ya kudhamini ligi hiyo, Mwakalebela alisema: “ligi hii ni moja ya ligi nyingi za chini zinazoweza kusaidia kuibua vipaji vinavyoweza kuboresha mchezo huu mjini Iringa.
Alisema akiwa mmoja wa wadau wa soka nchini, ameamua kurudi nyumbani Iringa na kushirikiana na wadau wengine kuinua mchezo huo.
“Pamoja na udhamini wangu, natoa wito kwa wadau wengine wajitokeze kuziunga mkono timu zetu ili malengo tuliyonayo katika sekta hiyo yaweze kufikiwa,” alisema.
Timu zitakazoshiriki ligi hiyo ni pamoja na Gangilonga FC, Mkimbizi United, Ilala FC, Feed Force FC, Miyomboni FC, Mkwawa FC, Black Eagle FC, Iringa Downtown FC, Upendo Shooting Stars, Black Cheaters FC na Young Boys.

MDOMO WAMPONZA MWENYEKITI WA CHADEMA IRINGA ..................

Mwenyekiti wa Chadema Iringa Mjini
MDOMO  wamponza mwenyekiti  wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Iringa Mjini, Frank Nyalusi ameingia matatani baada ya kudaiwa kutoa tuhuma zisizo za kweli  dhidi ya Kamanda wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Iringa, Salim Asas, kwa lengo la kujipatia umaarufu.
Katika mkutano wa hadhara uliofanywa na Chadema hivikaribuni kwenye uwanja wa Mwembetogwa mjini Iringa, Nyalusi ambaye pia ni diwani wa kata ya Mivinjeni mjini Iringa, anadaiwa kutoa tuhuma zinazowahusisha vijana watatu ambao hata hivyo hakuwataja majina; kwamba walitumwa na Kamanda huyo wa UVCCM kwenda kumdhuru.
Taarifa za uhakika zilizoufikia mtandao huu zimedai Asas kwa kupitia wakili wake, Alfred Kingwe amekwisha mkabidhi Nyalusi hati ya madai (Demand Note) inayomtaka kukanusha tuhuma hizo ndani ya siku 14 vinginevyo atafikishwa mahakamani.
Kwa kupitia hati hiyo ya madai Nyalusi anatakiwa kuitisha mkutano katika eneo lile lile alilotolea tuhuma hizo na kukanusha madai hayo yanayoelezwa kupikwa kwa lengo la kuchafua wasifu wa Asas na kumuongezea Nyalusi umaarufu.
Katika kumnurusu Nyalusi dhidi ya mkono wa sheria endapo atashindwa kuitisha mkutano huo, baadhi ya viongozi wa chama hicho wanadaiwa kumpigia magoti Bwana Asas ili suala hilo limalizwe kiungwana.
Mmoja wa viongozi wa chama hicho, Abou Changawa alisema; “tunamtafuta Bwana Salim, tunajua ni muungwana, tunataka suala hili tulimaze kiungwana; kama itashindikana kuitisha mkutano wa hadhara basi tutafanya mkutano na waandishi wa habari ili kuiweka sawa taarifa hiyo.”

MAISHA YA KIJIJINI

December 28, 2014

KAMPUNI YA MAZIWA YA ASAS YAJA NA MWONEKANO MPYA

Furaha ya  bidhaa mpya ya  asas Dairies Ltd  katika  mwonekano  mpya
Hivi ndivyo  maziwa  hayo  yanavyoonekana kwa  sasa 
                                               Na  Matukiodaimablog
Kampuni ya maziwa ya Asas Dairies Limited imewapongeza wateja  wake kwa  kuendelea  kutoa ushirikiano kwa  kutumia bidhaa  zake .

  Afisa masoko wa kampuni ya maziwa ya Asas  Dairies Ltd ya mkoani Iringa Bw Jimy Kiwelu alisema  hayo  leo  wakati akitoa  salam  za mwaka mpya 2015 na  kutambulisha mwonekano mpya  wa  kisasa  zaidi wa chupa  za maziwa  ya kampuni   hiyo kwa  sasa.

Alisema  mbali  ya mafanikio makubwa  ambayo kampuni  hiyo  imefanikiwa  kuyafikia kwa kuendelea kupata tuzo ya  ubora  wa  maziwa  kwa  miaka takribani  miwili  sasa  bado  kampuni  hiyo  imejipanga kuendelea kuboresha na kuongoza .

Kuwa  katika  kuhakikisha wanaendelea  kushikilia nafasi ya  kwanza na ubora wa maziwa nchini Tanzania   hivi  sasa tayari kampuni hiyo  imekuja na mwonekano mpya  wa maziwa  yake kwa kuwa  katika  chupa tofauti  na zile  za mwanzo .

Hata hivyo  alisema  kuwa  kuanzisha mwonekano  mpya  wa chupa  za maziwa  hayo  kumekwenda   sambamba na  kuongeza  ubora  zaidi  wa  bidhaa  hizo  hivyo kuwakata watumiaji wa bidhaa  zao  kuanza  kufurahia  kuaga mwaka 2014 na  kuukaribisha  mwaka 2015 kwa  kutumia maziwa yenye  mwonekano tofauti na  ule  wa  mwanzo .
                                     Mwonekano  wa  zamani 
Pia alisema kampuni  yake  imekuwa  mbele  katika  kuchangia maendeleo  ya mkoa  wa Iringa kama sehemu ya kutambua ushirikiano mkubwa  wa kampuni kwa maendeleo ya Taifa .

Kiwelu alitaja moja kati ya  shughuli ambazo kampuni imepata  kusaidia kuwa ni pamoja na kuhamasisha  jamii ya  Iringa  na  watanzania  kupenda  kunywa maziwa  kwa afya badala ya  kutumia muda  wao  kuingiza  sumu mwilini kwa kunywa  pombe pia kampuni imepata kutoa  msaada wa madawati yenye thamani ya zaidi ya Tsh milioni 2.7 kwa shule za msingi tatu ambazo zilishinda katika mashindano ya uchoraji wa picha zinazoelezea umuhimu wa unywaji maziwa mashuleni

Mbali ya zawadi hizo kwa shule hizo tatu pia kampuni hiyo ilipata kuwanywesha maziwa wanafunzi zaidi ya 30,000 wa shule za msingi katika Manispaa ya Iringa.

Shule hizo zilizopatiwa msaada wa madawati ni pamoja na Hoho iliyoshika nafasi ya kwanza na kupata madawati yenye thamani ya Tsh milioni 1 ,Mlangali iliyoshika nafasi ya pili na kupata madawati ya Tsh.750,000 pamoja na St Dominic iliyopata madawati yenye thamani ya Tsh 500,000.

Ndege ya AirAsia yapotea na abiria 160

Shirika la ndege la AirAsia linasema kuwa limeanzisha shughuli ya kuitafuta ndege yake iliyopoteza mawasiliano na kituo cha kuelekeza safari za ndege dakika 45 baada ya kuondoka kwenye mji wa Surabaya nchini Indonesia.

Zadi ya watu 160 walikuwa ndani ya ndege hiyo ya Airbus 320 iliyokuwa safarini kwenda nchini Singapore.

Wengi wa abiria waliokuwa ndani ya ndege hiyo wanatoka nchini Indonesia.
Msemaji wa wizara ya usafiri nchini Indonesia amesema mawasiliano yalipotea kati ya visiwa vya Kalimantan na Java.

Wataalamu wa safari za ndege wanasema kuwa huenda ndege hiyo iliishiwa na mafuta

LIPULI FC YAILALUA FRIENDS RANGERS BAO MOJA KWA NUNGE...!


 REFA  pamoja na wasaidizi wake wakisindikizwa na polisi baada ya vurugu kutokea baada ya mechi kumalizika ambapo Lipuli Fc aliibuka ushindi wa bao moja lililofungwa na mshambuaji machachali Vedatus Josephat (Balloteli) katika dakika nne kipindi cha kwanza katika uwanja wa samora jana. Lipuli kwa sasa inashika nafasi ya pili katika ligi hiyo ikiongzwa na Majimaji ya Songea na Team Friends Rangers wanashika nafasi ya tatu kwa kuwa na pointi 21. (FRIDAY SIMBAYA)

TUNACHOTA LULENGA...!


Wakazi mtaa wa Isoka B Manispaa ya Iringa, mkoani Iringa ambao hawakufamika majina yao mara moja wakichota maji kwenye mpira wa maji uliopasuka. Ni kawaida kukuta hali kama hii sehemu nyingi za ambao watu wanapasuwa bomba la maji kunakopelea mamlaki ya maji safi na taka (IRUWASA) kukosa mapato. (FRIDAY SIMBAYA)

MAGAZETI LEO JUMAPILI


December 27, 2014

DR. SHEIN AFUNGA MASHINDANO YA RIADHA UWANJA WA AMAAN ZANZIBAR

unnamedRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akikabidhi Kombe la Ushindi wa Jumla kwa Kassim Hussein Saleh na fedha tasilimu Shilingi Millioni  Moja akiwakilisha wilaya ya Mjini  iliyopata medali 17 za zahabu,13 fedha na 5 za Shaba katika ufungaji wa Mashindano ya Riadha katika Wilaya kumi za Unguja na Pemba aliyoyafunga leo katika uwanja wa Amaani Studium (kushoto) Kaimu Waziri wa Habari,Utalii,Utamadunu na Michezo pia Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdilahi Jihadi Hassan [Picha na Ikulu.] unnamed1Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi zawadi Mtoto  Sofia Kombo Makame aliyekimbia umbali wa kilomita nyingi kutokana na umri wake katika mashindano ya Riadha zawadi hiyo alipewa wakati wa ufungaji wa Mashindano ya Riadha katika Wilaya kumi za Unguja na Pemba   katika uwanja wa Amaani Studium leo Mjini Unguja,[Picha na Ikulu,] unnamed2Mwenyekiti wa  Chama cha Riadha Zanzibar Abdulhakim Cosmas Chasama alipokuwa akitoa salamu za Chama Riadha mbele ya Rais wa Zanzibar na   Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein wakati wa ufungaji wa mashindano ya Riadha kwa Wilaya ya Kumi za Unguja na Pemba katika Uwanja wa Amanaan Studium Mjini Unguja leo.
[Picha na Ikulu.]
unnamed3Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake ya ufungaji  wa Mashindano ya Riadha katika Wilaya kumi za Unguja na Pemba aliyoyafunga leo katika uwanja wa Amaani Studium [Picha na Ikulu.] unnamed4Wanamichezo kutoka wilaya ya Kaskazini A Unguja na Kusini Unguja wakiwa katika uwanja wa Amaan Studium wakati wa ufungaji  wa Mashindano ya Riadha katika Wilaya kumi za Unguja na Pemba aliyoyafunga leo katika uwanja wa Amaani Studium yaliyofungwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein [Picha na Ikulu.] unnamed5Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Baraza  la Michezo Bi Sharifa Khamis (katikati) akiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Riadha Zanzibar Abdulhakim Cosmas Chasama (kushoto)  baada ya kutoa nishani kwa wakimbiaji wa mashindano ya Riadha wakati wa ufungaji katika uwanja wa Amaan Studiam leo,[Picha na Ikulu.]