Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

November 30, 2013

WATANGAZAJI RADIO EBONY FM WAKIJUMUIKA KTK SHOW KALI YA MTIKISIKO 2013 IRINGA -LIVE

 watangazaji  wakali  wa  radio  ebony  fm  Sogg,Bony, Christina na Eddo wakiwa ktk show ya mtikisiko uwanja wa Samora usiku huu ni show kali kweli
AJALI MJINI IRINGA USIKU HUU

 TAXI  inayoegeshwa  eneo la Posta  mjini Iringa  imegongwa  vibaya  eneo la Idara ya maji mjini Iringa usiku huu na  watu kadhaa kunusurika  kifo  ajali  hiyo  imetokea  mida  ya saa 2.30 usiku huu hakuna aliyepoteza maisha  zaidi ya mfanyakazi wa kituo cha mafuta cha Gapco mshindo kujeruhiwa


 Hili ndilo gari lililosababisha ajali  wakati  likijaribu  kupiga yutani katika barabara kuu ya Iringa - Dodoma


BREAKING NEWS , CHADEMA CHAZIDI KUMEGUKA MWENYEKITI CHADEMA MKOA LINDI, MJUMBE BARAZA KUU TAIFA NA MKUTANO MKUU. KATIBU OFISI YA KATIBU MKUU WA CHAMA MAKAO MAKAUU mwenyekiti  wa  Chadema  Taifa Bw Freeman Mbowe
Aliyekuwa  naibu  katibu mkuu Chadema Bw Zitto Kabwe
.................................................................................................................


NDG: WANA HABARI:
Kwanza kabisa ninawashukuru kwa kuitika wito wangu.
Jina langu naitwa ALLY OMARY CHITANDA,nimejiunga CHADEMA mwaka 2003 nikitokea NCCR –MAGEUZI.

Nyadhifa  nilizowahi kuzishika na kukitumikia Chama ni:-
           
Kuanzia mwaka 2004- Mjumbe wa Baraza kuu Taifa  nikiwakilisha vijana Bara niliendelea kuaminiwa na Chama na kupewa kazi nyingine za kukitumikia Chama, nimewahi kuwa  Afisa wa Vijana Makao Makuu, Afisa wa sheria na Haki za binadamu Makao Makuu, Katibu wa Kamati ya muda ya Baraza la Vijana Taifa (BAVICHA) kwa sasa ni Mjumbe wa Mkutano Taifa nawakilisha Nachingwea, Mwenyekiti wa Mkoa wa Lindi tangu  tarehe 26/05/2013.Pia ni Afisa Mwandamizi  Ofisi ya Katibu Mkuu Makao makuu Dsm.
vile vile kwa kipindi kirefu sasa nimekuwa nikifanya shuhuli ya uandishi wa kumbukumbu za sekretarieti ya chama kama KATIBU WA SEKRETARIETI YA KAMATI KUU.
Hivyo sasa, pamoja na mambo  mengine yapo masuala nyeti na muhimu ninayoyafahamu na ikibidi kuwaarifu watanzania kwa njia mbali mbali pindi itakaponihitaji kufanya hivyo.

Ndugu zangu wanahabari, nimewaita ili kupitia nyinyi niwaambie Watanzania wenzaqngu juu ya hali ya kisiasa ilivyo hasa ndani ya Chama chetu. Itakumbukwa kuwa tarehe 20-21/11/2013 Kamati kuu ya Chama ilikaa pamoja na mambo mengine ilifanya maazimio ya kuwavua nafasi za Uongozi ndani ya Chama alikuwa Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara Mhe. ZITTO KABWE na Mjumbe wa Kamati kuu wa kuchaguliwa Mhe. Dr. FITILA MKUMBO, kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kwa sababu:-

(a)  Mhe. ZITTO KABWE (Mb) alishiriki kusaidia Wabunge watatu wa CCM kupita bila kupingwa kenye Majimbo yao ya Uchaguzi 2010.

(b)  Kuandaa mkakati waliouita mabadiliko ya Chama 2013. Mkakati uliolenga kumuwezesha Mhe. Zitto kushinda nafasi ya Uenyekiti wa Chama Taifa endapo angekubali kugombea.

(c)  Mhe. Zitto alishindwa kutimiza majukumu yake ndani ya Chama kwa kutoshiriki pamoja na Viongozi wenzake kwenye matukio makubwa yaliyokikumba Chama kama:-
(i)            Maandamano ya Arusha.
(ii)          Operesheni zilzofanyika Morogoro na Iringa nk.

MAAMUZI MENGINE YA UBORESHAJI WA MAKAO:
     Ni kweli kuwa pamoja na mambo mengine Baraza kuu la Chama iliridhia pendekezo lililetwa kwake na Kamati Kuu kuhusu jambo hili.Na katika utekelezaji wake Kamati Kuu ya juzi iliridhia kuwa, uteuzi wa Wakurugenzi watano ambao ni:-
1.    Mkurugenzi wa Oganaizesheni Mhe. Singo Kigaila Benson.
2.    Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mahusiano ya ndani Mhe. John Mnyika (Mb).
3.    Mkurugenzi wa Fedha na uwekezaji Mhe. Anthony Komu.
4.    Mkurugenzi wa Bunge na Halmashuri Mhe. John Mrema.
5.    Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama Mhe. Wilfred Lwakatale.

Uteuzi huu hauonyeshi sura ya Kitaifa Wakurugenzi wote watano ni Wakristo kanakwamba CHADEMA hakuna Waislamu wenye uwezo wa kushika nafasi hizo.

Lakini pia hauzingatii mgawanyo wa kijamii kwa kuwa kati ya kurugenzi hizo sita wakurugenzi wanne kati yao wanatokea mkoa mmoja wa kilimanjaro

Na uteuzi huu unakwenda sambamba na kuboresha maslahi yao kwa kuongeza posho, -kutoka Tshs. 800,000/= za awali na sasa itakuwa ni kuanzia Tshs. 1,500,000-2,500,000/= kwa Mkurugenzi na kutoka Tshs. 6,800,000/= kwa Afisa Mwandamizi na sasa ni Tshs.1,000,000-1,500,000/=.

Pamoja na kwamba uboreshaji uliridhiwa, lakini katika mpango ulioridhiwa na Baraza kuu ni pamoja na kulipa Posho kwa Makatibu wa Wilaya na Mikoa. Hawa ndio watendaji muhimu katika Ujenzi na Uhai wa Taasisi hii lakini, hawakuangaliwa wala kuguswa  badala yake wanatakiwa kujitolea tu kwa hali na mali.

Mimi kama nilivyotangulia kusema hapo awali, kuwa niko kwa kwa miaka 10 sasa na nimeshiriki kwa kiasi kikubwa katika Ujenzi wa Chama  hiki.Sioni sababu ya kutoharakisha kulipa posho ya Mkatibu wa Wilya na Mikoa pamoja na watendaji wengine na badala yake tunaharakisha kujilipa posho nono sisi watendaji wa Makao Makuu, wakati hawa wa ngazi za chini wanamaeneo makubwa ya Kiutendaji na wanafanya kazi katika mazingira magumu kwa kujitolea hata Ofisi zao wanajitolea wenyewe.

MAAMUZI YA KAMATI KUU.
Ningependa kuwaambia wanachadema na watanzania kwa ujumla, maamuzi haya ya kamati kuu ya kuwavua uongozi zitto kabwe na dkt mkumbo ni maamuzi ya kijuha na yanayowafanya watanzania sasa waangalie mara mbili mbili kama hawa watu wapo makini na huo ukombozi wanaousema.
Tumekuwa tukiweka mikakati mbali mbali ya ushindi ili chama kishinde, kwa mfano, kabla hata ya kifo cha aliyekuwa mbunge wa arumeru mashariki, wakati tu ilipobainika anaugua, chama kiliandaa mkakati wa kushinda ubunge wa jimbo hilo na uchaguzi uliporudiwa mkakati ule ulitumika na kushinda.
Nikiwa mtendaji wa ofisi ya katibu mkuu, nimeshiriki pamoja na zitto kabwe na dkt Slaa kupanga mikakati mbali mbali mizuri na mibaya kwa nchi, lakini hatukuwahi kuitwa wasaliti, wahaini wala sina lolote baya. Ni fedheha leo mimi kuwa sehemu ya watu wanaomuita zitto kabwe ni msaliti. Siwezi kuendelea na ujinga huu na sipo tayari tena.

Si dhambi kumuhukumu mtu kwa kuwa anapanga mipango ya kukushinda kwenye uchaguzi, dawa ya mpinzani wako ni kumkabili.

Naomba nikiri kwamba nikiwa katibu wa sekretarieti tumekuwa tukilazimishwa mara kadhaa kuwashawishi wajumbe wengi kutowaunga mkono watu wenye misimamo thabiti ndani ya chama na badala yake tumekuwa tukitumia rasilimali za chama kuwajenga wajumbe ndio.

Kwa mfano hivi sasa tunapozungumza, wakati katibu mkuu wa chama anasema mjadala wa zitto kabwe umefungwa rasmi, amewaagiza wakurugenzi wa chama kuzunguza nchi nzima kusambaza waraka waliouandaa ukimchafua zitto. Hii si sawa hata kidogo, si vema kutumia rasilimali za chama kuwanufaisha watu binafsi kutimiza matakwa yao ya kisiasa.

Nafsi yangu haipo tayari kuendelea kuwa sehemu ya upotoshaji dhidi ya watanzania wenzangu.
Nafsi yangu inanikataza kabisa kuendelea kufumbia macho maovu yanayoendelezwa na chama changu.

Nafsi yangu imechoka kuendelea kushuhudia ubaguzi wa kidini na kikabila unaofanywa wazi wazi na viongozi wa chama changu.

Nafsi yangu imekataa sasa, haipo tayari tena kuwa kuwadi wa kuwahadaa Watanzania kuyafikia matarajio tunayowapa ambayo kamwe hayafikiki.

Kwa kuwa siamini kwamba kuvuliwa nyadhifa kwa zitto kabwe na dkt kitila mkumbo ni kwa sababu ya waraka wa ushindi, bali ninaamini kuvuliwa kwao ni kutokana na hofu ya uchaguzi, ubaguzi wa kikabila na kikanda.

Hivyo basi, nikiwa na akili timamu kabisa, leo tarehe 30.11.2013 nimeamua kujivua nyadhifa zangu zote nilizokuwa nazo ndani ya  chama.

Sioni tena sababu ya kuendelea kuwa MwanaCHADEMA, sioni tena sababu ya kuwa mwenyekiti wa CHADEMA MKOA WA LINDI, sioni tena sababu ya kuwa KATIBU WA SEKRETARIETI YA KAMATI KUU.
Kwa kuwa vipaumbele vya chadema ni kukijenga chama mikoa ya kaskazini. Basi sisi wananchi wa mkoa wa lindi tunawatakia kila la heri, na kwamba waendelee kukijenga chama chao huko huko waliko.Nashukuru wote ambao nilifanya nao kazi pamoja katika kutekeleza majukumu yangu.

Ahsante Sana

A.O. CHITANDA

0753418510

MWENYEKITI CHADEMA MKOA LINDI
MJUMBE BARAZA KUU TAIFA
KATIBU OFISI YA KATIBU MKUU- SEKRETARIETIMTIKISIKO 2013 WATIKISA IRINGA USIKU HUU UWANJA WA SAMORA TUPO -LIVE

msanii Jesca  Kihaga  kutoka  Kihesa  kilolo Iringa  akijimwaga  jukwaani  katika show kubwa  ya mtikisiko mjini Iringa  usiku  huu

MPASUKO CHADEMA WAZIDI KUSHIKA KASI ,WANANCHI WA JIMBO LA ARUSHA MJINI[CHADEMA] WAMPINGA HADHARANI KWA MABANGO MBUNGE WAO, GODBLESS LEMA


Soma Bango hilo, wafuasi wa CHADEMA jijini Arusha ,walioambatana na Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Monduli Bw. Amani Salenga wakionyesha bango hilo kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani) ,wakidai kuwa Mbunge Lema ndie chanzo cha vurugu kwenye Chama kwa kuanzisha kikundi cha vijana ambacho kimekuwa tishio kwa wale wanaojaribu kupingana na sera za Mbunge huyo. pia wamedai kuwa Arusha kwa sasa CHADEMA imegawanyika katika makundi mawili, amabyo ni CHADEMA ASILI na CHADEMA FAMILY.

MAHAFALI YA DARASA LA AWALI SHULE YA KIMATAIFA YA SOUTHERN HIGHLANDs MAFINGA YAFANA

Wanafunzi  wa  darasa la  kwanza  katika shule ya  Southern  Highlands  Mafinga  wakionyesha  ujuzi  wao
Wazazi  wakiwa katika  darasa la  maonyesha  ya  taalum kwa  wanafunzi  shuleni hapo  leo
Wanafunzi  wa darasa la kwanza  wakionyesha  uwezo  wao  katika kutumia kompyuta
 Mkurugenzi  mtendaji wa  shule  ya kimataifa  ya  Southern  Highlands  Mafinga  mkoani  Iringa Bi Mary  Mungai akitambulisha  wageni  mbali mbali ukumbini hapo leo  wakati  wa mahafali  ya  darasa la  awali
 Baadhi  ya  wazazi  waliofika katika mahafali ya shule  hiyo  leo
 Baadhi  ya  wahitimu katika mahafali  hayo
 Mjumbe  wa  bodi  Bw Nko akijitambulisha  mbele ya  wazazi
 Walimu na  wafanyakazi wa   shule  ya  Southern Highlands  Mafinga  wakijitambulisha  mbele  ya  wazazi  leoWanafunzi  wa darasa la  pili  wakionyesha michezo yao  leo

TANGAZO NAFASI ZA MASOMA NA KAZI 2014 SHULE YA SOUTHERN HIGHLANDS(ENGLISH MEDIUM)TANGAZO NAFASI ZA MASOMA NA KAZI 2014
SHULE YA SOUTHERN HIGHLANDS(ENGLISH MEDIUM) ILIYOPO MAFINGA MJINI WILAYA YA MUFINDI, MKOA WA IRINGA INAWATANGAZIA 
1. NAFASI  ZA MASOMO
·         DARASA  LA  1, 2, 3, NA 5 KWA  WANAFUNZI  WANAOTOKA  SHULE ZA KISWAHILI NA ENGLISH MEDIUM.
·         DARASA LA 4 NA 6 KWA WANAOTOKA ENGLISH MEDIUM TU.
USAILI  UNAFANYIKA   SHULENI SOUTHERN HIGHLANDS
· SOUTHERN HIGHLANDS SCHOOL IMEKUWA IKIFANYA VIZURI KATIKA MTIHANI WA TAIFA  WA DARASA LA SABA NA NI MIONGONI MWA SHULE BORA KITAIFA.
2. NAFASI ZA KAZI 2014
A. WALIMU WATATU WA MASOMO YAFUATAYO:  HISABATI, SAYANSI,
     JIOGRAPIA, HISTORI NA URAIA.
   SIFA: ELIMU YA DARAJA III AU STASHAHADA YA UALIMU(awe na CV)
MUHIMU:- WALIOFAULU SOMO LA KIINGELEZA WATAPEWA KIPAO MBELE
B. MWALIMU WA CHEKECHEA
SIFA: ELIMU YA MONTESSORI MIAKA MIWILI
KWA MAWASILIANO ZAIDI PIGA SIMU:
           
·         SHULENI                                       -   0262772661
·         KWA MWALIMU MKUU            –   0754209251
·         KWA MWALIMU MKUU MSAIDIZI  –  0756721040
·         KWA MKURUGENZI                              – 0754651966
P.O.BOX 34 Mafinga
southernhighland97@hotmail.com
Mwisho  wa  kutuma maombi kwa  wanaohitaji kazi ni tarehe 30/11/2013
KUMBUKA SOUTHERN HIGHLANDS MAFINGA  NI SHULE INAYOTOA ELIMU BORA NCHINI TANZANIA MLETE MWANAO APATE ELIMU  BORA

November 29, 2013

KASEBA,ALIBABA KUZIPIGA FRIENDS CORNER HOTEL

Japhet Kaseba

>

                             Alibaba Ramadhan        


Mabondia jafet kaseba na Alibaba Ramadhan wa arusha wanategemea kupanda ulingoni siku ya jumamosi ya tarehe 21 decemba 2013 katika ukumbi wa friends corner hotel.
Pambano hilo liloandaliwa na Ibrahim kamwe chini ya  BigRight promotion kwa usimamizi wa PST, pia litakuwa na mapambano  mengine tisa ya utangulizi likiwemo la ubingwa wa mkoa kati ya karage suba na bondia mkali anaechipukia kwa nguvu  Fadhili awadh[tiger]  katika uzito wa wealter[66kgs] pambano la raundi kumi.
Akizungumza na vyombo vya habari mratibu wa pambano hilo Ibrahim kamwe alisema zaidi ya hayo mapambano ya ubingwa , pia mahasimu wawili wa uzito wa juu lusekelo Daudi atazipiga na  Mbaruku kheri [ndota] katika marudio ya mchezo wao wa kusisimua uliokosa mshindi.
 Nae Adam yahaya [baby edo] atazipiga na Harman Richard, mkongwe enerst bujiku[tyson] atacheza na shah kasimu kukumbushia Enzi za akina Stanley mabesi , jocky hamis mkongwe wa zamani atazipiga na bondia sawa na mwanae  mbena rajabu, nae  issa omar  atazipiga na haji juma wa Tanga, moro best atapigana na shafii ramadhan.  Huku shaban bodykitongoji akizipiga na mwinyi mzengera. 
 Mabondia wote wameshasaini mikataba ya makubaliano ya mchezo huona wameshaingia kambini kujiandaa na mechi zao hizo ambazo zina upinzani wa hali ya juu.kinachoendelea kwa sasa ni kumalizia mchakato wa ulinzi toka kiwango security na jeshi la polisi

IBRAHIM ABBAS KAMWE
+255 713 501991

TAPELI WA KIZUNGU ANASAKWA:-TAARIFAA KWA VYOMBO VYA HABARI NA UMMA

 TAHADHARI:- KUNA TAPELI MWENYE ASILI YA KIZUNGU ANADAI YEYE NI RAIA WA AFRICA KUSINI MREFU ANAONEKANA SANA MITAA YA KINONDONI MANYANYA MIDA YA USIKU AMETAPELI WATU WENGI SANA AKIDAI KUA AMEIBIWA HOTELINI NA MWANAMKE NA ANADAI ANAISHI MBEZI KIMARA KWA WENYEJI WENGI WA KINONDONI WANAMFAHAMU NA WENGI WAMESHAMSIKIA NA WANADAI NI MSWAHILI CHUKUENI TAHADHARI NA TUKO KWENYE HARAKATI ZA KUMKAMATA KWASABABU AMESHA TAPELI WENGI AKIJIFANYA KUCHUKUA NAMBA ZA SIMU KWA AJILI YA KUREJESHA FEDHA HIZO TUNAOMBA WENYE TARIFAA ZAIDI WATUSAIDIE KWA USHIRIKIANO NA POLISI KUMTIA MBARONI IMETOLEWA NA MMOJA YA WALIOLIZWASHOW KUBWA YA MTIKISIKO 2013 KUFANYIKA KESHO JUMAMOSI KTK UWANJA WA SAMORA


Ile  show  kubwa kwa mikoa ya nyanda za  juu kusini ya Mtikisiko 2013  iliyoandaliwa na kituo  cha  radio  Ebony Fm inataraji  kufanyika kesho  jumamosi  katika  uwanja  wa Samora ,wasanii wakali  kibao  kuwasha moto .

WAZAZI WA WANAFUNZI WANAOSOMA SOUTHERN HIGLANDS MAFINGA KUKUTANA KESHO JUMAMOSI

 Baadhi ya  wanafunzi  wanaosoma  shule  ya  kimataifa ya  Southern Highlands Mafinga ,chini na  baadhi  ya  wazazi  wa wanafunzi hao

WAKATI  uongozi  wa  shule  ya  kimatiafa ya  Southern Highlands Mafinga  mkoani  Iringa  ukiwa na uhakika  mkubwa wa  wanafunzi  waliofanya mtihani  wa Taifa  wa darasa la saba mwaka  huu  kufaulu wote ,kesho jumamosi  shule  hiyo  imewaita  wazazi  wa wanafunzi hao  na  wengine wote wanaoendelea  kusoma  shuleni hapo.

Mwenyekiti wa bodi ya shule ya hiyo  ya Southern Highlands Mafinga Kitova Mungai alimweleza mwandishi  wa habari hizi  kuwa lengo  la  kuwaita  wazazi hao  ni kuweza  kujadiliana mambo mbali mbali ya kimaendeleo  katika shule  hiyo.

Alisema  kuwa  shule   hiyo  imekuwa na utaratibu  wa  kukutana na wazazi   wanaosomesha  watoto   wao  katika  shule  hiyo  kila mwaka kwa ajili ya kupokea  changamoto mbali mbali kama  njia ya  kuboresha  elimu  shuleni  hapo.

Kwani  alisema  kuwa kimsingi  kiwango  cha taalum shuleni  hapo kipo  juu na kuwa  hata   mwaka  mmoja shule  hiyo haijapata  kufelisha hata  mwanafunzi mmoja.

Bw  Mungai  alisema kuwa  kikao hicho  cha pamoja kati ya  wazazi na  uongozi  wa  shule  hiyo kitafanyika  kuanzia majira ya saa 2 asubuhi hadi saa 7 mchana  katika ukumbi wa  shule  hiyo.

Kwa  upande wake mkurugenzi mtendaji wa Southern Highlands Mafinga Bi Mary Mungai  aliwataka  wazazi kujitokeza kwa wingi katika kikao  hicho ikiwa ni pamoja na kupongeza benk ya wananchi Mufindi (MUCOBA) kwa jitihada mbali mbali  za kuunga mkono jitihada za elimu shuleni hapo kiasi cha kujitolea kiasi cha Tsh milioni 2.5 kwa ajili ya kuwafuingulia akaunti katika benk hiyo wanafunzi watakaofanya vema katika matokeo ya mtihani huo mwaka huu

Bi Mungai  alisema  kuwa  kuwa msaada huo wa MUCOBA ni heshima kubwa kwa shule yake na kuwa ni chachu ya shule hiyo kuendelea kufanya vema zaidi ili kuwavuta wahisani wa ndani na nje kuendelea kuiunga mkono shule hiyo.

Alisema MUCOBA hawajakosea kuunga mkono jitihada za elimu katika shule hiyo kwani kweli ni shule inayotoa elimu bora na toka ilipoanzishwa zaidi ya miaka 13 iliyopita shule hiyo haijapata kufelisha mwanafunzi hata mmoja.

Hata  hivyo baadhi  ya  wazazi  wanaosomesha  watoto  wao katika  shule  hiyo  wameendelea  kupongeza   jitihada zinazofanywa na shule hiyo kwa  kuendelea  kufanya  vema katika mitihani ya taifa na kuwa imani kubwa ya  wazazi ni kuona  shule hiyo inaendelea  kuwa shule  bora  mkoa wa Iringa na Tanzania kwa ujumla .

 

November 28, 2013

USAFI WA MITARO ENEO LA MAKUMBUSHO IMEKUWA TATIZO KUBWA,MAGONJWA YA MLIPUKO YANAWEZA KUTOKEA

div class="separator" style="clear: both; text-align: center;"> Huu ni mtaro ambao umeziba na maji hayaendi,na watu kutupa uchafu ndani yake kama unavyoonekana.
Juu ya huo mtaro kuna mgahawa wa chakula,ambao watu wanautumia kwa mahitaji ya chakula.
Kama picha inavyoonesha maji machafu yakiwa yametuama,na uchafu ukiwa umetupwa ndani yake.
Ikifika mchan watu hukaaa hapo juu na kupata chakula hii ni hatari kwa afya ya binadamu.

Ukifika maeneo ya makumbusho nyuma ya Jengo la Tigo maarufu mtaa wa kwa bwela kwa wauza viatu maarufu kwa wakina dada,hali ya usafi katika mitaro ya eneo hili ni ya kutisha ingawa imezungukwa na maofisi makubwa kama kampuni za simu na mabenki mengi.Dj sek blog ilifanya utafiti makini na kujione hali ya mitaro hiyo ikiwa katika hali mbaya kiusafi,Kwanza mitaro hiyo imeziba hivyo kusababisha maji kutuama na kupelekea maji hayo kuvunda na kuwa rangi ya njano.

Kingine cha kushangaza zaidi ndani ya mitaro hiyo watu hutumia kama sehemu ya kutupia uchafu kama mifuko ya rambo,makopo n,k.Jambo lingine ambalo ni la hatari zaidi ni eneo la juu ya mitaro hiyo kuna mgahawa ambao unauza chakula kwa ajili ya matumizi ya binadamu.Jambo la kujiuliza je watoa huduma katika mgahawa huo hawaoni hali hiyo ya uchafu ambao upo kwenye eneo lao?na je hawaoni kwamba ni hatari kwa afya za binadamu wanaokula eneo hilo?Tulipojaribu kuwauliza walikuwa hawana majibu ya kutoa.Tunaomba serikali ya mtaa wa makumbusho walione hili na kulishughulikia na sio kukaa ofisini mpaka magonjwa yatokee ndipo tuanze kuhangaika.(picha na Dj Sek Blog)

, TUTAKUKUMBUKA DUNIA MZOBORAMwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi-CCM, Mkoa wa Dar es salaam, RAMADHAN MADABIDA, leo amewaongoza waombolezaji katika maziko ya Mhariri Mwandamizi wa Magazeti ya Uhuru na Mzalendo, Marehemu DUNIA MZOBORA. 
 
          Maziko ya Marehemu MZOBORA, aliyefariki jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kutokana na kusumbuliwa na Shinikizo la Damu, yamefanyika katika Makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam.

          Maziko hayo pia yamehudhuriwa na waandishi mbalimbali kutoka vyombo vya habari nchini.

          Marehemu MZOBORA ambaye alizaliwa mwaka 1964 huko Mwandiga Mkoani Kigoma, alijiunga na Uhuru Publications Limited mwaka 1989 akiwa Mwandishi wa Habari Mwanafunzi, baada ya kumaliza Masomo ya Ualimu ngazi ya Cheti kutoka Chuo cha Kasulu, Mkoani Kigoma.

Kutokana na uwezo wake na kujituma kazini, alipanda vyeo na hadi mauti yanamfika alikuwa ni Kaimu Msanifu Mkuu wa Uhuru na Mzalendo.
Mungu ailaze roho ya Marehemu DUNIA MZOBORA mahali pema paponi. Amina.

CCM WAUTEKA MJI WA TUNDUMA

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akihutumia maelfu ya wananchi katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mwaka, mjini Tunduma, wilayani Momba, jioni hii, Nov 28, 2013, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kuzungumza nao njia ya kuzitatua, katika mkoa wa Mbeya.
 Wananchi wakiwa wamembeba Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakati wa mkutano mkubwa wa hadhara uliohudhuria na maelfu ya wananchi katika uwanja wa shule ya msingi Mwaka mjini Tunduma wilayani Momba mkoani Mbeya, leo
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye 'akihutoa dozi' alipohutubia katika mkubwa wa hadhara uliohudhuria na maelfu ya wananchi katika uwanja wa shule ya msingi Mwaka mjini Tunduma wilayani Momba mkoani Mbeya, leo
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akitoa 'dozi' katika mkutano mkubwa wa hadhara uliohudhuria na maelfu ya wananchi katika uwanja wa shule ya msingi Mwaka mjini Tunduma wilayani Momba mkoani Mbeya, leo
 Dk. Asha-Rose Migiro akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano uliofanyika  Uanja wa shule ya  Mwaka, Tunduma,leo
Katibu wa NEC, Siasa na Uhisiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro (katikati mwenye  miwani) akiselebuka na wananchi kwenye mkutano, Uwanja wa shule ya  Mwaka, Tunduma leo. Imetayarishwa na theNkoromo Blog --