Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

October 31, 2013

REDD'S UNI-FASHION BASH KUMEKUCHA MOSHI


Na Mwandishi Wetu, Moshi
KUMEKUCHA ndani ya Mkoa wa Kilimanjaro, pale wanamitindo na wabunifu walio katika vyuo vikuu watakapochuana kesho katika tamasha la ‘Redd’s Uni-Fashion Bash’, ndani ya Ukumbi wa Glessius uliopo mjini hapa.
 
Tamasha hilo linalochochea vipaji ndani ya vyuo hivyo, awali lilifungua pazia ndani ya Mkoa wa Mwanza na litahusisha pia vyuo vilivyopo katika mikoa ya Dar es Salaam na Iringa.
 
Akizungumzia tamasha hilo, Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Fimbo Butallah alisema, vyuo vinne vilivyopo mkoani humo ndivyo vinavyotarajiwa kushiriki.
 
Wanafunzi wabunifu na wanamitindo wanaotarajiwa kushiriki tamasha hilo wanatoka Chuo Kikuu cha Mwenge, Chuo Kikuu cha Tiba na Sayansi ya Afya Kilimanjaro, Tumaini na Chuo Kikuu cha Ushirika na Biashara.
 
Fimbo alisema, wanafunzi wa vyuo vyote vya elimu ya juu walio na mapenzi katika ubunifu na mitindo wanatarajiwa kushiriki shindano hilo, huku akiamini kutakuwa na upinzani mkali zaidi ya ule wa Mwanza. Burudani inatarajiwa kutolewa na msanii Jon Makini ‘Mwamba wa Kaskazini’.
 
Tamasha la awali lililofanyika Mwanza, kulikuwa na ushindani mkali katika mitindo ambapo Fahad Rajab kutoka Chuo Kikuu cha St. Augustine (SAUT) aliibuka mshindi akifuatiwa na Lucy Charles kutoka pia chuo hicho.
 
Fahad kwa ushindi huo alijinyakulia Sh 500,000 huku Lucy akitwaa Sh 400,000 na mshindi wa tatu Ally Thabit wa Chuo cha Biashara (CBE) akiondoka na Sh 300,000 huku Joseph Mmari wa SAUT aliyeshika nafasi ya nne pamoja na Victoria Newton pia kutoka chuo hicho aliyeshika nafasi ya tani kila mmoja akipata Sh 100,000.
 
Kwa upande wa wabunifu mshindi wa kwanza alikuwa Dotto Elius wa CBE aliyejitwalia Sh 700,000, akifuatiwa na Fahad Rajab wa SAUT aliyepata Sh 500,000 akifuatiwa na Rafaka Mtani wa Taasisi ya Uhasibu (TIA) aliyeondoka na Sh 300,000.
 
Washindi wa nne na watano walikuwa ni Amedias Amedia wa SAUT na Elizabeth Mtani wa TIA ambao kila mmoja aliondoka na Sh 100,000.
 
Meneja Habari na Mawasiliano wa TBL, Edith Mushi alisema katika tamasha la leo, fedha za zawadi zitakazotolewa zitakuwa kama zile zilitolewa kwa washindi wa Mwanza.
 
“Tunataka kuinua vipaji vya wanafunzi wa vyuo katika tasnia ya mitindo, kwa sasa wanafunzi katika mikoa iliyobaki wanatakiwa wajiandae mno, maana kuna upinzani mkubwa,” alisema Edith.
 
Kinywaji cha Redd’s Original pia ndicho kinachodhamini shindano la Redd’s Miss Tanzania na kinazalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).

WAFANYAKAZI WA KONYAGI WALIOENA KUANGALIA LIVE MCHEZO WA BARCELONA VS REAL MADRI, HISPANIA WAREJEA

Mfanyakazi wa Kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distilleries Limited (TDL), Khadija Madawili ambaye alikuwa kiongozi wa msafara wa wafanyakazi wa TDL waliokwenda kushuhudia pambano la Ligi ya La Liga ya Hispania kati ya Barcelona na Rael Madrid, akirejea jana kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam. Wafanyakazi watano wa TDL, waliteuliwa baada ya kampuni hiyo kushinda  Tuzo ya SABMILLER AFRICA MB COMPLEMENTARY BEVERAGE CATEGORY AWARD FOR F 13)
 Joseph Chibehe (kushoto) akilakiwa na mkewe baada ya kuwasili
                                             Chibehe akiwa na furaha baada ya kulakiwa na mkewe
 Bavon Ndumbati (kushoto), akilakiwa na ndugu yake. Katikati ni Michael Mrema
                                                              Bavon akiwa na furaha
                                                                 Mwesiga Mchuruza.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Konyagi ya Tanzania Distilleries Limited (TDL), David Mgwassa (katikati), akiwa na mabosi wa kampuni mama ya SABMILLER AFRICA.wakiwa wameshikilia tuzo hiyo ya  MB COMPLEMENTARY BEVERAGE CATEGORY AWARD FOR (F 13).

KAMPUNI ya Tanzania Distilleries Ltd, (KONYAGI) ambayo ni miongoni mwa kampuni tanzu za Kampuni ya Sabmiller South Africa, imeshinda tuzo ya utendaji bora wa bidhaa (SABMILLER AFRICA MB COMPLEMENTARY BEVERAGE CATEGORY AWARD FOR F 13). Sabmiller inamiliki zaidi ya viwanda 60 vya bia na vinywaji vingine duniani.

Baada ya ushindi huo, Mkurugenzi Mkuu wa TDL, Mgwassa ambaye alipambana mpaka kupata ushindi huo, aliamua kuwazawadia baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo, kwenda Hispania kushuhudia pambano la timu kubwa za Barcelona na Real Madrid lililofanyika mwishoni mwa wiki.

Wafanyakazi waliokwenda Hispania  na kurejea jana usiku kwa ndege ya Afrika Kusini ni; Joseph Chibehe, Khadija Madawili, Bavon Ndumbati, Michael Mrema na Mwesiga Mchuruza.

Wafanyakazi hao, walipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, walionekana kuwa na bashaha na kupokelewa na ndugu zao pamoja na baadhi ya wafanyakazi wenzao.

Akizungumza kwa niaba ya wenzie,Michael Mrema wa Kanda ya Kaskazini, alisema kuwa wanashukuru uongozi kuwapa zawadi hiyo, ambayo imewafanya kuwa na morari mpya wa kazi.

Pia anaseama walifurahi sana kushuhudia mechi hiyo kubwa ya timu za Barcelona na Real Madrid ambapo timu ya Barcelona waliyokuwa wanaishabikia kushinda mabao 2-1.

HII NI HATARI


 Mmoja wa wakazi wa mtaa huu aliye amua kujitoa na kushika kinyesi ili apate kuzibua chemba ambayo ilikuwa inamwaga maji bila kusimama kwa siku Sita
 Hali hii ilikuwa mbaya jambo ambalo wananchi waliamua kujitolea na kufanya wawezalo ili kuzibua
 Hali ni Tete eneo Hili ambapo sasa moja ya Chemba inazidi mwaga maji.. hapa kila mtu anatoa wazo lake nini kifanyike ili kuweza kuzibua eneo hilo ambalo maji yake yalikuwa hayapungui kumwagika bali kuongezeka..na mwisho wote waliona bora washike kinyesi kuliko kuendelea kuteseka.
 Ilikuwa ni Baada ya Kuhangaika sana wakazi wa eneo hili kwa kutumia nyenzo yao Duni ya nondo maalumu ya kuzibulia chemba waliyo jinunulia wenyewe  , hatimaye walifanikiwa kuzibua chemba moja na kuhamia chemba ya pili .
 Baada ya Chemba ya Juu kuzibuka , kasheshe ikahamia katika chemba ya pili ambapo sasa maji yote yalihamia hapo.
 Masikini mtazame Mama huyu alivyo Ruka juu na mtoto akiwa amemshika kihatari namna hii... hii ni adha ya haya maji taka.
 Wakazi wa eneo hili wakiwa wanakomaa kwa nguvu zote kuanza kuzibua chemba ya pili.
 Zoezi sasa linaendelea na hapa walikuwa wanaendelea kuzibua chemba ya 3 ambapo sasa  walifika kikomo baada ya kuonekana chemba hiyo ilikuwa imejaa matakataka ya kutosha pamoja na Mchanga . Na ndipo walipo pata taarifa kuwa DAWASCO wanakuja.
Wakiwa wamefika  kabisa na kujionea Adha ya kukanyaga maji Taka ...... huo nyuma ni mtambo maalum wa kuzibua Chemba 
 Wafanyakazi wa DAWASCO wakiwa wamefika katika eneo la tatizo na kuanza kuzibua chemba za maji taka ili kuwasaidia wakazi hao wasipatwe  na magonjwa , Kero ya maji mtaani na Harufu mbaya
 Wakiwa wanahakikisha kabisa kwamba tatizo limekwisha eneo hilo...
 Moja ya Chemba ambayo wakazi wa Mwenge walikuwa wamehangaika nayo sana mpaka kufanikiwa  kutoa maji taka hayo  yaende ikiwa inaangaliwa na wafanyakazi wa DAWASCO
 Wafanyakazi wa DAWASCO wakiwa wanaendelea kutoa takataka katika chemba sugu ili kuruhusu maji yapite
 Hii ni Baada ya Chemba Kuzibuliwa na wananchi wakishirikiana na DAWASCO Ambao walichelewa kufika eneo la tukio
 Maji yakionekana yanaendelea kukauka baada ya Chemba hizo kuzibuliwa
Hizi ni Takataka zilizo bakia baada ya kuzibua Chemba hizo ... 

Wananchi mtaa wa mwenge  waandamana na kufanya usafi kufuatiwa na kero kubwa ilyokuwa sugu na hatari katika afya zao, kero hiyo ikiwa ni kuziba na kufumuka  kwa chemba zinazo pitisha maji machafu maarufu kama  (majitaka )

Ikiwa nizaidi ya wiki mbili wakazi na watumiaji wa njia ya mwenge katika mtaa huo uliogeuzwa jina na kupewa jina mahususi na mazingira ya mtaa ambalo ni mtaa wa( kinyesi street) wamekumbwa na kero ya kufumuka kwa chemba za  maji taka na kuwa na harufu mbaya  hivyo wananchi wamehofia afya zao nakuanza kuzibua Chemba za maji hayo huku kila baada ya mwezi huletewa  Bili na kuweza kuzilipia bila ya wasiwasi .Lakini kibao kimegeuziwa kwa wananchi kuwa ndio wamiliki wa shirika la maji safi na taka (DAWASCO) leo hii waamua kuondoa adha hiyo iliyo dumu kwa muda mrefu bila ya ufumbuzi kwa kushika Kinyesi na maji machafu kutoka sehemu mbalimbali.

Hata hivyo wakazi walilalamika kuhusu  utendaji kazi wa dawasco kuwa ni mbovu kwa kuwa wame watafuta zaidi ya mara kadhaa  bila mafanikio

Aidha wananchi walionekana kuwa na moyo mmoja wa ushirikiano kufuatia harufu mbaya iliyokuwa ikitoka katika chemba hizo nakufanikisha kuzibua chemba zote katika mazingira magumu yanayo weza kusababisha maradhi mbalimbali kwa jamii husika wameongeza kuwa wana iomba mamlaka ya maji (DAWASCO) hususani kitengo cha majitaka kuweza kupita kila baada ya wiki moja ili kuweka mazingira mazuri/safi.(picha  na Dar es Salaam  yetu Blog)

SALAMU ZA PONGEZI ZAMIMINIKA KWA MALINZI


Jamal Malinzi

Rais mpya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, Jamal Malinzi ameendelea kupokea salamu za pongezi baada ya kushinda wadhifa huo katika uchaguzi uliofanyika Oktoba 27 mwaka huu.

Salamu nyingine za zimetoka kwa Rais wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Sepp Blatter ambapo amempongeza Malinzi kwa kuchaguliwa na kumtakia kila la kheri katika majukumu yake ya kuongoza mchezo huo nchini.

Blatter amesema ana uhakika ufahamu wake na uwezo wake katika uongozi ni muhimu katika kuimarisha maendeleo ya mpira wa miguu nchini, na kuongeza kuwa milango ya FIFA iko wazi wakati wowote anapotaka kujadili masuala yanayohusu mchezo huo.

“Nakutakia wewe na kamati mpya ya Utendaji iliyochaguliwa kila la kheri, nguvu, na kila aina ya mafanikio kwa changamoto zilizo mbele yenu,” amesema Rais Blatter katika salamu zake.

Wengine waliomtumia Rais Malinzi salamu za pongezi ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Kenya (FKF), Sam Nyamweya, Rais wa Heshima wa Shirikisho la Vyama vya Mpira wa Miguu Uganda (FUFA), Lawrence Mulindwa, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mwanza (MZFA) na Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Arumeru (ADFA), Peter Temu.

YANGA, JKT RUVU UWANJANI KESHO
Raundi ya 12 ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inaendelea kesho (Novemba 1 mwaka huu) kwa mechi kati ya JKT Ruvu na Yanga itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.

Viingilio katika mechi hiyo ni sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 kwa VIP A. Tiketi zitauzwa siku ya mechi uwanjani katika magari maalumu kuanzia saa 4 asubuhi.


Novemba 2 mwaka huu kutakuwa na mechi nne; Mgambo Shooting na Coastal Union (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga), Tanzania Prisons na Oljoro JKT (Uwanja wa Sokoine, Mbeya), Azam na Ruvu Shooting (Azam Complex, Dar es Salaam), na Mtibwa Sugar na Rhino Rangers (Uwanja wa Manungu, Morogoro).

Raundi hiyo itakamilika Novemba 3 mwaka huu kwa mechi moja ambapo Mbeya City itakuwa mwenyeji wa Ashanti United kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

Mechi za kukamilisha mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo zitachezwa Novemba 6 na 7 mwaka huu. Novemba 6 ni JKT Ruvu vs Coastal Union, Ashani United vs Simba, Kagera Sugar vs Mgambo Shooting, Rhino Rangers vs Tanzania Prisons na Ruvu Shooting vs Mtibwa Sugar.

Novemba 7 mwaka huu, Azam itacheza na Mbeya City wakati Yanga itacheza na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

DIWANI AIPIGA TAFU TIMU YA SOKA UHURU FM

 Diwani wa Kata ya Msongola, Ukonga, Dar es Salaam, Angel Malembeka (kulia) ameipiga tafu timu ya soka ya Uhuru FM, kwa kuipatia jozi mbili za jezi na mipira miwili ikiwa ni sehemu ya kuimarisha ushirikiano baina ya timu hiyo na kata yake. Pichani, Diwani huyo akikabidhi vifaa kwa uongozi wa timu hiyo, Angel Alikimali na Furaha Luhende, katika hafla fupi iliyofanyika nje ya Jengo la CCM mkoa wa Dar es Salaam, leo. Wakati Luhende ni Mwenyekiti wa timu hiyo,  Akilimali ambaye ni Kaimu Mkurugebzi Mtendaji wa Uhuru FM ni mlezi wa timu hiyo.
 Akilimali akimshukuru Masala Mabula ambaye ni mchezaji aliyeibuliwa kipaji chake katika michuano ya Malembeka Cup iliyomalizika hivi karibuni ambaye sasa anajiandaa kwenda Msumbiji kucheza soka la kulipwa. Masala alifuatrana na Diwani huyo (kulia)
Luhende na Akilimali wakifurahia vifaa hivyo baada ya kukabidhiwa na diwani
 Diwani na Akilimali wakiwa na baadhi ya waandishi na watangazaji wa Uhuru baada ya makabidhiano hayo.
Mtangazaji wa Uhuru FM, Mhina Dungumalo akimhoji diwani huyo baada ya makabidhiano Imetayarishwa na theNkoromo Blog --

KABILA ANYOOSHA MKONO WA DIPLOMASIA

 Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo amewataka wapiganaji wa makundi yote ya waasi mashariki mwa nchi yake kuweka silaha zao chini, baada ya kile kinachoaminika kuwa ni kusambaratika kwa kundi la M23.
Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Akihutibia taifa hapo jana (tarehe 30 Oktoba) kwa njia ya redio na televisheni, mara tu baada ya jeshi la serikali kuuteka mji wa Bunagana, Rais Kabila alilipongeza jeshi hilo na wale Umoja wa Mataifa kwa kulirejesha eneo la Rutshuru mikononi mwa serikali.
Hata hivyo, Rais Kabila akasema pamoja na ushindi huo wa kijeshi, diplomasia na mazungumzo baina ya Wakongomani yataendelea.
“Ninasisitiza wito wangu kwa wapiganaji wa kundi lililofurushwa kwenye mitaa ya Nyiragongo na Rutshuru kutua silaha zao chini kwa ikhari yao wenyewe kulingana na pendekezo la Nchi za Maziwa Makuu. Kinyume cha kufanya hivyo tutalazimika kuwapokonya silaha kwa nguvu. Wito wa aina hiyo hiyo unatolewa pia kwa makundi mengine ya wapiganaji ya kitaifa, kusitisha hatua zote za kijeshi kutasababisha wao na wengine kufaidika na mpango wa kuingizwa katika maisha ya kawaida.” Amesema Rais Kabila.
Kabila azionya nchi jirani, makundi ya kigeni
Wanajeshi wa Kongo wakipumzika baada ya vita vya kuwafurusha M23 mashariki mwa nchi hiyo. Wanajeshi wa Kongo wakipumzika baada ya vita vya kuwafurusha M23 mashariki mwa nchi hiyo.
Katika hotuba hiyo ya kwanza tangu taarifa za kusambaratika kwa kundi la waasi wa M23 mashariki kwa nchi hiyo, Rais Kabila aliyatahadharisha pia makundi ya wapiganaji ya kigeni yalioko nchini huko Kivu.
“Kuhusu makundi yaliosalia ya kigeni yakiwemo FDLR, LRA, ADF/Nalu na FNL yanayoendelea kutaabisha wakaazi wa Kivu ya Kusini na Kivu ya Kaskazini, ninayatahadharisha kutua chini silaha haraka sana. Vyenginevyo, makundi hayo yatapokonywa silaha kwa nguvu na yatachukuliwa hatua kama tunayoendesha hivi sasa.”
Katika hatua nyengine, Rais Kabila ametumia hotuba hiyo kuzionya nchi jirani,ambayo hakuzitaja jina, kwamba amani ya kudumu ya Kanda la Maziwa Makuu itatokana na utekelezwaji wa Mkataba wa amani wa Addis Ababa.
“Kwan nchi jirani, ninaziambia mara nyingine kwamba njia muafaka ya kuleta amani na ustawi wa ukanda huu, ni utekelezwaji wa dhati na kwa nia nzuri kwa Mkataba wa Amani wa Addis Ababa na vile vile Azimio Namba 2098 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Ninawahimiza kutekeleza wajibu wao kulingana na mkataba huo.”
Anyoosha mkono wa diplomasia
Wanajeshi wa Kongo wakifurahia ushindi dhidi ya M23. Wanajeshi wa Kongo wakifurahia ushindi dhidi ya M23.
Rais Kabila amesema ijapokuwa ushindi wa kijeshi umepatikana, lakini juhudi za kidiplomasia na kisiasa zitaendelea.
“Mtizamo wetu ni ule wa kutafuta suluhisho la mzozo wa Kongo kwa njia tatu: ya kijeshi, ya kisiasa na kidiplomasia. Na ndilo tunalofanya sasa. Ushindi wa kijeshi huko Kivu hauwezi kuvunja juhudi zingine za kisiasa na kidiplomasia.”
Kufuatia ushindi wa jeshi la Kongo dhidi ya waasi wa M23, Rais Kabila aliwapongeza wanajeshi na kusema wameungwa mkono na taifa nzima.
Vile vile, aliwapongeza wanajeshi wa Tanzania katika kazi wanayoifanya kwenye kikosi cha Umoja wa Mataifa na kutoa heshima zake na rambirambi za pole kwa familia ya wanajeshi wa Kongo na wale wa Tanzania waliopoteza maisha yao kwenye uwanja wa mapambano.
Rais Kabila alitoa wito wa kutokueko na ulipizaji kisasi baina ya Wakongomani.

WAKENYA WASHINIKIZA WABAKAJI WAKAMATWELiz alibakwa na watu waliomtupa kwenye shimo la choo na kumvunja uti wa mgongo
Mamia ya waandamanaji nchini Kenya wamewasilisha polisi hati ya kutaka kukamatwa kwa watuhumiwa waliombaka msichana huyo wa miaka 16.
Msichana huyo alibakwa na kundi la wanaume na kutupwa katika shimo la choo ambapo alivunjika mgongo wake.
Wanaume wanaotuhumiwa kumbaka msichana huyo waliamriwa na polisi kukata nyasi kama adhabu ya kitendo hicho.
Hati hiyo ya kutaka kuwafungulia mashitaka watuhumiwa wa ubakaji imetiwa saini na watu milioni 1.2 wakitaka watuhumiwa kukamatwa haraka na kuwafikisha mahakamani.
Waandamanaji hao wameelezea kukasirishwa na adhabu hiyo na kuhoji kwa nini polisi hawakufanya uchunguzi ili kumtendea haki msichana huyo.
Pia wanataka polisi waliowaadhibu washukiwa na kisha kuwaachilia, wakamatwe na kufunguliwa mashitaka.
Tayari wanawake milioni 1.2 wameunga mkono kampeini hiyo iliyoanzishwa na mwanaharakati Nebila katika mtandao wa kijamii wa Avaaz ulio na wanachama milioni ishirini na saba kote duniani na inaarifiwa idadi ya wanawake wanaopinga kitendo cha wabakaji na kile cha polisi kuwaadhibu kwa kukata nyasi, inaendelea kuongezeka.
Kampeini hii imekuja baada ya msichana Liz kubakwa na genge la wanaume sita ambao baadaye walimtupa ndani ya shimo la choo.
Liz alipata majeraha mabaya sana na hata kuvunjika uti wa mongo na sasa amelazimika kutumia kiti cha magurudumu na hadi sasa amefanyiwa upasuaji katika sehemu zake za siri.
Polisi waliwakamata watuhumiwa watatu kati ya sita waliodaiwa kumbaka msichana huyo, lakini baadaye wakawaachilia baada ya kuwaadhibu kwa kukata nyasi nje ya kituo cha polisi.

FUMANIZI LA AIBU IRINGA ASUBUHI YA LEO, ALIYEFUMANIWA ADAI ALIPIMA UKIMWI KABLA

 Njemba  linalotuhumiwa kuvunja amri na mke wa  mtu likiwa  limelama  kitandani huku  likiomba msamaha  kwa  kosa hilo
 Hapa  njemba  hilo  likiwa bado limejilaza kitandani kwa mke wa  mtu 
 Polisi  wakimshusha  kitandani mtuhumiwa   huyo
 Wananchi  wa Mtaa wa Mkwawa wakiwa  nje ya nyumba   hiyo na askari polisi
 Mgambo na   wananchi  wakiwa   wameweka ulinzi sawa  mlangoni
 Polisi  wakimpekua  mtuhumiwa huyo  baada ya kuficha simu yake
 Hapa  polisi  wakimtoa mtuhumiwa wa  fumanizi ndani ya nyumba
 gari  la  polisi  likijiandaa  kuondoka  eneo la tukio
 Kijana  mwenye mke  Bw  Kilave  kulia akishusha usafiri  wake wa Baiskeli  iliyotumika kwenda kufanya  fumanizi asubuhi ya leo 
 hapa   mtuhumiwa  huyo akishuka katika gari  la polisi  baada ya  kufika  kituo cha polisi

ASKARI  polisi  mjini  Iringa  wamefanikiwa  kuokoa maisha ya  njemba  mmoja mkazi  wa Ilala  mjini Iringa aliyefumaniwa asubuhi ya leo  kwa tuhuma  za kuvunja  amri ya  sita  na  mke  wa  mtu katika chumba  cha wanandoa hao.

Njemba  hilo lililofumaniwa limejitambulisha  kwa  jina na  Gilberty Mapunda (35) mzaliwa na Manda  wilaya ya Ludewa mkoa wa Njombe  ila  kwa  sasa  ni mkazi  wa Ilala mjini hapa.

 Tukio la  kufumaniwa kwa  njemba  hilo  limetokea majira ya saa 12.30 asubuhi  ya  leo  baada ya mume wa mwanamke  aliyefumaniwa kufika  ghafla  eneo la Mkwawa  jirani na klabu  cha pombe za  kienyeji  cha Mapinduzi  ambako ni nyumbani  makazi  ya  mwanamke huyo .

Hata hivyo katika  hali  ya  kushangaza  ni  pale  njemba  hilo kutaka  kumshikisha adabu mwenye  mke  kwa madai  kuwa   mwanamke  huyo alimweleza  kuwa hana  mume na mume  aliyekuwa nae ni ana mke  wake hivyo hakuona  kosa  yeye  kumsaidia kumpa  huduma mwanamke huyo ambae alikuwa akionyesha kumpenda  zaidi .

" Mimi  kaka  kweli  nilidanganywa na mke  wako  kuwa  wewe una mke  mwingine   hivyo haotafika  nyumbani hapo ....lakini naomba unisamehe ama  tumalizane kwani tambua  kuja  kwangu hapo ni kukusaidia kutoa  huduma kwa  mke wako ambae  mimi amenipenda pia"

Pia  alisema  kuwa kuhusu kuambukizana UKIMWI asiwe  hofu ya kumtazama wembamba  wake  kuwa ni mtu aliyeathirika  .

" Kaka naomba  unielewe  hii afya  yangu ya  wembamba  isikutishe na  kunipa adhabu kubwa ukajua  nimeathirika hapana  hii ni afya  yangu ya kawaida  .....kama  UKIMWI  mimi  nimetoka  kupima juzi  tu nipo salama kabisa kwa  hilo ondoa shaka"

Mume  wa mwanamke  huyo aliyejitambulisha kwa jina  moja la Kilave alisema  kuwa mke  wake anaitwa Beatrice Kisia amepata  kuzaa nae  wawili akiwemo  mmoja wa  kike na mwingine wa kiume  na hata nyumba hiyo  ambayo leo amemfumania mwanaume  huyo ni nyumba  ambayo ameijenga  yeye kwa ajili ya familia yake  hiyo .

Alisema kuwa mtuhumiwa  wa  fumanizi  hilo anatambua  vema  kama mwanamke huyo ni mke wake na kila  wakati  wamekuwa  wakipishana  akipeleka  huduma  .

Kilave  alisema  kuwa jemba hilo baada ya  kuingia katika chumba  chake walilazimika  kumtoa mtoto  mdogo ambae ni mgonjwa na  kumpeleka  chumba  cha  pili alichokuwa amelala  bibi  wa mtoto na  wao kuamua  kukitumia  kitanda hicho kwa mambo  yao.

Pia alisema  mwanamke  baada ya  kuona hali ni  tete  baada ya fumanizi alilazimika  kufungua mlango na  kukimbia nje  na  kumuacha mtuhumiwa  huyo akiendelea  kulala kabla ya  kufungiwa katika chumba hicho hadi  polisi  walipofika na  kumchukua .

Jeshi la  polisi  mkoa  wa  Iringa  limethibitisha  kuwepo kwa  tukio hilo na  kupongeza hatua ya  mwanaume  huyo  kutochukua  sheria mkononi .

Mtandao  huu  wa www.matukiodaima.com  umezungumza na kamanda wa  polisi mkoa  wa Iringa Ramadhan Mungi  juu ya tukio  hilo na amepata   kuthibitisha uwepo  wa  tukio  hilo.
MWISHO
....................................................................................................................................................................................

TANGAZO ! TANGAZO! SHAMBA HEKA 20 IRINGA LINAUZWA BEI POA

Shamba  hili heka 20  lililozungushiwa  miti ya  nguzo za  umeme na ndani ya  miaka miwili  unaweza  vuna mbao linauzwa  pia  shamba  hili linafaa kwa  kilimo cha mazao mbali mbali  kwani  lina  rutuba  ya kutosha iwapo ni mfugaji weweza litumia kwa ufugaji ama kujenga shule  ,kiwanda  n.k 

Shamba  hili  linauzwa Tsh milioni 11 maelewano  zaidi yapo 

Shamba  hili  lipo eneo  la Ifunda  Kibaoni  jirani na shule  ya sekondari  Lyandembela  kwa  mawasiliano tupigie simu 0754 026 299/0712 750 199 au 0789281030

October 30, 2013

RAIS WA CAF AMPONGEZA MALINZI

Jamal Malinzi

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Issa Hayatou amempongeza Jamal Malinzi kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) katika uchaguzi uliofanyika Oktoba 27 mwaka huu.

Katika salamu zake kwa niaba ya Kamati ya Utendaji ya CAF na familia ya mpira wa miguu Afrika, Rais Hayatou amesema uchaguzi huo unampa Rais Malinzi fursa ya kuupeleka mbele mpira wa miguu nchini Tanzania.

Amesema CAF ina imani uwezo wake katika uongozi, uzoefu na ujuzi katika mpira wa miguu havitausaidia mpira wa miguu Tanzania pekee bali Afrika kwa ujumla, na kuongeza kuwa ataendeleza ushirikiano uliopo ili kuwanufaisha zaidi vijana wa bara hili.

Rais Hayatou amemtakia Rais Malinzi kila la kheri katika kipindi chake cha uongozi na kumhakikishia kuwa CAF iko pamoja naye katika kusukuma mbele gurudumu la kuendeleza mpira wa miguu.

PAMBANO LA YANGA, MGAMBO SHOOTING LAINGIZA MIL 37/-
Pambano la Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Yanga na Mgambo Shooting lililochezwa jana (Oktoba 29 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingiza sh. 37,915,000.

Washabiki waliohudhuria mechi hiyo namba 46 iliyomalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 walikuwa 6,515 ambapo viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000.

Mgawo wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 5,783,644.07, gharama za kuchapa tiketi sh. 3,145,790 wakati kila klabu ilipata sh. 8,550,741.95.

Wamiliki wa uwanja walipata sh. 4,347,834.89, gharama za mchezo sh. 2,608,700.93, Bodi ya Ligi sh. 2,608,700.93, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 1,304,350.47, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,014,494.81.

SIMBA, KAGERA SUGAR KUUMANA KESHO
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inaanza raundi ya 12 kesho (Oktoba 31 mwaka huu kwa mechi kati ya Simba na Kagera Sugar itakayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.

Viingilio katika mechi hiyo itakayooneshwa moja kwa moja na Azam Tv kupitia TBC 1 vitakuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 kwa VIP A.

Nayo Yanga itashuka uwanjani Novemba Mosi mwaka huu katika mechi nyingine ya ligi hiyo dhidi ya JKT Ruvu itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Novemba 2 mwaka huu kutakuwa na mechi nne; Mgambo Shooting na Coastal Union (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga), Tanzania Prisons na Oljoro JKT (Uwanja wa Sokoine, Mbeya), Azam na Ruvu Shooting (Azam Complex, Dar es Salaam), na Mtibwa Sugar na Rhino Rangers (Uwanja wa Manungu, Morogoro).

Raundi hiyo itakamilika Novemba 3 mwaka huu kwa mechi moja ambapo Mbeya City itakuwa mwenyeji wa Ashanti United kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

Mechi za kukamilisha mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo zitachezwa Novemba 6 na 7 mwaka huu. Novemba 6 ni JKT Ruvu vs Coastal Union, Ashani United vs Simba, Kagera Sugar vs Mgambo Shooting, Rhino Rangers vs Tanzania Prisons na Ruvu Shooting vs Mtibwa Sugar.

Novemba 7 mwaka huu, Azam itacheza na Mbeya City wakati Yanga itacheza na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

BRAKING NEWS:11 WAFARIKI DUNIA KATIKA AJARI MBAYA YA TRENI NAIROBI


Na kayanda manyanya
Dereva wa treni hiyo anasemekana alinusurika ingawa ametoroka
Watu 11 wamethibitishwa kufariki katika ajali iliyohusisha treni na basi iliyokuwa imewabeba watu wakielekea kazini katika mtaa wa Umoja viungani mwa mji wa Nairobi.
Basi hiyo inayoaminika kuwa na watu 34 iligongwa na treni kwenye njia ya reli kuelekea mjini. Kwa mujibu wa shirika la Red Cross, idadi ya majeruhi imefika 34 na wamepelekwa katika hospitali kuu ya Kenyatta.
Baadhi ya waliojeruhiwa wanasemekana kuwa katika hali mbaya.
Walioshuhudia ajali hiyo wanasema kuwa basi hilo lilisukumwa umbali wa mita hamsini baada ya kugongwa kwa upande.
Inaarifiwa watu sita walifariki papo hapo na wengine wawili kufariki baadaye kutokana na majeraha waliyoyapata.
Wengine wengi wamejeruhiwa kwa mujibu wa shirika la msalaba mwekundu.
Mwandishi wa habari wa shirika la habari la AFP aliyeshuhudia ajali hiyo alisema kuwa basi iliharibiwa vibaya baada ya kugongwa kwa upande na treni ihiyo ilikuwa inasafiri kwa kasi kubwa.
Ajali hiyo imetokea asubuhi wakati wa msongamano wa watu na magari huku watu wengi wakiwa katika haraka kuu kuelekea kazini
CREDIT:BBC

RAIA WA DRC WAKIMBILIA UGANDA


 Na Kayanda Manyanya
Wakimbizi wa DRC wengi wana kimbilia usalama wao nchini Uganda
Melfu ya wakimbizi nchini Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo, wameingia nchini Uganda, huku majeshi ya serikali ya DRC yakipambana vikali na waasi wa M23.
Makabiliano makali kati ya pande hizo mbili yamepamba moto huku kukiripotiwa kutokea mashambulizi ya maombora karibu na mji wa Bunagana ulio kati ya mpaka wa DRC na Uganda.
Msemaji wa shirika la kuwahudumia wakimbizi la UNHCR, alisema kuwa wakimbizi elfu mbili wamevuka na kuingia Uganda hii leo na kuifikisha idadi ya wakimbizi hao hadi elfu tano.
Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa mapema wiki hii alisema kuwa kundi la waasi la M23 lsio tisho tena la kijeshi kufuatia ushindi kadhaa wa jeshi dhidi ya waasi hao ambapo waliweza kuthibiti miji iliyokuwa imetekwa na waasi hao.
Aliongeza kuwa waasi hao wametoeroka maeneo ya Bunagana na kwamba sasa wako katika kipnade kidogo cha ardhi karibu na mpaka wa Rwanda.
Wanajeshi wa DRC wakisaidiwa na jeshi la Umoja wa Mataifa( MONUSCO) walifanikiwa kudhibiti kambi ya kijeshi ya Rumangabo siku ya Jumatatu
CREDIT BBC

MBUNGE MWIDAU AWATAKA WANANCHI TANGA KUONGEZA JITIHADA ZA KIMAENDELEO


MBUNGE wa Viti maalum Mkoa wa Tanga Amina Mwidau (pichani kulia) (CUF), amewataka wananchi wa Mkoa wa Tanga kubadilika kwa kuwa na ari ya kujiletea maendeleo yao na jamii kwa ujumla.

Kauli hiyo ameitoa mjini hapa alipokuwa akizungumza na viongozi wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Tanga (Tanga Press Club).

Alisema kuwa ili maendeleo ya haraka yaweze kupatikana katika mkoa huo ni lazima jamii kubadili kwa kuwa na mawazo chanya.

“Maendeleo ni jambo muhimu sana na katika hili ni lazima tushirikiane kwa dhati. Binafsi ninapenda kupongeza juhudi za chama cha Waandishi wa habari Mkoa wa Tanga kwa kazi kubwa na nzuri wanayofanya katika kutangaza mkoa wetu.

“Nilikuwa nasoma na sasa kila wakati tutakuwa pamoja na wanahabari pamoja na wananchi wa mkoa wetu ili kuweza kuungana kwa pamoja katika juhudi za maendeleo za mkoa,” alisema Mwidau
Mwisho