Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

July 31, 2013

MENGI YAIBUKA MTOTO ALIYETUPWA NDIUKA

Mwenyekiti  wa serikali ya mtaa wa Ndiuka  A Siwema  Ally  akisoma barua  aliyoandikiwa  mwanamke huyo na polisi MakambakoSIKU  moja baada ya mwanamke  aliyetambuliwa  kwa  jina la Stella Mnyagani mwenyeji  wa Mabadaga Chimala wilaya ya  Mbarali mkoa  wa  Mbeya  atelekeza  mtoto  wake  wa  kiume  nje ya  duka  moja  eneo la Ndiuka  'A' katika Manispaa ya  Iringa.
 
Mengi  yafichuka  juu ya mwanamke  huyo  kutelekeza  mtoto  wake inasadikika  mwanamke  huyo alikuwa akifanya kazi ya  kuuza bar  katika  eneo hilo la Ndiuka na baadhi ya maeneo ya mji  wa Iringa.
Mashuhuda  waliobahatika  kumwona mwanamke  huyo  wanadai kabla ya  kutenda  unyama  huo  wa kutupa mtoto  mwanamke  huyo alikutwa katika mitaa mbali mbali ya mji  wa Iringa likiwemo eneo la Ofisi za Tanesco  akiwa amekaa kando ya  barabara  kabla ya  kuondoka  na kuelekea  eneo la Ndiuka ambako aliamua kumtekeleza mtoto  huyo .

Mtoto  huyo  wa  kiume anayekadiliwa  kuwa na  mwaka  mmoja alikutwa  juzi majira ya saa 2 usiku katika  eneo hilo la Ndiuka  'A' huku  akiwa na vifurushi  viwili  vya nguo  pamoja na dawa  za aina  mbali mbali .

Mwenyekiti  wa  serikali ya  mtaa  huo  wa Ndiuka  A Siwema  Ally  alisema  kuwa  mtoto  huyo  aliokotwa na  wasamaria  wema na kupelekwa  kwake  kabla ya  kuchukuliwa na  polisi na  kupelekwa  kituo cha yatima  cha Daily  Bread Life MInistries kinachomilikiwa na Neema Mpeli

Mwanamke  huyo pia  aliacha namba  za  simu ambazo ni  0766663281 inayomilikiwa na Kastori Mlyatage  pamoja na namba  ya Mahenge  wa  Mabadaga  0753493063  na  namba ya mama  Fatuma  0757 519270 pamoja na barua  inayoonyesha  alisaidia  kituo cha  polisi Makambako  kwa  ajili ya Kwenda SingidaAIRTEL TANZANIA YAFURURISHA BAADHI YA WATEJA WAKE

 Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (kushoto) akimkaribisha Ofisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya NMB, Waziri Barnabas katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Airtel kwa wateja wao jijini
Dar es Salaam jana.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (wa pili kushoto) akiwakaribisha baadhi  ya wateja wao katika hafla ya futari iliyoandaliwa na kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya.
 Baadhi ya wateja wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania wakichukua mlo wa futari iliyoandaliwa na kampuni hiyo jijini Dar es Salaamu juzi.
 Baadhi ya wateja wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania wakichukua mlo wa futari iliyoandaliwa na kampuni hiyo jijini Dar es Salaamu juzi.
 Mhariri Mtendaji Mkuu wa Mwananchi Communications, Bakari Machumu (wa pili kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Kolaso (kulia kwake) wakichukua mlo wa futari iliyoandaliwa na Airtel kwa wateja wake jijini Dar es Salaam juzi.
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Azam, Said Salim Bakhresa (wa pili kushoto),  akichukua mlo wa futari pamoja na baadhi ya wateja wa Airtel katika hafla iliyoandaliwa na kampuni hiyo kwa wateja wake
jijini Dar es Salaam juzi.
Baadhi ya wateja wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania wakifuturu katika hafla iiliyoandaliwa na kampuni hiyo jijini Dar es Salaamu juzi.

WAZIRI MKUU WA THAILAND AANZA ZIARA YA KIKAZI TANZANIA, AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS JAKAYA KIKWETE, IKULU


  Waziri mkuu wa Thailand Bi. Yingluck Shinawatra akiwasili nchini Tanzania kwa ziara ya siku tatu leo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
 Waziri mkuu wa Thailand Bi. Yingluck Shinawatra akikagua gwaride la heshima la vikosi vya ulinzi na usalama vya Tanzania mara baada ya kuwasili nchini Tanzania leo.
  Gwaride la vikosi vya ulinzi na usalama vya Tanzania likipita mbele ya jukwaa kutoa heshima kwa Waziri mkuu wa Thailand Bi. Yingluck Shinawatra (kulia) na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete wakati wa mapokezi ya kiongozi huyo leo jijini Dar es Salaam.
 Waziri mkuu wa Thailand Bi. Yingluck Shinawatra akiangalia vikundi vya ngoma akiwa na mwenyeji wake rais Jakaya Kikwete leo jijini Dar es salaam.
 Gwaride la vikosi vya ulinzi na usalama vya Tanzania likipita mbele ya jukwaa kutoa heshima kwa Waziri mkuu wa Thailand Bi. Yingluck Shinawatra (kulia) na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete wakati wa mapokezi ya kiongozi huyo leo jijini Dar es salaam.
 Rais Jakaya Kikwete (kulia) akimkaribisha Ikulu jijini Dar es salaam waziri mkuu wa Thailand Bi. Yingluck Shinawatra (kushoto) mara baada ya kuwasili nchini Tanzania kwa ziara ya siku tatu.
 Waziri mkuu wa Thailand Bi. Yingluck Shinawatra akiwa katika mkutano wa pamoja na viongozi wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam.
 Naibu Waziri mkuu wa Thailand ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Thailand Dr. Surapong Tovichakchaikul (kushoto) na Waziri wa Fedha wa Tanzania Mh. William Mgimwa (kulia) wakibadilishana hati za makubaliano ya kudumisha , kutunza na kuendeleza uwekezaji kati ya Tanzania na Thailand Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Kikwete akizungumza wakati wa mkutano wa viongozi wa Tanzania na Thailand walioongozwa na Waziri mkuu wa nchi hiyo Bi. Yingluck Shinawatra ambapo Tanzania na Thailand zimesaini mikataba minne ya makubaliano ya kubadilishana wafungwa, uendelezaji wa shughuli za uwekezaji, ushirikiano katika masuala ya Ufundi na ushirikiano katika sekta ya Nishati na Madini. Picha na Aron Msigwa – MAELEZO na TheNkoromoBlog

WAFUGAJI WATAKA KATIBA MPYA KUWARUHUSU KUUA SIMBA WANAOVAMIA MIFUGO YAO

Wafugaji  wakazi wa Mlowa  jimbo la Isimani  mkoa  wa Iringa  wakiwa katika mkutano wa kukusanya maoni ya katiba  mpya jana
Mfugaji  akitoa maoni yake  juu ya katiba  mpya  na  kulalamikia  simba  wanaoua mifugo  yao
Mwenzeshaji  Happy Kikoga  kutoka  kituo cha msaada cha sheria na  haki  za  binadamu akiwasomea  rasimu  ya  katiba wananchi  wa Mlowa Isimani
Mmoja kati ya  wanawake  wakazi wa Mlowa  akichangia katika mkutano huo kwa  kutaka  wanaopandikiza chuki  za kidini  kupewa adhabu kali.

WAFUGAJI jamii ya  kimasai na Mang'ati  wakazi  wa Mlowa  jimbo la Isimani  wilaya ya  Iringa  vijijini mkoani Iringa  wametaka katiba mpya ijayo  kuwaweza kuwatetea wafugaji kwa  kuingiza  kipengere  kitakachowaruhusu  wao  kuingia katika  hifadhi ya  Taifa ya  Ruaha  kuwasaka  simba  wanaoua mifugo  yao  kuwaua  .

Wafugaji  hao  walitoa  maoni hayo juzi  katika  ofisi  za serikali ya  kata  wakati  wakichangia rasmu ya katiba mpya  zoezi lililoendeshwa na kituo  cha  msaada cha sheria na  haki  za  binadamu.

Walisema  kuwa  Simba  wameendelea kuwatesa na  kila  wakati  wanaendelea  kuua mifugo yao na  pindi  wanapofanya msako  wa  kuwasaka  askari  wa  wanyamapori  wanawachukulia hatua  kali .

Hivyo  walisema  ili  katiba  ijayo  iweze kutambua haki za  wanyama  wengine na  pia  kutambua  uwepo  wa  wafugaji ni  vema kuingizwa  kipengere  kinachowapa nafasi  ya  kuwaua  simba wanaokula  wanyama  wao.

Mbali ya  kutaka  kuwekwa kwa  kipengere  hicho  bado  wafugaji hao  walitaka  kutambuliwa  rasmi  na katiba  ijayo badala  ya ilivyo sasa  ambapo  wamekuwa wakihamishwa  kama  wanyama .
Pamoja na  wafugaji hao kwa upande  wake wananchi  wa kawaida  wameeleza  kusikitishwa na hatua  iliyofikiwa ya mchakato  huo wa katiba  mpya  hatua ya  kukusanya maoni  juu ya rasmu wakati  wao hata katiba  iliyopita  hawaijui na rasmu  hiyo  hawajapata  kuoina .
 


July 30, 2013

UNYAMA WA KUTISHA ,MWANAMKE IRINGA ATELEKEZA MTOTOMwenyekiti  wa  serikali ya mtaa wa Ndiuka  A akionyesha  dawa  za mtoto huyo


Mtoto  aliyetelekezwa
Polisi wakifika eneo la  tukio

Polisi wakiingia  kwa mwenyekiti wa mtaa aliko mtoto

Mchango  kwa  ajili ya mtoto


Mwanamke  aliyetambuliwa  kwa  jina la Stella Mnyagani mwenyeji  wa Mabadaga Chimala wilaya ya  Mbarali mkoa  wa  Mbeya  atelekeza  mtoto  wake  wa  kiume  nje ya  duka  moja  eneo la Ndiuka  'A' katika Manispaa ya  Iringa.

Mtoto  huyo  wa  kiume anayekadiliwa  kuwa na  mwaka  mmoja alikutwa  jana majira ya saa 2 usiku katika  eneo hilo la Ndiuka  'A' huku  akiwa na vifurushi  viwili  vya nguo  pamoja na dawa  za aina  mbali mbali .

Mwenyekiti  wa  serikali ya  mtaa  huo  wa Ndiuka  A Siwema  Ally  alisema  kuwa  mtoto  huyo  aliokotwa na  wasamaria  wema na kupelekwa  kwake  kabla ya  kuchukuliwa na  polisi na  kupelekwa  kituo cha yatima  cha Daily  Bread Life MInistries kinachomilikiwa na Neema Mpeli

Mwanamke  huyo pia  aliacha namba  za  simu ambazo ni  0766663281 inayomilikiwa na Kastori Mlyatage  pamoja na namba  ya Mahenge  wa  Mabadaga  0753493063  na  namba ya mama  Fatuma  0757 519270 pamoja na barua  inayoonyesha  alisaidia  kituo cha  polisi Makambako  kwa  ajili ya Kwenda Singida

Picha  na habari zaidi  zitakujia