Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

June 30, 2013

LOWASSA AMTAKA OBAMA ASIZUNGUMZIE MAMBO YA USHOGA NA NDOA ZA JINSIA MOJA AKIWA TANZANIA

 

Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo yaNje na Ushirikiano wa Kimataifa, Edward Lowassa, amemtahadhalisha kujiepusha na kauli za kuunga mkono ushoga.

 
Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, ameliambia NIPASHE Jumapili ofisini kwake jijini hapa jana kuwa ushoga na hai za ndoa kwa watu wa jinsia moja vinaweza `kuiharibu’ ziara yake hapa nchini.
 
Mapema wiki hii, Rais Obama alikaririwa akizungumzia masuala hayo yanayotajwa kuwa ni moja ya haki za msingi za binadamu, alipokuwa Senegal, lakini akapingwa.

 
“Watanzania hawatalikubali na wataendelea kushikilia uhuru na heshima walizojengewa tangu awali, kwamba ushoga na ndoa za jinsia moja havikubaliki,” alisema.
Akiwa Senegal, Rais Obama alitaka serikali za Afrika kutoa haki kwa mashoga kama inavyotoa kwa raia wengine.
 
"Ninachotegemea, I pray and hope (ninasali na kutegemea) kwamba kuhusu mashoga na ndoa za jinsia moja, Rais Obama hatarudia kauli aliyoitoa kule Senegal,” alisema.

Aliongeza, "ninasema hivi kwa sababu Tanzania hatuamini katika ushoga, na endapo utawalazimisha Watanzania, watakukatalia na kushikilia uhuru na heshima waliyojengewa toka awali."

 AHIMIZA MAPOKEZI MAZURI
Hata hivyo, Lowassa aliwataka Watanzania kuiheshimu na kuitumiavema fursa ya kutembelewa na Rais Obama, hivyo wajitokeze kumlaki kwa wingi.

 
"Tutambue mataifa makubwa yanakimbilia maslahi ya karne inayofuata, kwa mfano Rais wa China, Xi Jiping siku moja baada ya kuapishwa kwake alikuja hapa nchini, " alisema.

 
Hivyo, alitoa wito kwa Watanzania kuhakikisha maslahi na fursa za kiuchumi zinakuwa za kwanza kulindwa, kwa kuwa ziara hiyo itafungua milango zaidi kwa wawekezaji kuja nchini.

 
Pia, Lowassa alisema ziara ya Rais Obama ni kielelezo cha amani na usalama uliopo, na kwamba itasaidia kuwavutia watalii na wadau wa sekta nyingine za maendeleo kuitembelea Tanzania.

 KITUO CHA KIJESHI
Kuhusu hofu na tetesi kuwa ziara hiyo imelenga taifa hilo kuja hapa nchini kufungua kituo cha kujiimarisha kiulinzi, Lowassa alisema Watanzania wanapaswa kufahamu kuwa tayari nchi hiyo ina kituo cha kijeshi nchini Kenya.

 "Tuangalie maslahi yetu tuachane na mitazamo hasi, kama ni kituo cha kijeshi tayari kipo Kenya, tujiulize kwa nini marais wa Marekani Bill Clinton na George Bush walivyofanyaziara zao hapa nchini hawakwenda Kenya," alisema.

 WALINZI WA NDANI KUWEKWA KANDO
Kuhusu ziara hiyo kutumia ulinzi wa kimataifa huku majeshi ya Tanzania yakiwekwa kando kwa ushiriki wa moja kwa moja, Lowassa alisema Rais wa Marekani ana kiwango cha juu cha ulinzi unaosimamiwa na nchiyake pekee.
 
"Ni sahihi walinzi wetu kukaa pembeni, huyu ni kama Rais wa dunia, lakini hata majeshi yetu yanafanya kazi ya ulinzi lakini sio kwamba yatakaa nyuma tu," alisema.
 
SUMAYE: TUMKARIBISHE

 Naye, Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye, alisema ziara ya Rais Obama haina ujumbe zaidi ya kuhimiza watu wajitokeze kumpokea.
 
Hata hivyo, Sumaye alikwepa kuzungumzia kwa undani hatua ya kuwafukuza wafanyabiashara kutoka kandoni mwa barabara, ili kupisha mapokezi ya Rais Obama.
 
“Ninachokielewa ni kuwa barabara ambazo wanapita viongozi kama Rais Obama zinatakiwa kuwa katikahali ya usalama na hivyo kutakiwa kuboreshwa,” alisema.

LIPUMBA: MAFANIKIO NI MADOGO KIUCHUMI
Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba, alisema mafanikio ya ziaraya Rais Obama yapo katika kujitangaza kimataifa kuliko kiuchumi.
 
Profesa Lipumba ambaye ni mchumi aliyebobea, alisema changamoto iliyopo ni kwamba bado biashara kati ya nchi mbili hizo siyo kubwa kama ilivyo kwa nchi kama China na Tanzania.
 
Alitolea mfano, mwaka 2012 bidhaa za hapa nchini zilizouzwa Marekani zilikuwa na thamani ya Dola milioni 66 ikilinganishwa na zile zilizouzwa China ambapo zilikuwa ni zaidi ya Dola milioni 500.

 
Alisema bidhaa zilizoagizwa kutoka Marekani zilikuwa na thamani ya Dola milioni 230 huku za kutoka China zikiwa na thamani ya zaidi ya Dola milioni 1,100. 

 "Utakubaliana nami kuwa mahusiano yetu na China ni makubwa kuliko Marekani licha ya nchi hii kutoa fursa kwetu ambazo hatujazitumia ipasavyo," alisema

 
Profesa Lipumba alisema Marekani kupitia mpango wake wa kusaidia Maendeleo ya Afrika (AGOA), ulitoa fursa kwa bidhaa za Afrika kuuzwa nchini humo bila ushuru, lakini Tanzania haikuitumia.

 Pia alisema utawala wa George Bush, uliisaidia Tanzania kupitia Mfuko wa Changamoto za Milenia (Millenium Challenge Compact (MCC) kupewa Dola milioni 700 kwa ajili ya kusaidia miundombinu na ujenzi wa nyaya za umeme kutoka bandarini hadi Zanzibar.

 "Pana uwezekano wa mpango wa pili wa MCC, Tanzania ikapata msaada wa kuimarisha miundombinu ya umeme, lakini pia kampuni za Marekani kuja kuwekeza hapa kwetu," alisema.
 
Alisema uwekezaji wa kampuni hizoutategemeana na wafanyabiashara wa hapa nchini pamoja na serikali kutumia fursa mbalimbali za nchi hiyo.

 
Katika hatua nyingine, Profesa Lipumba alisema ili nchi iweze kujikwamua na umasikini itatokana na jinsi itakavyotumia sera na juhudina siyo kutegemea msaada kutoka nje.
 
HOTELI ZIMEJAA

 Wingi wa wageni wakiwamo watakaofika kwa ajili ya ziara ya Rais Obama, umesababisha hoteli nyingi za jijini Dar es Salaam `kujaa’.

 
Uchunguzi wa NIPASHE Jumapili ulibaini kwamba kwa zaidi ya wiki sasa, hoteli nyingi hazikupokea wageni kutokana na kile kilichoelezwa kuwa, nyingine zililipiwa ingawa vyumba havikutumika kwa wakati.

 
POLISI: WASIO NA KAZI WASIJE MJINI
Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga, amewataka wananchi ambao hawatakuwa na mambo muhimu ya kufanya katikati ya jiji, wasifike huko kupunguza msongamano wa watu na magari baada ya kuwasili kwa Rais Obama.

 
Alisema, baadhi ya barabara zitafungwa kwa muda kwa ajili ya viongozi kuzitumia, hivyo kusababisha msongamano.

 
Hekaheka zimetanda jijini Dar es Salaam, ikiwa ni zaidi ya saa 24 kabla ya kuwasili kwa Rais Barack Obama.

 
Rais Obama, atawasili nchini kesho akitokea Afrika Kusini, ambapo pamoja na mambo mengine, alizungumza katika mkutano wa ‘viongozi vijana wa Afrika’ na kujibu maswali kutoka nchi tofauti.

 
Mkutano huo ulifanyika jana jioni huko Soweto nchini Afrika Kusini, ambapo alipokewaa na kujibu maswali kutoka Kenya, Uganda, Nigeria na Afrika Kusini kwenyewe.

 
Jijini Dar es Salaam, shughuli kadhaazikiwamo za ulinzi na usalama, zinafanyika kwa kasi na umakini kuhakikisha ziara ya Rais Obama inafanyika pasipo bughudha. kujibu maswali kutoka Kenya, Uganda, Nigeria na Afrika Kusini kwenyewe.

 
Jijini Dar es Salaam, shughuli kadhaazikiwamo za ulinzi na usalama, zinafanyika kwa kasi na umakini kuhakikisha ziara ya Rais Obama inafanyika pasipo bughudha.

 
Hata hivyo, sehemu kubwa inayohusu masuala ya itifaki, ulinzi na usalama yanafanywa na taasisi za Marekani, kwa kuzishirikisha taasisi za ndani kwa kiwango kidogo.

 
“Hawa jamaa (Wamarekani) wanapoingia nchi yeyote wakiwa naRais wao, shughuli nyingi na uamuzi wanafanya wao, sisi wa ndani inakuwa kushirikishwa kwa kiasi kidogo,” kilieleza chanzo cha NIPASHE Jumapili kutoka moja ya taasisi zinahusika katika ziara hiyo.

 
Maeneo kadhaa ya jijini humo, yaliendelea kudhibitiwa kwa ulinzi mkali na doria za mara kwa mara, huku kandoni mwa baadhi ya barabara wakionekana askari wa Jeshi la Wananchi (JWTZ).

 
Mathalani, kandoni mwa barabara ya Morogoro, eneo la Ubungo, walionekana askari wa JWTZ maarufu kama MP.

 
Shughuli nyingine zimehusisha pia operesheni zinazofanywa na polisi kwa kusaidiana na mgambo wa jiji, kuhakikisha watu na bidhaa zilizopokandoni mwa barabara zitakazotumika kwa ziara ya Rais Obama, vinaondolewa.

 
Magari yaliyowabeba polisi wenye silaha za moto na mabomu ya machozi, yalionekana katika mitaa kadhaa jijini humu, wakihakikisha operesheni hiyo inafanyika pasipo kikwazo kutoka kwa wahusika.

 
Kila palipofanyika operesheni hiyo, baadhi ya askari walifanya doria zamu kwa zamu, kuhakikisha kuwa bidhaa na watu walioondolewa, hawarejei.

 
Hata hivyo, waathirika katika operesheni hiyo walieleza kutofurahia, huku wakihoji ni kwa nini serikali haikuwaandalia mazingira mbadala kabla ya utekelezaji wake. 
 
Walisema miongoni mwao, wamekopa mitaji kutoka kwenye taasisi za kifedha, hivyo kusimamisha biashara zao ili kupisha ujio wa Rais Obama, kutawaweka katika hali ngumu kiuchumi.
 
“Ikiwa ujio wa Rais Obama unatutesa wafanyabiashara kiasi hiki, ni vigumu kuhimili maisha yetu, kwa sababu hatujui hatma yetu baada ya yeye kuondoka,” alisema mfanyabiashara Zena Rashidi wa Kariakoo.

 
Hata hivyo, wamachinga walionekana jana katika kituo cha mabasi cha Mwenge walipofukuzwa, wakiwa wanaendelea na biashara zao.

 Lakini walifanya hivyo kwa tahadhali ikiwamo kushika bidhaa chache mikononi, huku wakitumia 'janja' ya kupiga kelele za 'kumsifia' Rais Obama.

 
Walisikika miongoni mwao wakisema, 'praise to Obama' na wengine wakaitikia 'aaamen'. Walifanya hivyo zamu kwa zamu, lakini haikujulisha waliashiria nini.
 

BARABARA ZAPAMBWA
Aidha, barabara zote atakazopita Obama wakati wa ziara yake zimepambwa kwa bendera za Marekani na Tanzania; huku zikinakshiwa kwa picha yake ambayo imeandikwa 'President Barack Obama' karibu Tanzania.

 
Barabara hizo ni ile ya Nyerere kuanzia uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere, Ali Hassan Mwinyi, Mwai Kibaki na Bagamoyo.

 NIPASHE Jumapili imeshuhudia pichana bendera hizo zikiwa zimewekwa kwenye mabango yote yaliyo barabarani kuanzia Ikulu hadi kwenye barabara hizo huku usafi wa jiji ukionekana kuimarika zaidi.
 
Jana gazeti hili lilishuhudia karibu barabara zote, vijana wanaofanyakazi ya kuweka bendera na picha ya Obama wakifanyakazi hiyo.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

MWEZI WA SITA UMEISHIA ILA MWANANGU MAFUA NA MARALIA INAMTESA

 Mwanangu Flaviana Francis  Godwin akijaribu  kucheza na simu ya mezani kama njia ya  kujipa moyo kutokana na homa kali ya Marilia na mafua inayomsumbua ,kubwa  wadau  tuzidi kuombeana afya  izidi kwenda  sawa .

SWIGA MWAISUMBE NI MTANGAZAJI NA MCHEZAJI SOKA WA RADIO FURAHA FM MWENYE MVUTO UWANJANI

Jana nilipata kuichezea timu ya kituo cha radio Furaha FM Iringa ambao walikuwa na mchezo wa kirafiki na watuma salam mkoa wa Iringa mchezo uliomalizika kwa radio Furaha FM kuichapa bao 2-0 timu ya watuma salam, ila mbali ya ushindi mchezaji Swiga Mwaisumbe kulia kwangu wa Radio Furaha alikuwa ni kivutio uwanjani jinsi alivyowanyanyasa watuma salam kwa chenga chezea Swiga

 Mmiliki wa mtandao  huu mzee wa matukio  daima wa pili kulia akiwa na  wachezaji na watangazaji nyota  wa radio Furaha FM ambao wanafanya vema katika Tasnia na katika  soka  pia ,ilikuwa jumamosi  katika maadhimisho ya miaka mitatu ya kuanzishwa kwa radio Furaha FM

MAPINDUZI MAKUBWA YA UCHOMAJI NYAMA YAINGIA IRINGA NI KIHESA NJE YA RUNGWE GUEST HAKUNAGA IRINGA NZIMA

 Hii ni mishikaki  iliyotayarishwa tayari kwa kuchomwa

 Hii ni kuku  zilizoandaliwa kisasa  zaidi
 Uchomaji wa mishkaki ukiendelea
 Hii ni chachandu  kwa ajili ya kuongeza utamu  zaidi 

Kwa  miaka  mingi  wakazi wa  mkoa wa Iringa walikuwa  wakila nyama kwa  sana japo nyama ambayo haijachoma  kisasa zaidi  ,ila  sasa yameibuka mapinduzi makubwa  zaidi katika  uchomaji nyama yenye radha  ya hali ya juu ukifika na kula mshikaki mmoja eneo hilo  kamwe  hutaacha  kufika  kuendelea  kunya nyama eneo hilo ya Rungwe Lodge  Kihesa Sokoni ni  komesha mbaya kwa  wachoma nyama  Iringa awali  ilikuwa eneo la Zanjabir nje ya karibu na Hotel ya M.R ila  sasa hawa  wamefunika mbaya fika  jaribu muda  wao wa kazi ni kuanzia  saa 12 ;45 jioni .

SPELANSIA MHONDELE NI BINTI WA MIAKA 18 MWENYE NDOTO LA KULITANGAZA TAIFA KISOKA


Mwanadada  mkali  wa soka  Iringa na mikoa ya nyanda za juu  kusini Spelansia Mhondele  akionyesha uwezo wake  kisoka

Hapa  aklionyesha jinsi ya  kutuliza mpira  kwa gamba
Akionyesha mbinu ya  kumkabili  adui  kwa mpira  wa angani
Hapa  akijiandaa kuondoka na mpira  baada ya  kuutuliza  kutoka hewani
 

Timu ya  watuma  salam mkoa wa Iringa ambayo  binti Spelansia ( wa pili  kushoto waliosimama) alipata  kuonyesha soka la uhakika  jana wakati wa mchezo wa kirafikin kati ya  watangazaji wa radio  Furaha Fm na  watuma  salam mchezo uliomalizika kwa  watangazaji  kushinda  baada ya kuigagadua timu ya  watuma  salam mabao 2-0
.......................................................................................

Spelansia  Evaristo Mhondele ni  binti  wa miaka 18  mkazi  wa Kihesa katika manispaa ya Iringa mwenye  kipaji  cha hali ya  juu katika mchezo  wa mpira  wa  miguu mwenye ndoto  za kuj kulipa heshima  kubwa Taifa la Tanzania  katika soka la  wanawake .

“mimi nilihitimu masomo yangu ya  sekondari mwaka 2012 katika  shule ya  sekondari Mlamke katika Manispaa ya  Iringa na  nimepata  kuchaguliwa kujiunga na timu  za UMISETA katika mchezo wa  soka wanawake “

Nilianza  kucheza mpira  mwaka mwaka 2010 nikiwa katika mashindano ya UMISETA  yaliyofanyika katika Ifunda kwa wilaya ya  Iringa  ambako nilikwenda  kushiriki mchezo  wa Basketi  .

Baada ya  kufika  huku nilikuta kuna ushindani mkubwa katika mchezo huo ambao  nilichaguliwa na  hivyo baada ya   kuchujwa  wengi nikiwemo mimi katika mchezo huo  ndipo  nillipoamua  kubadili mchezo na  kuanza kucheza mchezo wa mpira wa  miguu kwa  kufanya mazoezi .

Nilifanya mazoezi  usiku na mchana na baada ya mashindano mengine ya  UMISETA ndipo nilipoamua  kuelekeza  nguvu  huko na kujiunga kabisa katika timu ya mpira wa miguu ya  wanawake .

Kujiunga kwangu na  timu ya  mpira  wa  miguu wanawake  kuniliwezesha  kupita hatua kwa  kuchaguliwa  kuwakilisha  mkoa  wa Iringa katika mashindano ya kanda ya  kusini  kwa  kuelekea  mkoani Ruvuma kwa mara  ya kwanza kufika katika mkoa  huo na baada ya kufanya vizuri huko  nilichaguliwa  kuwakilisha kanda  ya kusini katika mashindano ya kitaifa yaliyofanyika Kibaha mkoani Pwani .

“ Jitihada  binafsi nilizoonyesha  na  wachezaji wenzangu  tuliiwezesha  timu  yetu  kutoka  kanda ya nyanda za juu kusini  kushika nafasi ya  tatu kitaifa “

Mchezaji  huyo anadai kuwa  ndoto yake  kubwa katika soka  kuja kuchezea timu  kubwa  za  kitaifa ili   kuweza  kuonyesha uwezo  wake  zaidi .

“Kwa  sasa  nasuburi  ruhusa ya  mzazi  wangu  ili  kuweza  kuniruhusu   kujikita  zaidi katika michezo  ili  kuweza  kutafuta  fursa ya  kulitumikia  Taifa  langu  Tanzania katika michezo …..nilishindwa  kujiunga na  timu  za  wanawake  nje ya mkoa  kutokana na  wazazi  kunizuia kutokana na  wakati huo  nilikuwa masomoni “

Spelansia  anasema  kuwa  katika maisha  yake wakati akiwa  shule  kwa sehemu  kubwa alikuwa akiwaza  michezo zaidi  na  hasa  kuwa na ndoto ya  kuja  kuchezea timu kubwa za  mpira  wa miguu kwa  wanawake na yawezekana  hata kufeli kwake  kulitokana na mawazo ya  michezo .

Hata  hivyo anasema  kuwa kati ya mambo ambayo katika maisha  anaona  bado  kufanikiwa na hana ndoto ya  kukimbilia  kuolewa  wala katika  mahusiano na  wanaume kwa sasa ni kutokana na  kutotimiza  azma yake ya  kuchezea  timu  kubwa ya  soka  wanawake  nje ya  mkoa  wa Iringa .

Kwani amesema katika mashindano ya  UMISETA kwa jitihada  zake binafsi amepata  kuifungia  timu yake magoli matatu na  kuwa kwa  sasa baada ya  kuhitimu  elimu ya  sekondari amepata kuchezea  timu mbali mbali kama  Kwa kilosa FC , Sengo FC na  timu  ya  watuma  salam mkoa  wa Iringa  wanaume ambapo kwa upande upande wa  Sengo Fc nimepata  kufunga magoli mawili .

Pia  amesema  kuwa anaomba  chama  cha mpira  wa miguu  wanawake  Taifa  iwapo  kuna  nafasi ya  kusajili  wachezaji  wapya  kuweza  kumtazama hata  kumpa nafasi ya majaribio  ili aweze  kuonyesha kipaji chake .

Mwandishi  wa makala  haya  alipata  kushuhudia kandanda safi iliyoonyeshwa na mchezaji  huyo  Speransia wakati  wa mchezo wa kirafiki kati ya  timu ya  watuma  salam mkoa  wa Iringa na  timu ya  watangazaji  wa kituo cha  radio Furaha  Fm ambapo mchezaji Speransia  alipata  kuchezea timu ya  watuma salam na  kuwa binti  pekee katika  timu  hiyo  ya  wanaume  ila aliweza  kuwahenyesha  watangazaji wa radio  Furaha Fm japo  ndio  iliyoweza  kushinda kwa magoli 2-0 dhidi ya  watumasalam

Mwandishi  wa makala  haya ni milimiki wa mtandao  wa www.matukiodaima.com anapatikana kwa simu 0754 026 299 au 0789 281030 barua pepe francisgodwin2004@yahoo.com

WATANZANIA WAONDOLEWA HOFU JUU YA ZIARA YA RAIS OBAMA KESHO , BARABARA ATAKAZOTUMIA ZITANGAZWA

Rais Jakaya Kikwete kushoto akiwa na Rais Barack Obama
....................................................................................
 
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, SAID MECK SADICK, amesema serikali imechukua tahadhari zote katika kuhakikisha shughuli zote za wananchi za kibiashara zinaendelea kama kawaida wakati wa ziara ya rais wa Marekani Barack Obama.
 
Aidha mkuu huyo wa mkoa amesema katika kipindi hicho wafanyabiashara kutoka mikoani na ndani ya jiji wataendelea kuingiza bidhaa zao katika masoko kama kawaida bila kuzuiliwa, na kwamba si barabara zote zitakazofungwa na kutolea mfano wa barabara itakayofungwa kuwa ni barabara ya Nyerere ambayo wageni wengi hutumia na kwamba ziara hiyo haitaathiri maonesho ya 37 biashara maarufu kama sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwl. JULIUS NYERERE.
 
Rais wa Marekani Barack Obama anatarajia kuzuru Tanzania siku ya jumatatu ambapo miongoni mwa masuala atakayoangazia ni pamoja na kuhamasisha demokrasia na kukuza fursa za kiuchumi.
 
Maandalizi ya mapokezi ya Rais Obama yamezidi kupamba moto hasa katika jiji la Dar-es salaam ambapo ndipo kituo chake cha kwanza kwa rais huyo nchini Tanzania huku suala la usafi na matengenezo katika barabara nyingi Jijini likionekana kupewa kipaumbele tofauti na siku zote.
 
Pia abiria wa ndege na wale wa mabasi ya mikoani wametakiwa kuripoti mapema katika vituo vyao ili kuepuka kukosa usafiri siku hiyo ,huku akitaka mabasi ya mikoani ambayo yanaondoka baada ya saa 3 kuzingatia muda kwani baada ya saa 3 barabara zitafungwa hivyo kukosa kusafiri hadi ugeni utakapoondoka
 
Pia  jeshi la  polisi nchini na lile  ya Marekani likakuwa linaweka  rekodi ya matukio yote kwa maeneo yote ambayo Rais Obama atapita  hivyo kwa wale  watakaofanya vurugu  watafuatiliwa popote duniani
TUKIO HILI KWA UDHAMINI WA HOPE SERVICE STATION HAPA HUDUMA NI MASAA 24
Wengi hukimbilia kununua mafuta hapa HOPE SERVICE STATION eneo la CRDB barabara ya Iringa -Dodoma katikati ya mji wa Iringa kituo kinachouza mafuta masaa 24 ,wewe wasumbuka na nini jiunge na kituo cha wengi sasa .
KARIBU UJAZE MAFUTA KWENYE GARI YAKO HAPA HOPE SERVICE STATION TUPO JIRANI NA BENKI YA CRDB MIYOMBONI BARABARA YA IRINGA DODOMA
 

TIMU YA MBEYA CITY NA IGOWOLE SEKONDARI KUFUNGUA PAZIKA LA MASHINDANO YA KOMBE LA MUUNGANO MUFINDI 2013 LEO JUMAPILI


PAZIA la mashindano ya kombe la Muungano Mufindi 2013 kufunguliwa rasmi leo  jumapili june 30 katika uwanja wa shule ya Msingi Igowole kwa timu ya wenyeji lgowole Sekondari kucheza na Mbeya City katika mtanange huo unaotegemewa kwa na ushindano mkubwa kwa wababe hao wa soka.

Mashindano ya Kombe la Muungano Mufindi ni mashindano pekee yenye mvuto mkubwa kwa wadau wa michezo katika mikoa ya nyanda za juu kusini na ni mashindano ambayo yamefanikisha kwa kiasi kikubwa kwa mkoa wa Iringa ,Mbeya na Ruvuma kutoa wachezaji maarufu wanaochezea timu mbali mbali za nje ya mkoa wa Iringa .

Mratibu wa mashindano hayo, Daud Yassin ameueleza mtandao huu wa www.matukiodaima.com kuwa katika ufunguzi huo wa mashindano hayo mgeni rasmi atakuwa mkuu wa wilaya ya Mufindi Evarista Kalalu


Yassin alizitaja timu ambazo zinashiriki mashindano hayo kuwa ni pamoja na Holy Family toka Ruvuma, Mbaspo ya Mbeya, Zamaleki ya Njombe pamoja na timu ya benk ya wananchi Mufindi Mucoba FC wakati kutoka mjini Iringa timu ya Ipogolo FC na Rice FC ndizo zitashiriki mashindano hayo.


Pia alisema kwa mwaka huu mashindano haya yatakuwa na vituo viwili, Igowole na Uwanja wa wambi uliopo mjini Mafinga lengo ni kuwawezesha mashabiki na wadau wa michezo kushuhudia mashindano hayo.

TUKIO HILI KWA UDHAMINI WA HOPE SERVICE STATION HAPA HUDUMA NI MASAA 24
Wengi hukimbilia kununua mafuta hapa HOPE SERVICE STATION eneo la CRDB barabara ya Iringa -Dodoma katikati ya mji wa Iringa kituo kinachouza mafuta masaa 24 ,wewe wasumbuka na nini jiunge na kituo cha wengi sasa .
KARIBU UJAZE MAFUTA KWENYE GARI YAKO HAPA HOPE SERVICE STATION TUPO JIRANI NA BENKI YA CRDB MIYOMBONI BARABARA YA IRINGA DODOMA

U-'BUSY' WA WAZAZI KIBIASHARA UNAVYOATHIRI TAALUM KWA WANAFUNZI

Moja ya mazoko ya mzunguko (magulio) yaliokoa Wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro
Na Mwandishi Wetu, Rombo
 
LICHA ya kuwepo kwa shule za msingi na sekondari kwa Mkoa wa Kilimanjaro ambazo kwa kiasi fulani zinakidhi mahitaji, bado kuna changamoto kadha wa kadha ambazo zinaathiri maendeleo ya kitaaluma kwa baadhi ya maeneo. Wilaya ya Rombo ambayo ni moja ya wilaya za Mkoa wa Kilimanjaro ni miongoni mwa maeneo yanayokabiliwa na changamoto za kipekee kitaaluma hasa elimu ya sekondari.
 
Wilaya hii imefanikiwa kuwa na shule nyingi za sekondari hasa zile za Serikali licha ya kukabiliwa na changamoto kadhaa katika uendeshaji wa shule hizi. Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa wadau wa elimu wilayani Rombo, kuna jumla ya shule za Sekondari 48; yaani shule zinazomilikiwa na Serikali 41 huku zile za binafsi zikiwa saba tu.
 
Tofauti na maeneo mengine ya Tanzania idadi kubwa ya wazazi wilayani Rombo wana mwamko wa kuwapeleka watoto wao shule kupata elimu ya sekondari mara baada ya elimu ya msingi. Hatua hii pekee ya kumpeleka sekondari mtoto ni kutambua umuhimu wa elimu kiasi fulani kwa mtoto. Wapo pia wanaojitahidi na hata kulipa michango na mahitaji kwa wakati japo si wote.
 
Lakini kumpeleka mtoto shule na kutomfuatilia anafanya nini wakati gani na hata anaporudi nyumbani baada ya shule haitoshi. Uchunguzi mdogo uliofanyika katika baadhi ya maeneo ya mpakani mwa Tanzania na Kenya katika ndani ya Wilaya ya Rombo, yakiwemo maeneo ya Holili, Tarakea na Rongai imebaini licha ya baadhi ya wazazi kuwa na mwamko wa kuwapeleka sekondari watoto wao hawafuatilii maendeleo yao kabisa.
Moja ya masoko ya mzunguko (magulio) yalioko wilayani Rombo, Kilimanjaro.

Hali hii imesababisha wanafunzi hao kujihusisha na shughuli nyingine zaidi ya elimu za kutafuta fedha (biashara). Maeneo haya yapo mpakani sehemu ambazo zinashughuli nyingi za kibiashara na kazi ndogo ndogo za kufanya. Uchunguzi umebaini wapo wanafunzi ambao hufanyabiashara na kazi za vibarua ndogo ndogo huku wakiendelea na shule jambo ambalo linaathiri maendeleo yao kitaaluma na eneo zima.

Wapo wanafunzi wa sekondari ambao hufanya kazi za kuendesha pikipiki za abiria maarufu kama bodaboda mpakani na huku wakiendelea na shule, wapo pia ambao hufanya vibarua vya kubeba mizigo na hata kulimishwa kwenye mashamba hasa eneo la Kenya na kulipwa ujira wa siku. Shughuli hizi za utafutaji kipato zinapowanogea wengine huacha kabisa shule na kuendelea za shughuli za utafutaji kipato.
 
Wasichana wao hukimbilia kufanya kazi za ndani hasa kwa wenyeji wa Kenya na pia kufanya kazi za uuzaji vinywaji baa. Mji wa Loitokitoki uliopo mpakani kabla ya kuingia nchini Kenya ndio wenye idadi kubwa ya biashara na shughuli kama hizi ambazo hufanywa na wasichana wengine wakiwa wamekimbia shuleni ama baada ya darasa la saba bila kujali kama amechanguliwa kuendelea au kuishia mnjiani kutokana na uangalizi mdogo ki-malezi.
 
Ramadhan Ally ni mmoja wa wakazi wa Tarakea wilayani Rombo, anasema baadhi ya wanafunzi huamua kujiingiza kwenye shughuli za utafutaji kipato kutokana na usimamizi mdogo wa wazazi/walezi wao.
 
“Wapo wazazi ambao wamewaacha watoto wao chini ya uangalizi wa bibi au babu wao wapo ‘busy’ kibiashara nchini Kenya, wapo wazazi wengine huwashirikisha watoto wao kufanya vibarua vya mpakani ili kukuza kipato cha familia…sasa hali kama hii inamfanya mtoto asione umuhimu wa shule na wakati mwingine baadae uamua kuacha kabisa shule,” anasema Ally.
 
Anaongeza kuwa wapo baadhi ya wazazi hawawatimizii mahitaji ya shule watoto wao hivyo watoto kuamua kutafuta chochote wenyewe. Hili huwenda likawa na ukweli, uchunguzi uliofanyika katika sekondari za Tanya, Nduweni, Ngaleko, Urauri na Mbomai umebaini muitikio wa ulipaji wa ada na michango mingine kwa wazazi/walezi ni mdogo sana kwa wazazi. Kiujumla madeni ni mengi dhidi ya wanafunzi.
Moja ya masoko ya mzunguko (magulio) yalioko wilayani Rombo, Kilimanjaro.

Venance Mramba ni Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Sekondari ya Nduweni, katika mazungumzo na mwandishi wa makala haya anakiri mwamko mdogo wa waza/walezi kwa ulipaji ada na michango mingine shuleni hapo. “…Ukweli hapa madeni ya wanafunzi ni mengi ikiwemo ada na michango mingine…,” anasema Mramba.

Victus Kiwango ni Mkuu wa Sekondari ya Tanya iliyopo wilayani Rombo maeneo ya mpakani, anakiri pia mwamko mdogo wa wazazi kuchangia ada na michango mingine katika shule yake, anaongeza kuwa wapo wanaodiriki kusema kuwa uwezo wao kiuchumi ni mdogo wa ulipaji ada na michango mingine.
 
Hata hivyo kwa upande wake Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Sekondari ya Holili, Benson Samizi iliyopo eneo la Wilaya ya Rombo mpakani anabainisha kuwa mwitikio wa wazazi kufuatilia maendeleo ya watoto wao shuleni hapo ni mdogo kabisa. Anasema hata wanapo itisha mkutano wa wazazi shuleni hapo mwitikio huwa ni mdogo pia, wazazi wengi huagiza wawakilishi baada ya kuja wao wenyewe.
 
“…Changamoto nyingine shuleni kwetu ni u-’busy’ wa wazazi na biashara zao. Naamini wazazi wengi hapa hawafuatilii maendeleo ya watoto wao shuleni, mzazi utakuta unamuita kumshirikisha jambo kwa maendeleo ya manae lakini anatuma mwakilishi, majukumu yao kiusimamizi kwa mtoto anayatupa kwa mwalimu…sasa mwalimu hawezi kufanya kila kitu bila ushirikiano na mzazi,” anasema Samizi.
 
“Binafsi nilijaribu kufanya utafiti mdogo shuleni kwetu wa kuangalia ni kwa kiasi gani wazazi wanafuatilia maendeleo ya mtoto shuleni…lakini huwezi amini kwa mwaka mzima walikuja wazazi wawili tu wenyewe kuulizia maendeleo ya watoto wao, hapa unaweza kuangalia ni namna gani watu hawa wapo ‘busy’ na shughuli zao zaidi ya maendeleo ya mtoto shuleni. Hata ukiitisha kikao cha wazazi hawafiki robo tatu ya wanafunzi wanaokuja shuleni,” anasema mwalimu Samizi.
 
Aidha anakiri uwepo wa wanafunzi ambao hurubuniwa na kujiingiza katika shughuli nyingine nje ya masomo na wengine kuacha shule. Anasema kuwa kwa mwaka 2013 shule hiyo ilipewa jumla ya wanafunzi wa kidato cha kwanza 140 lakini walioripoti ni wanafunzi 85 tu, huku wengine 30 kupelekwa katika shule za binafsi. idadi iliyosalia hawajulikani walipo hadi sasa.
 
Anaongeza kuwa kuanzia mwaka 2011 hadi Mai 2013 jumla ya wanafunzi 7 walitiwa mimba na kesi zao kushughulikiwa katika hatua anuai.
 
Sim Msami Silayo ni Mwalimu Mkuu wa Sekondari ya Urauri iliyopo maeneo ya mpakani Wilaya ya Rombo, anasema tangu nyakati za ukoloni kulikuwa na kasumba ya wanafunzi kwenda kufanya vibarua maeneo ya mpakani anasema hali hii imeendelea mpaka leo. Anasema zipo baadhi ya familia zinautaratibu wa kwenda kufanya vibarua kwa makundi hivyo kuwaathiri baadhi ya wanafunzi.
 
Anasema kwa taarifa ambazo wanazo wapo baadhi ya mabinti hukimbia shule na kwenda kufanya kazi za uuzaji vinywaji baa na wengine kazi za majumbani hali ambayo uongozi wa shule umekuwa ukiendelea kupambana kukabiliana na changamoto hiyo.
 
Wakati hali iko hivyo wanafunzi kama Thabit Kayanda (si jina lake halisi) japokuwa ni mmoja wa wanafunzi wilayani Rombo wanamtazamo tofauti. “…Unapoona mzazi yupo ‘busy’ na biashara zake kiasi hata cha kutokutimizia mahitaji yako ya shule lazima uanze kujitengenezea maisha yako mwenyewe hivyo mtu unajikuta unaingia katika biashara au shughuli zingine kujipatia fedha.
 
 Na kama unafanya na kufanikiwa (kupata fedha) unajikuta unaona hakuna haja ya kuendelea na shule…kumbuka kila mmoja anasoma ili aje kupata fedha za kuendesha maisha yake, kama unaanza kufanikiwa chochote hakuna haja ya kuendelea na shule,” ni maneno ya Kayanda na mtazamo tofauti.
 
Hata hivyo mtazamo wa wanafunzi kama Kayanda na changamoto nyingine zilizopo wilayani Rombo haziondoi umuhimu wa elimu kwa kila mtoto. Hivyo kila mmoja na kila upande unakila sababu ya kuhakikisha unatimiza wajibu wake na elimu kupewa kipaumbele maeneo yote bila kujali changamoto zilizopo.

June 29, 2013

GAPCO TANZANIA YAINGIA MKOA WA TANGA KUFANYA PROMOSHENI YAKE YA GAPCO RELSTARMwakilishi wa Kampuni ya Gapco T LTD Bw. Atanas Jumbe kulia akimkabizi zawadi kwa Mwakilisha wa Ofisa utamaduni wa Mkoa wa Tanga Bi,Tima Koja wakati wa promosheni ya Gapco Relstar inayoendelea katika jiji laTanga jana eneo
picha na super D blog
Mwakilishi wa Kampuni ya Gapco T LTD Bw. Atanas Jumbe kushoto akimkabizi zawadi kutoka Kampuni ya Gapco Tanzania Bw,Amoody Amiri Koja wakati wa promosheni ya Gapco Relstar inayoendelea katika jiji laTanga jana eneo
picha na

Wasanii wa JCB Dominion wakitoa burudani wakati wa promosheni ya Gapco Relstar Oil inanayotengenezwa na Kampuni ya Gapco T LTD Eneo la Makolola Tanga kutoka kushoto ni Omar Salimu na Jafari Halawi picha na Blog ya Super D

Wasanii wa JCB Dominion wakitoa burudani wakati wa promosheni ya Gapco Relstar Oil inanayotengenezwa na Kampuni ya Gapco T LTD Eneo laMkwakwani Tanga kutoka kushoto ni Omar Salimu Halima Masoud na Jafari Halawi picha na BLOG YA SUPER D

Mwakilishi wa Kampuni ya Gapco T LTD Bw. Atanas Jumbe kushoto akimkabizi zawadi kutoka Kampuni ya Gapco Tanzania Bw, Keya Juma wakati wa promosheni ya Gapco Relstar inayoendelea katika jiji laTanga jana eneo kwa minji
picha na Blog ya Super D
Mwakilishi wa Kampuni ya Gapco T LTD Bw. Atanas Jumbe kulia akimkabizi zawadi kwa Mwakilisha wa Ofisa utamaduni wa Mkoa wa Tanga Bi,Tima Koja wakati wa promosheni ya Gapco Relstar inayoendelea katika jiji laTanga jana eneo

TANGA

Wawakilishi wa Kampuni ya Gapco wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuingia Tanga kwa ajili ya promosheni ya Gapco relstar Oil

MTANDAO WA FULL SHANWE SASA UPO HEWANI ..............Mtandao  wa Fullshangwe unapenda  kuwaomba radhi  wadau  wote kwa  kutokuwepo hewani  kutokana na  sababu  za  kiufundi ila kwa  sasa kila kitu  kipo  powa hivyo  karibuni kutembelea.

MEYA JERRY SILAA AWATAKA WATANZANIA KUTUNZA NA KULINDA AFYA ZAO ILI KUJENGA FAMILIA NA JAMII YENYE AFYA BORA.

IMG_2846
Wananchi wa Tanzania wameelezwa kuwa kazi ya kuboresha huduma za afya na afya ya mazingira na maji ni ngumu na kuwa inahitaji nguvu za pamoja kati ya jamii, halimashauri na wadau mbalimbali ili kupata mafanikio yaliyokusudiwa hasa ya uzuiaji wa magonjwa.
Akitoa nasaha wakati wa kufunga wa zoezi la utoaji wa huduma za afya kwa uwiano katika jamii kata ya Gombo la Mboto, Mgeni rasmi Mh. Jerry Silaa, Mstahiki Meya wa halmashauri ya Manispaa ya Ilala amesema huduma za afya na afya ya mazingira ni muhimu katika maisha ya kila siku ya binadamu.
Ameongeza kwa kuwapongeza sana wakazi wa Gomngo la mboto Markaz pamoja na viongozi wao kwa juhudi kubwa walioifanya katika kuhakikisha uwepo wa kituo cha tiba karibu na jamii na kuwa wanastahili kuwa mfano wa kuigwa na jamii zingine.
Aidha amesema hilo ni moja wapo katika utekelezaji wa agizo la Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika lengo lake la kupeleka huduma za tiba zikiwamo zile za zinazohitaji madaktari bingwa karibu na wananchi.
IMG_2792
Pichani juu na chini ni wakazi wa Gongo la Mboto wakimsikiliza Diwani wao ambaye pia ni Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa wakati wa kufunga zoezi la utoaji wa Huduma za Afya kwa Uwiano katika Jamii kata ya Gongo la Mboto.
IMG_2813
IMG_2798
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ilala Dr. Asha Mahita akielezea dhamira ya Idara katika kuendeleza Afya ya Jamii kwa kusogeza Huduma za Afya karibu na Jamii, Huduma hizo zinahusisha matibabu kwa magonjwa mbalimbali kama Magonjwa ya Moyo, Kisukari, Malaria, Macho, Meno, Afya ya Akili, Ushauri na kupima VVU kwa hiari, Elimu juu ya Uzazi wa Mpango na Afya ya Uzazi, Afya ya Mazingira, Lishe, na Jinsia, pia ametoa tathmini ya wakazi wa Kata ya Gongo la Mboto Markaz waliopatiwa huduma za Afya bure kwa zoezi lililofanyika kwa muda wa siku tatu ikiwemo Afya ya Akili, Kifua Kikuu na matibabu ya Ujumla.
IMG_2763
Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto ambaye pia ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akifurahia jambo na mmoja wa wakazi wa kata ya Gongo la Mboto aliyefika katika Zahanati hiyo kupatiwa Huduma ya Bure.
IMG_2869
Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akipima Presha wakati wa kufunga zoezi la Utoaji wa Huduma za Afya kwa Uwiano katika jamii ikiwa ni ishara ya kuhamasisha watu kujenga utamaduni wa kupima Afya zao.
IMG_2882
Wakazi wa Kata ya Gongo la Mboto wakipatiwa dawa za bure baada ya kufanyiwa vipimo wakati wa kutoa Huduma ya Upimaji Afya Bure kwa wakazi wa kata hiyo iliendehshwa kwa siku tatu.
IMG_2760
Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto Jerry Silaa akifurahi jambo na watoto waliofika katika Zahanati hiyo kupatiwa huduma ya Upimaji Afya bure.
IMG_2900
Mtaalamu wa Magonjwa ya Kisukari kutoka Kituo cha Afya Amana Dkt. Abushiri Rajabu akitoa maelezo kwa Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto Jerry Silaa kuhusu Elimu anayotoa kwa jamii kuhusiana na Ugonjwa huo.