Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

May 31, 2013

SERIKALI MBEYA YATAKIWA KUWAKUMBUKA WAKULIMA

Na Esther Macha, Mbeya 

 SERIKALI Mkoani Mbeya imeshauriwa kuweka mikakati ya kuweza kuwasaidia watu wasiojiweze hususan walemavu,vikongwe na watoto waishio katika mazingira magumu ili kuwaondoa na hadha wanazokumbana pindi wanapokuwa wakiomba kifedha kutoka kwa wasamalia wema hali inayowapelekea kunyanyapaliwa kwa kiasi kikubwa. 

 Wakizungumza na Mtandao huu mwishoni mwa wiki baadhi ya wananchi mkoani mbeya walisema kuwa serikali inapaswa kutambua kuwa watu walio katika makundi hayo wanauhitaji mkubwa wa kupatiwa misaada hususan kupatiwa huduma za afya bure .

 “Hii ni changamoto kubwa kwa serikali ambayo inatakiwa kufanyiwa ufumbuzi wa haraka kwa kuweka mikakati itakayosaidia kuwaondoa katika tatizo la kuzagaa mitaani na kuomba misaada kwa wasamalia wema”Alisema Mkazi wa jijini hapa Samson mwakifuna. 

Bw.Mwakifuna alisema kuwa si jukumu la serikali pekee kusaidiwa watu walio katika makundi hayo bali hata jamii na wadau tunapaswa kusaidia hususan mavazi,chakula na huduma nyingine za kijamii. 

 “Watu walio katika makundi hayo wamekuwa wakikubwa na changamoto mbalimbali na kwamba hilo nin jukumu letu sote kuwasaidia na kupiga vita vitendo vya kunyanyapaliwa vinavyofanywa na baadhi ya wasiokuwa na utu hususan kuwafanyia vitendo vya kinyama vya ubakaji”Alisema. 

 Aidha alifafanua kuwa ni wakati sasa wa jamii kutofumbia macho vitendo vya unyanyapaa unaofanywa kwa jamii kwa kuwafuchua watu wanaojihusisha na vitendo hivyo kwani vimekuwa vikiwanyima uhuru wa kuishi kwa amani na kuwa hatarisha na magonjwa hatari ya maambukizi ya virusi vya ukimwi.
 Mwisho.

MIKUTANO YA KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA NA NAPE TISHIO UPINZANI MAKETE,WANACHAMA 78 CHADEMA NA CUF WAJIUNGA


Katibu  mwenezi na itikadi  wa CCM Taifa  Ndugu Nape Nnauye akicharaza  solo  huku wanahabari  na mpiga picha mkuu  wa Jamboleo Richard Mwaikenda (katikati) na mhariri  wa Jambo leo Said Mwishehe wakiburudika  huku wakiendelea  kupata chochote wakati  wa  ziara   hiyo kijiji  cha Iniho wilayani Makete


              Mjumbe  wa  kamati  kuu  ya CCM Taifa Pindi  Chana  akisalimia  wananchi  wa  kijiji cha Iniho wilayani Makete       6Naibu Waziri wa Maji na mbunge wa jimbo la Makete Injinia , Dk. Bilinith Mahenge akiwahutubia wananchi wa kata ya Iniho wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kata hio wakati Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana alipotembelea kata hiyo 8Mkuu wa Wilaya ya Makete Bi. Josephine Matiro akizungumza na wananchi kuelezea jinsi serikali inavyotekeleza miradi ya maendeleo katika wilaya hiyo.9Wananchi wa Kata ya Iniho wakiwa katika mkutano huo 10Kikundi cha ngoma kikicheza ngoma ya asili ya kinyakyusa inayoitwa Ing’oma. 17Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi CCM Ndugu Nape Nnauye akiteta jambo na Mzee Pascal Sanga mjumbe wa shina la Singida  katika kata ya Tandala Wilayani Makete wakati katibu mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana alipotembelea katika kata hiyo leo 18 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akizungumza na wanachama wa chama cha mapinduazi katika shina la Singida kata ya Tandala wakati alipotembelea katika kata hiyo leo19Mzee Pascal Sanga Mwenyekiti  wa shina la Posta  katika kata ya Tandala Wilayani Makete akifungua kikao hicho baada ya Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana na ujumbe wake kutembelea tawi hilo. 22 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana na ujumbe wake akiongozana na Mkuu wa Wilaya ya Makete Bi. Josephine Matiro kutembelea tawi la Singida kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Makete Francis Chaula3Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi CCM Ndugu Nape Nnauye  akiwahutubia wananchi katika kata ya Iniho Wilayani Makete.

SERIKALI YASIKITISHWA NA TAARIFA ZILIZOCHAPISHWA MAGAZETINI

                


Fenella-Mukangara

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Serikali imesikitishwa na taarifa zilizochapishwa na gazeti la Mtanzania Jumapili ukurasa wa 19 toleo namba 7327 la tarehe 26 Mei mwaka huu yenye kichwa cha “DR. MUKANGARA ANA ROHO NGUMU HAJALI KITU” na ile ya gazeti la Rai la Alhamisi 30 Mei 2013 yote ya Kampuni ya New Habari (2006) Limited inayosema “ YA MUKANGARA YASIACHWE YAKAPITA”.
 
Taarifa hizo hazina ukweli na waandishi wa maoni hayo  wanaonekana kutaka kumchonganisha Waziri na wananchi kwa kuandika mambo ambayo hayana ukweli na yenye dhamira ya kumchafua Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Dr. Fenella Mukangara .
 
Ikumbukwe kwamba wakati Said Kubenea akimwagiwa tindikali na Ndimara Tigambwage akiumizwa na majambazi ilikuwa mwaka 2008 wakati huo Waziri Mukangara hakuwa Waziri wala hakuwa Mbunge .
 
Kadhalika mwandishi wa habari Richard Masatu alifariki huko Mwanza mwaka 2011, Waziri Mukangara alikuwa Naibu Waziri chini ya Dr. Emmanuel Nchimbi.
 
Masuala ya waandishi wa habari kuuawa na kuumizwa yako katika vyombo vya sheria  hivyo basi si sahihi kwa Waziri wa Habari kutoa kali kabla ya  vyombo husika havijamaliza kazi zake. Mara baada ya vyombo hivyo kumaliza kazi yao Wizara itakuwa na cha kuwaambia wananchi.
 
Vile vile ikumbukwe kwamba Serikali hufanya kazi kama kitu kimoja wakati wa utekelezaji wa majukumu yao mbalimbali ambayo yaweza kuingilia toka Wizara moja hadi nyingine , hivyo baada ya kutokea kwa kifo cha David Mwangosi waandishi wa habari waliandamana hadi Jangwani ambapo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dr. Emmanuel Nchimbi alikwenda viwanja vya Jangwani kutoa pole kwa Waandishi wa habari kufuatia kifo hicho kwa niaba ya Serikali lakini waandishi walikataa uwepo wake katika kusanyiko lile.

Hatua ya wanahabari waliokuwa wamekusanyika Jangwani kumkataa Waziri Nchimbi ilisababisha Serikali kushindwa kutoa pole zao ambapo zingejumuisha Serikali na wadau wote.
 
 
Kwa hiyo tunawaomba waandishi wa habari wanapoandika maoni au makala ni vema  wakawasiliana na wahusika au wanaowashutumu  ili nao wapate fursa ya kujitetea na sio kuwalisha mawazo ambayo hawakuwa nayo.
 
Aidha,waandishi wa maoni wasilazimishe matakwa na maoni yao binafsi yaonekane kuwa sahihi na hivyo Serikali lazima ifanye wanavyotaka wao na ni vyema wangepata muda wakamhoji Waziri mwenye dhamana ya habari wakapata ukweli kuliko wao kumuhukumu Waziri kwa kuwa tu wahariri wao wamewapa nafasi katika magazeti yao kuandika maoni yao ambayo ni potofu na yanataka kujenga chuki dhidi ya waziri mbele ya jamii
Vile vile ni jukumu la Waziri kuzisemea sekta za habari,Vijana,Utamaduni na Michezo zikiwemo Taasisi zote zilizopo katika sekta hizo na si vinginevyo.
 
Inashangaza kuona mwandishi wa maoni katika gazeti la Mtanzania Jumapili akihoji Waziri kuzungumzia sekta ya habari, vijana , utamaduni na michezo na Taasisi kama vile Shirika la Utangazaji na mbio za Uhuru na kuziita ni porojo.
 
Watoamaoni wameshindwa hata kuona mambo mazuri yaliyomo katika Kitabu cha Bajeti ya 2013/14 ikiwemo kuleta Bunge muswada wa uanzishwaji wa Baraza la Vijana , na Muswada wa kusimamia vyombo vya habari kwa ajili ya kuboresha maslahi na utendaji wa wanahabari ikiwemo kuwa na Bima wanapokuwa katika kazi hatarishi.
 
Hata hivyo Mheshimiwa Waziri anahuzunisha na vitendo vya kikatili ambavyo wanavyofanyiwa waandishi wa habari na hivyo kutoa wito kwa wananchi kuviachia vyombo vya usalama viendelee kufanya kazi yake
Kwa ujumla taarifa hizo zimemhuzunisha Mh. Waziri kwa kuwa amekuwa akishirikiana na anaendelea kushirikiana bila kuchoka na waandishi wa habari katika shughuli mbalimbali ziwe za raha na huzuni.

SERIKALI YASIKITISHWA NA TAARIFA ZILIZOCHAPISHWA MAGAZETINI

                


Fenella-Mukangara

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Serikali imesikitishwa na taarifa zilizochapishwa na gazeti la Mtanzania Jumapili ukurasa wa 19 toleo namba 7327 la tarehe 26 Mei mwaka huu yenye kichwa cha “DR. MUKANGARA ANA ROHO NGUMU HAJALI KITU” na ile ya gazeti la Rai la Alhamisi 30 Mei 2013 yote ya Kampuni ya New Habari (2006) Limited inayosema “ YA MUKANGARA YASIACHWE YAKAPITA”.
 
Taarifa hizo hazina ukweli na waandishi wa maoni hayo  wanaonekana kutaka kumchonganisha Waziri na wananchi kwa kuandika mambo ambayo hayana ukweli na yenye dhamira ya kumchafua Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Dr. Fenella Mukangara .
 
Ikumbukwe kwamba wakati Said Kubenea akimwagiwa tindikali na Ndimara Tigambwage akiumizwa na majambazi ilikuwa mwaka 2008 wakati huo Waziri Mukangara hakuwa Waziri wala hakuwa Mbunge .
 
Kadhalika mwandishi wa habari Richard Masatu alifariki huko Mwanza mwaka 2011, Waziri Mukangara alikuwa Naibu Waziri chini ya Dr. Emmanuel Nchimbi.
 
Masuala ya waandishi wa habari kuuawa na kuumizwa yako katika vyombo vya sheria  hivyo basi si sahihi kwa Waziri wa Habari kutoa kali kabla ya  vyombo husika havijamaliza kazi zake. Mara baada ya vyombo hivyo kumaliza kazi yao Wizara itakuwa na cha kuwaambia wananchi.
 
Vile vile ikumbukwe kwamba Serikali hufanya kazi kama kitu kimoja wakati wa utekelezaji wa majukumu yao mbalimbali ambayo yaweza kuingilia toka Wizara moja hadi nyingine , hivyo baada ya kutokea kwa kifo cha David Mwangosi waandishi wa habari waliandamana hadi Jangwani ambapo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dr. Emmanuel Nchimbi alikwenda viwanja vya Jangwani kutoa pole kwa Waandishi wa habari kufuatia kifo hicho kwa niaba ya Serikali lakini waandishi walikataa uwepo wake katika kusanyiko lile.

Hatua ya wanahabari waliokuwa wamekusanyika Jangwani kumkataa Waziri Nchimbi ilisababisha Serikali kushindwa kutoa pole zao ambapo zingejumuisha Serikali na wadau wote.
 
 
Kwa hiyo tunawaomba waandishi wa habari wanapoandika maoni au makala ni vema  wakawasiliana na wahusika au wanaowashutumu  ili nao wapate fursa ya kujitetea na sio kuwalisha mawazo ambayo hawakuwa nayo.
 
Aidha,waandishi wa maoni wasilazimishe matakwa na maoni yao binafsi yaonekane kuwa sahihi na hivyo Serikali lazima ifanye wanavyotaka wao na ni vyema wangepata muda wakamhoji Waziri mwenye dhamana ya habari wakapata ukweli kuliko wao kumuhukumu Waziri kwa kuwa tu wahariri wao wamewapa nafasi katika magazeti yao kuandika maoni yao ambayo ni potofu na yanataka kujenga chuki dhidi ya waziri mbele ya jamii
Vile vile ni jukumu la Waziri kuzisemea sekta za habari,Vijana,Utamaduni na Michezo zikiwemo Taasisi zote zilizopo katika sekta hizo na si vinginevyo.
 
Inashangaza kuona mwandishi wa maoni katika gazeti la Mtanzania Jumapili akihoji Waziri kuzungumzia sekta ya habari, vijana , utamaduni na michezo na Taasisi kama vile Shirika la Utangazaji na mbio za Uhuru na kuziita ni porojo.
 
Watoamaoni wameshindwa hata kuona mambo mazuri yaliyomo katika Kitabu cha Bajeti ya 2013/14 ikiwemo kuleta Bunge muswada wa uanzishwaji wa Baraza la Vijana , na Muswada wa kusimamia vyombo vya habari kwa ajili ya kuboresha maslahi na utendaji wa wanahabari ikiwemo kuwa na Bima wanapokuwa katika kazi hatarishi.
 
Hata hivyo Mheshimiwa Waziri anahuzunisha na vitendo vya kikatili ambavyo wanavyofanyiwa waandishi wa habari na hivyo kutoa wito kwa wananchi kuviachia vyombo vya usalama viendelee kufanya kazi yake
Kwa ujumla taarifa hizo zimemhuzunisha Mh. Waziri kwa kuwa amekuwa akishirikiana na anaendelea kushirikiana bila kuchoka na waandishi wa habari katika shughuli mbalimbali ziwe za raha na huzuni.

May 30, 2013

KIONGOZI WAKO AMETEKELEZA AHADI YAKE?

Mbunge wa Njombe Kaskarini Deo Sanga akihojiwa na mtandao huu. ====================================================================================== Na Gustav Chahe, Njombe VUGUVUGU la wananchi kutaka mabadiliko ili kuleta maendeleo linazidi kuchukua sura mpya katika maeneo mbalimbali mijini na vijijini baada ya wananchi kuwataka viongozi wao watimize ahadi walizowaahidi wakati wa kampeni za uchaguzi. Wananchi wa kata ya Lupembe iliyopo Mkoa wa Njombe wamewajia juu baadhi ya viongozi wa serikari kwa kuwataka kuwa wakweli kwa kile walichokiita kuwa ni kushindwa kutimiza ahadi zao walizoziahidi katika kipindi cha kampeni za uchaguzi mwaka 2010. Wakizungumza na mtandao huu kwa nyakati tofauti wakazi wa kata za Mfiliga na Lupembe wamemkumbusha Rais Jakaya Kikwete kutimiza ahadi yake aliyoiahidi wakati wa uchaguzi kwamba atakapo chaguliwa kuwa rais atakuwa na uwezo wa kuishawishi mahakama kumaliza mgogoro uliopo katika kiwanda cha chai Lupembe. Wakati wa kampeni za uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 Rais Kikwete aliwaahidi wananchi wa Lupembe kuwa akiwa rais atamaliza mgogoro huo wakati akiwahutubia wananchi hao kwenye mkutano uliofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi Wanyingi. Rais Kikwete aliahidi kuihimiza mahakama kuharakisha kutoa majibu ya kesi ya kiwanda hicho jambo ambalo halijafanyika hadi sasa huku chaguzi zingine zikikaribia kuanza. Walisema kumekuwapo na sitofahamu juu ya utekelezaji wa ahadi hiyo na nyingine nyingi zilizotumika kuwanadi wagombea katika kipindi cha kampeni mwaka 2010 jambo ambalo linazua hofu ya kuendelea na maisha magumu kwa wananchi hao. “Ni kweli kwamba tunatambua kiwanda cha chai Lupembe kesi yake ipo mahakamani na hatutaki rais aingilie uhuru wa mahakama bali bali tunachotka atimize ahadi yake ya kuihimiza mahakama katika kutoa haki ya kesi hiyo kama alivyoahidi” walisema. Pamoja na kumlalamikia rais juu ya ahadi hiyo, wamemtuhumu Mbunge wa jimbo la Njombe Kaskazini Deo Sanga alimaarufu kama “Ja People” kuwa aliahidi kulishughulikia jambo hilo pindi atakapochaguliwa kuwa mbunge. Inaelezwa kwamba Mbunge huyo alitoa ahadi hiyo mara kadhaa katika mikutano mbalimbali ya kampeni za kujinadi kwake na kwamba hadi sasa hakuna maendeleo yoyote kuhusu ahadi zake huo. Akijibu hoja hiyo Deo Sanga alikiri kuwa ni kweli kwamba ahadi hiyo ilizungumza katika kampeni zake na zile za Rais na juhudi za kutafuta ufumbuzi wa mgogoro huo zinaendelea japo kuwa hakuziainisha. “Zipo ahadi nyingi ambazo ziliahidiwa kipindi cha kampeni yangu na rais kwa wananchi wa jimbo la Njombe Kaskazini kama walivyo kueleza wananchi, lakini pia zipo ambazo tayari zimekwisha tekelezwa kwa kiwango kikubwa na nyingine bado zingali zinaendelea kufanyiwa kazi’ alisema Sanga.” Kuhusu mgogoro uliopo kati ya mwekezaji na wakulima wa kiwanda cha chai Lupembe, alisema uamuzi wa mahakama kuhusu kesi hiyo kwa sasa ipo ukingoni. Kiwanda cha chai Lupembe kilifungwa miaka kadhaa iliyopita kufuatia mgongaro wa kimasilahi uliojitokeza kati ya mwekezaji Nawab Mullar dhidi ya wananchi ambao awali ndiyo waliokuwa wamiliki wa kinda hicho.

TATIZO LA MAWASILIANO LAWATESA RUKWA


Wasafiri  wa  kijiji  cha Madope  wilaya ya  Ludewa mkoani Njombe  wakisafirisha mkaa huku  wakisafiri  kwa njia hatari  zaidi kama  walivyokutwa na mtandao  huu jana
..........................................................................................................
Na Elizabeth Ntambala
   Rukwa
Kila kukicha dunia inaendelea kusogezwa kuwa kijiji kama wataalamu wa mawasiliano wanavyosema, nahii ni kutokana na wanasayansi kuendelea kuvumbua vitu mbalimbali vya mawasiliano ambavyo vinatusaidia kuwasiliana na ndugu na jamaa popote pale walipo duniani.

Ni ukwel usiofichika kuwa tumepiga hatua kimaendeleo katika Nyanja ya mawasiliano, tungu kule tulikotoka enzi zile za kuandika barua na ujumbe kufika baada ya mwezi hadi miezi mitatu, na kwamba hali hii ilisababisha kuharakisha maendeleo.

Kwa sasa hali ile haipo tena kwani leo unatuma ujumbe wako na unafika baada ya sekunde kadhaa na kwamba hali hiyo inasaidia watu kufanya shughuli mbalimbali kwa muda mfupi.

Simu,komputa,televisheni na radio ni mojawapo ya nyenzo zinazosababisha watu kuwasiliana na kurahisisha shughili zao za maendeleo.

Wakati hayo yakiendelea katika maeneo mengine ya dunia, hali ni tofauti kwa wakazi wa kijiji cha kisa kilichopo kata ya milepa ambapo mawasiliano kwao ni kitu adimu kwa zaidi ya miaka kadhaa tangu watu waanze kuwasiliana.

Wakazi hao ambao simu kwao sio lazima kutokana na kutokuwa na kazi zaidi ya kusikiliza muziki, jambo ambalo linawasikitisha sana kuona wakazi wa vijiji jirani kuwa na mitandao na wakiendelea kufurahia huduma hiyo muhumu hasa kipindi hiki cha sayansi na teknolojia.

Joseph kazimoto ni mmoja wa waakzi wa kijiji hicho ambapo anasema kuwa wanalazika kupanda juu ya miti au sehemu zenye miinuko mikubwa ili kusaka mtandao,na pengine kukosa kabisa kutokana na upepo kuwa mkali na kusababisha mawimbi kutotulia.

Pia anasema mbali na kupanda juu ya miti wakati mwingine wanalazimika kwenda vjijiji jirani kusaka huduma hiyo, jambo ambalo linadaiwa kuwatesa sana kwani wanashindwa kuwasiliana na ndugu zao na kuhabarishana habari mbalimbali zinazotokea.
“Tunapanda juu ya miti ili tuweze kuwasilina na ndugu na jamaa, huku wengine wanashindwa kupanda kwenye miti, yaani kama tumetengwa na haya makampuni ya simu kwa sababu hayatujengei minara”anasema mwaulambo.

Wakazi hao wanaelekeza lamama zao moja kwa moja kampuni za simu hapa nchini kwa kutochangamkia fulsa ya kujenga minara katika kijiji hicho kutokana na mwingiliano wa watu mbalimbali hasa wafanyabiashara wanaofika kijijini hapo kununua mazao.

Kijiji hicho chenye utajiri wa mito inayotililisha maji yake ziwa rukwa, wakazi wake wanajishughulisha na shughuli za kilimo hasa cha mpunga ambapo ni moja kijiji kinachozarisha mpunga kwa wingi katika bonde la ziwa rukwa.

Wanasema kufuatia hali hiyo wanashindwa kutekeleza shughuli zao kwa wakati hasa zile zinazohitaji kuwasiliana na watu walio katika maeneo mengine, nakwamba wanaiomba serikali kupitia halimashauri ya wilaya ya sumbawanga vijijini kuwashawishi watu wa makampuni ya simu kwenda kuwekeza huko.

Pamoja na huduma zao kama kutuma au kutoa pesa kwa njia ya simu lakini kwa wakazi hao hilo haliwezekani kutokana na kusekana kwa mtandao(network).

KINANA ASEMA CCM SI CHAMA CHA MIUJIZA CHA KUTEKELEZA AHADI ZOTE

mbunge  wa  jimbo la Makete  na naibu  waziri  wa maji Dr Binilith Mahenge  akieleza kazi iliyofanywa katika  jimbo lake katika  kutekeleza ahadi za CCM
Wanahabari  waliopo ziara ya Kinana  Makete  wakipata  maziwa mtindi katika  kijiji cha Inihi
 
Katibu  wa Itikadi na uenezi Taifa  Nape Nnauye  akizungunza na wananchi wilaya  ya Makete  katika kijiji cha Ukwama
.........................................................
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, chama chake  kitaendelea  kuwaeleza  wananchi ukweli kuhusu utekelezaji wa ahadi  zake na kuwa chama chake  si chama cha miujuzi ambacho kinatekeleza  kila jambo.

Kinana alitoa kauli hiyo leo katika tawi la chama hicho la Singida, Kata ya Tandale, katika Wilaya ya Makete mkoani Njombe, ambako yeye na ujumbe wake wa kitaifa wa chama hicho wako mkoani humo kwa ajili ya  ziara ya siku saba ili kusikiliza kero za wananchi pamoja na kukiimarisha chama hicho.
Alisema kuwa, chama hicho hakiwezi kufanya kila kitu bali kile kilichoahidi katika ilani yake ya uchaguzi ndicho kitakachotendewa kazi kulingana na rasilimali zilizopo.

Kinana aliongeza kuwa, CCM hakiwezi kutoa ahadi za kimiujiza kwa kuwa hakuna kitu kama hicho huku akiwataka viongozi mbalimbali wa siasa kuwa wakweli na wawazi juu ya ahadi wanazozitoa kwa wananchi kwamba ziwe zinatekelezeka.
Aliongeza kuwa, chama chake ni lazima kiwaambie wananchi ukweli juu ya ambayo kina uwezo wa kuyafanya  nz yale ambayo hayawezekani kufanywa wakati huo.
Sambamba na hilo, Kinana, aliwataka viongozi chama hicho kuangazia ngazi ya taifa, kuwatembelea wanachama wake walioko katika ngazi ya matawi na mashina kwani huko ndiko waliko wanachama na kwamba viongozi ni watendaji tu.
Kwa mujibu wake, viongozi wote wa CCM wanapofanya ziara zao katika maeneo mabalimbali nchini, wanapokuwa wamemaliza kufanya vikao na kamati ya siasa ya mikoa husika, wanapaswa kuwatembelea wanachama walioko kwenye ngazi hizo za chini kwani huko ndiko uliko msingi wa chama hicho.
Kutokana na hilo aliongeza kuwa, msingi wa viongozi bora ni wale wanaopatikana katika ngazi hizo zxa chini.
Akitoa hotuba yake katika mkutano wa hadhara katika kijiji cha Ukwama kilichopo katika kata hiyo ya Tandale  Kinana, aliwaonya wakazi wa eneo hilo kujihadhari na viongozi wa siasa ambao wako tayari kumwaga damu ili wapate uongozi.
 Kwa mujibu wake, hakuna kiongozi mwenye kuweza kuwapatia ajira  Watanzania wote kwa mara moja akliongeza kwamba viongozi wa jinsi hiyo sio wa kufuatwa kwa kuwa si CCM wala wapinzani wanaweza kuwakamilishia Watanzania mahitaji yao yote kwa wakati mmoja.
Alisema kinachotakiwa ni kwa serikali kutengeneza mazingira ya kuwasaidia Watanzania ikiwa ni pamoja na ajira na kwamba ndio inachofanya kwa sasa.
Pia ameahidi kutekelezwa kwa mahitaji mbalimbali wilayani humo ikiwa ni pamoja na miradi ya maji, walimu,mbolea za ruzuku, nyumba za polisi.
Kuhusu upungufu wa walimu katika taasisi za elimu nchini, Kinana katika mkutano huo alisema kuwa, mwaka ujao utakuwa ni mwaka wa mwisho wa kumaliza tatizo la walimu nchini isipokuwa walimu wa masomo ya Sayansi na Hisabati tu kwani serikali imejipanga kwa ajili ya hilo.
Katika hatua nyingine zaidi ya wanachama wapya 100 wamejiunga na chama hicho wakitokea vyama vingine vya siasa na kuweka jiwe la msingi la ofisi ya wilaya hiyo Makete.
Naye Naibu Waziri wa Maji na Mbunge wa Jimbo la Makete, Dk.Binilith Mahenge, alisema takribani Sh.bil.1.6 zimetengwa kwa ajili ya kukamilisha uboreshaji wa barabara ya kutoka Njombe kuja Makete.
Katika ziara hiyo ya siku saba mkoani Njombe, akiwa ameambatana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye, alikuwa katika Wilaya ya Makete na kutwembelea mashina na matawi kadhaa ya chama hicho wilayani humo.
 

May 29, 2013

KINANA AMPA RUNGU FILIKUNJOMBE ATAKA AENDELEE NA MOTO WA KUWAPIGANIA WANANCHI WAKE


katibu  mkuu  wa CCM Taifa  Bw Kinana  Kushoto) akiwa na mbunge  wa  jimbo la Ludewa  Deo Filikunjombe leo jimboni Ludewa
..................................................................................................................................................... 
WAKATI  kukiwa na  tetesi  za chini  kwa  chini ndani ya  chama  cha mapinduzi (CCM) kuwa  chama  hicho kimekuwa  kikiwachukia  wabunge wa CCM wanaokishambulika  chama  hicho  bungeni akiwemo mbunge  wa  jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe na mbunge wa  jimbo la Mwibara Kang Lugola ambao  wamekuwa wakiipinga  serikali ,katibu mkuu  wa CCM Taifa  Abdulrahman Kinana amempongeza  mbunge  huyo na kumtaka aendelee na moto huo huo  wa  kuwapigania  wananchi  wake.
Hata  hivyo kabla ya  Kinana  kumpa rungu mbele ya  wsananchi mbunge Filikunjombe wananchi wa  jimbo  hilo walionyesha  kumbana  kiongozi huyo kwa  kuhoji  sababu ya wabunge  wa CCM bungeni  kufanya kazi ya kukipongeza chama  chao  huku  wengi  wao  wakiwa kimya (mabubu) katika  kuchangia na  wale  wanaochangia kama mbunge  wao Filikunjombe  wamekuwa  waklichukiwa kuwa ni  wapinzani ndani ya CCM . 
Hivyo  wananchi hao  kumweleza katibu mkuu  huyo aliyeongozana na katibu wa itikadi na uenezi  wa CCM Taifa  Nape Nnauye  kuwa wao  wataendelea  kumuunga mkono mbunge Filikunjombe kwa  vipindi  vingine  tena tena  vitatu vya miaka 15  tena  hadi mbunge mwenyewe  atakapoamua  kuacha  kugombea na iwapo watafanya mchezo  basi wao watamfuata  mbunge  huyo kokote atakakokuwa.
" Mheshimiwa  tunaomba  leo chama kitueleze  hivi  kwanini wabunge wa CCM wamekuwa  si msaada kwa wapiga  kura  wao muda  wote  wamekuwa  kimya  bungeni na  wale  wanaochangia  wanachangia kupongeza  chama .....sasa  tunaomba  kukueleza  kuwa sisi  tupo na mbunge  wetu  na hata  wana  CCM wanaojipitisha jimbo la Ludewa  wakiamini  sisi tutayumba  uwaeleze  kuwa CCM hatudanganyiki  "
Akizungumza jana  na  wananchi  wa  wilaya ya  Ludewa ambao  walikusanyika kwa wingi katika mkutano  wa hadhara  kwa lengo la kutaka  kusikia kauli ya CCM juu ya uamuzi  utakaochukuliwa kwa mbunge   wao kutokana na kuwepo kwa kauli  za chini kwa chini katika jimbo  hilo kuwa ziara ya Kinana jimboni  humo ni kutaka  kumshughulikia mbunge  huyo.
Akizungumza na  wananchi hao Kinana  alisema  kuwa lazima  wabunge  wa CCM kuiga mfano  wa Filikunjombe kwa  kuwasemea  wananchi  waliowachagua  na kuwa mbunge ambae  amekuwa hawasemei  wananchi  wake  bungeni hatoshi  kuwa mbunge . 
Hivyo  kuwataka  wananchi  kuwa makini kwa kuwaangalia  wabunge  wao  waliowachagua kuona  kitu gani  wanakifanya  bungeni na  kuwahukumu  kulingana na kile  wanachokifanya kama  hawawasemei  kuwa nao makini. 
Hata  hivyo Kinana aliwataka  wananchi hao  wanaounga mkono uamuzi  wa kuendelea  kumwongeza muda wa vipindi  vitatu Filikunjombe  kunyosha  mikono  juu na baada ya  wananchi  wote  kunyosha  mikono yao  juu alisema pia kwa upande  wake anaungana na wao na kuwa chama hakitafanya makosa kwa  kuwasaliti  kuwapa mtu mwingine katika  uchaguzi ujao wa mwaka 2015 . 
"Hata  mimi katibu  mkuu naungana na uamuzi wenu wa  kumwongeza muda Filikunjombe na  napenda  kuwahakikishia  kuwa CCM haitafanya makosa  itaendelea  kuwaachia Filikunjombe kama mlivyomchagua wenyewe  labda ashindwe  yeye " 
Katika  hatua  nyingine  Kinana alisema  kuwa CCM hakitafanya makosa  katika  kuwateua  wagombea wa nafasi mbali mbali na kuwa  watakaoendelea  kuteuliwa ni wale ambao  wanafanya  vizuri katika majimbo yao. 
Aidha  alikiri utendaji kazi  wa mbunge Filikunjombe na  kuwa ni m bunge  wa mfano katika  bunge na kuwa  hata  chama  kinapendezwa na uchapakazi  wake na  kuwa mbali ya  wananchi  wa  jimbo  hilo kumwita ni jembe  ila yeye kama Kinana anamfananisha mbunge  huyo na katapila kwani amekuwa hamwogopi mtu  katika utendaji kazi wake. 
Pia  alisema  kuwa  mbali ya Filikunjombe  kufanya kazi  vema  ila bado ni kijana anayejituma na  pia ni kwa kiasi ni mbabe katika kupigania  wananchi  wake .
Kuhusu shughuli  za kimaendeleo  zinazofanywa na mbunge huyo Kinana  alisema  kuwa wao kama  chama wanapendezwa na kazi  za mbunge  huyo na kuwa  toka anaanza  ziara ya  siku mbili hakuna hata  sehemu moja ambayo wanampinga  mbunge  huyo .
Awali akiwa katika  kata ya Mlangali wananchi  wa eneo  hilo walimkana mbunge wa  viti maalum mkoa  wa Njombe na mjumbe  wa kamati kuu  ya  CCM Taifa Pindi Chana kuwa hawamtambui mbali ya  kuuwakilisha mkoa  huo wa Njombe.
Wananchi hao  walimkana mbunge  huyo baada ya Kinana kuwauliza kama wanamtambua mbunge  huyo. 
Kwa  upande  wake Filikunjombe alisema mbali ya  kuanza mradoi mkubwa wa lami katika wilaya  hiyo ila bado kuna mradi  wa maji wenye thamani ya Tsh bilioni 1.5 ambao utaondoa adha ya maji katika  mji  wa Ludewa. 
Filikunjombe  alisema  kutokana na kuendelea  kuutamani ubunge  wake ataendelea  kuwatumikia vema  wananchi na kamwe siku  zote hatarudi nyuma bungeni katika  kuwapigania  wananchi hao .

May 28, 2013

BREAKING NEWzz: MSANII WA BONGO FLEVA ALBERT MANGWEA AFARIKI DUNIA..

 

Habari  zilizotufikia  ni  kwamba  msanii  Albert Mangwair  amefariki dunia  akiwa  Afrika  kusini

Taarifa zilizotufikia hivi punde ambazo bado hazijathibitishwa zinasema kuwa msanii Albert Mangwair amefariki dunia akiwa nchini Afrika Kusini alipokuwa amelazwa katika hospitali ya St Hellen.

DC SUMBAWANGA ALIA NA MAUWAJI YA WAZEE


Na Elizabeth Ntambala
Rukwa
MKUU wa Wilaya (DC) ya Sumbawanga, Mathew Sedoyeka, ameeleza kukerwa na matukio ya mauaji yanayotokana na imani za kishirikina na kuviagiza vyombo vya dola kuongeza nguvu ya kuwasaka watu wanaohusika katika matukio hayo.

Sedoyeka alitoa kauli hiyo kwenye kata mbalimbali alizofanya ziara ya kuelimisha wananchi kuachana na vitendo hivyo ambavyo vinaambatana na kuchomeana nyumba moto na kuharibu mali za baadhi ya wakazi ambao wamekuwa wakituhumiwa kuwa ni washirikina.

Akizungumza na wananchi wa Kata ya Lusaka jana, Sedoyeka alisema kuwa kuendekeza mauaji hayo ni sawa na kuishiwa fikra katika mapinduzi yanayohitajika ili kubadili mtazamo wa kifikra.

“Naamini watu wanaofanyiwa vitendo hivyo si wachawi bali wamekuwa wakionewa kutokana na jitihada zao za kujituma kufanya kazi na kupata mali, lakini mwisho wa siku wanaambiwa wamezipata kwa imani za kishrikina, jambo ambalo si la kweli,” alisema Sedoyeka.

Alisema vitendo hivyo vimejaa hila inayotokana na wivu na chuki kwa wakazi wa maeneo mbalimbali wilayani humo ambao wamekuwa wakitumia muda wao mwingi kuzalisha mali zao kwa kufanya kazi za kilimo au biashara.

“Utakuta mtu ana nyumba nyingi za kisasa na pengine anamiliki chombo cha usafiri na anafanya biashara watu wanamvamia wakimtuhumu na mauaji ya ndugu yake fulani, na wanaharibu mali zake na hata kumuua,” alisema.

Alisema amekuwa akijisikia vibaya anaposikia matukio ya watu kuuawa na kutolea mfano wa Juni mwaka jana takriban watu 24 waliuawa kwenye matukio tofauti wakihusishwa na imani za kishirikina.

TAIFA STARS YAANZA KUJINOA ADDIS ABABA

Taifa Stars imetua jijini Addis Ababa, Ethiopia leo (Mei 28 mwaka huu) alfajiri kwa ndege ya EgyptAir ambapo itaweka kambi ya wiki moja kujiandaa kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Morocco (Lions of the Atlas) itakayochezwa Juni 8 mwaka huu jijini Marrakech.
 
Stars iliyotua na kikosi cha wachezaji 21 imefikia hoteli ya Hilton, na imeanza mazoezi leo (Mei 28 mwaka huu) saa 12 jioni kwenye Uwanja wa Addis.
 
Kwa mujibu wa Kocha Kim Poulsen, Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itakuwa na vipindi (sessions) vinne vya mazoezi kabla ya kucheza mechi ya kirafiki na Sudan (Nile Crocodile).
 
Mechi dhidi yan Sudan itachezwa Jumapili kuanzia saa 11 jioni kwenye Uwanja wa Addis. Sudan ambayo pia imeweka kambi yake Addis Ababa kujiandaa kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia ilicheza mechi yake ya kwanza jana (Mei 27 mwaka huu) dhidi ya wenyeji Ethiopia na kulala mabao 2-0.
 
Wachezaji wanaounda Stars ni nahodha Juma Kaseja, nahodha msaidizi Aggrey Morris, Mwadini Ally, Ally Mustafa, Shomari Kapombe, Kevin Yondani, Erasto Nyoni, Haroub Nadir, Mwinyi Kazimoto, Frank Domayo, Mrisho Ngasa, Khamis Mchana, Amri Kiemba, Salum Abubakar, Simon Msuva, John Bocco, Vicent Barnabas, Mudathiri Yahya, Athuman Idd, Haruni Chanongo na Zahoro Pazi.
 
Kikosi hicho kinatarajiwa kuondoka Addis Ababa kwenda Marrakech alfajiri ya Juni 3 mwaka huu kwa ndege ya EgyptAir. Stars itatua siku hiyo hiyo Casabalanca na kuunganisha moja kwa moja kwenda Marrakech.
...................................................................................................................................
Boniface Wambura Ofisa Habari Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Addis Ababa +251 919910240

MBUNGE FILIKUNJOMBE AIONYA SERIKALI , ASEMA LUDEWA HAWATAKI VIWANDA ZA KUFUA CHUMA NA UMEME KUJENGWA NJE YA LUDEWA

 
 Katibu  mwenezi  na itikadi  wa CCM Taifa Bw Nape Nnauye  akisalimiana na  wananchi  wa Ludewa mjini leo
 Katibu  mkuu  wa CCM Taifa  Bw Kinana  akisalimiana na baba mzazi  wa mbunge  wa jimbo la Ludewa mzee Filikunjombe leo kabla ya kufanya mkutano  wake
 Umati  wa wananchi  waliofika  katika mkutano  huo  wa CCM Ludewa mjini  leo


katibu  mkuu  wa CCM Taifa  Bw Kinana  Kushoto) akiwa na mbunge  wa  jimbo la Ludewa  Deo Filikunjombe leo jimboni Ludewa
.....................................................................................................................................................
MBUNGE  wa  jimbo la  Ludewa  Deo Filikunjombe asema  ili  kuondokana na machafuko kama ya Mtwara  juu ya  sakata  la gesi ataka raslimali  za  wilaya ya  Ludewa kuanza  kuwanufaisha  wana  Ludewa  kwa kuhakikisha   viwanda vya  chuma na umeme kupitia miradi ya Liganga na makaa ya mawe zinajengwa ndani ya  wilaya  ya  Ludewa na si vinginevyo .

Alisema  iwapo  serikali itatimiza ushauri  wake kwa kujenga viwanda  vya chuma na umeme ndani ya wilaya  hiyo  yanayotokea  Mtwara kwa wana  Ludewa kamwe hayatatokea. 

Filikunjombe  alitoa kauli  hiyo leo  katika mkutano  wa hadhara  uliofanyika katika  uwanja  wa Ludewa baada  ya   katibu mkuu  wa CCM Taifa Abdulrahman Kinana  kumtaka  kuwaeleza  wapiga  kura  wake  jitihada mbalimbali  zilizofikiwa na  serikali ya  CCM katika kutekeleza ahadi mbali mbali katika jimbo  hilo. 

Alisema  kuwa  kiwanda  cha  chuma  kinachotokana na mradi  wa mchuchuma na Liganga  kujengwa  Shauri  moyo kwani  alisema   kuwa  wananchi  wa Ludewa  wanakubali kabisa  miradi  hiyo mikubwa  ya mchuchuma na ule  wa makaa ya mawe kuwanufaisha  wananchi  wote  wa Tanzania japo hawapo tayari  kuona   viwanda  vyake  vinajengwa  nje ya wilaya  hiyo.

" Naomba  niwasisitizie  wananchi  kuwa tayari  nimepata  kukutana na mheshimiwa Rais Jakaya  Kikwete  kuwa  bila Ludewa  kuwa na barabara  ya lami  bado  wananchi  hawatakuwa tayari  kuona miradi  hiyo mikubwa  inaanza kuwanufaisha  wananchi  wakati  wao barabara  zao ni mbovu .....hivyo  tayari   serikali kupitia  waziri wa ujenzi mheshimiwa Dkt John Magufuli ameahidi  kujenga barabara ya lami  Ludewa  hadi Njombe hivyo  mwaka 2014  itaanza kujengwa " 

Alisema  kuwa  mwaka jana serikali ilijengwa barabara Kilometa  moja na nusu  ila kwa mwaka  huu kilometa  10  zitajengwa  kama  sehemu ya  salama  za waziri  wa ujenzi kwa  wananchi  wa   wilaya ya  Ludewa.

" Naomba  kuwathibitishia  kuwa  mimi  mbunge  wenu  nipo na bado nautamani ubunge  hiyo  lazima  kiwanda  cha umeme  kujengwa ndani ya  wilaya ya  Ludewa  ili kutoa ajira  kwa  wana Ludewa si vinginevyo.....kiwanda   hicho cha umeme kitajengwa mchuchuma na kile  cha  kufua chuma kitajengwa Shauri moyo si vinginevyo" 

Kwa  upande  wake Kinana  alisema  kuwa  raslimali  za Taifa ni mali ya  watanzania  wote  na  kuwa  ushauri  wa mbunge Filikunjombe  juu ya ujenzi wa viwanda  hivyo utazingatiwa ilivyo  ili kuwanufaisha  pia  wananchi  wanaozunguka miradi  hiyo.

Hata  hivyo  alisema  kuwa ni  wajibu  wa viongozi  kuwajulisha  wananchi  kila kinachofanyika katika  maeneo yao  juu ya miradi  husika ili  kuwawezesha  wananchi pia kuweza  kwenda  sambamba na serikali yao . 

 Katika hatua  nyingine  Kinana amekemea  vikali tabia ya  wana  CCM wanaotafuta nafasi mbali  mbali  zikiwemo  za udiwani ,ubunge na Urais mwaka  2015  kuanza  kujipitisha kwa wana CCM sasa  na  kuwa watakaopatikana  wasije lalamika  kwa  kile  kitakachowakuta

Kinana alisema, katazo la wanachama kujipitisha-pitisha na kupiga kampeni za kuwania urais au nafasi yoyote kabla ya muda  halitoki midomoni mwa viongozi bali ni kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za Chama.

"Ndugu zanguni, nawakumbusha kwamba kwa hili hatuna mzaha nalo, hivyo hakikisheni kila mmoja wenu kama kiongozi hajihusishi kwa namna yoyote kushiriki katika kutumiwa na wanachama hao wanaojipitishajiptisha", alisema Kinana na kuongeza;

"Ni lazima Chama kiwe kikali kwenye jambo hili, kwa sababu kama kitawaacha watu hawa kukiuka taratibu na kanunzi za Chama wanazidi kukifanya chama kuwa na makundi mengi ambayo yatakipeleka pabaya," alisema Kinana

Kinana alisema,  kazi walioyonayo wale wote wanaokitakia mema Chama, ni kumuunga mkono Mwenyekiti, Rais Jakaya katika kazi ya kuhakikisha CCM inakamilisha utekelezaji ilani yake ya Uchaguzi kwa kiwango kinachostahili na siyo muda kujipitisha pitisha mtu binaafsi kwa wanachama huku utekelezaji wa ilani ukisinzia.

Alisema kuwa hivi sasa kazi ya CCM ni kuhakikisha inatekeleza ilani ya uchaguzi kwa kipindi kilichobaki cha miaka miwili ya nusu kabla ya kumalizi kwa awamu ya uongozi wa Rais Jakaya Kikwete.

"Ni wazi kazi yatu CCM ni kuhakikisha tunatekeleza ilani ya uchaguzi kwa vitendo na si mamneno kama wanavyofanya wengine. ni kazi kubwa imefanyika chini ya uongozi wa Rais Kikwete na katika kipindi cha miaka miwili iliyobaki tumedhamiria kuifanya zaidi",

Alisema moja ya maeneo ambayo licha ya kuwepo changamoto za hapa na pele lakini yamefanikisha sana utekelezaji wa ilani ya CCM,  ni kwenye Halmashauri mbalimbali nchini ambapo watendaji walio wengi wamekuwa wakifanya kazi kubwa ya kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kasi.

"Kwa kweli CCM lazima hawa tuwapongeze maana kuna wengine kazi yao imebaki kuwashambulia huku wakijua watendaji hao hawana fursa ya kujitete mbele ya jamii. chapeni kazi nasi tupo nyuma yenu, na kila wakati tutakuwa tukitambua juhudi na kazi kubwa mnayoifanya kwa jamii," alisema Kinana.

Akizungumzia uchaguzi mdogo wa madini unaofanyika katika kata mbalimbali nchini Kinana, alisema CCM itashinda uchaguzi huo kwenye kata zote 25  kutokana na mtandao wa chama chake na imani inayoonekana kuwepo kwa wananchi juu ya CCM.

May 27, 2013

KINANA: AWAJIA JUU WANAOJIPANGA KWA KUGOMBEA URAIS 2015


NA BASHIIR NKOROMO, IRINGA


KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana amesisitiza kwamba Chama kitamwadhibu bila huruma mwanachama yeyote anayejipitisha-pitisha katika maeneo mbalimbali na kufanya kampeni za kuwania urais kabla ya wakati.

Kinana alisema hayo leo wakati akizungumza na Kamati ya Siasa na mkoa wa Iringa, katika kikao maalum, kilichofanyika kabla  ya kwenda mkoani Njombe ambako ameanza ziara ya siku saba mkoani humo.

Kinana alisema, katazo la wanachama kujipitisha-pitisha na kupiga kampeni za kuwania urais au nafasi yoyote kabla ya muda  halitoki midomoni mwa viongozi bali ni kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za Chama.

"Ndugu zanguni, nawakumbusha kwamba kwa hili hatuna mzaha nalo, hivyo hakikisheni kila mmoja wenu kama kiongozi hajihusishi kwa namna yoyote kushiriki katika kutumiwa na wanachama hao wanaojipitishajiptisha", alisema Kinana na kuongeza;

"Ni lazima Chama kiwe kikali kwenye jambo hili, kwa sababu kama kitawaacha watu hawa kukiuka taratibu na kanunzi za Chama wanazidi kukifanya chama kuwa na makundi mengi ambayo yatakipeleka pabaya," alisema Kinana

Kinana alisema,  kazi walioyonayo wale wote wanaokitakia mema Chama, ni kumuunga mkono Mwenyekiti, Rais Jakaya katika kazi ya kuhakikisha CCM inakamilisha utekelezaji ilani yake ya Uchaguzi kwa kiwango kinachostahili na siyo muda kujipitisha pitisha mtu binaafsi kwa wanachama huku utekelezaji wa ilani ukisinzia.

Alisema kuwa hivi sasa kazi ya CCM ni kuhakikisha inatekeleza ilani ya uchaguzi kwa kipindi kilichobaki cha miaka miwili ya nusu kabla ya kumalizi kwa awamu ya uongozi wa Rais Jakaya Kikwete.

"Ni wazi kazi yatu CCM ni kuhakikisha tunatekeleza ilani ya uchaguzi kwa vitendo na si mamneno kama wanavyofanya wengine. ni kazi kubwa imefanyika chini ya uongozi wa Rais Kikwete na katika kipindi cha miaka miwili iliyobaki tumedhamiria kuifanya zaidi",

Alisema moja ya maeneo ambayo licha ya kuwepo changamoto za hapa na pele lakini yamefanikisha sana utekelezaji wa ilani ya CCM,  ni kwenye Halmashauri mbalimbali nchini ambapo watendaji walio wengi wamekuwa wakifanya kazi kubwa ya kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kasi.

"Kwa kweli CCM lazima hawa tuwapongeze maana kuna wengine kazi yao imebaki kuwashambulia huku wakijua watendaji hao hawana fursa ya kujitete mbele ya jamii. chapeni kazi nasi tupo nyuma yenu, na kila wakati tutakuwa tukitambua juhudi na kazi kubwa mnayoifanya kwa jamii," alisema Kinana.

Akizungumzia uchaguzi mdogo wa madini unaofanyika katika kata mbalimbali nchini Kinana, alisema CCM itashinda uchaguzi huo kwenye kata zote 25  kutokana na mtandao wa chama chake na imani inayoonekana kuwepo kwa wananchi juu ya CCM.

mwisho

KINANA: CCM IMEDHAMIRIA KUZOA KATA ZOTE 25

 katibu mkuu  wa CCM Bw Kinana akiagana na makada  wa CCM mkoa  wa Iringa
 Kada  wa CCM mjini Iringa Bw  Shukru Stivine  akisalimiana na katibu mkuu  wa CCM Taifa  Bw  Kinana  leo
 mgombea  udiwani  wa  CCM kata ya Mbalamaziwa  wilayani Mufindi Bw  Zuberi  Nyomolela  wa  pili  kushoto , wa kwanza  kushoto ni mwenyekiti  wa CCM mkoa  wa Iringa Bi Jesca Msambatavangu na kutoka  kulia wa kwanza ni katibu mwenezi na itikadi Taifa  Nape Nnauye  na katibu mkuu  wa CCM Taifa  Bw Kinana
 mgombea  udiwani  wa  CCM kata ya Mbalamaziwa  wilayani Mufindi Bw  Zuberi  Nyomolela  (kushoto) akiwana katibu mkuu  wa CCM Taifa Bw Kinana leo  wakati akimnadi katika  kijiji  cha Mbalamaziwa

 Katibu mkuu  wa CCM Taifa  Bw Kinana akiwapongeza  wanachama wa CCM kata ya  Mbalamaziwa ambao  walishindwa katika mchakato wa kura za maoni katika kinyang'anyiro cha  udiwani ndani ya CCM kata  hiyo
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia) akiwapongeza   wanachama wa CCM kata  ya Mbalamaziwa   ambao  wapo tayari  kumchagua mgombea  udiwani  wa  CCM kata ya Mbalamaziwa  wilayani Mufindi Bw  Zuberi  Nyomolela  (wa  pili kulia) anayeshuhudia  ni mwenyekiti  wa CCM mkoa wa Iringa Bi Jesca Msambatavangu


Katibu  mkuu  wa CCM Taifa  Bw Kinana na mwenyekiti  wa CCM mkoa wa Iringa Bi Jesca Msambatavangu  wakimpongeza mmoja kati ya  waliokuwa  wagombea wa nafasi ya udiwani  kata ya Mbalamaziwa Mufindi ambao  wamekubali kumuunga mkono mgombea  wa CCM
Mbunge  wa jimbo la  Ludewa Deo Filikunjombe (kulia) akiwa mbunge  wa  jimbo la Mwibara  ,Kangi Lugola walipo fika kumpokea katibu  mkuu wa CCM Taifa  leo
 NA BASHIR NKOROMO, IRINGA
CHAMA Cha Mapindizi (CCM) kimesema kimedhamiria kushinda kwenye kata zote 25 katika uchaguzi mdogo wa madiwani ambao kampeni zake zinaendelea katika kata mbalimbali nchini.

Hayo yamesemwa leo  na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana wakati akizungumza na wananchi katika kata ya Mbalamaziwa, wilayani Mufindi mkoani Iringa, ambako zinaendelea kampeni za udiwani katika kata hiyo. Katika Kata hiyo bendera ya CCM inapeperushwa na  Zuberi Nyamoleo.

"Kutokana na jeshi kubwa na wafuasi tulio nao na imani inayoendelea kuonyeshwa na wananchi kuiunga mkono CCM, tuna imani dhamira hii itafanikiwa bila shaka yoyote", alisema Kinana na kuongeza;

"Pale Mbinga katika Kata ya Lokindo CCM imeshapita bila kupigwa, wapinzani wenyewe wametuachia kwa sababu wameridhika kuwa tunafaa kiuwaongoza, na pele Iramba Vijijini, Chadema walijaribu kuchacharika lakini wameambulia matupu vijiji vinane vyote vimeenda CCM".

Kinana aliwapongeza wagombea wengine waliokuwa katika mhakato na  Nyamoleo kwa kuamua kuuga mkono mgombea wa CCM katika 'vita' hiyo ya kuwania udiwani katika kata ya Mbalamaziwa.

"Ninyi ni watu wa kuheshimika sana ndani ya CCM, mmefanya uamuzi wa busara kuamua kumsaidia mgombea wa CCM aliyejipita kwenye kura za maoni. Huu ndiyo ustaarabu na moyo wa dhati unaotakiwa kwa kila mwana-CCM", alisema Kinana.

Kinana alisema, wanachama walio bora ndani ya CCM ni wale wasio na ubinafsi kwa kung'ang'ania kila wanachotaka wapate na wanapokosa inakowa nongwa.

"Mwanachama lazima uelewe kwamba unapogombea nafasi yoyote inayowaniwa na wengi huwa kuna kushinda au kushindwa, sasa inapotokea umeshindwa ni lazima uendelee kuwa mwaminifu kwa chama ili kuhakikisha kinashinda", alisema.

Kinana alisema, pamoja na CCM kuwa na uhakika wa kutwaa kata zote, lazima wagombea watakaposhinda wawe watumishi wenye kujinyenyekeza kwa wananchi siyo kujinyayua mabega kana kwamba wao ndiyo bora kuliko wanaowaongoza.

"Tafadhalini sana, Chama hiki ni cha wananchi, diwani atakayeshinda ahakikishe  ushindi aliopata haugeuzi kuwa utukufu kwake kabla ya utumishi, huyo tutamshughulikia mara moja", alisema Kinana.

Kinana alipita katika kata hiyo akiwa njiani kwenda wilayani Njombe ambako anaanza ziara ya siku saba akifuatana na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.

mwisho.

UTENDAJI WA KINANA WAWAPAGAWISHA WANA CCM IRINGA ,ATUA IRINGA KABLA YA WENYEJI KUFIKA UWANJA WA NDEGE

ndege  aliyotumia  katibu mkuu  kusafiria  kuja  Iringa ndege ya abiria  ikiwa imesimama  uwanja  wa Nduli Iringa  huku viongozi  wakishindwa kuamini kama yupo ndani ,wakiamini ipo nyingine ila ghafla aliibuka katika ndege hiyo,picha ya  juu  KInana na Nape nyuma  yake  wakishuka katika ndege  hiyo  leo
mwenyekiti wa CCM mkoa  wa Iringa  Jesca Msambatavangu akimpokea  katibu mkuu  wa chama   cha mapinduzi (CCM) Bw Kinana  leo kushoto anayeshuhudia ni katibu wa CCM mkoa wa Iringa ,hii ilikuwa ni ghafla  sana kwa viongozi hawa


katibu mkuu  wa CCM Taifa  Bw .Kinana  akisalimiana na kada wa CCM  kutoka  chuo cha Tumaini Iringa Mwanahabari Saimon Belege


 Makada  kutoka  Tumaini Iringa
 Kinana akiteta  jambo na  diwani wa kata ya Nduli Bw Chonanga  leo
 Katibu  wa CCM mkoa wa Iringa na mwenyekiti  wake wakimwongoza Bw Kinana kwenda  V.I.P Room
 Hapa  ni ofisi  za CCM mkoa akivishwa skafu baada ya  kushindwa kuvishwa uwanja  wa Ndege nduli kutokana na kufika dakikta 20 kabla ya muda  uliopangwa  kuwasili


 Kamanda  wa UV CCM mkoa  wa Iringa  Salima Abri Asas  akisalimiana na katibu mkuu  wa CCM Taifa  Bw Kinana baada ya  kuwasili  makao makuu ya CCM mkoa  wa Iringa asubuhi ya leo,kinana  na Nape  wanaelekea  ziara  ya kichama mkoa  wa Njombe
 Bw  Asas  akipongezana na  Kinana  leoHabari kamili inakuja ....................