Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

April 30, 2013

MBEYA LEO SAA 9 USIKU NI MWISHO WA ANALOJIA

 
 
Na Esther Macha, mbeya
MAMLAKA ya mawasiliano Tanzania, imesema itazima mitambo yake ya mfumo
wa utangazaji wa Analojia Mkoani Mbeya  leo April 30 mwaka huu
majira ya saa sita usiku
.
Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja Uhusiano wa Mamlaka ya
Mawasiliano(TCRA) Inocenti Mungi, alisema uzimaji huo umekuja baada ya
mamlaka hiyo kukidhi vigezo vitano vilivyotolewa na serikali.

Alisema, maandalizi ya kuzima mitambo ya analojia ya utangazaji wa
televisheni kwa Jiji la Mbeya na vitongoji vyake yamekamilika kwa
kuwashirikisha wadau wa sekta ya utangazaji Mkoani Mbeya.

Alisema, tayari elimu kwa umma kupitia mbinu mbalimbali kuhusu
mchakato wa kuhamia katika teknolojia ya mfumo wa utangazaji wa
dijitali imetolewa na kwamba mpaka sasa asilimia 22 kati ya 24 ya
wanaopata matangazo ya televisheni ya analojia.

Aidha, meneja huyo alisema pia mamlaka hiyo imezingatia na kukidhi
vigezo vitano vilivyotolewa na serikali.

Alisema, moja ya vigezo hivyo hivyo ni kuhakikisha kabla ya uzimaji
wa mitambo ya analojia na kuingia Dijitali ni lazima mamlaka husika
kutoa elimu kwa wananchi, kuhakikisha eneo hilo tayari linamfumo wa
matangazo ya dijitali pamoja na kuonekana kwa chanel sita za ndani ya
nchi jambo ambalo limefanyika.

Aidha, Mungi alisema kuwa mabadiliko hayo hayatahusu matangazo kwa
njia ya utangazaji wa Satelaiti waya(cable) na radio na kwamba
wananchi waithubutu kutupa Tv zao za analojia bali wanunue vingamuzi
ili kupata matangazo ya digitali.

Hata hivyo alisema mamlaka hiyo imeonesha kuridhika na uzimaji wa
mitambo ya analojia kwa Mkoa wa Mbeya, baada ya kubaini kuwa mpaka
sasa ni zaidi ya wananchi elfu kumi na nne wanatumia mfumo wa dijitali
huku vingamuzi vikiwa zaidi ya 1000 kwa mkoa wa Mbeya.

WAKE WA MABALOZI WACHANGIA MIRADI YA KUJITEGEMEA ..................


1 6beb5

Ndugu zangu,

Februari 6 mwaka huu nilipata bahati ya kukutana na kuongea na wake wa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini. Ilikuwa ni nyumbani kwa Balozi wa Sudan.

Kwenye mazungumzo yangu ( Pichani) niliongelea umuhimu wa Jumuiya hiyo ya wake wa Mabalozi kuendelea kuchangia elimu ya wasichana waliokatishwa masomo.
Kwamba ni haki kupata elimu na pia kumpa msichana nafasi ya pili katika maisha.

Nikakumbushia historia ya Elimu ya Watu Wazima na Elimu Jamii kwa kutolea mfano nchi ya Sweden. Kwamba kwa hapa nchini Vyuo Vya Maendeleo ya Wananchi vimetokana na urafiki wa kati ya Rais wa kwanza wa Tanzania, Julius Nyerere na Waziri Mkuu wa Sweden aliyeuawa, Olof Palme.

Kwamba ni kutokana na ziara ya Julius Nyerere Sweden iliyopelekea avione Vyuo Vya Maendeleo ya Wananchi vya huko na kuamua kuiga mfano huo. Hapa nchini Vyuo hivyo vilianzishwa katikati ya miaka ya 70. Idadi ya vyuo hivyo kwa sasa ni 53.

Niakaelezea pia umuhimu wa elimu na namna binadamu tunavyopata maarifa. Kwamba tunapata maarifa kutokana na milango mitatu; Uzoefu ( Fronesis) Shule ( Episteme) na Vipaji ( Tekne). Nilifafanua hayo kwa kutolea mifano hai.

Na kwamba , wasichana hao wanaokatishwa masomo yao wengine kwa kubakwa na walimu wao nao wana uzoefu ambao, ukichanganywa na elimu ya darasani na vipaji vyao, wanaweza kwenda mbele kimaisha na kutoa mchango katika ujenzi wa nchi yao.

Juzi, kupitia Shirika la Karibu Tanzania Association, wake hao wa Mabalozi wametoa mchango wa takribani shilingi milioni 4 kusaidia miradi ya kujitegemea ikiwamo ufugaji wa kuku wa kienyeji na bustani inayofanywa na wasichana hao kwenye Vyuo Vya Maendeleo ya Wananchi vya Njombe, Ilula na Ulembwe.

Tunawashukuru kwa mchango huo, na kubwa kabisa, ni kwa wao kufikisha ujumbe, kuwa kuna umuhimu kwa wasichana waliokatishwa masomo kwa sababu ya uja uzito kupewa nafasi ya pili maishani.

Maggid Mjengwa,
Iringa.

NITAGOMBEA URAIS MWAKA 2015 IWAPO WANANCHI WENGI WATANIOMBA ---WAZIRI MEMBE

 

Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Bw ,Benard Membe akiwa na wanafunzi wa vyuo vikuu mkoa wa Iringa wanaotoka mkoa wa Mtwara na Lindi jana
Waziri Membe
Na Francis Godwin,Iringa
HUKU hali ya mambo ndani ya chama cha mapinduzi (CCM) kuwa si shwari kutokana na makada wake kuendelea kupigana vikumbo ikiwa ni sehemu ya harakati mbio za urais mwaka 2015 , waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Benard Membe ameibuka na kutoa ya moyoni kuwa atakuwa tayari kuwania urais mwaka 2015 iwapo wananchi wataona anafaa na watamtaka agombee nafasi hiyo.
Pia waziri Membe alisema kuwa hali ya nchi inavyokwenda kwa sasa si shwari kutokana na baadhi ya wabunge wa CCM na vyama vya upinzani kuendelea kuzungumza ovyo ovyo juu ya chama na serikali jambo ambalo ni hatari zaidi kwa Taifa.
Waziri Membe aliyasema hayo jana wakati akijibu maswali ya mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com kuhusu mbio hizo za Urais .
mtandao huu ulifanya mahojiano hayo mjini Iringa baada ya kumalizika kwa kongamano la wana vyuo vya elimu ya juu mkoani Iringa kongamano lililofanyika katika ukumbi wa St. Dominic ambako alikuwa mgeni rasmi waziri Membe alisema kuwa pamoja na kauli yake ya kwanza kwa Taifa kuwa muda bado kufika wa kufanya hivyo .
Waziri huyo alisema kuwa mbali ya kuwa muda wa kutangaza kuwania nafasi hiyo bado haujafika na chama chake kina utaratibu wa kutangaza mara baada ya muda kufika ila kwa mtazamo wake kama alivyopata kuueleza umma awali alipozungumza na vyombo vya habari juu ya mbio hizo za urais ,alisema kuwa anaheshimu sana taratibu za chama .
" Naomba kurudia tena mimi nilishapata kuueleza umma kuwa muda bado haujafika wa kutangaza kugombea Urais ....ila nasema hivi natagemea sana ushauri wa watanzania iwapo wataniona nafaa na kunitaka nigombee nitapima mawazo yao na iwapo ni wananchi wengi watakaoniunga mkono kutaka nigombee basi nitachukua fom na kuijaza ili nigombee nafasi hiyo kwani sauti ya wengi ni sauti ya Mungu " alisema waziri Membe
kuwa kama wananchi watasema jaza fom na nikaona ni sauti ya wengi nitajaza fomu ya kuwania kiti cha urais
Pia alisema kuwa hadi sasa hali ya nchi inazidi kwenda vibaya kutokana na kila mtu kuzungumza mambo bila kuthathimini na kuwa mbaya zaidi hata baadhi ya wabunge wa CCM nao wamekuwa si msaada kwa chama kutokana na mambo wanayozungumza dhidi ya serikali na chama.
Kuhusu mwenendo wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa sasa waziri Membe alisema kuwa kwa upande wake amepata kukaa bungeni zaidi ya miaka 15 toka bunge la spika Pius Msekwa hadi sasa chini ya spika Anne Makinda ila anachokiona ni baadhi ya wabunge kukosa maadili na kuzungumza mambo bila kuzingatia kanuni za bunge jambo ambalo ni hatari zaidi.
Alisema kuwa bunge linalotazamwa na watanzania ni lazima liwe bunge lenye mfano wa kuigwa na lenye kuzingatia maadili katika kuzungumza ila kwa sasa ndio maana bunge linaendelea kupoteza mwelekeo wake .
"Bunge linapoteza mwelekeo kutokana na mawazo ya baadhi ya wabunge wakifikiri wakisema ovyo na kutumia lugha kali katika kuzungumza basi wao ndio wanaonekana ni wabunge bora kitu ambacho hakipo ....kwani kuwa mbunge ni pamoja na kujiheshimu na kutumia lugha nzuri katika kuwakilisha wapiga kura wako bungeni"
Waziri Membe alisema kuwa kitendo cha baadhi ya wabunge kutotumia busara katika kujadili mambo bungeni si ubunge mzuri na watambue wazi kuwa wananchi wao wanawatazama na hukumu yao itatolewa mwaka 2015 katika uchaguzi mkuu kama hivyo wanachokifanya ni kuwawakilisha wananchi ama kujiwakilisha wao.
"Nawaomba wabunge kuwa wazalendo na kuwawakilisha wananchi waliowatuma badala ya kuligeuza bunge kama sehemu ya kuonyesha ujuzi wa kuzungumza ovyo ....nasema tuwaogope wananchi mwaka 2015 watatoa adhabu kwa kila mbunge kwa sasa wananchi wanakusikiliza na kunakutazama ila muda ukifika watakuacha"
Alisema kuwa wabunge wengi ni vijana na wanafikiri kusema vibaya juu ya CCM ndio ubunge bora ila watu watafanya uchunguzi wa kutembelea jimbo la mbunge husika na kuangalia kuwa amefanya nini katika jimbo lake na watakupima kwa kazi uliofanya na sio ukali wako bungeni.
Aidha waziri Membe alisema kuwa baadhi ya wabunge wa CCM wamekuwa ni msaada mkubwa kwa wananchi katika majimbo yao na pia wamekuwa msaada kwa chama na serikali chini ya Rais Jakaya Kikwete kwa kuwa msaada mkubwa wa kusukuma mbele maendeleo ya Taifa ila baadhi yao wapo kwa ajili ya kuonyesha uwezo wao wa kusema ovyo.

TAARIFA MBALI MBALI ZA KIMICHEZO KUTOKA TFF LEO


LIGI KUU YAINGIA RAUNDI YA 25
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inaendelea katika raundi yake ya 25 kesho (Mei Mosi) kwa mechi tano zitakazochezwa katika miji ya Dar es Salaam, Turiani, Morogoro na Mlandizi.
Licha ya kuwa tayari Yanga imetawazwa kuwa mabingwa wa VPL msimu huu (2012/2013), mechi dhidi ya Coastal Union itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni moja kati ya zitakazovuta macho na masikio ya washabiki wa mpira wa miguu nchini.
Mechi hiyo namba 172 itachezeshwa na mwamuzi Simon Mberwa kutoka Pwani akisaidiwa na Said Mnonga na Charles Chambea wote wa Mtwara wakati mwamuzi wa mezani atakiwa Hashim Abdallah wa Dar es Salaam. Kamishna wa mechi hiyo ni David Lugenge kutoka Iringa.
Viingilio katik mechi hiyo itakayoanza saa 10.15 jioni ni sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya bluu na kijani, sh. 8,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 15,000 kwa VIP C na B wakati VIP A itakuwa sh. 20,000. Tiketi zitauzwa uwanjani siku ya mchezo.
Mtibwa Sugar itakuwa mwenyeji wa African Lyon katika mechi namba 170 itakayochezeshwa na mwamuzi Dominic Nyamisana wa Dodoma kwenye Uwanja wa Manungu ulioko Turiani mkoani Morogoro. Nayo Kagera Sugar iliyo katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi hiyo itakuwa mgeni wa Polisi Morogoro kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi, Dar es Salaam na wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 7,000 uko tayari kwa mechi kati ya JKT Ruvu na Tanzania Prisons. Nayo Ruvu Shooting itakuwa nyumbani kwenye uwanja wake Mabatini ulioko Mlandizi, Pwani kuikabili Oljoro JKT kutoka Arusha.
MTANZANIA APEWA ITC KUCHEZA MSUMBIJI
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa mchezaji Yusuf Kunasa kucheza nchini Msumbiji.
Shirikisho la Mpira wa Miguu cha Msumbiji (FMF) lilituma maombi TFF kumuombea hati hiyo Kunasa anayekwenda kujiunga na timu ya Estrela Vermelha da Beira inayocheza Ligi Kuu nchini humo.
Kunasa ambaye msimu huu hakuwa na timu (free agent) amejiunga na timu hiyo akiwa mchezaji wa ridhaa (amateur). Zaidi ya wachezaji kumi kutoka Tanzania hivi sasa wanacheza katika klabu mbalimbali nchini Msumbiji.
MECHI YA SIMBA, POLISI MOROGORO YAINGIZA MIL 18/-
Mechi namba 163 ya Ligi Kuu ya Vodacom iliyochezwa juzi (Aprili 28 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa Simba kuibuka ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Polisi Morogoro imeingiza sh. 18,014,000.
 
Watazamaji 3,145 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambayo viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 3,564,252.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 2,747,898.31.
Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo waliokata tiketi hizo walikuwa 2,841 na kuingiza sh. 14,205,000 wakati idadi ndogo ya washabiki ilikuwa ya kiingilio cha sh. 20,000 kilichovutia washabiki 36 na kuingiza sh. 720,000.
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 1,812,331.75, tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 1,087,399.05, Kamati ya Ligi sh. 1,087,399.05, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 543,699.53 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 422,877.41.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

April 29, 2013

EXTRA BONGO YAZIDI KUWABAMBA MASHABIKI NDANI YA MEEDA SINZA

Mkurugenzi wa Extra bongo Ally Choki akiimba mbele ya mashabiki wake (Hawapo Pichani) ndani ya Ukumbi wa Meeda sinza jana Usiku wakati bendi yake ilipokuwa ikiburudisha pande pande hizo
Kushoto ni mwimbaji mahiri wa bendi ya Extra Bongo Athanas akiwa na Mwimbaji pekee wa kike wa bendi hiyo Khadija Mnoga a.k.a "Kimobitel" ambaye anatamba kwa sasa na wimbo wake wa "Mgeni" wakishoo luv mbele ya kamera yetu ndani ya ukumbi wa Meeda Sinza jana usiku wakati Bendi yao ilipokuwa ikitumbuiza pande hizo.
Kushoto ni mmoja wa marapa bora wa muziki wa dansi Totoo Ze Bingwa akirap ndani ya Meeda sinza wakati Bendi anayopigia mzigo Extra Bongo ilipokuwa ikitumbuiza pande hizo na kulia ni Banza Stone a.k.a Generale akimpa big up.
Maua ya Extra Bongo mzigoni
Wakata nyonga maarufu kwa sasa wa Extra bongo wakiongozwa na nyamwela wakiwapagawisha mashabiki waliohudhuria shoo hiyo ndani ya Meeda Sinza jana usiku
Waimbji bora wa Extra bongo kulia ni Rogert Hega a.k.a Katapila wakiimba ndani ya Meeda Sinza jana usiku
Rapa bora wa Extra bongo Kabatano (Kulia) akigani moja ya jimbo zao bora huku akipewa sapoti na nguli wa muziki wa dansi Banza Stone mwana masanja wakati bendi hiyo ilipokuwa ikitumbuiza maeneo ya Sinza katika ukumbi wa Meeda jana usiku.

WAZIRI MEMBE ATOA YA MOYONI WANAVYUO WAMGOMBEA


Wanachuo  Iringa  wakigombea  kupiga  picha ya pamoja na  waziri  wa mambo ya nje ya  ushirikiano  wa Kimataifa Bw. Membe  leo katika  ukumbi  wa St.Dominic mjini Iringa

Mkuu  wa wilaya ya  Kilolo Bw Gerald Guninita kushoto akiwa na waziri Membe leo

Baadhi ya  wachangiaji  wa mada katika  kongamano  hilo la  wanavyuo  Iringa  wakiwa katika  picha ya pamoja na waziri Membe

Mwenyekiti  wa CCM mkoa  wa Iringa Jesca Msambatavangu wa tano kulia akiwa na  waziri Membe na mwenye shati jekundu ni mwanahabari nguli  Simon Belege

Picha  zaidi ni yaliyoaliyoyasema  waziri Membe katika mahojiano maalum  na mtandao huu utayapata  hapa kesho

TANGAZO KWA WALIOSOMA SHULE YA MALANGALI SEKONDARI KUKUTANA

unapenda kuwatangazia wale wote waliosoma Shule kongwe iliyoanzishwa mwaka 1928 (MALANGALI SECONDARY SCHOOL) kuwa tarehe 5 May 2013, Mnakaribishwa kuhudhuria Get together party itakayoambatana na majadiliano ya namna tutakavoanzisha Umoja wa Wana-Malangali, shughuli hiyo itafanyika Ubungo pale LAND MARK HOTEL kuanzia saa 8.00 mchana.
Kufika kwako ndo kufana kwa shughuli hii, njoo tukumbushane habari za Ki-DCC, Ulefi, maparachichi ya kule bustani, Isimikinyi nk. Unaombwa kuwajulisha na wengine woote waliosoma Malangali iwe ni O level au A level, tufike bila kukosa.
Ahsanteni!
Kwa mawasiliano zaidi:-
Anangisye Kefa 0714 319802/0753 667515
Cosato Chumi 0784 272411
Agnes Nyakunga 0653 223880/0754 947659
Mr. Chongolo 0758250425

WAZIRI MEMBE ASEMA YEYE NI KIONGOZI SAFI HANA TUHUMA ZA RUSHWA ........

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Benard Membe ataka  kiongozi ama mtu yeyote anayeweza  kutoa  tuhuma  zake dhidi ya Rushwa  kujitokeza hadharani na kumtaja .

Waziri  Membe  alitoa kauli  hiyo leo   katika  ukumbi  wa  ST. Dominic mjini Iringa  wakati akizungumza na  wanavyuo  vya  mkoa  wa  Iringa katika  kongamano  la vyuo vya elimu ya juu mkoani Iringa.

Alisema  kuwa yeye ni miongoni  mwa  viongozi  safi na hajapata  kutoa wala  kupokea rushwa  kwani ana uzalendo mkubwa kwa Taifa  lake  la Tanzania.


 Hata  hivyo amewataka  wasomi wa  vyuo  vikuu  mkoani Iringa  kuongeza  jitihada katika elimu  ili  kuweza  kuja  kuwa  viongozi  wazuri na kuwa  ni vigumu  kuwa  kiongozi mzuri  bila elimu.

Alisema  kuwa  ili  kuwa na  serikali  bora  ni vema  suala la elimu  likapewa  kipaumbele na  wasomi wa  vyuo  vikuu  kuongeza  jitihada zaidi katika  elimu  ili hata  pale  wanaposimama kugombea nafasi  za uongozi ni lazima  wawe  wenyewe  kuwa na uelewa mpana  ili kiongozi bora  atakaye  simamia miji

Kwani  alisema  kuwa  hivi  sasa  kuna ushindani mkubwa wa elimu katika ulimwengu na kama wanafunzi  wataendelea  kufanya mchezo katika  elimu  upo  uwezekano mkubwa wa kuendelea  kushindwa katika soko la ajira.

Hata  hivyo  alisema  kuwa suala la  uzalendo  linahitajika  zaidi kwa  viongozi  ili  kulifanya Taifa  la Tanzania  kuendelea  kuheshimika  ndani na nje ya nchi  ya  Tanzania .

" Mimi   kuna  wakati mmoja mwaka  2005  nikiwa mbunge  nilipata  kuchukua usafiri  wa Taxi ya  kukodi kutoka uwanja  wa Ndege  wa  mwalimu Nyerere  hadi nyumbani  kwangu na nikiwa njiani  dereva wa  taxi  niliyokodi  alianza  kueleza ubaya  wa Tanzania  toka mwanzo hadi mwisho na nilipofika karibu na nyumbani  nilimsimamisha na kumwambia kuwa  sitakulipa pesa yako .....kweli  watanzania  tumekuwa ni  watu  wa kuelezea ubaya  wa Taifa  bila kuangalia  tunazungumza na nani"

Aidha alipingana na  watu ambao  wamekuwa  wakizitolea  nchi ndogo na kuilinganisha na  Tanzania ambalo ni Taifa  kubwa  ukilinganisha na baadhi ya nchi barani Afrika ambazo ni ndogo zaidi

Kuhusu  suala la rushwa  waziri Membe  alisema kuwa  kiongozi  bora  ni yule ambae anachukia  rushwa kwa  vitendo na kujali zaidi  maslahi ya Taifa  badala ya  kuangalia maslahi  binafsi .

Bila  kumtaja  kiongozi  yeyote  ama mtu  yeyote  waziri Membe  alisema  kuwa ni lazima  suala la Rushwa  kukemewa na kila mmoja  wetu na kuwa  ni vigumu  kuwa  kiongozi bora kama utakuwa  ukipokea Rushwa.

Kwa  upande  wake mchokoza mada katika  kongamano  hilo
Dr. Bukaza Chachage alimpongeza  waziri Membe  kwa kauli yake  ya  kuwataka  wale  wote  wanaweza kumtuhumu  kupokea  Rushwa  kupita  mbele na kusema hadharani .

Dr  Chachage  alisema  kuwa  iwapo  viongozi  wote  watasimama majukwaani kama waziri Membe na  kueleza usafi  wao  kuna uwezekano mkubwa wa Taifa kurejea katika misingi ya azimio la Arusha .

TANGAZO KWA WALIOSOMA SHULE YA MALANGALI SEKONDARI KUKUTANA

unapenda kuwatangazia wale wote waliosoma Shule kongwe iliyoanzishwa mwaka 1928 (MALANGALI SECONDARY SCHOOL) kuwa tarehe 5 May 2013,   Mnakaribishwa   kuhudhuria Get together party itakayoambatana na majadiliano ya namna tutakavoanzisha Umoja wa Wana-Malangali, shughuli hiyo itafanyika Ubungo pale LAND MARK HOTEL  kuanzia saa 8.00 mchana. 
Kufika kwako ndo kufana kwa shughuli hii, njoo tukumbushane habari za Ki-DCC, Ulefi, maparachichi ya kule bustani, Isimikinyi nk. Unaombwa kuwajulisha na wengine woote waliosoma Malangali iwe ni O level au A level, tufike bila kukosa.
 
Ahsanteni!
 
Kwa mawasiliano zaidi:-
Anangisye Kefa   0714 319802/0753 667515
Cosato Chumi   0784 272411
Agnes Nyakunga   0653 223880/0754 947659
  Mr. Chongolo 0758250425

April 28, 2013

MKE WA WAZIRI MKUU MH TUNU PINDA AMEZINDUA DVD YA KWAYA YA KANISA LA TAG MWENGE

Mke  wa  waziri mkuu mama Tunu Pinda akiwa anaonyesha DVD yenye jina la Mungu Wetu Halinganishwi iliyo imbwa na kwaya ya Kanisa la Tag Mwenge wanaoshuhudia ni kulia kwa Mama Pinda ni Mchungaji kiongozi Abdiel Mhini kulia mwenye kilemba ni Mchungaji Grace Mainoya anayefuatia ni Askofu wa jimbo la Mashariki Kaskazini Spear Mwaipopo Mama Tunu Pinda alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Dvd hiyo iliyoizindua leo picha na Chris Mfinanga
Mama Tunu Pinda akiwa anasoma risala kwa waumini wa Kanisa la TAG kabla ya kuzindua dvd picha zote na Chris Mfinanga

SAKATA LA MACHINGA KUTII KAULI YA MBUNGE MSIGWA , LACHUKUA SURA MPYA IRINGA

polisi Iringa  wakiwa katika  eneo la Mashine tatu ,kuondoa mawe na magogo ambayo yalitumika  kuziba barabara hiyo kama  sehemu ya  kushinikiza  serikali  kuwaruhusu kuendelea  kufanya kazi ya umachinga  eneo hilo  lisiloruhusiwa
Kamati ya  ulinzi na usalama ya wilaya ya Iringa ikiwa  imekutana mchana  huu kwa  kikao cha dharula  kufuatia Machinga  kutekeleza kauli ya mbunge Msigwa  ya kuvunja sheria
Hii  ndio hali halisi  iliyopo  eneo la mashine tatu baada ya machinga  kurejea  eneo hilo leoKAULI mbunge wa jimbo hilo Mchungaji Peter Msigwa (Chadema) kuwataka wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) kurejea kufanya kazi katika eneo la barabara ya Mashine tatu
nusuru asababishe machafuko makubwa eneo hilo kati ya  polisi na Machinga.
 
Msigwa ambae aliitoa kauli hiyo mwanzoni mwa  wiki  iliyopita  katika mkutano wa wabunge wa chadema waliosimamishwa bungeni ,mkutano uliofanyika katika uwanja wa Mwembetogwa mjini hapa,kwa kuwataka Machinga kurejea eneo hilo na iwapo mtu atafika kuwanyanyasa basi wana----!!!?
Machinga hao jana wameitikia kauli hiyo kwa kurejea eneo hilo na kupelekea askari wa kutuliza ghasia (FFU) kutanda eneo hilo na kushindwa kutumia nguvu zaidi ya kuwataka wafanyabiashara hao kuendelea na shughuli zao eneo hilo .
Wakizungumza na mwandishi  wa habari hizi eneo la tukio  wafanyabiashara hao  walisema  kuwa  wamelazimika  kurejea  katika  eneo  hilo baada ya mbunge  wao Mchungaji Msigwa  kuwaruhusu  kufanya biashara katika  eneo hilo ambalo mwanzoni  walihamishwa na kupelekwa Mlandege .
Hivyo  walisema  ilikuwa ni  vigumu kwao kuondolewa na  polisi katika  eneo hilo ambalo mbunge kama mwakilishi  wao bungeni na vikao  vya baraza la madiwani amewaruhusu .
“ujue  tulianza  kuwashangaa sana polisi wa FFU kufika katika  eneo hili na mabomu ya machozi kutaka kutotoa  wakati wao wenyewe  walikuwepo katika mkutano  wa Chadema pale mwembetogwa ambapo mbunge wetu Msigwa alituruhusu kurejea  eneo hili….kweli  tungeshindwa kulielewa jeshi la  polisi iwapo  wangetumia nguvu kutuondoa  sisi  wakati aliyetoa kauli ya  kuturuhusu anafahamika “
 
Kwa  upande  wake mwanasheria  wa Halmashauri  ya Manispaa ya Iringa, Innocent Kihaga alisema  kuwa eneo hilo kisheria limepigwa marufuku kwa  biashara  za umachinga na  kuwa kwa mtu ambae atapatikana akifanya biashara hapo faini yake ni shilingi 50,000 ama kifungo cha miezi sita jela ama vyote kwa pamoja.
Hatua  hiyo ya machinga  kurejea  katika  eneo hilo la barabara imeonyesha  kuichanganya  serikali ya  mkoa  wa Iringa na  kulazimika  kukutana kwa masaa kadhaa na kamati ya  ulinzi na usalama.
 
Akizungumzia suala  hilo mwenyekiti  wa kamati ya  ulinzi na usalama ya wilaya ya Iringa na kaimu mkuu  wa  mkoa  wa Iringa Dr Leticia Warioba ambae ni mkuu  wa wilaya ya Iringa  alisema  kuwa serikali  ya mkoa  inapinga kwa  nguvu zote kitendo cha wafanyabiashara hao kurejea  eneo hilo.
Dr Warioba alisema  kuwa anashangazwa na hatua ya  mbunge  Msigwa  kuwaruhusu  wafanyabiashara hao  kuvunja sheria  wakati mbunge  huyo katika  vikao  vya baraza la madiwani katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa ni diwani ni katika maamuzi ya  kuwatoa wafanyabiashara  hao alishiriki .
 
Hata  hivyo Dr Warioba  aliwataka wafanyabiashara  hao kwa  jumapili  ijayo  kutofanyabiashara  eneo hilo na kuonya  wale  wote watakaokiuka kauli  hiyo na sheria iliyowekwa  juu ya kutofanya biashara  katika maeneo yasiyo rasmi.
Wakati huo mbunge wa jimbo la Mbeya mjini ,Joseph Mbilinyi (MR SUGU) jana  ameonekana katika Manispaa ya Iringa akiingia katika mashine ya kutoa pesa ATM ya NMB iliyopo nje ya jengo hilo la Manispaa ya Iringa na kusalimiana na viongozi wa Manispaa waliokuwepo nje ya jengo hilo.

BREAKING NEWS...IRINGA SI SHWARI MVUTANO KATI YA MACHINGA NA POLISI WATISHIA USALAMA

Machinga wakiendelea na  shughuli zao kama kawaida  eneo la mashine  Tatu asubuhi  hii kutokana na kauli  ya mbunge Msigwa kuwaruhusu kurejea ,chini polisi  wakiwa eneo hilo

Hali  si  shwari katika Manispaa ya Iringa baada ya kauli   mbunge  wa  jimbo hilo Mchungaji Peter Msigwa (Chadema) kuwataka wafanyabiashara  wadogop wadogo (machinga) kurejea kufanya kazi katika eneo la barabara  ya Mashine  tatu kutekelezwa na machinga  hao.
Msigwa ambae  aliitoa kauli hiyo April 23 mwaka  huu katika mkutano wa wabunge wa chadema  waliosimamishwa  bungeni ,mkutano  uliofanyika katika  uwanja  wa Mwembetogwa  mjini hapa,kwa  kuwataka Machinga  kurejea  eneo hilo na iwapo mtu atafika  kuwanyanyasa  basi wana----!!!?
Machinga  hao  leo  wameitikia kauli  hiyo kwa  kurejea  eneo hilo na kupelekea askari  wa  kutuliza ghasia (FFU) kutanda  eneo hilo na kushindwa  kutumia nguvu  zaidi ya  kuwataka wafanyaiashara hao  kuendelea na shughuli  zao  eneo hilo .

April 27, 2013

MTOTO ALIYEKUWA AKISUMBULIWA UVIMBE SHINGONI AMEFARIKI DUNIA


  Mtoto  huyo ni mkazi  wa mjini Iringa na babake BW. Godfley Mofuga anafanya kazi ya kuendesha daladala amefariki  dunia akiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili akisubiri matibabu baada ya  kuchukuliwa vipimo .

Mtandao  huu  wa www.francisgodwin.blogspot.com na www.matukiodaima.com unawashukuru wadau wote ambao mlijitolea michango yenu kwa ajili ya  kumsafirisha mtoto huyu kwenda  kuanza matibabu ila kazi yake mola haina makosa

KLABU YA SIMBA YAMPONGEZA HANS POPPE KWA KUREJEA SIMBA


Ismail Rage
MWENYEKITI wa Simba, Mhe, Ismail Aden Rage, amemshukuru aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya klabu, Zacharia Hans Poppe, kwa kukubali kurejea kushikilia nyadhifa zake zote.
Poppe alitangaza kujiuzulu nyadhifa zake za uongozi ndani ya Simba Machi 7 mwaka huu, kutokana na hali ya migogoro iliyokuwapo wakati huo.
Hata hivyo, Rage alikataa kujiuzulu huko kwa Poppe na akasema atamshawishi abadili maamuzi kwa manufaa ya Simba.
“Napenda kutumia nafasi hii kuwaarifu wana Simba popote walipo kwamba Poppe amerejea na yuko tayari kuitumikia Simba kama Mjumbe wa Kamati ya Utendaji na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba,” alisema Rage.
Kwa upande wake, Poppe alisema amerejea Simba kutokana na utulivu ulioanza kujitokeza klabuni na kwamba nia yake ni kuhakikisha klabu inafanya usajili mzuri na wa kiwango kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu.
Imetolewa na
Ezekiel Kamwaga
Ofisa Habari
Simba SC

POLISI ARUSHA WASEMA MBUNGE LEMA KUFIKISHWA MAHAKAMANI KWA UCHOCHEZI

Mbunge Lema
.............................................................
MAMBO yamezidi kumwendea kombo Mbunge wa Arusha Mjini, (Chadema) Godbless Lema baada ya Jeshi la Polisi kutangaza rasmi kwamba itamfikisha Mahakamani, siku ya Juma tatu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Liberatus Sabas amesema kwamba Mbunge huyo hawezi kuachilia huru kwa sababu mashtaka dhidi yake yameshakamilika na atafikishwa Mahakamani siku ya Juma tatau.

"Hatuwezi kumwachia kwa sababu anatarajia kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili"alisema Sabas.

 Wakati Kamanda huyo akitoa msimamo huo, taarifa za ndani ya Jeshi hilo zinaeleza kwamba Mbunge huyo amehojiwa kwa zaidi ya saa nane sasa na bado yuko katika chumba maalum kwa mahojiano zaidi na maofisa wa Polisi huku akitakiwa kuonyesha ujumbe mfupi wa vitisho aliyodaiwa kuwa ametumiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mulongo.

Katika hatua nyingine Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Arusha, imekuwa na kikao kirefu kinachoongozwa na Mkuu wa Mkoa Mulongo na kwamba ajenda kubwa inayojadiliwa ni tukio zima la vurugu zilizotokea katika Chuo cha Uhasibu mkoani humo.
 
 Lema alikamatwa usiku wa kuamkia leo baada ya Askari wa Jeshi la Polisi kumfuata nyumbani kwake na kuzingira nyumba yake kabla ya zoezi la kumchomoa ndani ya nyumba hiyo kufanyika.

Mbunge huyo anatuhumiwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo kosa la kuchochea vurugu katika chuo hicho baada ya kutokea mauaji ya Mwanafunzi Henry Koga aliye uawa kwa kuchomwa kisu juzi akirejea chuoni hapo kutoka kwenye matembezi yake, hata hivyo haijajulikana mara moja sababu za kuawa kwa mwanafunzi huyo wala watuhumiwa hawajakamatwa.(
chanzo habari mpya.com)

MBUNGE WA CCM NKASI APINGA MATUMIZI YA MBOLEA YA MINJINGU KUWA HAIFAI

 
 
Na Elizabeth Ntambala FG Blogu Rukwa

Mbunge wa Nkasi, Ali Keisy (CCM) ameilaumu Serikali kwa kutokuwa na mpango mzuri kwa wakulima wa Mkoa wa Rukwa, kwani imeshindwa kuwaondolea kero kubwa ya mbolea ya Minjingu ambayo ilipelekwa muda mrefu na kuonekana mbovu.

Keisy alisema Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika ilipanga kuwasaidia wakulima wa ukanda huo mbolea ya ruzuku, lakini ilibainika mbolea yote tani 1,000 iliyopelekwa Mkoa wa Rukwa ilikuwa haifai.

“Hata hivyo, naishangaa Serikali yangu, hivi kweli huyo Minjingu ni nani na kwa nini ameiweka Serikali mfukoni kiasi hicho, mbona hamumshughulikii,” alihoji.

Alishangazwa na kitendo cha wizara hiyo kuendelea kuweka mbolea hiyo kwenye maghala kwa muda mrefu, huku wakisingizia kuwa watapeleka mbolea nyingi kuihuisha na kwamba, ni makosa kwani wangepaswa kukamatwa wakati huo baada ya kuifikisha.

Pia, Keisy alilaumu Serikali kwa kuendelea kuagiza mchele kutoka nje ya nchi, ilhali Tanzania kuna mchele mwingi wenye ubora ambao hauna soko.

Keisy alisema kama Serikali itakuwa makini kuwatengenezea miundombinu wakulima wa mpunga, haitapata tabu ya kuagiza mchele kutoka nje ya nchi.,liitaka Serikali iwe makini katika suala la kilimo nchini.

MBUNGE LEMA AKAMATWA NA POLISI ARUSHA
Baada ya mabishano ya muda mrefu nyumbani kwa kada huyu na Mbunge wa Arusha mjini na uvamizi wa Polisi wakati wa usiku wa manane, Mh. Lema alikubali kukamatwa na kuchukuliwa na gari la polisi usiku na kupelekwa kituo kikuu cha polisi Arusha( Central Polisi)
 
Kukamatwa kwake kulikuja baada ya polisi kuvunja mlango na kuingia ndani na kuendesha msako wa nguvu humo ndani  Vitu kama laptop, ipad, simu vipo mikononi mwa police.
 
Safari ya Lema kuelekea polisi ilisindikizwa na msululu wa magari ya makada waliojitokeza kumsupport kuelekea kituo cha polisi.

Baada ya kumfikisha Lema Central police Arusha alisachiwa na kuingizwa ndani Lema alikuwa ameambatana na magari ya wafuasi wa Chadema waliomsindikiza ili kushuhudia kinachojili hapo kituoni.

Baada ya kumtupa ndani,polisi waliwafukuza wafuasi hao wa Chadema hapo kituoni na kuwaambia hawatakiwi kuonekana hapo.

BREAKINGNEWSSS .........PAROKO WA RC IFUNDA APOTEZA MAISHA KATIKA AJALI AKITOKA MSIBANI NJOMBE


                Hili ndilo gari ambalo  limesababisha  kifo cha paroko ( picha na Gogers Stivin Mselu wa FG Blogu Mafinga)
             ............
PAROKO  wa kanisa la RC parokia ya Ifunda Alphonce Mhamilawa amefariki  dunia katika ajali mbaya ya gari  iliyotokea katika eneo la Saba  saba Mafinga wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.

Mashuhuda  wa  ajali  hiyo wameueleza mtandao  huu  wa  www.francisgodwin.blogspot.com  kuwa ajali  hiyo ilitokea  majira ya saa 2 usiku  wa  kuamkia  leo wakati paroko  huyu akitoka mkoani Njombe katika  shughuli  ya Mazishi

Mmoja kati ya mashuhuda  hao Bw  Saugo Ndemo  alisema  kuwa paroko  huyo alikuwa akiendesha gari dogo Paina ya Toyota  Hilux (Pick Up) yenye  namba  za usajili  T434 APP mali ya Kanisa la Roman Katoliki Parokia ya Ifunda.

Ndemo  alisema  kuwa chanzo  cha ajali  hiyo ni Paroko  kuligonga gari aina ya Lori  kwa  nyuma na kuwa lori  hilo halikuweza  kusimama .

Alisema  kuwa  paroko  huyo alifia eneo la tukio baada ya  ajali  hiyo  iliyopelekea  kichwa  chake  kupasuka .

Mmoja kati ya askari  wa usalama barabarani ambae hakutaka  kutaja jina lake kwa  kuwa si msemaji  mkuu  wa  jeshi la  polisi alisema  kuwa  chanzo cha ajali  hiyo ni mwendo kasi.

Pia alisema   kuwa lori ambalo  paroko  huyo aliligonga  linasadikika  kuwa lilibeba mbao huku  likivutana na  lori  jingine na baada ya ajali  hiyo halikuweza  kusimama .
....................................

Picha  za ajali  hii mbaya  zitakujia hivi punde hapa
HABARI  HII KWA  UDHAMINI MKUBWA  WA  KITUO CHA MAFUTA CHA HOPE SERVICE STATION HAPA HUDUMA NI MASAA 24


Wengi hukimbilia kununua mafuta hapa HOPE SERVICE STATION eneo la CRDB barabara ya Iringa -Dodoma katikati ya mji wa Iringa kituo kinachouza mafuta masaa 24 ,wewe wasumbuka na nini jiunge na kituo cha wengi sasa .

KITUO CHA MAFUTA CHA HOPE SERVIRCE NI MABINGWA WA UUZAJI WA MAFUTA MKOANI IRINGA
KARIBU UJAZE MAFUTA KWENYE GARI YAKO HAPA HOPE SERVICE STATION TUPO JIRANI NA BENKI YA CRDB MIYOMBONI BARABARA YA IRINGA DODOMA