Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

March 31, 2013

WAZIRI WA VIWANDA AKAGUA UJENZI WA KIWANDA CHA SARUJI LINDI


Waziri wa Viwanda na biashara,Abdallah Kigoda
akipata taarifa fupi ya kazi za ujenzi wa kiwanda cha Simenti toka kwa
Mkurugenzi wa Meis Industries,Merey Ally Saleh

........................................................................................................................

Na Abdulaziz,Lindi

Zaidi ya  dola milioni 30 zinatarajia kutumika kwa ajili ya ujenzi wa
kiwanda cha Lindi simenti ambacho kimeanza ujenzi wake mapema mwenzi
feb  na  kinatarajia  kumamilika baada ya miezi 14 kuanzi sasa.

Hayo yamebainishwa na mkurugenzi mtendaji wa Meis Industries company
Ltd,, Merey Ally Saleh alipokuwa anazungumza na waziri wa viwanda na
biashara Abdala Kigoda wakati alipotembelea kuangalia maendeleo ya
ujenzi wa kiwanda hicho .

Meley alisema kukamilika kwa ujenzi wa kiwanda hicho kutasaidia
kuajiri watu zaidi ya 1000 na kitakuwa na uwezo wa kuzalisha tani 600
hadi 700 za sement kwa siku ambayo Itasaidia wakazi wake kupata bidhaa
hiyo kwa bei nafuu kuliko hivyo sasa.


Alisema kiwanda pia kitatumia raslimali zinazopatikana  hapa nchini
kwa asilimia 95 na asilimia tano bidhaa za kutoka nje ambazo ni
kemikali za kuumulia udongo  na kufanya kuwa sementi.

Kwa upande wake waziri wa viwanda Abdalah Kigoda ameipongeza  kampuni
ya Meis kwa kitendo cha kufikiria kujenga kiwanda hicho  na kueleza
kuwa kitakuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo kwa mikoa ya kusini
Lindi na Mtwara  na kupunguza tatizo la ajira lililopo.

Kigoda alisema kiwanda hicho kitakuwa cha nne kwa ukubwa ambacho
kinatumia raslimali za  ndani kwa asilimia kubwa kama vile viwanda vya
Twiga sementi, Tanga sementi na Lindi Sementi.

Alisema  serikali inaona juhudi za wawekezaji  na hivyo basi  iko
katika utaratibu wa kuondoa changamoto cha ukosefu wa umeme ambao
umekuwa kero kubwa kwa wawekezaji wa viwanda hapa nchi kwa kuharakisha
miradi ya uvunaji wa gesi kwa ajili ya nishati hiyo

DAMU YA WATANZANIA INAYOMWAGIKA ITAULIZWA: ASKOFU

Maandamano kuingia kanisani kwa ajili ya maadhimisho ya Siku Kuu ya Pasaka katika Kanisa la kiaskofu Parokia ya Kihesa Jimbo Katoliki la Iringa hii leo. Wenye mavazi mekundu na meupe ni kwaya ya Mt. Cecilia.


Wanakwaya wa Kwaya ya Mt. Cecila wakiimba kanisani wakati wa Misa Takatifu.

Romed Kavenuke mwalimu na mpiga kinanda wa kwaya ya Mt. Cecilia Kwaya Kuu akipiga kinanda wakati wa Misa Takatifu ya Pasaka. Parokia ya Moyo Mt. Yesu Kihesa Jimbo Katoliki la Iringa.

Waamini wakiwa kanisani wakati wa Misa Takatifu
--------------------------------------------------------------------
ASKOFU Jimbo Katoliki la Iringa Mhashamu Tarcisius Ngalalekumta amesema damu ya watanzania inayomwagika juu ya ardhi ya, wahusika wa matukio hayo wataulizwa na Kristo aliyejitoa sadaka kwa ajili ya ukombozi.

Gustav Chahe mwandishi wa mtandao huu anaripoti kuwa Mhashamu Ngalalekumtwa ameyasema hayo leo wakati wa maadhimisho ya Misa Takatifu ya Pasaka iliyofanyika katika Kanisa la Kiaskofu Parokia ya Kihesa jimboni humo.

Askofu  Ngalalekumtwa ambaye pia ni Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania alisema kuwa inatia shaka kwa wahusika wa matukio hayo kuwa huenda wakawa si watanzania ambao wamejaliwa upendo na ushirikiano pamoja na kuheshimiana.

Amesema wapo baadhi ya watu wanaowafanya wenzao kuishi kama wakimbizi jambo ambalo ni kinyume na mpango wa Mungu aliyesema watu wote waishi kwa ushirikiano na upendo kwa kusaidiana katika kudumisha amani ya mtu binafsi na ya taifa kwa ujumla.

“Tuendelee kuwa wanyonge? Hii ni balaa! Hii ni nchi yetu lakini kwa nini wengine wawe kama hawana haki?” amehoji askofu Ngalalekumtwa.

Hata hivyo alisema wenye dhamana ya kulinda usalama na kuruhusu mambo haya kutendeka hakuna haja ya kuendelea katika nafasi hizo kwa sababu wameshindwa kuwajibika kutimiza haki za watanzania.

“Tuliombee Taifa letu. Na hao wenye dhama ya kulinda usalama wa taifa hili na kuzembea  hawana haja ya kuendelea kuongoza nafasi zao kwa sababu wameshindwa. Njia yao hao ni motoni tu kwa sababu kazi ya Kristo ni kudumisha amani na upendo” amesema.

Amesema binadamu ana akili fupi, finyu na ndogo ambayo anahitaji msaada wa Kristo aliyejitoa kwa ajili ya kuwakomboa wanadamu ili apate nguvu na kuongezewa ufahamu wa mambo.

“Binadamu ana kila aina ya dhuruma, ana kila aina ya ufidhuli na ana kila aina ya manyanyaso lakini Kristo pekee ndiye anayetaka tuwe wapole na watu wenye kujitathimini na kuomba msamaha n msaada kwake” amesema.

Amesema kiongozi anayependa kutumia mabavu katika kazi na maamuzi yake hana tofauti na viongozi waliomsulibisha Yesu msalabani.

“Ukiona unatafuta sababu ya kugombana na Kristo ujuwe una shida kichwani na mwisho wake ni mbaya. Kiongozi asiyetambua hayo ni mfidhuli na fisadi” amesema.


MAKAHABA RAIA WA RWANDA MATATANI DODOMA

WANAWAKE watatu raia wa Rwanda wanaosadikiwa kuendesha biashara ya ukahaba mjini Dodoma wamekamatwa na
kupewa siku tatu kuondoka nchini, huku wawili kati yao wakikutwa na vidonge vya kupunguza makali ya virusi ya Ukimwi (ARVs).

Kukamatwa kwa wanawake hao ambao ni Esperance Hagenimana (28), Vestina Zaninika (27) na Ziada Mukamurera (25), kunafuatia mmoja wao Esperance kwenda kutoa taarifa kituo cha polisi kuwa alikuwa ameibiwa fedha taslimu Sh 800,000 na hati ya kusafiria.

Lakini, Polisi walipofika nyumba ya kulala wageni waliyofikia iliyopo eneo la Area D walikuta wanawake wengine wawili ambao walikuwa wakikaa chumba kimoja na Esperance.

Uchunguzi wa Polisi ulibaini kuwa mwanamke huyo hakuibiwa na kubaini wote si raia wa Tanzania. Hata hivyo kilikosekana kifungu cha kuwashitaki ndipo waliamua kupeleka sakata hilo Uhamiaji ili liweze kushughulikiwa.

Kulingana na maelezo yao, Esperance alitangulia kuja nchini kisha kuwaita wenzake ambao ilikuwa ni mara ya kwanza kuja nchini, lakini hata hivyo alisema kuwa, kumekuwa na makundi ya wanawake kutoka Rwanda wanaokuja nchini kipindi cha Bunge na hata mwaka jana kuna kundi lilikuja wakati wa mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kulingana na uchunguzi uliofanywa na Uhamiaji, wanawake hao waliingia nchini na kujitambulisha kuwa walikuja Dodoma kufanya biashara ya vitenge, lakini hawakuwa hata na kitenge kimoja ambacho kingeweza kuwaonesha kuwa walikuwa wakifanya biashara hiyo.

Juhudi hizo za Uhamiaji zinadaiwa kuwafikisha hadi klabu moja maarufu ya usiku iliyopo eneo la Area D ambapo walinzi wa Kimasai walikiri kuwafahamu wanawake hao na walikuwa wakiwafuata nyumba ya wageni waliyofikia kama mtu alikuwa akiwahitaji na walikuwa na ni wateja wa klabu hiyo ya usiku.

Alipoulizwa kuhusu suala hilo, Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Dodoma, Norah Massawe alikiri kukamatwa kwa wanawake hao na polisi na kukabidhiwa Uhamiaji.

Alisema mwanzoni wanawake hao walidai kuwa walikuja Dodoma kwa ajili ya kununua vitenge kwa ajili ya biashara na waliposhikiliwa na Polisi kwa siku kadhaa waliomba kurudishwa nchini kwao.

Alisema wawili kati yao walikutwa wakiwa na vidonge vya ARVs, lakini haijafahamika moja kwa moja kama walikuwa wagonjwa au la.

“Siwezi kusema walikuwa ni makahaba bali wanahisiwa hivyo kutokana na biashara waliyosema wanafanya kutoeleweka na hata maelezo ya walinzi wa klabu ya usiku kuwa walitambuliwa kama wateja wao, kwa kweli hilo siwezi kulithibitisha,” alisema.

Aliwataka wananchi kuwa makini na watu wasiowafahamu kwani hivi sasa Mkoa wa Dodoma umekuwa na mwingiliano mkubwa wa watu hasa katika kipindi cha Bunge.

Mwandishi wa habari hizi, alimtafuta Mratibu wa Ukimwi Mkoa wa Dodoma, Audrey Njelekela ambaye alisema kuwa, wamekuwa wakitoa elimu kuanzia ngazi ya Mkoa hadi mtaa ambapo kuna timu ya Mkoa ya Ukimwi na hata kwenye halmashauri kuna waratibu ambao wamekuwa akitoa elimu juu ya masuala mbalimbali yanayohusu Ukimwi.

Alisema kuwa kwa sasa kiwango cha maambukizi kwa Mkoa wa Dodoma ni asilimia 2.9 kwa takwimu za mwaka 2011 na 2012 ikilinganisha na takwimu za mwaka 2007 hadi 2008 ambapo kiwango cha maambukizi kilikuwa asilimia 3.3.

Alisema kuwa waratibu wa ngazi ya halmashauri wamekuwa wakitoa elimu juu ya kujikinga na maambukizi ya Ukimwi kwenye maendeleo mbalimbali ikiwemo klabu za usiku.

Alisema kwa kuwa kondomu zinasambazwa maeneo mbalimbali yakiwemo ya starehe ni vyema wananchi kuhakikisha wanazitumia. “Matumizi ya kondomu ni muhimu sana kwani maeneo ya klabu za usiku na maeneo mengine ya starehe watu wengi wanachukuana tu lakini wanakuwa hawafahamiani,“ alisema.

Alisema kuwa kutokana na mwingiliano mkubwa wa watu katika Mkoa wa Dodoma hasa kipindi cha Bunge, umakini zaidi unahitajika.

CHANZO: HABARI LEO

WAKRISTO WATAKIWA KUJIEPUSHA NA BIASHARA HARAMU

Mara baada ya ibada ya kubariki moto, mshumaa wa Pasaka
----------------------------------------------------------------------------------------------------------
WAKRISTO nchini wametakiwa kujiepucha na biashara zisizo za halali zinazowaumiza wengine kwa kuhatarisha amani, upendo na mshikamano vilivyotunu kuu ya nchi hii.

Mwandishi wa mtandao huu Gustav Chahe anaripoti kuwa haya yamezungumzwa na Mhashamu askofu Tarcisius Ngalalekumtwa wa Jimbo Katoliki la Iringa alipokuwa akihubiri katika Misha ya Mkesha wa Pasaka iliyofanika katika Kanisa la Bikira Maria Consolata Parokia ya Mshindo jimboni humo.

Ngalalekumtwa alisema wapo baadhi ya watu wanaofanya biashara haramu huku wakijua kuwa wanawaumiza wengine bila kujali.

Askofu Ngalalekumtwa ambeye pia ni Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania alisema binadamu ananuka kwa kufanya matendo ya aibu na kuwafanya wengine kuwa kama watumwa.

“Tunanuka, tumeoza na uchafu uliogandamana kwa miaka mingi unaotokana na matendo machafu ya kuwafanya wengine kama watumwa” alisema.

Alisema Mungu anawataka kuwa ni watu wenye kulinda utu wao na uumbaji wake kwa kufanya yale ambayo kila mmoja anayapokea na kuridhika katika maisha yake.

“Sisi ni watoto wa aliye chanzo cha wema na aliye na utakatifu. Hivyo, tusiwe wafu na “tulemwakuva twivafu”, tutumie akili zetu kutenda yale yaliyo na maana kwa manufaa ya upendo na haki kwa kila mmoja” alisema.

Amewataka kutokuwa na hofu ya kuilinda imani yao kwa kuwa Mungu pekee ndiye mwenye mwokozi wa kweli na kuwataka wapuuze yale yasiyoijenga jami iwe kwa maneno, vitendo au kwa kulazimishwa.

“Simameni imara katika kuikiri imani yenu ili iweze kuratimu mawazo, matendo, maneno hata mahusiano sisi kwa sisi na mahusiano yetu na Kristo ikiwa ni pamoja na mahusiano ya kisiasa hata kidini” alisema.

Alisama kwa Mkristo heshima, utii na upendo ni zawadi ya pekee waliyo jaliwa na Mungu kwa ajili ya kuziunganisha jamii katika kitu kimoja zinazoelewana bil kudharauliana na kufarakana katika maisha.

“Kuweni watu wema, wapenda haki, heshima, huruma, upole, wema na unyenyekevu usio na unafiki. Msiache upepo wa dunia hii izimishe mwanga, upendo wenu, huruma yenu, utii wenu na upole wenu. Jivisheni vazi la haki lenye kutenda mema” alisema.

Hata hivyo alisema mtu asiyekuwa na imani ni sawa na kuwa uchi na ndicho chanzo cha kufanya mambo machafu na ya ajabu yasiyompendeza Mungu na wanadamu wenzake.

“Kama huna imani ni sawa na kuwa uchi tena uko ovyo. Kristo anayamulikisha maisha yetu kwa nuru ya utukufu wake ili tuachane na giza. Hakuna mwokozi mwingine wa wandamu isipokuwa Yesu wa Nazareti” amesema.

Katika Misa hiyo vijana 15 walipewa Sakramenti ya ubatizo na Kipaimara.

UCHAGUZI KENYA ULIKUWA HURU NA HAKI ,KENYETTA NI RAIS


Mahakimu wa mahakama kuu wakitangaza uwamuzi wao kuhusiana na kesi ya Odinga

Mahakama Kuu Kenya yasema Uhuru alichaguliwa kihalali

Uhuru Kenyatta alichaguliwa kihalali, mahakama yasema
Uhuru Kenyatta alichaguliwa kihalali, mahakama yasema
 ...........................................................................................................................................
Mahakama ya juu zaidi nchini Kenya, imeamua kuwa rais mteule Uhuru Kenyatta atasalia kuwa rais mpya wa Kenya baada ya kusema kuwa uchaguzi ulifanywa kwa njia huru na ya haki.
Uchaguzi wenyewe ulifanyika tarehe nne mwezi Machi, ambapo hesabu ya kura ilimpa ushindi Kenyatta kwa zaidi ya laki nane.
Rais wa mahakama hiyo jaji mkuu Willy Mutunga alisema kuwa mahakama imekubali kwa kauli moja kuwa uchaguzi ulifanywa kwa njia ya huru na wazi na kuwa Kenyatta na mgombea mwenza wake walichaguliwa kihalali.

Uamuzi huu una maana kuwa Uhuru Kenyatta ndiye ataapishwa kama rais mpya wa Kenya tarehe tisa mwezi ujao

Kesi hiyo iliwasilishwa katika mahakama ya juu zaidi na mpinzani mkuu wa Kenyatta, Raila Odinga baada ya uchaguzi uliofanyika mapema mwezi huu.

Matokeo rasmi yalionyesha kuwa Uhuru alishinda uchaguzi kwa kumpiku Raila kwa asilimia 50.07 huku Raila akipata asilimia 43.28. Matokeo haya yalizuia kufanyika kwa duuru ya pili ya uchaguzi kwa kura 8,100.

Bwana Odinga aliishutumu tume huru ya uchaguzi na mipaka kwa kuhujumu matokeo ya uchaguzi ili kumpa ushindi Uhuru Kenyatta.

Uchaguzi wa urais, wabunge na wajumbe wengine wa serikali, ulifanyika tarehe nne mwezi Machi, ukiwa wa kwanza tangu uchaguzi uliokumbwa na ghasia mwaka 2007 na kusababisha vifo vya watu zaidi ya elfu moja.

Bwana Kenyatta na mgombea mwenza wake ,William Ruto,wanakabiliwa na kesi katika mahakama ya jinai kwa kuchochea ghasia za mwaka 2007. Hata hivyo wamekanusha vikali mashtaka.

Mahakama ya juu zaidi inaweza kuthibitisha ushindi wa Kenyatta au kuubatilisha uamuzi wa wakenya na hivyo kuitisha uchaguzi mpya.

Vyovyote matokeo yatakavyokuwa kuna wale watakaoghadhabika mno.
Rais anayeondoka mamlakani, Mwai Kibaki amewataka wakenya kuwa watulivu na kukubali uamuzi wa mahakama lakini wengi wanatagemea sana idara ya mahakama ambayo imekuwa na mageuzi makubwa na ambayo sasa watu watu imani nayo.

Mawakili wa Odinga wanasema kuwa kesi yao ilihusisha madai ya kuhujumu hesabu ya kura pamoja na matatizo ya usajili wa wapiga kura na vile vile matatizo ya mitambo ya usajili wa wapiga kura.

Mnamo Ijumaa mahakama ya juu zaidi ilidurusu matokeo ya kura katika vituo 22 vya kupigia kura. Na pande zote mbili zilisema matokeo yalithibitisha misimamo yao.

Kenyatta ameutaja uchaguzi huo kama ishara ya kukuwa kwa demokrasia Kenya na ulifanywa kwa njia ya amani.

Tume ya uchaguzi, pia imesisitiza kuwa uchaguzi ulikuwa huru licha ya hitilafu za kimitambo
Wachunguzi wa kimataifa nao walisema kuwa uchaguzi ulikuwa huru na wa haki na kuwa tume huru ya uchaguzi uliendesha uchaguzi huo kwa uwazi.

RAIS KIKWETE AIFARIJI FAMILIA YA MAREHMU ADOLAR MAPUNDA Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo wakati alipokwenda kutoa pole nyumbani kwa Mkurugenzi Mkuu mstaafu wa  TTCL Marehemu Adolar Mapunda huko Tegeta, Dar es salaam jana Machi 29, 2013. Marehemu Mapunda, ambaye pia alipata kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Tanzania Standard Newspapers na Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo wakati alipokwenda kutoa pole nyumbani kwa Mkurugenzi Mkuu mstaafu wa  TTCL Marehemu Adolar Mapunda huko Tegeta, Dar es salaam jana Machi 29, 2013. Marehemu Mapunda, ambaye pia alipata kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Tanzania Standard Newspapers na Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji mjane wa  marehemu Adolar Mapunda huko Tegeta, Dar es salaam jana Machi 29, 2013. Marehemu Mapunda, ambaye pia alipata kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Tanzania Standard Newspapers na Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, alifariki usiku wa kuamkia jana.

 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiifariji familia ya marehemu Adolar Mapunda huko Tegeta, Dar es salaam jana Machi 29, 2013. Marehemu Mapunda, ambaye pia alipata kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Tanzania Standard Newspapers na Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, alifariki usiku wa kuamkia jana.

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na mtoto wa  marehemu Adolar Mapunda huko Tegeta, Dar es salaam jana Machi 29, 2013. Marehemu Mapunda, ambaye pia alipata kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Tanzania Standard Newspapers na Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, alifariki usiku wa kuamkia jana.

 Waziri wa Uchukuzi Dkt Harrison Mwakyembe akiweka saini katika kitabu cha maombolezo wakati alipokwenda kutoa pole nyumbani kwa Mkurugenzi Mkuu mstaafu wa  TTCL Marehemu Adolar Mapunda huko Tegeta, Dar es salaam jana Machi 29, 2013. Marehemu Mapunda, ambaye pia alipata kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Tanzania Standard Newspapers na Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

 Picha ya Marehemu Adolar Barnabas Mapunda
PICHA NA IKULU

HERI YA PASAKA KWA WADAU WOTE WA MTANDAO HUU

mtandao huu unaungana na wakristo wote katka kila kona ya dunia kukutakia heri na baraka ya pasaka....kriso kafufuka tufurahi haleluya
heri ya pasaka wadau

KWA HUDUMA YA KISASA YA UCHIMBAJI WA VISIMA VIREFU NCHINI TANZANIA

BUSIGER DRILLING COMPANY   ni  jibu lako  sasa  kwa  huduma ya uchimbaji  visiwa nchini Tanzania
 Iwapo  wewe ni taasisi ,kampuni ama mtu  binafsi wahitaji kumiliki  kisima cha maji cha kisasa kwa  gharama nafuu  zaidi ,usipate  shida  sasa
 Ni  wachimbaji maarufu  wa visiwa vya  kisasa kwa  gharama nafuu  zaidi
Wasiliana nasi kwa namba 0774100 100 tutakufikia  popote  ulipo ndani ya Tanzania

March 30, 2013

BREAKING NEWSSSS MAHAKAMA KENYA YATUPILIA MBALI PINGAMIZI LA ONDINGA YAMPA USHINDI KENYETTAMAHAKAMA ya Juu Kabisa nchini Kenya imeamua leo kuwa Uhuru Kenyatta alichaguliwa kwa haki kuwa Rais wa nne wa nchi hiyo, na kutupilia mbali pingamizi lililowekwa na mgombea Raila Odinga aliyedai kwamba kura zilichakachuliwa na mashine za uchaguzi zilijaa kwikwi.
Uamuzi huo umesafisha njia kwa Uhuru Kenyatta kuingia Ikulu. Anatarajiw kuapishwa wiki ijayo kwenye Machi 9, 2013 hivi.
“Ni uamuzi wa mahakama hii kwamba walalamikiwa wa tatu na wa nee walichaguliwa kwa haki”, alisema Jaji Mkuu wa Kenya Willy Mutunga, akimaanisha Kenyatta na mgombea mwena na Naibu Rais William Ruto wameshinda kihalali.

Jaji Mkuu huyo alisema mahakama imetekeleza wajibu wake katika muda huo wa kihistoria. “Sasa ni juu ya Wakenya, viongozi wao, taasisi za kijamii, sekta binafsi na vyombo vya habari kutekeleza wajibu wao kuhakikisha umoja, amani, utaifa na maendeleo ya taifa vinahifadhiwa”, aliongezea.
Rais mteule wa Kenya huyo alimshinda mpinzani wake kwa asilimia 50.07 dhidi ya asilimia 43,28 za Odinga.


MATUKIO HAYA KWA  UDHAMINI MKUBWA WA   HOPE SERVICE STATIONAL WALIOPO IRINGA MJINI ENEO LA CRDB NA GAPCO ENEO LA MSHINDO
 
 Ni  kituo  bora cha mafuta mkoa mzima  wa Iringa na mikoa ya nyanda za juu  kusini ,karibu Iringa mjini karibu kujaza mafuta katika kituo cha HOPE SERVICE STATIONAL kilichopo eneo la CRDB na kituo pacha cha GAPCO MSHINDO
 
 Tupo kiukombozi  zaidi fika  ukombolewe  hapa kwa mafuta  yenye ubora
 


March 29, 2013

CHONDE CHONDE ULEVI !!!? NOMAAAAAAAA!!!


 Meneja wa Club ya V.I.P mjini Iringa Mick akiwa  amezima baada ya kunya viroba na kisichana kwa  kuonyesha uwezo  wake na baada ya dakika 20 akazima kama hivi ,hapa nalazimika  kukumbuka ule ujumbe wa  chonde chonde! ulevi Nomaaaaaaaaaa!?
 Hii ni karibu Pasaka kweheri ijumaa kuu
 Mlinzi  wa eneo la TFA akijaribu kumsaidia baada ya polisi kufika na kuamua kumwacha kutokana na ugonjwa wake wa pombe kutokuwa na daktari wa kutibu
 
 Wasamaria  wema   wakimtazama meneja huyo chapombe akiwa amezima
 Hapa idadi ya walinzi  ikiendelea  kuongezeka eneo la tukio mjini Iringa usiku huu
Ukisema ulevi noma wapo watakaosema ulevi ni sehemu ya kupoteza mawazo ila kwa tukio hilo kila mmoja anaweza ungana nami kuwa kweli ulevi noma hapa ni eneo na TFA mjini Iringa ambapo hadi sasa meneja  huyu wa Club ya V.I.P akiwa amezima kwa kunywa pombe kupita  kiasi

RAIS JAKAYA KIKWETE, MAKAMU WAKE DKT. BILAL, WAZIRI MKUU, MIZENGO PINDA WASHIRIKI KUAGA MWILI WA ALIYEKUWA MBUNGE WA CUF DAR LEO


Rais Jakaya Kikwete, akiweka saini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chambani CUF, Salim Hemed Khamis, aliyefariki dunia jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa baada ya kuuguaa ghafla wakati akiwa katika Kikao cha Kamati ya Bunge cha Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika Ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam juzi. Marehemu mefariki kwa ugonjwa wa shinikizo la damu.
Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Waziri Mstaafu, Edward Lowasa, na viongozi wengine wakishiriki shughuli ya kuaga mwili wa marehemu Salim Hemed Khamis, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chambani Visiwani Pemba kupitia CUF, aliyefariki jana mchana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Shughuli za kuaga mwili wa marehemu zimefanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, leo Machi 29, 2013. 
Katibu wa Bunge la Jamhuri, John Joel, akisalimiana na Samuel Sitta, katika Ukumbi wa Karimjee wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu Salim Hemed Khamis, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chambani Visiwani Pemba kupitia CUF, aliyefariki jana mchana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Shughuli za kuaga mwili wa marehemu zimefanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, leo Machi 29, 2013.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya ndugu wa marehemu wakati viongozi wakiondoka kwenye ukumbi wa Karimjee baada ya kushiriki katika shughuli za kuaga mwili wa marehemu, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chambani Visiwani Pemba, Salim Hemed Khamis (CUF), aliyefariki jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, na Naibu Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Adam Malima, wakizungumza nje ya ukumbi wa Karimjee, baada ya kushiriki shughuli ya kuaga mwili wa marehemu,Salim Hemed Khamis, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chambani Visiwani Pemba kupitia Chama cha CUF, aliyefariki jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Waombolezaji wakibeba jeneza lenye mwili wa marehemu,Salim Hemed Khamis, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chambani Visiwani Pemba kupitia Chama cha CUF, aliyefariki jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, wakiingiza kwenye gari tayari kuelekea uwanja wa ndege kwa safari ya kuelekea Pemba kwa maziko, yatakayofanyika leo. Picha na OMR.

MUNGA AWATAKA WANASIASA KUACHA KUAMUA BILA KUSIKILIZA WATAALAM KUHUSU ELIMU

 
  Bw Joseph J. Mungai  akifafanua jambo  wakati  alipowasilisha  barua  yake  ya  wazi  kwa  tume  ya elimu ya kufeli kwa asilimia 60 kwa wanafunzi wa kidato cha nne  mwaka jana 
...............................................................................................
 
ALIYEKUWA waziri  wa  elimu na mbunge mstaafu  wa  jimbo la Mufindi Kaskazin Joseph Mungai  awaonya  wanasiasa  kuacha  kuamua bila  kuzingatia ipasavyo utafiti na ushauri wa kitaaluma kuhusu Elimu ya Taifa letu.

Mungai aliyasema hayo leo  wakati akiwasilisha barua  yake ya wazi  kwa tume ya elimu  ya kufeli kwa asilimia 60 mtihani wa kidato cha nne mwaka 2012 iliyoundwa na  waziri mkuu Mizengo Pinda .

Alisema  kuwa ili  kukuza  kiwango cha elimu nchini ni  vema  wanasiasa  wakaachana kabisa na utaratibu  wa  kuingilia na kutoa ushauri wao katika elimu bila kuwasikiliza wataalam kwani  kwa kufanya  hivyo kunachangia  elimu  kuyumba .

“Ninawapongeza kwa kuteuliwa na ahsante kutupa fursa wadau wa elimu kuwaletea maoni na  au/ushauri”

“Mimi ni mdau wa elimu, niliyewahi kuwa Mwenyekiti mwanzilishi wa Mufindi Education Trust (MET) iliyoanzisha katika wilaya ya Mufindi        na kuziendesha  kwa mika      zaidi    ya 10 Sekondari  9 za: (1) JJ Mungai (2) Sadani ( 3) Itengule  ( 4) Igowole ( 5) Itandula ( 6) Mgololo ( 7 ) Kibengu ( 8) Mdabulo na ( 9) Nyololo; ambazo sasa ni za serikali. Aidha nimewahi kuwa waziri wa Elimu na Utamaduni  mwaka 2000 hadi 2005”

Alisema  kuwa  Kufeli mwaka 2012 kidato cha Nne (KIV) kwa asilimia 60 halikuwa tukio lililoibuka ghafla bali waliofeli ( Division 0) mtihani huo waliongezeka kutoka mwaka 2007:9.7% ; 2008:16.3%; 2009:27.5%; 2010:49.6%; 2011:46.4% na sasa 2012:60%

Mungai  alisema  kuwa Kabla ya hapo waliofeli kidato cha Nne (KIV) WALIPUNGUA kutoak mawka 1998:24:3%:; 1999:20.0% 2000:21.6% 2001:22.6%, 2002:12.7%; 2003:12.2%, 2004:8.7%, 2005:10.7%, 2006:10.9%, na 2007:9.7% wastani wa kufeli 2004 hadi 2007 ni 10%.

Tazama hotuba ya bajeti ya Waziri wa Elimu na Utamaduni ya mwaka 2005/2006 kielelezo Na. 75.4 ukurasa wa 100; na BEST ( Basic Statics in Education, National Data) ya miaka  husika.

Wakati Kati ya 2004 na 2007 waliofeli kidato cha Nne  walikuwa wastani wa 10% ambayo   inavumilika. Kwa nini kati ya 2007 na 2008 kulikuwa na mruko kutoka 9.7% hadi 16.3%? Huo ukawa ndio mwanzo wa kuonge zeka  kila    mwaka    hadi kufikia 60%       ya mwaka huu!!!!! Wizara ya Elimu na OWM-TAMISEMI baada   ya  matokeo mabaya ya mwaka 2010 walifanya  “utafiti kudadisi sababu   za ufaulu huo mbaya” na taarifa yake ipo kwenye maktaba a Wizara” na iliandaliwa kauli ya waziri isomwe Bungeni”, lakini  hadi leo haikusomwa.   Ukweli ulifichwa; na mficha ugonjwa kifo kitamuumbua. Nukuu zangu kutoka Taarifa moja     isiyo   ya siri ya ndani    ya wizara ya Elimu.
 
“Kwa maoni yangu maboresho ya Elimu ya Serikali ya Awamu ya Tatu ambayo  yanaweza kusomwa katika maandiko   mawili    ya Wizara   ya Elimu     yaitwayo: (a) Nyaraka za Elimu 1999 hadi 2005, na ( b) Sheria ndogo za Elimu au kanuni za Elimu zilizotungwa kuyapa maboresho   hayo uzito w akisheria yamepelekwa NYARAKA ZA KALE (ACHIVES) kabla  ya wakati wake….Maboresho yamewekwa kando moja     baada ya jingine  au  hayakusimamiwa ipasavyo na Elimu yetu imerudi  ilivyokuwa kabla  ya mwaka 2000”
 
Kuhusu  ushauri  wake kwa elimu ya Tanzania  alisema  kuwa  Elimu ni nyenzo muhimu   sana kuliko zote katika kuboresha nguvu kazi ya Taifa na kuchochea  maendeleo  ya nchi ameamua kutonyamaza na kuwa muwazi kabisa, ingawaje mimi ni mwanasiasa  niliyestaafu. Kwa hiyo NASHAURI mambo yafuatayo:
 
Kwanza  kuwe na utaratibu  sahihi wa kupanda madarasa kwa ufaulu ( achievement based progression)  uliowekwa na waraka wa Elimu Na. 1& 2 wa 2002 urejeshwe na uimarishwe   bila  kuchelewa kuasnzia Darasa la kwanza,  la pili na la Tatu ambayo      Mwalimu Mkuu siku zote anayo madaraka    ya kukalilisha, kama mwanafunzi   hajazijua “K” 3: kusoma, kuandika na kuhesabu.
 
Alisema Mungia  kuwa jambo la  pili  ni tume ya Mhe. Waziri Mkuu ifanye kwanza REJEA ya maandiko ya Wizara ya Elimu  niliyoyataja akatika 4(a) na (b) hapo  juu yaliyomo maboresho ya         elimu ya 2002-2005 yaliyofanikisha kufaulu vizuri  katika   Elimu ya Msingi na Sekondari miaka       ya 2004-2007; badala ya kutumia muda mwingi na fedha nyingi kugundua upya gurudumu.
 
Wakati jambo la tatu alisema ni Taasisi  ya Elimu   Tanzania ( Tanzania  Institute of   Education –TIE) iagizwe na iachiwe  kutekeleza wajibu  wake wa kisheria chini ya Sheria ya Elimu ya 1995 wa kuandaa na kuboresha mitala.
Pia wanasiasa tuache kuamua bila  kuzingatia ipasavyo utafiti na ushauri wa kitaaluma kuhusu Elimu ya Taifa letu.
 
“Kutokana  na uamuzi mbaya na kuchelewa kuchukua  hatua ya marekebisho kila inapobidi; Elimu yetu imerudi ilikokuwa  kabla ya mwaka 2000. Rika zima la kielimu limepotea!!!sasa tunavuna kilichopandwa vibaya. Kwa hiyo TUJISAHIHISHE kwa kuacha kuingilia na kuamua bila kuzingatia  utafiti na ushauri fwa kitaaluma ili tusije kuumbuliwa tena na matokeo mabaya kama    hayo ya kidato cha Nne   ya mwaka 2012. Aidha inafaa matokeo ya mitihani    yawe yanatangazwa kwa uwazi hata kama ni mabaya kwa sababu, narudia “ anayeficha maradhi       kifo kitamuumbua”
MWISHO 
 MATUKIO HAYA KWA  UDHAMINI MKUBWA WA   HOPE SERVICE STATIONAL WALIOPO IRINGA MJINI ENEO LA CRDB NA GAPCO ENEO LA MSHINDO
 
 Ni  kituo  bora cha mafuta mkoa mzima  wa Iringa na mikoa ya nyanda za juu  kusini ,karibu Iringa mjini karibu kujaza mafuta katika kituo cha HOPE SERVICE STATIONAL kilichopo eneo la CRDB na kituo pacha cha GAPCO MSHINDO
 
 Tupo kiukombozi  zaidi fika  ukombolewe  hapa kwa mafuta  yenye ubora
 

HABARI KUTOKA MAKETE MKOANI NJOMBE LEO

 
 
 
 
mkuu wa shule ya msingi Ukwama wilayani Makete Ebayoti Amani Malila ametoa shukurani za dhati kwa kupokea mradi wa ujenzi wa vioo katika shule yake mradi huo umetorewa na  AMREF.
 
 Akizungumza na wanahari shuleni hapo katika wakati wa ukaguzi wa mradi huo bwana  Malila amesema amepokea kwa furaha kubwa  sana  kwani amewatoa  katika  hali mbaya ya kiafya  sasa wanaelekea  hali nzuri kiafya  ambapo huko nyuma walikuwa na vyoo ambavyo wanafunzi walikuwa wakijitegemea  kuchota maji ya kutumia katika  vyoo hivyo  lakini  wanashukuru  mradi huu ukikamilika .
 
akiendelea Malila amesema kuwa watoto watapata huduma nzuri ya choo kwani  maji yamejengewa ndani kwa ndani na watanawa maji yanayotiririka  kwenye Bomba hata hivyo aliongeza  mradi huu umejari  hata watoto  waremavu  na vilevile  uwapo  wa maji  chooni  tofauti na kuchota  na kwenda nayo chooni  na hali ya mlipuko wa magonjwa utapungua kutokana wanafunzi kula kinyesi kibichi kutokana nakushika vyombo vya chooni kwakukosa maji tiririka chooni.
Pia ameongeza kuwa idadi ya watoto na kubwa kuliko vyoo vilivyojengwa kwani vinahitajika nyoo 15 na vilivyojengwa Mashimo 9 hivyo upungufu mashimo 6 kwa vyoo bora vya kisasa tunategemea  kwamba kama  shirika la AMREF litawasaidia tena liwajengee matundu  6 watashukuru sana. PICHA

 kwaupande wake mwalimu WINFRIDA MALUNGU amesema mradi huu  umepokea  kwa mikono  miwili na umewakomboa  sana ,kutoka vyoo vya shimo na kwenda kisasa inasaidia  wanafunzi  kwenda  na wakati pia  kuwaepusha na magonjwa  mabilimbali  kama Vichocho, na Kuhara na  matumbo.

Nae  Mwanafunzi SAMSONI KENETJ SANGA amesema vyoo vya zamani  vilikuwa ni vya shimo  na havikuwezesha  walemavu  kupata huduma hiyo kiurahisi. Wanashukuru  AMREF  kwa msaada huo  na wanaahidi  kutunza vizuri


  akimalizia kushukuru mwenyekiti wa kijiji hicho bwana NEHEMIA SANGA anashukuru AMREF  na ushiriki wa wananchi  kwa kupokea  na kujenga  mradi  huo Shuleni hapo pia  ameongeza kuwa mradi huo utapunguza usumbufu  wa kila mwaka  kuchimba shimo  kwani kwa muda mfupi  yalikuwa yanatitia .
 
Hivyo  sasa  maendeleo yataongezeka  kwa kwakukombolewa /kujengewa  vyoo bora na AMREF.

 Mradi huo ambao unajengwa katika shule hiyo kwa lengo la kuwasaidia wanafunzi kupata huduma bora ya choo ili kukinga na magonjwa ya miripuko ambapo mradi huo unadhaminiwa na AMREF kwa kushirikiana na wana nchi kwani shirika hilo hutoa vifaa huku wananchi wakichangia katika nguvu

MAJERUHI WA GHOROFA DAR WAFIKIA 18 WANNE WAPOTEZA MAISHA

  Jitihada za kuwaokoa watu zikiendelea, huku nondo nyembamba zikionekana na kuacha maswali miongoni mwa mashuhuda wa tukio hilo.
  Jitihada za kuwaokoa watu zikiendelea.
 Jitihada za kuwaokoa watu zikiendelea.

Taarifa  zilizotufikia mchana  huu zinadai  kuwa  idadi ya majeruhi  wa ghorofa  lililoporomoka  jijini Dar es Salaam imefikia  18  wakati  watu  wanne  wanadaiwa  kupoteza maisha na jitihada za uokoaji  bado  zinaendelea . 

MATUKIO HAYA KWA  UDHAMINI MKUBWA WA   HOPE SERVICE STATIONAL WALIOPO IRINGA MJINI ENEO LA CRDB NA GAPCO ENEO LA MSHINDO
 
 Ni  kituo  bora cha mafuta mkoa mzima  wa Iringa na mikoa ya nyanda za juu  kusini ,karibu Iringa mjini karibu kujaza mafuta katika kituo cha HOPE SERVICE STATIONAL kilichopo eneo la CRDB na kituo pacha cha GAPCO MSHINDO
 
 Tupo kiukombozi  zaidi fika  ukombolewe  hapa kwa mafuta  yenye ubora
Tunasafirisha  mafuta kwa magari yetu na  wafanyakazi  wenye sifa ya utoaji  huduma
 
 
 
 Huu ni ukombozi kwa  wote  mkoani Iringa acha  kuuliza  kituo  cha mafuta  uliza HOPE SERVICE STATIONAL CRDB NA  GAPCO MSHINDO ndilo  jibu sahihi la  swali lako
 Wengi hufurahia  huduma  zetu kwani ni ukombozi  wa  wengi mjini Iringa
 Hapa kazi ni masaa 24 bila kulala na ubora  ule  ule  siku  zote