Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

February 28, 2013

MTOTO WA MWENYEKITI WA KIJIJI TANANGOZI IRINGA AJINYONGA KATIKA OFISI YA KIJIJI


Katika hali ya kusikitisha  mtoto wa  mwenyekiti wa serikali ya  kijiji cha Tanangozi katika wilaya ya  Iringa vijijini  Doto Kikoti ameamua kujinyonga katika ofisi ya kijiji  hicho inayoongozwa na babake mzazi kama njia ya kupinga kuwekwa kizuizini katika ofisi hiyo.

Tukio hilo  limetokea  usiku  wa kuamkia leo  baada ya kijana  huyo kutuhumiwa  kufanya  vurugu kubwa  katika kijiji  hicho na mzazi  wake  kuamua kumkamata na kumfungia katika  ofisi hiyo ya  kijiji kwa usalama  wake.

Wakizungumza na mtandao huu  wa  www.francisgodwin.blogspot.com mashuhuda wa  tukio  hilo  wamesema kuwa kijana  huyo alijinyonga kwa kutumia suluali  yake  akiwa ndani ya ofisi  hiyo baada ya mwenyekiti  wa kijiji  hicho ambae ni babake mzazi  Bw Narbeti Kikoti kumfungia katika ofisi hiyo.

Mwili  wa  kijana huyo umetolewa eneo la  ofisi hiyo majira ya saa 5 asubuhi  leo na kupelekwa nyumbani kwa  wazazi kwa ajili ya maandalizi ya mazishi.


MAPYA YAIBUKA SAKATA LA MTUHUMIWA WA MAUWAJI YA MWANGOSI , WAANDISHI WATIMULIWA


Hapa mtuhumiwa  huyo akikimbiziwa mahabusu ili kukwepa picha ya  wanahabari leo
Hapa akiingizwa mahakamani leo

                                        
Huyu ndie mtuhumiwa wa mauwaji ya Daudi Mwangosi

SAKATA la mtuhumiwa  wa   mauwaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha Chanel Ten mkoani Iringa marehemu Daudi Mwangosi askari  wa FFU mwenye namba G2573 Pasificus Cleophace Simoni (23),limeendelea  kuchukua  sura  mpya  baada ya wanahabari  kunusurika  kichapo  kutoka kwa askari  polisi ambao  walikuwa  wakiwazuia  kusogea katika  chumba  cha mahakama  kusikiliza  kesi  hiyo .

Askari  polisi hao  wakiwa  zaidi ya  10  waliweza kutumia nguvu  za  ziada katika kuwathibiti wanahabari  wa vyombo mbali mbali  waliofika  kusikiliza na kuripoti mwenendo wa kesi hiyo  namba  1 ya mwaka 2012  ya mauwaji ya mwanahabari mwenzao ,Mwangosi  aliyeuwawa septemba 2 mwaka 2012  katika kijiji cha Nyololo wilaya ya Mufindi wakati wa polisi walipokuwa  wakitumia nguvu  kuwatawanya wafuasi wa chama  cha  Demokrasia na maendeleo  (CHADEMA)  aliokuwa katika shughuli za ufunguzi  wa matawi ya chama  hicho.

Hata  hivyo  moja kati ya mbinu  waliyopata  kuitumia  leo  wakati mtuhumiwa huyo akifikishwa mahakamani hapo ni  kuwafukuza  waandishi  wa habari  eneo hilo la mahakama na kumtoa mtuhumiwa huyo kwa  kificho cha hali ya  juu kwa  kumweka katikati ya  watuhumiwa  wa makosa mingine zaidi ya 8 huku mtuhumiwa akijificha sura  yake  kukwepa kamera za waandishi na baadhi ya askari  wakimkinga ili  kukwepa  kupigwa  picha.

Tukio  hilo  lilitokea muda wa saa 6.10 mchana  wakati mtuhumiwa  huyo askari  Saimoni alipokuwa akitolewa na  watuhumiwa  wengine  kutoka  chumba cha mahabusu ya mahakama  ya hakimu mkazi  mkoa  wa Iringa na kumpeleka katika  chumba cha mahakama ya wazi  kwa ajili ya  kesi hiyo  kutajwa tena.

Hivyo  katika hali ya  kushangaza ni pale askari  hao  kuwataka  wanahabari hao  kusongea  umbali  wa mita  710 kutoka  eneo la Mahakamani  hiyo  wakati mtuhumiwa   huyo akiingizwa katika  chumba  hicho  cha mahakama ya  wazi  mbele ya  hakimu mkazi  wa mahakama ya  mkoa  wa Iringa  Gladys Barthy  ili  kesi  hiyo  iweze  kutajwa  kwa zaidi ya mara  ya tano  sasa bila upelelezi  kukamilika.

Uamuzi  huo  wa askari  hao  kuwataka  wanahabari  hao  kusimama  umbali  wa mita 710 kutoka chumba  cha mahakama  ulionyesha kuwashangaza  hata  baadhi ya  wananchi  waliofika  kusikiliza  kesi na kuwawekea  dhamana  ndugu  zao  na kulazimika  kuungana na  wanahabari  kupinga  uamuzi  huo na kupelekea  askari  hao  kuwafukuza  pia  wananchi hao na kuwataka waungane na  wanahabari kuondoka eneo hilo la  chumba  cha mahakama.

Mbali ya  wanahabari hao  kunyanyasika  wakati mtuhumiwa  huyo akipelekwa  chumba  cha mahakama  kwa ajili ya  kesi hiyo kutajwa  bado  askari  hao  kabla ya  gari la mahabusu  (karandinga)  kufika na watuhumiwa eneo hilo la mahakama  mida ya saa 5.30 asubuhi  bado askari hao  walionyesha  kuwanyanyasa  wanahabari  hao na  mara kwa mara  kuwatawanya kwa kauli nzito za maneno kuwataka  kuondoka maeneo waliyokusanyika  kwa madai  hawapaswi  kusikiliza  kesi hiyo kwani  haipo  katika mahakama ya wazi jambo ambalo  halikuwa  la kweli.

Wakizungumza  juu ya uamuzi  huo  wa askari hao  kutumia  nguvu  za ziada katika kuwathibiti  wanahabari hao  baadhi ya  wananchi  walisema  kuwa  kinachofanywa na jeshi la  polisi mkoani Iringa ni kuzidisha jazba  zaidi kwa  wananchi na kuwa  hawakupaswa  kuwazuia  wanahabari  kutimiza  wajibu  wao.

Alisema Wistone kalinga  kuwa  hata  wao  wananchi  wanashindwa kujua  sababu ya  polisi  kumficha  mtuhumiwa  huyo wakati tayari amefikishwa mahakamani na  kuwa kinachofanywa na polisi ni  kuzidi kulipaka matope  jeshi la polisi na kuondoa kabisa  dhana ya  polisi jamii na ulinzi shirikishi pia uhuru  wa vyombo  vya habari katika  kulitumikia Taifa na  wananchi  wake.

Sanjari na  wananchi hao kushangazwa na tukio  hilo la  polisi kuzuia  wanahabari  pia kwa upande  wake mahakama  hiyo ya hakimu mkazi  mkoa  wa mkoa  wa Iringa  mheshimiwa  Barthy alisema  kuwa  kitendo  kilichofanywa na polisi hao  kuwazuia  wanahabari  si maagizo ya mahakama na kuwa  wanahabari hao  walikuwa  huru  kuingia  kusikiliza  kesi hiyo na  kuhabarisha  umma kwani  hakukiwa na siri wala hakuna maagizo ya mahakama  ya kuwataka  polisi  kuwafukuza  wanahabari mahakamani hapo.

"Kwanza  nawapa pore  sana  kwa misukosuko mlioipata  ....ila  mimi nilikuwa ndani   ya  mahakamani  sikujua  kinachoendelea  huko nje  ya  mahakama ila  nawahakikishieni  kuwa  kesi  hii ilikuwa ikisikilizwa katika mahakama ya  wazi na mlikuwa  huru   kusikiliza " alisema hakimu  huyo akiakimhoji mmoja kati ya  viongozi  wa  polisi kuhusu polisi hao  kunyanyasa  wanahabari na kuwataka  kutorudia kufanya   hivyo  tena.

Mwendesha mashitaka  wa  serikali Blandina Manyanda  aliiomba mahakama  hiyo  kupanga tarehe nyingine ya  kutajwa kwa  kesi hiyo na kuwa  upelelezi  bado haujakamilika na mahakama  hiyo  kupanga tarehe  14 machi ambapo  kesi hiyo  itafikishwa mahakamani  hapo kwa ajili ya kutajwa.
HABARI HII KWA UDHAMINI MKUBWA WA KITUO  CHA MAFUTA CHA  HOPE SERVICE STATION IRINGA ,AIRTEL MTANDAO  BORA TANZANIA ,DUKA LA JEZI ORIJINO LA  CLASSIC JERSEYSMSHINDO IRINGA NA PLANET 2000 COMPUTERS&ELECTRONIC PAMOJA NA  FAMARI STORE IRINGA
 KARIBU  UJAZE MAFUTA KWENYE GARI YAKO HAPA HOPE SERVICE STATION TUPO JIRANI NA BENKI YA CRDB MIYOMBONI BARABARA YA IRINGA DODOMA ,
KWA JEZI NA VIFAA VYA MICHEZO KARIBU CLASSIC JERSEYS TUPO MSHINDO MJINI IRINGA AMA  WAWEZA PIGA SIMU 0756 422 491
 Airtel mtandao bora nchini Tanzania
 Huduma ya kutuma na kupokea  pesa kwa haraka  zaidi ni Airtel Money

ZAWADI ZA MASHINDANO YA MPINGA CUP ZATANGAZWA


Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani  SACP. Mohamed Mpinga akionyesha moja ya jezi zitakazotumika katika michuano  ya mpinga cup itakayoanza leo jijini Dar es saalam chini ya udhamini wa Airtel, Rotary club, Mr.Price, Home Shopping Center  pamoja na Baraza la Taifa la Usalama Barabarani

Kiongozi mkuu  maandalizi ya Mashindano ya Mpinga Cup ametangaza zawadi mbalimbali zitakazotolewa kwa timu zitakazoshiriki katika michuano ya Mpinga Cup inayoshirikisha waendesha pikipiki maarufu kama bodabado wa jijini dar esa saalam yanayotegemea kufanyika leo katika viwanja vya Oysterbay police kwa muda wa wiki moja.
Akitangaza zawadi hizo ASP Emilian Kamwanda ambaye ni msaidizi Mwandamizi wa polisi na Kiongozi wa maandalizi ya michuano ya mpinga cup alisema” leo tunayo furaha kutangaza zawadi mbalimbali za washindi katika mashindano hayo ambayo yana lengo la kutoa elimu ya usalama barabarani kwa waendesha pikiki (bodaboda). Na zawadi hizi ziko kama ifuatavyo
Mshindi wa kwanza atapata Kombe, Pesa taslimu shilingi million moja, jezi  set moja, kofia ngumu (helmet) 15 pamoja na mpira 1, mshindi wa pili atapata pesa taslimu shilingi laki tano, jezi seti moja , kofia ngumu (helmet) 15 pamoja na mpira 1 na mshindi wa tatu atapata  pesa taslimu shilingi laki tatu, , kofia ngumu (helmet) 15 pamoja na mpira 1,

Aidha zawadi zitatolewa kwa Mchezaji bora na Goalkeeper bora ambapo  kila mmoja atapata  pesa taslimu shilingi laki moja,  vocha za kufanya manunuzi Mr Price zenye thamani ya Laki moja na kofia ngumu (helmet) 1
Timu tano zitakazoshindwa pia hazitaondoka hivihivi , zitazawadiwa kila moja mipra na kofia ngumu Helmet.
Mashindano ya Mpinga Cup yameandaliwa na Jeshi la polisi kupitia Kikosi cha Usalama Barabarani na kudhaminiwa na Airtel, Rotary club, Mr.Price, Home Shopping Center  pamoja na Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, ili kutoa elimu kwa waendesha pikipiki juu ya sheria mbalimbali za usalama , kuimarisha uelewa wao wa matumizi ya barabara kwa lengo la kuendelea kudhibiti  ajali za barabarani pamoja na elimu ya Polisi jamii. 
Mashindano haya yanatarajiwa kutimua mbio kuanzia tarehe leo katika viwanja vya Polisi Oysterbey   kwa kushirikisha timu 8 za waendesha pikipiki. Mpinga Cup itaendelea katika mikoa ya Kipolisi ya Ilala na Temeke na hatimaye kutafuta mshindi wa mkoa wa Dsm.


Mpinga Cup Prize announcement
The chairperson of Mpinga Cup preparation committee has announced various prizes for winners of Mpinga cup competition that will involve Bodaboda drivers in Dar es salaam  scheduled to take place  today at the Oysterbay police grounds for a week .
 
Announcing the prizes the assistant senior police and the chairperson of the Mpinga cup preparation committee ASP Emilian Kamwanda said "today we have the pleasure to announce various prizes for the winners in this contest which aimed at providing education on road safety for motorcycle drivers. We have prizes of different categories as follows
The First winner will receive a Cup,  cash prize of one million shillings,  one set of jerseys,15 helmet  and one ball,  the second winner  will receive cash prize of five  hundred thousand shillings,  set of jerseys,15 helmet  and one ball,   and the third winner to receive  cash prize of three hundred thousand shillings , 15 helmet  and one ball,
Furthermore there will be prizes for the best player and best goalkeeper each will be rewarded cash prize of one hundred thousands, shopping voucher for Mr. Price worth one hundred thousand and one helmet 
Five looser teams will also rewarded each team balls and helmet
Mpinga Cup competition organized by the Police Force through the Road Safety Task Force and sponsored by Airtel, Rotary club, Mr. Price, Home Shopping Center and the National Road Safety Council, aim to provide education for motorcycle operators on various safety rules strengthen their understanding of the use of the road in order to keep control / reduce  road accidents

This tournament is expected to kick off today at the Oysterbay police grounds involving eight teams of motorcycle operators in Kinondoni Region. Mpinga cup will continue in Ilala and Temeke regions and eventually finding the winner of Dar es Saalam Region.
 

HUU NI UNYAMA WA POLISI MAKETE WAUA MWALIMU KWA RISASI KISA HAKUVAA HELMENT YA PIKIPIKI

-->


Mwili  wa  mwalimu aliyeuwawa  kwa  kupigwa  risasi na  polisi Makete  kisa kutovaa Helment (kofia ya  pikipiki),tunaomba  radhi kwa  picha  hizi
  Hivi  ndivyo mwalimu  wa  sekondari ya Kitulo  Casto Sote Kawamba alivyouwawa na  polisi
Tunaomba Ladhi kwa picha za kutisha na endelea kutembelea mtandao huu kwa habari zaidi(Tunaomba Radhi kwa picha za kutisha na endelea)

............................................................................................................................................................

Mwalimu mmoja wa shule ya sekondari kitulo wilayani makete aliyefahamika kwa jina la casto sote kawamba ameuawa kwa kupigwa risasi na askari wa jeshi la polisi Makete

Akizungumza na  mtandao  huu  wa www.francisgodwin.blogspot.com  mkuu wa polisi wilaya ya Makete SP Peter Kaiza kuhusu tukio hilo lililotokea eneo la benki ya NMB tawi la Makete jana majira ya saa moja na robo alisema  kuwa mwalimu huyo alikuwa anakwenda kupata huduma za kibenki kupitia mashine ya  kutolea  pesa ya ATM akiwa na pikipiki ndipo alipo amuliwa na askari mmoja aitwae Jose Msukuma  na  kukutwa na umauti  huo .

 Inadaiwa  kuwa kisa cha mauwaji yake ni madai kutovaa kofia hiyo na baada ya  kuitwa na askari hao alikaidi amri na kutaka kumgonga askari huyo aliye kuwa lindo.

Nae mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Makete Idd Nganya ambaye ndie mwajiri wa marehemu amesema kuwa mwili wa marehemu bado umehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya makete wakati utaratibu wakusafirisha mwili huo kwenda kwao mbeya kwa ajili ya mazishi ukiendelea

Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo ambaye jina lake limehifadhiwa amesema kuwa askari hao walikuwa wakiomba fedha kwa mwalimu huyo na baada ya kukataliwa ndipo walipo anza kumshushia kichapo na alipo wazidi walilazimka kutumi asilaha na kumpiga begani kwa risasi  

Walimu wenzake na marehemu ambao walifika hospitali kujua kuhusina na kifo cha mwalimu mwenzake wameeleza  kusikitishwa na tukio hilo  na kulifananisha na tukio la kikatili machoni pao 

Mganga mkuu mfawidhi ambaye ni msemaji wa hospitali ya wilaya ya makete Dr Michael Gulaka amesema kuwa wao walipokea mwili wa marehemu na sio majeruhi
HABARI HII KWA UDHAMINI MKUBWA WA KITUO  CHA MAFUTA CHA  HOPE SERVICE STATION IRINGA ,AIRTEL MTANDAO  BORA TANZANIA ,DUKA LA JEZI ORIJINO LA  CLASSIC JERSEYSMSHINDO IRINGA NA PLANET 2000 COMPUTERS&ELECTRONIC PAMOJA NA  FAMARI STORE IRINGA
 KARIBU  UJAZE MAFUTA KWENYE GARI YAKO HAPA HOPE SERVICE STATION TUPO JIRANI NA BENKI YA CRDB MIYOMBONI BARABARA YA IRINGA DODOMA ,
KWA JEZI NA VIFAA VYA MICHEZO KARIBU CLASSIC JERSEYS TUPO MSHINDO MJINI IRINGA AMA  WAWEZA PIGA SIMU 0756 422 491
 Airtel mtandao bora nchini Tanzania

WAZIRI MKUU AZINDUA MPANGO MKAKATI WA GS1 TANZANIA

 

 Waziri Mkuu Mizengo Pinda Picha akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mpango mkakati wa GS1 Tanzania.
 Waziri Mkuu akionyesha kitabu cha mpango mkakati
Bodi ya GS1 Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja ( Picha zote na Adam H. Mzee)

WACHEZAJI WA TIMU YA MIGOLI ZAIDI YA 10 WAPATA AJALI

Wachezaji wa timu ya Migoli Fc  Jerry John kulia na Godfrey Utenga kushoto wakiwa katika Hospitali rufaa ya mkoa wa Iringa baada ya kupata ajali ya gari wakitoka katika mchezo wa mpira wa miguu dhidi ya Home Town ya Mtera ajali iliyotokea jana jioni eneo la Migori mpakani mwa Iringa na Dodoma.(picha na Denis Mlowe)

LINDI WAPINGA MILA ZILIZOPITWA NA WAKATI


 Wadau mbalimbali waliohudhuria mdahalo wa Jinsia na Maendeleo
uliofanyika wilani Kilwa
 Na Abdulaziz,Lindi

Imeelezwa kuwa Baadhi ya mila na desturi  zilizopitwa  na wakati
ambazo zinaendelezwa hivi sasa zinachangia kwa kiasi kikubwa tabia ya unyanyasaji  wa kijinsia ikiwemo ya ushirikishwaji  watoto wa kike kwenye vikao vya kifamiliavinavyojadili ndoa na Talaka ikiwa pamoja na kuchangia maamuzi

Pamoja na kila jamii kuzingatia ,kulinda na kudumisha mila na desturi
zake  lakini kuna haja ya kuzichambua  upya ili kuzipata zile nzuri
zinazofaa kwa  na kuhakikisha zile zinazokandamiza wanawake
zinatokomezwa.

Hayo yameelezwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Mji Mdogo wa
Masoko wilayani Kilwa,Bw Peter Amos Malekela alipokuwa akifunga na
kufungua katika Midahalo miwili iliyofanywa katika Jimbo la Kilwa
kusini na Kilwa kaskazini iliyoendeshwa na Mtandao Mwavuli wa Asasi
zisizo za Kiserikali Wilayani Kilwa (Kingonet)

Malekela aliwataka wanawake kuachana na mila hizo kandamizi na badala
yake wajitokeze kufanyakazi  za maendeleo ikiwemo kugombea nafasi mbalimbali masuala ya siasa ili wawe miongoni

mwa viongozi wa kufanya maamuzi  mbalimbali katika maeneo yao.
“Mafanikio yoyote  mwanamke  ndiye anastaili  kupongezwa kutokana na
jukumu alilonalo katika familia, hivyo ni vyema taasisi za  mbalimbali
na wadau wa maendeleo  na wana siasa wakawaonyesha wanawake njia za
kuleta mbadiliko katika familia na taifa kwa ujumla’.Alimalizia
Malekela

Awali akitoa maelezo mafupi ya Mdahalo huo,Katibu Mtendaji wa
Kingonet,Omary Mkuwili alieleza kuwa Asasi yake ipo kwa ajili ya kutoa
elimu mbalimbali kupitia midahalo kwa Lengo la kufikisha elimu na
kupokea Mawazo mbalimbali kwa wasiopewa nafasi kusikika  ili kuchangia
maendeleo ya Kilwa na Mkoa wa Lindi

Aidha aliwaasa Washiriki wa Mdahalo huo kuachana na Imani zilizo
potofu za kujenga akilini kuwa Mwanamke akifanikiwa katika maisha
wanadhani  yupo mwanaume nyuma yake  amemwezesha mafanikio hayo lakini
hapana wapo wanawake mwenye uwezo wa kiakili, mali na utendaji kuliko
wanaume huku akibainisha kwa kiasi kikubwa  ndio viongozi  na washauri
wakuu kujenga utamaduni na kusisitiza  kusaidia na kuchangia shughuli
za  kuwajengea uwezo wanawake  ili kuharakisha maendeleo.

Midahalo Hiyo miwili iliyofanyika katika Kata ya Chumo na Kilwa Masoko
ikiwa na lengo la kujadili suala la jinsia inavyochangia maendeleo na
kuendeshwa na  mtandao wa mashirika yasiyo kuwa yakiserikali wilaya
Kilwa(KINGONET) kwa ufadhili wa The foundation for the civil Society

KUMEKUCHA SIMBA HIKI NDICHO KIKOSI KAMILI KITAKACHOKWENDA ANGOLA

KIKOSI kamili cha Simba kinaondoka jijini Dar es Salaam kesho kikiwa na msafara wa watu 18, wakiwamo wachezaji 18 na viongozi saba.
 
Wachezaji wanaoondoka ni Juma Kaseja, Abel Dhaira, Nassor Said Masoud, Amir Maftah, Koman Bili Keita, Juma Nyoso, Shomari Kapombe, Salim Kinje, Ramadhani Chomboh, Amri Kiemba, Haruna Moshi, Kiggi Makasi, Abdallah Seseme, Amri Kiemba, Haruni Chanongo, Mrisho Ngassa, Felix Sunzu na Abdallah Juma.
 
Viongozi ni Zacharia Hans Poppe, Muhsin Balhabou, Patrick Liewig, Jamhuri Kihwelo, Dk. Cosmas Kapinga, James Kisaka na Kessy Rajab.
 
Simba inaondoka kwa ndege ya Shirika la Ndege la Kenya (Kenya Airways) majira ya saa 11:10 alfajiri na inatarajiwa kufika Luanda, Angola majira ya saa nne asubuhi.
 
Timu itafanya mazoezi ya mwisho jijini Dar es Salaam leo jioni kabla ya kuelekea kambini ambapo wachezaji watapumzika kusubiri muda wa safari.
 
Mechi kati ya Simba na Libolo itachezwa Machi 3 (Jumapili ijayo) katika Uwanja wa Calulo uliopo katika mji wa Calulo jimbo la Kwanza Sul (Kwanza Kusini).
 
Imetolewa na
Ezekiel Kamwaga
Ofisa Habari
Simba SC

BREAKING NEWSSss...POLISI MAKETE WAUA MTEJA WA BENKI KWA RISASI , MUUWAJI AKAMATWA

Askari  wa  FFU mkoani Iringa  wakimwadhibu kwa  kipigo aliyekuwa mwandishi wa Chanel Ten mkoa  wa Iringa marehemu Daudi Mwangosi (wa  pili kushoto) kabla ya  kuuwawa kwa bomu septemba 2 mwaka 2012 katika  kijiji  cha Nyololo Mufindi.(picha na maktaba ya mtandao huu)  
.....................................................................................................................................................................
WAKATI  mtuhumiwa  wa  mauwaji ya aliyekuwa mwandishi  wa kituo cha runinga cha Chanel Ten mkoani Iringa  Daudi Mwangosi Daudi Mwangos, askari wa FFU mwenye namba G2573 Pasificus Cleophace Simoni (23) akitarajiwa kufikishwa tena mahakamani  leo kwa kesi hiyo kutajwa ,askari  wilaya ya Makete  mkoa wa Njombe  wadaiwa  kufanya mauwaji ya  kinyama kwa kumpiga mteja wa benki ya NMB kwa risasi .
Huku  askari  askari  mmoja nayetuhumiwa kufanya  unyama  huo aliyetambulika kwa  jina moja la Jose akishikiliwa na  jeshi  la  polisi kufuatia mauwaji hayo ya  kinyama.

Tukio  hilo  limekuja  huku  bado watanzania   hasa  wakazi  wa  mikoa  ya Iringa  na Njombe  wakiwa bado hawajasahau  mauwaji ya  kinyama  yaliyomkuta  mwanahabari Daudi Mwangosi  ambapo kesi hiyo  bado ikiendelea kutajwa na  wanahabari waliokuwepo eneo la tukio  siku ya mauwaji  wakisubiri  kuchukuliwa maelezo yao kama mashahidi  wa kesi hiyo pindi  itakapoanzwa kusikilizwa.

Mwandishi  wa  wetu  wa mtandao huu wa   www.francisgodwin.blogspot.com  kutoka  Makete  Njombe anaeleza  kuwa   tukio  hilo  wamedai kuwa  mauwaji hayo ya  kinyama  yametokea jana  jumatano majira ya saa 1.20 usiku baada ya mteja  huyo aliyekuwa na  usafiri  wa  boda  boda  kufika  eneo hilo la  benki kwa lengo la  kuchukua  fedha  .

Imedaiwa  kuwa  aliyepigwa  risasi anatambuliwa  kwa  jina la Casto  Kawambwa  mkazi  Mbalizi  mkoani Mbeya  na kuwa  baada ya  kupigwa  risasi alikimbizwa  katika  Hospitali ya  wilaya ya Makete  ambako inadaiwa kabla ya  kupatiwa matibabu amefariki  dunia  .

Kutokana na tukio hilo  jeshi la  polisi  liliwazuia  wanahabari  kutimiza  wajibu  wao kwa  kupiga  picha  wala kusogea eneo hilo la Hospitali na badala yake  kuweka  ulinzi mkali eneo hilo la Hospitali ili  kuzuia  wanahabari  kusogea  eneo hilo .

 Hata  hivyo  mmoja kati ya  askari ambae   jina lake halikufahamika mara  moja alisikika  akidai kuwa  chanzo cha mteja  huyo wa benki  kupigwa  risasi  alikuwa akihisiwa  kuwa ni jambazi na  hivyo  baada ya  kufika  eneo hilo  kwa usafiri  wake wa  piki  piki (boda boda )  walihisi kuwa amefika  kwa ajili ya  kufanya  vitendo vya uporaji katika  benki  hiyo na hivyo  askari katika hali ya  kujihamia aliamua  kumpiga  risasi .

Jitihada za  kumtafuta  kamanda  wa  polisi  wa  mkoa  wa Njombe  ili  kuzungumzia  undani  wa  tukio  hilo  linafanyika na mtandao huu .
 
 
HABARI HII KWA UDHAMINI MKUBWA WA KITUO  CHA MAFUTA CHA  HOPE SERVICE STATION IRINGA ,AIRTEL MTANDAO  BORA TANZANIA ,DUKA LA JEZI ORIJINO LA  CLASSIC JERSEYSMSHINDO IRINGA NA PLANET 2000 COMPUTERS&ELECTRONIC PAMOJA NA  FAMARI STORE IRINGA
 KARIBU  UJAZE MAFUTA KWENYE GARI YAKO HAPA HOPE SERVICE STATION TUPO JIRANI NA BENKI YA CRDB MIYOMBONI BARABARA YA IRINGA DODOMA ,
KWA JEZI NA VIFAA VYA MICHEZO KARIBU CLASSIC JERSEYS TUPO MSHINDO MJINI IRINGA AMA  WAWEZA PIGA SIMU 0756 422 491
 Airtel mtandao bora nchini Tanzania
 Huduma ya kutuma na kupokea  pesa kwa haraka  zaidi ni Airtel Money

February 27, 2013

RAIS KIKWETE ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA JKT JIJINI DAR ES SALAAM LEO

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea zawadi ya saa toka kwa  Mkuu  wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Raphael Muhuga huku  Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Vuai Shamsi Nahodha, Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange wakishuhudia. Saa hiyo imeandaliwa na makamanda wa JKT kumpongeza Rais Kikwete kwa kurejesha mafunzo ya jeshi la ulinzi kwa mujibu wa sheria kuanzia mwaka huu.

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na kada mbalimbali za Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) alipotembelea leo February 27, 2013PICHA NA IKULU
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa juu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) jijini Dar es salaam alipotembelea leo February 27, 2013. Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Vuai Shamsi Nahodha, Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange pia wapo.
HABARI HII KWA UDHAMINI MKUBWA WA KITUO  CHA MAFUTA CHA  HOPE SERVICE STATION IRINGA ,AIRTEL MTANDAO  BORA TANZANIA ,DUKA LA JEZI ORIJINO LA  CLASSIC JERSEYSMSHINDO IRINGA NA PLANET 2000 COMPUTERS&ELECTRONIC PAMOJA NA  FAMARI STORE IRINGA
 KARIBU  UJAZE MAFUTA KWENYE GARI YAKO HAPA HOPE SERVICE STATION TUPO JIRANI NA BENKI YA CRDB MIYOMBONI BARABARA YA IRINGA DODOMA ,
KWA JEZI NA VIFAA VYA MICHEZO KARIBU CLASSIC JERSEYS TUPO MSHINDO MJINI IRINGA AMA  WAWEZA PIGA SIMU 0756 422 491
 Airtel mtandao bora nchini Tanzania
 Huduma ya kutuma na kupokea  pesa kwa haraka  zaidi ni Airtel Money
 
 wengi  hufurahia  huduma  hii ya airtel Money kwani  n i rahisi  zaidi na haina usumbufu
Airtel mtandao bora nchini Tanzania

BUNGE LA TANZANIA KUSHIRIKIANA KWA KARIBU NA BUNGE LA NAMIBIA

aSpika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne S. Makinda (kushot)  akimkaribisha Balozi wa Jamhuri ya Namibia nchini Tanzania Balozi Japhet Issack alipomtembelea ofisini kwake leo.Pamoja na mambo mengine Balozi huyo amemuomba Spika Makinda kuimarisha uhusiano  na Bunge la Namibia kwani kuna mambo mengi Bunge hilo linaweza kujifunza kutoka Tanzania.
b Spika Makinda akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na Balozi wa Namibia nchini Tanzania ambapo amemhakikishia Balozi huyo kuwa Bunge la Tanzania lipo tayari kushirikiana na Bunge la Namibia na kuona ni maeneo yapi ambayo yatawafaidisha wananchi wa  nchi mbili hizi. Aliainisha maeneo ya mafunzo na kujenga uwezo kuwa ya kipaumbele.
Na Prosper Minja-Bunge.