Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

January 31, 2013

PICHA PENDWA KWA LEO HII HAPA

  
 
 
Askari Polisi wakimbeba Mlemavu kumtoa nje baada ya mlemavu huyo kuonekana akikimbia huku akiwa hana nguo alipokuwa akijaribu kuingia katikati ya uwanja, alipoulizwa mlemavu huyo alisema kuwa alikuwa akielekea kumpongeza Mbuyu Twite, baada ya kuachia shuti kali lililomkuna vilivyo na kutinga wavuni hivi karibuni (picha na amanimtanzaniablog)

WILAYA YA KILWA LINDI, WAANZA KUNUFAIKA NA GESI ASILIA


Mkuu wa wilaya ya Kilwa Abdallah Ulega akishuhudia utiaji wa sahihi
wa mkataba huo wa miaka mitatu
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa,Addo Mapunda
akitiliana saini na  Bi Anne Devilliers,Mratibu wa Mradi wa mpango wa
ufundishwaji wa Lugha ya Kingereza kwa njia ya teknorojia ya kisasa
(Techonoroji Enhanced Edcation) TEE-TZ chini ya ufadhili wa kampuni ya
Pan African Energy,inayojishughulisha na kazi ya uchimbaji,usambazaji
na uuzaji wa gesi asilia ya Songosongo
Na  Abdulaziz Video mwandishi  wa www.francisgodwin,blogspot.com ,Lindi

WANAFUNZI wapatao 1,580 wanaosoma Shule tisa za Sekondari,wilayani
Kilwa, mkoani Lindi,watanufaika na mpango wa ufundishwaji wa Lugha ya
Kingereza kwa njia ya teknolojia ya kisasa TEE-TZ chini ya ufadhili wa
kampuni ya Pan African Energy,inayojishughulisha na kazi ya
uchimbaji,usambazaji na uuzaji wa gesi asilia ya Songosongo.

Mradi huo wa miaka mitatu,utagharimu jumla ya Sh, ya
Sh,144,945,218/-zitakazotumika kujenga misingi bora ya Lugha ya
kingereza kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza kuanzia  mwaka 2013.
Hayo yameelezwa na mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo,
Adoh Mapunda,alipokuwa akitoa taarifa katika hafla fupi ya kutiliana
na saini ya utekelezaji wa mpango huo.

Mapunda alisema mpango huo,utakaochukuwa takribani muda wa kipindi cha
miaka mitatu,umeanza rasmi mwezi  huu kwa wanafunzi wapatao 1,580 wa
kidato cha kwanza kutoka Shule tisa za Sekondari zilizopo katika
wilaya hiyo.

Amezitaja Sekondari zitakazonufaika na mpango huo kuwa ni,Kilwa day
iliyopo mji mdogo wa masoko, Mtanga, Songosongo, Mbuyuni,
Kinjumbi,Miteja,Mingumbi,Kikanda na Sekondari ya wasichana ya Ilulu.

Mkurugenzi Mapunda alisema mafunzo hayo kwa kuanzia yatakuwa ni ya
wiki sita,yameanza rasmi hivi karibuni na kwamba walimu wapatao 30
wakiwemo (12) wa kigeni (Volunteers) wakiwemo na walimu wazawa (18).

“Hizi Shule tisa kila moja italazimika kutoa walimu wawili
watakaopatiwa mafunzo kwa ajili ya kuendesha mpango huu katika Shule
zote hizo”Alisema Mapunda.

Aidha, Mapunda alisema kupitia ufadhili wa mpango huo wa mafunzo ya
kingereza,Halmashauri ya wilaya itaendesha semina/warsha kutoa stadi
za kufundishia masomo hayo kwa Sekondari hizo tisa zenye walimu
wapatao (71).

Mapunda alisema mafunzo hayo ni nyongeza kwa walimu wote waliopo
katika Shule hizo tisa za mafunzo ya kingereza ya aina mbili,TEE-TZ
itakayoendeshwa kwa ufadhili wa ubalozi wa Marekani,(RELO-Regional
English Language Office kwa Sh,24,158,480/-.

Katika ufadhili wa mafunzo hayo ya TEE-TZ na RELO jumla ya
Sh,169,103,698/-ndizo zitakazotumika kwa ajili ya utekelezaji wake.

Mratibu wa mradi huo,kutoka kampuni hiyo ya Pan African Energy,Anne
Devilliers,amesema lengo la mpango huo ni,kutaka kuwawezesha wanafunzi
waelewe masomo yao kwa elimu ya Sekondari na kuongeza viwango vya
ufaulu katika mitihani yao ya kidato cha nne.

Devilliers akasema imebainika kwamba wapo wanafunzi waliowengi
wamekuwa hawafanyi vizuri katika masomo na mitihani yao,kutokana na
kutoielewa vyema Lugha ya Kingereza.

Mkuu wa wilaya hiyo ya Kilwa, Abdallah Ulega, ameipongeza kampuni ya
Pan African Energy,na akasema kwamba kwa kiasi furani itasaidia
kuboresha kiwango cha elimu ndani ya wilaya hiyo,mkoa na Taifa kwa
ujumla.

Mpango huo,ulianza kwa majaribio katika wilaya ya Mafia mkoani
Pwani,mwaka 2010 na 2011,baada ya kuona mafanikio yake,ndipo uongozi
wa wilaya ya Kilwa,ukaamua mpango huo kupelekwa ndani ya wilaya yao.
Mwisho.

ASKARI POLISI NA MTUHUMIWA WA MAUWAJI YA MWANGOSI WAKIMBIA CHUMBA CHA MAHAKAMA ,HAKIMU AGEUKA MBOGO .....

Hapa mtuhumiwa  huyo akikimbiziwa mahabusu ili kukwepa picha ya  wanahabari leo
Hapa akiingizwa mahakamani leo
                                                          wanahabari  wa  radio  nuru Fm wakifanya mawasiliano kujua mtuhumiwa  huyo kama amefikishwa mahakamani ama bado ,hii ilikuwa mida ya saa 4 asubuhi kabla ya mahakama hiyo kuanza

                                        
Huyu ndie mtuhumiwa wa mauwaji ya Daudi Mwangosi

SAKATA la mtuhumiwa wa mauwaji ya  aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha Chanel Ten mkoani Iringa marehemu Daudi Mwangosi limezidi kuchukua  sura  mpya baada ya askari waliomfikisha mtuhumiwa  huyo wa mauaji  askari  wa FFU mwenye namba G2573 Pasificus Cleophace Simoni (23) kumtibua hakimu na kuageza mtuhumiwa huyo kurudishwa tena kizimbani kwa kudharau mahakama hiyo.

Tukio  hilo lilitokea leo  majira ya saa5.35 kwa  askari  hao watatu ambao majina yao hayakuweza kufahamika mara moja  kumshusha  kizimbani mtuhumiwa  huyo wa mauwaji na kumkimbizia mahabusu kama njia ya kukwepa kupigwa picha na wanahabari  waliokuwepo hapo lilitokea mara baada ya mahakama hiyo kuombwa kutaja tarehe nyingine ya  kutajwa kesi hiyo.

Huku  bado mahakama ikiwa inaendelea kwa hakimu kutaja tarehe ya kesi hiyo namba  ya mauwaji kesi namba 1 ya mwaka 2012 mtuhumiwa wa mauwaji alishuka kizimbani  huku akivaa kofia yake ya sweta (mzula)na miwani ya giza na kuanza  kushuka jukwaani kabla ya hakimu kumtaka mtuhumiwa huyo kutovalia kofia hiyo kizimbani huku kabla ya mahakama  kumalizika.

Wakati hakimu  huyo akijiandaa kusimama ili kuhitimisha shughuli za kimahakama kwa siku  hiyo ghafla alijikuta anabaki na mwanasheria  wa mahakama ,kalani wake ,wanahabari ,askari mmoja na ndugu  wawili wa mtuhumiwa huyo  huku askari  watatu wenye silaha  na mtuhumiwa huyo  wakiwa tayari wameondoka ndani ya chumba cha mahakama hiyo.

“Mbona hao askari wanamtoa mtuhumiwa  bila utaratibu wa mahakama hebu  mwanasheria waambie wamrudishe ndani mtuhumiwa ....huu si utaratibu mbona  wanafanya fujo mahakamani  hao” alisikika akisemahakimu mkazi  wilaya ya Iringa Dyness Lyimo

Hata  hivyo pamoja na jitihada za mwanasheria   wa  serikali Adolf Maganda kuwaita  kwa  sauti  askari hao  kuwataka  kumrudisha  ndani ya mahakama mtuhumiwa huyo  bado askari  hao  walizidi kukimbia na mtuhumiwa kwenda nae mahabusu na baada ya dakika kama 5 hivi ndipo mwanasheria  huyo aliporejea na askari hao na mtuhumiwa ambae hata  hivyo hakwenda kusimama  kizimbani na badala  yake alikwenda upande wa  kushoto wa mahakama  hiyo ambako alikuwa amekaa mwanzoni kabla ya mahakama  kuanza na kuketi katika  kiti huku akiwa amevaa miwani na kofia  yake.

Kutoka na  tukio  hilo hakimu  huyo alilazimika  kuwahoji askari hao  watatu kwa vurugu  hizo  walizozifanya kwa kuwauliza swali moja  pekee  kuwa  wanaona walichofanya ni  sahihi na askari hao kuomba msahama  kuwa samahani mheshimiwa.

Mwendesha mashtaka  wa jamhuri Adolf Maganda aliiomba mahakama hiyo kutaja tarehe nyingine ya kutajwa tena  kesi hiyo ambayo ilitajwa Januari 27 na mtuhumiwa huyo kushindwa kufika kutokana na tatizo la ugonjwa  lililokuwa likimsumbua .


Hata  hivyo mahakamani  hiyo  liahirisha  kesi hiyo  hadi  Februari 14 mwaka huu kesi hiyo itakapofikishwa mahakani hapo kwa  kutajwa tena.

Mtuhumiwa  huyo anatuhumiwa  kumuua kwa    bomu aliyekuwa  mwandishi  wa habari wa Chanel Tena  mkoa  wa Iringa  marehemu Mwangosi  septemba 2 Septemba mwaka jana  katika kijiji cha Nyololo Wilaya ya Mufindi Mkoa wa Iringa  wakati  wa vurugu kati ya  polisi na wafuasi wa  Chadema .kinyume na kifungu cha sheria namba 148 kifungu kidogo 5A.i cha makosa ya jinai. Kwa mujibu wa kesi za jinai, sheria kifungu 196 kanuni ya adhabu Cap. 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002,
MWISHO

January 30, 2013

VIWANGO VYA KUKODI GREDA LA MANISPAA YA IRINGA VYATAJWA


Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa, Theresia Mahongo  
Na  Frank Leonard ,Iringa 
HALMASHAURI ya Manispaa ya Iringa imependekeza viwango viwili tofauti vitakavyotumika kukodi mtambo wake wa kuchonga barabara (greda).
Mtambo huo ulinunuliwa hivi karibuni kwa zaidi ya Sh Milioni 581 zilizokopwa kutoka benki ya CRDB. 
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, Theresia Mahongo alisema kwa wateja wa nje watakodi mtambo huo kwa Sh 800,000 kwa saa kumi.
“Na iwapo kata au mamlaka ya serikali itahitaji kulitumia gharama itakuwa Shilingi 250,00 kwa saa kumi,” alisema.
Pamoja na gharama hizo, Mahongo alisema wateja watalazimika pia kugharamia mafuta na dereva.
Aliyasema hayo kwenye kikao cha makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2013/2014 na mapitio ya bajeti ya mwaka 2011/2012 na Julai hadi Desemba, 2012.
Akiwasilisha mapendekezo ya mapato na matumizi ya halmashauri kwa mwaka 2013/2014, Mahongo alisema wanakadiria kukusanya zaidi ya Sh Bilioni 23.3 kutokana na vianzoa mbalimbali.
Alisema kati ya mapato hayo zaidi ya Sh Bilioni 20.2 ni ruzuku kutoka serikali kuu na Sh Bilioni 3.1 kutoka vyanzo vya halmashauri.
Wakati huo huo, kikao hicho kilipokea maoni yaliyotolewa na kamati mbalimbali za kudumu za halmashauri hiyo.
Baadhi ya maoni hayo ni pamoja na kuboresha masoko ya Kihesa na Mashine Tatu ili yasadie kuongeza mapato ya halmashauri.

HUYU NDIE MWANGOSI NILIYEMZOEA ,MUUWAJI WAKE KUPANDISHWA MAHAKAMANI KESHO

Marehemu Daudi Mwangosi akiwa na kamera ambayo alikuwa nayo kabla ya kulipuliwa kwa bomu ,hapa akiwa katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha Iringa kuhamasisha utalii wa ndani kwa wanahabari na watanzania
Daudi Mwangosi kulia akiwa na Mahija Zayumba kutoka Nuru Fm na katibu msaidizi wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) Francis Godwin ambaye pia ni shemeji yake ,hapa ni ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha wakati wa wanahabari Iringa walipotembelea hifadhi hiyo April 26 mwaka huu Kwa hisani ya Francis Godwin Blog
Daudi Mwangosi akiwa katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha hapa akitoka kuamka tayari kwa kwenda kutazama Tembo aliyekufa na kuwasaka Simba ,kiatu ,suruali na Laptop hiyo ndivyo alivyokuwa navyo hata siku ya kifo chake Nyololo
Daudi Mwangosi akiwa katika picha ya pamoja na Sima Bingileki siku aliposhinda uenyekiti wa IPC ,Sima alikuwa mpinzani wake katika nafasi hiyo
Daudi Mwangosi akiwa na Sima Bingileki na Oliver Motto siku wanachama wa IPC walivyofanya ziara Pemba
Daudi Mwangosi akiomba kura kwa wanachama wa IPC ili kuwa mwenyekiti wao
Daudi Mwangosi (kulia) akiwa na Rais wa umoja wa vilabu vya waandishi wa habari nchini Keneth Simbaya (katikati) na katibu mtendaji wa IPC Frank Leonard siku alipokwenda kushiriki sherehe ya mwanahabari Conrady Mpila wa kitulo FM kuoa ,harusi ambayo bado kufanyika na alipania kwenda kushiriki huko Makete Njombe
Hapa Daudi Mwangosi akitaniwa na mmoja kati ya wanahabari kutoka Kitulo Fm kunywa pombe aina ya Mbege ambayo aligoma kunywa kutokana na kutokuwa na kawaida ya kunywa pombe ya aina yoyote ile
Daudi Mwangosi (katikati) akiwa na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Mhe.Ritta Kabati na mkuu wa chuo cha Tumaini Iringa Profesa Nicholaus Bangu siku ya mkutano wa wadau wa habari uliofanyika ukumbi wa Manispaa ya Iringa
Daudi Mwangosi (wa pili kulia) akiongoza wanahabari Iringa kuvuka daraja la kamba lililopo hifadhi ya Taifa ya Ruaha wakati wa ziara yao ya kuhamasisha utalii wa ndani iliyofanyika mwaka huu.

Tulitaniana ,  tulicheka , kucheza pamoja tulishauriana na tulivutana kwa  kufundishana ila leo ninafikiri juu ya hatma ya kifo  cha Daudi Mwangosi na mwisho  wa kesi ya mtuhumiwa wa mauwaji yake ambae Januari 31 siku ya Alhamis atafikishwa mahakamani.

Binafsi  kila ninaposikia kesi hii  inatajwa mahakamani najisikia  kutokwa na machozi na wakati  wote namkumbuka Mwenyekiti  wangu ambae alilazimishwa kuondoka duniani kwa  kuuwawa  kinyama pale Nyololo  wilayani Mufindi mbele ya macho yangu .

Ni misiba  mingi  imetokea na wanahabari wengi na ndugu  zangu wengi  nimepata  kuwazika akiwemo babangu mzazi  ila siwakumbuki kama leo  ninavyokumbuka mauwaji ya Mwangosi napata wakati mgumu  zaidi  kusahau kilichotokea ila nasukumwa  zaidi kutaka  kujua mwisho  wa mtuhumiwa wa mauwaji haya kama itakuwa vipi .

Sitamani  kwenda mahakamani  kusikiliza  kesi inayotajwa  ila najikuta nimefika mahakamani kuendeleza simanzi hasa pale ninapomushuhudia mtuhumiwa na  kusikitia namba  ya kesi  hiyo na jina la Mwenyekiti  wangu Daudi Mwangosi 

KATA YA KIPAWA KUZINDUA AWAMU YA PILI YA MRADI WA MAZINGIRA BORA KWA ELIMU BORA

Diwani wa Kata ya Kipawa Manispaa ya Ilala, 
Bonnah Kaluwa, akizungumza katika mkutano na 
waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu awamu 
ya pili ya Mradi wa Mazingira Bora kwa Elimu Bora 
utakao zinduliwa kesho katika Kata hiyo. Kushoto ni 
Meneja wa Mradi huo Regina Ogwai. Mradi huo utafadhiliwa na nchi ya Marekani.
Diwani wa Kata ya Kipawa Manispaa ya Ilala, 
Bonnah Kaluwa, akizungumza katika mkutano na 
waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu awamu 
ya pili ya Mradi wa Mazingira Bora 
kwa Elimu Bora utakao zinduliwa kesho katika Kata hiyo.
 Kushoto ni Meneja wa Mradi huo Regina Null. 
Kulia ni Ofisa Mtendaji wa Kata hiyo Said Fundi.


Diwani wa Kata ya Kipawa Manispaa ya Ilala, 
Bonnah Kaluwa, akizungumza katika mkutano na 
waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu awamu 
ya pili ya Mradi wa Mazingira Bora kwa Elimu Bora 
utakao zinduliwa kesho katika Kata hiyo. Kushoto ni 
Meneja wa Mradi huo Regina Ogwai. Mradi huo 
utafadhiliwa na nchi ya Marekani.

Na Dotto Mwaibale

DIWANI wa Kata ya Kipawa Bonnah Kaluwa amesema Kata yake inahitaji zaidi ya sh.milioni 217 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya sekta ya elimu katika Kata hiyo iliyopo Manispaa ya Ilala.

Hayo aliyabainisha Dar es Salaam leo katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu uboreshaji wa elimu katika kata hiyo na kuwa leo watazindua awamu ya pili ya mradi wa kuboresha mazingira bora ya elimu katika Kata hiyo.

Alisema katika tathmini walioifanya  awali wamebaini kila shule inahitaji jumla ya sh.milioni 31 ili kupata matundu 16 ya vyoo walimu pamoja na wanafunzi katika shule zote zilizopo katika kata hiyo.

"Mahitaji ya vyoo hivi ni kwa shule zote saba za kata ya Kipawa zikiwemo mbili za Sekondari na tano za msingi" alisema Kaluwa.

Alisema mradi wa kwanza walifanikiwa kupata sh.milioni 155,500,000 ambapo waliweza kununua madawati 500 ya shule za msingi, 480 ya sekondari na viti 100 vya shule ya awali na kuchimba kisima cha maji katika kila shule.

Alisema katika awamu hii ya pili wamelenga kujenga vyoo na madarasa ambapo watu mbalimbali wamealikwa wakiwemo watu wa Marekani ambao wameonesha nia ya kusaidia mradi huo.

Alisema awali kata hiyo ilikuwa na changamoto ya ukosaji wa maji mashuleni na madawati lakini kwa sasa kero hizo zimekwisha  kutoka na ushirikiano wa wadau mbalimbali waliojitolea kuchangia maendeleo ya kata hiyo hasa katika sekta ya elimu.

Alizitaja shule hizo zilizopo katika kata hiyo ambazo zitanufaika na mradi huo kuwa ni Minazi Mirefu, Airwing, Mogo, Kipawa na Majani ya Chai.

Kwa upande wake Ofisa Mtendaji wa Kata hiyo Said Fundi alimshukuru Diwani huyo kwa kuiwezesha kielimu kata hiyo na kupunguza changamoto zilizopo ikiwemo ya ukosefu wa maji katika shule hizo.

Kaluwa alitumia fursa hiyo kuwaomba wadau mbalimbali wa elimu na afya pamoja na wazazi kujitokeza kwa wingi kufanikisha mradi huo wenye malengo ya kuboresha elimu ya msingi na sekondari katika kata hiyo.

BREAKING NEWS......MOTO WATEKETEZA KIWANDA CHA CHEMI COTEX DAR

Moto mkubwa umezuka na unakiunguza kiwanda cha vipodozi cha ChemiCotex kilichopo huko Africana njia ya Tegeta jijini Dar es Salaam.

Chanzo cha moto huo hakijafahamika ingawaje inahisiwa kuwa huenda ni hitilafu iliyotokana na fundi aliyekuwa akichomelea kitu ndani ya kiwanda hicho.

Wahusika wakuu wa kiwanda hicho hawakuwa katika eneo husika ili kutoa maelezo zaidi. Taarifa zinasema kuwa magari ya kikosi cha zima-moto yalipowasili, watu walianza kuyarushia mawe kiasi cha kutishia usalama wa watu wengine ambao waliamua kuondoka kutoka katika eneo la tukio.

Jitihada  za  kumtafuta kamanda  wa  polisi  wa  kanda maalum ya Dar es Salaam Suelein Kova  bado zinaendelea baada ya simu yake  kuita bila  kupokelewa .(picha na wavuti)

WASANII IRINGA WATOA USHAURI WA BURE KWA LULU WATAKA AOKOKEWapenzi  wa  muziki  filam mkoani Iringa  wametoa onyo kwa msanii Elizabeth Michael maarufu Lulu aliyetoka kwa  dhamana  mahabusu kufuati  tuhuma ya kesi yake ya mauwaji ya msanii mwezake Stivin Kanumba ,kuwa anapaswa  kutumia muda huu kuwa  jirani ni kanisa badala ya  kupenda starehe za dunia.

Wakizungumza na mtandao huu  wa  www.francisgodwin.blogspot.com wasanii hao Johari John na Kevin Sanga  walisema  kuwa dhamana ya Lulu ni mapenzi ya Mungu  hivyo mbali ya  kutoka mahabusu kwa dhamana bado anapaswa  kuishi kwa utulivu zaidi muda  wote ikibidi kuanza  kuwa karibu na kanisa.

Hata  hivyo John alitaka  waumini wa madhehebu mbali mbali kuendelea  kumwombea msanii  huyo ili Mungu aendelee  kusimama upande  wake.

Wasanii hao  walisema  kuwa  suala la msanii  huyo  kuendekeza  kujirusha kwa  sasa asilipe nafasi katika maisha yake na badala yake  kumgeukia Mungu  zaidi na kuachana na mambo ambayo hayampendezi mwenyezi Mungu.

Kimbunga Felleng Kutua Afrika Mashariki


Taarifa kwa umma: Uwezekano wa matukio ya mvua kubwa

Taarifa Na. 20130129-02

Muda wa Kutolewa Saa za Afrika Mashariki Saa 12:00 Jioni

Daraja la Taarifa:

1:Taarifa 2:Ushauri 3:Tahadhari 4:Tahadhari Kubwa:

Ushauri

Kuanzia:

Tarehe 30 Januari, 2013 Mpaka: Tarehe  01 Februari, 2013

Aina ya Tukio Linalotarajiwa

Mvua kubwa (zaidi ya milimita 50 katika kipindi cha saa 24 kilasiku)

Kiwango cha uhakika: Wastani

Maeneo yatakayoathirika Baadhi ya maeneo ya mikoa ya Rukwa, Iringa, Mbeya, Njombe,Ruvuma, Morogoro, Lindi, Pwani, Mtwara na maeneo jirani na mikoa hiyo.

Maelezo:

Kuwepo kwa kimbunga “FELLENG” kaskazini-mashariki mwa,Madagascar ambacho kinavuta upepo wenye unyevunyevu.kutoka Congo kupitia maeneo tajwa hapo juu.

Angalizo:

Wakazi wa maeneo hatarishi, watumiaji wa Bahari na nchi kavuwanashauriwa kuchukua tahadhari. Aidha taasisi zinazohusika na Maafa zinashauriwa kuchukua hatua stahiki.

Maelezo ya Ziada

Mamlaka inaendelea kufuatilia mwenendo wa kimbunga hicho,na kutoa mrejeo (updates) kila itakapobidi.

IMETOLEWA NA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

RAIS JOSEPH KABILA WA DRC ATUA DAR LEO KWA ZIARA YA SIKU MOJA


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimjpokea Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) alipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam mchana wa leo Januari 30, 2013

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha maafisa mbalimbali Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) alipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam mchana wa leo Januari 30, 2013


  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mgteni wake  Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wakmiangalia ngoma za utamaduni alipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijijni Dar es salaam  mchana wa leo Januari 30, 2013
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wakiingia hoteli ya Hyatt  Kilimanjaro jijini mchana wa leo Januari 30, 2013
PICHA NA IKULU

TAIFA STARS KUIKABILI CAMEROON ‘FIFA DATE’

Tanzania (Taifa Stars) itacheza na Cameroon katika moja ya mechi za kirafiki za Kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA)- FIFA Date zitakazofanyika duniani kote Februari 6 mwaka huu.

Mechi hiyo itafanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 11 kamili jioni. Kikosi cha Cameroon kinachoundwa na wachezaji wengi wa kulipwa wanaocheza katika nchi mbalimbali duniani kitaanza kuwasili nchini Februari 3 mwaka huu.

Nchi kadhaa ziliomba kucheza na Taifa Stars katika tarehe hiyo ya FIFA, lakini Kocha wa Stars, Kim Poulsen ameamua kucheza mechi hiyo dhidi ya Cameroon ambayo nahodha wake ni mchezaji nyota wa kimataifa, Samuel Etoo Fils.

Congo Brazzaville, Equatorial Guinea, Rwanda na Swaziland nazo zilikuwa zimeomba kucheza dhidi ya Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager. Ukiondoa Swaziland iliyotaka mechi hiyo ichezwe Dar es Salaam, nyingine zilitaka kucheza nyumbani kwao.

Wakati huo huo, Kocha Kim Poulsen atakutana na Waandishi wa Habari kuzungumzia maandalizi ya mechi hiyo ikiwemo kutaja kikosi ambacho atakitumia. Mkutano huo utafanyika saa 5 kamili asubuhi kwenye ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).


Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)