Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

November 30, 2012

MAHAFALI YA 5 YA CHUO KIKUU CHA RUAHA IRINGA LEO KTK PICHA


Mtumishi  wa Manispaa ya Iringa Bw Msunza akiwa na familia yake  mara baada ya  kuhitimu katika  chuo  hicho cha RUCO leo

 Umati  wa wananchi  waliofika katika mahafali hiyo  leo wakiwa katika  viwanja  vya chuo cha Ruco Iringa
 Wahitimu na ndugu  wa wahitimu  wakichagua  picha  zao ili kuzinunua baada ya kupigwa na wapiga picha wa kujitegemea

 Meneja  wa vipindi radio Nuru Fm Godfrey Ngulla akiwa na mkewe katika mahafali hiyo leo

MADIWANI MANISPAA YA IRINGA NA ILALA WADAIWA KUDANGANYWA KIWANDANI

 Haya ni mazingira ya  kiwanda cha  Dabaga  ambayo yanaongoza kwa  kuwa harufu kali kutokana na uchafu

Zikiwa  zimepita siku chache toka madiwani  wa Halmashauri ya Ilala jijini Dar es Salaam na wale wa  Manispaa ya Iringa  kufanya  ziara  katika kiwanda cha Dabaga Vegetable kilichopo Ipogolo na  kuvutiwa na hali ya  usafi  wa kiwanda  hicho  , wafanyakazi wa  kiwanda hicho  wafichua siri wadai madiwani  walidanganywa juu ya usafi.

 Wakizungumza na mtandao  huu wa www.francisgodwin.blogspot.com wafanyakazi wa  kiwanda hicho ambao  waliomba majina yao kuhifadhiwa  kwa usalama  wao  ,walidai kuwa  wakati wa  ziara ya madiwani hao  uongozi  wa kiwanda  hicho  ulilazimika  kufunga  kiwanda  kwa  muda ili  kupisha  ziara  hiyo kutokana na mazingira ya  kiwanda hicho  kuwa machafu.

Kwani  walisema  kuwa kwa kawaida  mazingira ya  kiwanda  hicho ni machafu  zaidi na kuna haja ya  viongozi hao  wakiwemo madiwani  wa Manispaa ya Iringa  kujenga utamaduni wa  kufanya ziara za ghafla katika  viwanda  hivyo  ili  kuona hali halisi badala ya  kufanya ziara  zenye taarifa kama hiyo  iliyofanyika na kupelekea  uongozi wa kiwanda hicho  kujiandaa kwa usafi zaidi.


Wafanyakazi hao  walisema harufu mbaya ya uchafu iliyomo ndani ya kiwanda hicho hata  wao wafanyakazi  imekuwa ikiwaweka katika  wakati mgumu  ila madiwani walikubali  kudanganywa kwa zawadi ndogo ndogo  walizopewa  wakati wa ziara  hiyo na kuwa kuna haja ya madiwani hao hasa kamati ya afya  na mazingira  kufika  kufanya ukaguzi  katika  kiwanda hicho na viwanda vingine mjini Iringa .

BOB CHORA AMNG'ARISHA IBRAHIMU CLASS 'KING CLASS MAWE'

Msanii wa Sanaa ya Uchoraji Jeremia Makimata 'Bob Chora' akichora moja ya bango la kumuhamasisha bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kwa ajili ya mpambano wake unaokuja zidi ya bondia Saidi Mundi wa Tanga utakaofanyika Desemba 9 katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba jijini Dar es salaam
 Msanii wa Sanaa ya Uchoraji Jeremia Makimata 'Bob Chora' akichora moja ya bango la kumuhamasisha bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kwa ajili ya mpambano wake wa DESEMBA 9
MOJA YA BANGO LILILOCHOLWA NA BOB CHORA
Msanii wa Sanaa ya Uchoraji Jeremia Makimata 'Bob Chora' akichora moja ya bango la kumuhamasisha bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kwa ajili ya mpambano wake unaokuja zidi ya bondia Saidi Mundi wa Tanga utakaofanyika Desemba 9 katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba jijini Dar es salaam 
Msanii wa Sanaa ya Uchoraji Jeremia Makimata 'Bob Chora' akichora moja ya bango la kumuhamasisha bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kwa ajili ya mpambano wake unaokuja zidi ya bondia Saidi Mundi wa Tanga utakaofanyika Desemba 9 katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba jijini Dar es salaam (picha na Supr D Blog)

KAMPUNI YA WELLNESS TANZANIA YAENDESHA SEMINA JUU YA USTAWI WA MWAJIRIWA JIJINI DAR

Mtaalamu wa Ustawi wa mwajiriwa Bw. Doug Bramsem akitoa somo katika semina juu ya Ustawi wa Mwajiriwa iliyofanyika hoteli ya Sea Cliff jijini Dar es Salaam. Semina hiyo ilikuwa na lengo la kuwawezesha washiriki kujua nini maana ya Ustawi wa Mwajiriwa, jinsi ya kuendesha kampuni na kupata faida na kujua historia ya Ustawi wa Mwajiriwa nchini Tanzania na kumjenga mfanyakaziwako kuwa bora na kutatua ustawi wake katika kampuni zao
 Mtaalamu wa Ustawi wa mwajiriwa Bw. Doug Bramsem akikazia neno.
Washiriki wakifuatilia semina.
Mtaalamu wa magonjwa ya akili kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha magonjwa ya akili, Prof. Gad Kilonzo akizungumzia Ustawi wa Mwajiriwa.
 Mtaalamu wa mambo ya Saikolojia, Bi. Lisa Finke kutoka GIZ akitoa somo katika semina hiyo.
 Mtaalamu wa Ustawi wa mwajiriwa, Dkt. Hilde Basstanie kutoka GIN akitoa somo la ugonjwa wa Ukimwi jinsi ya kujilinda makazini.
 Washikiri wakifuatilia kwa makini semina hiyo.
Mmoja ya washiriki wa semina hiyo, Bw. James Lwanga kutoka hospitali ya Kadic iliyopo Bukoto, Uganda akielezea mambo mbali mbali yanayofanyika katika jamii nchini kwao.
 Washiriki wakifuatilia kwa makini semina.
  Mtaalamu wa Ustawi wa mwajiriwa,  Dkt. Hilde Basstanie (kwanza kulia) kutoka GIN akiwa na washiriki wengine wakifuatilia kwa makini.
Washiriki wakiwa makini kupata somo (picha na
Cathbert Angelo Kajuna,)

MAHAFALI YA TANO YANAFANYIKA LEO CHUO CHA RUAHA IRINGA


Wadau  wakiwa katika majadiliano binafsi kabla ya mahafali  leo

Hawa ni wadao  wa mtandao huu Bw Makwega kutoka DW (kulia ) Lesuya  ambaye ni mhitimu  leo
 Meneja  wa  vipindi wa Radio  Nuru Fm Iringa Godfrey Ngulla (kushoto) akipongezana na mwenzake Manford Kasebele kabala ya mahafali ya  chuo  kikuu cha Ruco leo Ngulla alikuwa akichukua masomo ya  sheria katika  chuo  hicho na ni mwanasheria  wa  kujitolea katika  chama cha  wapangaji mkoa  wa Iringa ambapo mmiliki wa mtandao huu ni mwenyekiti wa chama  hicho
Wadau  wakiwa katika majadiliano binafsi kabla ya mahafali  leo

wafanyabiashara  wa maua  wakiendelea na kazi