Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

October 31, 2012

KIINGILIO REDD'S MISS TANZANIA CHAWEKWA WAZI

WAKATI zikiwa zimesalia siku mbili kabla ya Redd’s Miss Tanzania 2012 kupatikana na kila mshiriki akibaki kujiuliza nani atatwaa taji hilo, kiingilio cha kushuhudia shindano hilo kimetajwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino walio waandaaji, Hashim Lundenga, alisema kiingilio kitakuwa Sh 100,00 huku kukiwa na burudani za kufa mtu.

 Mshidi atajitwalia gari pamoja na fedha taslimu Sh milioni 8, katika kinyang’anyiro hicho kinachotarajiwa kufanyika kwenye ukumbi wa hoteli ya Blue Pearl uliopo jengo la Ubungo Plaza, Dar es Salaam keshokutwa.

 Lundenga alisema warembo watano wamefanikiwa kuingia hatua ya 15 Bora ya Redd’s Miss Tanzania kutokana na kushinda katika mashindano madogo.

 Warembo hao ni Lucy Stephano aliyeshinda Miss Photogenic, Mary Chizi aliyetwaa taji la Miss Sports Lady, Babylove Kalala aliyeshinda Miss Talent, Magdalena Roy aliyetwaa taji la Top Model na Miss Personality, Happiness Daniel.

 Lundenga alisema, burudani siku hiyo itatolewa na msanii wa muziki wa kizazi kipya, Diamond Platinum, Winfrida Josephat ‘Rachel’ pamoja na yule wa ngoma za asili, Wanne Star. “Tumekamilisha kila kitu, naamini atapatikana mrembo mkali zaidi ambaye atatuwakilisha vema katika mashindano ya dunia,” alisema.

Lundenga alisema, tayari tiketi zinauzwa katika vituo kadhaa ambavyo ni Regency Park Hotel, Rose Garden, Share Illusion, Mlimani City, City Sport Lounge, Giraffe Hotel, Ubungo Plaza na katika ofisi za Lino.

Shindano la Redds Miss Tanzania 2012 linadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia kinywaji cha Redds Original.

UHABA WA MAFUTA IRINGA WAANZA KUTOWEKA

Pamoja na tatizo kubwa la mafuta lililoukumba mji wa Iringa kwa zaidi ya wiki sasa ,hali hiyo kwa leo imeanza kurejea katika nafasi yake bada ya malori ya mafuta kushusha mafuta katika vituo mbali mbali

PANGAMAWE TELCOM NJOMBE NI JIBU LAKO ....

SIMU NA CAMERA NI KWA PANGAMAWE SHOP MJINI NJOMBE PEKEE


Samsung Galaxy S

Camera za kila aina ndani ya duka la Pangamawe

Pia Sofa za aina mbali mbali zinapatikana katika duka la Pangamawe Njombe mjini

Bila kusahau vitanda vya kisasa na bora zaidi

Wengi hufika Pangamawe kupata simu za kisasa za kijanja zaidi
Usisumbuke kutafuta duka la simu ulinza Pangamawe Matelephone
Vifaa vya simu kama chaji za aina zote n.k


Kwa mawasiliano piga simu 0767502000 utahudumiwa popote ulipo

RAIS KIKWETE AZINDUA BARABARA HAI ,MBOWE APONGEZA


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokewa na Mkuu wa Wilaya ya Hai Mhe Novatus Makunga katika eneo la sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Kwa Sadala-Masama wilayani hai leo
 Akihutubia
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisaidiwa kuzindua jiwe la msingi na Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe Freeman Mbowe katika eneo la sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Kwa Sadala-Masama wilayani hai leo
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipongezwa na kupewa shukurani na Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe Freeman Mbowe katika eneo la sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Kwa Sadala-Masama wilayani hai leo
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Miundombinu Mhe John Pombe Magufuli Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe L:eonidas Gama na Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe Freeman Mbowe wakikata utepe mojawapo ya magreda katika eneo la sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Kwa Sadala-Masama wilayani hai leo
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Miundombinu Mhe John Pombe Magufuli Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe Leonidas Gama na Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe Freeman Mbowe katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Kilimanjaro baada ya uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Kwa Sadala-Masama wilayani hai leo
  (picha na Ikulu)

AMREF YAWAKUSANYA VIJANA IRINGA KTK KONGAMANO

 
 
Na Denis Mlowe - Iringa

Maadhimisho ya siku ya afya ya uzazi kwa vijana kwa mwaka 2012 yaliyoandaliwa na wizara ya afya kitengo cha uzazi na mtoto kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali la AMREF na wadau wengine yamefanyika mkoani Iringa katika ukumbi wa Highland Hall na kuhudhuriwa na rika za watu mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari.

Maadhimisho hayo yaliyokuwa na kauli mbiu ya "Andaa taifa bora kwa kuwekeza katika afya ya uzazi wa vijana" mgeni rasmi alikuwa katibu tawala wa mkoa aliyewakilishwa na msaidizi wake pia yalihudhuriwa na naibu meya wa manispaa Gervas Ndaki, mkuregenzi wa manispaa na mwakilishi wa vijana yalikuwa na lengo la kuongeza ufahamu kwa vijana katika suala zima la afya ya uzazi kwa vijana.

Mratibu wa maadhimisho hayo kutoka AMREF, Ndugu Meshack Mollel amesema kwamba wizara ya afya kupitia AMREF na wadau mbalimbali wamewezesha maadhimisho hayo kufanyika kwa mara ya kwanza mkoani hapa na ni kitu cha kujivunia kwa mkoa wa iringa kwa kuwa mwaka jana lilifayika jiji dar es salaam na litakuwa faida kubwa sana kwa vijana wa mkoa huu katika kujadili na kuwa na ufahamu mkubwa sana katika suala zima la afya ya uzazi kwa vijana na kutetea na kujenga afya bora kwa vijana wote.

Afya ya uzazi kwa vijana yamekuwa na mafanikio makubwa sana kwa vijana tangu yalipoanzwa kufundishwa kwani yamefanikiwa kushirikiana kwa vijana katika kubadilishana uzoefu na utaalamu juu ya afya ya uzazi kwa vijana, aidha yamewezesha vijana kujenga uwezo wa kutetea hoja mbali mbali za kuimarisha afya ya vijana katika uzazi

Aidha afya ya uzazi kwa vijana ina changamoto kubwa kama kuwa na majukumu kwa wadau kutotekelezwa ipasavyo na mabadiliko ya mara kwa mara ya uongozi katika asasi mbalimbali ni changamoto nyingine katika afya ya uzazi kwa vijana na kutokuwa na chombo cha kitaifa kinachounganisha wizara zote.

Mratibu wa afya ya uzazi na mtoto katika manispaa ya Iringa Dr. Mariam Mohamed (picha no 0073) amesema kwamba kuna vituo 42 ndani ya manispaa vinavyotoa huduma ya afya ya uzazi kwa vijana.

"Vituo hivyo vinakumbana na changamoto ya upungufu wa watumishi wa afya ya huduma rafiki kwa vijana, ushiriki mdogo wa wazazi katika kupata elimu ya uzazi kwa vijana aidha mfumo wa ukusanyaji wa taarifa na vituo kutokuwa na alama ya utambulisho ndio changamoto" alisema Dr Mariam Mohamed

Aliongeza kwa kusema matarajio ya manispaa ni kuongeza watumishi katikam vituo mbali mbali aidha kushirikiana na jamii katika kutoa elimu ya afya ya uzazi kwa vijana na kusimamia takwimu na kushirikiana na wadau wa mikoa Njombe, Mbeya katika elimu ya afya ya uzazi.
DROO YA PILI YA SHINDA NOAH YAFANYIKA, WASHINDI WAZIDI KUPATIKANA

Mshindi wa Kompyuta aina ya Dell, Rehema Kigadye wa Tegeta akiwa amepozi na zawadi yake.
DROO ya pili ya Bahati Nasibu ya Shinda Noah inayoendeshwa na Kampuni ya Global Publishers wachapishaji wa magazeti ya Ijumaa Wikienda, Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa na Championi leo imewapata washindi wengine katika Viwanja vya Karume, jijini Dar.

Meneja mkuu wa Global, Abdallah Mrisho (kulia) akimkabidhi zawadi mmoja wa washindi wa papo kwa papo.
Washindi waliopatikana katika droo hiyo na kujinyakulia zawadi tofauti ni, Rukia Vitali wa Boko, Dar (TV Flat Screen), Leah  Andrew wa Mwananyamala (Simu aina ya Samsung Galaxy), Rehema Kigadye wa Tegeta (Jezi) huku wengine wakijinyakulia zawadi za papo kwa papo (kama wanavyoonekana pichani).
 
Mfanyakazi wa Global, Jimmy akimwelekeza mshiriki namna ya kujiunga kwenye shindano.
  
Droo ikichezeshwa.
   
Afisa Masoko wa Global, Benjamini Mwanambuu (kulia) akimkabidhi zawadi ya T- shirt mmoja wa washiriki waliojitokeza.

(PICHA/HABARI: ERICK EVARIST/GPL)

USAFIRI WA GARI MOSHI WAPOKELEWA KWA SHANGWE DARBi. Rose Ngauga akizungumza  na mwandishi wetu aliyemtembea ofisini kwake kujua mawili matatu kuhusiana na usafiri huo.


Abiria wakigombea kupanda treni kutoka katikati ya jiji kueleke Ubungo.
Kamera yetu leo ilitua katika ofisi ya mkuu wa kituo kinachodili na usafiri huo, Bi. Rose Ngauga na kuzungumza mambo kadhaa kuhusiana na usafiri huo.
Ngauga alisema kuwa usafiri huo siyo nguvu ya soda kama inavyodaiwa na baadhi ya watu na kwamba utakuwa endelevu.
Wanafunzi wakipanda katika behewa lao maalumu tayari kwa safari.

Bi. Rose akimuonyesha mwandishi wetu (hayupo pichani) tiketi zinazotumika kwa abiria wa kawaida na wanafunzi.
Abiria wakiwa katika dirisha la kukatia tiketi.
Wanafunzi wakikata tiketi katika dirisha maalumu kwa ajili yao.
Kichwa cha treni kikiunganishwa na mabehewa kabla ya kuanza safari.
Abiria wakiwa wameketi ndani ya behewa wakisubiri kuanza safari.
Mkuu wa Kituo cha Reli, Bi. Rose Ngauga akikagua mabehewa kabla ya gari moshi kuanza safari leo saa 9.40 alasiri.
...akikabidhiwa ripoti.
Gari moshi likiwa katika mwendo na baadhi ya abiria wakionekana wakichati na simu.
Mwandishi mwanadamizi wa Global Publisher, Haruni Sanchawa  akishuka kutoka katika treni hiyo  maeneo ya Ubungo Maziwa ambako treni hiyo umalizia safari yake.
Abiria wakishuka kwenye treni.
Pamoja na usafiri huo kuanza, mafundi wa shirika la reli bado wanaendelea na ukarabati  wa reli kama wanavyoonekana pichani.
(HABARI PICHA : Haruni Sanchawa / GPL)

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO MKUU WA NANE WA JUMUIYA YA WAZAZI CCM-TAIFA, MJINI DODOM

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Nane wa Jumuiya ya Wazazi CCM-Taifa. Mkutano huo unafanyika sambamba na uchaguzi wa Viongozi wapya wa Jumuiya hiyo, katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Chuo cha Mipango, mjini Dodoma leo Oktoba 31, 2012. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na William Malecela, wakati akiondoka kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Chuo cha Mipango, mjini Dodoma leo Oktoba 31, 2012 baada ya kufungua rasmi Mkutano Mkuu wa Nane wa Jumuiya ya Wazazi CCM-Taifa. Mkutano huo unafanyika sambamba na uchaguzi
Makamu wa Rais  akisalimiana na  wajumbe