Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

August 31, 2012

ABIRIA WA BASI LA EVA MARIA WAKWAMA STENDI
mzee wa matukio daima akiwahoji abiria hao baada ya kukwama stendi(picha na Pius Kadinde)

Abiria wa basi la Eva Maria ambao walipaswa kusafiri kutoka Iringa mjini kwenda Ismani wamekwama katika stendi kuu ya mabasi ya mikoani mjini Iringa baada ya wahusika wa basi hilo kutojulikana walipo.

Abiria hao wamedai kuwa walipaswa kuondoka majira ya saa nane mchana ila hadi sasa saa 10 jioni basi hilo halijulikani lilipo.

DR SLAA AMTOLEA UVUVI WAZIRI SAMWEL SITTA, AFICHUA SIRI NZITO KATI YAKE NA SITTA

katibu mkuu wa Chadema Dkt Slaa akionyesha baadhi ya vielelezo kwa wanahabari leo mjini Iringa
Dkt Slaa akiwa katika mkutano wake na wanahabari mkoa wa Iringa katika ukumbi wa Hoteli ya M.R

SIKU moja baada ya waziri wa Afrika Mashariki na mbunge wa jimbo la Urambo Mashariki Samwel Sitta kumrushia kombora mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe kuwa ,katibu mkuu wa Chadema Dkt Willbroad Slaa aibua tuhuma nzito dhidi ya waziri Sitta amwita msaliti .

Dkt Slaa amedai kuwa waziri Sitta ndie alikuwa katika makubaliano ya kuja kugombea uspika kupitia Chadema ila alisaliti pamoja na kukubaliana vizuri kuwa angekihama chama chake CCM.

Dkt Slaa alitoa tuhuma hizo leo mjini Iringa alipozungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya M.R alisema ilikuwa Mei mwaka 2010, Sitta ambaye hivi sasa ni Waziri wa Afrika Mashariki alipokutana na viongozi wa Chadema na kuonesha dhamira ya kujitoa CCM na kujiunga na chama chao ila alionyesha usaliti wa hali ya juu.

Alisema kuwa katika mazungumzo hayo yaliyoendelea kufanywa katika kipindi chote cha bunge la bajeti lililokuwa la mwisho kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, Dk Slaa alisema katika masharti yake ya kujiunga na Chadema, Sitta ambaye kwa wakati huo alikuwa Spika, alitaka apewe nafasi ya kuwania urais kupitia chama hicho na vikao vilikuwa vikifanyika ofisini kwake Dodoma.

Alisema ameamua kutoa siri hiyo baada ya kiongozi huyo (Sitta) kunukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari juzi akidai kwamba Dk Slaa ni mtu pekee ndani ya Chadema ambaye ni tishio kwa urais katika uchaguzi ujao, huku akimponda Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe kwamba ni mchezesha disco.

Hata hivyo alisdai kushangazwa na waziri Sitta kuanza kuzungumzia mambo ya watu badala ya kujibu hoja na kuwa Chadema haipendi kuzungumza habari za watu, inazunguma maendeleo. Kwa muda mrefu tumemuhifadhi Sitta lakini baada ya kupeleka mashambulizi sehemu isiyohusika sasa tunampiga ngumi za tumbo na uso

Dkt Slaa alisema kuwa wakati akitaka aandaliwe mazingira ya kujiunga na Chadema na kupewa nafasi ya kuwania urais, Sitta alidai ana kundi la wabunge zaidi ya 55 waadilifu kutoka katika chama hicho ambao angetoka nao pamoja CCM na kuhamia Chadema kabla ya bunge kuvunjwa.

Alisema kwa kuwa Chadema haina ubinafsi, ilihadi kuyafanyia kazi maombi yake ya kuwania urais kwa uzito mkubwa hata hivyo katika mazingira ya kushangaza aliwatelekeza.

Dk Slaa alisema Sitta ambaye uzoefu wake katika siasa na umakini wake katika kushughulikia maendeleo ya nchi umeanza kuwatia shaka watanzania, alisahau jinsi alivyowatelekeza kabla ya Uchaguzi Mkuu na baada ya uchaguzi huo akaja na hoja mpya kitaka Chadema wampe nafasi ya kuwania uspika kwa kile alichodai kuwepo kwa mizengwe ndani ya CCM.

Katika mazingira ya kushangaza badala ya kufikia uamuzi wake wa kuhamia Chadema kama dhamira yake ilivyomtuma, Sitta aliwatelekeza tena akidai kwamba atajiunga na chama hicho mpaka pale atakapokwenda jimboni kwake Urambo na kutangaza rasmi kujiondoa CCM.

Alisema kiongozi huyo aliyekuwa akitaka msaada wa viongozi wa Chadema ili afanikiwe kujiunga na chama hicho na hatimaye kupewa nafasi ya kuwania nyadhifa alizokuwa akitaka ameanza kuwatusi hadharani viongozi hao akiwemo Menyekiti wake Mbowe.

Alisema kauli inayotolewa na Sitta kwamba Mbowe ni mchezesha disco inadhihirisha jinsi asivyo makini jambo linalowafanya waanze kuitilia shaka elimu na uzoefu alionao katika kuendesha shughuli za serikali.

“Sita anataka kutuambia kwamba watu wanaocheza disco wakiwemo mawaziri wengi tu wanaokutwa kwenye kumbi za burudani wanatenda dhambi na ni uhalifu kufanya hivyo?,” alisema.

Alisema kama biashara hiyo ya Mbowe inafanywa kinyume na sheria za nchi, serikali inasubiri nini kufuta leseni yake.

Kuhusu uongozi na namna ya kupata viongozi ndani ya chama hicho, Dk Slaa alisema sio kazi ya Sitta akuwapangia utaratibu.

“Sitta hajui kwamba duniani hakuna chuo cha kusomea uwaziri, ukatibu mkuu, na hajui kwamba Mwalimu Julius Nyerere hakuwa na uzoefu wakati akipewa madaraka ya kuongoza taifa hili na kwamba hata wasaidizi wake nao walipata uzoefu baada ya kupata madaraka,” alisema.

Alisema Sitta ni kiongozi mnafiki na atakumbukwa zaidi alipokuwa Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwasababu kuna hoja mbalimbali zilizowasilishwa na wabunge wa upinzani kuhusu ufisadi alizizima.

Alisema kuzimwa kwa hoja hizo ikiwemo ya Mkataba uliogubikwa na utata wa Buzwagi, unadhihirisha jinsi naye alivyotumia madaraka yake vibaya kwa kujenga ofisi ndogo ya Spika ambayo yeye aliita ya mbunge jimbo kwake Urambo.

Alisema wakati serikali imeridhia ofisi za wabunge zijengwe kwa kiasi cha fedha kisichozidi Sh Milioni 40 kwa kuzingatia upatikanaji wa fedha, ofisi hiyo ya Urambo ilijengwa kwa Sh Milioni 350.

“Kauli zinazotolewa na Sitta kuhusu chama chetu zinadhihirisha jinsi alivyomnafiki na asivyofaa jambo lililosababisha hata CCM wamemnyime nafasi ya kuwania kugombea kwa mara nyingone tena nafasi ya Uspika,” alisema.

Dk Slaa na viongozi mbalimbali wa chama hicho wako mkoani hapa, wakisubiri waanza mikutano yao ya vugugugu la mabadiliko walilolipa jina la M4C baada ya kuzuiwa na jeshi la Polisi kufanya mikutano yao katika kipindi chote cha sensa.

Wakati huo huo Dkt Slaa ameshindwa kutolea ufafanuzi juu ya kiasi cha fedha walizotenga kwa ajili ya mikutano yao ya M4C inayoendelea hapa nchi huku akiishia kudai kuwa fedha zinazotumika ni fedha zinazotokana na ruzuku ya serikali na michango ya wananchi bila kutaja kiasi hicho cha fedha.


kumbuka haya yote kwa udhamini wa Tanzania Unique Tours

TANZANIA UNIQUE TOURS NI UHAKIKA KWA SAFARI ZA MAENEO YA VIVUTIO NCHINI

Magari ya kisasa yanayotumika kusafirisha watalii katika maeneo ya vivutio hapa nchini kutoka kampuni ya Tanzania Unique Tours
Hapa ni safari salama na Tanzania Unique Tours
Watalii wakiwa wamepanga foleni ofisi za Tanzania Unique Tours kwa ajili ya kukodi

ofisi zetu zipo nyumba ya jengo la Highlands Hall(Behind Highland Hall) jirani na posta ya mkoa wa Iringa ,Manispaa ya Iringa ,P.O.Box.384 Iringa Mob.+255 656 187139/0759248284
Tanzania Unique Tours
Service;
> Mountain Climbing /Trekking
>To Organize safari& Tours
> Hotels Accommodation .
CONTACT
Tell+225(0)02702425
Cell;07155961433
Email Info2@tanzaniauniquetours.com
website.www.tanzaniauniquetours.com
BOFYA HAPA KWA TAARIFA SASA KWA TAARIFA ZAIDIMATOKEO UVCCM IRINGA VIJIJINI YATANGAZWA ,MWENYEKITI MPYA AKABIDHIWA KITI GIZANI

Mwenyekiti mpya UVCCM Iringa vijijini Benitho Kayugwa akieleza mikakati yake baada ya kutangazwa mshindi

Vijana wa UVCCM Iringa vijijini wakiwa wamembeba mwenyekiwa wao mpya

Haya ndio matokeo ya uchaguzi UVCCM Iringa vijijini


Hata hivyo kutokana na kukatika ghafla kwa umeme kutokana na Hitirafu iliyotokea Ipogolo mwenyekiti huyo alijikuta akikabidhiwa kiti hicho gizani .

Huku akiendelea kuwahutubia vijana kwa kutumia mwanga wa tochi za simu za mikononi kabla ya katibu wa mbunge jimbo la Isimani Thomas Malenga kujitolea kukimbia nyumbani kwake kuchukua taa

MLIPUKO WA UMEME WASABABISHA TAHARUKI IPOGOLO IRINGA

wananchi wa Ipogolo mjini Iringa wakitazama mita iliyopasuka kutokana na hitirafu hiyo ya umeme


Mlipuko wa umeme wasababisha taharuki kwa wakazi wa Ipogolo katika manispaa ya Iringa jana usiku na kupelekea wananchi kuyakimbia makazi yao kwa muda.

Wananchi hao waliyakimbia makazi yao baada ya kutokea hitirafu ya umeme eneo la Ipogolo na kusababisha mlipuko mkali wa umeme hivyo kupelekea wananchi kuyakimbia makazi yao kwa muda.

Tukio hilo lilitokea majira ya saa 2 usiku na kupelekea mji mzima wa Iringa kukaaa gizani kwa muda wa nusu saa kabla ya shirika la ugavi wa umeme nchini Tanesco kufika eneo hilo na kujaribu kutatua tatizo hilo .

Wakazi wa eneo hilo waliueleza mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com kuwa mlipuko huo ulisababishwa na moja kati ya nyaya kubwa za umeme kukatika na kupelekea Transifoma kulipuka japo hakuna madhara yoyote kwa binadamu wala hakuna nyumba iliyoteketea kwa moto

MKURUGENZI MANISPAA YA IRINGA AWAANGUKIA WASIO HESABIWA

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Teresia Mahongo akihamasisha sensa katika Radio Furaha FM jana
Mtangazaji wa Radio Furaha Fm akiwa kazini
Mtangazaji wa kipindi cha wanawake Radio Furaha Tukusuga James akimuuliza maswali ya sensa mkurugenzi Mahongo

Mkurugenzi wa manispaa Iringa Bi. Theresia Mahongo amewataka wananchi wa Manispaa ya Iringa kutumia vizuri muda uliosalia ili kuweza kuhesabiwa katika zoezi la Sensa ya watu na makazi .

Aidha amesema endapo mwananchi yeyote atakuwa hajahesabiwa mpaka kufikia siku ya kesho afike ofisini kwake Manispaa ili aweze kuandikishwa katika zoezi hilo.

Amesema zoezi hili ni la siku saba na linatarajiwa kuhitimishwa siku ya jumamosi hivyo bado wananchi wanayonafsi ya kutoa taarifa zao.

Akizungumza katika studio za redio Furaha katika kipindi maarufu cha mwanamke na jamii amewataka wanawake wenye watoto wenye ulemavu kutoona aibu kutoa taarifa juu ya watoto wenye ulemavu kwani kila mtoto anazaliwa kwa maksudi maalum

pia amesisitiza kuwa ni vema taarifa zikatilewa na mkuu wa kaya katika kaya husika ili kuepuka kupatikana kwa takwimu zisizo sahihi

Hivyo amesema iwapo mwananchi wa Manispaa ya Iringa anatatizo ama hajahesabiwa mpaka sasa anaweza kupiga namba 0784476944 ili aweze kuhesabiwa kabla ya muda haujakwisha.

Wakati huo huo mkurugenzi huyo amekemea tabia ya baadhi ya wananchi wa Manispaa ya Iringa kuchoma moto madampo ya kuhifadhia takataka

MHARIRI MKUU WA THEHABARI AFANYA KWELI ....

Mhariri Mkuu wa Thehabari.com, Joachim Mushi (kushoto) akigonganisha glasi na mkewe Hilder Mwaipopo juzi (Agost 25) kwenye hafla ya harusi yao.
Hapa ilikuwa ni wakati wa Mr & Mrs Joachim Mushi kufungua muziki.
Bi. Hilder Mwaipopo (kulia) akijiandaa kumnywesha mvinyo mumewe Joachim Mushi kwenye hafla ya harusi yao iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

TIMU YA SIMBA KUJIPIMA NA NAIROBI CITY JUMAPILI


TIMU ya Simba inatarajia kucheza mechi dhidi ya timu ya soka ya NAIROBI CITY STARS siku ya Jumapili ijayo katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Kaluta jijini Arusha.

Timu hiyo kutoka Kenya ndiyo iliyocheza na Simba jijini Dar es Salaam katika tamasha la Simba Day.

Awali Simba ilikuwa imepanga kucheza mjini Tanga WIKIENDI HII lakini kutokana na mabadiliko ya programu ya mazoezi ya benchi la Ufundi, Wekundu wa Msimbazi sasa watabaki Arusha hadi Septemba nne mwaka huu ili kukamilisha programu yote bila ya usumbufu.

Hali ya kikosi cha Simba ni ya utulivu kabisa na mazoezi yanafanyika kwa mchanganyiko wa mazoezi ya uwanjani na GYM.

Hakuna majeruhi yoyote hadi sasa na wachezaji wote wanafanya mazoezi kama kawaida.

Juma Kaseja

Kwenye mechi mbili za kirafiki zilizopita jijini Arusha, mlinda mlango namba moja wa Simba, Juma Kaseja, hakudaka na badala yake waliodaka ni Wilbert Mweta na Waziri Hamadi Mwinyiamani.

Kudaka kwa makipa hao ni mipango tu ya mwalimu na Kaseja hana maumivu yoyote na anafanya mazoezi kwa nguvu sana kujiandaa na msimu ujao.

Kama ilivyo ada, Kaseja atadaka siku ambayo mwalimu ataamua akae langoni

Felix Sunzu

Kuna baadhi ya vyombo vya habari vimeanza kuandika vichwa vya habari vyenye lengo la kuuza magazeti kutokana na kufiwa kwa mchezaji wetu huyu.

Simba SC inapenda kutumia nafasi hii kuviomba vyombo vya habari na wadau wengine kumuacha mchezaji huyu aomboleze msiba huu na siku yake ya kurudi itakapofika, klabu itatangaza.

Mussa Mudde

Simba SC inafahamu kiu ya vyombo vya habari kuhusiana na kutaka kujua masuala ya usajili wa wachezaji wake wa kigeni. Ukweli ni kwamba taarifa yoyote itakayotoka leo au kesho itakuwa haijaiva bado na klabu isingependa kutoa taarifa ambazo hazijaiva bado.

Tutatoa taarifa rasmi na kamili wakati mchakato mzima utakapokuwa umekamilika. Kwa hiyo, Simba haitatoa tamko lolote kwa sasa kuhusu usajili wa wachezaji wake wa kigeni hadi kila kitu kikamilike.

Tunaahidi kwamba hilo litafanyika haraka iwezekanavyo ili kiu yenu itimizwe.

Tunatanguliza shukrani

Imetolewa na

Ezekiel Kamwaga
Ofisa Habari
Simba SC
30/08/2012

August 30, 2012

JESHI LA POLISI MAKAMBAKO LAWASHIKILIA WAWILI KWA KUGOMA KUHESABIWAMwandishi wa mtandao wa www.francisgodwin.blogspot.com Condeadi Mpila toka Makambako ana ripoti......Ikiwa imesalia sikumoja kumalizika kwa zoezi la Sensa Jeshi la Polisi Mkoani jombe lina wa shikilia wakazi wawili wa Halmashauri ya Mji wa Makambako kwa tuhuma za kugoma kuhesabiwa.

Kamanda wa Polisi Mkoani Njombe Kamishina msaidizi wa Polisi Bw Fulgence Ngonyani amewawataja wanao shikiliwa kuwa ni Bw Athuman saidi kivanga[32]mkazi wa kahawa mji mwema na Yasisin shaibu[32]mkaziwa wa kipagamo mjini makambako.

Bw. Ngonyani alisema watuhumiwa kwa makusudi wakiwa wanafahamu kuwepo kwa sensa ya watu na makazi iliyoanza rasmi Agosti 26 kitaifa wao kwa nyakati tofauti Agosti 29 walikataa kutoa taarifa zao kwa makarani kwa kisingizio cha imani yao na msimamo wa dini yao.

Alisema kwa kuwa ni kinyume cha sheria kugoma na kuhesabiwa kwa kisingizio cha imani ya dini yao ni imani potofu zozote kwa mujibu wa sheria zinazotawala.

Watuhumi wote wawili leo watafikishwa mahakamani kujibu shitaka linalowakabili.

BREAKING NEWS.....DC WA ZAMANI WA MBARALI HAWA NGURUME AFARIKI DUNIA

Rais Jakaya Kikwete amlilia Ngurume

Marehemu Hawa Ngurume

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ametuma Salamu za Rambirambi kwa Familia ya aliyepata kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Mama Hawa Ngulume kufuatia taarifa za kifo chake kilichotokea katika Hospitali ya Jeshi Lugalo, Jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa kwa matibabu akisumbuliwa na ugonjwa wa Saratani. Mama Hawa Ngulume amefariki leo tarehe 30 Agosti, 2012.

Katika Salamu zake hizo, Rais Kikwete amesema Marehemu Hawa Ngulume, enzi za uhai wake, alikuwa kiongozi shupavu aliyesimamia maamuzi yake katika majukumu muhimu ya kitaifa kwa lengo la kuwaletea wananchi maendeleo katika sehemu zote alizotumikia akiwa Mtumishi wa Umma, na baadaye alipopewa wadhifa wa Mkuu wa Wilaya alioutumikia katika Wilaya za Singida Mjini katika Mkoa wa Singida, Kinondoni Mkoani Dar es Salaam na mara ya mwisho katika Wilaya ya Mbarali, Mkoani Mbeya.

“Nilimfahamu Marehemu, enzi za uhai wake, kama Kiongozi Mwanamke shupavu aliyesimamia kikamilifu maamuzi yake, na hivyo kuthibitisha ukweli kwamba wanawake wakipewa fursa wanaweza”, amesema Rais Kikwete katika kuomboleza kifo chake.

“Kutokana na msiba huo mkubwa, natuma Salamu za Rambirambi kutoka dhati ya moyo wangu kwa Familia ya Marehemu, Mama Hawa Ngulume kwa kuondokewa na Mhimili muhimu na Kiongozi wa Familia. Natambua machungu mliyo nayo hivi sasa kwa kumpoteza Mama wa Familia, lakini nawahakikishia kuwa niko pamoja nanyi katika kuomboleza msiba huu mkubwa”, ameongeza kusema Rais Kikwete katika Salamu zake.

Rais Kikwete amewataka wanafamilia ya Marehemu wawe na moyo wa uvumilivu na ujasiri wakati huu wanapoomboleza msiba wa mpendwa wao kwani yote ni Mapenzi yake Mola. Amesema anamuomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema aipokee na kuilaza mahala pema peponi Roho ya Marehemu Mama Hawa Ngulume, Amina.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu.

Dar es Salaam.

30 Agosti, 2012

KAMANDA UVCCM IRINGA AWAPA SOMO VIJANA IRINGA VIJIJINI

kamanda wa UVCCM wilaya ya Iringa vijijini Arif Abri akifungua mkutano wa uchaguzi wa UVCCM wilaya ya Iringa vijijini leo
Wajumbe wakiwa wamependeza kwa sare zilizotolewa na kamanda huyo na mbunge Lukuvi na Mgimwa
Waandishi wakipewa kadi za CCM Leo


CHANGAMOTO imetolewa kwa vijana wa Chama cha mapinduzi ( UVCCM) wilaya ya Iringa vijijini mkoani Iringa kufanya kazi kwa kujituma zaidi badala ya kuendelea kulalamika vijiweni bila kufanya kazi.

Changamoto hiyo imetolewa Leo katika ukumbi wa Sekondari ya Mwembetogwa mjini Iringa na mgeni rasmi katika mkutano mkuu wa uchaguzi wa UVCCM ambaye pia ni kamanda wa UVCCM wilaya ya Iringa vijijini Arif Abri .

Abri amesema kuwa hivi sasa imejitokeza tabia ya vijana kulalamika juu ya hali ngumu ya maisha hata kuhoji juu ya maisha bora huku sehemu kubwa ya vijana hao wakiendelea kushinda vijiweni jambo ambalo ni kinyume na harakati za kujitafutia maisha bora kwa kila mtanzania.

Hata hivyo amewataka vijana hao kuendelea kujishuguulisha na shughuli za Uzalishaji mali ikiwa ni pamoja na kujiunga katika vikundi vya kiuchumi ili kuiwezesha serikali kuweza kuwasaidia mikopo yenye masharti nafuu.

Abri amesema kuwa vijana ambao ni tegemeo kubwa katika Taifa bado wanalojukumu kubwa la kuendelea kuwavuta vijana wenzao ambao wanakimbilia vyama vya upinzani.

wakati huo huo Abri amewapongeza wanahabari watano mkoani Iringa ambao wamejiunga na UVCCM wilaya ya Iringa vijijini.

Katibu wa UVCCM wilaya ya Iringa vijijini Frank Kibiki aliwataja wanahabari walioniunga na CCM kuwa ni meneja wa IT Ebony Fm Eliud Kalokola , Flora Kamaghe kutoka gazeti la Uhuru, Zuhura Zukheli kutoka radio Qibra ten ,Wiliam Muro kutoka gazeti la kwanza jamii na NEEMA Mgulanga mwanahabari wa kujitegemea .

MWISHO

UVCCM IRINGA VIJIJINI KUPATA VIONGOZI WAKE LEO


wajumbe wa mkutano mkuu wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Iringa vijijini wakiwa katika mkutano mkuu wa uchaguzi ndani ya ukumbi wa Mwembetogwa mjini Iringa

RC IRINGA AFUNGUA KIKAO CHA RCC AONYA HALMASHAURI

Mkuu wa mkoa wa Iringa Dkt Christine Ishengoma akifungua kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa (RCC)
Wajumbe wa kikao cha RCC mkoa wa Iringa wakiwa katika kikao hicho katika ukumbi wa Siasa ni kilimo asubuhi hii