Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

June 30, 2012

TRAFIKI MKOA WA MBEYA WALIVYOGEUZA KAZI HIYO MTAJI ,KILA KONA WAPO ILA BADO AJALI KILA WAKATI

Askari wa usalama barabara mkoa wa Mbeya wakiwa wametega eneo la Igawa
Mmoja kati ya madereva akikabidhi kitu kidogo kwa askari wa usalama barabarani
Askari hawa wakisubiri magari kama walivyonaswa na kamera ya mtandao huu
Hapa ni eneo la Chimala mizani askari wakiwa kila kona
Hapa ni mbele kidogo na Chimala
Mkuu wa usalama barabarani Taifa naomba kuuliza hivi ni uwepo huu wa askari wa usalama barabarani mkoa wa Mbeya ni kwa faida ya nani hasa ? mbona ni kundi kubwa ya askari ila ajali kila wakati na madereva bado wanakosa imani na askari hawa ambao wanatajwa kuongoza kwa rushwa? pili ndio kusema hakuna kazi nyingine ya kufanya askari hawa ?

Wadau nitawaletea ripoti kamili ya vitendo vya askari wa usalama barabarani mkoa wa Mbeya jinsi wanavyosumbua barabarani kuliko mikoa yote ya Tanzania

AJALI KAMA HIZO ZINATOKANA NA UCHAKAVU WA MABASI PIA

Basi chakavu linalofanya safari zake kati ya Mafinga na Mdabulo wilaya ya Mufindi likiwa limekwama baada ya kushindwa kupanda mlima

DEIDRE LORENZ KAINGIA KWENYE MAPENZI NA TANZANIA


Marathon 1991 Onesmo Ngowi baada ya kukimbia mbio hizo

Mcheza sinema maarufu wa Marekani Deidre Lorenz ameahidi kuleta wacheza sinema wenzake na kushiriki kwenye mbio za mwaka kesho za mt. Kilimanjaro Marathon zitakazokuwa zinatimiza miaka 23 tangu zianzishwe mwaka 1991.

Lorenz aliyekimbia mbio za mwaka huu ambazo zilipewa jina la “mbio za kutimiza miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika” na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) amesema kuwa atakuja na timu yake ya wapiga picha ili kupiga picha vivutio kadhaa vya Tanzania ikiwa ni pamoja na mlima Kilimanjaro. Qwiji hili la sinema za Santorini Blue, The Great Fight, Perfect Strangers na nyingine nyingi ameelezea kuipenda sana Tanzania. “Sikutegemea kuikuta nchi nzuri kama hii” alisema mcheza sinema huyo ambaye ameshawahi kuchaguliwa zaidi ya mara 4 kugombea tuzo maarufu za Oscar. “Sasa nimeamini kuwa mlima Kilimanjaro ni mali ya Tanzania na nitautangaza katika sinema zangu zote”aliendelea kusema Deidre Lorenz.mcheza sinema huyu ambaye ameingia kwenye mkataba na kampuni kubwa ya Google hivi karibuni ili kuuza sinema zake katika mtandao aliielezea Tanzania kama nchi nzuri na yenye watu wakarimu sana. Mbio za Mount Kilimanjaro Marathon zilianzishwa mwaka 1991 na Marie Frances anayetoka katika jiji la matajiri la Bethesda nchini Marekani baada ya kuombwa na balozi wa zamani wa Tanzania nchini Misri. Tangu kuanzishwa kwake mbio hizi zimekuwa zinaleta watalii matajiri katika mji wa Moshi kupanda mlima Kilimanjaro na kukimbia mbio hizi zinazojulikana kama Seven Continental Races.

Hakuna masharti yote ya kukimbia mbio hizi na watanzania wanaoshiriki katika mbio hizi huwa hawatozwi pesa za kiingilio.

Kwa kutambua mchango wake katika uchumi wake Manispaa ya Moshi iliibadilisha jina barabara ya zamani ya Bustani Ale na kuiita Marie Frances Boulevard ili kumuenzi mama huyu aliyejitolea maisha yake kuutangaza mlima Kilimanjaro.“Kila siku napokea ujumbe kutoka nchi mbalimbali niende huko kuanzisha mbio za marathon lakini kwa sasa basi” alisema mama huyo aliyekuwa mtayarishaji wa vipindi vya televisheni ya ABC kabla ya kunzisha Mt. Kilimanjaro Marathon.

Alisema kuwa mwaka jana yeye na Rais wa klabu ya Mt. Kilimanjaro Marathon mtanzania Onesmo Ngowi walifanya makubaliano ya Ethiopia Airlines (ET) jijini Addis Ababa kuzifanya mbio hizo kuwa za kimataifa zaidi. “ET walikubali kutoa ufadhili kwetu na pia kugharamia kushiriki kwetu katika mbio za New York Marathon, Boston Marathon na Los Angelos Maratthon ili kuitangaza vyema Tanznaia” alibainisha Frances.

Katika makubaliano hayo, Ngowi na Frances pia wataanzisha mbio za “King Solomon Marathon” zitakazofanyika katika jiji la Addis Ababa nchini Ethiopia.

Deidee Lorenz amefungua pazia kwa watu mashuhuri kushiriki katika mbio za marathon nchini Tanzania na ni jukumu la Watanzania kuchangamkia fursa zinazoletwa na ujio wao.Imetumwa na:Grace Soka

Afisa Uhusiano

MT. KILIMANJARO MARATHON 1991

SAFARI NI SAFARI KUFIKA NI MAJALIWA

Wakazi wa Rungwe mkoani Mbeya wakiwa wamepanda katika lori wakisafiri kwenda vijijini japo hapa naweza kusema safari ni safari kufika ni majaliwa

NI MAISHA BORA AMA BORA MAISHA ?

Hii ni nyumba ambayo inatumika ni vigumu kuamini ila elewa hivyo

Safari ya kufanikiwa katika maisha bora kwa kila mtanzania ama kwa viongozi pekee

Hii ni nyumba ya mmoja kati ya wakazi wa kijiji cha Igoda wilaya ya Mufindi mkoani Iringa ni vigumu kuamini kama ni kweli bado watanzania wapo kwenye safari ndefu ya kusaka maisha bora na pia waweza kujihoji kuwa hayo ni maisha bora ama bora maisha ?

MUSTAFA HASSANALI AWAZAWADIA WASHINDI MISS DAR INTERCOLLEGE 2012

Mbunifu wa mavazi wa kimataifa Mustafa akimkabidhi zawadi ya gauni lenye thamani ya shilingi 500,000 Miss Dar Intercollege 2012 Hilda Edward ofisini kwake leo, anayeshuhudia ni mratibu wa shindano hilo, Dina Ismail.


Mbunifu wa mavazi wa kimataifa Mustafa akimkabidhi zawadi ya gauni lenye thamani ya shilingi 300,000 Mshindi wa pili wa Miss Dar Intercollege 2012 Jamila Hassanofisini kwake leo, anayeshuhudia ni mratibu wa shindano hilo, Dina Ismail.
Mbunifu wa mavazi wa kimataifa Mustafa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa kitongoji cha Miss Dar Intercollege katika shindano la Miss Higher Learning 2012, Hilda Edward na mshindi wa pili Jamila Hassan pamoja na mratibu Dina Ismail ofisini kwake leo,

HALI YA DK STEVEN ULIMBOKA NI MBAYA APELEKWA INDIA KWA MATIBABU ZAIDI

Wananchi wakiwa na hamu ya kumuona Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Steven Ulimboka wakati gari lililombeba likiwa limesimama katika lango la kuingilia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam leo, tayari kusafirishwa kwenda India kutibiwa baada ya hali yake kuzidi kuwa mbaya. Picha zaidi uk. wa 3. (NA KAMANDA WA MATUKIOBLOG)
Wanaharakati wakiwa na mabango walipokwenda Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam leo, kumsindikiza Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Steven Ulimboka aliyekuwa anasafirishwa kwenda India kutibiwa baada ya hali yake kuzidi kuwa mbaya( na Full Shangwe Blog)

MWANARIADHA WA JESHI AGOMEA KAMBI OLIMPIKI

KOCHA wa Riadha wa Timu ya Tanzania inayotarajiwa kushiriki mashindano ya Olimpiki London, Julai 27 hadi Agosti 12 mwaka huu, Zakaria Gwandu, ameelezea kusikitishwa na kushangazwa kwa mchezaji Faustine Mussa kutojiunga na wenzake kambini, Mkuza Kibaha.

Akizungumza na Mwandishi wa Habari hizi Gwandu, alisema, wakati timu ikitarajiwa kuondoka nchini Julai 8 mwaka huu, Mussa ambaye ni mwajiriwa wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), ndiye pekee hawajatia mguu kambini hapo, jambo linalomweka katika wakati mgumu wa kutekeleza programu zake.

“Kwa kweli sielewi kinachoendelea kuhusiana na mchezaji huyu Faustine Mussa, sijui tatizo ni kwa mchezaji au mwajiriwa wake, kwani barua ya kuombewa ruhusa Chama cha Riadha (RT), kilikwisha ituma kwa mwajiri wake muda mrefu, lakini mchezaji hadi sasa hajatokea kambini,” alilalamika Kocha huyo.

Timu ya riadha itakayoshiriki michezo ya Olimpiki London nchini Uingereza, inaundwa na wachezaji wanne, Zakia Mrisho, Samson Ramadhani, Msenduki Mohamed na Faustine Mussa, ambaye bado hajaripoti kambini.

SHANGINGI LA MLALAHOI

mtoto mkazi wa Luhunga katika wilaya ya Mufindi akitengeneza taili la baiskeli yake ya kienyeji maarufu kwa jina la kigereti na hiki kwao ni sawa na shangingi
Hapa imetengemeea tayari kwa safari
Hapa vipi wadau imekaa poa ?

WAKALI BONGO MOVIE WAWAKUMBUKA WAGONJWA HOSPITAL YA BOMBO TANGAWasanii wa Bongo Movie wakiongozwa na Mwenyekiti wao Jacob Steven "JB" wakiwa kwenye picha ya pamoja na Muuguzi Msaididi wa Hospitali ya Rufaa ya Bombo jijini Tanga.Wasanii hawa wametembelea Hospitali ya Bombo mapela leo asubuhi kwa ajili ya kukabidhi msaada wa Vyandarua katika hospitali hiyo,ikiwa ni sehemu ya kupiga vita ugonjwa wa Malaria unaopoteza maisha ya watanzania wengi katika maeneo mbali mbali ya nchini.Msaada huo umekabidhiwwa hospitalini hapo kwa hishani ya kampuni ya Bia Tanzania Kupitia kinywaji Chake cha Grand Malt ambao ni wadhamini wakuu wa Tamasha la Filamu za Kitanzania (Bongo Movie) linalozinduliwa leo hii kwenye Viwanja vya Tangamano Jijini Tanga.Picha na Othman Michuzi
Wasanii wa Bongo Movie wakiwa wamezunguka kitanda cha Mmoja wa Mama aliejifungua watoto Mapacha katika Wodi ya Wazazi wa Hospitali ya Bombo Jijini Tanga mapema leo asubuhi wakati walipofika kutoa Msaada wa Vyandarua kwa hisani ya Kampuni ya Bia Tanzania kupitia Kinywaji chake cha Grand Malt ambao ni wadhamini wakuu wa Tamasha la Filamu za Kitanzania (Bongo Movie) linalozinduliwa leo hii kwenye Viwanja vya Tangamano Jijini Tanga.Picha na Othman Michuzi

Msanii wa Bongo Movie,Mayassa Mrisho akikabidhi Chandarua kwa Mama aliejifungua watoto mapacha kwenye hospitali ya Bombo,Tanga mapema leo asubuhi.Picha na Othman Michuzi.

HAPPY BIRTHDAY YA KHADIJA MKADAMU YAFANA NDANI YA SANTORIN BEACH MJINI LINDI

Keki ya Birthday ya khadija Mkadamu
MTOTO WA KHADIJA MKADAMU NA MTOTO WA MWANAHAMIS
MKADAMU WAKICHEZA KIDUKU KATIKA SHEREHE YA KUMPONGEZA MAMA YAO
KUTIMIZA MIAKA 34

ARAFA WAD AU NAO HAWAKUWA NYUMA KATIKA ,MAMBO FULANI NDANI YA SANTORIN BEACH TAREHE 29 JUNE NI SIKU AMBAYO KHADIJA MKADAMU aka AJUZA Akifurahia kutimiza miaka 34 toka azaliwe PICHA NA ABDULAZIZ VIDEO
MTOTO KHADIJA MKADAMU aka AJUZA WA MIKUMBI AKIKATA
KEKI KATIKA SHEREHE YA KUTIMIZA MIAKA 34 ILIYOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA
SANTORIN BEACH BAR NDANI YA MANISPAA YA LINDIAMU

REDDS MISS UBUNGO 2012 NI IRENE SIZARI

Redds Miss Ubungo 2012, Irine Sizari (katikati) akipunga mono baada ya kuvukwa taji hilo na kupata tiketi ya kushiriki Miss Kinondoni 2012. Kushoto ni Mshindi wa Pili, Mwantumu Mustafa na kulia ni Mshindi wa tatu, Antonia Nyaragwinda. Shindano hilo limefanyika Juni 29, 2012 kuamkia Juni 30.(na Blog ya Full Sangwe)

RAIS KIKWETE AKUTANA NA WATENDAJI WAKUU WA MAKAMPUNI MBALIMBALI YA KIMAREKANI WANAOTEMBELEA TANZANIA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na Watendaji Wakuu wa Makampuni mbalimbali kutoka Marekani walipomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 30, 2012 katika ziara yao ya siku kadhaa ya kuvumbua tanzania (Discover Tanzania VIP CEOs tour) iliyoandaliwa na ubalozi wa Tanzania Marekani. Hii ni mara ya pili kufanyika ziara kama hii, ambapo pamoja na kuwakaribisha tena Rais Kikwete alisema amefurahishwa sana kwa wageni hao kuchagua kutembelea hifadhi za wanyama za kusini mwa nchi (Selous na Ruaha) vyenye wanyama wengi na vivutio ambavyo havipatikani kwingine kokote kama vile makundi ya mbwa mwitu ambayo kwa muda mrefu sasa yametoweka mbuga za Kaskazini.

PICHA NA IKULU

HII NI AIBU KUBWA KWA WABUNGE WASIO NA MADEREVA

Spika wa bunge Anne Makinda
BAADA ya kushindwa kuwalipa madereva wao aibu nyingine yaibuka kwa kwa wabunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania ni baada ya baadhi ya wabunge hao ambao walikuwa wakijiendesha wenyewe kudaiwa kuwatumia madereva wasio na sifa (madeiwaka) kuwaendesha pindi wanapokwenda bungeni kama njia ya kuficha aibu ya kujiendesha wenyewe.

Pamoja na wabunge hao kukwepa aibu hiyo ya kujiendesha bado baadhi ya wabunge ambao wamekuwa wakiongoza kwa kuwalipa fedha chini ya kiwango madereva hao wametishia kuwafukuza kazi madereva wao iwapo watatoa siri ya malipo kidogo wanayolipwa kwa sasa jamboleo jumapili limeelezwa.

Madereva hao wameueleza mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com kuwa baada ya kutolewa kwa siri ya malipo ambayo wabunge hao wamekuwa wakiwalipa madereva ,wabunge hao wamekuwa wakiwatolea vitisho mbali mbali kwa madai kuwa malipo kidogo ambayo wanalipwa kwa sasa ni makubaliano ya wawili hivyo iwapo siri hizo zitavuja kwa vyombo vya habari basi watafukuzwa kazi .

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa sharti la kutotaja majina yao madereva hao walisema kuwa wabunge hao wameanza kutoa vitisho mbali mbali kwa madereva wao kwa madai kuwa iwapo watawataja majina wataharibu sifa kwa wapiga kura wao .

Alisema mmoja kati ya madereva hao kuwa iwapo wabunge hao wataendelea kuwapunja maslahi yao basi watakosa uvumilivu dhidi yao na badala yake watawaanika majina yao kama ambavyo walivyo kusudia kufanya hivyo kama njia ya kudai haki yao.

Kuwa kama wabunge hao watachukia na hatua hiyo basi watawaachia magari yao huko huo bungeni na wao kurudi majimboni kufanya kazi za kilimo badala ya kuendelea kutumikishwa bila malipo ya maana .

“Tunaomba wabunge wetu ambao ndio mabosi wetu kuwa na huruma na kuacha vitisho kwetu …kwani iwapo tutafanya kazi kwa kutishana sisi madereva ndio ambao tunaweza kuwatisha wao zaidi kwani siri zao zote tunazijua na hatutaki kuzitoa sasa ila kama watatumia jazba na kutufukuza basin a sisi tutaona ni vema liwalo na liwe tutawaanika”

Kwani alisema kuwa kwa kuwa sehemu kubwa ya madereva hao wanaopunjwa haki yao ni wabunge wanatokea katika majimbo husika iwapo mbunge atawafukuza kazi kwa wao kusema ukweli juu ya posho ndogo wanazowalipa basi watakwenda kuwashtaki kwa wapiga kura majimboni .

“Hata hapa tunavumilia tu kwani siri za wabunge sisi ndio tunaozitunza sasa wao kama watatanguliza hasira mbele badala ya utu sisi tutakwenda mwaga sumu majimboni kwani wakiwa majimboni wanajisifia kuwa wametoa ajira kwa vijana kwa kazi hiyo ya udereva wakati hawatulipi chochote”

Undani wa habari hii utausoma kesho katika gazeti la Jamboleo jumapili

FAN CITY LODGE NA NAF BLUE VIEW HOTEL MTWARA NI WADHAMINI WAKUU WA UZINDUZI WA ALBAM YA HAKUNA JIPYA YA MSANII MASANJA MKANDAMIZAJI IRINGA

Uzinduzi huo wa albamu ya hakuna jipya chini ya juu iliyoimbwa na msanii nguli Emanuel Mgaya a.k.a Masanja Mkandamizaji wa orijino komedy itazinduliwa katika uwanja wa Samora Iringa siku ya tarehe 15 /7/2012 ,mbali ya Naf Blue View Hotel na Fan City Lodge wadhamini wengine ni mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com ambao utarusha Live uzinduzi huo,Radio Ebony Fm, Overcomers Fm na mbunge wa viti Maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati (CCM) wadhamini wengine bado mnakaribishwa

MISS REDD'S IRINGA NI AIBU TUPU , CHIFU JAJI AZOMEWA UKUMBINI

Huyu ndie Naomi James ambaye ametawazwa usiku huu kuwa Miss Redd's mkoa wa Iringa na kuzawadiwa kitita cha shilingi 500,000
Mshindi wa taji la Miss REdd's 2012 mkoa wa Iringa Naomi James kati kati akiwa na mshindi wa pili Sarah Utiku na Catherine Mfupi ambaye ni mshindi wa tatu mara baada ya kutangazwa usiku huu ndani ya ukumbi wa Highlands mjini Iringa
Msaidizi wa chifu jaji msomi Saimon Belenge akiokoa jahazi lisizame baada ya wadau wapenzi na mashabiki wa onyesho hilo kuanza kumzomea chifu jaji Bw Tasha Jimi ambaye ni mratibu wa Miss Redd's mikoa ya kusini baada ya kuchemka kutaja namba ya mshindi wa pili katika onyesho hilo
Hawa ndio waliopenya nafasi ya tano bora kati ya washiriki 12 waliopanda jukwani wa kwanza kushoto ni Amisa Zuber, SArah Utiku, Naomi James ,Winfreda Felix na Catherine Mfupi
Wadau wa urembo leo wakiwa wamevalia nguo za heshima kiasi
Warembo wakiwa katika picha ya pamoja na washindi na washiriki wa onyesho hilo
Mgeni rasimi Naibu meya wa Manispaa ya Iringa Gervas Ndaki ( wa pili kushoto) akiwa na afisa michezo na utamaduni Manispaa ya Iringa Bw.Kadinde na mratibu wa onyesho hilo Bw Dosi
Hawa ndio majaji wa onyesho hilo katikati ni Tasha Jimbo aliyetaka kuvuruga onyesho dakika za mwisho
Msomi Saimon Belege (kulia) akicheka baada ya chifu jaji kushoto TashaJimy kuvuruga kazi yao
Madau Saimon Belege akiwa na mshindi wa taji la Miss Iringa mwaka jana na mshindi wa leo katika shindano ya Redd's Miss Iringa Naomi James


Huyu ndiye Tasha Jimy aliyezomewa kwa kushindwa kujua tofauti kati ya namba 4 na mbili hivyo kujikuta akizomewa ukumbini.

Habari zaidi utaipata juu ya kasoro za onyesho hilo

June 29, 2012

BLOG MPYA MAALUM YA MISS UTALII TANZANIA/MISS TOURISM


Miss Utalii Tanzania, tofauti na mashndano mengine ya urembo, ni zaidi ya shindano la urembo, kwani linalenga katika kutangaza na kuhamasisha Utalii,Utamaduni, Mianya ya Uwekezaji,Elimu,Afya ya Jamii,Utalii wa ndani,Utalii wa kitamaduni,Utalii wa Michezo na Utalii wa Mikitano Kitaifa na kimataifa. Shindano hili pia linahamasisha vita dhidi ya Umasikini,Iharibifu wa mazingira,uwindaji haramu,Uvuvi Haramu,Ujinga,Maradhi, Tamaduni kongwe na Potofu. Miss Utalii Tanzania pamoja na uchanga wake, tangu kuanzishwa kwake mwaka 2005, ni shindano lenye mafanikio makubwa kuliko shindano jingine lolote nchini kitaifa na kimataifa kwani pamoja na kuipa heshima Tanzania ya kuwa wenyeji wa shindano la Dunia la Miss Tourism World 2006, shindano hili ndilo lililo andika historia ya Tanzania kutwaa taji la kwanza la Dunia kabla na baada ya uhuru, pale tulipo twaa taji la Miss Tourism World 2006, pia shindano hili ndilo pekee nchini linashikilia rekodi ya kutwaa mataji ya dunia katika kila shindano tulilo shiriki,tumetwaa mataji 6 ya dunia tangu 2005. Kutokana na mafanikio haya , Tumepewa heshima ya kuaandaa shindano la Dunia la Miss Umoja wa Mataifa mwaka 2013 hapa Tanzania. Ni shindano pekee nchini ambalo washiriki wake hawavai mavazi ya kuogelea, bali mavazi ya heshima yasiyo mdhalilisha mvaaji wala mtazamaji na yaliyo buniwa na kushonwa kwa malighafi za tanzania tu.
Link yetu ni : http://www.misstourismorganisation.blogspot.com


Facebook Page: https://www.facebook.com/MissUtaliiTanzania


E-Mail: missutaliitanzania@gmail.com
Asanteni sana.
Miss Tourism Organisation Tanzania.

YANGA KUANZIA KWA ATLETICO KOMBE LA KAGAME


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Mabingwa watetezi wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame) wataanza kutetea ubingwa wao Julai 14 mwaka huu dhidi ya Atletico ya Burundi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Nicholas Musonye ametangaza ratiba ya michuano hiyo leo (Juni 29 mwaka huu) katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Timu 11 zitashiriki katika michuano hiyo itakayoanza Julai 14 hadi 28 mwaka huu ambapo kwa siku zitachezwa mechi mbili (saa 8 mchana na saa 10 jioni) huku Tanzania Bara ikiwakilishwa na Yanga, Simba na Azam. Mechi ya kwanza siku ya ufunguzi (saa 8 mchana) itakuwa kati ya APR ya Rwanda na Wau Salaam ya Sudan Kusini.

Kundi A lina timu za Simba, URA ya Uganda, Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) na Ports ya Djibouti. Azam, Mafunzo ya Zanzibar na Tusker ya Kenya ziko kundi B.

Yanga inaunda kundi C lenye timu za APR ya Rwanda, Wau Salaam ya Sudan Kusini na Atletico ya Burundi.

Timu nane zitaingia robo fainali itakayochezwa Julai 23 na 24 mwaka huu. Kundi A na C kila moja litatoa timu tatu kwenda robo fainali wakati B litatoa timu mbili.

El Merreikh ya Sudan, Red Sea ya Eritrea, Coffee ya Ethiopia na Elman ya Somalia hazitashiriki katika mashindano ya mwaka huu ambayo yanafanyika Tanzania Bara kwa mwaka wa tatu mfululizo kutokana na sababu mbalimbali.

Coffee haitashiriki kwa vile ligi ya Ethiopia inaanza Julai 14 mwaka huu wakati El Merreikh wikiend ya Julai 13-15 mwaka huu itakuwa na mechi ya michuano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).

Bingwa wa michuano hiyo atapata dola 30,000, makamu bingwa dola 20,000 na mshindi wa tatu dola 10,000. Michuano hiyo itaoneshwa moja kwa moja (live) na Televisheni ya SuperSport.

KAGAME CUP 2012 FIXTURE

Sat. 14th July 1 APR vs WAU SALAAM Uwanja wa Taifa 2pm

2 YANGA vs ATLETICO Uwanja wa Taifa 4pm

Sun. 15th July 3 AZAM vs MAFUNZO Chamazi 4pm

Mon. 16th July 4 VITA CLUB vs PORTS Uwanja wa Taifa 2pm

5 SIMBA vs URA Uwanja wa Taifa 4pm

Tue. 17th July 6 ATLETICO vs APR Uwanja wa Taifa 2pm

7 WAU SALAAM vs YANGA Uwanja wa Taifa 4pm

Wed. 18th July 8 VITA CLUB vs URA Uwanja wa Taifa 2pm

9 PORTS vs SIMBA Uwanja wa Taifa 4pm

Thu. 19th July 10 ATLETICO vs WAU SALAAM Uwanja wa Taifa 2pm

11 MAFUNZO vs TUSKER Uwanja wa Taifa 4pm

Fri. 20th July 12 PORTS vs URA Uwanja wa Taifa 2pm

13 YANGA vs APR Uwanja wa Taifa 4pm

Sat. 21st July 14 AZAM vs TUSKER Uwanja wa Taifa 2pm

15 SIMBA vs VITA CLUB Uwanja wa Taifa 4pm

Sun. 22nd July REST DAY

QUARTER FINALS

Mon. 23rd July 16 B2 vs C2

17 A1 vs C3

Tue. 24th July 18 C1 vs A2

19 B1 vs A3

Wed. 25th July REST DAY

SEMI FINALS

Thu. 26th July 20 Winner 16 vs Winner 17

Thu. 26th July 21 Winner 18 vs Winner 19

Fri. 27th July REST DAY

FINALS AND 3rd PLACE PLAY OFFS

Sat. 28th July 22 Loser 20 vs Loser 21

23 Winner 20 vs Winner 21

Boniface Wambura

Ofisa Habari

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Powered by Sorecson : Creation de site internet