Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

May 31, 2012

PONGEZI KWA KAZI NZURI UNAYOIFANYA KWA JAMII

Mwanamke Edina Panzi aliyefungiwa na mhindi kwa kushindwa kulipa deni

Mim ni mmoja ya wanaotembelea blog yako mara kwa mara karibia kila siku napreciate kazi yako brother UNAFANYA KAZI NZURI KWA JAMII, MFANO HILO SAKATA LA HUYO MHINDI NA WAPO WENGI WANAO NYANYASA WATANZANIA WENZETU, ILA WAPIGANAJI WACHACHE KAMA NYIE, HONGERA SANA BROTHER ENDELEA HIVYOHIVYO JAPO KUNA CHANGAMOTO NYINGI KATIKA KAZI YENU,
BY MAISHA AMBANGILE
IFM - DSM imetumwa na Maisha Ambangile

Nb.Mmiliki wa mtandao huu wa www.francisgodwin na wadau wote tunaungana kukupongeza ndugu Maisha Ambangile kwa kutambua mchango wetu katika kuhabarisha kutoka moyoni tunasema ahsante kwa kupongeza si wote wanaweza kupongeza

Imetolewa na Francis Godwin mmiliki wa mtandao huu

Profesa Mbele Anasema: " Warembo Wengine Hawa Hapa!"

Siku chache zilizopita, niliweka makala kuhusu mrembo hapa katika blogu yangu. Lengo langu lilikuwa kuchochea mjadala kuhusu suala la urembo, ambalo, kama nilivyogusia, nimelijadili katika kitabu cha Africans and Americans: Embracing Cultural Differences.

Nimeona picha nyingine ya warembo katika mtandao wa Facebook, ambayo naileta hapa. Sisi tuliokulia vijijini Afrika tunaweza kusema kuwa ingekuwa bora kama hao warembo wangejisitiri vizuri zaidi kimavazi. Lakini huenda hao si wa-Afrika. Hapa Marekani, kwa mfano, wakati wa joto, watu wengi huvaa vivazi ambavyo kwetu tunaviona si vya heshima, lakini hapa wanaona ni sawa. Mtembelee:
http://hapakwetu.blogspot.com

KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE AHIMIZA UTUNZAJI MIRADI MKOANI RUVUMA

Kaimu Katibu Tawala wa wilaya ya Nyasa Bi Happy Msanga (kushoto) akikabidhi Mwenge wa uhuru kwa Kaimu Katibu Tawala wilaya ya Mbinga Bw.Iddi Mponda baada ya kumaliza mbio zake katika wilaya ya Nyasa.Tukio hili limefanyika leo katika kijiji cha Chunya wilaya ya Mbinga
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Kapteni Honest Mwanossa akichanganya mchanga ili kuweka jiwe la msingi la jengo la ofisi ya mkuu wa wilaya ya Mbinga hivi leo.


Watanzania wameaswa kutumia miradi mbalimbali ya maendeleo inayogharimu fedha za umma kiasi kikubwa ili iweze kudumu na kumsaidia Mwananchi kupiga hatua za maendeleo.

Mwandishi wa www.francisgodwin.blogspot.com kutoka Ruvuma Muhidin Amri anaripoti kuwa Rai hiyo Imetolewa jana na kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka huu Kapteni Honest Mwanossa wakati akifungua hosteli ya wasichana katika shule ya sekondari ya Mbambabay wilaya ya Nyasa mkoa wa Ruvuma.

Alisema si busara kuharibu miradi hiyo ambayo serikali imekuwa ikihangaika kutafuta fedha katika vyanzo mbalimbali badala yake watu wachache wanaotumia vibaya kuharibu miradi hiyo.

Kapteni Mwanossa alishauri kushirikisha wananchi katika shughuli zote za maendeleo ili wawe ni walinzi wa mali yao kuliko kuwatenga hali inayoweza kuleta manung’uniko .

Aliongeza kusema ikiwa viongozi wa serikali kuanzia kijiji,mtaa,kata na hatimaye wilaya na mkoa watawashirikisha wananchi katika miradi haiwezekani kuwa na matatizo kwani wananchi watailinda ili iendelee kunufaisha Jamii kwa kipindi kirefu na hii itasaidia kuondoa umasikini katika Jamii.

Kapteni Mwanossa aliwataka viongozi kuwa wa mfano miongoni mwao ili miradi inayoibuliwa na hatimaye kutekelezwa kwa kushirikiana na wananchi iwe bora na yenye thamani iliyokusudiwa.

Mwenge wa Uhuru upo mkoani Ruvuma na utakimbizwa katika Halmasahauri zote sita za wilaya na Manispaa ambapo miradi mbalimbali ya maendeleo inazinduliwa,kuwekewa mawe ya msingi,kukaguliwa na kufunguliwa.


WAZIRI LUKUVI AKUBALI KUWEKWA KITIMOTO NA WAPIGA KURA WAKE JUMAMOSI HII,WAZIRI DKT MGIMWA HOFU YATANDA

Mhe.Wiliam Lukuvi


WAZIRI wa nchi ofisi ya waziri mkuu (sera na uratibu wa bunge) Wiliam Lukuvi awa mbunge wa kwanza wa chama cha mapinduzi (CCM) kukubali kuwekwa kitimoto na wapiga kura wake katika mwendelezo wa midahalo ya wabunge na wapiga kura wao.

Lukuvi ambaye ni mbunge wa jimbo la Isimani amekubali kuwekwa kitimoto katika mdahalo huo uliopangwa kufanyika Juni 2 siku ya jumamosi katika ukumbi wa Hima kata ya Isimani majira ya asubuhi .

Hatua ya Lukuvi kukubali kuwekwa kitimoto imekuja huku zikiwa zimepita siku chache toka mbunge wa jimbo la Kilolo kupitia CCM Prof. Peter Msolla kukwepa kushiriki mdahalo kama huo uliofanyika katika ukumbi wa Upendo Ruaha Mbuyuni wiki iliyopita .

Mbunge Prof Msolla ambaye amepata kuwa waziri wa mawasiliano Sayansi na Teknolojia alikwepa mdahalo ulioandaliwa na azaki za kiraia mkoani Iringa chini ya uratibu wa asasi ya ISICO .

Mratibu wa midahalo hiyo Raphael Mtitu alisema kuwa midahalo hiyo ambayo ilianza kwa mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa(Chadema) imepangwa kufanyika majimbo manne ya mkoa wa Iringa na ambayo ni Iringa mjini ,Kilolo ,Kalenga na Ismani .

Hata hivyo aliwataka wabunge wote kushiriki katika midahalo hiyo ambayo imelenga kuwakutanisha wabunge na wapiga kura wao ili mbunge kuweza kueleza kile alichokifanya na wananchi kuhoji ama kupatiwa ufafanuzi juu ya ahadi zilizotolewa wakati wa kampeni ama mambo mbali mbali ya kimaendeleo ambayo yanafanyika ama hayafanyiki katika jimbo husika.

Mtitu alisema kuwa mtandao huo umeandaliwa na mashirika yasiyo ya Kiserikali katika Mkoa wa Iringa ( Iringa Civil Society Organization [ICISO- UMBRELLA]) kwa kushirikiana na mitandao ya AZAKI ya Halmashauri ya manispaa ya Iringa (Iringa Municipal Civil Society Organization – IMUCISO), Iringa vijijini (Iringa Rural Non-Governmental Organization – IRUNGO) na Kilolo (Kilolo District Non-Governmental Organzations Umbrella – KIDINGOU),

Pia alisema kuwa midahalo hiyo imelenga kuwaongezea uelewa wananchi ili waweze kushiriki kikamilifu katika masuala ya kijamii na kiuchumi yanayohusu ili waweze kumiliki michakato ya kuleta maendeleo yao badala ya kutegemea serikali na wahisani pekee.

Mradi huo utatekelezwa kwa njia ya makongamano, midahalo na mikutano ambapo itaandaliwa katika majimbo yao ya uchaguzi katika majimbo ya Kalenga, Isimani, Iringa mjini na Kilolo na Kila jimbo litafanyika midahalo isiyopungua minne.

Pia alisema kwa jimbo la Kalenga mdahalo kama huo utafanyika siku ya Juni 4 katika ukumbi wa Kijiji cha Ifunda kibaoni na kuwa waziri wa fedha na uchumi Dkt Wiliam Mgimwa atakutakana na wapiga kura wake

Hata hivyo aliwataka wabunge wote kushiriki katika midahalo hiyo inayowapa fursa wapiga kura kuongea na mwakilishi wao Mwenyekiti wa Halmashauri moja kwa moja ili waweze kutoa dukuduku zao na kuuliza maswali na kujibiwa papo hapo
· Wananchi wapate kujua shughuli alizozifanya/atakazofanya sehemu mbalimbali ndani ya jimbo/wilaya pamoja na utekelezaji wa ilania ya chama chake, ahadi za Rais pamoja na viongozi wengine wa kitaifa

Mtitu alisema midahalo hiyo haifungamani na itikadi ya chama chochote cha kisiasa na kuwa hata wananchi wanaofika katika midahalo hiyo hawapaswi kuja na bendera wala sare ya chama chochote cha kisiasa.
MWISHO

RAIS KIKWETE AFUNGUA MKUTANO WA BENKI YA MAENDELEO AFRIKA - AFDB


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua Mkutano wa Mkuu wa Mwaka wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Africa afDB katika ukumbi wa AICC jijini Arusha leo Mei 31. 2012(picha na Ikulu)
Wabunge Pamoja na Viongozi wa tawi la chadema Washington DC Watembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani

Baada ya kazi pevu ya uzinduzi wa tawi la Chadema jijini Washington Dc wabunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamtembelea rasmi Balozi wa Tanzania nchini Marekani.


Balozi wa Tanzania Nchini Marekani na Mexico Mhe. Mwanaidi Sinare Maajar akipata picha ya pamoja na Mbunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Peter Msigwa ndani ya Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani


Wabunge wa Chadema Mhe. Peter Msigwa wapili kushoto, Mhe. Nassari Joshua, Al-Marufu Dogo Janja, (Watatu kulia), ofisa wa ubalozi Mhe. Peter Msigwa, Kaimu Balozi Mhe Lilian Munanka pamoja na viongozi wa tawi la Chadema Washington Dc wakipata picha ya pamoja na balozi Mhe. Mwanaidi Sinare Maajar baada ya kumtembelea rasmi siku ya Jumanne Mei 29,2012 Washington Dc Nchini Marekani.Mbunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Peter Peter Msigwa akipata picha ya pamoja na waTanzania waishio nchini Marekani, ndani ya Ubalozi wa Tanzania Washington Dc. (Picha na swahilivilla.blogspot.com

Serikali ya Tanzania yasaini mkataba wa msaada wa Euro milion 10

NA GLADNESS MUSHI WA FULLSHANGWE-ARUSHA
Serikali ya Tanzania imesaini mkataba wa msaada wa euro million 10.
sawa na shillingI za kitanzania billion 19.9 kutoka serikali ya
Fanland kwa mwaka wa 2012 na 2013.

Akisaini mkataba huo waziri wa fedha Dk william Mgimwa amesema
serikali ya fanland imekuwa na huusiano wa mda mrefu na serikali ya
Tanzania na imeweza kusaidia miradi mbalimbali kwa lengo la kuinua
maisha ya watanzania kuondokana na umasikini.

Amesema miongoni mwa miladi iliyowahi kufadhiliwa na serikali ya
fanland ni pamoja na miradi ya kilimo,ambapo mradi huo uligalimu
kiasi cha euro million 9,mradi wa kuboresha upatikani wa umeme pamoja
na mradi wa kuboresha mawasiliano ICT uliogalimu euro million 5 pamoja
na miladi mingine kama mradi wa kufuga nyuki na mradi wa kutunza
misitu uligharimu euro laki 27,24,300.

Akizungumza na waandishi wa habari mbale ya waziri wa fanland Bibi
Haidi Hautala amesema serikali itahakikisha misaada hii inalenga
sehemu husika ili kuweza kuinua maisha ya watanzania katika maswala ya
kiuchumi.

Amehaidi serikali ya Fanland kuwa fedha hizo zitasimamiwa ipasavyo na
kwamba pamoja na chi ya Tanzania kukabiliwa na hali ya umasikini
lakini tadhimini itakuwa inatolewa kwa miladi husika ili pale
pakapohitajika msaada mwingine ulenge katika miladi mingine.

Serikali ya Tanzania yasaini mkataba wa msaada wa Euro milion 10

NA GLADNESS MUSHI WA FULLSHANGWE-ARUSHA
Serikali ya Tanzania imesaini mkataba wa msaada wa euro million 10.
sawa na shillingI za kitanzania billion 19.9 kutoka serikali ya
Fanland kwa mwaka wa 2012 na 2013.

Akisaini mkataba huo waziri wa fedha Dk william Mgimwa amesema
serikali ya fanland imekuwa na huusiano wa mda mlefu na serikali ya
Tanzania na imeweza kusaidia miradi mbalimbali kwa lengo la kuinua
maisha ya watanzania kuondokana na umasikini.

Amesema miongoni mwa miladi iliyowahi kufadhiliwa na serikali ya
fanland ni pamoja na miradi ya kilimo,ambapo mradi huo uligalimu
kiasi cha euro million 9,mradi wa kuboresha upatikani wa umeme pamoja
na mradi wa kuboresha mawasiliano ICT uliogalimu euro million 5 pamoja
na miladi mingine kama mradi wa kufuga nyuki na mradi wa kutunza
misitu uligharimu euro laki 27,24,300.

Akizungumza na waandishi wa habari mbale ya waziri wa fanland Bibi
Haidi Hautala amesema serikali itahakikisha misaada hii inalenga
sehemu husika ili kuweza kuinua maisha ya watanzania katika maswala ya
kiuchumi.

Amehaidi serikali ya Fanland kuwa fedha hizo zitasimamiwa ipasavyo na
kwamba pamoja na chi ya Tanzania kukabiliwa na hali ya umasikini
lakini tadhimini itakuwa inatolewa kwa miladi husika ili pale
pakapohitajika msaada mwingine ulenge katika miladi mingine.

MWANAMKE ALIYEMTUPA MTOTO CHOO CHA SHULE APATA DHAMANA.

MAHAKAMA ya wilaya ya Lindi,imempatia dhamana mshitakiwa Aluminata Alois Kimisa (38) anayekabiliwa na Shitaka la kujaribu kumuuwa mtoto wake mchanga aliyemzaa usiku wa mei 19 mwaka huu.

Mwandishi wa www.francisgodwin.blogspot.com kutoka Lindi Abdulaziz Video anaripoti kuwa ,Uamuzi wa kumpatia dhamana mshitakiwa huyo umetolewa mei 28 mwaka huu na Hakimu wa mahakama ya wilaya hiyo,Liliani Lugalabamo, baada ya kupitia vifungu mbalimbali vya Sheria.

Mshitakiwa Aluminata mei 22 mwaka huu,alifikishwa mahakamani hapo akikabiliwa na Shitaka la kujaribu kumuuwa mtoto wake kwa kumtumbukiza kwenye Shimo la Choo.

Akitoa uwamuzi huo,Hakimu Lugabamo akitumia ibara ya 6 na 7 ya Human right alisema kila mtu ana haki sawa mbele ya Sheria,hivyo kutokana na mshitakiwa ana mtoto mchanga ambaye anatakiwa kuwa karibu zaidi na mama anampatia dhamana,huku akiamuru kupatiwa mtoto wake kwa ajili ya kumnyonyesha.

Pia Hakimu huyo amemuagiza mshitakiwa huyo kuripoti mahakamani hapo kila siku ya ijumaa saa 2:30 asubuhi.

Mwanamke huyo amefikishwa katika mahakama ya mkoa huo,mei 22 mwaka huu,na kusomewa shitaka lake na mwanasheria wa Serikali, Juma Maige.

Aluminata alitinga mahakamani hapo, akiwa amevalia nguo aina ya vitenge na kujifunika kanga huku kichwani akiwa amefunika nywele zake kwa mzura wa rangi ya kahawia,huku dada zake wakiwa wamekibeba kichanga hicho.

Mwisho.

Bonanza la Michezo Arusha na wabunge wa Kenya

Mwenyeketi wa Arusha Wazee Danford Mpumilwa na watoto wake Rhoda na Tuli ambaye ameshavaa medali ya ushindi.
Captain wa timu ya Arusha Wazee Wilson akipokea kombe kutoka kwa Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Abdi. Katikati ni mwanakamati wa Wazee Guindo.

Ni wakati wa Kiduku na Mpumilwa
Kamati ya ufundi ya time ya Arusha Wazee Sports Club.

Timu ya Arusha Wazee (jezi nyekundu) na Wabunge wa Kenya baada ya mechi yao.

Tanzania ni Salama kwa Watalii


Kushoto ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyarandu akiwasisitizaa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuwa vurugu zilizotokea Visiwani Zanzibar hazikuathiri utalii visiwani humo. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Bw. Ibrahim Mussa.(picha na habari na
TulizoKilaga)

Kufuatia vitendo vya vurugu zilizozuka hivi karibuni katika maeneo kadhaa ya Mji wa Zanzibar baada ya mitandao ya kimataifa imekuwa ikiripoti taarifa za kuwepo kwa hali ya wasiwasi kwa watalii wanaotaka kuja kutembelea Visiwa hivyo.

Kama Waziri mwenye dhamana ya masuala ya Utalii, ningependa kuwahakikishia wageni, ambao tayari wako nchini, na wale ambao wanajiandaa kuja, kuwa vurugu hizo ambazo zimeshadhibitiwa na Serikali hazikuathiri utalii. Mjini Zanzibar pamoja na maeneo ya vivutio vya utalii kote nchini.

Hadi hivi leo napotoa taarifa hii, amani imetawala Mji Mkongwe Zanzibar na hakuna taarifa yoyote ya uharibifu wa maeneo ya vivutio vya utalii vya Zanzibar wala kuchomwa kwa hoteli ama kudhulika kwa raia yeyote wa kigeni. Hivyo nasisitiza kuwa Zanzibar nisehemu salama kwa watalii.

Vilevile, Siku chache kabla ya tukio la Zanzibar, kulikuwa na matukio manne ya watalii kuporwa katika maeneo ya Masaki jijini Dar es Salaam. Uporaji huo ulitendwa na watu waliokuwa kwenye magari au pikipiki ambao waliwapora watembea kwa miguu.

Serikali inawahakikishia wananchi na jumuiya ya kimataifa kuwa hayo yalikuwa matukio ya pekee na ya kimataifa kuwa hayo yalikuwa matukio ya pekee na ya kupita na hatua zimechukuliwa na Jeshi la Polisi kuongoza usalam kwa wakazi na watalii.

Nachukua fursa hii kuwahakikishia wageni kwamba kila juhudi zimechukuliwa kuhakikisha kuwa usalama wa watalii unadumishwa pamoja na faraja wakati watakapotembelea Tanzania.

Daima tukumbuke kuwa, Tanzania ni kisiwa cha amani na nchi imenuia kudumisha sifa hiyo nzuri.


Karibu Tanzania.

Mhe. Lazaro Nyalandu

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii
30 Mei, 2012


MEYA MANISPAA YA LINDI ALUMBANA NA MBUNGE WAKE.

Bw.Salum Khalfani Bar’wani,(MB)

WANANCHI katika Halmashauri ya Manispaa ya Lindi, wametakiwa kutomsikiliza pamoja na kupuuza kauli zinazotolewa na mbunge wa Jimbo hilo, Salum Khalfani Bar’wani,(CUF) kwa madai kwamba matamshi anayoyatoa yanawapotosha kwa lengo la kujitafutia umaarufu ya kisiasa.

Mwandishi wa www.francisgodwin.blogspot.com kutoka mkoani Lindi Abdulazizi Video anaripoti kuwa Kauli hiyo imetolewa na Meya wa Manispaa hiyo, Frank Magali (CCM) alipokuwa akihutubia wananchi katika uwanja wa Fisi mjini hapa,

Akihutubia wananchi waliojitokeza kumsikiliza, Magali akasema kauli anazotoa mbunge huyo kwamba hapati ushirikiano na uongozi wa Manispaa hiyo akiwemo mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Ahamadi Said Sawa pamoja na baadhi ya madiwani wake sio za kweli.

Meya huyo akasema Mbunge Bar’wani hakuna jambo lolote linalohusu maslahi ya wananchi, alilolifikisha katika Ofisi za Halmashauri hiyo na kukataliwa.

Akasema kuhusu hoja ya mikataba ya upatikanji wa matrekta matano kutoka Suma JKT haijafikishwa katika Ofisi ya mkurugenzi, hivyo kauli anazozitoa kuwa amekataliwa sio za kweli huku akimtaka mbunge huyo ampelekee Ofisini kwake muhutasari unaoonyesha kukataliwa kwa hoja yake kwenye vikao vyetu.

Meya huyo akatamba kwa kusema kama mbunge huyo atamuonyesha mkataba huo wa matrekta kutoka Suma JKT uliokataliwa yeye yupo tayari kujiudhuru nafasi aliyonayo.

Frank Magali akasema tayari kama Halmashauri ya Manispaa hiyo wameagiza matrekta manne ambapo moja kati ya hayo alidai tayari limeshafika na litapelekwa kata ya Msinjahili

“Ndugu zangu huyu mbunge wetu awaambii ukweli,kauli zote anazowaambieni sio za kweli kwani tayari halmashauri yetu imeshaanza zoezi hilo ili kuwaondolea wakulima tatizo la kutumia vijembe kidogo maarufu kwa jina la kingondola” Alisema Magari.

Kuhusu hoja ya Sh, 328.0 milioni zilizotolewa na Rais Jakaya Kikwete juu ya huduma ya maji kwa wakazi wa vijiji vya Chikonji na Kineng’ene, meya huyo akasema uongozi hawazitambui, bali wanachotambua ni Sh,325.0 milioni ambazo zipo kwenye mchakato.

Aidha,kwa upande wa kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa Hotel ya kitalii eneo la Mitwero Chuo cha Ufundi (Veta) meya huyo akasema tayari halmashauri hiyo imeshatenga hekari zisizopungua saba na kama kuna mfadhili yupo tayari kufanya hivyo milango ipo wazi.

Pia amewaomba wananchi pamoja na mbunge huyo kuondoa tafauti zilizopo na kuendelea kushirikiana kuleta maendeleo katika Jimbo lao la Lindi.

Baada ya matamshi hayo,mstahiki meya huyo alikaribisha maswali matatu,ambapo mwalimu Fadhili Makumbuli, alianza kwa kumrekebisha kauli zake kwa kusema Katika mikutano yake mbunge huyo hajazungumzia mikataba,bali alichokisema anakosa ushirikiano kutoka kwa uongozi wa manispaa hiyo, akiwemo na mkurugenzi huyo katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Jimbo la Lindi, ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa matrekta matano kama alivyoelekezwa na uongozi wa kampuni ya Suma JKT.

Pia, Makumbuli alitaka kufahamu matrekta hayo manne yalipitishwa katika kikao kipi cha Baraza la madiwani,au ni vipi walikaa kimya hadi mbunge huyo alipotoboa siri hiyo.

Hata hivyo mkutano huo haukuweza kumalizika kwa wakati uliopangwa baada ya wananchi kuanza kuzomea kwamba kauli anazozitoa ni za kutaka kujikosha mbele ya Jamii.

Katika mikutano mbalimbali anayoifanya mbunge Salum Bar’wani,amekuwa akilalamika kwamba anakosa ushirikiano na uongozi wa manispaa hiyo, wakiwemo na madiwani wa Chama cha tawala kwa kile anachokieleza ni kutokana na itikadi za kisiasa.