Matukio Daima

Tembelea kila siku kwa habari na matukio mbali mbali..

Matukio Daima

Kwa Habari za Kitaifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Kimataifa.

Matukio Daima

Kwa Habari za Uchumi na Biashara.

Matukio Daima

Kwa Habari za Michezo na Burudani.

April 30, 2012

MAJINGILI 3,030 WAKIWA NA RISASI 778 NA GOBORE 239 WAKAMATWA HIFADHI YA TAIFA YA RUAHA IRINGA

Askari wa wanyamapori katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha mkoani Iringa wamefanikiwa kukamata majangili 3,030 wakiwa na silaha aina ya Shotgun 15 gobore 239 na risasi 778.

Mkuu wa idara ya ulinzi katika hifadhi ya Ruaha Paul Gwaha aliyasema hayo wakati wa ziara ya wanahabari kutoka vyombo mbali mbali vya habari mkoani Iringa walitembelea hifadhi hiyo kama njia ya kuutangaza utalii wa mikoa ya kusini mwa Tanzania.

Alisema kuwa silaha hizo zimekamatwa katika misako mbali mbali inayoendelea katika hifadhi hiyo kwa kipindi cha mwaka 2008 hadi sasa na kuwa jumla ya mikuki 77 ,kokoro 4337 na mitumbwi 1589 imekamatwa pia katika eneo hilo la hifadhi ya Taifa ya Ruaha.

Mkuu huyo wa alisema kuwa katika msako huo jumla ya nyavu 29,978 ,ndoano 70184 na siala nyingine mbali mbali zilizokamatwa katika misako hiyo ni 117,961.

Mkuu wa hifadhi hiyo ya Ruaha Iringa Stepheno Qolli Alisema kuwa shughuli za ulinzi katika hifadhi hiyo zimekuwa zikifanywa na askari wa hifadhi kwa ushirikiano wa mradi wa ujirani mwema wa uhifadhi wa mali hai Idodi na Pawaga (MBOMIPA) .

Hata hivyo alisema kasi ya watalii wanaofika kutembelea hifadhi hiyo ya Ruaha bado si kubwa ukilinganisha na idadi ya watalii wanaotembelea hifadhi za kaskazini na kuwa bado kuna haja ya kuongeza nguvu zaidi katika kuzitangaza hifadhi hizo za mikoa ya kusini ikiwemo hifadhi ya Ruaha .

Kwani liasema kuwa hifadhi hiyo ya Ruaha Iringa ndio hifadhi inayoongoza kwa kuwa na wanyama wengi zaidi na ndio hifadhi ya kwanza kwa ukubwa Tanzania ila bado idadi ya watalii wanaofika kutembelea si nzuri sana .

KUMEKUCHA MISS UKONGA NA TABATA WAANZA KUJINOA

Miss Ukonga 2012 walio chuchumaa wakiwa katika picha ya Pamoja na wartembo wa Miss Tabata 2012 wakati walipofanya mazoezi ya pamoja jana.


WAREMBO wa vitongoji viwili vya Ukonga na Tabata jana walifanya mazoezi ya pamoja katika kuleta ushirikiano na kujenga urafiki baina ya warembo hao katika fani ya urembo.

Warembo wa Tabata waliwatembelea wenzao wa Ukonga katika kambi yao ya mazoezi iliyopo Ukonga Hill Tech Bar maeneo ya Minazi Mirefu au maarufu Banana.

Vitongoji vya Ukonga na Tabata warembo wake watakao shinda wanataraji kukutana katika Kambi ya kanda ya Ilala kabla ya kwenda kushiriki shindano la taifa la Miss Tanzania 2012.

Wakizungumza jana baadhi ya warembo wa Ukonga wamesema ushirikiano wao huo na wenzao wa Tabata unawapa uwezo wa kijiamini na kupata nafasi ya kujifunza kile ambacho wenzao wanakifanya au wamejifunza ikiwa ni pamoja na utembeaji, uongeaji wa kati wa kujitambulisha na vitu vingine vingi.

“Tunawashukuiru sana waandaji wetu, maana mbali ya kuwa tunapata wageni wa aina mbalimbali ambao ni wadau wa urembo lakini leo tupo na washiriki wenzetu wa tabata ambao tunaimani tutakutana katika shindano la Ilala”, alisema Amina Sangawe.

Nae Suzanne Deodatus ambaye ni Mshiriki kutoka Tabata alisema wamepata fursa ya kujifunza mambo kabdhaa na wamefurahi sana kuwatembelea warembo wa Ukonga na kufnya nao mazoezi ya pamoja.

Mapema Mwezi huu warembo wa Ukonga waliwasindikiza Miss Tabata 2012 katika show yao kubwa ya Utambulisho iliyofanyika katika Ukumbi wa Dar West Tabata.
Shindano la Miss Ukonga 2012 linataraji kufanyika Mei 5, mwaka huu na lile la Tabata linataraji kufanyika mapema mwezi Juni.zaidi bofya hapa

MASHINDANO YA 10 BORA WA MASUMBWI KUFANYIKA MAY 4

MASHINDANO ya kumi bora ya mchezo wa masumbwi yanatarajia kufanyikamei 4 katika ukumbi wa Panandi Panandi Ilala Dar es Salaam akizungumzana waandishi wa habari Kocha wa kimataifa wa mchezo wa Ngumi RajabuMhamila 'Super D' alisema vijana wengi wamejitokeza kushirikimichuano hiyo yenye lengo la kupanga viwango vya mabondia.


Aliwatajabaadhi ya mabondia watakaopambana siku hiyo ni Ibrahim Classatakaezichapa na IdiMnyeke, Amiri Macho atazidunda na West Scorpion,Charo Issa na HamisNassoro,Athumani Sadara na Abuu Mtambwe, Hassan Mijugu ataoneshanakazi na Saidi Ally, Sandari Nyambara na Pascal Ignus.


Pamoja na mapambano mengine yatakayokuwa katika uzito tofauti tofautivijana wengiwamejitokeza hivyo tunaomba sapoti ya aina yoyote kutoka kwa wadau wamchezo wa masumbwikufanikisha mashindano hayo yaliyoandaliwa na Kinyogoli Fondition kwaajili ya kuwapangakatika viwango mbalimbali vya ubora wa wachezaji,

Alitaja baadhi ya maitaji kwa siku hiyo ni kuwa maji kwa wachezajiwakati wakiwaulingoni,zawadi za kuwatia moyo wachezaji pamoja na madawa mbalimbaliyatakayotumika kwaajili ya kuwapatia mabondia huduma ya kwanza alisema Super D.Kwa yoyote mwenye nia ya kusaidi mashindano hayo kwa namna moja aunyingine anawezakuwasilianana kocha Mkongwe Habibu

Kinyogoli kwa namba ya simu 0655928298 auunaweza fika katika klabuya Amana CCM iliyopo Ilala Dar es Salaam vilevile waweza kuwasilianana kocha Super D0713/0787-406938 au unaweza fika Klabu ya Ashanti Iliyopo Ilala Sokola Mitumba kwa mawasiliano zaidi

MIAKA 50 YA UHURU NI ELIMU YA KIBONGO


mr FRANCIS pokea taarifa za kusikitisha ambazo bado zinapatikana katika Tanzania iliyo na uhuru zaidi ya miaka 50.hii shule ipo Kijiji cha Kitete Kata ya Uchindile Wilaya ya Kilombero Morogoro. ndugu mtazamaji naomba uangalie kwa makini hali halisi ya shule hii ya msingi ambayo ni miongoni mwa shule zilizopo hapa Tanzania milango na madirisha huwezi tofautisha kuwa kipi kinatofautiana na kingine .Hii ni dalili mbaya ambayo itamkatisha tamaa hata mwalimu ambaye utamwambia kuwa aende kufundisha serikali itazame vitu kama hivi.Je? hii ni shule au gofu.(picha na mdau
Adam Mgovano)

BREAKING NEWS.....MBUNGE WA JIMBO LA SUMBAWANGA MJINI AVULIWA UBUNGE NA MAHAKAMA

aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Sumbawanga Mjini kwa tiketi ya CCM Mhe. Aeshi Hillal akiwa katika mazungumzo waziri mkuu Mizengo Pinda (kulia)
aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Sumbawanga Mjini kwa tiketi ya CCM Mhe. Aeshi Hillal akiwa katika mazungumzo na Rais Jakaya Kikwete

Mahakama imetengua ubunge wa aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Sumbawanga Mjini kwa tiketi ya CCM Mhe. Aeshi Hillal hivyo kuanzia sasa jimbo hilo lipo wazi kwa ajili ya uchaguzi mwingine kama ilivyo kwa jimbo la Arusha mjini .

WANAUME TUWAJIBIKE


Babu mkazi wa jiji cha Tungamalenga wilaya ya Iringa vijijini akiwa amembeba mjukuu wake kama alivyonaswa na kamera ya mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com ,ama kweli wanaume tuwajibike kulea familia kama hivi

TRAFIKI IRINGA MPO ? BASI NUSURU LIUE ASUBUHI HII

Abiria wakishuka katika basi hilo baada ya kunusurika ajali

Hapa abiria wakijaribu kuzuia basi hilo la kampuni ya Upendo kwa mikono baada ya kutaka kugonga nyumba kwa kutokana na dereva kushindwa kukata kona
Basi hili kuu kuu linalofanya safari zake kati ya Iringa na Idete wilaya ya Kilolo asubuhi hii nusuru lisababishe ajali mbaya katika eneo la M.R barabara kuu ya Iringa -Dodoma mjini Iringa baada ya kushindwa kukata kona kutokana na ubovu wa basi hilo ,hivi Trafiki Iringa mnakagua mabasi haya ama mnangoja ajali zitokee ?

CHUO CHA ELIMU MKWAWA KUNANI?

Wanafunzi wa chuo cha elimu Mkwawa Iringa asubuhi ya leo wakiwa wametawanyika katika ofisi za mkuu wa chuo ,japo wanafunzi hao wamezuia wanahabari kushiriki katika mkusanyiko huo usio rasmi hivyo twajiuliza chuo cha elimu Mkwawa Kunani?

HIFADHI YA RUAHA IRINGA YAZIDI KUWAVUTA WANAHABARI IRINGA

Twiga akiwa katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha Iringa
Wanahabari Daud Mwangosi na Mahija Zayumba wakipiga picha ya pamoja na mmiliki wa mtandao huu Bw Francis Godwin( kushoto) katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha
Godfrey Mushi
Dereva wa gari la wanahabari Iringa akiwajibika hifadhi ya Taifa ya Ruaha
Katibu mtendaji wa IPC Frank Leonard akiwa na mwanahabari Tumain Msowoya katika gari la wanahabari ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha
Vicky Macha na Anita Boma kulia
Oliver Moto na Laurian Mkumbata
Mmiliki wa mtandao huu ambaye pia ni mwandishi wa magazeti ya Rai na Mtanzania Bw Francis Godwin akiwa na mtangazaji wa Nuru Fm Mahija Zayumba
Anita Boma akipiga picha na twiga
Godfrey Mushi akivuka daraja la mto Mdonya

April 29, 2012

WAANDISHI WA HABARI IRINGA WAFANYA UTALII KATIKA HIFADHI YA TAIFA YA RUAHA

Mwandishi wa habari wa ITV mkoani Iringa Laurian Mkumbata akichukua mto ruaha kuu katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha baada ya mto huo kujaa maji ,huu ni utalii wa ndani na uhamasishaji wa utalii kwa watanzania
Mmiliki wa mtandao huu Bw Francis Godwin (wa pili kulia) ambaye ni naibu katibu wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) akiwa na wanahabari wengine katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha ,kulia ni Oliver Moto .kutoka kushoto Hapines Matanzi ,Sophia Mpunga na Paulina Kuye
kazi inaendelea ya kutangaza utalii wetu wa ndani hakika Ruaha ni zaidi ya hifadhi Tanzania
Mwandishi wa Chanel Ten mkoani Iringa na mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa Daud Mwangosi akichukua matukio katika hifadhi ya taifa ya Ruaha Iringa
Mwandishi wa Star TV na radio Free Afrika Iringa Oliver Moto akiweka sawa kamera yake ili kuchukua matukio katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha Iringa
Kutoka kushoto ni Sophia Mpunga (Radio Country Fm) Anita Boma (uhuru) Frank Leonard (habari leo na ni katibu wa IPC ) na Paulina Kuye (nuru FM) wakiwa katika hifadhi ya Ruaha Iringa
Tupo tayari kuutangza utalii wa ndani kwa watanzania
Mwanahabari Sophia Mpunga wa radio Country Fm , Tumain Msowoya wa Mwananchi ,Mahija Zayumba (Nuru Fm)Alein Philip (Ebony Fm ) Godfrey Mushi ( The Guradian ) na Anita Boma (Uhuru )wakivuka daraja hilo la kitalii katika hifadhi ya Ruaha Iringa
Mwanahabari Alein Philip wa Ebony Fm ,Happines Matanzi wa Tanzania daima Iringa ,Paulina Kuye wa Nuru na Laurian Mkumbata wa ITV wakivuta daraja la mto Mdonya katika hifadhi ya Ruaha
Wanahabari wakivuka daraja la kamba ya mto Udonya katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha hakika ni zaidi ya utalii iwapo utafika hifadhi ya Ruaha Iringa
Mwanahabari wa radio Country Fm Iringa Sophia Mpunga (kushoto ) akiwa na mwandishi wa radio Nuru Fm Mahija Zayumba katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha huku nyuma yao kukiwa na twiga
Mwanahabari Paulina Kuye wa Nuru FM akipiga picha na Twiga katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha wakati wa ziara ya wanahabari mkoa wa Iringa katika hifadhi hiyo ya Ruaha
Wataka kujua dhidi ya Swala ?
Mwandishi wa habari wa ITV mkoani Iringa Laurian Mkumbata akijiweka sawa kwa kuchukua matukio katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha baada ya ziara ya siku tatu ya kuhamasisha utalii wa ndani katika hifadhi hiyo kubwa kuliko zote Tanzania
Mwandishi wa habari wa Nipashe Iringa VickyMacha akipata maelezo kutoka kwa mtaalam wa hifadhi Bw Marando
Madereva wa gari la wanahabari wakishangaa wanyama katika hifadhi hiyo ya Ruaha
Wanahabari mkoani Iringa wameanza kuhamasisha utalii wa ndani katika hifadhi ya Ruaha kama njia ya kuwahamasisha zaidi watanzania kupinda kutembelea hifadhi hiyo ya Ruaha Iringa ambayo ni hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania ila pia kuhamasisha utalii katika hifadhi za mikoa ya kusini ikiwemo ya Kitulo, Katavi na Ruaha ambazo bado zipo nyumba kwa uhamasishaji.